Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

ULEVI WA MADHABAHU

Uraibu wa Madhabahu

ULEVI WA MADHABAHU

Sayansi ya Uraibu wa Kuzungumza 

Unaikumbuka siku ya kwanza kuongea katika umati wa watu? Maranyingi hisia za Hofu hutawala sana. Wengi huogopa Kwa kuhisi aibu, kuwaza wataonekanaje iwapo hoja zao zitaonekana dhaifu. Asilimia kubwa huamua kuishia tu kukaa kimya. Uhalisia hubadilika ghafla baada ya kuanza kuongea. Hoja inapopokelewa vibaya Kwa kukosolewa, kupuuzwa, au kuchekwa huwa-Fanya wazungumzaji kujisikia vibaya sana hata Saikolojia zao kubadilika kabisa. Wengine hupoteza kujiamini milele, wengine huwa wakatishaji Tamaa zaidi Kwa wazungumzaji wengine wajao. Wengine hupambana ili kuja kuwathibitisha wakosoaji wao kuwa walikosea. Lakini uhalisia huwa watofauti kabisa pale hoja zinapopokelewa vizuri. Wazungumzaji hujisikia Raha ambayo kamwe hawakuwai jisikia, huwa na motisha zaidi, na wengi wao safari ya uzungumzaji huanzia hapo.

Kwanini Kuna Raha ya Kuhutubia Umati

Umewahi jiuliza kwanini watu wengi huota ndoto siku Moja wakihutubia umati mkubwa wa watu? Unahisi kwanini watu wengi hupenda kuwa wazungumzaji katika makutano makubwa ya watu, je hayo ni mafanikio yaliyolenga mtazamo upi, Uchumi, Saikolojia, au siasa? 

Ukweli ni kuwa, hakuna jambo lenye Thamani katika maisha ya mtu zaidi ya kuutumia Uhuru wake wa kuamua kuelekeza Umakini wake "Attention'. Mtu mmoja anaweza sema gari Lina Thamani sana, au ghorofa kubwa ni ndoto yake kuu kulimiliki, lakini kama Mwanadamu mmoja ataamua kutoona Thamani juu ya vitu hivyo, bado atavipuuza kana kama ni uchafu tu. Binadamu Kwa kujua Thamani ya huu Uhuru wa mtu kibiolojia husukumwa kufanya vitu vyenye Kuvuta tu Umakini wa watu. Na hii Ndiyo sababu ya Nguo zote nzuri, Vyakula vyote vizuri, vitu vyote vizuri vilivyopo sokoni au mitandaoni, vimelenga tu kuuvuta Uhuru wako wa Umakini. 

Katika Sayansi ya Ubongo inafahamika kuwa uelekeo wa macho wa mtu ndiyo Taa Pekee ya kukuonesha unaelekea wapi Uhuru huu wa Umakini wa Mwanadamu. Kitu unachokiangalia ndicho kinadhihirisha kipi ulichokiona Cha Thamani. Unaweza elewa hili kupitia mfano wa Mtaalamu wa Ubongo "Louann Brizendine' aliyeandika, 'Wanaume wengi huangalia maumbile ya wanawake ya uzazi Kwa kuwa kwao sex huwa na Thamani sana kibiolojia. Hoja ya muhimu ni hii, Mwanadamu anayetazamwa na watu wengi maana yake idadi kubwa ya wanadamu wamekubali kuona Thamani yake hata wakatumia Uhuru wao wa Umakini kumtazama. Kisaikolojia hili humfanya Mwanadamu anayetazamwa kupata motisha kubwa sana.

Msingi wa hisia za kutamani kuwa mbele ya umati wa watu Hauna tofauti na msingi wa hisia za wanawake kutamani kutazamwa hata Kwa kuvaa Nguo za nusu utupu. Kwa kuwa kadri mtu anavyotazamwa ndivyo anavyopata motisha zaidi kupitia kuzalishwa Kwa homoni za Raha "dopamine' katika Ubongo, watu wote wanaotazamwa sana baada ya muda hupata uraibu wa kutamani kuendelea kuwa katika umati wa watu.

Msingi wa Uraibu wa Kutazamwa

Miongoni mwa hoja zenye msisimko sana katika biolojia ya asili ni kwanini Kiini Cha macho ya Binadamu kiwe cheusi, na kuzungukwa na rangi nyeupe. Kwanini kisingekuwa Cha kahawia au kikazungukwa na rangi nyeusi kama Kwa viumbe wenginewe wengi. Binadamu ana rangi nyeupe kuzunguka nyeusi ili kufanya awe na uwezo mkubwa sana wa kutazama Kwa Umakini kuona mwonekano wa sura ya kitu Kwa kina. Binadamu ana uwezo mkubwa sana wa kuzisoma sura. kipindi binadamu anatazama hutazama zaidi sura akilenga macho. Mahitaji makuu yote matatu ya uhai yamejikita katika macho, yaani kutazama Chakula kilicho tayari kuliwa, kutazama mwenza aliye tayari Kwa uzazi, na kutazama hatari na kujikinga. 

Macho ni zaidi ya mlango wa kutazama ili kuona, macho ni mlango wa kuungana kihisia' na kiroho. Macho hubeba Siri ya Nini kilicho ndani ya akili au Moyo wa mtu. Mfumo wa kuungana kupitia kuona huwa Moja Kwa Moja katika Ubongo wa mbele "Mirror neuron system". Kadri unavyotazamana na watu wengi unazidi kuunganishwa kiakili na jumuiya inayokutazama. Hii huwa-Fanya watu waliozoea kuwa katika umati wa watu kupata Wakati mgumu sana wanapokuwa wenyewe.

Unapotazamwa na watu wengi Kwa mara ya Kwanza huwa unakuwa na Hofu sana na mashaka. Hii hutokana na kupatwa na hisia ya Hofu ya kugunduliwa udhaifu wako. Watu wengi ambao huenda katika umma wa watu hujali sana kuhusu mwonekano wao wa mavazi, mpaka mwonekano wa sura zao. Hata baada ya tukio watazamwaji huendelea kuwaza namna walivyotafsiriwa na watazamaji wao kupitia mwonekano wao, au matendo waliyoyatenda wakitazamwa. Hapa Ndipo huzaliwa uraibu wa Kutazamwa. Kwa kuwa Binadamu Kwa asili huwa wakosoaji zaidi wa wanachokiona kabla ya kukubaliana nacho kama watagundua ni Cha kipekee, marazote watu Wanapokuwa mbele ya umati wa watu huwa na hisia za Hofu ya kukosolewa. Ili kuweza kuendelea kudumu katika Presha hii ya kusimama mbele ya wakosoaji, Ubongo Huchochea sana motisha Kwa kuzalisha "dopamine na endorphins", hii husaidia kushusha kupaniki ambako kungetokana na "adrenaline'. 

Kadri dopamine na endorphins zinavyomfanya mzungumzaji kujiamini sana, basi huzidi kuweza kutawala hisia zake za Hofu "sympathetic pressure". Ubongo huzalisha zaidi dopamine watazamaji wanapoonesha mwitikio mzuri wa hoja, mfano Kwa kuongeza Umakini, kuonyesha furaha, au kuonyesha kukubaliana. Ubongo huanza kujidanganya kupitia huu msisimko kuwa mtazamwa ana upekee sana, ubora sana, kipaji sana, au hata mvuto sana, hoja ambayo Haina ukweli. Watu wengi hutazama kinachoonekana zaidi, zaidi ya kilicho Bora zaidi. Mtazamwaji anapotoka katika mazingira ya kutazamwa huisi upungufu sana wa motisha, sawa na mlevi anapokuwa mbali na pombe. Hii humfanya kuanza kuwaza Tena namna gani anaweza itumia ili aweze Tena kupata nafasi ya kuwa kwenye umati wa watu.

Watazamwaji huanza kushuka "IQ'

Kila mtu anayetazamwa sana, au anayepaswa kuzungumza Kwa Kila ndani ya Wakati mfupi, Hupungukiwa uwezo wa kufikiria "Thinking Capacity'. Hii ni Kwa kuwa, Msingi wa Akili ni uwezo wa kuwa mwenyewe "introversion', kupata motisha zaidi kupitia kujijibu maswali binafsi kuliko kujibu maswali ya watu, na kutofanya vitu Kwa madhumuni ya kupokelewa na jamii kubwa ya watu ambayo tayari wengi huwa na uwezo mdogo wa kufikiria.

Watazamwaji kupitia motisha kubwa ya 'dopamine, na endorphins" wanapozungumza, Ubongo wao huwa katika mawimbi ya kasi sana 'beta waves" ili kuendana na spidi ya midomo yao ya kuzungumza. Hii huwa-Fanya kuwa kihisia' zaidi Kwa kuwa kufikiria huenda katika kasi ndogo sana ya Ubongo, ambayo huitaji Utulivu sana na kutokuwa na hisia ili kutoshindwa kuchambua hoja Kwa kina. 

Dakika 2 zinatosha kujua IQ ndogo ya mzungumzaji 

Huwa akizungumza ili kupata motisha zaidi kupitia mazungumzo yake. Hoja zake huwa ndefu zikiongezeka zaidi muda unavyosonga. Kadri anavyozungumza Ubongo wake Kwa kuwa huwa haupo katika fikra zaidi, upo kihisia' zaidi, huzungumza hoja rahisi zinazofahamika lakini Kwa ujasiri sana, na huku akizikazia sana ili kupata Umakini wa wasikilizaji au watazamaji wake. Wazungumzaji huweza kutumia mara tatu zaidi ya muda waliopanga kuutumia kuzungumza Kwa kuwa hupoteza ramani ya mazungumzo yao. Kwa kuwa IQ yao huwa ndogo, hujadili hoja nyepesi na kutumia muda mwingi kuzielezea kama ambavyo uwezo wao mdogo wa kuelewa huitaji muda mwingi zaidi kuzinyambua.

Watumishi wa Umma na Ulevi wa Mazungumzo

Hasa Kwa Afrika, taasisi za Umma, taasisi za Dini, na hata mihadhara ya umma, mingi huisha bila kuwa na mafanikio Kwa kuwa nyakati nyingi za mikutano yao huishia Kwa mazungumzo ya walevi wa dopamine na endorphins wenye IQ ndogo sana wanapozungumza. 

Kwanini kuzungumza ni Ulevi?

Kadri unavyozungumza Ubongo hutoka katika mfumo wake wa hisia za changamoto 'limbic system-"anxiety, depression, stress" , na kuingia katika chaneli za kuzungumza ambazo hulenga Kuufungua zaidi mwili ili uweze kujiachia. Hiki kitendo huufanya mwili kushusha mzigo wa stress toka "Sympathetic state mpaka "Parasympathetic relaxing state". Mzungumzaji marazote hujisikia Raha Kwa kuwa mishipa yake hutanuka ili kuruhusu hewa na damu zaidi, huhema Kwa kutoa hewa zaidi na Kuvuta hewa ndani katika vituo vya mazungumzo yake. Hali hii ya "PSNS' ndiyo hufanya watu wanapozungumza kuweza kulia, kutoa machozi, kuonyesha hisia zao, na hata kufichua udhaifu wao sawa kabisa na walevi wa pombe.

Kibiolojia sauti hutoka kama namna ya kujilinda, au kuhitaji, kuliko hata kama namna ya kuhitaji mawasiliano ya mara Kwa mara. Sauti kibiolojia ni mfumo wa mwili kutetea udhaifu wake, na ndiyo maana wanyama wengi hawazungumzi maneno, lakini hulia mara tu baada ya maumivu, au wanapokuwa wahitaji wa kitu walichokikosa. Wanawake na watoto wengi huzungumza zaidi Wenda Kwa kuwa huwa wahitaji zaidi. Huwezi tenganisha kuzungumza sana na kuwa kihisia sana. Watu wengi wenye akili nyingi huwa Sio wazungumzaji sana, na hutumia muda mfupi sana kuzungumza.

Usanii wa maneno na Mvuto wa Mazungumzo 

Watu wengi hushindwa kuelewa hoja kuwa, kama uzungumzaji Hauna uhusiano na uwezo mkubwa wa kiakili, Kwanini miongoni mwa watu mashuhuri sana Duniani ni wazungumzaji baadhi, aidha wasanii baadhi, au Viongozi baadhi, au hata wanasayansi baadhi. Ukweli ni kuwa, uwezo wa kufikiria hoja Wakati wa kuzungumza ni kipaji Cha watu wachache sana. Wengi wa wazungumzaji mashuhuri kama Mwanasaikolojia "Jordan Peterson', Mchungaji "Myles Munroe', Martin Luther king Jr, Mwanafizikia 'Richard Feynman, Mtaalamu wa Ubongo 'Jack kruse", Msanii kama " Tupac Shakur, Waigizaji kama Steven Kanumba, na wenginewe wengi. Watu Hawa historia za maisha yao huonyesha kuwa walikuwa ni watu wakutafakari sana maisha yao. 

Wengi huwa wazungumzaji lakini Wenda ni asilimia 1% tu ya maisha yao huitumia katika kuzungumza. Huwa ni watu wa kufikiria sana, kusoma sana, kuwaza sana, na Ubongo wao hutanuka sana kiufahamu. Mazungumzo yao ni sehemu ndogo sana ya maisha yao ya ukimya. Watu huvutiwa sana Kwa hoja zao lakini husahau kuwa watu hawa hutamani kuibadilisha Dunia kupitia Maarifa yao Kwa midomo yao, Sio kwamba hutamani kubadilishwa na Dunia kupitia midomo yao. Hawa ni watu kamili Sio walevi wa Mazungumzo.

Siri ya Akili kupitia kukaa kimya

Wayahudi hufahamika Kwa uwezo wao mkubwa wa kiakili, lakini hakuna ambaye hujiuliza kwanini wengi wao huwa hivyo. Sio wayahudi tu, watu wengi wenye akili nyingi huwa si wazungumzaji sana. Akili Sio Mizizi ambayo Kila mmea huzaliwa nayo, akili ni matunda mazuri ambayo Mimea baadhi tu hufanikiwa kuwa nayo makubwa zaidi. Akili hutengenezwa kupitia safari ndefu ya maswali mengi yanayotafuta majibu, hoja nyingi zinazosikilizwa zaidi ya kuzungumzwa, nyakati nyingi za ukimya katika kutafakari majibu, na hatimaye Ubongo huanza kutengeneza tafsiri mpya "patterns' baada ya miaka mingi ya kupambana kuunganisha doti.

Wayahudi huwa na maktaba, au Maabara ambazo watoto hushinda ndani wakisoma na kufuatilia kazi za wazazi wao. Wengi wa wayahudi huishi katika Nchi za ugenini hivyo huwa Sio watu wakijamii sana, wengi wao huwa na nyakati nyingi zaidi wakiwa wenyewe wakijenga mapenzi zaidi katika taaluma zao, kuliko wenzao ambao hujenga mapenzi zaidi katika jumuiya zao wakipiga soga na kujadili hoja za juujuu za kuwaburudisha. 

Mwenye akili nyingi huzoea kuelewa Kila maana ya taarifa iliyo mbele yake, na hivyo hujali sana taarifa anayoitoa. Wenye akili hushindwa kuendana na jamii za watu wengi ambao maneno yao huwa kama maboksi ya hewa, mepesi yasiyo na maana za msingi. Wazungumzaji wengi wanapoulizwa maswali ya kujaribiwa usahihi wa hoja zao, hutumia maneno mengi sana, na hisia nyingi kumpinga Mtoa hoja kuliko hata kuijibu. Hii huanza kutengeneza matabaka kati ya wenye akili na wazungumzaji. Wenye akili hupenda sana kusoma, au kuwafuatilia wenye akili wenzao ambao huwaburudisha Kwa namna yao ya utazamaji wa mambo. Takwimu zinaonyesha uwezo wa kuzingatia wa watu wengi umefikia mpaka sekunde 10-30 tu, hii ni ishara kuwa watu wengi hawawezi kabisa kusoma na kufikiria.

Mfumuko wa Wazungumzaji wenye IQ ndogo katika Mamlaka

Inashangaza sana karibia taasisi zote kubwa za Umma, kuanzia taasisi za Dini, Elimu, Jumuiya, binafsi, na zaidi Siasa, nyingi zimejaa wazungumzaji wenye uwezo mdogo sana wa kufikiria. Swali huja, ni kwanini wengi wa Viongozi huwa na uwezo mdogo sana wa kufikiria? Jibu Pekee la swali hili ni kuwa; wengi wa Viongozi huchaguliwa au huteuliwa kutokana na sifa zao za Uzungumzaji. Siasa, Elimu, mpaka Dini, hulenga Viongozi ambao huwa ni wazungumzaji sana Kwa kuwa hawa, huwa na muda mwingi sana wa kuzungumza na watu, Tena huwa na mazungumzo ya kihisia' sana. Kwa kuwa wengi wao huwa na uwezo mdogo sana wa kufikiria, huwa na ujasiri sana wa kutoa hoja za kustaajabisha ambazo kisaikolojia huwasisimua sana watu hata wakajaribu kuwachagua. Kiongozi anaweza zungumza Kila siku bila hata kutumia siku Moja kukaa kujifunza. Kadri anavyozungumza ndivyo anavyotamani kuzungumza zaidi kutokana na uraibu wa "dopamine', hii humfanya kupambania zaidi nafasi za uongozi Kwa kuwa humpatia umati wa watu wengi zaidi wa kuwahutubia.

Viongozi wengi hugundua kuwa uwezo wao ni mdogo sana kuliko heshima wanazopatiwa Kwa nafasi zao. Hii huwa-Fanya kuwakataa watu wenye akili Kwa gharama zozote zile katika nafasi za uongozi ambazo wangeweza wapatia. Binadamu yupo haraka sana kugundua uwepo wa mtu aliyemzidi uwezo wa kufikiria, na Kila inapotokea Hali hii, Ubongo wa mgunduzi huwa hatiani sana Kwa aidha kukubaliana na ukweli, kujishusha, na kujifunza, au Kwa kuona mashaka, kuhisi udhaifu, na kuanza Vita za kihisia kama chuki, wivu, na fitina, au hata uzushi na mitego ya uharibifu, ili kumuangamiza mwenye akili na kujithibitishia usalama. Kwa kuwa wenye akili wengi tangia udogoni huzoea vita na changamoto za namna hii, wengi wao huzoelea kufanya vitu vyao wenyewe, nje na Taasisi, wengi wakiwa ni wagunduzi, huwa mbali kabisa na Taasisi kubwa za kijumuiya. Ni rahisi sana Kwa wenye akili kukubalika wanapofariki, au wanapokuwa wazee sana, hii ni Kwa kuwa huwa hawatishi Tena kama walipokuwa katika ujana wao.

Siri ya Ujasiri wa Wazungumzaji 

Miongoni mwa vitu vinavyowashangaza sana wanasaikolojia ni namna wazungumzaji wenye IQ ndogo, hujiamini sana mbele ya watu ambao nyakati kadhaa huwa na uwezo mkubwa sana wa kiakili kuliko hata wao. Kibiolojia hii Sio hoja ngumu, sababu kuu ni kuwa; wazungumzaji wengi kutokana na kuwa huwa kihisia' sana, wakiwa na motisha kubwa ya 'dopamine na endorphins", huku wakiwa na uwezo mkubwa sana wa kutuliza Presha ya paniki "adrenaline', wengi wao huwa katika mfumo wa hisia za motisha sana "Euphoria'. Hii huwa-Fanya kutoweza kufikiria vizuri wanapozungumza, wengi wao hushindwa kuwaza Nini wasikilizaji wao hufikiria, na kama ambavyo unapokuwa katika Hali nzuri husahau kabisa hata kama muda unaenda, watu Hawa pia huweza maliza muda mrefu sana wakizungumza hoja zao rahisi bila kujua.

Hofu marazote unapozungumza ni ishara ya Ubongo wako kuwaza kuhusu akili ya wasikilizaji. Siri ya mtu mwenye akili ni kuwaza anapofanya jambo lolote Lile, na hii Ndiyo sababu wenye akili si wepesi wa kukurupuka, kuzungumza, na hata kufanya matendo ya kihisia' kama sex. Mwenye akili huwa ni mwoga sana wa kukosolewa, na hii humfanya kukosoa sana hoja yake yeye mwenyewe akiifanyia utafiti hata kabla ya kuizungumza, na anapoizungumza, wasikilizaji hushangazwa sana Kwa kuwa huwa tayari ana majibu ya maswali ambayo wao hata huwa bado hawajaanza kujiuliza. 

Hoja nyingi sana za watu wenye akili huwa ni matokeo ya utafiti na uchunguzi uliofanywa miaka na miaka, na ajabu zaidi ni kuwa, huwasilishwa Kwa Wakati mfupi sana hata dakika zisizozidi 30 au Lisaa limoja. Hoja za wazungumzaji wengi wenye IQ ndogo huwa ni maoni, visa, au hoja zilizojengwa ndani ya muda mfupi sana, nyakati nyingine hata kipindi Cha mazungumzo yao, na hutumia muda mwingi sana kuziwasilisha, hata zaidi ya Lisaa na masaa.

Afrika na kushamiri Kwa watu wenye IQ ndogo 

Ijapokuwa wasomi wengi Waafrika hukataa kuwa Afrika haina watu wengi wenye IQ ndogo, lakini ukweli huu hufahamika Kwa karibia Waafrika wengi sana, hasa wakazi wasio wasomi wa Elimu za juu. Kama Sheria ya asili inayosema, " kitu chochote utakachokitumia kitakuwa Bora zaidi, na kinyume chake", Waafrika Sio watumiaji wakubwa sana wa Akili katika kuumba, na Wenda test za IQ kama zingepima ufanisi wa matumizi ya misuli na ufasaha wake, basi Afrika ingeongoza Kwa Hilo. Haimaanishi Kwa kuwa Waafrika hawakugundua maandishi, Pikipiki, au ndege, na kijiko, ndiyo sababu hawana IQ kubwa, Hapana! Ugunduzi una historia Pana sana, na Tena kama Misri ni Afrika basi wagunduzi wakwanza kabisa Wenda ni Waafrika. Hoja ni kuwa, Afrika haikuwa katika Bonde lenye dhiki za kuwafanya watu wafikirie ili kuishi, jiografia hii ilichochea jenetikia katika namna ya "Epijenetikia' kutengeneza Saikolojia ya Waafrika kutohisi wanahitaji Kujua na kufikiria Kwa kina ili waishi.

Ukiwa Msomi mdogo unaweza hisi Afrika ina wasomi wengi wenye akili nyingi Kwa kuwa wapo Wahandisi wa ndege na Rocket kutoka Afrika, wapo Wataalamu wakubwa Wamaroboti toka Afrika, Wapo Madaktari na wanasayansi wakubwa wanaotoka Afrika, lakini ukiendelea zaidi, utagundua wengi wao huwa Sio watu wenye akili nyingi sana, wengi wao huwa watu wenye aidha kumbukumbu kubwa sana, au Wenda taarifa nyingi sana. Asilimia kubwa sana siwezi kadiria ya Waafrika, uwezo wao wa kufikiria ni mdogo, na Wala hawajali kwanini wafikirie. Waafrika ni watu wa kihisia' sana, na hata muziki wa Afrika Duniani unafahamika Kwa kuchochea sana hisia. Waafrika ni Wabinafsi sana, Wana Biolojia ya ndani ya kujitegemea bila kuhitaji Chochote kile, Kwa yeyote yule. Nchi za Afrika zinaongoza Kwa makundi, na makabila mengi sana, Mwafrika Kwa wastani ameridhika katika Hali yake kama msemo unaosema, "Mpumbavu tayari analo jibu".

Toka nilipokuwa mdogo mpaka nahitimu masomo yangu ya Shahada ya Udaktari sijawahi ona katika jamii zangu, Afrika, watu wakijiuliza kwanini Dunia inazunguka jua, au kwanini tuna siku Saba za wiki, sijawahi ona mikutano ambayo watu wanaweza poteza dakika yao hata Moja kujiuliza Kwanini Ng'ombe ana manyoya na Binadamu hana. Waafrika wanachojali zaidi Leo atakula Nini, familia yake inaweza kuishi, na hata akienda kusali, hujali zaidi Mungu atamsaidiaje katika mahitaji yake, Sio kujua Mungu aliwezaje kuumba Dunia nzima Kwa siku sita. Watu Hawa wasiojali Kujua lolote ndiyo haohao Madaktari wengi ambao hata hawajui kwanini asilimia 90% ya Mfumo wao wa maisha Sio asili yao, Wauza madawa wasiojua asilimia 90% ya madawa yao hayakutumika Karne Moja tu nyuma, Wahandisi wasiojua asilimia 90% ya Teknolojia zao zinazidi kumwondoa Mwanadamu katika asili yake, hakuna anayejiuliza. Siku watakayojiuliza ni pale watakapogundua hakuna kitabu kilichoandikwa na Babu yao wanachokitumia shuleni.

Afrika imejaa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiria Sio Kwa kuzaliwa, ila kutokana na Laana ambazo kitaalamu ni udhaifu unaorithishwa vizazi na vizazi. Hata wanapoibuka watu wachache wenye uwezo mkubwa wa kiakili, idadi kubwa ya wazungumzaji wenye IQ ndogo ambao ndiyo wenye Nguvu kubwa zaidi kijumuiya huwamaliza na kuwapoteza, na kumbuka, hakuna mfumo wa kumbukumbu Afrika Kwa yeyote yule. Hii Ndiyo stori ya kwanini Afrika imeshamiri zaidi watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiria.

..