Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

USHAHIDI WA GHARIKA YA NUHU

USHAHIDI WA GHARIKA YA NUHU

Mabadiliko Yanayotokana Na Maji Ya Gharika Ya Nuhu

Kiwango kikubwa cha maji katika dunia yaliyotoka katika vilindi ndani ya dunia, kilipelekea mafuriko yaliyoifunika dunia nzima. maji haya hayakuwa yaliyokuwa na hydrogen na oksijeni pekee, bali yalikuwa ni maji ambayo yanakiwango kikubwa sana cha madini, na hasa ni mabaki ya miamba na maudongo, au kiwango kikubwa cha matope ya lava kutoka ndani ya dunia. Kwa pamoja haya yote yaliyokuwa yamebebwa na maji haya, huitwa ‘’Sediments’’. 

Kiwango kikubwa sana cha sediments kilitoka pamoja na maji, na kufunika sehemu kubwa sana ya dunia kutokana na mazingira yake ‘’topography’’. Miamba na matabaka makubwa leo hii tunayoyaona, yakiwa misingi au ngazi za milima na miinuko, yalikuwa ndiyo matope katika maji haya yaliyotoka katika vilindi vya maji ya ndani ya dunia. Kama nilivyoonesha awali kabisa kipindi naelezea miamba, nikaonesha kuwa idadi kubwa ya miamba ambayo imefunika sehemu kubwa ya dunia ya leo, imetokana na asili ya lava, au magma. Unaweza jiuliza kuwa kama magma huwa asili yake ni ndani ya dunia ‘’volcanoes’’, sasa imekuwaje dunia iwe na kiwango kikubwa cha magma kama ambayo inaonekana hivi leo. Angalia idadi ya miamba ya Igneous rocks, sedimentary rocks, na metarmophic rocks, iliyopo katika dunia ya leo, je imetoka wapi? Au ni kweli kulikuwa na milipuko ya volcanoes huko awali ya uumbaji wa dunia kama wanasayansi wa mabadiliko wanavyoamini?

Ukweli ni kuwa, haya yote yalikuwa ni matokeo ya matope ya lava ya gharika kuu ya nuhu. Supercritical water iliyeyusha kiwango kikubwa sana cha miamba ya ndani ya dunia na kuitoa nje. maji yalitoka ndani ya dunia yakiwa na presha kubwa sana, na yakaanza kusambaa katika uso wa dunia katika kila kona ya dunia. Matukio yafuatayo yalitokea yakiambatana na kazi ya msukumo wa maji haya ya matope ya lava.

Ulainishwaji na maji katika ardhi ‘’liquefaction’’

Hiki ni kitendo ambacho ni kama ambavyo mafuriko yanapotokea, kwanza kabisa hupelekea ardhi na miamba kunyonya maji na kulainika. Unaweza kumbuka kipindi unadidimia katika matope yaliyosababishwa na mvua za kawaida kabisa, hebu jaribu kutafakari maji yenye nguvu ya kulainisha ‘’scw’’, yaliyo kwenye uso wa dunia tena kwa siku 150. Unaweza pata taswira namna dunia ilikuwa imelainika kwa kiwango kikubwa sana. Hiki kitendo cha kulainika kiliambatana na dunia kuwa na tope kubwa sana la miamba, hasa ile niliyoiita ‘’sediments’’, ambayo ilitoka kutoka ndani ya dunia. Miamba katika sediments ilisambaa maeneo yote ya dunia, na hata ulainikaji wa dunia ulikuwa katika sehemu zote za dunia.

Fizikia ya namna maji yanaweza kunyakua matabaka ya ardhi na udongo

Unaweza vuta picha kwanini kingo za bahari nyingi zimejawa na mchanga, au miamba midogo midogo. au kwanini mafuriko yakishapita, hupelekea kufukiwa kwa mimea, Wanyama, na hata vyanzo vya maji, na miinuko kadhaa kwa mchanga.

Hii hutokana na tabia ya mawimbi ya maji, ambayo siku zote yanapokuwa yakielekea chini, hunyakua matabaka ya chini kwa kuzunguka molekuli za hiko kitu, na kisha hukisambaza hata kikawa chepesi ‘’less dense’’, Na yanaporudi, basi hukiacha kile kitu kikiwa katika hatua nyingine, ambayo huwa ni mbele ya awali, kutokana na uelekeo wa mawimbi ya maji.

Hebu fatilia jaribio hili dogo ‘’experiment’’

Hili ni kontena lina maji na miamba midogo kidogo. Presha ya maji ni ya kawaida.

Kisha nikaongeza miamba mingi Zaidi.

Matokeo: Presha ya maji huongezeka sana. kiwango cha miamba iliyojuu ya kontena hufanya maji yawe na presha kubwa ya kutaka kupanda, kwa kupenyeza katikati ya miamba iliyoongezwa.

maana ya jaribio ni nini?

Uwepo wa maji mengi katika au ndani ya sediments, uliyafanya yawe na presha kubwa sana. presha hii iliyafanya yasababishe mabadiliko mengi sana katika jiolojia ya dunia. Hebu tutazame mabadiliko kadhaa yaliyo matokeo ya kitendo hiki.

Utengenezwaji Wa Matabaka Katika Ardhi Na Milima ‘’Layers Stratifications’’ 

Miongoni mwa vitu vinawachanganya sana wanasayansi wa mabadiliko au evolution, ni uundwaji wa matabaka. Msingi wa sayansi ya Lyell ya ‘’Uniformitarianism’’, yaani mabadiliko kupitia muda mrefu sana, kuelezea kuwa kila tabaka ni matokeo ya mabadiliko ya mamilioni ya miaka, huwa inawachanganya sana. maana kuna kila sababu ya kupingana na nadharia hiyo, iliyo na mapungufu mengi sana kama tutakavyoyaona. na pia sababu kubwa Zaidi inayowachanganya ni namna nadharia hii ninayoielezea inavyo jibu vizuri, na kuweza kuthibitishwa kwa majaribio ya kisayansi, na sio tu nadharia za kufikirika.

Ukichukua chombo kikubwa sana, na kisha ukaweka maji mengi, halafu kisha ukaanza kuweka mchanganyiko wa aina mbali mbali za udongo au mchanga, na kisha ukakoroga, na kisha ukaacha itulie, baada ya muda utaona matabaka sawasawa na aina za vitu ulivyoviweka.

Hebu tazama vielelezo vifuatavyo.

Changanya aina hizi zote na kisha koroga utapata mchanganyiko uliofanana.

Baada ya kuchanganya mchanganyiko wako, na ukawa mkorogo wa aina moja kama huo, utakapokaa baada ya muda ukiuacha utulie utapata matokeo yafuatayo.

Maana ya jaribio hili ni nini?

Kama ambavyo matabaka haya yalivyojipanga katika hili kontena bila kujali kiwango cha mkorogo wake, hivyo hivyo na baada ya maji ya gharika kuchukua kiwango kikubwa sana cha sediments, basi matabaka yale yakaanza kujipanga katika uso wa dunia kulingana na uzito wao ‘’densities’’.

Ushahidi wa nadharia hii juu ya uundaji wa matabaka katika dunia

uwepo wa matabaka ya aina moja ya miamba katika ardhi dunia nzima

Ukirejea sehemu iliyopita ambapo tuliiona aina ya milima mikunjo, Ambayo hufanya kuonekana kirahisi kwa matabaka haya, lakini hata ardhi huonesha aina hii hii ya matabaka kirahisi sana.

Unaweza tazama matabaka yanavoonekana katika mlima huu, hebu tazama pia katika picha hizi za chini. Hii huitwa Grand Canyon, tutaiangalia vizuri baadae kidogo. Unaweza tazama matabaka yanavyodhihirisha nadharia yetu.

To be continued...