Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SHERIA YA PILI YA MALEZI katika ulimwengu wa kisasa

 

#2 ASIYEJALI HALI YA MAWINGU (UJAUZITO), HATALIMA.


Ukiona shamba limestawi sana mimea, mfano; ukiona mahindi ni mazuri, marefu, majani yake yana rangi nzuri, na yana watoto wazuri, kipi kinachokujia akilini? Udongo wake una rutuba nzuri, una maji yakutosha, matunzo yake ni mazuri, na mbegu iliyotumika pia ni bora. Kumbe unapoona muhindi ni sawa na ungekuwa unaona udongo, maji, matunzo, na mbegu. Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa Mtoto tumboni. Mtoto anahitaji pia Virutubisho bora sana kwa mama yake, Mama ni kama Udongo, Maji, na hewa kwa Mtoto.

Lakini jambo ambalo wengi hawalitambui ni kuwa; Mama haongozi Uundwaji wa mtoto tumboni, inahitaji mfumo bora wa kihomoni na kimetabolikia wa mama, na tena zaidi, inahitaji Mfumo imara zaidi wa uundwaji wa mtoto tumboni unaoratibiwa na maji, usumaku, na mwanga. Afya ya mtoto inaanza na afya ya mama yake. Bahati mbaya sana wanawake wengi wa kizazi hiki ndiyo masoko ya mifumo hatarishi  yote ya kiafya.


Nimekuwa nikitambua kuwa Vyakula vya kisasa kama Soda, Chipsi za viazi, Chili sauce, Kuku wa kisasa ‘’Broiler’’ wakukaanga, Nyama za Makopo, Burger, Pizza, Chocolates, n.k. kuwa ni vyakula halali kwa wanawake, na havina madhara kwao, mpaka nilipokuwa daktari. Wanawake wamejihalalishia vyakula sumu vyote kuwa ni vyakula bora kwao, kwasababu tu vinawasisimua sana. Sishangai kama mtaalamu wa Ubongo kwa kuwa najua, sehemu ya Ladha ya Chakula kwa wanawake katika Ubongo ‘’Insula cortex’’ imeendelea zaidi. Hii inawafanya kuwa waraibu wa vyakula vya kusisimua kwa urahisi zaidi ya ilivyo kwa wanaume. Hili ni tatizo kubwa sana.

Mjamzito Katili Hachagui Chakula!

Kabla ya yote, dalili ya kwanza ya Ujauzito ni Kichefuchefu, unajua kwanini? kwasababu Ubongo wa Mama hujiboresha zaidi katika sensa zake za hamu ya kula, ambazo zinahusiana na sensa za hisia za harufu. Mabadiliko haya humfanya kuhisi kichefuchefu hata kwa mabadiliko madogo tu ya harufu au ladha. Ubongo hufanya hivi kumaanisha; sasa Mama ana mtoto ambaye inambidi amlinde asimuathiri kwa kula vitu hatarishi, maana mtoto ni rahisi sana kudhulika hata kwa sumu kidogo tu za vyakula.

Vyakula vya kisasa vyote vimejaa kemikali za utunzaji ‘’Preservatives’’ ambazo ni sumu hatari sana kwa binadamu. Wanawake wote wanaotumia bidhaa hizi wakiwa wajawazito wanapelekea kemikali sumu kujaa katika mifumo yao ya damu. Sumu hizi hupenya na kuingia katika Mfumo wa damu wa mtoto kupitia ‘’Placenta’’. Kwa kuwa Ubongo wa mtoto kuanzia Wiki ya saba huwa umeshaanza kuundwa, kemikali hizi huanza kuathiri ubongo moja kwa moja. Tafiti zinaonyesha mpaka mwezi wa saba wa mtoto, Sensa zake za Ladha huwa tayari zimekamilika kumaanisha; Mama anapokunywa soda, na mtoto naye anaihisi. Hii ni hatari, inapelekea watoto kuzaliwa wakiwa tayari waraibu.


Katika Ubongo, kuna sehemu kadhaa ambazo huwa wazi, hizi sehemu huitwa ‘’Circumventricular organ’’. Hizi sehemu huwa na kazi ya kupima na kusensi hali ya damu katika mwili, kuna nini? Kuna upungufu gani? Sehemu hizi huusisha pia sehemu ambayo kuna tezi kuu ya mwili ‘’Pituitary’’, na sehemu ya Ubongo inayotawala mfumo wote wa homoni, metaboliki, na nishati ya mwili. Kwa utumiaji hatari wa bidhaa za Kisasa, sehemu hizi huanza kusensi na kujazwa na kemikali sumu. Matokeo yake, sehemu hizi huanza kutengeneza uvimbe mdogo sugu, huu huathiri uzalishwaji wa homoni, huathiri Muitikio wa Ubongo kwa homoni za insulini na leptini. Matokeo yake watoto huja kuzaliwa wakiwa tayari waraibu, wana shida za kihomoni, shida za ukuaji, na hata shida za kiakili kama Usonji.

Ipi ni kazi kuu ya Ini? Ni kulinda Ubongo. Ini hupokea kila kitu kutoka katika Utumbo kupitia mfumo wa damu unaoitwa ‘’Portal Circulation’’. Ini huchuja sumu zote na kuruhusu Virutubisho tu na damu safi kwenda kwenye ubongo. kemikali sumu ambazo nyingi hutoka katika;

·         Vyakula vyote vya kisasa, vya makopo, vya viwandani, na visivyo vya asili

·    Vyakula vyote vyenye mabaki ya madawa ya madawa ya kuua Magugu na Wadudu ‘’pesticides’’

·         Vyakula vyote vya wanyama walio na mabaki ya madawa ya vimelea ‘’Antimicrobials’’

·         Matumizi ya visisimuaji ‘’Stimulants’’ katika vyakula, rangi za vyakula,n.k.

Mama Mjamzito anatakiwa kula nini?

Mungu hakuwahi kumchagulia mwanadamu ale nini, ila alimwambia tu asile Matunda ya Mti wa katikati. Na hivyo ndivyo ilivyo hata katika Amri kumi, Mungu hasemi ufanye nini, ila anakuambia tu, Usifanye jambo fulani, mfano; Usizini, Usiibe, Usidanganye... Hoja ni kuwa, Endapo ukiachana na Vyakula hatarishi vilivyoorodheshwa hapo juu, kila Maeneo tayari huwa na utaratibu wa vyakula bora kwa ajili ya wajawazito. Na kwa ajili ya faida ya Kizazi cha kisasa, Ni muhimu kuzingatia vyakula vifuatavyo kwa ajili ya wajawazito

·   Ni vema zaidi, Miezi sita kabla ya kupanga kupata ujauzito mwanamke kuanza kufuata utaratibu bora wa ulaji kwa ajili ya mwanae (kama ilivyokuwa ikifanywa zamani, Rejea Kitabu cha Weston Price ‘’Nutrition and Physical degeneration’’)

·   Vyakula vyenye Protini kamili. Zamani Wamaasai na jamii nyingi walitumia Damu mbichi kidogo, ambayo siisapoti sana kwasababu zangu za Kiimani, lakini hoja ni kuwa; ina protini nyingi. Wanaume wanapaswa kuwapatia wake zao wajawazito Nyama za Maini kutoka kwa wanyama waliojihakikishia kuwa hawajafugwa kwa madawa, Wanapaswa kuwapatia Mayai ya kienyeji hasa ya kuchemsha, Protini za mimea kama Soya, Mbegu kama Maharagwe, Supu za wanyama wa kienyeji, Maziwa, na Samaki. Hizi protini ndizo matofali katika ujenzi wa tishu za mtoto tumboni.



·      Vyakula vyenye Mafuta ya Omega-3 zaidi ya Omega -6, na pia vyenye mafuta wastani ya SFA. Mafuta haya unaweza yapata kupitia Supu za wanyama wa kienyeji, Maini, Samaki, Mayai, Siagi, Mafuta ya samli, Mboga za majani kama Spinachi, Brocolli, Mchicha, Karanga, Korosho, n.k. Mafuta haya ndiyo msingi wa kutengeneza Cholesterols ambazo zinatengeneza homoni zote kwa mama na mtoto. Mwili wa mtoto unahitaji sana mafuta ilikuwa na uwezo wa kutoathirika au kuumia wakati wa kujifungua.


·         Maji na Matunda. Mjamzito anahitaji sana maji ili kutopata changamoto ya Upungufu wa damu. Asilimia 93% ya damu ni maji, wajawazito kwa kunywa maji hujiepusha na upungufu wa damu unaotokana na damu nyingi kuelekea kwa mtoto.



Wanawake wengi huwa na shida ya kujaa maji katika miguu wanapokuwa wajawazito. Sababu zipo nyingi, lakini Upungufu wa presha ya damu kutokana na upungufu wa damu, na presha ya mtoto tumboni kukandamiza mishipa ya damu kupandisha kwa urahisi damu sehemu za juu za mwili, ni miongoni mwa sababu zinazopelekea damu katika sehemu za chini za miguu, kukaa kwa muda mrefu sana kiasi cha kuruhusu maji kupenya sana katikati ya tishu, na kupeleka kujaa kwa miguu maji. Kwa kunywa maji, presha ya damu hurejea kuwa na nguvu ya kusambaa isituwame sehemu moja. Mama anapokunywa maji, mfumo wake wa damu na wa mtoto wake unazidi kuwa bora, na usambazaji wa virutubisho unakuwa bora zaidi.

·         Madini na matunda. Ni vyema kwa wajawazito kutumia sana mbegumbegu kama Korosho, mbegu za maboga, alizeti, ufuta, matunda kama maparachichi, nyama nyekundu marachache, maziwa, na kubadilisha badilisha mboga za majani. Wanawake wajawazito maranyingi sana hupenda kula udongo, ukweli ni kuwa; wengi wao hupungukiwa sana madini chuma, na hata Calcium.


Na hii ndiyo sababu wengi wa wanawake baada ya kujifungua huwa na shida za meno, Meno yao hulegea sana. Sababu kubwa ni upungufu wa madini ya Calcium ambayo mengi sana huenda kujenga mifupa ya watoto.

·         Vyakula vya wanga vinapaswa kuliwa kwa wastani sana. Hii ni kwa kuwa, huwa na hatari sana ya kupelekea kunenepa kwa njia ya uzazi. Wanga kwanza huwa na uraibu sana, na hili huwapelekeaa wanamama wajawazito kula sana, matokeo yake hujikuta wakiridhika sana na vyakula vyenye kusisimua tu pasipo virutubisho na uhitaji.


Ili kupambana na tatizo hili, suluhisho pekee ni Kutotumia vyakula vya wanga vya kukaangwa, visivyo na kambakamba kama Sembe, ngano, na mchele kwa wingi. Kwa kutokana na hali za umasikini za jamii zetu, ni muhimu kwa wanaume kuchanganya aina mbalimbali za wanga ili walahu kupunguza tatizo hili. Mchanganyo wa Mahindi, Mtama, Mihogo, Ndizi, Oats, na hata na Karanga au mbegu za maboga na kuusaga, unaweza tengeneza Unga ambao una kiwango kikubwa cha Kambakamba na Virutubisho, na Wanga isiyovunjika kirahisi ‘’Resistant starch’’.

·         Wajawazito wanapaswa kutambua asili haitambui Ujauzito kama Ugonjwa, na hakuna kiumbe ambaye hushinda akilala ndani kwasababu ya ujauzito, hata kama ni mdogo kama Mjusi. Ulaji wowote ule bila kushahabiana na kazi ndogondogo, lazima utapelekea utunzwaji wa chakula kwa namna ya mafuta, na matokeo yake; Namna pekee ya kuzaa itakuwa ni Kisu.



Mjamzito Gaidi husikiliza Miziki ya Singeli na Amapiano


Ni lazima kwa mjamzito aliye na tamaa ya kuwa na mtoto aliye na afya nzuri ya mwili na kiakili, kutambua kuwa mawimbi ya muziki, hupenya hata kufikia DNA za mtoto. DNA za mtoto huwa bize sana kutokana na uumbwaji wa viungo vya mtoto. Shughuli zote za DNA katika utengenezaji wa Mwili wa mtoto huratabiwa na mfumo wa mawimbi ya usumaku na umeme mdogo wa seli, ambao huratibiwa na tabia za Maumbile mbalimbali ya maji ‘’Hydrogen bond angles’’. Shughuli zote hizi huathiriwa kwa kusikiliza miziki mibaya mfano ya mawimbi ya 440HZ ambayo ndiyo imejaa katika miziki ya kisasa.

Miziki kama ya singeli, inaenda kwa mawimbi ya fastafasta sana, hata biti 250bpm kwa dakika. Hizi huathiri mawimbi ya ubongo, na maumbile ya maji, na matokeo yake huathiri shuguli za DNA kama ripoti za NCBI zilivyoonesha, kwenye tafiti ya Madhara ya mawimbi ya miziki katika biolojia ya viumbe. Miziki ya Amapiano nayo ina mabiti mengi sana yanayopigwa kwa wakati mmoja ‘’Polyrhythms’’, ambayo huwa na matokeo hatari sana katika biolojia, unaweza rejea kitabu changu juu ya madhara ya miziki katika biolojia ya mwili.

Sio Miziki Peke yake, na Filamu za Usiku!


Mawimbi toka katika Vifaa vya kielektroniki kama Televisheni, Simu, na Mitambo mikubwa ya umeme na Minara kwa maeneo ya mijini, huwa na madhara makubwa sana katika uundwaji wa mtoto tumboni.

Mawimbi haya ambayo unaweza yaita ‘’nnEMF’’, na mawimbi ya blue ‘’blue frequencies’’, nimeyaelezea sana katika vitabu vyangu. Matokeo yake ni mabaya sana, kwa kuwa mwili hutumia mawimbi mapana ‘’broad bands’’ katika kuwasiliana, lakini mawimbi haya huwa yamenyooka katika aina moja tu ‘’specific i.e, Monochromatic’’.

Hii huathiri mfumo mzima wa taarifa kati ya mama, na ukuaji wa mtoto.  Na hii ndiyo sababu, watoto wengi wanazaliwa kabla au baada ya siku zao, lakini pia, watoto wengi wanaendelea kukua hata katika kipindi ambacho hawakupaswa kuendelea kukua, na kupelekea kuwa wakubwa kupita njia ambayo wangepaswa kupita. Haya yote ndiyo yanachochea zaidi kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida, na kutegemea upasuaji.

Mwanamama mjamzito msomi ambaye anashinda usiku katika taa za kisasa, anapaswa kujua kuanzia sasa, taa zinamfanya aendelee kuwa katika hali ya stress ya mwili ‘’SNS’’ inayohamasisha chaneli ya kutozalisha homoni ya HPA, na hii inakinzana na uzalishwaji wa homoni zote zinazotegemea mfumo wa ‘’PSNS’’ ambao huwa chini kwa kushinda kwenye mianga usiku.

Taa za usiku huwa zinapelekea Upungufu wa Oksijeni mwilini kwa kubadilisha hali ya mbeba Oksijeni ‘’Hemoglobin’’ kumfanya awe na madini chuma yenye Oxidation state ya 3+. Hii huathiri mfumo mzima wa taarifa wa mtoto kuwa kuanzia mwezi wa Saba hakupaswa kuendelea kukua Kichwa, na ndiyo maana; Seli nyekundu za mtoto zina Nyuklia kumaanisha mtoto anahitaji taarifa za nje kwa kupitia seli za mama zisizo na nyuklia.

Watoto wengi siku hizi huwa na Vichwa vyenye Maumbile Mabaya, sababu kubwa ni Kuathiriwa kwa mfumo wa taarifa wa Mtoto wa muda sahihi wa kufunga jointi za kichwa chake. Jointi zinapofungwa kabla ya wakati, Ubongo unapokuwa mkubwa hupelekea kichwa kutanuka aidha kwa mbele kama jointi za ‘’Corona sutures’’ ziliwahi kufunga. Na kichwa kutanuka kuelekea pembeni, kama jointi za ‘’sagital sutures’’ ziliwahi kufunga. Haya yote ni makosa ya mitindo mibaya ya maisha.

Ipi ni Zawadi Kubwa kwa Mke wako Mjamzito?


Kama mwanaume anatakiwa kumpa zawadi kubwa mke wake mjamzito, basi ni kumuonesha Upendo. hakuna kitu kibaya kwa mjamzito kama Stress. Na hii ndiyo sababu, Wanawake wengi hujikuta wakiishiwa maziwa kabisa ya kunyonyesha watoto wao wanapozaliwa.

Mwanamke anapokuwa katika ujauzito huwa anaingia katika mabadiliko makubwa sana ya kihomoni. Mabadiliko haya humpelekea kuwa na kiwango kikubwa sana cha homoni kama za Progesterone ‘’PGs. Homoni hizi katika Ubongo huwafanya kuwa kama watumiaji wa madawa ya kulevya. Ubongo hufanya hivi pia kwa kuwa unatambua, Mwanamke mjamzito huwa ana stress nyingi sana zinazotokana na homoni za Cortisol zinazotoka kwa mtoto wake, mabadiliko ya mwili pia huufanya hata ubongo wake kupungua kwa size ‘’Volume’’, haya yote humfanya kuwa katika hali mpya ya ulimwengu.


Kiwango kikubwa cha homoni za cortisol kwa mjamzito humfanya kuhitaji sana vitu vya kumliwaza. Na hii ndiyo sababu ya wajawazito baadhi kuwa na tabia za ajabu, ambapo wengine huwa na hasira sana, wengine hula sana, n.k. Wanaume wanapaswa kutambua kuwa ni wajibu wao kuwaliwaza wake zao kwa kuwa na ukaribu nao sana, kuwasikiliza, kupata muda mwingi wa kujadili kuhusu mtoto wao, na hata kufanya sex kama itabidi. Haya yote yanalenga kuurejesha mfumo wa mwili kutulia ‘’PSNS’’.  Mfumo huu unapokuwa imara mwili wa mama huanza kuzalisha Maziwa yakutosha, kupitia kusisimuliwa kwa homoni za Prolactin toka mfumo wa HPG’’.

Je Mtoto Anasikia akiwa Tumboni?

Mtoto anasikia lakini haelewi maana ya maneno. Hili wala halina ugumu kulielewa, Mbwa haelewi Lugha za binadamu, ila anajua hali ya Mpendwa wake. Ni vyema sana Madaktari kufundishwa ‘’Quantum Physics’’ ili waweze kutambua kuwa, Ubongo wa Mama, na Ubongo wa Mtoto, na Mioyo yao wote, Ipo katika Balansi ya Mfumo wa Nishati ya Umeme sumaku ‘’Resonant Vibrational Energy’’. Hii balansi ndiyo huratibu mfumo wa mawasiliano ya mwili wa mama na mtoto, na mfumo huu unapokuwa imara kimawasiliano ‘’Coherent’’, basi matokeo yake ni Uimara wa Afya ya mama na mtoto. Unaweza gundua tatizo katika Mfumo wa moyo wa Mama kwa kupima mawimbi haya, kama inavyofanywa hospitalini kwa kutumia ‘’ECG’’, au ‘EEG’’ kwa Ubongo.

Mama anapokuwa katika stress, kupitia uhusiano mkubwa uliopo kati ya Ubongo na Moyo. Zipo seli za Ubongo ‘’Neurons’’ zaidi ya 40,000 zinazotoka kwenye Moyo kwenda kwenye Ubongo. Kumbuka Ubongo ndiyo unapokea damu nyingi zaidi toka kwenye Moyo, na kemikali ya Oksijeni toka kwenye Damu, ina tabia ya Usumaku ‘’Paramagnetic’’, Huu mfumo upo umeungana ‘’Entangled’’, na hii ndiyo sababu unaposhtuka tu, au sisimka, Moyo husisimka sambamba na taarifa katika Ubongo, haiitaji Taarifa za polepole za safari za Mabadiliko ya kemikali za Neva ‘’Action potentials’’ kama wanavyofundishwa wanafunzi wa Biolojia. Hii ina maanisha, Kwa Maumivu yeyote ambayo mama anaweza pitia, Na mtoto wake huyahisi mara moja, na vivyo hivyo kwa furaha.

Mama anapokuwa na huzuni sana, mtoto wake huanza kuathiriwa kabla ya kuzaliwa. Watu wengi sana ambao Mama zao waliwazaa wakipitia hali ngumu, huja kuwa na tabia za upekee sana. Na hii inatokana na hali ngumu ambazo huanza kuzipitia pasipo kuzielewa zina maana gani.