LUSIFA DHIDI YA ULIMWENGU WA ROHO #7
ULIMWENGU WA ROHO
Hakuna Ulimwengu wa Roho
Ni muhimu tena narudia vitu vikuu vitatu
katika uhai wa binadamu, na hata kiumbe mwingine yeyote yule aliye hai. Mwanga,
Maji, na Usumaku. Hivi ndivyo vitu ambavyo vipo katika kiini cha uhai wa
kiumbe, hivi ndivyo injini ya maisha. nimeshaeleza katika sehemu iliyopita,
mwanga husisimua mabadiliko ya mifumo ya umeme ya seli, kama uzalishaji wa
chembechembe za elektroni, ambapo mwili kwa kutumia chembechembe zake kama
melanin hata na haem, zinapozalisha hizi
elektroni huzalisha zaidi mwanga ndani ya seli, ambao huu huchochea mabadiliko
ya maumbile ya maji katika namna mbalimbali za ajabu kama mshindi wa tuzo ya
mwanasayansi bora ‘’Nobel Prize’’ Prof. Montagne alivyogundua namna maji
yanaweza tunza na kuunda kumbukumbu hata za vimelea katika namna za ajabu kabisa.
Maji haya yanapotengeneza maumbile ya tofauti, hupelekea mabadiliko mbalimbali
ya seli, ambayo haya huchochea tabia tofauti tofauti za kiusumaku, kutokana na
tofauti za chaji katika molekuli za maji, na huu usumaku ambao huzalishwa ndiyo
huchochea na kuongoza matendo mengi sana ya kibiolojia.
Mwili hutumia hizi injini kuongoza matendo
yake mengine yote, ambayo huwa ni mithili ya ‘’Automatic processes’’, mfano,
utengenezaji wa protini, marekebisho ya jenetikia ‘’epijenetikia mfano
DNA-methylation, au Histone acetylation’’, uundwaji wa seli ‘’mitosis na
meiosis’’, uzalishaji wa nishati ambao ndiyo msingi wa matendo haya katika
Mitochondria, na kila kiungo husukumwa kutoka katika mifumo hii mikuu Kutenda
sawasawa na kazi yake, yaani kama ni neva za fahamu, basi usisimkaji utaenda
kulingana na majukumu yake.
Lusifa anatambua kuwa wasomi wengi hawajui
iwapi Roho ‘’Spirit’’ katika mwili wa binadamu inayoongoza uhai, yaani mithili
ya Pumzi ya Mungu. Na anajua ni wasomi wachache sana ambao wanatambua kiwango
cha Biolojia kwa undani mpaka katika kiwango cha hii biolojia ya chini kabisa
‘’Quantum Biology’’. Kiufupi kiini cha Gari ni Joto, Mafuta, na Oksijeni. Kwa hivi ndivyo huzaliwa Moto wenye kupelekea
kutanuka, na kupoa kwa Pistons, na huko ndiko hubadilishwa kutengeneza mzunguko
wa tairi na gari kutembea. Kwa magari ya
umeme, sababu ingerudi kuwa umeme na usumaku, na kwa hivi matairi huzunguka na
kuliendesha gari. Mara ngapi watu wamekuwa wakijua sheria hii lakini hawawezi
yatengeneza magari yao yanapoharibika? Je ni kweli kwa kuwa na joto, oksijeni
na mafuta tu tunaweza pata gari? Miaka mingapi imepita watu wakiwa na vitu
vyote hivi, ila mpaka karne ya 18 na 19, kutoka kwa kina James’s watt mpaka
Carl benz ndo tunapata injini za kwanza za kutengeneza magari yetu?
Jibu ni kuwa, Gari ni matokeo ya maelfu ya ufundi ambao kiini cha utendekaji wake ndizo hizo sheria kuu tatu. Gari linapoharibika unahitaji fundi kwa kuwa ni yeye tu mwenye maarifa ya kuelewa namna sheria hizi anavyozibadilisha kuwa utendaji. Wengine wote wanaelewa tu kiini cha utendaji wake. Binadamu pia tunaelewa kiini cha maisha ni maji, nuru na usumaku. Lakini hakuna anayeweza kutumia vitu hivi kuunda uhai zaidi ya fundi mwenyewe ambaye ni Mungu, na ndiyo maana hata mtu anapokufa, ni kama gari linapoharibika, ni muumbaji tu anayeweza mrekebisha. Wasomi wengi dhaifu wana mitazamo ya upungufu ‘’reductionists’’, yaani, kuna kiini ambacho kinaweza elezea msingi wa utu wa mtu ‘’consciousness’’, hakuna hiko kitu.
Roho ya Mungu ‘’Spirit’’ ndiyo inaendesha msingi wa uhai wa kila kiumbe, hiyo Roho ya uhai ndiyo inashikilia, inaelewa, imeumba, mawasiliano katika hiki kiwango cha biolojia ya chini kabisa. Ipo katika viwango vya maji, na nuru, na taarifa ambazo marazote huwa ni usumaku na umeme. Utakuta Yesu akijiita ‘’Nuru ya ulimwengu, au Maji ya uzima, au Neno au kweli’’. alipoonekana Yesu kwa Danieli, au Petro, Yakobo na Yohana, aling’aa kwa mithili ya umeme na usumaku, ambao uliwafanya walipomtazama kuishiwa nguvu kama tu ambavyo huwa kwa mtu ambaye angeona walahu mionzi mikali sana ya mwanga. Roho hii inapoongoza matendo ya kibiolojia, huwa inakuwa tu ikiwasha mifumo ambayo inapowaka sasa, inakuwa kama Redio baada ya kuichaji inavyofanya kazi, kila sehemu hufanya kazi yake. Kwa upande wa ubongo, unapowaka ubongo, ni kama umeme unapopita kwenye waya, lazima utatengeneza usumaku. Huo ndiyo utambuzi ‘’consciousness’’, kadri ubongo unavyokuwa umeendelea zaidi kama kwa binadamu na sokwe au tembo na samaki dolphin, ndipo utendaji kazi wa sehemu nyingi zaidi unavyoonyesha akili zaidi. Na sio kuwa kuna nafsi na vitu vingine, hizo ni falsafa za kishirikina. Binadamu sio watofauti sana na Wanyama, ni familia ya Wanyama. Tofauti ya binadamu na sokwe ni ndogo sana, na ndivyo ilivyo kwa panya pia, maana sote tu Mammalia. Lakini je ni nani anayeweza zungumzia nafsi ya panya? Kwani hawana maisha yote kama sisi ukiachana tu na ibada? Hata Biblia inasema Sabato iliwekwa kwa mwanadamu, na si panya! Wenda wana namna yao pia ya kuabudu, hata wao sio special sana, vipi kuhusu sisimizi, au kuhusu fangasi? Hoja ni kuwa, hakuna nafsi mbali na ubongo, hakuna roho mbali na ubongo kwa mantiki ya nafsi.
Kumbuka, kila kitu unachokijua au tabia Fulani
unayoitenda ipo kwenye tishu na seli za ubongo, na tunaweza ipoteza kama
tutakuathiri katika sehemu husika. Unapoona mcha Mungu anasali, kama
utamuathiri sana sehemu za ‘’Ventralmedial Prefrontal Cortex’’ usidhani kama
atakuwa yuleyule. Na ndivyo watu wanavyopata shida maeneo kadhaa hata wanasahau
kila kitu. Hakuna ulimwengu wa roho tofauti na ubongo. ni kwamba ubongo kama
kila sehemu ya mwili, huwa na mfumo wake wa umeme ambao huambatana na kazi
zake. Na huo mfumo wa umeme, kitaalamu ndiyo tunasema ni matokeo ya kiwango
kikubwa cha nishati katika ubongo kutoka vitu vyetu vikuu vya uhai, yaani,
ubongo unachukua oksijeni nyingi zaidi, unamadini na maji mengi zaidi hasa
ndani ya kimiminika chake kinachoitwa ‘’CSF’’, unafyonza mwanga mwingi zaidi,
ndiyo maana unasensa za mwanga nyingi zaidi ‘’melanopsins’’, una damu nyingi
sana ‘’haem’’ na mwisho, una
chembechembe za nishati za seli ‘’mitochondria’’ nyingi zaidi. Hii inatosha
kumfundisha mtu kutambua, Mungu alimuumba mwanadamu toka katika udongo akiwa na
mifumo yote hii, kisha akampulizia pumzi yake, ambayo hiyo sasa nayo siyo kuwa
iliongeza kitu kwa mwanadamu, bali iliiwasha tu hii mitambo, na kuishikilia
kama dereva anavyoendelea kuongoza usukani wa gari lake. Ni dhambi kwa Mtu
kusema, wala kufundisha watu, kuwa kuna ulimwengu wa roho, hizo kitaalamu ni
shida za kiakili ‘’altered states of consciousness’’, na tunaweza zitengeneza
kwa kutumia mapigo mbalimbali ya miziki, madawa ya kulevya, meditations, n.k.
Lengo la Lusifa katika sehemu hii ni kuwa,
kama watu hawatajua ni nini hasa kilicho injini ya uhai wao, na afya zao za
ubongo na mwili kwa ujumla. Kwa siri sana ataathiri vitu hivi muhimu sana kwa
afya za watu hawa, na kisha atawaonesha hata hivyo wao ni sehemu ya mbali zaidi
na mwili wao, bado wao wanaweza wasiguswe, kwa kuwa wao ni roho. Wengine
husema, ukiathiri mwili, unaweza kuathiri na roho. Wengine husema matendo yao
hayana uhusiano na roho zao.

Join the conversation