Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

KATAA ENERGY DRINK❌🖐️

Energy Drink ni hatari Kwa afya, ni Sumu Kwa afya ya Moyo, Ubongo, na nishati ya mwili.

 JE WAJUA MAAJABU YA ENERGY DRINK:


Energy drink karibia zote Zinajazwa Vifuatavyo;

  • Caffeine: kisisimuaji Cha Ubongo kinachotengeneza hisia ya kusisimka.
  • Sukari/Sweeteners: zinatengeneza hisia za utamu (mfano., sucrose, glucose, aspartame).
  • Taurine: ni protini wanayoamini inasaidia kuwezesha sukari ivunjwe haraka.
  • Vitamini B: (B3, B5, B6, B12) wanaamini zinasaidia metaboliki za kuzalisha nishati
  • Mabaki ya Mimea kadhaa: Ginseng, ginkgo, biloba, guarana (inaongezea caffeine). Hizi Kwa lugha nyepesi ni kama visisimuaji vya asili.
  • Glucuronaloctone: inahusiana na matabolikia za glucose.
  • L-Carnitine: hii protini wanaamini inasaidia kivunjavunja mafuta.

Hatari!

Mtu mmoja anaekunywa chupa moja tu, tena kale kadogo ka 500mls ka Energy drink. ni sawa na mtu anaekunywa juisi yenye Vijiko 14 mpaka 16 vilivyojaa sukari!! 

Ubongo huona hii hatari na kuanza mpango wa kurekebisha mfumo wa kuhisi sukari, na Dopamine huzalishwa kwa kiwango kikubwa sana, kwa maana hii ni zaidi ya mhemko au Reward ya kawaida. Hii shida hupelekea matatizo kwenye Moyo, mfumo wa damu, n.k. kama tutakavyoendelea kulitazama tatizo hili.

Tafiti zinaonesha kuharibiwa kwa Ubongo Kwa unywaji wa Energy Drink, na hii ni kupitia kuathiriwa Kwa uzalishaji wa vitoa taarifa, homoni, na kemikali za ubongo au ‘’Neurotransmitters’’. Pia hupelekea ongezeko la uwezekano mkubwa wa matatizo ya umakini, au ‘’attention deficit disorder’’.

USILOJUA KUHUSU ENERGY DRINK!

Haziongezi nishati yeyote mwilini, zinachofanya ni kuchochea msisimko katika Ubongo, na misisimko hiyo huusiana na kusisimuliwa Kwa mapigo ya Moyo, na ndiyo maana Kuna ushahidi wa Moja Kwa Moja wa unywaji wa Energy Drink na kuongezeka Kwa mapigo ya Moyo Kwa wiki nzima hata kama mtu atakunywa chupa Moja tu.

Energy Drink pia Zina kemikali nyingi ambazo wanakemia wamezijaza kana kama Zina mchango katika matabolikia za mwili, lakini ukweli ni kuwa huishia TU kuwa kama kemikali sumu zingine. Nyingi zake hazisaidii chochote, hazina ushahidi zaidi ya takwimu za Randomized trials ambazo nyingi zimejaa Maslahi ya kibiashara. 

Mtumiaji wa Energy Drink baada ya muda lazima atapata changamoto za Moyo, shida za Ubongo, na hii ni kutokana na kuathiri balansi ya metabolikia za sukari na mfumo wa damu, vitu ambavyo ni msingi wa fiziolojia zote za ubongo.


SARATANI NA AFYA YA MFUMO WA CHAKULA KUTOKANA NA LADHA ZA KISASA

Kemikali kadhaa za Ladha mfano moja inayoitwa ‘’diacetyl-2,3-pentanedione’’ ambayo huwa na ladha kama ya butter, au fananishia na zile za kwenye wine, na hata beer nyingi. Kemikali hii imeonekana kuwa na hatari au risk kubwa ya kupelekea saratani ya mapafu. Hii ilichapishwa na ‘’international journal of occupational and environmental health’’.

Taarifa nyingi za risk za saratani, na matumizi ya hizi kemikali za Ladha za kisasa, bado zinafanyiwa kazi au utafiti. Na hii inatokana na mashaka makubwa sana juu ya hivi vitu.

Tatizo la saratani linatokana hasa na tabia ya hizi kemikali kupelekea madhara ya moja kwa moja ya sehemu za msingi za ndani za seli. mfano kuwa sumu, au kuongeza kiwango kikubwa cha chembechembe za uharibifu zinazoitwa ‘’free radicals’’. Hizi huathiri seli za mwili mpaka kiini cha ndani chenye DNA. ambapo huko kuna chembechembe nyingine nyingi zinazoshughulika na kutawala uundwaji wa kila seli na tishu ya mwili kama inavyopaswa. 

Haya madhara ni kama ambavyo ikitokea umeharibu jiko, basi mapishi yote lazima yataleta kitu cha tofauti, na hicho kitu ndicho saratani. Lakini pia saratani hutokea kutokana na tabia ya hizi kemikali kudidimiza mifumo ya seli za kinga za kujilinda, na kurekebisha matatizo yanayotokea kipindi cha uundwaji wa kijenetikia. Mfano kazi za seli ‘’Cytotoxic T cells’’ ni kuua seli za saratani. Na hizi kemikali huathiri mfumo huu wa kinga na kupelekea seli hizi za saratani ziendelee kukua.

Kemikali katika Energy Drink huwaathiri na hata kuwaua viumbe hai kama bakteria wa tumboni. hata bakteria wa tumboni nao huzidiwa na hizi sumu na hawana namna ya kujikinga nazo. Maana huwa wakitutegemea kama chanzo cha virutubisho, na hivyo unavyowapa kemikali hizi, ni sawa na unajipa dawa ya kuwamaliza. Utakapoathiri huu uhusiano, au ‘’eubiosis’’, basi utapelekea madhara katika mfumo mzima ule nilowahi utaja wa ‘’Microbiome-gut -brain axis’’.