CODE YA 03, MAREKANI #
Code Ya 03
Watawala wakubwa wa Marekani waligundua kuwa wana changamoto kubwa ya pili katika nchi yao, ambayo inawafanya kushindwa kuwa na mamlaka na nguvu kama watawala wa nchi nyinginezo japokuwa zipo chini yao, na hiyo changamoto ni kuwa, Nchi ya marekani nguvu kubwa zaidi ipo kwa watu. Tena kuanzia watu wa chini kabisa, mpaka watu wa tabaka la kati ‘’middle class’’. Kumbuka kama tulivyoona awali tabaka la juu kabisa la Mabilionea na watoto wa kifalme ‘’Royal families’’, lina asilimia ndogo sana ya watu. Nchi ya marekani ilikumbwa na changamoto hii ya kutokuwa na nguvu kwa watu wachache, na hii ilichochewa na falsafa yao ya Demokrasia, na maendeleo ya Kibepari.
Kwa upande wa Nchi ilikuwa imefanikiwa sana kimaendeleo, lakini kwa upande wa watawala, ilikuwa bado sana haijaendelea. kwa upande wa kiutawala Nchi za mashariki zilikuwa zimeendelea zaidi, hii ni kutokana na mifumo yao ya kiutawala. Ndoto kubwa ya Marekani ilikuwa ni kuja kupata namna ambayo itaweza kuwa na nguvu za kuwatawala watu kwa kila namna. Sio tu kuwatawala katika mantiki ya kiuongozi, bali kuwatawala kuanzia kiuchumi, mpaka kiakili. Watu wengi duniani hawajui kuwa adui mkubwa zaidi wa Marekani sio Raia wa Mashariki, Adui mkubwa wa Marekani ni raia wa marekani. Raia wa marekani ni watu ambao Teknolojia na Uhuru viliwapa Nguvu sana ya kiakili, kiuchumi, kijamii, na wakawa na hamasa kubwa katika kila Taasisi kubwa duniani, katika kila Nchi duniani, unaweza gundua hata leo hii kuwa wamarekani ndiyo watu wenye Mchango mkubwa zaidi katika kila fani yenye motisha kubwa katika elimu, katika dini, na hata katika haki na misaada ya amani. Wamarekani ndiyo watu wanaopinga matendo maovu ya nchi yao kuliko hata mataifa wanayoteswa na Marekani. Katika kuelekea karne ya 20, Viongozi wa siri, Timu za wanasayansi, na Matajiri wachache walionyuma ya mashirika makubwa sana ya Kijasusi ya marekani kama ‘’DARPA, DoD, CIA, na mengineyo kadhaa’’ waligundua namna pekee wanayoweza kuwatawala watu kirahisi sana. Namna hii haikuwa ngeni, ila ilikuwa ni namna ya kutumia Teknolojia ileile, katika utaalamu wa kitofauti sana sasa.
Kwa Mara ya kwanza Marekani sasa iligundulika kuwa unaweza kuitawala akili ya mtu, sio kwa kutegemea tu vipachikwa katika Ubongo ‘’Brain implants’’, bali kwa kutumia mionzi. Ugunduzi huu ulishakuwa ukifahamika nchi za Urusi ambazo wao walikuwa wakizitumia sana kutawala watu wao, ila kwa marekani ilikuwa bado ni teknolojia ngeni. Marekani ambao awali waliwekeza sana katika teknolojia za anga ‘’Space science’’, waligundua teknolojia za anga haziwezi kuwapa faida kubwa katika vita hii mpya ya kutawala watu. Kiwango cha Pesa ambacho kiliwekezwa kwenye misheni kama za kwenda Mwezini, kwenda sayari za Mbali kilishushwa sana, sasa hivi kiwango kikubwa cha Pesa kikaanza kuwekezwa katika sayansi za Biolojia za kiwango kidogo zaidi, zikiwa zimelenga zaidi kufuatilia namna bora kabisa za kutawala biolojia za viumbe. Kulikua na namna mbili za project ambazo zilikuwa na matokeo makubwa zaidi kwa nchi ya marekani. Project za kwanza zilikuwa kupitia Makampuni Binafsi ambayo yalikuwa na interest kwa nchi. Na haya unaweza yakuta kwa kuangalia project kama za Biolojia za molekuli ambazo sasa zilikuja na maendeleo makubwa ya teknolojia za kuinjinia jenetikia za viumbe. Na hapa ndipo unakutana na teknolojia kama za MONSATO za kubadilisha jenetikia za viumbe, mfano ni utengenezaji wa mimea ya GMO, ambayo ilikuwa na nguvu kubwa kama unavyoweza gundua kupitia muitikio wa Raisi George Bush. Teknolojia zote za mtindo huu wa kucheza na jenetikia za viumbe na biolojia ya molekuli kwa lengo la kuchochea uzalishaji wa viumbe, utengenezaji wa bidhaa za kisasa, n.k. zilikuwa na lengo kubwa sana kwa nchi ya marekani. Project zingine ambazo zilikuwa chini ya Makampuni na watu binafsi watakao kuwa na shea na Serikali ni kama Space X ambayo inamilikiwa na Elon musk, tangia zamani Marekani ilikuwa na utaratibu wa kushea na matajiri project ambazo mwishoni tutaona malengo yake. Na ndiyo maana unaweza kukumbuka namna Bill Gates alivyokuwa akihamasisha sana hatua zichukuliwe dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa hata kwa mbinu za kuhamasisha kushusha uzalianaji wa watu. Serikali kwa upande wa pili kupitia mashirika yake ilikuwa ikisimamia tafiti zote kuhusiana na uwezo wa kutawala ubongo na mazingira kwa mionzi mbalimbali.
Haikuwa kazi rahisi kwa lolote kati ya project hizo kuu mbili. Kulikuwa na upinzani mkubwa sana kama ambavyo unaweza kuona kupitia vita kali iliyokuwepo kati ya wanasayansi kama Robert Becker dhidi ya Serikali, hasa baada ya kuumbua madhara makubwa ya kiakili ya mawimbi ambayo yalikuwa yakivuja toka nyaya za Mitambo ya Meli za kijeshi ‘’US Navy’’. Katika zama hizi ilishafahamika kuwa unaweza kuathiri biolojia ya kiumbe kwa kutumia tu mawimbi, na tena, sio mawimbi makubwa ambayo mtu anaweza yagundua, ni mawimbi madogo sana ‘’Extreme longer frequencies, au ELF’’. Kulikuwa na maelfu ya tafiti mithili ya Mtaala ‘’syllabus’’ ambayo mtu angeweza kuanza kusoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho, na akajua A-Z. unaweza kuligundua hili kwa kusoma kitabu cha Alexander van Widjk. ufupi ni kuwa, Serikali ilitambua kuwa kwa kuruhusu elimu hii ifahamike kama elimu zingine, itapoteza mbinu zake za kuweza kuwatawala. Jose Delgado alionyesha kuwa unaweza kumsisimua ng’ombe kwa mfumo wa umeme mdogo sana akawehuka. Alan Frey aliyekuwa Mwanafizikia na mtaalamu wa Radar alionyesha kuwa kwa kummulika mtu na mawimbi ya 300Mhz mpaka 3Ghz katika vituo maalamu ‘’pulse rates’’, unaweza kumfanya asikie sauti kichwani mwake bila hata uwepo wa hizo sauti. Alikwepo Ross Adey ambaye alionesha mawimbi madogo sana (extreme low intensity EMFs kama 1uW/cm²) unaweza athiri hata Biolojia za viumbe kama ukuaji wao, n.k. zilifanyika tafiti za kuweza kuathiri akili za watu hata wakiwa mbali sana bila kujijua na zikafanikiwa. Marekani kumbuka awali ilipitia kipindi hicho cha kulengwa awali nao katika Ubalozi wao na Russia, ambapo walilengwa kwa mawimbi madogo ya Woodpecker ambayo yalikuwa katika wastani wa fequency za 10Hz, hizi zinafanania sana na frequency za Ubongo, mawimbi haya yanapomulikwa kwa mtu katika saizi fulani ‘’Amplitudes’’ na frequencies, ndipo yalipochochea shida kama za Saratani, na magonjwa ya ajabu ambayo yalikuja kupelekea vifo vya watumishi wengi sana katika Ubalozi wa Marekani. Na kutoka pale Marekani ikaibuka na mipango mikubwa zaidi, huku ikiibuka vita baridi ya Kutawala hali za watu na mazingira.
Marekani walishatambua kinachofanyika ni hatari sana kwa watu, na hivyo tafiti zote zinazohusiana na shughuli za anga, na shughuli za akili za watu, zilifanywa katika vitengo vya siri tu vya kiulinzi. Mtazamo huu ulilenga kuwafanya watu wasielewe kinachoendelea kutokea. Upande wa Pili wa afya ambao ndio uliopaswa kuwa mstari wa mbele zaidi kulijua hili, ilitengenezwa namna ionekane kana kama hizi ni sayansi zisizothibitishwa, na hazina uhalisia. Mfumo wa elimu ulizidi kuboreshwa kujikita katika falsafa zile za kuegemea Biolojia ya jenetikia na molekuli. Mfumo huu ulilenga kumfanya kiumbe kama mfumo wa kemikali, na sio kama uhalisia ambao ni mfumo wa mawimbi na umeme.
Mfumo wa kemikali ulilenga kuzingatia kujaza kilichopungua, na kupunguza kilichojaa. Mfumo huu ulichochewa zaidi na mashirika makubwa ya Kibiashara ya Marekani ya Madawa ‘’Big Pharma’’, ambayo yalijengwa na falsafa za wawekezaji wa awali kabisa kama kina Rockefellers. Hawa waliwekeza katika uundwaji wa madawa, na kadri magonjwa yalivyozidi kuongezeka walizidi kuingiza fedha zaidi. Watu hawa walishagundua ukitawala mfumo wa elimu, umeshatawala Nchi. Kwa mara ya kwanza wakachochea zaidi mitaala ya elimu ambayo haitahusisha elimu za kuelewa kiini kabisa cha uhai, uwezo wa mwili wa kujiponya, na mwanafunzi akapatiwa muda mfupi sana wa kujifunza kuhusu misingi ya uhai, akipatiwa muda mrefu zaidi wa kujifunza kuhusu namna ya kutibu kwa kutumia madawa, miongozo iliyowekwa, na kufuata utaratibu uliokwisha kuwekwa. Taaluma ya afya ikatenganishwa sana, kiasi kwamba mtaalamu mmoja hana maarifa kamili kuhusu Afya na uhai. Mfano, Daktari sio mtaalamu wa maabara, hiyo ni kazi ya mtu wa maabara ‘’Lab scientist’’, Daktari sio mtaalamu wa madawa, hiyo ni kazi ya mtu wa madawa ‘’Pharmacist’’, Daktari sio mtaalamu wa Lishe, hiyo ni kazi ya ‘’Nutritionist na Dietitian’’, Daktari sio mtu Vifaa vya uchunguzi kama X-Rays, hiyo ni kazi ya ‘’Radiology’’, idadi ya Wabobezi wa taaluma moja moja kama wataalamu wa Mifupa tu ‘’Orthopedic surgeons’’, au wa Tumbo ‘’Gastroenterologist’’, au wa wa Ubongo ‘’Neurologist, neurosurgeons, psychiatrists’’, n.k. ikaongezeka sana. unaweza usielewe hili kwa hatua ya kwanza, ukihisi inasaidia sana kiutendaji, na ufanisi, likimpunguzia mzigo mtu mmoja, lakini hii falsafa ilianza kuondoa wataalamu wanaoweza kugundua na kuchunguza taarifa toka kila mlango linapoweza pitia.
Wabobezi wa Viungo, na ubobezi wa fani huua Uwezo wa kidaktari, kwa kuwa mwili hutenda marazote kama kitu kimoja, Madaktari wakubwa wote hupimwa kwa upana wao wa kimaarifa ya kitabibu katika mwili mzima. elimu ya udaktari inapaswa kuongezewa muda hata kama ni miaka 10, ambayo mtu angeanza mapema, ila ingetengeneza watu wasiobobea kwenye Vimelea lakini hawajui hata seli za figo. Asilimia kubwa ya madaktari hata hawajui madhara ya soda kwa kuwa sio fani yao. Ni ngumu sana kupata wabobezi kama Robert Lustig ambaye yupo kitengo cha watoto lakini anajua madhara ya sukari za viwandani. Inahitaji uwezo wa kuzaliwa wa mbobezi wa Upasuaji wa Ubongo kama Jack Kruse kujua madhara ya WiFi katika Biolojia ya Ubongo. na adui mkubwa wa watu hawa huwa ni wenzao madaktari wanaowashangaa. Marekani ilichochea falsafa za Ubobezi kama ilivyo falsafa yake ya Tenganisha ili utawale. Mifumo ya afya ilishamiri wataalamu ambao walifanya kazi kwa ajili ya mamlaka, na sio wagonjwa. Maendeleo makubwa ya Biolojia za molekuli yalipushi biashara za vyakula vya kisasa kwa kuchochea sana uzalishaji wa mazao ya kisasa, visisimuaji, wanyama wa kisasa, haya yote yalikuwa na madhara makubwa sana kwa watu, na hakuna ambaye angeweza kuyagundua kirahisi.
Sasa Marekani iliweza kufanikiwa kutengeneza uwanja wake wa kufanya tafiti za kutafuta namna gani inaweza kutawala akili za watu, huku dunia nzima ikiwa haina wa kugundua nini kinachoendelea. Kama unaweza mficha daktari asijue kinachoendelea, hakuna mtu mwingine katika taifa anaweza kukuletea changamoto. lakini kama unaweza kumtuliza Raia wa Marekani akakaa kimya, hakuna binadamu mwingine duniani anayeweza kusimama. Ukizingatia na Nchi za Mashariki ambazo hazina Uhuru wa kuzungumza wa raia mmoja mmoja, au hakuna raia wenye nguvu za kusukuma tafiti za mapenzi yao wenyewe, tofauti na marekani ambayo huwa na wasukuma tafiti kifedha wengi sana. Ukija Nchi za Afrika ndiko hata bado hawajui tafiti ni nini. Hebu tuangalie siri gani ambayo Marekani ilizifikia baada ya mafanikio haya.

Join the conversation