Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

TANZANIA NA GHARIKA KUU

Tanzania na Gharika kuu

TANZANIA NCHI YANGU NA GHARIKA 

Miongoni mwa vitu vinavyonishangaza sana ni nchi ya Tanzania. nchi ya Tanzania ni nchi ambayo ni ndogo kwa kuilinganisha na saizi ya Afrika nzima, na Dunia kwa ujumla. lakini ni nchi ambayo ina maajabu makubwa Zaidi katika sayansi ya jiografia. Ukiangalia katika ramani ya dunia au ya Afrika, utaiona nchi ya Tanzania ikiwa imepambwa na matokeo makubwa Zaidi ya gharika ya nuhu. Hebu tazama kwanza ramani zifuatazo kabla hatujaiangalia kiundani nchi hii.


kutokana na hizi picha, taarifa ya kwanza unayoweza pata kuhusu upekee wa Tanzania ni namna ambavyo iko katikati ya Matengano makuu ya Plate za Bara la Afrika.

Tanzania imebebwa au pitiwa na bonde la ufa ‘’rift valley’’ ukiifanya kuwa katikati ya mipaka miwili mikuu, yaani bonde la ufa, na bahari ya hindi.

Tanzania inaonyesha kuwa ilikuwa katika kani ya msukumo wa kumeguka, na kuwa kisiwa. kushindwa kwa msukumo huo, ambao unaonekana kuanzia katika mid atlantic ridge, kulipelekea kiwango kikubwa cha kani iliyopelekea bonde la ufa, lililopelekea kuwepo wa plate za Arabian na Somalia.

Bonde la ufa lilipelekea kiwango kikubwa sana cha nishati ya joto kwa msuguano, na pia kutengeneza njia nyingi sana zilizoachilia upenyo wa magma kupita tokea chini. Na hii ikapelekea kuundwa kwa milima mingi sana ya volcano, ikiwemo mlima Kilimanjaro. lakini pia kupitia kuangalia mikoa mingi ya kaskazini, mpaka kanda za juu za ziwa, kuna idadi kubwa sana ya milima iliyoambatana na mawe. 

Sayansi ya uundwaji wa mawe maeneo ya mwanza na mikoa mingine.

Kabla sijaanza kuelezea kiundani ni namna gani mawe katika mikoa hii yaliweza kuundwa, ni muhimu msomaji kutambua kuwa, Bonde la ufa ambalo ndio chanzo kikubwa cha matukio haya, lilisababishwa moja kwa moja na kupanda kwa mid atlantic ridge, katika hatua ya kwanza kabisa ya kutokea kwa gharika ya nuhu. Unaweza rejea picha chini ili uone bonde la congo linavyofuatana na ukanda wa bonde la ufa la Tanzania.


Kutokana na hizi picha na nadharia yetu, unagundua kuwa sehemu yote ya kaskazini ya Tanzania ilikuwa katika Compression, ilikuwa ikiinuliwa kwa kani kubwa sana, kiasi cha baada ya kushindwa kuendelea kusukumwa kuelekea bahari ya hindi katika Plate ya Somali, basi ilipelekea mgawanyo wa plate au mpasuko au bonde la ufa.

Kumbuka Gharika ilisababisha maeneo mengi haya kuwa na maji, na hivyo basi, kuinuka kwa plateau. kwanza kulipelekea kiwango kikubwa cha maji kukusanyika katika bonde la ufa, na kuunda ziwa Tanganyika, ziwa nyasa, ziwa rukwa, ziwa mweru, ziwa kivu, ziwa Edward, ziwa albert, ziwa turkana, na mengineyo kwa upande wa nchi nyingine zilizopitiwa na bonde hili. 

Kitendo cha Bonde la ufa kupita katika sehemu mbili, kilipelekea Plateau na miinuko hii katika pande mbili, kutengeneza Bonde kubwa kwa mfanano wa Funnel. Ambalo lilipokea kiwango kikubwa sana cha maji, na kuzalisha ziwa kubwa Zaidi duniani Ziwa Victoria.

Chanzo cha mawe

Mawe mengi ni matokeo ya Miamba ya Magma, ambayo iliweza kupata nafasi ya kuonekana na kupanda juu kupitia aidha; Baada ya magma kuganda, magma hizi zilikuwa zikiganda umbali kadhaa chini ya tabaka la juu la dunia. Hizi magma kutokana na kitendo cha Dunia kupitia compression, basi zilisukumwa juu kama mithili ya zile miamba za michanga ‘’ sand moulds’’. Kiwango kikubwa sana cha maji yaliyokuwa yakimwagika, kuelekea bonde la ziwa Victoria, yalimomonyoa ardhi laini yote ya juu na kuacha matabaka ya miamba ya magma iliyokuwa imeganda, na hii ndiyo namna ambayo imetokea kwa maeneo mengi sana ya ukanda huu wa kaskazini, na kanda ya ziwa.

Kushoto nikiwa katika hifadhi ya kigosi Geita na kulia nikiwa katika ziwa Victoria Mwanza.


Unaweza jiuliza ni kwa namna gani mtu angeweza kuelezea uundwaji wa mawe haya makubwa, tena yaliyo katika uhusiano mkubwa baina ya yenyewe. Hii inatosha kuelezea nguvu ya magma na pia bila kutambua Compression effect, huwezi elezea namna miamba hii ingeweza ibuka na kutokea juu.

Pichani nikiwa Dodoma, unaweza tazama kiwango kikubwa cha mchanga katika mji wa Dodoma. mchanga Unaonyesha idadi kubwa ya maji yaliyopita hapa awali, kutokea nyanda za kaskazini na kuelekea kanda za pwani na Morogoro hata baharini. Rejea ramani hii ya Tanzania.

Unaweza kuona namna mkoa wa Morogoro ulivyo na mito mingi sana. hii inatokana na kazi kubwa yakusafirisha ‘’drain’’ maji iliyofanyika tokea awali. 

Nikiwa Morogoro. Mito na maporomoko ya namna hii ipo kwa wingi sana katika ukanda wa morogoro.


Kumbuka kanda hizi kuu mbili, yaani za juu na za kusini. ndiyo pande kuu mbili za Tanzania. Utakapoenda mkoa kama Iringa, bado utakutana na aina ile ile ya tabia kama utakazo zikuta njombe na Mbeya, na ndivyo ilivyo mikoa mingi, tofauti hasa huwa kutokana na umbali wake toka usawa wa bahari, lakini katika aina za jiolojia utakazozikuta, zote huendana na nadharia yetu. Mfano bado utashuhudia aina ya miamba midogo Iringa ambayo ni mabaki ya magma, ‘’unaweza fika Tosamaganga’’, utakutana na dalili nyingi za mipasuko midogomidgo ya ardhini.

Idadi Kubwa Ya Madini Tanzania.

Nchi ya Tanzania ina kiwango kikubwa sana cha migodi mbali mbali kuanzia ya Dhahabu, mpaka Almasi na Tanzanite. Hii ina maana kubwa sana, hasa ukiangalia maeneo migodi hii ilipo. Hebu angalia ramani ya migodi chini. unaweza ona mikoa ile ile ambayo awali ilikuwa imeathiriwa na bonde la ufa, na kuwa juu, ndiyo yenye madini mengi zaidi. Hiyo ni sawa na kusema, madini mengi yaliyokuwa yameyeyushwa na Supercritical water, na maji kupanda juu na kupoa, yalipelekea madini haya kujiunda kupitia ‘’precipitation’’. na hivyo basi, kitendo cha bonde la ufa kusababisha compression, kulipelekea miamba hii kupanda juu ya matabaka kadhaa. Nadharia ya mabadiliko haiwezi elezea uumbaji wa miamba ya madini. maana density yake huyahitaji kuwa ndani kabisa ya dunia. 


Isimila Pillars Kutoka Iringa ‘’Canyons’’ 


unaweza pia zielezea kupitia nadharia yetu.                     

Je Wajua? Ukiwa Tanzania Huitaji Kwenda Popote Kujifunza Sayansi Ya Asili

Mapango Ya Amboni Tanga


Hakuna namna ya kuelezea mapango haya Zaidi ya kurejea gharika ya nuhu, iliyopelekea maji mengi yaliyokuwa yakitoka kanda za kaskazini, yakiwa na presha, hata kutengeneza mapango katika maeneo yaliyokuwa na sedimentary rocks nyingi juu ya chaneli za maji kuelekea baharini. Rejea katika ramani ya amboni, ni maili chache sana toka baharini, kwa usawa ule ule wa bahari ukilinganisha na maeneo ya karibu yake.

Mchanga Olduvai Gorge Unaotembea ‘’Shifting Sand Dunes’’ 

Inashangaza sana upekee wa eneo hili, ambalo pia limejawa na mabaki mengi kiasi cha kuwafanya wanasayansi wasiojua Biblia, hata kusema Binadamu wa kwanza aliishi hapa. Hii ni sawa na kusema, binadamu wa kwanza alikuwa Mtanzania. Si kweli, binadamu wa kwanza alikuwa adamu, maana ukiendelea kuwasikiliza watakuambia alikuwa sokwe. Ila cha muhimu ni kuwa, Tanzania ni Zaidi ya special place.

Madini Ya Tanzanite ‘’The Only Pure Blue Diamond of the Universe’’.

Uundwaji wa Diamond huwezi anza kuelezea bila ya gharika, maana unahitaji madini pure ya kaboni, na kisha unahitaji mgandamizo wa tabaka la juu. Mazingira hayo yote hayawezekani bila supercritical water, na mgandamizo wa sedimentary rocks.

Mlima kilimanjaro ni mlima mrefu zaidi, ziwa viktoria ni kubwa zaidi, ziwa Tanganyika ni refu zaidi, madini ya Tanzanite ni ya pekee zaidi, plate yake ni ya pekee zaidi, yapo maajabu mengi zaidi na hata watu wake ni wakarimu zaidi, Tanzania ndiyo nchi pekee yenye Makabila mengi zaidi, lakini bado ikawa na Amani ya kweli kwa muda mrefu zaidi.

.....To be continued