CHAKULA HAKIDUMU MWAKA KWENYE KOPO! ANTIOXIDANTS SCAM‼️
MATUMIZI YA ANTIOXIDANTS BANDIA
Hizi huongezwa kwenye chakula ili kuzuia kisiharibike. Kwa kawaida neno ‘’antioxidants’’ lina maanisha ‘’anti-oxidation’’. Oxidation ni kitendo cha kuongeza oksijeni kwenye kitu, au kitendo cha kupoteza madini chaji ‘’ions na electrons’’ kutoka kwenye kitu.
chakula ili kiharibike stori yake huanzia hapa, ndani ya chakula huwa kuna mafuta hata kama ni kidogo. Haya mafuta yakiungana na oksijeni hupelekea chakula kuoza. watu hutumia hizi kemikali ili kuzuia madhara haya ya oksijeni
Kisayansi kwa aina zote za mafuta yale yasiyo ganda, mfano ya mimea au ‘’unsaturated fats’’. haya mafuta siku zote huwa katika muundo wake yana kaboni mbili ambazo unakuta zimeshikana kwa ‘’double bond’’. Sasa basi, siku zote vyakula unapoviweka kwenye mwanga, au Oksijeni. Oksijeni huenda kuungana na zile unsaturated fats, na kuunda ‘’free radicals’’. Na hizi free radicals huendelea kuungana zaidi na unsaturated fats, na kuunda free radicals nyingi zaidi mfano kemikali zinazoitwa ‘’Peroxides’’, ambazo hizi kwa Pamoja huchangia harufu mbaya inayopatikana kitu kinapoharibika.
Kadri muda unavyozidi Kwenda, ndivyo free radicals nyingi zaidi zinapoundwa na chakula kuharibika zaidi.
KWANINI CHAKULA HUWA KINAKUWA CHA NJANO AU CHEUSI KINAPOZIDI KUHARIBIKA
Kuna matendo mawili yanayosababisha unjano kwa chakula.
1.Unjano unaosabaishwa na Enzymes ‘’enzymatic browning’’
Kuna kimeng’enyaji au enzyme moja inayoitwa ‘’Polyphenol oxidase’’ au PPO. Hii huanza kuungana na kemikali zilizopo kwenye tunda zinazoitwa ‘’Phenolic campounds’’ baada ya tunda kukomaa. Na kisha huungana au ‘’react’’ na kuunda vitu viwili ambavyo ni ‘’Quinone’’ na ‘’maji’’. Na hiyo Quinone huungana tena na chembe za protini au ‘’Amino acids’’, na kuunda Melanini. Hizi melanini ndizo hupelekea rangi ya unjano na Weusi chakula kinapozidi kuharibika.
2.Unjano usiosababishwa na Enzymes ‘’Non-enzymatic browning’’
Huu tutaenda kuuangalia vizuri katika sehemu tutakayo zungumzia unjano. Lakini kwa sasa ni muhimu kutambua kuwa kuna aina mbili za matendo ya kibiolojia yanayoweza pelekea kukatokea unjano kwenye vyakula bila ya kutumia ‘’enzymes’’ ambayo ni; ‘’Mailard Reaction’’ na pili, ni ‘’Caramalization’’.
Matendo haya huusisha mabadiliko yanayohusisha ‘’Joto, kiwango ya uasidi ‘’pH’’, na kiwango cha mvuke. Kwa upande wa mailard reaction, kama tutakavyo iangalia zaidi kwa sehemu za mbele, huusisha badiliko la muungano wa chembechembe ya Protini ‘’amino acid’’ na chembechembe ya sukari ‘’Glucose’’. Na chembechembe hizi mbili zinapoungana, na kuendelea na mabadiliko mengine, huja kuhitimisha kwa uundwaji wa chembechembe zinazoitwa ‘’melanoids’’ . na hizo ndizo husababisha Rangi za njano, na upekee wa Ladha. Mfano wa haya mabadiliko, huwa katika upishi wa Nyama.
Lakini kwa upande wa Caramalization, hii huusisha badiliko la sukari kwa kuvunjwa kupitia joto kali, na kuendelea kubadilika ikivunjika kuwa vipande vidogo zaidi, na baadae kuanza kufanya mabadiliko mengine zaidi ya kimaumbo, na kupelekea uundwaji wa chembechembe zinazoitwa ‘’Caramelins’’. ambazo ndizo huleta rangi za unjano. hizi unaweza ziona kupitia kuangalia bidhaa kama mikate, ambayo ikipikwa, ganda la nje huwa la njano.
UTENDAJI WA ANTI OXIDANTS
‘’Anti oxidants’’ zinaweza kuzuia chakula kisiharibike kwa kuzuia kupitia Kwenda kwenye lile badiliko la kuunda ‘’Free radical’’, na kuungana na free radicals. hizi anti oxidant huwa na chembechembe huru za chaji za electrons. Hizi huungana na free radical huru iliyopo, na kisha huzuia uharibikaji zaidi wa chakula. Mfano Katika hii picha hapa chini, unaweza ona namna hiyo R:H ambayo ndiyo antioxidant, ikitoa hydrogen yake kwa ile free radical yenye N na kanukta kwa chini. Kwa namna hiyo hiyo, madhara ya oksijeni ya kuharibu vyakula vya mafuta huishiwa nguvu, na chakula hupunguza spidi yake ya kuharibika.
Matendo haya ya antioxidant kuzuia chakula kisiharibike, huwa hayafanywi kuzuia tu mafuta, bali hata kwa protini pia. Na namna ya utendaji huwa ya mfanano mmoja.
KWANINI ZIWE NA MADHARA KAMA ZINAFANYA KAZI NZURI YA KUTUNZA CHAKULA?
Antioxidants hazina madhara. Ila antioxidants za kisasa ndizo zenye madhara. Katika vyakula vya asili kuna kiwango kikubwa sana cha antioxidants. Mfano, Vitamin E, kuna Vitamin C, kuna Selenium, kuna Carotenes, kuna madini ya Zinc n.k. hizi zote kwa Pamoja huulinda ubongo wenye mafuta mengi sana, usidhuliwe na hizi free radicals za oksijeni au ‘’Reactive oxygen species’’.
Madhara huletwa na hizi antioxidants za kisasa ambazo huwa na ajenda kubwa zaidi ya kutunza vyakula kwa muda mrefu. Mfano wa hizi antioxidants za kisasa ni BHA na BHT. Kemikali hizi zinafanana kazi na anti oxidants za asili. Lakini kemikali hizi kama ambavyo zinatumika sana, ndivyo pia zinafahamika sana kwa sifa zake kuu za;
KUSABABISHA SARATANI AU CANCER
BHA na BHT zote zipo katika kundi la kemikali zinazoitwa ‘’phenolic antioxidants’’, changamoto kubwa ya kemikali hizi ni tabia zake za kuyeyuka kwa wepesi sana. na pia tabia zake za kuyeyuka baada ya matokeo ya joto ‘’thermal regulation’’. Kemikali hizi zimeonekana kuwa na tabia za kuungana na Nyuklia za seli, na kisha kuwa chanzo kikubwa cha kufeli kwa ufanisi wa DNA hata kupelekea wimbi kubwa la saratani. Zipo aina mbali mbali za saratani kwa kundi hili la antioxidants za kisasa
BHA imeonekana kusababisha saratani ya tumbo, na saratani za kibofu cha mkojo.
TBHQ imeonekana kusababishsa saratani ya uvimbe katika Tumbo, na pia kusababisha madhara katika DNA.
Madhara ya kemikali hizi zinazotumika sana yaliwahi zifanya zifungiwe kwa nchi ya Japan, Marekani na Ulaya.
HUATHIRI MFUMO WA HOMONI WA MWILI ‘’endocrine disruptor’’.
Antioxidants hizi za kisasa zilipojaribiwa kwa Wanyama zimeonekana kusababisha mvurugo wa utendaji bora wa mfumo wa homoni wa mwili. BHT imeonekana kuathiri mfumo wa homoni, na kuhusika na madhara ya sumu yanayoathiri Ini, Mapafu, Mfumo wa damu, Figo, na mfumo wa uzazi. BHT imeonekana kusababisha kushuka katika kiwango cha homoni ya kiume ya ‘’Testosterone’’ na kuathiri ubora wa mbegu za kiume ‘’sperm quality’’. Pia BHT imeonekana kuhusiana na kuongezeka kwa umbile la Ini, utendaji mbovu wa figo, uvimbe kwenye mapafu, na kupungua kwa kiwango cha Potassium.
Pia zipo takwimu nyingine nyingi zinazoonesha namna BHT imekuwa ikihusiana na tatizo la uvujaji wa damu mwilini, au ‘’hemorrhage’’. Kushoto ni namna unaweza zisoma kemikali hizi katika vikaratasi au ‘’labels’’ zinazoonesha vilivyomo kwenye chakula. Lakini kulia inaonesha picha ya vyakula baadhi tu vyenye BHT na BHA.
KWA HIYO TUACHE KUTUNZA VYAKULA KWA MUDA MREFU?
Ni swali lenye hisia kali sana hasa baada ya kujua madhara ya antioxidants zinazotumika kutunza chakula, na huku likiwa na hisia za kuhisi yawezekana mwandishi ni mpinzani asiyetambua jitihada kubwa zinazotumika kupambana dhidi ya tatizo hili kubwa, la kutaka kutunza chakula kwa muda mrefu, kikiwa na ubora ili kusaidia jamii. Lakini kabla swali hili halijajibiwa, muulizaji angepaswa kujiuliza pia, Je hapaswi kujua anavyouwawa?
Jibu ni hili, Katika blog zangu nilizoelezea Siri za Industrial Military complex mwanzoni kabisa nilisema kuwa tatizo hili ni feki, sio tatizo halisi. Ni sawa na muuaji wa makusudi anapojiliza msibani.








Join the conversation