SIRI ZA VITUNZA CHAKULA "PRESERVATIVES"🚯✖️
‘’PRESERVATIVES ‘’vitunza chakula’’
Hizi ni jumla ya kemikali zote ambazo zinazuia vimelea vya kuharibu chakula vishindwe kuharibu chakula. Pia zimejikita katika kuzuia oksijeni isiharibu chakula. Kwa hiyo hapa huusisha sana
1.Viua vimelea vyote viharibuvyo vyakula au ‘’antimicrobials’’. Mfano vitu vinavyoua ‘’bakteria, fangasi, Minyoo na hata wadudu.
2.Vizuia unjano ‘’antibrowning’’, hapa ni kama nilivyo elezea katika blog ya antioxidants za kisasa.
3.Vizuia madhara ya oksijeni ‘’antioxidants’’.
Toka miaka ya kale huko zamani zimekuwepo njia nyingi za kutunza chakula ili kikae kwa muda mrefu. Kama vile Kukausha, kutumia Chumvi, Sukari, na kutumia moshi. Sasa hivi kuna teknolojia kadha wa kadha, kama vile kutumia chupa, Kugandisha, Kutumia friji, n.k. na kadri teknolojia ilivyozidi zaidi, imefikia katika matumizi ya vitunza chakula vya kisasa, vinavyotokana na viumbe hai, ‘’organic’’, au visivyo hai ‘’inorganic’’.
Vitunza chakula maarufu sana visivyotokana na viumbe hai, ‘’inorganic’’ huusisha Suphuric dioxide, Nitrates, na Nitrites. Na hizi hutumiwa katika muundo wa gesi, na pia yaweza tumika katika hali ya kimiminika. Mfano, ‘’sulphorous acid’’. Pia hutumika kama ‘’Sulphites za sodium,Potassium na Calcium. Na hizi huzuia unjano kutokea katika vyakula. Pia huzuia ukuaji wa fangasi.
Hutumika katika kutunza Juisi za matunda, na hata matunda makavu. Hufahamika kwa sifa ya kuharibu Vitamin B, na kutunza Vitamini C. pia Huambatana na hatari za Asthma.
Nitrite za sodium na Potassium, ambazo hutumika katika kutunza nyama, zimeonekana kuhusiana na changamoto za saratani ‘’carcinogenicity’’. Hizi zimezuiliwa katika nchi nyingi sana za ulaya. Zimezuiliwa kwa sababu huwa zinaunda kemikali zinazoitwa ‘’Nitrosoamines’’ ambazo ni hatarishi. Na pia huvuruga mfumo wa matendo ya kibiolojia, ‘’metabolism’’ kwa Watoto, na vichanga.
Sodium nitrite husababisha maumivu ya kichwa, allergy za Ngozi ‘’skin rashes’’ na pia huathiri utendaji wa Tumbo.
Kwa upande wa vitunzaji, vinavyotokana na viumbe hai ‘’organic’’, maarufu zaidi ni ‘’Benzoic acid, pia 4-hydroxy benzoates, salicyclic acid, parachlorobenzoic acid, proprionic acid, sorbic acid na sodium diacetate. Mara nyingi hutumika katika kutunza vyakula vya mikate na unga.
Benzoic acid na Benzoates hutumika sana katika kutunza vyakula vya makopo, juisi za matunda, yoghurt, Sauces na Margarines tofauti tofauti.
Benzoic acid zimeonekana kusababisha ‘’matatizo katika Ngozi ‘’ huitwa ‘’urticaria’’,na matatizo ya msisimko wa juu wa mwili ‘’hypersensitivity’’ kwa tartrazine.
NAMNA VITUNZA VYAKULA ‘’preservatives’’ VINAVYOUA KINGA
SODIUM BENZOATE
Hiki ni kitunza chakula maarufu sana. Na pia kimepitishwa na shirika la afya ‘’FDA’’ kama dawa dhidi ya kutatua matatizo ya mzunguko wa urea ‘’urea cycle disorders’’ kwa Watoto. Na hiki kitunza chakula pia kina sifa ya kuua vimelea. Hapa karibuni pia kitunza chakula hiki kimeonekana kuwa na umuhimu sana katika kurekebisha mfumo wa kinga ya kujikinga dhidi ya matatizo ya allergy za ubongo, katika majaribio ‘’experimental allergic encephalomyelitis’’.
Hii ni kutokana imeonekana ikipambana dhidi ya uvimbe, na pia kuzuia kupotea kwa mafuta yanayozunguka neva za fahamu, au ‘’demyelination’’. Pia imeonekana kupambana na changamoto za magonjwa yanayosababishwa na mwili kujiathiri wenyewe ‘’autoimmune diseases’’, kwa kuzuia uvimbe na na kuzuia kuzalishwa sana kwa seli zinazoitwa ‘’T-Cells, Mevalonate Pathway, Inos, NF-kB, TNF-α, IL-1β, Th-1 na pia huzuia kugandamana kwa molekuli na kuongeza Tregs.
MADHARA MAKUBWA YA SODIUM BENZOATE
Inaonyesha kuhafifisha Oksijeni katika seli ‘’deprive oxygen in cells’’. Pia imeonekana kuathiri mfumo wa kinga wa mwili. Na pia imeonekana kusababisha saratani. Pia zina uwezo wa kuhafifisha virutubisho vya mwili katika kiwango cha seli, kwa kuzizuia oksijeni kufikia seli. Na kuna kipindi huzizima kabisa seli kwa ukosefu wa oksijeni.
Sodium Benzoate zilionekana kuathiri kujiwasilisha kwa CD8 za T-Cell, na pia kuathiri na kushusha kiwango cha cytokines ambazo ni Interleukins (IL4, IL6, IL17) na Interferons (IFN-γ). Hizi zilionekana kwa seli za bandama ‘’splenocytes’’ zilizokuwa zimesisimuliwa na con A. lakini pia sodium benzoate ilionekana kushusha kiwango cha molekuli kinga zingine, za Interleukins(IL6), Interferons (IFN-γ ), na Pia molekuli inayoitwa ‘’Tumor necrosis factor’’ (TNF-α) kwa seli za bandama ‘’splenocytes’’, zilizokuwa zimesisimuliwa na LPS kwa kipindi cha masaa 48, toka mtu atumie bidhaa hizi. Hizi zote ni molekuli za muhimu sana kwa ajili ya kinga, na zinaonekana kuathiriwa moja kwa moja.
MADHARA MAKUBWA YA SODIUM NITRITE
Kwa panya waliopatiwa kemikali hii maarufu ya kutunzia vyakula, kwa kiwango cha 100mg/kg ya uzito. Walionesha kupungua kwa kiwango kikubwa sana cha seli za kinga za mwili ‘’lymphocytes’’. Lakini pia, kulionekana na ongezeko kubwa sana la seli za kujikinga na mashambulizi ‘’Neutrophils’’.
Imeonekana Sodium nitrite kupunguza utendaji wa seli za kuua saratani ‘’Natural killer cells cytotoxicity’’. Sodium nitrite imeonekana kusababisha uvimbe ‘’inflammation’’, ambao ndiyo unasababisha kujaa kwa zile seli za kujikinga na mashambulizi ‘’neutrophils’’, na seli zinginezo za kuwaondoa/kuwameza wahatarishaji, hizi seli huitwa ‘’macrophages’’.
Inapotokea kuna vimelea na hizi seli zimefika "Macrophages", baada ya muda mfupi huzalisha kiwango kikubwa cha kemikali sumu ambazo ni ‘’hydrogen peroxide’’, hizi pia unaweza ziita ‘’oxidant’’, huua kila kilichopo hapo, na ndiyo maana, hata katika mazingira yetu, kemikali hizi za hydrogen peroxides hutumika kusafisha vidonda. Kwa hiyo hizi kemikali, huaribu kabisa tishu na seli. Na matibabu ya sodium nitrite, yameonekana kusababisha ongezeko kubwa la kiwango cha kemikali inayoitwa MDA au ‘’Malondialdehyde’’ kwenye korodani ‘’testes’’, TNF-α na IL-1β.
MADHARA MAKUBWA YA SODIUM SULFITE
Takwimu zinaonesha toka miaka 30 iliyopita, sodium sulfite ndiyo imekuwa kitunza chakula kinachotumika zaidi duniani kote. Pamoja na kukubalika kwake hata na mashirika makubwa ya chakula. Lakini bado sodium sulfite imeonekana kuhusiana na kushusha uzalishaji wa Leptin baada ya kuwekwa na LPS. ‘’haya ni mafuta’’ kutoka katika seli za mafuta ‘’adipocytes’’.
Madhara haya yameonekana kubadilika kwa namna unabadilisha kiwango cha utumiaji na wakati. Yapo mengi katika tafiti hizi, lakini ni muhimu ukatambua, Leptin hizi zinazo chezewa, ndizo zinazo tawala mfumo wa Kuhisi Hamu ya kula, au ‘’appetite’’, zina umuhimu katika kazi za mfumo wa homoni, na ubongo ‘’neuroendocrine’’. na pia zina umuhimu katika kutawala mfumo wa nishati wa mwili. Na pia inahusiana na matendo mengi ya kifiziolojia.
SUMMARY YA JUMLA YA MADHARA KATIKA MFUMO WA KINGA KWA MATUMIZI YA VIONGEZWA KWENYE CHAKULA
1.Kugandamiza uzalishaji, ujiwasilishaji na utendaji wa molekuli kinga ‘’Interleukins’’ (IL), Interferons (IFN), ‘’ Tumor necrosis factor’’(TNF),
IL1, IL-1β : Sunset yellow, sodium benzoate, sodium nitrite,nitric oxide
IL2: Sunset yellow
IL4: Sunset yellow, propionic acid
IL6: Sunset yellow, Nitric oxide, colorant curcumin
IL10: Nitric oxide, colorant curcumin,propionic acid, cinnamaldehyde
IL12: Nitric oxide,
IL17: Sunset yellow
IL18: Nitric oxide
IFN-β: Sunset yellow
IFN-γ: Nitric oxide, colorant curcumin, proprionic acid
TNF-α: Sodium benzoate, sodium nitrite,colorant curcumin
TNF-β: Sunset yellow
TGF-β: Nitric oxide, sunset yellow
NF-kB: Cinnamaldehyde
Bcl-2 & Bax: Aspartame
2.Kuharibu seli za neva za Ubongo, na kusababisha ongezeko la mihemko, na sumu moja kwa moja kwenye seli za Neutrophils. -hasa ni Monosodium glutamate.
3.Allergy na matatizo ya Misisimko ya mwili kupita kawaida. ‘’hypersensitivity’’-Tartrazine 4.Kushusha Kinga ya mwili, na kuzuia uwezo wa mwili kujikinga kupitia ‘’inflammation’’-Nitric oxide
5.Kuathiri mfumo wa homoni kupitia uzalishaji wa homoni leptin, kwa sodium sulfite, na pia kuathiri seli za kujikinga na saratani ‘’NK-cytotoxicity’’ kwa Sodium nitrite
TUMIA UBONGO, CHAKULA NI KIUMBE HAI, HAKIWEZI KUISHI MIAKA KIKISHAKOMAA..




Join the conversation