KATAA LADHA BANDIA ZA VYAKULA
LADHA BANDIA ‘’artificial flavours’’
Ladha sitaizungumzia sana kama tulivyokwisha izungumzia kwa sehemu zilizokwisha pita. Ladha ni mjumuisho wa kemikali na harufu zilizopo katika chakula au kitu. Kwa mfano Ladha ya Limao hutokana na chembechembe za asidi ya ‘’citric acid’’.
lakini pia, huambatana na harufu nzuri ‘’aroma’’ ambazo huambatana nayo. Limao sio matokeo ya Citric acid tu, limao lina kemikali nyingi sana mfano: Maji, Sukari ‘’glucose, fructose na sucrose’’, Vitamin C ambayo pia huitwa ‘’ascorbic acid’’, Vitamin B ambazo kuna B1 ‘’thiamine’’, B2 ‘’riboflavin’’, B3 ‘’niacin’’, B5 ‘’pantothenic acid’’, B6 ‘’pyridoxine’’ na B9 ‘’folate’’.
Kuna Madini Mfano; ‘’Potassium, Calcium, Magnesium na kiwango kidogo cha Iron na Phosphorus’’. pia kuna ‘’flavonoids’’, kuna Mafuta. Mfano, ‘’Limonene, Pinene, Terpenes. Pia kuna Polyphenols, hizi hulitunza limao kwa kuondoa oksijeni ‘’anti oxidant’’, pia kuna Pectin, hizi ndiyo zile hufanya juisi kuwa nzito nzito, hizi ni kambakamba au ‘’fibers’’ ambazo huyeyuka, kuna Organic acid zingine kama ‘’malic acid’’, kuna chembechembe za Protini au ‘’amino acids’’, kuna Carotenoids hizi zipo kidogo ila zipo, ndizo zile za rangi, kuna chembe za Harufu ‘’volatile compounds’’ hapa zipo mbalimbali ila ni makundi ya ‘’aldehydes na ketones’’.
Limao hili la asili lina viwango maalumu mfano:
Nishati-22 calories
Maji-89%
Protini-0.3g
Wanga-6g
Mafuta-0.2g
Vitamini C-38.7mg ( hii ni asilimia 43% ya kiwango kinachohitajika na mwili cha vitamin C kwa siku)
Potassium-103mg
Na zinginezo nyingi zaidi kuweza kuziorodhesha.
Sasa unaweza pata picha namna Ladha za vitu vya asili zilivyo Complex na zinaonesha utaalamu mkubwa sana katika uundwaji wake. utengenezaji wa Ladha hakuna namna ya kuuelezea zaidi ya kurejea maajabu ya uumbaji wa Mungu katika siku ya tatu. Hii ni kwa sababu mtu anayeamini Mabadiliko ya viumbe kama yanaweza leta Ladha hizi, hawezi kujibu kwanini malimao yote tokea sehemu mbalimbali duniani yaliamua yaishie kwenye Ladha hii iliyo standard ya malimao yote leo duniani? Yaani kipi kiliyakwamisha yasiendelee! mengine yakawa na asilimia ambazo zikabadilisha kabisa mtazamo wetu juu ya Ladha za limao? Hii Maana yake ni kuwa, tayari yaliumbwa yawe na Ladha hii tu.
Sasa basi, kutokana na ukuaji wa teknolojia ya Bioteknolojia za Molekuli, hizi ni teknolojia za kuweza kuona hata molekuli ndogo, na kuweza kutumia tabia za matendo ya kikemikali ya molekuli hizi ili kuweza kuunda matokeo mfanano au unayoyataka. Teknolojia hii imefungua njia ya kuweza kuiga miundo kadhaa ya vitu vya asili, mfano, kupitia kuona hizo takwimu za jumla ya chembechembe za limao, basi imekuwa rahisi hata bila kutumia limao, mtu kuweza kuchukua hizo chembechembe na kuziunganisha, na kuunda kitu mfanano kabisa na Limao. Na hiki ndiko kiwanda cha ‘’Vitia Ladha vya Kisasa’’.
MAAJABU YA KUFELI KUUNDA VITIA LADHA VYA KISASA
Ingawa ilitegemewa labda itawezekana kuunda kemikali moja kwa moja sawa na zile za asili. lakini uhalisia wake ni kitu kisichowezekana kabisa. Kwanza kutokana na Complexity ya mahesabu ya Ladha za asili. kuunda hiyo Ladha ya limao, kuna maelfu ya chembechembe ambazo zinahitaji maelfu ya mahesabu, na sio kuchanganya changanya tu. kuunda Ladha mfanano kabisa na limao tu, mahesabu yake yameshindikana, halafu kuna msomi mmoja anaamini kuwa Ubongo uliumbwa kwa mabadiliko, kama ungeulizwa hivi kweli usomi ni maarifa, ungejibuje? Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa.
Kuunda Ladha mfanano kabisa na vitu vya asili haiwezekani kwa sababu, Mabadiliko ya chembechembe zile ni kidogo Sanaa, na badiliko la kiwango kidogo sana hubadilisha kabisa Ladha. Hii ni sawa na hoja ya awali ya kuwa, mahesabu yake ni magumu kuyafuatisha. chembechembe zilizo kwa uchache sana, ambazo pia huwa hazipatikani kwa urahisi, huleta mjumuisho wa Ladha ya mwisho, na hivyo, kuhitaji utaalamu mkubwa sana na malighafi.
Mpangilio wa chembechembe ambao huitwa ‘’Stereochemistry’’ ni shughuli ngumu sana. Hii inahusu zaidi Mchanganyo utakaaje? Mpangilio wa asili wa molekuli huwa na maumbo magumu kuyaiga. kwa kuwa, utaalamu wake ni mkubwa sana kuweza kuufatisha. Ladha hujumuisha matokeo ya mazingira husika Kama joto, udongo, ulimaji n.k, na haya yote katika maabara hayawezekani, Mwisho na kubwa pia, Ladha ya kitu sio matokeo ya kemikali tu, bali na harufu. Ambazo nazo zipo kwa mahesabu yake maalumu. Hivyo kuunda Ladha za kisasa ni vigumu kwa kupungukiwa uwezo wa kitaalamu, na uwezo wa kutawala matendo yote yaliyopaswa kufatiliwa katika uundwaji mzima, hii kiufupi tu ina maanisha kupungukiwa utaalamu.
VITIA LADHA VYA KISASA
MFANO LADHA ZA KISASA NA LADHA ZINAZOFANANIA
Kemikali hizi zote ndizo zilizojaa kwenye mabidhaa ya kisasa Kama vile ice cream za kisasa, Yoghurt, Biskuti, pipi, Ladha kwenye maziwa, Juisi, vitafunwa vitamu vya aina mbalimbali za kisasa n.k
Pia kuna udanganyifu kwa baadhi ya makasha ambayo yanaonesha kana kwamba kuna ‘’Natural flavours’’, uongo huu sio wa kweli, na unaficha madhara hatari zaidi ya kemikali ziletazo madhara kama za ‘’Monosodium Glutamate’’ .
VICHOCHEA LADHA ‘’flavour enhancer’’ MONOSODIUM GLUTAMATE. ‘’MSG’’
Hizi ni kemikali ambazo huwekwa kwenye vyakula ili kuongeza msisimko wa Ladha. Hizi kemikali huenda kuongeza msisimko wa sensa, au receptors za kuhisi Ladha za utamu wa umami. Umami ni yale mageti yaliyokuwa ya T1R1/T1R3 yaliyokuwa yakihisi Ladha za protini. kama vile nyama. Kwa hiyo, hizi kemikali ambazo huwa kwenye vyakula vingi. Mfano, supu mbalimbali na vyakula kama katika Picha hapo juu, hufanya mtu kuhisi Ladha zaidi anapokula chakula.
Kundi hili la vichochea Ladha, halina MSG peke yake , zipo kemikali zingine kama ‘’ribonucleotide disodium inosinate’’ pia kuna ‘’disodium guanylate’’. Matumizi ya monosodium glutamate ni makubwa sana. kwa mfano, huzalishwa zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka kwa takwimu za marekani.
MADHARA YA VICHOCHEA LADHA NA LADHA ZA KISASA KWA AFYA
MADHARA KWA UBONGO
Monosodium glutamate ‘’MSG’’ inatambulika kuwa sumu kwa seli za ubongo ‘’Neurotoxin’’. Hii inatokana na tabia ya msg kuharibu nyuklia mojawapo ya ubongo inayoitwa ‘’Arcuate nucleus’’. kama ilivyofanyiwa utafiti kwa panya. Nyuklia hii ipo kwenye sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Hypothalamus’’. Nyuklia hii kazi yake kubwa hufahamika kama kitovu cha matendo ya kibiolojia ya kuwezesha utendaji sahihi wa homoni, nishati, na virutubisho vya vyakula.
MSG hubadilishwa na kuwa ‘’glutamic acid’’. Ambayo kama tulivyoiona kwa sehemu zilizopita, huwa na tabia ya kusababisha msisimko wa seli za ubongo. ambapo tuliona ilikuwa ikiathiri utendaji wa geti la ‘’NMDA’’, ambalo tuliona lilikuwa la muhimu sana katika kushughulika na kutengeneza kumbukumbu Pamoja na kujifunza.
Baadhi ya watumiaji wa ‘’MSG’’ wamewahi kuripoti kutokewa na hali kadhaa kama vile, ‘’Kukakamaa kwa sura, misuli ya kifua, kuhisi maumivu kama ya kuwaka moto katika sehemu ya juu ya mwili, Pamoja na maumivu ya kichwa. Na tatizo hili kwa China huitwa ‘’Chinese restaurant syndrome’’, limeitwa hivi kutokana na mazingira yake ya utokeaji wake kwa mara ya kwanza china.
MSG imeonekana kuhusiana na matatizo mengi ya mfumo wa ubongo wa matendo yasiyo ya hiari, mfumo unaoitwa ‘’Sympathetic nervous system’’. Na madhara yake makubwa kabisa yamekuwa ni Pamoja na Kuhisi kizunguzungu ‘’dizziness’’, ambayo hii inahusisha sehemu nyingine nyingi za ubongo za juu, Kuharisha, hali ya kichefuchefu, na maumivu ya tumbo. Pia kwa panya waliopewa kwa muda mrefu, walionesha mishtuko mingi kwenye mabega, ambayo ilikuwa ni rahisi kuchanganya na mishtuko ya kifafa ‘’epilepsy’’.
Pia kuna madhara ya sumu hizi ‘’neurotoxins’’. Ambayo yamekuwa yakiathiri hata mfumo wa homoni wa mwili ‘’endocrine system’’, na hii imepelekea shida ya kupungua kwa homoni za ukuaji, homoni za Prolactin zinazohusiana na matendo mengi ya uzazi, kama uzalishaji maziwa, na kupungua kwa homoni za kijinsia ‘’sex hormones’’.
Matumizi ya hivi vitu yanapaswa kutupa mashaka sana. Na kutumia aina nyingine ya ‘’Protein hydroxylates’’ ni hatari zaidi, maana hii huusiana na kiwango kikubwa zaidi Cha ‘’Glutamate’’.
MADHARA KWA UPANDE WA LADHA ZA KISASA
Nyingi ya hizi kemikali za Ladha za kisasa kama zile vanilla wanazozipenda wengi. Mwilini huwa ni mithili ya vitu vigeni, na kwakuwa haziwezi kumeng’enywa na enzymes za mwili, basi moja kwa moja hutambuliwa na mwili kama sumu za mwili. Huko mbele nitaeleza kwanini mara nyingi, kuna uhusiano wa ongezeko la uwezekano wa mashambulizi ya saratani, ‘’carcinogenicty’’, na utumiaji wa bidhaa hizi. Hebu tuangalie taarifa zilizopo juu ya madhara ya utumiaji wa bidhaa hizi za Ladha za kisasa, au artificial flavours.
HUATHIRI TABIA YA MTINDO WA KULA ‘’KIAKILI’’ NA KUPELEKEA URAIBU WA CHAKULA ‘’addiction’’
Kumbuka umeudanganya ubongo. mfano, umeuambia kuwa umekunywa juisi ya chungwa, na kumbe sio kweli chungwa, ila tu ni kemikali zenye Ladha ya chungwa. Sasa basi, Ubongo huwa ukitambua kuwa kila chakula huusiana na virutubisho vingine vingi sana vinavyohusiana na hiko chakula. Kwa hiyo, unapotumia basi Ubongo huchochea zaidi utumiaji wa juisi hii feki, ukiamini utapata virutubisho vingi zaidi kama vile vitamini na vinginevyo, lakini madhara yake, Ubongo huambulia tu kujijazia sumu.
Hii ni sawa na ningesema binti anayemkubali kijana kwa kuamini atapata pesa zake, na kumbe huyo kijana hana pesa yoyote, anaigiza tu, na hatima yake binti anaishia kujijazia tu hatari za magonjwa ya zinaa. Kwa hiyo Ubongo huchochea mapenzi yake juu ya juisi hizi, au biskuti, au vitafunwa, ukiamini utapata faida kubwa zaidi ya virutubisho, na hii hali hupelekea matumizi makubwa sana ya hizi kemikali za Ladha za kisasa.
Matumizi haya makubwa ya Ladha za kisasa, husababisha misisimko mikubwa sana ukilinganisha na kemikali za asili. hii ni kwa kuwa, kemikali hizi hutengenezwa kwa lengo la kibiashara. Na pia ili kuchukua mapenzi yote ya mtu juu ya bidhaa husika. Hapa kuna siri kubwa sana ya kuweza kuteka akili ya mtu na kusababisha uraibu.








Join the conversation