Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MASWALI YA GHARIKA, DINOSO, & MENGINEYO

Maswali juu ya Gharika na Dinoso

Maswali Yaulizwayo Sana Juu Ya Mijadala Ya Sayansi ya Gharika.

Usumaku Wa Dunia ‘’Earth’s Magnetic Field’’

Miongoni mwa mada zinazoleta changamoto kubwa Sana ni juu ya asili ya usumaku wa dunia. " Origin of earth's magnetic field". Katika sayari za miamba tatu tena zinazofanana yaani Venus, Dunia, na Mars, Hakuna usumaku katika sayari mbili zote zinazoizunguka dunia, lakini Kuna kiwango kikubwa Sana Cha usumaku kwa sayari ya Dunia. Usumaku huu unatokea wapi? Kwanza kabisa Hakuna ubishi kuwa dunia ilishakuwa na kiwango Cha usumaku toka awali, lakini siyo kikubwa Kama hiki Cha leo. ambacho ni Mara zaidi ya elfu mbili ya sayari zote za miamba zikijumlishwa. Majibu ya swali hili hutoka pande zote za nadharia, Kati ya nadharia ya mabadiliko, na nadharia ya Gharika.

Ukianza na nadharia ya mabadiliko, ambayo huitwa "Dynamo theory”. Hawa huamini kuwa, ndani ya dunia Kuna kiwango kikubwa Sana Cha magma inayozunguka. Magma hii kutokana na Nishati kubwa ya joto, imeweza kupelekea uwepo chaji zinazoweza pitisha umeme. Nishati hii pia huaminiwa kusababishwa na Nishati ya madini ya mionzi, ambayo huzalisha Nishati za nyuklia. Na kutokana na sababu hizo, hizi chaji zinazozunguka hutengeneza umeme ambao hupelekea kuzalishwa kwa usumaku, Kama ilivyo Kawaida kuwa usumaku husababishwa na chaji za umeme. nadharia hii ni nzuri kwa kuielezea, lakini imeshindwa kuwa na ushahidi. Hakuna magma zinazozunguka ndani ya dunia. haiwezi kuelezea kwanini usumaku wa dunia huwa ukibadilika badilika kulingana na maeneo, na hata muda. Haiwezi kuelezea kwanini vipimo vya Seismograph"vipimo vya kupima usumaku" huonesha kuwa, ndani ya dunia kabisa katika "Earth's core" Kuna kiwango kikubwa Sana Cha usumaku, ukilinganisha na kwa nje, na ili Hali ndani katika kiini Cha dunia, Hakuna magma inayozunguka?

Nadharia ya Gharika ya Nuhu inatoa majibu yote ambayo nadharia ya mabadiliko ya Dynamo imeshindwa. Kutokana na Gharika iliyopelekea uji uji mwingi wa miamba, kwa kipindi Cha mpasuko kuanzia maeneo ya ndani ya dunia. Mabadiliko Yale yalisababisha kiwango kikubwa Cha madini mazito, madini ya chuma, kutelemka na kujikusanya kwa pamoja. Hii ni kumaanisha kuwa, kabla ya Gharika, mgawanyo wa madini ya chuma ulikuwa Kama mithili ya mchanga uliochangamanika na sabuni ya unga na maharagwe, huwa ni mchangamano usio na mpangilio maalumu, na wala huwezi kupata kwa kiwango kikubwa sifa za kitu kimoja kimoja, kwa kuwa, huwa vimejichanganya hata visiwe na nguvu ya kimoja kimoja. 

Ila Sasa, chukulia picha hii, unapochanganya maji mengi Sana katika mchanganyiko huu, sabuni itayeyuka, maharagwe yataelea na mchanga utajikusanya na kushuka chini. Hivyo hivyo, Gharika ilipelekea madini mazito ya chuma kutelemka hata ndani kabisa ya dunia, na huko kulipelekea madini haya kujipanga hata kusababisha usumaku. Usumaku unatokana na kuwa, madini haya ya chuma huwa na chembechembe za sumaku zinazoitwa "magnetite" au Iron oxide. Kuna ushahidi mkubwa Sana wa uwepo wa madini haya ya magnetite, ambayo Yana kiwango kikubwa Sana Cha usumaku, kitendo Cha usumaku wa dunia kuwa mkubwa zaidi katika kiini Cha dunia, kinathibitisha kuwa kulikuwa na Gharika na madini mazito yalishuka chini.

kwanini usumaku hubadilika kulingana na maeneo"magnetic reversals"

Usumaku hubadilika kutokana na kiwango Cha Nishati iliyopo katika magma, yenye madini haya ya magnetite. Siku zote hufahamika kuwa, joto huathiri au kuua usumaku. na ndiyo maana, ukiichoma sumaku hupoteza usumaku wake, hii hutokana na kuwa joto hubadilisha mpangilio wa chembechembe ndogo zaidi za atomu, za chembe za usumaku. Hivyo Basi, kama maeneo mawili yenye magma, moja lingekuwa na joto Kali, na lingine la baridi. Basi hilo lililo la baridi, huwa na usumaku mkubwa zaidi kuliko eneo lililo la Moto. Na matokeo haya ukiyalinganisha na graph za magnetic reversals, Basi utaona moja kwa moja udhihirisho wa nadharia yetu.

kumbuka

Usumaku "magnetic fields" pamoja na kuwa na matokeo mengi Chanya katika maisha ya viumbe. Kama vile matokeo chanya juu ya ufanyaji kazi wa matendo ya kibiolojia ya ndani kabisa ya mwili, katika hatua za awali za maisha, husaidia ndege ambao hujua uelekeo kupitia mionzi ya usumaku n.k Hakuna ushahidi wa umuhimu wa kiwango kikubwa Sana Cha usumaku wa dunia katika kuwezesha maisha.

Pia sayari hizi zinazopakana na dunia, pamoja na kuwa na miamba. Hazina sehemu ya ndani yenye joto kama ilivyo dunia, na pia hazina maji kama ilivyo dunia. Sababu hizo zinatosha kuonesha nguvu ya gharika katika sayari ya dunia.

kipi chaweza kuwa chanzo cha kupungua urefu wa maisha baada ya gharika?

Kuna watu waliokuwa wakiamini katika nadharia ya ‘’canopy theory’’, yaani dunia ilizingirwa na tabaka la maji angani, nadharia hii tulishaiona kuwa ina makosa. na wala haipaswi kuaminiwa maana kwao sababu kubwa ni mionzi kutoka katika anga la juu la dunia, ‘’cosmic uv rays’’ ndiyo ilishusha urefu wa Maisha, baada ya mvua ya gharika kulimaliza tabaka hili. Hiyo siyo sababu ya kweli, kwanza hata mionzi peke yake haina Ushahidi wa nguvu ya kutosha ya kushusha miaka. na ndiyo maana, hata baada ya gharika kiwango cha mionzi ili hali kilikuwa kikiongezeka, lakini hakikuwa na nguvu ya kushusha Zaidi uhai, na mpaka leo karne ya viwanda, bado viwango vya urefu wa Maisha ni wastani wa miaka sabini ya dunia ya kale. 

Sababu kubwa ambayo tunaweza itazama ni athari katika mfumo wa mwanga, maji, na usumaku. Maani hizi ndizo nguzo kuu za uhai katika kiwango cha chini cha seli. Uhai wa kiumbe unategemea sana ubora wa chembechembe za nishati, kwa wanyama ‘’Mitochondria’’, na kwa mimea ni ‘’Chrolophyll’’. Kwa pamoja chembechembe hizi zinahitaji sana mfumo imara wa maji, ambayo pamoja na mwanga ndiyo hutengeneza chakula kupitia kwa mimea ‘’Photosynthesis’’, na kwa wanyama kupitia ‘’Electron transport chain’’. Baada ya gharika kiwango kikubwa cha maji kiliathiriwa hata kushamiri maji mazito ‘’Deuterium’’, ambazo hizi huifanya ATPase synthase katika Mitochondria ku ‘’run slow’’, na huo ndiyo mwanzo wa spidi ya maisha kushuka, kumbuka hata mgawanyo wa mabara uliwafanya wengine kuwa maeneo yanayopata mwanga kwa udhaifu zaidi, na takwimu zinaonyesha vifo huongezeka kadri unavyopungukiwa na vipindi toka kwenye mwanga wa jua. 

Kiwango cha Neutrons kilichoshamiri hata katika hewa ya Kaboni, kilifanya kaboni-14 ishamiri zaidi, na kupelekea mimea na viumbe wote walioivuta kutokuwa na ufanisi mkubwa zaidi wa metabolikia zao, maana uhai ni uhandisi wa kaboni katika chaneli kama za methionine cycle, folate, polyamine, urea, kreb’s cycle, threonine, n.k. Tofauti za mzunguko wa dunia, kupunguwa kwa jamii za mimea za chakula baada ya gharika, ambako kuliambatana na vita ya kutafuta mbadala kwa ulaji wa wanyama, pia kunaweza elezea mwanzo wa shida za upungufu wa madini, virutubisho, na uhitaji wa ugunduzi mfano wa teknolojia zilizomtoa zaidi mwanadamu kutoka katika asili na kuathiri zaidi uhai. Unaweza jifunza zaidi hili kwa kurejea sehemu ya tano ya kitabu cha Ubongo wa mtu mweusi.

Kumbuka kiwango cha kaboni-14, ambayo ilitengeneza wastani mkubwa baada ya gharika, kaboni-14 huwa na asili ya kuisha kimionzi ‘’radioactive decay’’. kama yalivyo madini mengine ya mionzi. Hivyo basi, uwepo wa kaboni -14 nyingi kwenye mimea, mpaka Wanyama, kaboni hii ambayo huenda kushughulika na kila molekuli ya uhai ya mwilini, kuanzia kwenye DNA mpaka tishu za Ngozi na mifupa, husababisha makosa madogo madogo katika ufanyaji kazi wa mwili, kupitia mabadiliko kama ‘’mutations’’ n.k sababu hizi na zinginezo kwa ujumla wake, zina nguvu kubwa sana ya kupunguza ufanisi wa kazi wa mwili na kuuzeesha.

Muhimu kuzingatia ni kuwa, kushamiri kwa Neutrons zilizopelekea madini mengi kuwa mazito, na hasa katika maji ‘’deuterium’’, na kupungukiwa mzunguko thabiti wa mwanga wa jua kwa masaa 12, na vipindi vya giza, kulichochea zaidi kushuka kwa uhai pamoja na sababu zingine za upungufu wa virutubisho, shida za hali za hewa, na gunduzi zilizomdhoofisha zaidi mwanadamu.

kwanini mungu aumbe maji chini ya dunia, akijua kuwa yatakuja kuunda bomu?

Kwanini Mungu aumbe mfumo wa jenetikia unaoweza fanya makosa ‘’mutations’’ ili hali anajua unaweza leta kifo na majanga ya afya? Maswali haya na mengineyo yote, yanapaswa kujibiwa baada ya kutambua kuwa, Mungu aliruhusu Kifo baada ya adamu kumkubalia nyoka ili hali aliambiwa ukila tunda hakika utakufa. Hivyo kauli ya Mungu ya hakika utakufa, ilitimia baada ya dhambi. Na ndiyo iliyopelekea kila Mungu alichokiumba kwa ajili ya uhai wa milele, kianze kuishiwa uwezo na kuharibika polepole. ni kama ambavyo adamu hakufa ghafla, naye alikufa baada ya muda wa miaka mia tisa 900+ na hata mutations hufanyika kidogo kidogo. 

Neema ya Mungu ndiyo pekee inayotoa muda wa mtu kurejea uhai wa milele tena, kwa kumpokea Yesu. na sio kujiaminisha katika Dunia ambayo hata usipomwamini Mungu haimaanishi kuwa utaondoa madhara ya mabadiliko ya nchi. Mfano, kuyeyuka kwa mabarafu makubwa, tsunami, volcano au matetemeko, magonjwa, uzee n.k, Mungu aliumba toka kwenye maji, na baada ya gharika dunia mpya ilianza tokea kwenye maji, na ndiyo maana mtu hubatizwa akizamishwa na kuibuliwa tokea kwenye maji. lakini hiki ni kielelezo tu kuwa, Kifo kiliruhusiwa kutimiza kauli ya Mungu mwenyewe, ndiyo maana, huwezi kikimbia. njia ni mbili utake ufe, usitake utakufa. 

Baadhi huuliza kwanini Aruhusu ilihali anajua ingeleta changamoto? 

Katika muktadha mpana hili swali lingekuwa rahisi kama tutaangalia huu mfano; kijana mmoja kwa kiburi chake amemtukana Boss wake, na bila kusikiliza ushauri wa kwanini asiondoke na gari kutoka kwa Boss wake, amechukua gari ya Ofisi na kuondoka nayo kwa hasira, asijue njia anayopitia ni Mbuga ya Simba, na Gari litaishia mafuta katikati ya safari, Sasa kijana huyu yupo anazingirwa na Simba na hana mbinu ya kutoka! Swali la kwanza anajiuliza, kama Boss ni mwema na alijua litamkuta hili kwanini alimuacha apande hili gari? Pili anajiuliza Kama Boss ana utajiri wa kutosha kwanini gari liishe mafuta?

Haya maswali yote ni magumu kwa mtu asiyetumia sheria za msingi za kufikiria ‘’primary level thinking’’. Kujua sio Kuamua, Boss alijua litampata janga ila hakumpangia hilo, na ndiyo maana Nuhu alihubiri kwa miaka 120 bila mtu mmoja kumzingatia wakimwona ni Kichaa. Swali la Pili ni ishara ya kiburi na dharau, ni kama lililoulizwa na mwizi msalabani ‘’Kama wewe kweli ni Mwana wa Mungu, jitoe na ututoe na sisi’’. Kila sekunde ya mwanadamu sio bahati, Mungu ameshikilia kani za asili zisimmalize mwanadamu, Gharika ni sehemu tu, umewahi jiuliza kuhusu kinachozuia sayari zisipoteze orbits tukagongana tukafa wote, hata tu Maji ya Baharini hakuna anayeweza elezea kwanini yapo pale tusipatwe na Tsunami, usipojua hili jepesi, huwezi kuelewa kwanini kuna Gravitation katika uso wa dunia, ni kipi chanzo? Mungu anatulinda na mengi zaidi ya hayo, halengi kutumaliza, ametupa neema ya siku chache katika ulimwengu huu ambao hata usipomuamini lazima utakufa, kutufanya tuzirekebishe njia zetu kwa kumwamini, ila kumbuka kuwa imeandikwa, ‘’kwanini uwe Mpumbavu hata kufa kabla ya siku zako”

kama mungu aliumba kila kitu, je yeye aliumbwa na nani?

Haya ni maswali ya kifalsafa, mara nyingi huwezi ya jibu kwasababu za kisayansi, Bali unaweza yajibu kwa sababu za kimaana. Maana ya kuamini kuna Mungu ni kuwa, kuna Kisicho na mwanzo na kinaumba mwanzo. Kama mtu akiuliza Mungu aliumbwa na nani? Namna nzuri ya kumsaidia mtu huyu ni kuliweka swali lake kama hivi, Je kuna uwezekano wa kitu kutokuwa na mwanzo? Na kisha umwelekeze kuwa, wanaoamini Mungu wote wanakubaliana kuwa yupo asiye na mwanzo, ambaye ndiye afanyaye mwanzo wa vyote. Sasa hawezi tena kuniangaisha kuniuliza mwanzo wa Mungu ni nani, maana atakuwa kama anauliza ipi ni namba nyuma ya infinity? Huo unaitwa wendawazimu.

Unaweza msaidia baada ya kumjibu swali lake kwa kumuonesha kuwa, hata yeye hajijui yupo kundi gani, maana wote wasioamini Mungu wanaamini pia sio kila kitu kina mwanzo. Mfano, space haina mwanzo, nishati haina mwanzo, sheria za asili hazina mwanzo, na hata hisabati haina mwanzo. Yaani, hata kabla ya dunia kuwepo, moja kujumlisha moja ilikuwa ni mbili. Kwa hiyo, hawa watu ni kama wanasema upo uwezo usio na mwanzo, ila sio Mungu, hii yote ni kukimbia sheria ya Mungu.

Mungu haumbwi, kuumbwa ni kuletwa katika mstari wa muda ‘’time dimension’’ na pia ni kuletwa katika uwepo ‘’space dimension’’ na mwisho ni kuumbwa maarifa sisi ni kama magari ndiyo maana, ukikata mshipa wa damu wa moyo usiungwe, utakufa. hiyo ni ‘’information intelligence’’. Mungu ndiye aliyeumba, basi hiyo ina maana kuwa, yeye yuko nje ya dimension hizi. Hayuko ndani ya muda, maana huwezi anzisha muda kama na wewe uko ndani ya muda, ndiyo maana yeye hujua kesho toka jana, yeye ni jana na leo au mwanzo na mwisho, niliandika awali. kama ukiishi miaka mia, utasema kuwa umekua sana, je na Mungu nae amekua? Jibu ni Hapana kwa kuwa, yeye ameshakamilika, yeye ni Mungu. Na nikasema kuwa, Mungu aliumba muda kwa ajili yetu sisi, kipimo cha kazi, na ukuaji wetu. Na binafsi namshukuru Albert Einstein kwa jambo moja tu kubwa zaidi, nalo ni kuonesha kuwa muda ni kitu kinachoweza pindishwa, na hii inadhihirisha zaidi uwezo wa Mungu wetu katika uumbaji wake, na pia nadharia ya relativity ya Einstein nayo inatanua ukubwa wa Mungu zaidi ya alipoishia Newton, bila hata kujali mitazamo binafsi ya wanasayansi husika.

Je naweza jaribu kisayansi uwepo wa Mungu, mfano kupitia vipimo

Biblia inazungumzia neno ‘’jaribu’’ katika pande mbili. Pande chanya Malaki 3:10 na hasi zaburi 95:9

Inaeleweka ninaposema kumjaribu katika namna mbili, hata wewe unaweza kubali kujaribiwa na mtu, ila katika hali chanya. ukitaka kumuona Mungu kisayansi unaweza kama ninavyofanya mimi, na wengine wengi. Ambapo tunashuhudia kila alichokisema katika asili zetu. Ila changamoto kubwa wengi hutaka kujaribu uwepo wa Mungu katika namna za kibinadamu. Hii ni kufanya kisio kuwa ‘’kama lilivyo jiwe linavyoruka, ndivyo malaika wanavyoruka’’, binadamu tumeathiriwa kuona vitu vikitendeka katika levo za juu kabisa za kueleweka kibinadamu. kama nyani wangekataa kuna utendaji wa akili Zaidi yao, kwa kuishi tu porini, na kutojua kuna binadamu, wangekuwa wanajidanganya sana kama binadamu tunavyojidanganya. 

Hakuna maabara duniani ya kufanya njia za kibinadamu za kumwona Malaika, wakati hata tu kuona magnetic fields hatuwezi, hatuwezi kueleza tu namna mchakato mzima wa uhai wetu wenyewe unavyoendelea, hakuna anayejua namna ubongo unachakata ufahamu ‘’consciousness’, hakuna anayejua hata nini hasa kinasukuma ulimwengu unaosambaa ‘’expanding universe’ n.k. hayo ni kadhaa tu ya maswali ambayo tulipaswa kuwa na majibu, na kisha tupande juu sasa kimtazamo. Lakini kutaka kumuona Mungu, au mbingu, kwa macho, na Galaxy tu alizoziumba tunaziona tu kwa mbali, au hewa tu aliyoiumba tunahitaji microscope, nahisi kosa kubwa sana ni kutokuwa makini na udhaifu wako, kipindi unataka kuchukua hatua kubwa Zaidi.  

je wanyama aina za dinoso waliishi miaka milioni 245 mpaka 66 huko nyuma? je wanathibitisha mabadiliko ya viumbe kwa kutokuwepo siku hizi? 

Dinasaurs ni Wanyama ambao mifupa ya mabaki yao mingi sana imepatikana, tena sehemu tofauti tofauti. Dinoso hawakuishi miaka milioni 200 huko nyuma, na wala hakuna Ushahidi. kwa maana maeneo ambayo mabaki haya yanapatikana, pia hupatikana na mabaki ya viumbe wengine. namna mabaki haya yamehifadhiwa ni moja kwa moja sawa na kila tulichokiona kilichofanywa na maji katika utengenezaji wa mabaki ya Wanyama ‘’fossils’’, rejea picha chini.



Picha inaonesha mabaki ya nyayo za binadamu zikiwa chini, na kisha dinoso akija kukanyaga kwa juu, hii ni kumaanisha Wanyama walikuwa wakikimbia gharika. na hata picha ya kulia pia unaona kwato nyingi za dinoso, hii tayari inaweza kumfanya mtu atambue kuwa, hakuna utofauti wa miaka milioni 60 Kati ya binadamu na dinoso, wote waliishi katika kipindi cha zama moja. Dinoso wangeweza patikana chini kidogo katika ufukiwaji kutokana na uzito wake, lakini sio kwa kiwango chochote chenye maana ya kuleta mtazamo wa matabaka yaliyotengana kizama zilizopishana.

Maswali Kadhaa Kuhusu Dinoso

je dinoso wangewezaje kukaa katika safina ndogo kama ya nuhu?

Nuhu asingechukua dinoso wakubwa kama huyu anaeoneshwa kwenye hii picha. Angechukua tu dinoso wadogo au Watoto.

Je dinoso wangewezaje kuishi na binadamu? wasingeweza maliza binadamu wote?

Kwanza utawala wa binadamu hautokani na ukubwa wake, maana hata Tembo ni wakubwa sana ukilinganisha na binadamu. lakini bado binadamu hutawala. Pili kwasisi wataalamu wa Wanyama tunatambua kuwa, kadri mnyama anavyokuwa mkubwa sana, ndivyo anavyozidi kuwa na dalili za kuwa mla majani ‘’herbivores’’, hii ni kutokana na kuwa, Wanyama hawa wakubwa huwa hawana sifa nyingi za uwindaji kama kujificha, kukimbia, na kupata idadi kubwa ya Wanyama wa kuwala mpaka akatosheka. Na kwa mantiki hii, kuna uwezekano mkubwa Zaidi wa kuwa, Dinoso wote wakubwa walikuwa ni wala majani.

Kama dinoso waliishi na binadamu. wako wapi leo?

Wana historia kadhaa huamini kuwa, dinoso ambalo ni jina la kiingereza lililoanza kutumika miaka ya 1800’s. halikurekodiwa kutumika kuzungumzia visa vya dinoso, ila yapo majina mengi sana kutoka jamii mbalimbali ambayo yalitumika kumaanisha mnyama huyu. Kama vile ‘’Dragon’’ jina hili limetumiwa sana hasa maeneo ya china, hasa kwa visa vya mashujaa walioweza kumuua mnyama huyu hatari, ipo michoro mingi sana ya awali ambayo ilikuwa na picha ya dinoso. Na inavyoonekana mnyama dinoso, alikuwa ni mnyama hatari, na alikuwa anatishia jamii. na kulikuwa kuna sera kubwa za kushindana na jamii za Wanyama hawa, kama ambavyo jamii za zamani zilikuwa zikijikinga na Wanyama kama simba. 

Kutokana na uhalisia kuwa hata hali ya dunia baada ya gharika haikuwa yenye kusapoti sana Maisha ya Wanyama wakubwa, kama wale ambao huitaji maeneo yenye vyakula vingi na maji na hewa. Basi hata uzalianaji wao ukapungua. Lakini una kila sababu ya kuamini idadi ya visa vingi vinavyoelezea watu waliokutana na dinoso, hata miaka hii, wengi wao huzuiwa kabisa kutoa taarifa. Wapo walio na visa vya kushambuliwa kabisa, namrejea mwandishi pia wa kitabu cha ‘’Champ’’ ambae anahakikishia jamii kukutana na mnyama huyu, ambaye alimshambulia na kumuua mume wake, hata akafa, naye alipona kwa shida. Pia vipo visa kwa maeneo ya kongo, ambapo wananchi kadhaa wanakiri kukutana na Wanyama hawa wa dinoso.



Unaweza fatilia taarifa hizi na nyingine nyingi. Msomi wa kweli huwa hakubaliani na taarifa za upande mmoja, na kupuuza shuhuda zikisha kuwa nyingi kutoka kwa watu. Uwepo wa dinoso mpaka leo, kama utathibitishwa utaharibu kila msingi wa biolojia ambayo haianzi na Mungu, kwa kuwa huo ndiyo utakuwa mwisho wa mwisho wa nadharia ya mabadiliko. kama ilivyokuwa walipogunduliwa samaki aina ya coelacanth, ambao waliaminiwa kuwa walikwisha potea miaka mingi huko zamani

Je Ni Kweli Kuna Mabadiliko Ya Hali Ya Nchi ‘’Ongezeko La Joto Duniani’’? Na Ni Kweli Binadamu Ndie Chanzo?

Swali la kwanza Jibu ni kweli, kuna ongezeko la joto duniani ‘’global warming’’. Na hii ndiyo sababu pia ya kuongezeka wa uyeyukaji wa barafu, iliyo katika mabara ya Antarctic, Greenland, na sehemu zingine. Pia kitendo cha kuongezeka kwa joto, kuna pelekea kiwango kikubwa Zaidi cha hewa ya kaboni dioksaidi, kutoka katika maji na kuingia katika anga.

Swalli la pili jibu ni hapana. Kiwango cha kaboni dioksaidi ambayo binadamu anaizalisha, ukijumlisha na shughuli zote toka mapinduzi ya viwanda, ina mchango mdogo sana katika kiwango cha kaboni dioksaidi inayozalishwa duniani. Kwanza, binadamu hasababishi uyeyukaji wa barafu katika mabara, na hata kabla ya miaka ya 1800, tayari dunia ilikuwa ikipitia zama za barafu. na zama za barafu zilianza baada ya gharika. Binadamu hana uwezo wa kuongeza au kuzuia chochote kadri barafu linavyozidi kuyeyuka.

Makosa makubwa sana ni kuamini kuwa, hewa ya kaboni dioksaidi ndiyo inayosababisha ongezeko la joto ‘’global warming’’ badala ya kuamini kuwa, kiwango cha joto ndicho kinachopelekea ongezeko la kaboni dioksaidi. Kosa lingine ni kuamini kuwa, hewa ya kaboni dioksaidi huwa mara zote ina madhara, bila kutambua kuwa, pia huboresha uoto wa asili kwa kuhamasisha ukuaji wa mimea. Kosa la tatu ni kuamini kuwa, zama za sasa kuna mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi, ukasahau kuwa dunia iko katika kipindi cha kutulia kidogo ukilinganisha na zama za awali, ambapo, kulikuwa na kiwango kikubwa cha matetemeko, volcano, kupasuka kwa mabara, zama za barafu, zama za joto, kuanguka kwa vimondo n.k.

Uwepo wa taarifa za aina moja duniani siku zote huaribu ubora wa taarifa, ni vema watu wakawa na taarifa tokea pande zote, hata kama zinakinzana. Wapo wengi wanaotoa taarifa kuhusu hali ya sasa ya dunia, ilivyo bora hata kwa kamera za satalaiti zilizo juu angani. jamii nyingi zimekuwa zikipitia changamoto za hali za hewa, lakini katika namna zilizozoeleka, na wakati mwingine, hata hali bora Zaidi ya zilizopita. Lakini watu siku zote hung’ang’ania kuegemea upande mbaya wa mabadiliko.

Dunia ina namna nyingi sana za kukabiliana na mabadiliko ya hali za hewa, tena yenyewe. na ndiyo maana, mfano siku za baridi au maeneo yaliyo na baridi, utaona mawingu ‘’cloud cover’’, hasa wakati wa usiku, hii ni kwa lengo la kupunguza kiwango cha joto kisipotee kwa wingi wakati wa usiku. na maeneo yenye joto, au siku za joto pia, utaona anga likiwaa jeupe, hii ni ili kupoteza joto lisizidi. Zipo namna nyingi sana kwa kuzielezea, na hata kuna baadhi ya shahidi zimeonesha namna maji katika mabara, hujibalansi na maji katika bahari, ili kupunguza madhara ya ongezeko la kimo cha bahari baada ya kuyeyuka kwa mabarafu. na hata uelekeo wa upepo, hulenga kubalansi kiwango cha hali ya hewa.

Vitu vya kuwa makini ni namna vijana wengi wamewekwa mbele katika vita hii ya mabadiliko ya tabia ya nchi. Vijana wengi hawana taarifa za kutosha kuhusu graph za hali za dunia kwa zama mbalimbali. na ni rahisi kulipuka kwa hisia za hofu na woga. Mtazamo hatarishi na mbaya kabisa Zaidi, ni kuona binadamu wenzao kama chanzo cha uharibifu wa dunia. hii inaweza pelekea kuamini hata upungufu wa binadamu unaweza okoa dunia. na kusahau kuwa, binadamu ndio kitovu kikubwa Zaidi cha Maisha na sio mawe.

Nashauri wasomi wawe ni watu wenye kutafsiri matokeo, wakiyalinganisha na uhalisia wake. Haimaanishi kama ukiwa unatembea unaweza okota pesa, basi kutembea kunaweza kuwa chanzo cha mapato au mradi. Namaanisha, haina maana kwa kuonekana vyanzo vya nishati za makaa ya mawe, na Mafuta vinaweza leta madhara ya hewa ya kaboni, basi tayari nishati hizi ni hatari na umeme ni mbadala bora Zaidi, bila kuangalia hali za wananchi. Ni muhimu kutafuta asilimia za faida, na hasara, na kisha kuzilinganisha, na mwisho kuchukua hatua bora Zaidi.

Kisichoweza badilishwa ni kuwa, yako mabadiliko ya hali ya nchi ambayo ni kweli yanashtua, yapo yanayochochewa mfano na Teknolojia za kubadili Hali za hewa "Geoecological engineering", na zaidi zaidi ni makubwa yanayokuja huko mbeleni. Soma kitabu chako cha Biblia toka ufunuo 13, mpaka ufunuo 18. Ukitaka unaweza amini, ila pia usipotaka unaweza amini sayansi ya big bang ambayo nayo inakwambia miaka mamilioni baadae, nishati ya dunia itaisha na italipuka. Sasa machaguzi ni ya kila mtu.

Kama mungu yupo kwanini kuna njaa, vifo, magonjwa na umasikini?

 ‘’Wenye haki hawaachwi na Mungu’’ inahitaji hisabati kuelewa hili.

Maisha ya Duniani Asiye na dhiki:70± Mwenye dhiki:70± Mwaminifu: 70± Si mwaminifu:70±

Lakini Mwaminifu:(70±) +milele.

Milele (infinity) ±70=Milele.

Hivyo basi Maisha ya mkristo mwaminifu iwe ni kwenye dhiki, au raha, hayana mantiki maana miaka ya duniani ni michache sana, dunia ya leo ili ufurahie sharti uwe na matatizo ya kiakili, au saikolojia. unawezaje furahia utajiri wa mali na heshima, ili hali nje ya geti lako, kuna harufu za maiti za Watoto waliotupwa kwa kukosa chakula na kutelekezwa. nchi nyingi zinalia na ukame na magonjwa, ardhi imeshaharibiwa n.k, 

haya majanga yote yanamaanisha yalipaswa yaimalize dunia moja kwa moja kupitia kifo, lakini iko njia ya kurejea tena uhai, tena katika ulimwengu usio na dhiki kwako tu, bali hata kwa mdudu aliyechini ya viatu vyako. Na huo ni ulimwengu ambao kama una miaka 30, basi unaweza ufikia baada ya miaka 40±. Simaanishi kuwa baada ya kifo utaenda mbinguni au kuzimu. Ila namaanisha, baada ya miaka hiyo hautakuwa na uwezo tena wa kuchagua, na njia pekee itakayokuwa imebaki ni kufumba na kufumbua. 

Kumbuka ukifa na kukaa kaburini hata miaka 1000, hakuna muda utakao kuwa ukiuhisi, maana hauna cha kuhisi, ukifa umekufa haupo hakuna akili wala muda. Na hivyo basi, kama ukitenda mema, utakachohisi ni kuwa Yesu amerudi. Ukiamua kuendelea kumtukana kama wanafizikia wa leo kina Neil de grass Tyson, carl sagan, brian greene, Lawrence, hawking Stephen, Richard dawkins n.k pia unaweza fanikiwa ila mwisho huthibitisha maana ‘’the end justifies means’’

kwanini supercritical water haikuunguza safina na samaki wote na kuua kila kitu?

Maji ya scw yalitoka na presha kubwa sana, hata yakaenda nje ya dunia, hayakupoteza joto maana joto kubwa lilisafiri kwa njia ya mawimbi yanayoelekea juu ‘’convection’’, na sio joto linalosambaa pembeni ‘’radiation’’. mfano, ukiwasha mshumaa au jiko la gesi, unaweza sogeza mikono yako hata kutaka kabisa kuukumbatia moto kwa pembeni, bila kuungua. lakini ukiweka juu, utaungua sana. Hivyo nishati kubwa ya joto haikusambaa kuingia duniani, na pia kumbuka, hewa si kipitishio kizuri cha joto, ‘’poor conductor of heat’’, huwa na ‘’inertia’’, na mwisho maji haya yaliwahi sana kupoa, kutokana na badiliko la presha ‘’rejea sifa za supercritical water’’.

Dunia ina mamilioni ya aina za wanyama. je wote waliingia kwenye safina?

Dunia ina maelfu ya makabila ya watu, tena tuliotofautiana hata mionekano, ila wote tulitoka kwa Nuhu na mkewe na Watoto wao. Siku zote Biblia haitumii ‘’species’’, biblia hutumia ‘’kinds’’. Yaani, ukichukua mbwa wawili, tayari baada ya muda unaweza pata aina zote za mbwa kutokana na asili ya jenetikia kufanya mabadilisho ‘’variations’’. Na sayansi hii sasa hivi ina nguvu sana kutokana na ugunduzi wa hamasa ya mazingira katika jenetikia za viumbe ‘’Epigenetics’’. Viumbe wengine wengi kama samaki, na wadudu wasingewekwa kwenye safina.

***************---------------------------**********"""