KIMBIA RANGI ZA KISASA
RANGI ZA VYAKULA ‘’FOOD DYES’’.
Hizi ni kemikali zinazowekwa kwenye vyakula ili kuvipatia rangi za kuvutia. Mara nyingi rangi hupendezesha mwonekano wa chakula. Kwa asili vyakula vinapokuwa vikiiva huwa vinabadilika rangi, na kuwa rangi inayopendezesha macho, na pia, kuashiria ukomavu wake. Mabadiliko ya rangi ni mabadiliko ya kikemikali, yanayopelekea kuundwa kwa chembe zenye mwonekano mpya, tofauti na wa awali.
Mabadiliko haya huchochewa na hali za hewa kama jotoridi, oksijeni, vimeng’enyaji au enzymes, na hata viumbe wadogo, na mwanga. Kwa asili, vyakula vingi huwa na rangi za aina za kufanana Ambazo ni njano,rangi ya chungwa na nyekundu. ni mara chache sana utaona vyakula vikiiva na kuwa na rangi ya Bluu. kwa kuwa, rangi zile hupendelewa kwa asili yake yakuweza kuonekana sana. Na vyakula vyake vya ndani, mara nyingi huwa vyeupe, na sio vyeusi.weusi huambatana sana na vitu visivyoliwa kama mbegu. Hivyo ndivyo ubongo wa Wanyama ulivyo kwa asili ukivutiwa pia kwa hizo rangi za chakula.
UONGO WA KWANZA WA AKILI
Ubongo wako ukiona rangi ya njano au ya chungwa au nyekundu, huamini kuwa hilo ni tunda zuri lililokwisha kukomaa, na linapaswa kuliwa. Lakini kumbe hapa linapatiwa rangi tu isiyo ya asili, na wala haimaanishi kabisa ukomavu wa chakula.
KWANINI VYAKULA VINABADILIKA RANGI VIKIKOMAA?
Jiulize kwanini ndizi yako huwa ya njano ikikomaa, au kwanini nyanya huwa nyekundu. au kwanini mizabibu huwa na rangi ya wekundu wa damu ya mzee n.k. jibu ni kuwa, siku zote matunda haya huwa yanakuwa na rangi za awali. Ambazo zinachochewa zaidi na uwepo wa kemikali zinazoitwa ‘’Chrolophyl’’. Hizi huchangia sana kwa ile rangi ya awali ya ukijani.
Lakini pia yapo matunda ambayo yanapokuwa mabichi huwa hayana rangi ya kijani, sababu huwa hapahapa ikijikita katika tofauti za viwango, aina, na miungano na kemikali zingine. Na kadri muda unavyozidi Kwenda, na tunda likizidi kukua, mfumo wa homoni unaoongozwa na homoni moja ya mmea inayoitwa ‘’Ethylene’’ huanza kuzalishwa zaidi, kama inavokuwaga kwa homoni za uzazi kwa mtu anavyozidi kupevuka. hii hutawala mabadiliko ya kikemikali kwa kuhamasisha kuvunjwa kwa zile kemikali ‘’Chrolophyll’’ kwa kupitia enzyme inayoitwa ‘’Chrolophyllase’’. Na homoni hii hufanya kazi sana tunda linapokuwa limekwisha komaa. Ni kama enzyme ‘’rennin’’ inavyofanya sana kazi baada ya mtoto kuzaliwa, na kuanza kunyonya.
Sasa kitendo cha Chrolophyllase kuvunja ile chrolophyll husababisha ‘’kemikali zingine au pigments’’ zianze kuonekana. Na hapa hasa, huwa ni kemikali zinazoitwa ‘’Carotenoids’’. ambazo hizi, ndizo sababu kubwa ya rangi za njano, au mfanano wa njano kutokea, baada tu ya tunda kukomaa. Mfano kwenye maembe, ndizi n.k.
Lakini pia hata bila kubadilika sana kwa baadhi ya matunda, unaweza kuyatambua yakikomaa kutokana na kupungua kwa rangi zake za kijani ya asili, na hii ni kutokana na kupungua kwa chrolophyll. Pia zipo kemikali zingine ambazo hutokeza baada ya kuvunjwa kwa chrolophyll, nazo hizo huitwa ‘’Anthocyanins’’. Hizi ndizo hupelekea rangi za wekundu, bluu, na papo ‘’purple’’. Mfano, kwenye mizabibu,mazambarau n.k. lakini pia, huwa kuna kemikali zingine zinazoitwa ‘’Betalains’’. Ambazo, huwa na rangi za njano na wekundu. Kwa Pamoja kemikali hizi na zingine chache, hupelekea tuone vile tunaona kwa matunda mengi. Tazama hii picha, na kisha uone Mungu alivyo wa ajabu.
RANGI HUISHIA WAPI MWILINI?
Rangi zote za asili huvunjwa vunjwa na mwili na kuleta virutubisho ndani ya mwili. Mfano, mwili huwa na vimeng’enya au enzymes zinazoitwa ‘’Carotenoid Oxygenases’’. hizi huusisha enzymes kama vile ‘’Beta-carotene 15,15’-dioxygenase’’ ambazo huzivunja zile rangi za njano za beta-carotene, na kutengeneza Vitamini A mbili zinazoenda kusaidia Jicho. Zipo pia nyingine za carotenoid kama ‘’Beta-carotene 9’,10’-dioxygenase’’ ambazo hizi huvunja zile rangi za njano.
Rangi nyekundu zinazosababishwa na Anthocyanins, huvunjwa na vimeng’enyaji au enzymes zinazoitwa ‘’Glycosidases’’ mfano, moja huitwa ‘’Beta-glucosidase’’. hii huvunja ule wekundu na kuzalisha chembe za sukari. Pia kuna ‘’Beta-galactosidase’’. hizi huvunja ule wekundu katika ‘’anthocyanins’’, kutokana na kuvunja mhimili wake unaoitwa ‘’glycosidic bond’’. Pia zipo enzyme nyinginezo zinazoitwa ‘’Methyltransferases’’. Hizi hubadilisha zaidi matokeo ya umeng’enyaji wa anthocyanins ili ulete chembe zitakazofyonzwa na kutumika na mwili vizuri zaidi. Na kwa upande wa kemikali za ‘’Betalains’’, hizi huvunjwa na enzymes au vimeng’enyaji vinavyoitwa ‘’Peroxidases’’ .
Kwa pamoja mwili hutumia rangi za asili za matunda vizuri sana kujinufaisha kwa virutubisho.
KUHUSU RANGI ZA KISASA?
Rangi za kisasa kama ambavyo zinajitambulisha, huwa ni rangi zisizo za asili. Na rangi hizi hutengenezwa kwa dhumuni la kutengeneza mwonekano mfano wa ule wa asili wa vyakula vilivyokwisha kukomaa. Na rangi hizi ni rahisi ‘’simple’’ ukilinganisha na za asili. ambazo ni za kitaalamu sana ‘’complex’’. Haiwezekani kuunda rangi kama za asili, Maana formula zake ni ngumu kuzifikia, na hivyo, teknolojia nyingi za vyakula hutengeneza tu rangi ambazo hudanganya macho, lakini zikishafika kwenye ulimi, mwili hautambui Combination zake wala kuzitambua.
Hii ni sawa na wewe kama ni mwanaume upewe mwanamke mzuri kimwonekano, lakini kwa ndani ni mwanaume. ni rahisi kumpokea, lakini pale utakapomchukua ndivyo kizaazaa huibuka ukiwa naye ndani. Ndivyo mwili pia na hizi rangi, huvutiwa nazo zikiwa kwenye chupa, lakini zikishaingia mwilini shughuli huanza.
RANGI ZA KISASA NI ZIPI?
Hayo ni majina na rangi zake. Ukiona ina rangi ya njano, kama hapo juu inavoonekana moja kwa mfano, basi ndo ujue iliyotumika ni kemikali ya Tartrazine, ukiona rangi ya chungwa ujue sio chungwa ni rangi ya ‘’sunset yellow’’.
Ukiona bluu ujue ni hiyo ‘’Brilliant blue. Na zote kwa Pamoja. Rangi hizi hutengenezwa maabara, na sio kwenye maabara ya asili.
HATARI KUBWA ZA RANGI HIZI ZISIZO ZA ASILI
Kuna Ushahidi mkubwa sana wa madhara ya:
ALLERGY
kwa watumiaji wengi wa rangi, tena hasa rangi zinazoitwa au zilizo group la ‘’azo-dyes’’. Na hii imepelekea baadhi ya nchi kama Norway kuzifungia kabisa. Ukisikia allergy maana yake mwili haukitaki hiko kitu kiasi cha kujisisimua sana hata kujidhuru wenyewe au ‘’Hypersensitivity’’. Kama nilivyosema awali kemikali hizi ni wageni mwilini, wala mwili hauzitambui, ila umedanganywa. Na allergy zina madhara tofauti tofauti kulingana na mtu.
Mfano wa rangi zinazobabisha sana allergy ni Pamoja na ’’Amanranth’’ ambazo huonekana ‘’Nyekundu’’, kuna ‘’Azorbins’’ nazo nyekundu, kuna ‘’Brilliant black’’ hizi huonekana nyeusi, kuna ‘’Sunset yellow’’ hizi huonekana kwa rangi ya chungwa, na mwisho wa mfano pia kuna ‘’Tartrazine’’ambazo huonekana za njano.
Tafiti zinazonesha mfanano wa madhara na hata kwa rangi zisizo za group hili la ‘’azodyes’’. ila tu kuna utofauti wa kiwango cha madhara.
Kuna Ushahidi wa madhara yaliyopelekea ‘’Asthma, na Rashes ambazo ni kama tupele tudogo hivi watu husema twa allergy’’, homa ‘’hay fever’’,kupungukiwa uono ‘’blurred vision’’ na mengineyo.
MATATIZO YA UBONGO KWA KIWANGO CHA KITABIA
Tafiti kadhaa zimeonesha Rangi nyingi husababisha mhemko mkubwa wa shughuli za ubongo ‘’hyperactivity’’. Na pia zinaonesha matokeo ya matatizo katika tabia ‘’behavioral disorders’’ kwa watumiaji.
JARIBIO KWA WATOTO
Katika jaribio moja kwa Watoto, kundi la Watoto walipewa wale jumla ya rangi 8 katika vyakula vya kisasa ‘’Cookies’’, Na baada ya masaa matatu;.
Matokeo ya jaribio
Baadhi ya Watoto walionesha changamoto ya kuathiriwa uwezo wa utambuzi, katika uwezo wa kimiondoko, au kuuondosha mwili. Mfano, kusimama, kuchukua ,kutembea n.k au unaweza isema kama ‘’impaired perceptual motor performance’’.
Pia baadhi walionesha kuwa na mhemko mkubwa wa kitabia’’increases hyperactive behavior’’. Huku madhara yakiwa makubwa zaidi kwa Watoto wadogo zaidi. Hii ni sawa na ukute mtoto hata kwa tatizo dogo ameonesha muitikio au response kubwa sana. Na ndivyo tabia za Watoto wa siku hizi, bila shaka msomaji unaweza shuhudia.
Baadhi walionesha kuathiriwa uwezo wa kujifunza, na kuwa na uwezo mdogo wa kuweka umakini ‘’short attention span’’. Pia walionesha hali ya lawama zaidi ‘’whine’’ na kuonesha matokeo ya hasira ‘’tantrum’’
HUATHIRI KINGA YA MWILI ‘’affect immunity’’
Kundi la azodyes limetafitiwa kuonesha likiathiri sana kinga za mwili. Hii ni kupitia kusababisha seli za kugandisha damu kujikunyata kwa Pamoja ‘’platelet aggregation’’. Pia zimeonekana kuathiri chembechembe inayoitwa ‘’Prostaglandin synthetase na thromboxane’’, hizi huwa mstari wa mbele sana katika kuongoza utendaji wa kujikinga. Zipo taarifa pia za baadhi kuipinga hoja hii, lakini hiyo sio sababu ya kutoamini taarifa zilizo thibitishwa pia na watafiti wengi.
Baadhi ya vitia rangi kama ‘’Caramels’’. hizi mara nyingi hutokana na sukari ambayo ikibadilishwa, mfano kwa kuchomwa, huwa nyeusi au huweza kubadilishwa rangi, na kuwa kahawia. hizi zimeonesha kuchangamana na Ammonia. Ambayo hii huwa na madhara ya kudidimiza seli za kinga za mwili zinazoitwa ‘’Lymphocytes’’. Caramel huwekwa sana kwenye soda ya Pepsi.
Pia kemikali ya rangi za wekundu za ‘’Canthaxantin’’ inayotumika katika kutengeneza ukahawia wa kisasa. imeonekana kutengeneza chembechembe kama za aina za mchanga au ‘’crystalline’’ katika Jicho sehemu ya kuona ‘’retina’’
Sunset Yellow ambayo huruhusiwa kwa kiwango cha (100-200mg/kg). imeonesha hata kwa kiwango kinachoruhusiwa bado inasababisha mabadiliko ya chini sana ya hatari ya mfumo wa kinga. Kumbuka rangi hii ya njano ni maarufu sana, lakini kwa chini sana inadhoofisha mfumo wa kinga. Kivipi?
hii rangi imeonekana kugandamiza au suppress matendo ya kibiolojia, ya kijenetikia, yanayofahamika kama ‘’mitosis’’ ya uundwaji wa seli za kinga, za kwenye bandama au spleen, katika seli zinaitwa ‘’splenocytes’’. kwa kuzuia vihamasishaji vya matendo haya. Lakini pia, zimeonesha kuathiri uwezo wa seli hizi wa kutambua hatari, au zisizo hatari, au husemwa kama ‘’mixed lymphocyte reaction’’. hii ni kama ambavyo mwili hutambua seli za damu uliyopewa na mtu mwingine bila kujikinga nazo.
Bado rangi hii imeonesha hatari kubwa sana kwa kuathiri namna seli ya kinga inavyojiwasilisha kwa dhumuni la kinga. Hii ni namna ambapo seli hutambulika kwa kazi maalumu ya kujikinga na hatari Fulani tu. Na hapa moja kwa moja tunazungumzia CD au ‘’Clusters of Differentiation’’. Utasikia mfano CD1,CD2,CD3 n.k. kila CD, seli huwa na upekee wa kuwa na molekuli husika kadhaa tu, ili kujilinda na aina kadhaa tu za matatizo. Rangi ya Njano hii imeonesha kuathiri kabisa uwezo wa seli hizi kujiwasilisha kwa namna hiyo, mfano huathiri CD3,CD4 na CD8 katika seli za kinga zinazoitwa T-Cells. Lakini pia huleta madhara kwa CD-19 kwa B-Cells.
SAYANSI YA SELI ZA KINGA ZINAZOATHIRIWA NA RANGI YA KISASA YA CHAKULA
Mtu akisema T cells kwa ufupi anamaanisha seli za kinga zinazozalishwa kwenye mfupa, na kukomaa katika tezi inayoitwa ‘’Thymus’’ au tezi kidari. Hizi upekee wake huwa hujikita kujikinga kwa kutumia seli. yaani seli ndizo zinazojikita kupambana na hatarishi. Rangi huziathiri CD-3 ambazo huwa kwa seli za T zote. na hizi ni muhimu maana, ndizo hushiriki katika kuunda geti au sensa kuu ya T-Cell yoyote ile, au inaitwa ‘’T Cell Receptor (TCR) Complex.
Pia Rangi huathiri CD4 Ambazo hizi huwa muhimu sana katika kuchochea T-Cells zinazoitwa T-Helper cells zinazohusika baada tu ya kukutana na kihatarishi. Hizi CD4 hujibandika katika geti mojawapo linaloitwa MHCII au ‘’Major Histocompatibility Class II’’ ambalo huwa lipo kwenye seli za kukamata vihatarishi mfano seli zinazoitwa ‘’Macrophages’’. Sasa hizi CD4, hudaka hizi seli za macrophages katika hiyo MHCII. Mfano, ambazo unakuta zimebeba kimelea, na baada ya kumdaka huyu mwenzake kwa kushikilia MHCII, basi T-Helper kama anavyojiita ‘’seli msaidizi’’, huja. na kwa Pamoja, hawa huzalisha vitoa taarifa kwa mfumo wa kinga wote. Hivi vitoa taarifa huitwa ‘’Cytokines’’. Rangi ya njano, au ‘’sunset yellow’’. huathiri vitoa taarifa vinavyo tambulika kama ‘’Interleukins (IL2,IL4,IL6,IL17).
Viashiria hivi hutoa mawasiliano juu ya taarifa tofauti tofauti, pia vipo viwasilianaji vingine vinavyo itwa ‘’Interferions(IFN-β). na pia kuna zingine huitwa ‘’TNF-β’’. Taarifa kutoka kwa viashiria hawa, husisimua namna mbalimbali ambazo mwili unaweza kutumia kumuua huyu hatari aliyeshikiliwa. Ikiwemo, na kutengeneza kinga yake kwa siku zijazo. Lakini Rangi pia huathiri CD-8, ambazo hizi huwepo kwa seli za kuua zinazoitwa ‘’Cytotoxic T-Cells’’, hizi seli huua seli zote zilizoathiriwa au za saratani. Hebu vuta picha sasa namna unavyoathiriwa na rangi zako kwa unywaji wa bidhaa za viwandani.
B cells huwa ni seli ambazo huzalishwa toka kwenye mfupa, na kukomalia huko huko. kwenye kiini cha mfupa au ‘’Bone Marrow’’. Seli hizi hujikita katika kutengeneza kinga ambayo haitumii seli Kwenda vitani moja kwa moja. bali hutumia uzalishaji wa kemikali, ambazo huenda vitani. Na kemikali hizi, au chembechembe hizi, huitwa ‘’Antibodies’’.
Kwa hiyo, kikiingia kihatarishi, basi mfumo wote kama nilivyouelezea awali, wa wale seli walinzi ‘’macrophages’’, watamdaka mhalifu. hawa pia huitwa ‘’Antigen presenting cells’’. na kisha hawa macrophages wenye kihatarishi, wataonekana kupitia sensa zao au receptors MHCI/MHCII. na kisha zile seli za CD4/CD8, husensi na kujishikisha. kisha, aidha huzalisha zile kemikali za taarifa ‘’cytokines’’ kuwataarifu hawa sasa B-Cells. Ambao kama walikuwa tayari wanamtambua, hubadilika na kuwa seli za Plasma, au za kazi, ambazo huzalisha chembechembe ‘’Antibodies’’. Ambazo, husambaa na kukutana na yule mhalifu na kumfunika ‘’opsonization’’. na hatua nyingine nyingi za kummaliza/kumuua, na kumtoa nje kama uchafu.
Lakini pia huweza kutumika njia ya kumuua kupitia seli za wauaji, hii hasa huwa kama waliodakwa ni seli za virusi au saratani. Kwa upande wa B-Cells, Rangi hudhuru seli zenye CD-19. Ambazo kazi zake kubwa zaidi ni kuhamasisha seli zingine zote za B kukua, na kuendelea. hivyo unaweza pata picha kwa mtumiaji wa rangi hizi namna vimelea na vihatarishi vinavyokufurahia.
TATIZO BAYA ZAIDI LA RANGI ZA KISASA LILILO JIFICHA
Zinadanganya Ubongo na Zinazoelesha Ubongo uongo. zinahafifisha ukweli katika ubongo. Ubongo ukishadanganywa kila kitu huaribika. Kuanzia yale tuliyoweza yagundua, kama baadhi hapo juu, na mengine ambayo bado hatujayafikia mpaka sasa.
Hebu vuta picha unavyoghadhabika unapoona picha ya mrembo mwenye rangi fulani kwenye mtandao ni tofauti na uhalisia wake, pale unapokuwa ulivutiwa naye kwa taswira ya mtandao, na ukamgharamia. Ndivyo ubongo pia. Mahesabu ya gari ni makubwa sana, lakini kosa dogo tu la kuweka maji badala ya petroli huaribu kila kitu. ndivyo ilivyo, haijalishi ubongo ni complex kiasi gani, uongo kidogo huaribu kila kitu. Ni kama pia chanjo ya virusi kidogo sana, hujenga mabadiliko ya mwili mzima. Uharibifu hauna kiasi siku zote.










Join the conversation