Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

CODE YA 02, MAREKANI#

Nyuma ya Marekani

 CODE YA 02

Marekani ambayo sasa ilikuwa juu zaidi kiuchumi na kijamii, ilikuwa inatumia mfumo wa kuwapa watu uhuru na kuwachochea kiteknolojia. ikiwaruhusu watu kufanikiwa zaidi, na kuikuza zaidi nchi yao kiuchumi kupitia kodi na mzunguko mzima wa huduma na ajira. Mfumo huu uliwapa zaidi watu na matajiri nguvu, kuliko hata serikali kwa namna fulani. Marekani ilikuwa ni Nchi ya watu haswa kama ilivyo maana ya Demokrasia, yaani ‘’Serikali ya watu, toka kwa watu, na kwa ajili ya watu’’. Hii ilikuwa ni ajenda yao kuu tangia enzi za Benjamin Franklin. Kama ilivyo kawaida ya watu wanapokuwa juu, tayari huibuka matatizo. Changamoto kubwa mbili ambazo zilitokea zilikuwa kwanza ni Nchi za Mashariki, kuanzia Asia mpaka Uarabuni, China, na Japan. Hapa tatizo lililoanza ni kuwa, nchi hizi zilionekana kuwa na ajenda maalumu kabisa ya kutafuta namna za kurejea katika nafasi yao ya kutawala dunia nzima. Kumbuka Utajiri mkubwa zaidi wa Dunia upo Mashariki mwa Dunia, hii ni kutokana na uwepo wa Watu wengi zaidi, na pia uwepo wa vyanzo vikuu vya nishati hasa Mafuta, na Makaa ya mawe. Mashariki imekaa kusapoti Biashara kirahisi zaidi na Dunia nzima. Nchi za Mashariki waligundua kuwa kama wanataka kuwa juu haiwapasi Kuruhusu Uhuru hata kidogo, hii ni kutokana na uwepo wa makundi mengi sana, na pia hali za watu zilikuwa duni sana. Watu wa Mashariki kuanzia na Falsafa za Karl Marx waligundua wanapaswa Kuishi Nchi nzima kama Familia moja, ambayo Baba na mkewe tu ndiyo watakuwa wanasimamia kila kitu, na Nyumba nzima hakuna mtu atakayekuwa anamiliki chochote kile, kila mtu atakuwa tu akipangiwa majukumu, na akipangiwa ataishije ndani ya familia. Mfumo huu wa Kijamaa ‘’Communist’’ ambao ulikuja kuchochewa rasmi na Raisi wa kwanza wa Russia ‘’Vladmir Lennin’’, uliingia rasmi kwa mapinduzi makubwa ya mwaka 1917, Mapinduzi ambayo yalipelekea kuondolewa mpaka Kifo cha mfalme wa Mwisho wa Russia Mfalme Czar.

Mfumo wa Kikomunisti hauko kijamaa kama wengi wanavyohisi. Mfumo huu huwafanya watu wote ndani ya nchi mithili ya maroboti. Ambao mnaweza kupangiwa kuanzia kazi utakayofanya, ratiba ya kazi yako, mshahara utakaolipwa, Dini utakayoabudu, na nyakati nyingi hata Idadi ya watoto utakaoruhusiwa kuzaa, kama ilivyo China. Adui mkubwa wa Ukomunisti alikuwa ni Dini ya Ukristo. Hii ilitokana na falsafa za ukristo za kuwa mtu ana uhuru wa kuamua lolote, pili Mungu ndiye aliye juu ya yote, tatu umasikini na utajiri zote ni hali za kupokelewa, na mwisho taasisi za dini huwa na nguvu hata kuingiliana na mamlaka ya nchi. Ujamaa kwanza umejengwa katika kutoamini Mungu, dini ya ujamaa ni Marxism yaani ‘’No God’’, na hiyo ndiyo Dini utaiona utakapofika tu China, inayoitwa ‘’Buddha’’. Ujamaa umelenga Serikali ndiyo kiini cha Nguvu zote, na agizo linapaswa kufuatwa bila majadiliano, hakuna uhuru wa kuamua unachotaka, watu wanapaswa kufuata kilichokubaliwa na jamii yote na kusimamiwa na serikali, sio kwamba kuna Demokrasia ya kuwazingatia watu wachache, Ujamaa ulilenga Kufanya Nchi kuwa na Nguvu mpaka mwisho. Ni kama kila mtoto afanye kila kitu kwa lengo la familia kuu tu, sio mambo yake. Mfumo huu ulichochea sana maendeleo, ijapokuwa historia rasmi zinaonyesha ulimwaga damu ya wakristo zaidi ya Milioni 13, lakini zisizo rasmi zinajumuisha umwagaji wa damu wa wakristo zaidi ya Milioni 100+, na tena ukimwaga mamilioni ya damu za Vichanga ambao walipaswa kuuwawa wanapopata Mimba watu zaidi ya maagizo, au mimba za watoto wa jinsia isiyohitajika kwa wakati huo. Historia inatambua mwanzo wa kukua kwa falsafa za kikomunisti, kulienda sambamba na kuanzishwa kwa mitaala ya elimu iliyokataa uwepo wa neno ‘’Mungu’’ katika vitabu vyote, na huu ndiyo ulikuwa mfumo mpya wa elimu hata leo, kuanzia miaka ya 1920’s, ambapo elimu zote mpaka marekani walikubaliana na falsafa za kutokuwepo kwa Mungu, tofauti na wasomi wote wa kabla ya miaka hii.


Mfumo wa Ukomunisti ulichochea maendeleo makubwa sana ndani ya muda mfupi, na hii ndiyo sababu China toka ijiunde kikomunisti rasmi mwaka 1949, ilitumia miaka 22 tu kuwa juu namba mbili kiuchumi duniani toka ianze mageuzi ya kiuchumi iliyoanza mwaka 1978. Hii ni sawa na kusema, nchi za Ukomunisti zilianza kuwa na nguvu sana kiuchumi jambo ambalo lilikuwa na nguvu sana ya kivita ya kiutawala dhidi ya marekani. Ukiachana tu na nchi hizi za ukomunisti, bado mashariki ya kati ilikuwa na nchi nyingi sana za kiarabu. Nchi hizi zilikuwa na utajiri mkubwa zaidi wa mafuta. Mafuta ndiyo nishati kubwa zaidi ya dunia katika kuendesha viwanda vyote, magari yote yanayosambaza biashara, Meli zote za mizigo, biashara ya mafuta ndiyo ilikuwa kiini cha aidha viwanda vya kiteknolojia, au biashara za vyakula. Nchi hizi za kiarabu zilizokuwa na falsafa za kufanania na ukomunisti, ila zenyewe zikiwa chini ya falsafa za Kiislamu, zikaanza nazo kuwa na mtazamo wa kuungana kuanzia enzi za Saddam Hussein, Gamer abel Nasser, Muhammad Ghaddaf, n.k. hizi nazo zikaongeza stress kwa Marekani.

Nchi ya Urusi nayo ilikuwa juu sana, na tena, hii ilikuwa na presha zaidi katika teknolojia ya anga dhidi ya Marekani. Mfano, Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, mataifa mawili makubwa—Marekani (USA) na Umoja wa Kisovieti (USSR)—yalishindana kwa nguvu kwenye Space Race kwa kuajiri wanasayansi wa roketi wa Kijerumani waliokuwa sehemu ya mpango wa V-2, akiwemo Wernher von Braun ambaye baadaye alihusika sana na NASA. Mataifa haya yalielewa kuwa teknolojia ya anga (space technology) ni sawa na teknolojia ya makombora (missile technology), hivyo aliyedhibiti anga ya juu angeweza pia kutawala kijeshi na kiitikadi duniani. Mwaka 1957, USSR ilizindua Sputnik 1, satellite ya kwanza ya bandia, na baadaye Sputnik 2 iliyomtuma Laika (mbwa wa kwanza kwenda angani). Mwaka 1959, Luna 2 ya USSR ilifika Mwezini, na mwaka 1961, Yuri Gagarin akawa binadamu wa kwanza kuzunguka Dunia akiwa ndani ya Vostok 1. Marekani ilijibu kwa kuanzisha NASA mwaka 1958, kisha Project Mercury iliyompeleka John Glenn kwenye orbit mwaka 1962, na kuendeleza Gemini Program kwa majaribio ya Kutembea mwezini (spacewalk na docking). Rais John F. Kennedy wa Marekani alitangaza mwaka huo huo kuwa Marekani ingefika Mwezini kabla ya kumalizika kwa miaka ya 1960, na hivyo kuanzisha Apollo Program. Ingawa kulikuwa na changamoto kama ajali ya Apollo 1, mafanikio yalifikiwa kupitia Apollo 8 (ya kwanza kuzunguka Mwezi) na Apollo 11 mwaka 1969 ambapo Neil Armstrong na Buzz Aldrin walikuwa wanadamu wa kwanza kutembea juu ya uso wa Mwezi. Hoja kubwa nataka tu kuonyesha namna Marekani ilivyozidi kupewa presha na Nchi za Mashariki ijapokuwa tayari ilikuwa juu.

Miongoni mwa vita zingine za siri sana ambazo Marekani alishindana na Urusi, ambayo tutaiona zaidi, na unaweza isoma kupitia kitabu cha Robert O Becker, mwanasayansi aliyeheshimiwa kwa kushirikishwa katika tuzo mbili kubwa zaidi duniani ‘’Nominated for Nobel prize’’, kitabu cha ‘’Body electric’’, ni kuwa, Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Urusi ilianza kufanya utafiti wa kina kuhusu jinsi ya kutumia miale ya umeme na mawimbi ya sumaku (electromagnetic waves) kudhibiti akili ya binadamu. Waligundua kuwa kwa kutumia mawimbi ya ELF (extremely low frequency), microwaves, na nguvu za kielektroniki za mwili (bioelectricity), waliweza kuathiri hisia, usingizi, tabia ya kuwehuka, na hata uwezo wa kufikiria wa binadamu. Teknolojia hii iliitwa psychotronics, na ikajumuisha hata majaribio ya kuwasiliana kwa njia ya telepathy au kusoma mawazo. Urusi pia ilihusishwa na matumizi ya teknolojia hizi katika upelelezi na usalama wa taifa, ikiwemo kupeleka mawimbi ya microwave ‘’Woodpecker frequencies’’ kwenye balozi za Marekani ili kuathiri afya na utendaji wa wafanyakazi wa kibalozi. Kwa miaka hiyo ya 1950 hadi 1980, walikuwa mbele kwa hatua nyingi katika uelewa wa jinsi umeme wa mwili wa binadamu unavyofanya kazi, wakiona hilo kama silaha mpya ya vita baridi.Marekani ilipogundua kuwa ipo nyuma kwenye uwanja huo wa vita vya kisaikolojia, ilianza haraka miradi ya siri ya kijeshi kama vile matumizi ya dawa, hypnosis, na baadaye wakahamia kwenye kutumia mawimbi ya umeme na sumaku.

Walianza kufanya majaribio ya kisayansi jinsi ya kutumia mionzi isiyo unguza kudhibiti tabia, kuathiri hali ya mtu, au hata kuwasiliana moja kwa moja na ubongo bila kutumia sauti. Kwa hatua hii, Marekani iliamua kujenga kituo maalum cha teknolojia ya hali ya juu kilichoitwa HAARP (High-Frequency Active Auroral Research Program), hii unaweza isoma katika kitabu cha Nick Begich, kinachoitwa ‘’Angels don’t play this HAARP’’, hiki kilikuwa kituo ambacho kilikuwa na uwezo wa kutuma mawimbi ya nguvu ya redio kwenye tabaka la juu la anga (ionosphere), na kuyarejesha mawimbi ya ELF ardhini, ambayo yalikuwa na uwezo wa kuathiri mifumo ya kisaikolojia ya binadamu na mazingira. Japokuwa HAARP ilielezewa kwa umma kama kituo cha utafiti wa hali ya hewa na mawasiliano, ilibeba uwezo wa kijeshi wa hali ya juu wa kudhibiti akili za watu kwa mbali, kuvuruga hali ya hewa, au hata kuathiri mzunguko wa mifumo ya kijamii au kisiasa.Hivyo basi, vita vya kimyakimya kati ya Urusi na Marekani vilivuka mipaka ya silaha za kawaida na kuingia kwenye uwanja wa ushawishi wa akili kwa njia za kisayansi. Urusi ilianza kwa nguvu na kufanya mafanikio makubwa katika kuelewa jinsi ya kutumia bioelectricity kudhibiti tabia ya binadamu, lakini Marekani ilikimbiza kwa kasi zaidi, ikajenga miundombinu imara ya kiteknolojia kama HAARP ambayo ilifanya iwe na uwezo mkubwa wa kisayansi, kijeshi na kiusalama duniani. Vita vya baridi havikuishia kwenye roketi na silaha za nyuklia pekee — vilifika hadi kwenye msingi wa fahamu na ufahamu wa mwanadamu. Na hapa msomaji unapaswa kuwa makini zaidi.

Kama ambavyo ni rahisi sana kumtawala mtoto wako anayekuwa mikononi mwako, changamoto hii ya kwanza ya marekani ya Ukuaji mkubwa na wa fasta sana wa Dola za mashariki uliweza kuumudu kwa kutumia mbinu kuu zifuatazo, kwanza iliwatenganisha ‘’divide’’ kwa kuwatengenezea matabaka, na hili unaweza liona kwa namna hukubaliana na kupingana na dola kadhaa za kiarabu. Pia marekani ilitengeneza mfumo wa kuwasapoti, ikilenga kuwa na maslahi ya milele kwa dola zote zinazokua, na kuwapatia masharti ya kibiashara, ambayo yatawanyima faida nchi za washindani wao. Huu mtazamo unasapotiwa pia na mchambuzi wa kimataifa wa kisiasa na maendeleo ya Kiuchumi, Professa Jeffrey Sachs wa Chuo cha Columbia aliyefanya kazi sana Umoja wa Ulaya ‘’EU’’, shirika la benki la Dunia ‘’WB’’, ‘’IMF’’, na Umoja wa Mataifa katika mkakati wa malengo ya maendeleo ya Ujumla ‘’UN’’. Jeffrey Sachs anaeleza kuwa Marekani imeendesha mikakati ya muda mrefu katika Mashariki ya Kati kwa lengo la kulinda nafasi yake ya udhibiti wa dunia, hasa kupitia ushawishi wa mafuta na usalama wa kijiografia. Marekani ndiyo iliyoanzisha taifa la Israel kama sehemu ya mkakati wake wa kisiasa na kiusalama, kwa lengo la kupata chombo cha kisiasa na kijeshi cha kudhibiti eneo hilo. na pia kama silaha ya propaganda dhidi ya mataifa ya Kiarabu na Umoja wa Kisovieti wakati wa Vita Baridi. Kwa kushirikiana na washirika wake wa Kiarabu kama Saudi Arabia, Misri, Jordan, na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Marekani imekuwa ikihamasisha migogoro ya ndani na ya kikanda, ikiwemo kuhamasisha vikundi vya kigaidi na vikundi vinavyopingana ili kuweza kuwagawa mataifa hayo na kuimarisha udhibiti wake kwa sera ya “divide and rule” (gawanya na utawale). Mpango huu unahusisha pia ushawishi wa kijeshi na kiusalama kwa njia ya NATO, ambapo Marekani imeweka nguvukazi katika maeneo muhimu kama Ghuba ya Uajemi na njia za mafuta ili kulinda maslahi yake ya kiuchumi na kisiasa, pamoja na kuingilia vita vya kuondoa au kudhoofisha serikali zinazompa wakati mgumu kama ilivyokuwa Iraq, Libya, na Syria.

Kwa upande wa sera zake za kijeshi na kisiasa, Marekani imeanzisha na kuendeleza mikakati ya “regime change” kwa nia ya kuweka serikali rafiki zinazotekeleza maslahi ya Magharibi. Kupitia CIA na msaada wa kijeshi, Marekani imeweza kuingilia siasa za nchi mbalimbali za Kiarabu, ikihamasisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na mabadiliko ya serikali kwa lengo la kudhibiti ushawishi wa kibeberu na kiuchumi. Israel, iliyoundwa kwa msaada wa Marekani kama sehemu ya mkakati huu, inaendelea kuwa mshirika mkuu wa Marekani katika kuhakikisha usalama wake dhidi ya maadui wake wa jadi kama Iran na makundi ya wapinzani wa Palestina. Mikakati hii ya Marekani imesababisha mgawanyiko mkubwa wa kisiasa, uchumi hafifu, na mizozo ya kijamii katika eneo la Mashariki ya Kati, huku wakazi wake wakikumbwa na vita, ukosefu wa maendeleo, na hasira kali dhidi ya uingiliaji wa kigeni. Mataifa ya NATO pia yameathirika kwa ushawishi huu wa muda mrefu wa Marekani.

Je! Marekani Imefanikiwa kutawala Mashariki?

Hii ni siri ya 2 tu inayoelezea tena changamoto ya kwanza tu ya Marekani ya kutetea utawala wake dhidi ya Nchi za magharibi, ambapo mpaka mwaka 1991 kipindi Russia inagawanyika tena toka dola ya Ukomunisti, tayari Marekani ilishaonyesha ubabe wake mkubwa sana, huku ikifanikiwa kuangusha dola zote za kiarabu zilizotaka kukua kwa kuwaua viongozi wake, na pia kuchochea migogoro isiyoisha mashariki yote. hii ni hatua ya mwanzo hebu tuangalie zaidi siri inayofuata.

..To be continued..