SHERIA YA TATU YA MALEZI katika ulimwengu wa kisasa
#3 MAZIWA YA MAMA NI YA MTOTO
Kabla ya yote tambua kuwa; Mtoto anapaswa kunyonya kwa Miaka 2. Miezi 6 ya kwanza inapaswa kuwa ni Maziwa tu. Takwimu zinaonyesha Uhusiano upo mkubwa sana ‘’Corelation’’ kati ya Mafanikio ya Mtoto kiuchumi, kiakili, kijamii, kiafya hata kuishi Maisha marefu, na Muda mrefu alionyonya kuzidi wenzake walionyonya kwa muda mfupi.
Asili imeandaa maziwa ya mama kwa ajili ya kuwezesha ukuaji na maendeleo ya mtoto. Kama ambavyo viumbe vimetofautiana, ndivyo ilivyo pia maziwa yao. Maziwa ya Mama ni maziwa ya binadamu, sio maziwa ya ng’ombe. Ukionja maziwa ya mama utagundua sio matamu sana kama maziwa ya ng’ombe, unajua kwanini? ni kwasababu maziwa ya mama hayana Protini nyingi sana, na madini mengi, maziwa ya mama yana Mafuta mengi sana.
Na ukweli ni kuwa, maziwa ya mama yana mafuta mengi kwa kuwa Ubongo wa
mtoto unahitaji mafuta mengi sana kwa ajili ya maendeleo ya Ubongo. Asilimia
zaidi ya 60% ya tishu za ubongo ni Mafuta, hasa aina ya ‘’DHA’’, ambayo ndiyo
hupatikana zaidi katika maziwa ya mama. Tofauti
ya ubongo wa binadamu na Ng’ombe ni Ukubwa, ubongo wa binadamu ni mkubwa sana
ukilinganisha na maumbile yake ya mwili. Ng’ombe haitaji ubongo mkubwa,
anahitaji misuli mikubwa sana, na hii ndiyo sababu maziwa yake yana protini
nyingi sana, hasa aina ya Casein, tofauti na protini ya Whey ambayo ni laini na
ipo kwa wingi zaidi kwa binadamu.
hii tafiti inaonyesha kadri mtoto anavyonyonya zaidi, ndivyo akili, au IQ yake inavyokuwa kubwa zaidi.
Maziwa ya Mama yana chembechembe nyingi sana zinazoitwa ‘’HMO, au Human Milk Oligosaccharides’’. Hizi chembechembe ni za umuhimu sana katika kutengeneza chakula cha bakteria wazuri walio katika mfumo wa umen’enyaji wa mtoto, pia zinatengeneza chembechembe za seli kinga za mwili. Maziwa ya mama yana kiwango kikubwa sana cha chembechembe za seli kinga kama ‘’Secretory IgA’’, homoni, seli za mama ambazo hutoka katika mwili wake kupitia maziwa na kuingia kwa mtoto.
Kubwa zaidi, Maziwa ya mama yana Mafuta mengi sana ya umuhimu katika
utengenezaji wa Ubongo ‘’Long chain PUFAs’’, haya ndiyo msingi wa Uwezo mkubwa
wa kiakili wa mtoto, na afya yake ya Macho. Tofauti na maziwa ya Ng’ombe,
maziwa ya mama hayana Madini mengi kama ya ‘’Calcium, Sodium, Phosphorus,
n.k.’’, sababu kubwa ni kuwa; Bado Figo za mtoto hazina uwezo mkubwa wa kuchuja
kemikali hizi, na Maziwa ya mama huwa yakibadilika kila muda unavyoenda kwa
kuhusiana na ukuaji wa mtoto.
Je Maziwa ya Ng’ombe ni Mabaya kwa Mtoto?
Maziwa ya Ng’ombe yanapaswa kutumika kama zinavyotumika Dawa. Kama Mama ni mgonjwa, na hana maziwa, busara bila shaka ni kutumia maziwa ya ng’ombe kama dawa kumsaidia mtoto. Na hii inatokana na mfumo wa maisha ya kibinafsi ya zama hizi, zamani inapotokea mama amepatwa na shida, au amefariki, jamii ingetafuta mwanamke mwingine anayenyonyesha kumsaidia mtoto wa mwenzake. Na kama mtoto angekuwa akipatiwa maziwa ya ng’ombe, damu mbichi ya ng’ombe kidogo, na vyanzo vingine vya protini vya asili vingetumika kumsapoti zaidi mtoto, hata matokeo ya ukuaji wa mtoto huwa tofauti kidogo na wenzake. Watoto wengi huja kuwa wenye nguvu sana, wakubwa, na pia huwa na hasira sana.
Ukweli ni kuwa; maziwa ya ng’ombe hayawezi mfanya mtoto awe kama
ng’ombe, ila humfanya mtoto kupungukiwa na baadhi ya chembechembe, na kujazwa
sana na baadhi zisizohitajika. Mwili wa mtoto hutumia nguvu sana kuchambua vinavyohitajika,
na kutumia nguvu sana pia kuchuja visivyohitajika. Jambo hili huathiri ufanisi
wa matendo mengi sana ya kibiolojia, ikiwemo na ukuaji bora wa mfumo wa mwili
na akili.
Matiti ni ya Maziwa sio ya kuhamasisha Ngono
Kuna wimbi kubwa sana la wanawake wenye uraibu wa uzinifu katika zama hizi, ambao kwao ni mara kumi wapunguze kipindi cha watoto wao kunyonya, huku wakijidanganya kuwa watafanya matiti yao yaendelee kuonekana ya kitoto wakiendelea kuvutia wanaume. Matokeo yake wengi huishia kuja kupata Kansa za matiti, na watoto wao huwadhoofisha sana kiafya. Mwanamke mwenye akili anapaswa kumnyonyesha mwanae mpaka anapokomaa kabisa kiukuaji kama walivyofanya wamama wazamani.
Vyakula vya kumsapoti Mama anayenyonyesha
Vyakula vya protini kama mayai, samaki, karanga, maziwa, yogurt, siagi,
maziwa ya soya, hasa vya kuchemshwa, ni sapoti nzuri sana ya uzalishaji wa
maziwa na ubora wake. Upande wa wanga, Mchanganyo mzuri wa Unga au Uji wa
ulezi, mfano wenye; mtama, mihogo, viazi vitamu, mahindi, ngano kidogo, oats,
na ndizi unafaa sana.
Kama kuna matunda wanawake wajawazito wanapaswa kutumia sana, ni Maparachichi. Haya yana kiwango kikubwa sana cha Vitamini B vyote ikiwemo na Folate (B9) ambayo wengi wa wenye upungufu huwa hatarini kuzaa watoto wenye mgongo wazi, yana madini ya magnesium, zinc, na madini chuma. pia yana kiwango kikubwa sana cha Anti oxidants zinazoondoa kemikali sumu, na kuponyesha tishu za mwili. Matunda mengine ni Mapera, Mapapai, na Machungwa kutokana na kiwango chao kikubwa cha Vitamin C, hii huwasaidia sana kutoathirika ngozi kutokana na hali ya ujauzito. Wanawake wajawazito wanapaswa kutumia sana Maembe, na kutafuna Carrots, mawese, au juisi za Ubuyu ili kutoathirika na upungufu wa Vitamin A.
Kwa ajli ya madini chuma; nyama nyekundu, maini, maharagwe, matunda
kama maparachichi, mboga za majani kama Mchicha, kisamvu, na Spinachi zenye B9
pia husaidia sana. Vyanzo vya Madini ya Calcium ambayo husaidia kuzalisha
maziwa ni; Maziwa, Yogurt, Samaki wanaoliwa na mifupa yao kama Dagaa, na
mwisho; ni maji kwa wingi zaidi. Asilimia 88% ya maziwa ni maji, Mama anapaswa
kunywa maji lita kuanzia 2.5 mpaka 3 kwa siku nzima. Anapaswa kutumia Supu za
moto, Juisi za matunda ila zisizo na sukari, matunda kama matikiti maji, Maji
ya madafu, na Maziwa fresh.
Vyakula vya Kumuanzishia Mtoto anayenyonya
Mtoto kuanzia miezi 6 anahitaji sana maziwa, lakini Maziwa yanapopungukiwa virutubisho kutokana na mitindo dhaifu ya kiafya ya wamama wengi, watoto huitaji zaidi virutubisho kama madini chuma, na virutubisho, na nishati zaidi.
Mtoto anapaswa kupewa vyakula Laini vya Ndizi, Maparachichi, Mapapai, Maembe
kidogo, Maboga, Viazi vitamu, Carrots, Viazi mviringo, Supu ya mchicha
iliyosagwa vizuri, n.k.
Kwa ajili ya madini mtoto anahitaji Mayai hasa kiini, Nyama laini
iliyosagwa, Maini kidogo mara moja kwa wiki, Maharagwe au njegele, Uji wa Ulezi
au mtama, oats. Ugali unapaswa kulainishwa sana na supu, na pia unaweza
changanya na kiwango kidogo kama kijiko kidogo cha mafuta ya kupikia ya nazi,
au ya alizeti mabichi, lainisha zaidi na Parachichi.
Mtoto anatakiwa kulishwa kidogo japo mara 2 au 3 tu kwa siku. na
anatakiwa kupewa vijiko 2 au 3 tu kwa mlo huku akiendelea kunyonyeshwa. Mama
anapaswa kuanza na chakula kimoja laini zaidi, na kila baada siku 3 ndo
anaongeza na kingine kipya.
Kamwe Usimpe mtoto awali kipindi ana miezi sita Chumvi, sukari, asali,
maziwa ya ng’ombe, Chai yeyote ile, juisi, soda, pilipili, vyakula vigumu kama
karanga, karoti, au vyakula vya kukaanga. Utaratibu wa kuwapa chakula laini
watoto unapaswa kuendelea mpaka wanapofikia miaka 3 au 4 kwasababu ya uwezo wao
wa kutafuna huwa bado mdogo. Kuanzia miezi 9 mpaka 10 mtoto anaweza kuanza
kupewa vipande laini vya vyakula kama ndizi laini ashike kwa vidole vyake.
Matokeo ya kupuuzia huu mpangilio wa ulaji kwa mtoto ni madhara ambayo
atayapata siku zake za mbeleni.
Kwanini Maziwa hayatoki kwa Baadhi ya Wamama?
Zipo sababu nyingi, lakini sababu kubwa zaidi ni stress za mwili. Mwili unaweza ingia kwenye stress kutokana na upungufu sana wa madini na maji, au hali anayopitia mama kipindi cha kunyonyesha. Kwanza ni Muhimu kutambua hii biolojia ndogo, Mwanamke hutoa maziwa kupitia mfumo wa Ubongo wa ‘’PSNS’’. Huu mfumo huzima mtu anapokuwa na stress sababu mfumo wa Ubongo wa ‘’SNS’’ ndiyo huwa ON.
Mwanamke anapokuwa sawa akiwa hana stress, sehemu ya Ubongo ya
Hypothalamus husisimua sehemu ya nyuma ya Tezi ya Pituitary kuzalisha homoni
kuu mbili, Oxytocin na ADH. Homoni ya Oxytocin ambayo huzalishwa anapofurahia
Sex hata akazalisha uteute kwenye uke, na aka bond na mme wake, ndiyo hiyohiyo
husisimua Tezi za Matiti ‘’Mammary glands’’, kuzalisha Maziwa Mtoto wake
anaponyonya matiti.
Na hii ndiyo sababu wanaume hupenda kunyonya matiti ya wake wao
kuwasisimua kihisia. Hii homoni huenda sambamba na homoni ya ADH. Hii huwa na
kazi moja ya kwenda Kuzuia Maji yasipotee kwenye Figo kwa Mkojo. Lakini pia
huiminya mishipa ya damu kuchochea zaidi mzunguko wa damu ili kuwezesha
utengenezwaji zaidi wa maziwa. Ubongo hutumia homoni ya Prolactin kuwezesha
uzalishaji wa maziwa baada ya kusisimuliwa na hizi homoni zingine.
Wanawake wanapokuwa na stress nyingi za maisha, hasa kipindi anapokuwa
ananyonyesha; Mwili wa mama hubakia katika hali ya stress ambayo huishia
kuzalisha homoni za Cortisol, na kutozalishwa homoni zote za uzalishaji na
utengenezwaji wa maziwa. Mfumo wa stress ambao huitwa ‘’HPA’’ husisimua tezi ya
adrenali sehemu yake ya nje na kuzalisha homoni za stress zaidi ‘’Cortisol’’,
hizi hushusha maziwa kwa kuzuia isizalishwe Prolactin inayozalisha maziwa, na
Oxytocin inayoyafanya yatoke.
Vyanzo vikubwa vya stress hata kushuka kwa maziwa ni migogoro ya
familia, kushinda sana usiku katika mianga ya taa za kisasa, kutazama sana
usiku sinema, kutonyonyesha kwa muda mrefu sana, na mitindo yote mibaya ya
ulaji niliyokwisha ielezea.

Join the conversation