USINYWE CHAI, KAHAWA, & COKE♨️
Kahawa"coffee",Chai "tea", & Cocoa
Kahawa "coffee"
Mmea huu baada ya kuvunwa, vipeke vyake hufunguliwa na Kisha huvundikwa katika maji. Baadae hukaushwa katika jua, na hii huwa ni kahawa nyepesi. Kahawa nzito huandaliwa kwa kukausha kwanza mbegu zake na Kisha kuondoa viini vyake. mbegu zake hukaangwa na sukari hata kuunda rangi yake ya Weusi. Kahawa huwa na ladha ya kusisimua kutokana na uwepo wa kemikali zinazoitwa "alkaloid". Kemikali hizi zilizopo kwenye kahawa huitwa "caffeine"
Chai " tea"
Mmea wa chai ambao kisayansi huitwa"Camellia sinensis", hutumika kutengeneza chai kupitia hatua kadhaa. Hatua huanza baada ya kuvunwa majani yake. Majani husambazwa na kukaushwa na kukandamizwa na chuma chenye joto. Hii hupelekea kemikali za Polyphenols na enzymes kadhaa kuzalishwa. uvundaji au fermentation huanza, ambao hupelekea uundwaji wa kemikali zenye ladha ya upekee wa chai. Chai pia huwa na kemikali ya "caffeine" na kemikali nyingine ya kusisimua inayoitwa "theophylline".
Chai huwa na kemikali za " hydrogenated glucose syrup, sorbitol, mannitol, xylitol, lacticol na isomalt". Kiwango kikubwa Sana Cha kemikali za "Polyphenols" zinazoitwa "tannins", huwepo katika chai, lakini Kuna kitu ni muhimu Sana kukifahamu.
Kwanini Wanyama hula majani huku wakitembeatembea?
Zipo sababu nyingi lakini miongoni mwa sababu za msingi Sana huwa ni tabia ya mimea inapokuwa ikiliwa. Mnyama anapokuwa akila majani ya mimea, ile mimea ambayo huwa ikiliwa hutambua kuwa Kama italiwa mpaka mwisho kabisa basi itaathiri kiini Cha mmea, na unaweza kushindwa kuendelea kukua.
Na hivyo Basi, mmea ukishaliwa kwa kiwango kadhaa, huzalisha kemikali sumu ambazo huwa ni chungu, na mnyama anapozila, huziona ni chungu Sana na kuhama katika Hilo eneo analokula, na kwenda eneo lingine. Kwa hiyo hiyo ni namna ya asili ya Mimea kujilinda ili isiharibiwe kwa kuliwa kwa mimea hata ikashindwa kuendelea kuzaliana kabisa.
Namna ambayo wavunaji wa chai hufanya kipindi wanavuna chai, moja kwa moja hufanana na Aina hii ninayoizungumzia. Hukata majani juujuu Sana ya mchai na kupelekea mimea hii kuzalisha sumu nyingi Sana. ambazo zote huchanganywa na hatma yake huendelea zaidi huvundikwa na kuunda sumu zaidi.
Chai na Vimelea
Hata uweke nini kwenye chai hakuna vimelea Kama bakteria watakaovutiwa nayo. Bakteria wanatambua kuwa Kati ya kinyesi na chai, angalau kinyesi kina virutubisho kidogo lakini chai sio tu haina virutubisho, bali pia ni sumu.
Watu wengi wanaoipenda chai huipenda kutokana na ladha yake na asili yake ya kusisimua. Kama utampatia mtu Aidha chai ikiwa katika asili yake ya powder au kahawa, na ukamwambia ailambe, na akuambie ladha yake, tafsiri zake zote zitakubaliana na tafsiri ya ladha za sumu. Baada ya kuiandaa chai, harufu nzuri ambayo huwa Maranyingi ikiambatana na utambuzi wa ladha, huifanya iwe tamu hasa ukichangia na asili ya kemikali zake zinazou sisimua ubongo.
Cocoa
Hii inatokana na mmea unaoitwa "theobroma cacao". Cocoa nayo hupitia hatua zilezile za maandalizi Kama ya wenzake, yaani huvundikwa, na madhara ya kuvundikwa hupelekea kuundwa kwa "acetic acid" ambayo huondolewa. Cocoa hukaangwa na hatimaye hubakiwa na asilimia 1% ya theobromine.SIFA YA COCOA, COFFEE NA CHAI KWA PAMOJA
Hizi zote huwa na kemikali za msisimko katika ubongo, kemikali za kundi la "alkaloid".
Kemikali hizi ni: CAFFEINE, THEOBROMINE, na THEOPHYLLINE
Kemikali hizi zote hupatikana toka katika mimea, na huko hazipatikani Kama vyakula vilivyomo ndani ya wanga, au protini, Hupatikana toka Aidha majani, au mizizi, au magamba. Hiyo inatosha kumuelezea mtu kuwa hata asili haikuziandaa hizi kemikali Kama vyakula.
Mfano mzuri ni namna ambavyo "theophylline" hutumika Kama dawa ya kulegeza bronchus katika mapafu "bronchial dilator", hii humsaidia mgonjwa wa asthma, na wengineo. lakini ajabu ni kuwa, Kuna mtu anakunywa kila siku kwenye chai. Hebu tuangalie madhara ya jumla yanayotokana na utumiaji wa kemikali hizi na Kisha nitasema nini hasa ndilo tatizo kuu.
Inapozidi/ Overdose ya Caffeine huleta shida za ghafla kama zifuatazo;
Madhara ambayo huwa hayajidhirishi Kwa kiwango kikubwa sana lakini huwepo ni Kukosa usingizi, maumivu ya kichwa, anxiety "kutojisikia kutulia kwa hofu", irritability "kutotulia kihisia", depression "msongo sugu wa Mawazo". Kama mtu atatumia bila chakula tumboni basi atajisikia mitetemeko tumboni, mwili huongeza joto, agitation "Hali ya kutotulia kabisa kihisia", kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kuongezeka kwa kuhema, kuwa na mapigo ya moyo yasiyo sawa "irregular heartbeats", kupoteza maji mengi, kutetemeka, kuanguka na kushikwa na wazimu "convulsions", Mshtuko, kupoteza fahamu, na kufa.
Huchochea kuzaliwa kwa watoto wenye shida ya maumbile "teratogenic effects", kuuwawa kwa mtoto tumboni, na Wakati mwingine kumeng'enywa kabisa Kwa Mtoto tumboni "fetal resorption". Huchochea kupungua Sana kwa uzito wa mtoto tumboni, matatizo ya mfumo wa mifupa, n.k. Matatizo haya yote yametofautiana kutokana na kiwango kilichotumika, na muda wa utumiaji.
SAYANSI YA KUATHIRI UBONGO KWA KUTUMIA KAHAWA,CHAI, NA KOKOA
Kemikali za Caffeine, Theophylline, na Theobromine, ndizo kemikali zinazowafanya watu waendelee kuipenda kahawa ijapokuwa ni chungu. hii ni kutokana na tabia zake za kuusisimua Ubongo. Sehemu hii tunaangalia sayansi nyuma yake, na matokeo ya tafiti nyingi zilizokwisha ripotiwa hasa na shirika la kuaminika zaidi la utafiti la NCBI.
Caffeine ambayo ndiyo sumu kubwa, na pia msisimuaji mkubwa zaidi, huwa inafanya yafuatayo.
Huchochea uingiaji wa madini ya Calcium kuelekea ndani ya seli. Matokeo siku zote ya kujaa kwa calcium ndani ya seli huwa ni kuifanya seli iwe na chaji Chanya zaidi kwa ndani, na hii hupelekea seli ya ubongo kusisimka zaidi kama tulivyoona katika sehemu iliyopita.
Kumzuia mmeng’enyaji au ‘’enzyme’’ anayeitwa PDE au ‘’Phosphodiasterase’’. ambaye huyu huwa akikinzana na ujazo wa kemikali inayoitwa ‘’cAMP’’, na huyu enzyme anapozuiliwa, hupelekea kiwango kikubwa sana cha cAMP, ambacho husababisha kuongezeka kwa matendo ya kibiolojia, au shughuli za ubongo ‘’brain metabolism’’.
Hukinzana ‘’antagonistic’’ na homoni au neurotransmitter ya Ubongo inayoitwa ‘’Adenosine’’. Kemikali hii ndani ya ubongo kazi yake kubwa zaidi huwa ni kuongoza mfumo wa mzunguko wa kulala na kuamka wa kila siku Kwa kusisimua hisia ya kulala . Na pia kemikali hii huwezesha hali ya kutulia kiakili ‘’relaxation’’. Kemikali hii ya adenosine hupatikana zaidi katika sehemu kuu tatu za ubongo; sehemu ya ubongo wa mbele unaotawala kufikiri na tabia, ubongo wa ndani ‘’basal ganglia’’ unaotawala matumizi ya nguvu katika miondoko yote ya mwili, na mwisho kwenye sehemu ya ubongo wa kumbukumbu ‘’hippocampus’’.
KWANINI WATUMIA KAHAWA HUUKIMBIA USINGIZI?
Sababu kubwa zaidi ni Caffeine kuiblock adenosine ambayo ndiyo ilikuwa ipelekee Usingizi. Lakini pia katika mzunguko wako wa mchana na usiku, Ukifika usiku kupitia ule mzunguko wa fiziolojia nzima ya kulala unaoitwa ‘’circadian rhythm’’, Zipo homoni zingine ambazo pia huwa zikihusika kama ya ‘’melatonin’’. Hii huzalishwa zaidi kipindi giza linapoingia. homoni zote hizi hufanya kazi kwa kushirikiana na kemikali zingine, na hasa humchochea homoni ‘’GABA’’, ambaye huyu sasa huongeza mgandamizo wa shughuli za ubongo, na hata kupelekea hali kama ya ku paralyze na mtu hulala.
Sasa basi anachofanya caffeine ni Kwenda kukaa, na hatimaye kuzuia sehemu ambayo adenosine alipaswa kukaa, na hii sasa, ndiyo hufanya mtu asihisi usingizi. Kwa hiyo mtu alipopaswa kulala, pamewekwa sumu na hakuna kulala tena.
Kwa watumiaji hutumia hii kama faida ya kuhisi kuwa wana uwezo wa kukamilisha shughuli walizopaswa kuzikamilisha, kwa kupewa faida ya muda zaidi. Lakini maswali ya msingi ni kuwa, je fiziolojia nzima ya mwili inalichukuliaje swala hili? Na je, ubongo umeridhia matendo haya? Na je, kuna umuhimu gani wa kulala? Na vipi kuhusu madhara mengine ya caffeine kama tutakavyoona.
Tafiti zinaonesha kuwa, caffeine huongeza matendo au shughuli za ubongo ‘’brain metabolism’’. Swala hili nilishalielezea hapo juu linatokana na kumzuia PDE.
KWANINI CAFFEINE ZIWE SUMU HIVI?
Hizi sio sumu zisizo na mipango maalumu. Zina malengo maalumu kabisa. Mimea imezitengeneza kwa lengo la kumlewesha mmalizaji wa sehemu zake. Hizi sumu ni kama ‘’Bunduki’’ na sio ‘’Jiwe’’. Yaani bunduki ipo maalumu kwa kuua, na ndivyo zilivyo caffeine.
Tafiti zinaonesha ukiachana tu na tabia ya caffeine kuongeza shughuli za ubongo, lakini pia caffeine huwa inapunguza kiwango cha damu kinachopita katika ubongo ‘’decreases cerebral bloodflow’’. Caffeine imeonekana kuchochea seli za ubongo za homoni ya ‘’Norepinephrine’’
KWANINI HUSEMWA KAHAWA KIDOGO NI NZURI KWA AFYA ?
Ni mara chache sana kukutana na jarida litakalo kuambia madhara ya caffeine moja kwa moja, lisikushauri juu ya faida kadhaa za caffeine. Na mara nyingi hii hutokana na tendo hilo la juu, la caffeine pia kuwa na tabia ya kuchochea ‘’norepinephrine’’. Hizi norepinephrine ni miongoni mwa kemikali au neurotransmitters za ubongo zenye kazi nyingi sana za maana katika ubongo. Miongoni mwa kazi zake kubwa, na ambazo huwafurahisha zaidi wanywaji kidogo wa kahawa ni kama zifuatazo.
Hutengeneza hali ya kujisikia vizuri ‘’mood regulation’’, kwa kawaida hii homoni ya ‘’norepinephrine’’ huwa ikihusiana sana na sehemu za hisia, na kuzifanya zikae sawa. Huboresha kumbukumbu na kujifunza, hizi norepinephrine huusika katika matendo ya uundwaji wa miunganiko, katika seli za ubongo kipindi cha kuunda kumbukumbu ‘’neurosynaptic’’, na kwa hivyo, ‘’ne’’ husaidia kuufanya ubongo kuwa na hali nzuri ya kujifunza, huongeza muamko, na hali ya umakini.
Mara nyingi norepinephrine huzalishwa katika mazingira ya kumfanya mtu awe makini zaidi, na hoja hii hufanana na hoja nyingine ya kuwa, norepinephrine hutawala mfumo wa matendo yasiyo ya hiari ya mhemko "sns", kupitia mfumo unaoitwa ‘’autonomic nervous system’’. Na mwisho kabisa, norepinephrine hujihusisha na kutawala uwezo wa kukabiliana na changamoto, ambazo huwa zinaitwa ‘’stress’’, au ‘’stress response’’.
Kahawa huchochea uzalishaji wa homoni ya ‘’Dopamine’’, homoni hii huusika na matendo ya kimsisimko na kujikia vizuri. Na hii ndiyo hali ambayo huwachochea watumiaji kutumia na kutumia zaidi hii kemikali.
Hoja hizi na zinginezo za hali za raha, ambazo watu huwa wanazipitia kutokana na matumizi ya kahawa, huwa ndiyo sababu kubwa ya kuchochea matumizi ya kahawa. Na pia, wengine hutumia ajenda ya kuwa, kwa sababu hatari ya kuwa mraibu kutokana na matumizi ya kahawa ni ndogo, basi ni vyema tu kutumia kahawa.
Hoja hizi huwa zikihamasishwa sana, na hasa na watu wenye mitazamo ya kibiashara zaidi. lakini uhalisia ni kuwa, hebu tusome ili tujue ni kivipi watu huchezea akili za watu.
UHARIBIFU WA CAFFEINE
Kutoka shirika la NCBI. Caffeine ambayo ni familia ya kemikali sumu iitwayo ‘’methylxanthine’’. Hizi kemikali zote za hii familia ikiwemo na zote zilizo kwenye chai, na kokoa, zimeonekana kuathiri uwezo wa misuli katika miondoko ‘’locomotor activity’’, na huwa na madhara kidogo katika saikolojia za watumiaji.
Athari katika kujifunza, kumbukumbu, na uwezo wa kuchakata taarifa, zinatokana na kemikali ya methylxanthine kuathiri muamko wa ubongo, ufatiliaji ‘’vigilance’’, na hali ya ubongo kupata fatiki ‘’fatigue’’.
Theophylline huongeza kiwango cha cAMP, ambayo tulishaona madhara yake ni kuongeza matendo ya kibiolojia.
Huwepo matatizo ya kitabia kutokana na madhara ya ‘’Xanthine’’ kwenye adenosine receptors.
Matumizi ya Caffeine kwa muda mrefu, hupelekea matokeo yafuatayo katika kiwango cha receptors za kemikali za ubongo katika utafiti wa panya.
Adenosine receptors ziliongezeka kwa asilimia 20%. Muscarinic receptors na nicotinic receptors ziliongezeka kwa 40-50%. GABA receptors ziliongezeka kwa asilimia 65%. Serotonergic receptors ziliongezeka kwa asilimia 26-30%
TAFSIRI YA MATOKEO HAYA
Haya matokeo yana maanisha kuwa, kadri mtu anavyotumia kahawa. Huwa anaua receptors za ubongo wake za kuhisi kemikali hizo juu za ubongo. Na sasa basi, ikifikia kiwango Fulani, ubongo huona utaishiwa kabisa na sasa basi huongeza uzalishaji wa receptors hizo ili ikitokea wewe unaziua kwa kunywa kahawa au chai, Basi na wenyewe unajitahidi kulipia deni lako au ku ‘’compensate’’ .
TAFITI YA MADHARA YA KAHAWA KWA WATOTO WA SHULE
Watoto wadogo ambao wameshaingia katika gurudumu la uuaji wa mtindo mpya wa Maisha, huteseka sana katika kujitahidi kubalansi mzunguko wa usiku na mchana. shughuli nyingi za mashuleni huwahitaji kutumia usiku ili kumalizia kazi za shuleni. Hali hii huwafanya wakeshe Usiku wakisoma na kuenda kesho yake wakiwa na uchovu zaidi.
Swala hili huongezeka kila siku, na mzunguko wao ulioathiriwa huwapa ugumu sana kuwa na umakini hasa Kwa wakati wa mchana. Watoto hawa huzitegemea siku za weekend ili kulipia madeni ya usingizi wa wiki nzima. Hali hii huwa sivyo kama walivyo tarajia. kwa kuwa, kulala sana katika siku za weekend, kunaonekana kuzidisha kuu disturb mfumo wa kulala na kuamka ‘’sleep wake cycle’’. Na hili tatizo Linaitwa Delayed sleep Phase Disorder (DSPD).
Tafiti zaidi zikafanyika kuhusu namna ambazo Watoto hawa hutumia Ili kupambana na madhara haya. Tafiti zikagundua kuwa,
Matumizi ya kahawa, na juisi au vinywaji vyenye caffeine, mfano; Kahawa, Chai, Soda za Coke, Energy Drink, n.k. kwa Watoto yamekithiri sana. Watoto huzitumia sana ili kujiwekea umakini pale ubongo unapoonesha kuchoka. Sasa tafiti zimeonesha, Watoto wote ambao huwa wakitumia vinywaji hivi, na kisha wakaenda kulala, yafuatayo hutokea.
Kuchelewa kwa kuanzishwa kwa usingizi. Hii inakupa taswira ya namna ambavyo tayari neurotransmitters za ubongo zinakuwa zimeathirika, na hizo ndizo zinazotawala na matendo mengine ya mwili.
Kupungua kwa nguvu ya usingizi ‘’sleep intensity’’. Kupitia camera za ubongo za ‘’EEG’’, watumiaji wa vinywaji vyenye caffeine, hasa energy drinks. Wameonekana kuwa na usingizi wa juu juu. Hali hii huathiri mwili mzima kwa kuwa, usingizi una maana kubwa sana katika mwili, na ubongo, na utu wa mtu. Kwa hiyo Watoto hawa huwa wanaingia katika msiba mkubwa sana.
FAIDA ZA USINGIZI KISAYANSI
Huboresha kumbukumbu. mtu anapolala ubongo wake huingia katika hatua ya pili ya uundwaji wa kumbukumbu za muda mrefu, na kitendo hiki huathiriwa mtu anapokuwa halali au hapati usingizi mzito wa kumtosha.
Hubalansi homoni za ubongo ‘’neurotransmitters’’, ubongo huunda kiwango cha neurotransmitters zitakazohitajika kwa kazi zaidi, na uundaji wa kumbukumbu zaidi, na misisimko au motivation zaidi.
Huchuja na kuondoa sumu zilizopo mwilini. katika ubongo matendo ya kuongoza na kujenga tishu za ubongo na zinginezo zilizoathiriwa hufanyika zaidi mtu anapolala.
Mfumo wa kinga hutegemea sana kulala, tafiti zinaonesha kuwa mtu anapolala, mwili huzalisha kiwango kikubwa sana cha ‘’Cytokines’’ ambazo tuliziona zikiwa katika mstari wa mbele zaidi katika kuimarisha kinga ya mwili.
Tafiti zimegundua pia kuwa, uvimbe au ‘’inflammation’’ katika tishu mbalimbali za ubongo hupungua mtu anapolala, kwa mfano, mtu ambaye utamnyima usingizi kwa muda mrefu, ataonesha dalili za kuwa na uvimbe zaidi ya mtu ambaye alikuwa akilala.
Tarehe 14 mwezi wa kumi 2023 jarida linaloitwa ‘’journal of nuerochemistry’’ lilitangaza utafiti wa Yann vannobaeys, na wenzake. Ambao waligundua namna mtu asipolala inavyopaswa huishia kuathirika kwa matendo kuanzia kiwango cha jenetikia, yaani ( changes katika molecular signaling, madhara katika gene transcription, madhara katika uundwaji wa protini ‘’protein translation’’, mabadiliko ya maumbo ya dendrites za seli za ubongo n.k) huu ni kama ule msemo wa utotoni uliokuwa ukisema, ‘’lala ukue, ukikua utajua’’.
KIPI WASICHOKIJUA WATUMIAJI WA KAHAWA
Katika kiwango cha tabia ya mtumiaji yeyote wa kahawa, Hawezi kujua uwezo alioupoteza hata kama atakuwa ana uwezo kiasi gani. Pili mtumiaji wa kahawa hawezi kuwa na maamuzi mazuri na ustahamilivu wa changamoto kama mtu wa aina yake asiyetumia. Mtumiaji wa kahawa hawezi kukimbia ukweli wa tafiti za kisayansi wa namna anauathiri ubongo wake Pamoja na matendo ya biolojia yake, kwa kusema kuwa ni madogo hayamdhuru sana.
Watumiaji wa kahawa, chai, na cocoa, wote huuchoma ubongo wao kama jua linavyolichoma bati. haijalishi ni kwa kiasi gani bado bati huonekana imara, ila huwa linaisha.
Kama kizazi cha watumiaji wa bidhaa hizi kitakuwa hakiathiriwi sana na bidhaa hizi, basi tutegemee kuwa na idadi kubwa ya watu wapole, wavumilivu, wenye kujifunza ,wenye kukumbuka mausia, wenye kiasi, wenye akili za ugunduzi, na wasio penda migogoro. Na kama sivyo, basi hayo ndiyo madhara ya kitabia yaliyo zaliwa katika ubongo.
KWANINI MIMI SITUMII CHAI, AU KAHAWA?
Kahawa, Chai, Kokoa, Coke, na vyote vyenye kemikali za methylxanthine kama Caffeine vinachochea kupotea Kwa maji mwilini. Jambo lolote linalochochea upotevu wa maji linachochea kupungua Kwa Lifespan & Healthspan kama tulivyoona katika Blog nilizoelezea Siri ya maisha Marefu.
...ajabu zaidi: wanywaji chai huiongeza na sukari "sucrose", hutumia na Wanga zenye sukari + mafuta ya Mbegu❌
Vitu vidogo vidogo ndivyo vinatengeneza vitu vikubwa#



.jpg)









Join the conversation