Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

GHARIKA & CRATERS KWENYE MWEZI

Gharika na Craters kwenye Mwezi

Ushahidi Wa Uwepo Wa Craters Kwenye Mbalamwezi

Tofauti ya mbalamwezi na sayari ya dunia ni kuwa, mbalamwezi haijizungushi katika mhimili wake wenyewe, inajizungusha tu katika mhimili wa kuizunguka dunia. Kwa hiyo upande wa mbala mwezi unaoitazama dunia hubakia uleule siku zote. na sasa basi, hili linaendelea kudhihiridha nadharia hii katika namna hii. Upande mmoja tu wa mwezi ndiyo huwa na Mashimo makubwa, au Craters. Ambazo pia zinaonyesha uwepo wa maji katika mwezi, na hata lava katika mwezi. 

Je ni kitu gani ambacho kingepelekea craters kwenye mwezi, tena kwa upande mmoja tu. ukitazama upande wa karibu wa mwezi, ‘’near side’’ uko vizuri kabisa ‘’smooth’’. lakini upande usiotazama dunia, ndio huwa na mashimo, na hata dalili za mlipuko pamoja na maji.

Kitu cha kushangaza Zaidi ni kuwa, ndani ya mwezi ni kwa baridi na sio kwa joto kama ambavyo baadhi wangefikiria. kwa hiyo hoja ya milipuko ya volcano inaishiwa nguvu. na pia itashindwa kuelezea milipuko ya upande mmoja tu.

Ajabu tena ambalo hata msomaji wangu mzuri ungekwisha tambua ni kuwa, kuna Ushahidi wa uwepo wa chembechembe za Maisha ‘’organic compounds’’ katika mwezi. sasa je, hebu unganisha craters kwenye upande mmoja tu, mabaki ya milipuko ya lava, uwepo wa maji na organic compounds, je hizi hazituthibitishii tu kuwa kulikuwa na miamba na maudongo yaliyobebwa na maji, na kutengeneza mavimondo, yaliyogongana na mwezi, na kusababisha hizo dhahama katika mwezi?

Kumbuka hakuna nadharia ya mabadiliko ambayo inaweza elezea namna yoyote ile ambayo mwezi ungeweza kuundwa. Mwezi hupingana na kila nadharia inayojaribu kuuelezea. Mfano, nadharia za kuwa mwezi ulikuwa ni matokeo ya migongano ya sayari, na kipande chake kikawa ni mwezi, au namna yoyote ile ya mpasuko kutoka kwenye sayari. Nadharia za namna hii zote hufeli kwa kuwa, mwezi miamba yake isingeweza kuwa hata na kiwango kidogo cha baridi, wala maji yaliyopo, kama ni milipuko iliyotokea awali. maana tayari maji yote yangesha vuka ‘’evaporate’’. Miongoni mwa changamoto kubwa sana ambayo inawatesa watu ni kiwango cha Vumbi lililopo katika mwezi ‘’moon dust’’. Wanasayansi wasioitambua gharika ya nuhu, huamini kuwa mwezi siku zote huwa ukipokea mavumbi, au meteoritic dusts. Ambazo huwa ni matokeo ya jua ‘’solar wind’’ na sasa basi, kutokana na calculations nyingi sana ikaonekana na NASA kana kwamba kuna kiwango kikubwa sana cha mavumbi katika mwezi. ambayo yataharisha hata mtu atakae tua katika mwezi ‘’APPOLO’’. lakini kumbe makosa yalikuwa ni kuamini kuwa spidi ya mavumbi ilikuwa ni sawa katika vipindi vyote. na wao hukadiria kuwa kuna kipindi cha miaka bilioni 4.5 iliyopita, kwa hiyo kuna vumbi la kutosha, kumbe uhalisia ni kuwa, moon dusts zilikuwa ni matokeo ya mlipuko hasa uliotokana na vitu kutoka duniani. na hata Appolo walipoenda waligundua kuwa vumbi halikuwa jingi sana.

Mwezi uliumbwa na Mungu mwenyewe katika siku ya nne ya uumbaji. na sio matokeo ya mlipuko wowote ule wa sayari ya dunia dhidi ya sayari nyingine, na wala sio mabilioni ya miaka.

Picha inaonesha craters kwenye mwezi kwenye upande wa mbali, hii ni kusema kuwa baada ya migongano. upande huu wenye craters ndiyo uliokuwa ukiitazama dunia. na migongano ilifanya upoteze nishati na kupanda juu ‘’swing’’ dhidi ya upande mzito sasa, uliokuwa mbali kutazama dunia. Hii ni kama ukiweka kitu kwenye maji, upande mzito Zaidi ndo huwa unaingia ndani, na hapa ilikuwa hivi hivi.

Milipuko pia katika mwezi ilipelekea kupungua kwa nishati ya mzunguko ya mwezi ‘’orbital energy’’ na kupelekea kupungua kwa siku za mzunguko wa mwezi. Craters kwenye mwezi na dalili za maji katika mwezi, zote zinarejea kwa gharika ya nuhu.

To be continued...