Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

GHARIKA, PLUTO, & SAYARI YA MARS

Gharika, Pluto, na Sayari Mars

Pluto Changa ‘’Young Pluto’’

Picha za pluto zinaionesha kuwa na sura ya uchanga. na kuwa sio sayari ya miaka mingi kama ambavyo wengi wangetamani. Pluto ina milima ya barafu, tena barafu ya kaboni monoksaidi. Huwezi elezea hili swala kwa kutumia nadharia za mabadiliko, ambazo zinaitaka kuwa ya miaka mingi ‘’mabilioni’’. lakini ndiyo kwanza hii pluto inaonyesha haina muda mrefu, nukuu za baadhi ya wanasayansi wa anga, husema kuwa, ‘’hawajawai ona sura changa kama ya pluto’’. Ukweli ni kuwa, hizi zote zilitoka duniani katika kipindi cha gharika ya nuhu. Pluto ina uwepo wa milima bila craters, na milima yake ni ya kaboni monoksaidi ‘’CO’’ ambayo inadhihirisha kuwa, milipuko ya pluto ya barafu iliyokuwa ndani ilipelekea hewa hii kutoka nje, ambapo kuna baridi kali ya -382°F. na kwa kuwa CO huganda tu katika nyuzi -313°F, basi nyingi ili ganda na kushuka katika uso wa Pluto na kuunda vimilima.

Pia pluto huonekana na rangi ya wekundu, kuashiria uwepo wa madini ya Chuma au Iron kwa kiwango kikubwa kama vilivyo vitu vingine kama vimondo, hata asteroids, Ambazo zimetoka katika gharika. ambako ndani ya dunia kuna kiwango kikubwa cha Iron.

Asili Ya Chembechembe Za Uhai Na Maji Katika Sayari Mars.

Sayari ya Mars ni miongoni mwa sayari maarufu sana duniani. hasa kutokana na stori nyingi, hata filamu nyingi, ambazo hutumia ‘’science fiction’’, kuonyesha kana kwamba kulikuwa na maisha katika sayari ya Mars. Lakini ukweli uko hivi, Mars ina hali ya hewa ya -80°Fahrenheit au nyuzi -62.22°Celcius. hii ni hali ya hewa ndogo sana kusapoti Maisha ya kiumbe yeyote yule, na hii ni kutokana na kuwa, mars iko mbali kidogo na jua ukilinganisha na dunia. Pia sayari ya Mars haina anga ‘’atmosphere’’. Au ina uwepo wa katabaka kadogo sana kama unaweza ita ka ‘’anga’’ kadogo ambako kana gesi kidogo sana za kaboni dioksaidi, argoni, mvuke wa maji, nitrogen, na oksijeni. kwa kiwango ambacho hakiwezi sapoti Maisha, maana hata maji huwa barafu. 

maajabu ya sayari ya Mars yanayo hitaji gharika ya nuhu tu kuelezea.

uwepo wa miamba iliyo na michirizi ya maji

Kwakweli ni ajabu kuona kulikuwa na maji ya kimiminika katika sayari ya Mars. Ambapo katika mars maji hayawezi kuwepo yataganda ndani ya sekunde tu. hebu tazama picha zifuatazo hapa chini. 

Hizi picha zote zinaonesha kazi iliyofanywa na maji ya mmomonyoko ‘’erosion’’ katika ardhi ya sayari ya Mars. na sasa swali linakuja maji yalitoka wapi? Wapo wanasayansi ambao hawajui sayansi hii ya gharika ya nuhu, na hujaribu kusema kana kwamba kulikuwaga na volcano katika sayari ya Mars, na ikapelekea maji kuja sehemu za juu. lakini bado hufeli kwa maana, kwa baridi ya kwenye mars, hata kukaribia umbali mchache sana tayari maji yangeshaganda. na bado hakuna Ushahidi wa uwepo wa maji katika miamba ya chini ya Mars.

jibu sahihi 

Kutokana na vimondo au Comets ambazo awali zilikuwa zimetoka dunia zikiwa katika space, ziligongana na sayari ya Mars na kupelekea kiwango kikubwa cha nishati ya msuguano, na joto, iliyopelekea kuyeyuka kwa barafu ambazo zilikuwa ziko kwenye vimondo tokea duniani, na maji haya yaliyo yeyuka, ndiyo yaliyopelekea maji hayo ambayo matokeo yake tunayaona. na pia kuna kiwango kikubwa sana cha Craters katika Mars. Ambazo zinadhihirisha migongano hiyo. na mwisho kabisa uwepo wa anga dogo, ni matokeo pia ya hewa zilizokuwa katika meteorites awali kabla ya kugongana. yaani zimetoka duniani. Na leo hii kama kuna mabaki ya chembechembe za uhai zitaonekana katika sayari ya Mars, basi asili yake ni duniani.


Hii ni picha ya Gale crater iliyopo katika sayari ya Mars. Kumbuka pia sayari ya Mars haina magnetic field kama ilivyo venus. na hata mbeleni tutaona ilivyokuwa kwa sayari ya dunia. pia ilikuwa awali na usumaku kidogo.


To be continued