Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MAJANGWA& MILIMA BAADA YA GHARIKA

MAJANGWA& MILIMA BAADA YA GHARIKA

 Jangwa la sahara ‘’sahara desert’’

Najua msomaji mdadisi lazima atakuwa na hamu ya kujua chanzo cha jangwa hili, ambalo limechukua sehemu kubwa sana ya dunia. Katika tafiti zangu kikubwa nilichokigundua kuhusu jangwa la sahara ni kuwa, hakuna tofauti kubwa sana ya nadharia za uundwaji wake, baina ya pande mbili za sayansi, yaani ya gharika kuu, na inayofundishwa kwa mitazamo mingine. Japokuwa haimaanishi kuwa wanakubaliana moja kwa moja na kilichoandikwa katika nadharia hii. Hebu tuangalie miongoni mwa sababu za jangwa hili la sahara lililopo Africa ya magharibi, na kaskazini.

Jangwa la sahara liliwahi kuwa sehemu nzuri kabisa ya ukijani. Tafiti zinaonesha jangwa hili lilikuwa na kiwango kikubwa sana cha mimea, lakini pia kiwango kikubwa sana cha maji. Miongoni mwa vitu vilivyoonekana ni pamoja na uwepo wa mabaki ya ziwa, ambalo linaaminiwa lilikuwa ziwa kubwa Zaidi kuwahi kutokea katika jangwa la sahara.

swali la kwanza: maji yalitoka wapi?

Moja kwa moja kutoka katika nadharia yetu, tunakumbuka kuwa baada ya dunia kupasuka. Upande wa Pacific ulikuwa wa moto sana, kiasi kwamba ulipelekea mvuke mwingi sana, ambao ulipofika maeneo ya latitude za juu na chini ya dunia, ambazo zilikuwa zimepoa sana au za baridi sana, uliganda na kusababisha kiwango kikubwa cha barafu. ambazo ndizo zilizopelekea zama za barafu ‘’ice age’’. Sasa basi, upande huu wa Sahara ulikuwa katika maeneo ya karibia na Equator, ambapo kulikuwa na kiwango cha joto la kawaida bado. na hivyo ilipelekea mvuke huu ulipofika maeneo haya ya sahara, kusababisha mvua nyingi sana. Na mvua hizi zilikuwa nyingi kwa kipindi cha miaka karibia karne, na ndizo ambazo zilipelekea maji mengi hata ya kuweza kutengeneza mito mikubwa na hata maziwa kadhaa. Pia unaweza tazama maziwa mengi yapo yakizunguka ukanda huu wa sahara na hata equator ya leo. pia utaona mvua nyingi zilipelekea maziwa na mito mingi. sahara ilikuwa kijani yenye maji na ndiyo maana, miongoni mwa makumbusho makubwa ya kale ya michoro yaliyopo katika mapango ya sahara, yanaonyesha uwepo wa maji mengi na viumbe wengi sana hapo zamani. 

swali la pili: ilikuwaje likawa jangwa? 

Miongoni mwa sababu kubwa sana, ilikuwa ni badiliko la kuzunguka kwa dunia, ‘’Earth tilt’’. Dunia ilizunguka kutoka katika namna iliyokuwa imeegama zamani, mpaka iliyopo sasa. Badiliko hilo lilipelekea kubadilika kwa tabia nyingi sana za nchi, ambapo kwa upande wa sahara ilikuwa hivi. Kutoka katika sehemu mpya lililopo jangwa la sahara, utaona nyuzi 30° juu na chini katika anga lake kuna kiwango kidogo sana cha mawingu, ambapo inatokana na kusambaa kwa mawingu kuelekea kusini na kaskazini. hii ni mithili ya maji yaliyopo mlimani, hushuka kuelekea pande zote. Na sasa basi, hii ililiacha eneo hili likiwa huru kupokea kiwango kikubwa sana cha mionzi ya jua, na pia likipoteza kiwango kikubwa sana cha maji. Hii ni miongoni mwa sababu za kuchangia utengenezwaji wa jangwa la sahara.

Kumbuka jangwa la sahara ni asilimia 50% tu linahusisha milima iliyojaa michanga, linasehemu zingine kubwa sana ambazo ni kame na zina mazingira mengine.

Yapo majangwa mengine pia huaminiwa kuundwa na sababu zingine. Ila ukirejea picha chini, unaweza ona namna majangwa mengi huundwa katika maeneo yenye ukanda unaofanana, unaweza pata picha juu ya uhusiano wa majangwa, na sehemu yake katika dunia.

Mabaki ya uwepo wa historia ya maji katika jangwa la sahara.


Miamba ya mchanga ‘’liquefaction plumes’’

Miongoni mwa vitu ambavyo nadharia ya gharika tu inaweza vielezea ni miamba ya mchanga. Unaweza jiuliza ungewezaje elezea vitu kama vifuatavyo.



Kama ni msomi unayetumia nadharia za mabadiliko ya jiolojia kujibu maswali. hakuna namna unaweza tegua huu mtego, unahitaji nadharia ya gharika kuelezea hii miamba ilivyoweza kuundwa.

Kutumia miaka hata milioni kuelezea mabadiliko haya haiwezekani, wala haiwezi leta uhalisia. Hebu tuangalie namna sayansi ya gharika kuu inavyoweza tusaidia jibu haya maswali kirahisi kabisa.

Kwa kawaida mchanga ni aina ya chembechembe pekee ambazo huwa na uhusiano mzuri Zaidi na maji. hasa kutokana na tabia yake ya kuyaachia maji nafasi ndani, hii imewezesha mchanga mwingi Zaidi kubebwa na maji muda wote. na ndiyo maana, pwani zote huwa zikijaa michanga. Sasa basi, supercritical water yalikuwa na idadi kubwa sana ya chembe hizi za michanga, na kadri maji haya yalipokuwa yakipanda, yalifikia hata levo ya matabaka kadhaa ya ardhi. Sasa hapa unaweza tumia picha yenye kielelezo rahisi kabisa chini.

Hatua ya kwanza ni mchanga ambao unakuwa umepanda kutoka chini, lakini uko chini ya matabaka umegandamizwa.

Hatua ya pili huusisha mabadiliko ya dunia, hasa mikunjo ya matabaka ‘’compression’’. Ambayo huupa upenyo mchanga wenye maji kupanda katikati ya matabaka mazito.

Hatua ya tatu huusisha mchanga kugandamana, ambapo ili kufanya hivyo unahitaji kemikali za kusimenti. Ambazo zimetoka kwa madini ya silica ndani ya Quartz. Ambazo ni matokeo ya joto la supercritical water.

Ushahidi Zaidi ni uwepo wa matobo katika miamba hii, ambayo huonesha kuwa maji yaliyokuwa katika miamba hii yaliendelea kuvuja yakitoka.

je wajua milima hutoa maji

Kiwango kikubwa cha milima kimekuwa ndiyo chanzo cha maji, na chemchemi kwa miaka mingi katika jamii kadha wa kadha. bila watu kujua kuwa maji hayo yalikuwa ni matokeo ya maji ya gharika au ‘’supercritical water’’. Ambayo yalikuwepo katika kutengeneza milima mingi, na kadri muda ulivyokuwa ukizidi Kwenda, hata baada ya milima kuundwa maji haya yalikuwa yakitoka kidogo kidogo, na katika chaneli ndogondogo tokea ndani ya milima. Tazama mashimo katika mlima huu.