HATARI YA MAJI NA VINYWAJI BARIDI SANA 🧊🍹🥂❌
MADHARA YA VINYWAJI BARIDI SANA
Watu wengi wanakunywa vitu vya baridi kali sana mithili ya barafu. watu hawa hukata kiu mara moja bila wao kujua kwanini? haya yote ni matatizo madogo kwa mtu asiye fahamu, lakini ni hatari sana. Hebu tuangalie nini hasa hutokea mtu anapokunywa maji ya baridi kali sana, au barafu.
SAYANSI YA KUHISI KIU YA MAJI
Mtu anapokuwa na kiu ya maji hupitia mfululizo wa matendo. Kiufupi unapokuwa na kiu ya maji hasa huwa kuna mambo mawili; kuna ongezeko kubwa sana la kiwango cha chumvi au sodium katika damu, au kuna upungufu wa kiwango cha maji katika mishipa ya damu. Hizi hali zote mbili ndizo vitoa taarifa ya kuwa mtu ana kiu ya maji.
Tatizo hili huanza kugunduliwa katika figo ambako huko kuna vichujaji vya damu, ambavyo huwa na sensa za kujua mabadiliko ya kemikali katika damu au ‘’osmoreceptors’’. Ambazo kwa figo zipo kwa seli zinazoitwa ‘’macula densa’’, na figo hupima pia mabadiliko ya presha ya damu kupitia sensa za Presha ‘’baroreceptors’’ katika seli za ‘’juxtaglomerular ‘’. Ambazo huwepo katika mshipa wa damu unaoleta damu kuingia kwa figo ‘’afferent arteriole’’.
Hizi sensa zote mbili baada ya mtu kupata kiu huanza kuzalisha kemikali inayoitwa ‘’renin’’. Kemikali hii huingia kwenye damu mpaka itakapo kutana na kemikali mwingine anayeitwa ‘’angiotensin I’’. renin humbadilisha enzyme huyu kuwa angiotensin II. Ambaye husambaa kwenye damu mpaka atakapoelekea kwenye kichwa au ubongo. Angiotensin II kabla ya kuingia kwenye ubongo hukutana na geti katika ubongo la BBB au ‘’blood brain barrier’’, pale hukutana na kikundi cha seli au ‘’clusters of cells’’ za makundi makubwa mawili yaani SFO au ‘’subfornical organ’’ na OVLT au ‘’organum vasculosum of lamina terminalis’’.
Hizi seli zenyewe zikishamuona huyu angiontensin II hujua tu kuna shida ya maji, na huwasiliana na sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus. Huzungumza na nyuklia moja ya hypothalamus inayoitwa ‘’median preoptic nucleus’’ na kumwambia kuhusu ANGII. ambapo sasa huyu MPO huanzisha tabia za kutafuta maji.
Angiotensin II huenda na kwenye Tezi kuu upande wa nyuma ‘’posterior pituitary glands’’, na huko humchochea homoni anayeitwa ‘’Vasopressin au Antidiuretic hormone’’, huyu yeye hurudi kwenye figo na kuzuia maji yasitolewe, lakini pia huongeza mgandamizo katika mishipa ili kusaidia kubalansi presha ya damu hata kama kuna upungufu wa maji. Pia huwa kuna homoni nyingine ambayo nayo huwa ikisisimuliwa, huitwa aldosterone. Hii huchochea madini ya sodium kufyonzwa kurudi kwenye figo yasitoke kwa njia ya mkojo.
Zipo sehemu nyingine zinazohusiana na swala hili, hasa ni sensa zingine za kugundua kushuka kwa presha ya damu kwenye mishipa ya damu ‘’arterial baroreceptors’’. Pamoja na sensa za kugundua kushuka kwa kiwango cha ujazo wa damu katika ubongo sehemu ya medulla oblangata. Sensa hizi huitwa ‘’cardiopulmonary receptors’’. Sensa hizi zote zikigundua tatizo hili la uhitaji wa maji hutuma taarifa Kwenda ndani tena katika ubongo, katika eneo linaloitwa ‘’area postrema’’ na ‘’nucleus tractus solitarius’’, huku hufanya kazi moja kubwa ya kusambaza taarifa Kwenda katika kila sehemu ya ubongo, kutaarifu kuhusu swala la maji na kuanzisha mkakati wa kupata maji.
SAYANSI YA HATARI YA KUNYWA MAJI YA BARIDI KALI SANA AU BARAFU
Madhara ya upoozaji; maji yakiwa ya baridi sana hupooza mdomo na koo kwa haraka sana, na kumbe ubongo umeshazoea hiyo hali utaifikia baada ya kunywa maji mengi. Kwa kuifikia kwa haraka sana hiyo hali, hamu ya maji hukata ghafla maana Ubongo hukadiria kiasi Cha maji Kwa kutumia pia sensa za jotoridi. Ubongo umeumbwa kujua viwango vya maji ya hali ya hewa ya kawaida na sio baridi kali. Ni kama una mahesabu ya pikipiki halafu wewe unaupatia baiskeli, madhara yake ni kuwa unadhani umefika kumbe bado.Changamoto ya umezaji. maji ya baridi huathiri sana umezaji na misuli ya koo la chakula. Hii ni kama wewe ukishika kitu cha baridi sana baada ya muda utajikuta auhisi kitu. Na ndivyo hii misuli pia, hupoteza mahesabu ya maji, na huisi yameshapita mengi sana, na kuwa sasa yanatosha, kumbe bado mtu hajanywa ya kutosha. Hii inahusiana na Changamoto ya Neva za fahamu. Kilichokuwa kinapaswa kupeleka taarifa kuhusu kiwango cha maji yaliyopita mdomoni umekishtua kwa baridi kali mpaka kimehisi kimepitiwa na maji mengi sana, na sasa kinapeleka taarifa kuwa kiwango cha maji sasa kimetosha.
Changamoto ya nishati. Taarifa hutoka tumboni Kwenda kwenye ubongo kusema, kuna shida ya baridi kali sana tumboni kutokana na maji Baridi na mengi sana. Na ubongo huisi changamoto ya maji imeisha na imebakia tu changamoto ya baridi, swala hili hupelekea mwili kuanza Tena kutumia nishati kuongeza Joto la tumboni, hili hupelekea kupotea zaidi Kwa maji ili Hali mtu alikuwa bado ana kiu ya maji.
Changamoto ya tumbo. maji Baridi sana tumboni hulisababisha tumbo kujikunyata kama mtu anavyojikunyata akipatwa na baridi. Na hali hii ya kujikunyata hufanya kiwango kidogo cha maji yaliyopo tumboni kuwa kana kama ni kikubwa sana kiasi kwamba ubongo kuhisi hakuna changamoto tena ya maji.
Sababu hizi zote kwa Pamoja zinazungumza neno moja tu, kuuchezea ubongo Au udanganyifu wa milango ya fahamu.
Kumbuka..
Zaidi ya asilimia 60-75% ya uzito wa watu ni maji. Hakuna namna ya kuelezea umuhimu wa maji kwa maana maji ndiyo uhai wenyewe, hata dunia na vyote vilivyomo vilianza kuumbwa na Mungu kutoka kwenye maji. Maji ni ya msingi sana, idadi kubwa sasa ya watu wanakimbilia bidhaa za baridi sana kwa kufurahia misisimko kama ile niliyokwisha ielezea awali namna inaua watu. Inasikitisha sana Kuna wale ambao wao hupenda hata zile juisi zilizo barafu kabisa wasijue namna zilivyo hatari kwa afya zao.
MADHARA YA KULA CHAKULA NA KUNYWA VINYWAJI BARIDI SANA
Mfumo wa chakula hupata shock. Haya ni madhara unapokula kitu cha baridi sana hata mwili unashindwa kukivumilia. Mwili huchukua hatua nyingi za kutengeneza joto kama mtu ambavyo angetetemeka anapopigwa na baridi kali, na madhara yake kwa mfumo mzima wa chakula ni shock.Kupungua kwa uwezo wa mwili kupata maji. Hii ni kwa sababu mwili hutumia muda mwingi sana kutengeneza joto ili kupooza ubaridi kuliko kuja kuyachukua maji.
Maumivu ya kichwa ‘’migraine’’, hii huwa na sababu nyingi lakini mojawapo ni zile za juu zilizokuwa zikitokana na changamoto za ubongo na maji ya baridi.
Husababisha kufeli kwa mmeng’enyo bora wa chakula na ufyonzwaji wa virutubisho. Hii ni kwasababu siku zote kunapokuwa na baridi kali mishipa ya damu huingia ndani zaidi ya mwili, kitendo cha kuingia ndani kabisa hupelekea chakula kushindwa kufyonzwa vizuri zaidi kama ambavyo kingefyonzwa kusingekuwa na baridi kali.
Huathiri uvunjwaji wa chakula. Siku zote vimeng’enyaji vya chakula ‘’enzymes’’ huwa vinafanya kazi katika nyuzi joto maalumu, na hivyo Baridi kali sana huathiri utendaji wake na umeng’enywaji wa chakula kwa ujumla.
Huleta madhara katika mapigo ya moyo. Hii hutokana na tabia yake ya kusisimua mshipa wa neva ya kumi ya ubongo, au ‘’vagus nerve’’, Tumbo husababisha mishtuko ‘’reflex’’ Ambayo hushusha mapigo ya moyo, hupelekea kizunguzungu n.k
Ugandishwaji wa mafuta. Ni kama unavyoona supu ikipoa inavyoganda. Ndivyo ilivyo pia kwa mafuta uliyokula tumboni ikitokea umekunywa kitu cha baridi sana, mafuta huganda na kusababisha ugumu zaidi katika kuvunjwa vunjwa na mwili.
Kama Asili ingehitaji Barafu, ungeiona ikitamalaki..






Join the conversation