ELEWA KASHA LA UNACHOKULA "FOOD LABEL"🧃
VIYEYUSHA MAFUTA ‘’Emulsifiers’’ NA VIBORESHA MKOROGO ‘’Stabilizers’’.
Hivi viyeyushaji au ‘’emulsifiers’’ kama jina lake linavyomaanisha, hutumika kama unatengeneza juisi au mchanganyiko ambao mfano una mafuta na maji, na vinginevyo. Kwa kawaida michanganyo hii hujitenganisha. Na sasa basi, ukiweka hizi kemikali husaidia kuyeyusha mchanganyiko wote hata uwe juisi nzuri iliyojichanganya vizuri kabisa. Hizi ndizo mara nyingi huwepo kwenye ‘’Peanut Butter’’, na ‘’Margarines’’. mfano blue band za mikate.
Mfano wa hizi emulsifiers, kuna za asili kama vile ‘’Lecithin inayotokana na soya, na mafuta mengine ya mimea’’. Emulsifiers za kisasa huusisha: Staeryl tartrate, complete glycerol esters, partial glycerol esters, propylene glycerol esters,sorbitan esters of fatty acids,cellulose ethers, sodium carboxymethyl cellulose na acetic na tartraric acid esters za monoglycerides na diglycerides.
Unaweza ziona kemikali hizi namna ambavyo huwa zikionekana katika labels za vyakula katika Picha ya kwanza kabisa.
VIBORESHA MKOROGO ‘’Stabilizers’’
Hizi kazi yake ni kushikamanisha vitu vigumu ‘’solid’’, na vimiminika ‘’liquid’’, katika mkorogo ili visitenganike. Hizi hutumika sana mfano kwenye ‘’Ice Cream’’ ambapo hufanya mchanganyiko kuwa mzuri ukishikamana bila kutenganika kitabaka. Hizi hutumika pia katika maandalizi ya keki ‘’cake’’, michanganyo ya vyakula, Cheese, Salad na Supu.
Stabilizer nyingi zinazotumika huwa ni Gundi za Mimea au ‘’plant gums’’. Na zipo kimakundi Mfano kuna za kutoka kwenye magugu ya miti ‘’tree weed’’ kama ‘’arabic, ghatti.’’kuna zinazotoka kwenye magugu ya baharini ‘’sea weed’’ mfano ‘’agar, algin.’’ na kuna zinazotoka kwenye viini vya miti ‘’wood pup’’ mfano ‘’cellulose, methyl cellulose..’’. unaweza kuona stabilizer katika labels chini.
MADHARA YA STABILIZERS NA EMULSIFIERS
Tafiti toka NCBI zinaonesha matumizi ya emulsifier yamehusiana na matatizo mengi sana katika mfumo wa chakula ‘’intestinal disturbances’’. Zimeonekana kuathiri uwezo wa ukuta wa utumbo, na hii imepelekea urahisi wa vimelea vingi zaidi kupita na kuhatarisha kinga. Pia hupelekea kuvimba kwa utumbo, na ugonjwa wa kuvimba kwa utumbo unaoitwa IBD au ‘’Inflammatory Bowel Disease’’.
Na hii inatokana na kuwa, hizi emulsifier ni viyeyushaji au ‘’surfactants’’, yaani kama vile zilivyo sabuni. Na kibaya zaidi ni kuwa, bado haifahamiki kiwango maalumu kabisa kinachopaswa kutumika kwa ajili ya vyakula, hii inahatarisha zaidi matumizi yake.Tafiti imeonesha pia, huusiana na madhara yanayoathiri utendaji wa matendo ya kibiliolojia au ‘’metabolic reactions’’. Pia utafiti umeonesha, matumizi ya stabilizers nayo yamepelekea kuongezeka kwa madhara katika utumbo ‘’intestinal stress’’, kuharibika kwa utumbo, na pia kuvimba kwa utumbo.
Pia matumizi ya hizi kemikali yameonekana kuhusiana na kuathiriwa kwa mfumo wa tumbo, na flora wa tumboni ‘’gut microbiota’’. Na hii huambatana na matatizo mengine mengi zaidi. Lakini pia kuna baadhi ya kemikali tafiti kadhaa zimezionesha kuwa zina athari kubwa za kusababisha kutokea kwa saratani ‘’carcinogenicity’’. Na nyingine huwa zikifungiwa kabisa.
KWANINI ZINALETA MADHARA YA MTINDO HUU?
Hii ni kwasababu vyakula vingi vya kisasa vinapotengenezwa, huwa havina michanganyiko ambayo imekaa kibiashara na kuvutia. Na njia pekee huwa ni kuangalia inawezekanaje kuvifanya viweze kuvutia zaidi, na sio ni kwa namna gani vinaweza mfaidisha mtumiaji. Na kwa hivyo basi, namna pekee ya kukufaidisha mtumiaji ni kupitia kuvipunguzia madhara.
VIYEYUSHAJI ‘’SOLVENTS’’
Hizi kama zinavyojitaja, hutumika kuyeyusha michanganyiko yote ya chakula, ili iweze kuunda mchanganyiko mmoja ulio bora. Hizi hulenga kuyeyusha Ladha, Rangi, Antioxidants na Vitamini vyote kwa Pamoja, na kuvifanya viwe chakula kimoja.
Nyingi ya hivi viyeyushaji huwa na hatari za kiafya. Na matumizi yake yamekuwa yakizuiliwa katika baadhi ya nchi. Nyingi ya hivi viyeyushaji vimeonekana na hatari kubwa sana za utokeaji wa saratani. ‘’carcinogenicity’’. Mfano wa kemikali hizi zinazotumika kama viyeyushaji ni Pamoja na : Light Petroleum, Trichloroethylene, Methanol, Benzyl alcohol, Glycerol acetate, Castor oil, Ethyl acetate, Butan-1-ol, Butyl acetone, Acetone, Butanone, Diethy ether na Carbon dioxide.
UNAWEZA KUISHI BILA SUMU?.....


.jpg)



Join the conversation