Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

UBIZE NI UTUMWA#

Siri ya Ubize

Hauko Bize

Kila mtu yupo bize na kazi yake, na ni rahisi kuhisi Kwa namna watu wengi walivyo makini na kazi zao, au mambo wanayoyafanya, basi wengi wapo timamu kuelewa kwanini wanafanya wanayoyafanya, lakini ukweli ni kuwa, asilimia kubwa ya watu si zaidi hata ya panzi na panya ambao nao wako bize siku nzima. Mtu mmoja ambaye hajui Sayansi zaidi ya kuijua ni Nini Kwa jina, anaweza hisi ya Nini kujali kujua kwanini naishi kama ninaishi, hii Ndiyo sababu nikasema kama Cha kujali ni kuishi, basi ni kweli Kobe anayeishi miaka zaidi ya 150 ni zaidi ya asilimia 90% ya watu wengi wa Karne hii, wanaoishi wakijali kula, kupendeza, kuzaa, na kulea jambo ambalo hata Nguruwe hufanyiwa kabla ya kuchinjwa akishanenepa zaidi. 

Asilimia kubwa ya watu wako bize kutafuta namna ya kuishi, hasa zaidi Nchi masikini kama za Afrika. Idadi kubwa ya watu wako bize Sio tu Wakati wa siku, bali mpaka Usiku wakifanya kazi na mawasiliano. Hii inathibitisha ni kwanini Zama zote za Binadamu watu wengi zaidi huangamia, wachache sana hupona. Hata katika Biblia zama za Nuhu walipona watu name kati ya Mabilioni, zama za Lutu walipona watatu kati ya maelfu. Biblia inasema pia nyakati za mwisho Njia Pana iendayo upotevuni wataenda wengi. 

Watu wapo bize Kwa kweli, lakini bize kutafuta namna ya kuishi. Inashangaza sana katika asili wanyama waliobize sana kula hasa jamii za Nyumbu, swala, na wenginewe wengi, huishia kuliwa marazote. Wanyama wanaotawala nyika kama Simba, au Chui, marazote huwa na muda mrefu zaidi wa kutokula toka walipokula, sawa na kutafakari, mtazamo huu nimeudadavua Kwa kina sana kisayansi katika Siri nyuma ya Sayansi ya Kufunga na uwezo wa Ubongo. Kiwango Cha Ubize ni kikubwa sana kadri unavyoshuka katika viwango vya utajiri, Matajiri wengi huwa wapo huru sana kufanya mambo yao, kuzungukazunguka, kuwafikiria watumishi wao, n.k. tabaka la kati huwa bize sana kuhangaikia kuweka imara Uchumi wao, tabaka la chini huwa bize zaidi ya Mchwa, Hawa hawana hata muda wa kupumua nyakati kadhaa.

Ukisoma historia utagundua Waafrika walikuwa bize sana kabla ya Ukoloni, na hii ni kutokana na mfumo wao wa uzalishaji ulikuwa si Kilimo haswa, ulikuwa uwindaji. Kilimo huwa kinawapa watu Msimu wa kutulia pale wanapotoka kuvuna kusuburia Msimu mwingine. Kuwinda kuliwafanya Waafrika Kila baada ya muda mfupi kuwaza kwenda Tena porini, hii ni sawa na kauli ya kuwa walikuwa bize sana. Watu masikini hata Leo wako bize sana kuliko matajiri katika kutenda mambo Yaleyale. Waafrika walitawaliwa kirahisi sana na wazungu kutokana na kuwa, walikuwa sawa na Tembo wenye Nguvu lakini hawajui lolote zaidi ya shughuli Moja tu, kuamka na kutembeatembea kutafuta Chakula. 

 Toka nianze kusoma historia za Utawala, jambo linalojirudiarudia zaidi ni moja, Watu wachache, wanaofikiria sana, hutawala watu wengi, wenye manguvu, watendaji sana. Watumwa huwa bize siku nzima, hutembea nyakati kadhaa hata Kwa miguu na mikono, lakini watawala wao hutembelea Farasi huku wamebeba minyororo na mijeredi. Ubize wa watumwa upo palepale hata Leo, Tofauti Pekee iliyopo ni kuwa zama hizi Watumwa hutembelea mpaka Magari, huishi mpaka kwenye maghorofa, huwa na Smartphones, lakini bado huwa chini ya watawala wachache. Ambao ndiyo wanajua oparesheni zote ndani ya chips za Vifaa elektroniki vyote, Algorithms nyuma ya AI na Drivers za Software, 'social scores", wanaelewa Nini kipo ndani ya soda, au Ngano inayoliwa, wanajua kupandisha na kushusha Thamani ya pesa, wanajua kucheza na Vinasaba mfano, "chromosome 2', au "FGF genes' zinazohusiana na Dopamine' katika Ubongo, wanajua kusukuma ajenda za kisiasa, vita, au mitazamo ya kijamii, kiufupi hakuna jipya.

Watu wengi wajinga huisi Dhahabu ina Thamani kubwa, lakini vitu vyenye Thamani kubwa zaidi Duniani hakuna hata kimoja kinachohitaji Dhahabu, Wala Dhahabu Haina Thamani yoyote Ile zaidi ya kuwa watu wengi hawajui Thamani ya Dhahabu inadhihirisha Thamani ya Ubongo "imani'. Kila kitu chenye Thamani Duniani kimetoka katika Ubongo wa Mtu aliyefikiria. Siri zote za Nguvu na mamlaka katika Ulimwengu zimejificha nyuma ya Ubongo, hata Biblia katika Mithali inasema, ' Linda Moyo wako kuliko yote uyalindayo". Watu waliobize kamwe hawawezi jua Siri hii Kwa kuwa Binadamu hakuumbwa kuwa bora zaidi katika utendaji, Mchwa Wenda waliumbwa hivyo. Binadamu aliumbwa kuwa Bora zaidi katika kufikiria, na hii Ndiyo sababu niliandika katika sehemu ya Sayansi, hata Utumbo mdogo wa mtu umerefushwa zaidi ili aweze kutumia muda mfupi zaidi katika kula, Tena Vyakula vilivyopikwa, tofauti na Sokwe anayetumia masaa 6-10 kula tu.

Dhumuni la kitabu hiki nikumfanya msomaji atambue Ubize huu wa mfumo wa Maisha ya Leo, una ajenda kubwa ya kuwaficha watu wasijue tukio kubwa zaidi lililokwisha wafikia watu, La Dhiki kuu zaidi ya Ukoloni mambo Leo, au Bomu la nyuklia la Hiroshima. Watu hawajui wameshachelewa hata hivyo kujiokoa nyakati hizi, Luka 17: 26-29, imeandika, Kama nyakati za Nuhu, na Lutu, watu walikula na kunywa zama hizi zote na kujikuta washachelewa kujiokoa walipodondokewa na kitu kizito. Belshaza aliposhiba sana na kufurahia, huo Usiku ndiyo Dunia iliandikwa historia ya Ufalme' mpya wa "Medi na Uajemi". Falme zote hata Ugiriki "Alexander the great ' & Rumi zilianguka zilipokuwa imara zaidi Kwa kujiamini. Biblia imeandika "Usikiapo Amani basi ujue mwisho umefika". Leo hii asilimia kubwa ya watu hawajui namna Magharibi inavyoanguka, au angushwa, makusudi, Kwa malengo yenye ajenda nyeti sana tutakazozigusia sawa na tabiri za Ufunuo. Lakini ni nani asiyejua namna Wamagharibi walivyokuwa na Viburi, na ubize wa Maisha Kwa kadri walivyokuwa wakitajirika. Kiufupi uwe Kwa Umasikini, au utajiri, Mfumo wa Maisha unakutaka uwe bize ili usitumie Ubongo.

Lengo la kitabu hiki Sio kukwambia umesimama uwe makini usianguke, ni kukwambia umeanguka, Anza kuchukua hatua usimame. Kitabu hiki ni matokeo ya Maarifa yanayotokana na kumcha Bwana. Ijapokuwa kinabebwa na hoja nzito za Sayansi, falsafa, na historia, lakini Elimu katika kitabu hiki haipo katika Fungu la Maarifa yanayokosekana Kwa watu wanaongamia "Hosea 4:6'. Maana wasomi wengi zaidi ndiyo wagonjwa wakubwa zaidi wakiakili na kimwili, Kwa kuwa Elimu ndiyo huwa-Fanya watoto kuwa bize, toka wanajifunza kuongea mpaka wanapong'oa meno Kwa Uzee, Tena kuwa bize kufuata maelekezo na maagizo yaliyokwisha pitishwa. Arthur Schopenhauer aliwahi sema, 'zipo nyakati zinakuja ambazo watu wasiosoma watakuwa na Akili timamu kuliko wasomi", na Nietzsche alithibitisha hili Sio tu Kwa Wasomi wa Elimu za Jumuiya, bali hata Elimu za Dini. Mungu akusaidie kuelewa somo hili fupi la kuelewa mtego mdogo sana ambao unapaswa kuujua ili uweze kutoboa Wakati wowote toka Sasa patakapochafuka zaidi.

...