MABAKI "FOSSILS" YA GHARIKA KUU
Uwepo Wa Mabaki Ya Wanyama Katika Matabaka Kulingana Na Jamii Zao Na Pia Katikati Ya Matabaka
Miongoni mwa vitu vinavyowachanganya sana wanasayansi wa mabaki ya viumbe hai ‘’Palaentologist’’, ni namna ambavyo mabaki ya viumbe hai yanavyoundwa katika dunia. Kilomita kadhaa unaposhuka katika baadhi ya matabaka, huonekana mabaki ya viumbe vilivyoishi awali, swali kubwa je, viumbe hivi vimefikaje katika maeneo yale ya chini kabisa? Utakutana na mabaki ya Wanyama, na pia mabaki ya mimea, na muda mwingine hata na vitu vilivyokuwa vikitumika zamani kama vile mapanga, mishale, visu n.k
Changamoto hizi zimepelekea wanasayansi wote wasiotambua sayansi hii ya gharika, kukimbilia nadharia yao kwa kusema kuwa, miaka mingi nyuma viumbe wale waliishi katika dunia. na kisha wakafa, na baada ya kufa mabadiliko ya muda mrefu ya mamilioni ya miaka yalipelekea wakafukiwa kabisa, na kuibuka kwa tabaka jipya kabisa juu yao. na hivyo basi, watu hawa wakishikiriana na wanabiolojia ya mabadiliko ya evolution, hukubaliana kuwa, Tofauti za matabaka zinamaanisha tofauti za zama za viumbe. na huendelea mbali kabisa kwa kusema kuwa, matabaka ya chini kabisa yana maanisha kuwa, hao viumbe waliishi miaka ya nyuma kabisa. na matabaka ya juu yanamaanisha kuwa, ni viumbe walioishi karibuni. Na watu hawa huamini yawezekana kukawa na upatikanaji wa mabaki ya viumbe waliokuwa katikati ya mabadiliko ‘’transition fossils’’ katikati ya haya matabaka. Watu hawa huchukua mabaki yanayopatikana matabaka ya chini kabisa, na kusema kuwa hao ni viumbe walioishi miaka ya nyuma sana. na wakati huohuo hulinganisha na mabaki katika matabaka yanayopatikana juu, na kusema hao ndiyo viumbe wa siku za karibuni.
Kila tabaka wao wamelipatia zama mithili ya kipindi ambacho viumbe Fulani tu waliishi. Mfano, hebu tazama matabaka yafuatayo na majina waliyoyapatia na kisio la viumbe walioishi zama hizo.
Unaweza tazama namna kila tabaka huaminiwa kuwa ni la viumbe walioishi mamilioni ya miaka huko nyuma, hata miaka bilioni 2.5 iliyopita. msingi mkuu wa hizi nadharia umetokana na nadharia ya Charles Darwin, ya mabadiliko ya evolution. na ndiyo maana unaona katika hiyo picha wakiweka katika ngazi za chini kabisa viumbe wadogo kabisa kama bakteria. hapo wanamaanisha kuwa, tumetoka huko, na pia utaona wameweka mafuvu makubwa chini kumaanisha, hata binadamu walianza toka jamii zinazofanana na masokwe. pia nadharia ya Big Bang ni msingi wa hii nadharia, ndiyo maana unaweza ona katika ngazi ya chini kabisa kulia imeandikwa dunia iliundwa miaka Bilioni 4.6. na mwisho hutumia nadharia ya Charles Lyell ya Uniformitarianism ya uumbaji wa matabaka polepole. na ndiyo maana kila tabaka limeoneshwa kutumia miaka mingi sana kumaliza zama zake.
Changamoto Na Kufeli Kwa Nadharia Za Mabadiliko
kuwepo kwa wanyama wa aina tofauti na wa ngazi tofauti za nadharia yao ya mabadiliko katika tabaka moja.
Mara nyingi sana watafiti wa mabaki, wameshuhudia maelfu ya Wanyama wa zama tofauti kutokana na nadharia ya mabadiliko, wakiwa katika tabaka moja. hii inapingana na nadharia zao zote kwa pamoja. Pia inathibitisha nadharia hii ya gharika ya nuhu, hebu tafakari unawezaje elezea uwepo wa mnyama wa ardhi kama dinoso kuwa sehemu moja na samaki.
Uwepo wa miti iliyosimama katikati ya matabaka.
Kutokana na mtazamo wao, kila tabaka ni la miaka mingi. Sasa iweje uwepo mti katikati yao. Hii inathibitisha kuwa matabaka ni matokeo ya muda mfupi, kama nilivyokwisha elezea awali. hebu tazama picha chini.
Hii inafanya nadharia nzima ionekane haina uhalisia.
kushindwa kuelezea kwanini mabaki yote ya viumbe huonekana wakiwa katika hali ya ghafla, au kushtukizwa.
Idadi kubwa sana ya Wanyama wameonekana wakiwa mithili ya kukimbia, au wameonekana wakiwa wanafanya shughuli Fulani. na sio vifo vya kawaida ambavyo vimefuatiwa na kufukiwa kwa miaka mingi ya bwana Lyell.
Mfano tazama picha chini.
Samaki huyu amefukiwa ghafla akiwa anakula chakula chake, ambacho ni samaki mwenzake. Huu ni uthibitisho kuwa ilikuwa ni gharika ya ghafla.
kushindwa kuelezea mabaki ya viumbe katika mazingira yasiyo yao ya asili.
Unaweza kuta samaki akiwa yuko katika mlima, au akiwa pamoja na Wanyama wasio wa baharini, na namna nyingine za aina hii. Hii inatuthibitishia moja kwa moja kuwa, gharika ya nuhu ndiyo ilikuwa chanzo kikubwa Zaidi.
Mfano, tazama picha hizi toka milima mirefu Zaidi duniani.
Picha hizi unazoweza zipata katika mitandao, zinaonesha tu namna jamii hushtuka zinapokutana na mabaki ya Samaki katika vilele vya milima. Wamefikaje? Walipaswa kujua hii sayansi ya kweli.
kushindwa kujibu sababu za kusambaa kwa mabaki ya nyangumi hata kwenye majangwa yaliyombali kabisa na bahari.
Mfano tazama picha hii.
Changamoto ya mazingira ya utunzaji wa mabaki bila gharika
Hakuna kitu inaweza elezea kuhusu inawezekenaje kukawa na mazingira ya kutunza hata mabaki ya vitu laini, kama wadudu, na mabawa yao laini kabisa. Maana bila ufukiwaji wa matabaka ndani ya muda mfupi tu kama kwa gharika, utapelekea kumomonyoka kwa kila sehemu hata isibakie sehemu moja. Mfano tazama picha hii.
Hitimisho ya changamoto za nadharia za mabadiliko
Haziwezi elezea hasa kwanini leo hii hatushuhudii matabaka yoyote yale yakiundwa, wala pia hatushuhudii mabaki yoyote yale ya viumbe yakiundwa. Hii yote ni kutokana na kutozingatia nini sayansi inasema kwa kukimbia kurejea kwenye Biblia.
Nini Hasa Kilifanyika Katika Gharika Ya Nuhu Kuunda Mabaki Haya ‘’Fossils’’
Kiwango kikubwa sana cha maji yaliyokuwa na matope mengi yalisambaa katika ulimwengu. na wanyama wengi walikuwa wakiyakimbia kwa kutafuta maeneo yenye miinuko. na uwezo wa kukimbia gharika uliambatana na aina ya mnyama, uwezo wake, mazingira yake n.k. mfano, ni vigumu sana kukutana na mabaki ya binadamu kwa kuwa binadamu wana akili, na hivyo wengi wao walikuwa maeneo ya juu sana hata pale iliposhindikana kabisa. Viumbe wengi baada ya kufukiwa na kiwango hiki cha maji, yenye sediments, uundwaji wa mabaki haya bado haukukamilika. yalitukia matendo yafuatayo.
Viumbe hawa ndani ya sediments walishushwa katika matabaka tofauti tofauti kulingana na uzito wao ‘’density’’, mfano, wale wazito walididimia chini Zaidi ukilinganisha na wale wepesi.
Idadi kubwa sana ya Wanyama, na mimea, iliyokusanywa katika matabaka kadhaa, Haikuwa na uzito mkubwa sana ukilinganisha na miamba. hii ni kama ambavyo magogo na maiti huwa yakielea juu ya maji. Na hivyo basi, kadri ambavyo mabaki haya yalipokuwa ndani ya maji, yakifukiwa na matabaka ya juu ya miamba, basi yalikuwa yakitengeneza tabaka linalotenganisha vilivyopo chini, na vilivyo juu. Ambalo Walter Brown aliliita ‘’Water Lensing’’. Na tabaka hili pia lilikuwa lipo katika presha kubwa, ambayo kama ungetokea upenyo basi lingepanda juu.
Na hii ni sababu ya baadhi ya mabaki huonekana yakiwa katika namna ya kupanda juu, au kutoka katika sehemu za chini. Kielelezo rahisi kabisa cha kuelewa hili, ni jaribu kutengeneza picha umekandamiza gogo ndani ya maji, mpaka halionekani kwa kulikalia. halafu unaweza tafakari namna ukitokea upenyo wa wewe kuteleza, namna gogo litapanda juu. Hii husaidia kujibu baadhi ya maswali magumu kabisa nadharia za mabadiliko haziwezi jibu, mfano, kwanini baadhi ya sehemu za milima au matabaka, huwezi kuona mabaki! ila sehemu zingine unaweza ona mabaki? Wao kwa kushindwa kujibu, huanza kujibu kuwa wenda matabaka hayo yasiyo na mabaki, yalikuwa miaka kabla ya Maisha kuwepo. Majibu hayo hata wao wenyewe huona kuwa hayana mantiki, maana tayari yote inaonekana ni miamba iliyo katika namna moja. Jibu rahisi ni kuwa, mabaki haya yalikuwa katika mgandamizo wa matabaka ya juu, na ilipofikia wakati wa mikunjo katika dunia ‘’compression’’, ile ambayo niliielezea kuwa chanzo cha milima, basi mabaki mengi yaliyokuwa katika katika levo zile za chini, yalipanda juu kwa kielelezo cha wewe ukiinama ukaliacha gogo peke yake. Tazama kielelezo chini, na kisha picha mojawapo inayoelezea maeneo hayo yawatiayo mashaka wanasayansi wa mabadiliko ya evolution.
Tabaka la juu ni miamba mizito, tabaka la kati ni mabaki na tabaka la chini ni maji na miamba mingine.
Baada ya dunia kupitia kipindi cha mkunjo ‘’Buckling’’ kama nilivyoelezea katika uundwaji wa milima katika sehemu za nyuma.
matokeo ya kitendo hiki:
tazama picha chini
Ushahidi Wa Gharika Ya Nuhu Kupitia Mabaki Ya Makaa Ya Mawe,Fossils Za Miti ‘’Petrified Trees’’ Na Mafuta.
makaa ya mawe
Ili uweze kutengeneza makaa ya mawe unahitaji vitu vya msingi vifuatavyo; Maji yenye joto kali, Mazingira yasiyo na oksijeni, Na Mazingira yenye presha au mgandamizo mkubwa.
‘’petrified trees’’
Ili uweze kutunza miti hii unahitaji; Maji yenye madini ya kutosha, Madini yaliyo katika maji yanapaswa kuingia katika mmea, na maji haya mara nyingi huitaji madini ya silica. Ambayo huja kuunda madini ya quartz.
Mafuta ‘’Oil’’
Ili uweze kuunda mafuta unahitaji vifuatavyo; Unahitaji joto kali, Unahitaji presha kubwa, na Viumbe wa kutosha kuunda mafuta. Sasa basi katika vitu hivyo vikuu vitatu, unaweza gundua makubwa zaidi katika nadharia yetu ya gharika ya nuhu kupitia hoja zifuatazo.
Ni mazingira gani unaweza pata mimea ikajikusanya katika mazingira yanayofanana, tena kwa kiwango cha kuzalisha kiwango kikubwa cha makaa ya mawe, kama yaliyo katika migodi ya makaa ya mawe ya leo. Kwa kupitia tu akili za kawaida, kila mtu anajua leo hii hakuna mgodi wowote wa makaa ya mawe unaweza jitengeneza, hata kama ni mdogo. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, ilihitajika gharika ya nuhu tu kuikusanya mimea mingi katika muda mmoja. na ukweli kuwa zamani kulikuwa na mimea mingi kuliko leo, ndiyo sababu tosha zaidi kuweza elezea kwanini kuna makaa ya mawe mengi sana.
Ni mazingira gani tunaweza pata Joto kubwa, kiasi cha kuweza kuwezesha utengenezaji wa makaa ya mawe? Uundwaji wa makaa ya mawe unahitaji mazingira ya mimea kufukiwa ghafla kwa Pamoja, na tena joto la ghafla katika mazingira maalumu. kama sivyo huwezi pata makaa. Kutumia joto la matokeo ya kufukiwa kwa muda mrefu, na ili hali ikijulikana hakukuwa na tukio la kuikusanya kwa wingi, hata kama ni imani ya miaka sio mamilioni kama wanavyosema, ikawa mabilioni, bado haiingii akilini wala haina uhalisia. Gharika ya nuhu ilikuwa ndio chanzo cha maji ya moto sana ‘’supercritical water’’. haya yaliwezesha mimea ile ambayo ilikuwa imefukiwa na matabaka ya sediments, kuweza kuunda makaa ya mawe. sediments ziliifunika mimea, na hivyo kuondoa kabisa hewa ya oksijeni. na hivyo kuchochea makaa ya mawe.
Ili utengeneze Petrified trees kama mmea kwenye picha chini. Unahitaji kiwango kikubwa cha maji ya moto, na yenye silica. Je ni kitu gani kingeweza sababisha hali hizo? Kama sio Gharika ya Nuhu, unawezaje elezea sababu za miti hii kuwa sehemu hizo hizo ambazo kuna makaa ya mawe, kama Colorado Plateau.
Picha hii ni miongoni mwa picha kubwa sana za historia, zilizopigwa zamani sana baada ya wachimbaji migodi ya makaa ya mawe, kushangaa kuuona mti uliokuwa ume hifadhiwa ‘’petrified tree’’. Inashangaza sana lakini picha kubwa ambayo unaweza tambua ni kuwa, kama ukimwona mbwa wa kufugwa katika mbuga za Wanyama mwituni, unaweza hisi labda ni aina tu ya mbwa mwitu, lakini ukimkaribia ukamkuta pia ana mnyororo shingoni, unapaswa kuwa makini na tafsiri yako. Unaweza elezea makaa ya mawe kwa mtu asiyeelewa uhalisia wa makaa ya mawe, lakini huwezi elezea petrified trees.
Robert Gentry miongoni mwa tafiti zake, aligundua uwepo wa Radiohalos katika baadhi ya makaa ya mawe, lakini pia hakuishia hapo, aligundua uwepo wa madini ya uranium karibu na migodi hii ya makaa ya mawe, na alipotafuta umri wa uranium na lead, aligundua kuwa vyote vinaonesha viliundwa pamoja karibia miaka elfu tatu nyuma. Hiyo bado inaweza isimtoshe mtu kutambua kuwa hayo yalikuwa ni matokeo ya gharika ya nuhu.
Uundwaji wa Mafuta ‘’oil’’ ni miongoni mwa vitu vya ajabu sana. Ambavyo vinatuthibitishia uwepo wa gharika ya nuhu. Miongoni mwa vitu vilivyogunduliwa ni kuwa, kupitia maji yenye joto, utengenezaji wa Mafuta hutokea kwa muda mfupi Zaidi kukiwepo na mazingira mengine. Leo hii ili kutengeneza kiwango kikubwa cha Mafuta yaliyopo katika migodi duniani, mtu angehitaji idadi kubwa sana ya viumbe huwezi kadiria, na tena viwe pamoja. Ni nini cha kutengeneza mazingira haya, Zaidi ya gharika ya nuhu. Hebu tazama ramani ya visima vikubwa Zaidi vya Mafuta duniani, karibia asilimia 94% vinapatikana katika sehemu moja ya Asia ya kati, je mtu angejiuliza, hakukuwa na mabadiliko ya kufukia viumbe katika maeneo mengine duniani? Kwanini visima hivi visingekuwa kwa idadi sawa tu na idadi ya kusambaa kwa viumbe duniani. Kuna hitaji Imani kubwa sana kukubaliana na nadharia hizi, hata kama itahitaji kulipwa.
Gharika ilipelekea Wanyama wengi sana kufa. na Wanyama hawa walikuwa wamefukiwa katika matabaka ya sediments. Kadri ambavyo dunia ilipokuwa ikipitia vipindi vya ‘’Compression’’ na ‘’fluttering’’ kama nilivyoelezea katika sehemu za nyuma. ilipelekea makundi ya Wanyama hawa, au mimea, kukusanyika katika mazingira yanayofanana. Hii ni sawa na leo hii ningekuwa na uwezo mkubwa sana, halafu nikachukua darasa la wanafunzi 100, kisha nikalitikisa tikisa ili kuwatoa wale watakao kuwa wamejishikilia katika madirisha, halafu baada ya hapo, kama nikiliinamisha hili darasa kuelekea upande mmoja, basi wanafunzi hawa wote mia watakusanyika katika uelekeo mmoja. Na hivi ndivyo pia ilifanyika dunia.
Kumbuka sayansi inayotumika inaelezea msingi wa utokeaji, hivyo basi msomaji anapaswa kuwa na taswira pana Zaidi ya matendo haya yakifanyika katika mazingira tofauti tofauti, lakini yakiwa na aina moja ya utokeaji, hii ni sawa na kusema, sheria ya kuunda milima ya Himalaya, ndiyo ya kuunda milima uluguru, ila haimaanishi milima Himalaya ni sawa kabisa na milima ya uluguru, hii ni kutokana na kuwepo kwa tofauti ndogo ndogo.
************--------------******-----------***********
To be continued
















Join the conversation