SHERIA YA KWANZA YA MALEZI katika ulimwengu wa kisasa
# 1 TENGENEZA RAMANI YA MAISHA YA MTOTO
Mtoto sio kiumbe mgeni duniani, Mtoto anapaswa kuanza kuishi katika
akili za wazazi wake kabla ya kuzaliwa kwake. Kabla Binti hajaolewa anapaswa
kufikiria namna anatamani mtoto wake aje kuwa, na namna atakavyomlea. Kijana wa
kiume aliyetimamu anapaswa kujua mtoto wake anapaswa kuwa nani, na anapaswa
kuandaa Jina la mtoto wake ambalo ndiyo maana anayohitaji mtoto wake awe.
Kwa mfano, mimi ni daktari lakini nilitamani sana kuwa mkulima,
mwanangu anapaswa kuwa option ya kutimiza ndoto zangu nilizotamani
kuzifanikisha ila nikafeli. Naanza kumfikiria mwanangu akiwa mkulima kujaza
gepu la matamanio yangu. Watoto sio viumbe wageni, ni sehemu yetu, Mwanangu ni
seli yangu. Ninapoandika vitabu, namwandikia mwanangu. ninaponunua shamba
nakupanda miti ya matunda, navuta taswira binti yangu akiwa chini ya mti mzuri
wa matunda. Ninapogundua kuwa Jina fulani lina sifa nzuri sana ya kufanania
hali ninayotamani mwanangu aje kuipitia, naliandika katika kumbukumbu zangu
litakuwa la mwanangu.
Asilimia kubwa ya watoto ambao huandaliwa njia za kupita na wazazi wao
hufanikiwa. Na ndiyo maana Waigizaji wakubwa ni watoto wa watengeneza filamu
wakubwa. Wanasiasa wakubwa na Marais ni
watoto wa Wanasiasa wakubwa. Wanasayansi wengi sana ni watoto wa
Wanasayansi. Wafanyabiashara ni hivyohivyo. Na hata Mwana wa Mungu ni Mungu!
Watoto ambao hupita njia zao na kufanikiwa sana huwa wachache sana, tena hasa
wale ambao huwa na vipaji na juhudi kubwa sana, na wengi wao huwa hawarudii
makosa ya kutowarithisha watoto wao.
Kama mpaka nilipokuwa na miaka 30 sikufahamu ipi ni njia bora ya kupita
ya kujikimu kimaisha, kwanini nitegemee mwanangu naye aje kujitafuta mwenyewe,
maana atatumia si tena miaka 30, bali hata 50. Mzazi anayezaa bila kuchora
ramani ya mwanae, hana tofauti na mkulima anaemwaga mbegu zake barabarani. Ni
usaliti wa hali ya juu, kama wewe umeshindwa kujipambania mwenyewe, kwanini ulete
kiumbe ambaye unajua atahitaji kukutegemea, na utamkimbia.
Watu wananiuliza kwanini sitaki kujenga Nyumba yangu hapa Mjini;
siwajibu. Maana sijengi kwasababu yangu, sijengi kwasababu ya mwanangu. Kijana
mwenye akili timamu anapaswa kuanza kuandaa ramani ya jiografia ya mwanae
ambaye yupo viunoni mwake, na ndani ya akili yake. Sijengi hapa mtaani
kwasababu kuna Watu wenye maadili mabaya sana watamshawishi vibaya mwanangu.
Sijengi pia kwa kuwa huu mji hakuna maji safi, maji ya Manispaa yameshamiri
makemikali dawa hatari kwa afya. Mbogamboga nyingi zina madawa, siwezi kufuga
hapa wanyama wangu wa asili. Sioni sehemu ambayo mwanangu atajifunza kulima
bustani, au kuchunga mbuzi, Miziki wanayopiga imejaa mada za Ngono na Migogoro
ya maisha, Kamwe siwezi kujenga hapa kwasababu za mwanangu.
Maisha ya Mwanadamu mpaka anapofikia hatua ya kuweza kuzalisha na
kulea, tayari ni mafanikio kwa asilimia
50%. Kuweza kumlea mwanae mpaka naye akafikia uwezo wa kuzaa, ni asilimia 100%
kamili. Asili ina tabia ya kuwafanya viumbe kuzalisha au kuzaa watoto waliobora
kuliko wao, na inapotokea hali za wazazi zikiwa mbaya sana, asili huwa inakataa
kabisa kuzaa au kuzalisha. Na hii ndiyo sababu zama hizi kuna shida nyingi sana
za uzazi, hii ni kwa kuwa; hali za maisha zimekuwa ngumu sana kiasi mifumo ya
viumbe yenyewe inakataa kuzaa kutokana na kuhofia hali ngumu sana kwa watoto.
Watu wananiuliza, kwanini sitaki Kuzaa au kuzalisha! Nashindwa kuwajibu
kwakuwa; siwezi si kwasababu zangu, ni kwasababu za mwanangu. Hali yangu ya kimaisha na ya jamii yangu
nilipo kwa sasa ni mbaya sana, kama mimi mwenye uzoefu mkubwa maisha
yananishinda, yanini nimlete mwanangu mzuri ambaye hajui hata kujipambania.
Hili sio ombi, wala sio Ushauri, Ni jukumu la kila binadamu kuandaa
Ramani ya mwanae, La sivyo Mungu, Jamii, na mwanao wote watakuhukumu kwa
kuendekeza hisia za Ngono bila kujua matokeo yake kwa Kiumbe asiye na hatia.
Ni aibu kubwa sana kwa mwanaume ambaye hajui hata jina la mwanae
ataitwa nani? Majina yote hata katika Biblia yalikuwa ni Maana na Matamanio ya
wazazi juu ya watoto wao, hata kama hayakuwa mara nyingine kama walivyotarajia.
Adamu na Eva walimwita mwanao wa kwanza Kaini, wakihisi Ni yeye atakayewaokoa
na Hali waliyokuwa nayo. Ni jukumu lako pia kuhakikisha umeshaandaa kijana
wako, au binti yako, anakuja kuwa nani.
Wazazi Wapumbavu!
Kama mzazi anapitia hali kama hizi chini, na bado akaamua kuzaa,
anakidhi maana ya moja kwa moja ya Mpumbavu. Kosa sio hali ngumu unayopitia,
kosa ni hali ngumu na bado kung’ang’ania kuzaa.
Mpaka sasa hivi maisha yangu ni magumu sana, sielewi hata njia ipi ya maisha naweza ipita ikaniletea mafanikio japo ya kujikimu binafsi. Mimi binafsi maisha yameshanishinda natamani hata kufa. Kiukweli siwezi kulea kwa sasa hivi kutokana na haya maisha yangu, ila hata mimi mbona hakuna aliyenijali nikiwa mdogo. Watu wananichukia sana sababu ya tabia zangu mbaya, na mali zangu za wizi. Mwenza wangu ana tabia mbaya sana, hawezi acha Ulevi uliokithiri, sizani kama atakuwa na uwezo wa kujali familia yangu. Huyu mke wangu ni malaya sana, inawezekana hata mtoto wangu nikabambikizwa. Lakini Potelea mbali, Mimi nazaa tu.
Huu upumbavu ndiyo chanzo cha Mimba nyingi zinazotolewa, Watoto wengi
wasio na makazi, watoto walio katika
makundi hatarishi kitabia, watoto wenye akili wanaoshindwa kuendelea na masomo,
kesi nyingi za watoto yatima, na utaanza kuona hizi dalili kwa baadhi ya
wazazi; utaona wakiwa hawana uzazi kwa mpango ilihali hali zao ni ngumu sana za
kimaisha. Maamuzi dhaifu ya mtindo huu yatahukumiwa siku moja.
Mambo Yakuzingatia sheria ya 1
·
Unataka mtoto wako aweje kibiolojia. Angalia hali ya mwenza unayetaka
kuzaa naye. Wewe ni Mfupi sana, sio mbaya ukizaa na mrefu saizi ili mwanao
asiwe mfupi zaidi. Hivyo hivyo kwa mrefu sana. Ni vizuri kutengeneza ‘’Genetic
diversity’’ kwa mwanao. Wazazi wasiofanana sana kijenetikia watoto wao huwa
wazuri sana na wenye kinga kutokana na sababu za kijenetikia. Kuzaa na ndugu
yako, au mtu mnayefanana sana kijenetikia ni hatari kama ambavyo hufanywa kwa
kuku wa Broiler, ambao ni matokeo ya ‘’Selective breeding’’.
·
Unataka mtoto wako aweje kitabia. Angalia tabia ya mwenza wako, jamii
atakayoishi, angalia shule atakazosoma, angalia burudani atakazoshiriki, filamu
atakazoziangalia, na pia angalia vitu vya kujishughulisha ambavyo atavifanya
hapo nyumbani kwako.
·
Unataka mtoto wako aweje Kiakili. Angalia Vyakula utakavyomudu
kumpatia, angalia Uelewa wa mwenza wako ambaye atashiriki kumfundisha mwanao,
angalia Vitabu ambavyo vipo kabatini mwako, angali kazi za kumshughulisha
mwanao awe bora kiakili. Wanaume wengi wasiozingatia shida za kisaikolojia za
wanawake wao ‘’Narcissistic’’ za kujipenda sana, hujikuta tayari watoto wao
wakiwa Wajinga kabisa ‘’Bogus’’ kutokana na kudekezwa na mama zao. Angalia muda
utakaoupata wa kuwa na mwanao, angalia pia shule, makundi ya marafiki, na
walimu watakaomfundisha mwanao.
·
Unataka mwanao aweje kiafya ya mwili. Ni muhimu kujua mwanao atafanya
mazoezi gani, kazi gani, na atakula vyakula gani.
·
Unataka mwanao awe kama wewe, au kama atakaokuwa nao. Ni vyema kuchagua
mazingira ambayo mwanao hatakuwa na muda sana na jamii kuliko kuwa na muda na
wewe.
·
Usisahau, Ni lazima mtoto kuwa chini ya uangalizi wa mzazi mmoja au
wote. Kama unahisi ‘’Housegirl’’ ni mzazi, ni vema ukazaa na ‘’Housegirl’’
kuliko kuzaa na Mwanamke ambaye ana thamini kutafuta Pesa kuliko uzao wa tumbo
lake. Toka wanawake walipoanza kutafuta hela haijawahi rekodiwa kuwa uchumi wa
familia umeongezeka. Ni muhimu kutokuwa limbukeni wa falsafa za ujamaa, ugumu
wa maisha ni matokeo ya Wabinafsi walio juu katika mifumo ya kimaisha, ila ni
busara hata katika mazingira magumu; Wazazi wapambane kwa hali na mali kuwa
karibu na watoto wao.
Hitimisho #1
Fumba macho yako, mwite kwa jina lake binti yako ambaye bado
hajazaliwa. Mtazame alivyo mzuri na afya. Tazama mazingira aliyopo. Kumbuka,
Maisha sio gharama; unahitaji chakula cha asili utakacholima au limiwa, makazi
hata kama nyumba nzuri ya nyasi, mavazi rahisi hata ya ngozi, na mwisho
unahitaji Upendo asilimia 100%. vingine vyote ni Tamaa na ulimbukeni.

Join the conversation