Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

LUSIFA DHIDI YA UHURU #6

LUSIFA DHIDI YA UHURU

 
Uhuru

Kama Nyoka

Sehemu kubwa kuhusiana na uhuru nimekwisha ielezea katika sura iliyopita. Binadamu kwa asili anatamani sana uhuru. Na kwa kutamani sana uhuru binadamu amekuwa hatarini sana hata kutamani kutopatiwa mwongozo wa nini anapaswa na nini hapaswi kufanya. Lusifa amewachochea watu kuhisi kuwa sheria za Mungu ni za kikatili sana, na kuwa, kadri watu wanavyoweza Kwenda mbali na sheria hizi, basi hisia zao za uhuru, na ubora wa maisha yao unaweza kuongezeka.

Uhuru tangia historia ya binadamu umekuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio ya binadamu. Hakuna uhuru duniani, wala popote pale. Hakuna uhuru kama umezaliwa. Kila kitu kinafata utaratibu na ndiyo maana kilikwepo na kitaendelea kuwepo. Hakuna uhuru wa kuamua utakunywa maji au petroli, unapojaribu kutafuta uhuru unatafuta kifo. Lusifa amejawa na sera za kuchanganya watu, ati uhuru ni bora kuliko maarifa! Na kwa mantiki hiyo watu wanaangamia kwa kukosa maarifa, na sio maarifa.

Lusifa amewavuta watu kufanya mapenzi kabla ya ndoa, wengine jinsia moja, wengine kwa mdomo, wengine kinyume na maumbile, wengine kaka na dada, wengine na Wanyama au hata roboti za mapenzi, wengine mme mmoja na wake wengi, n.k. Lusifa amewachochea watu kuwa huru kuua kwa mabomu ya nyuklia, kusema uongo kisa watanufaika, kutukana hovyo hovyo, kutokuwa na kiasi, kutoheshimu, kuvaa nusu uchi, kuchora tatoos na kula vyakula hatarishi kwa afya zao, n.k. Lusifa anajua kwa kuwa kila mwanadamu mpumbavu ndani yake kuna chembechembe ya ukaidi, anaojidanganya ni Uhuru. 

Lusifa amefanikiwa kuwapata wengi sana, kutokana na msingi wa ubongo. Ubongo haupendi kufikiria, au kufuata maelekezo, hasa unapokuwa tayari una stress, au umechoshwa na maisha. haya ni mahesabu ya lusifa. lusifa hutumia tamaa ambazo huwa amewatriki watu wake kuwa wanaweza zifikia kwa mafanikio sana kama watakuwa na uhuru.

Kama Joka

Nilishaelezea awali kuwa, Lusifa awali kabisa alikuwa na shida za kisaikolojia za kutamani sana kuwa kama Mungu. Lusifa alikuwa na tamaa sana. Na hakukuwa na namna ya kuzifikia tamaa zake kwa kutumia Logic, au maarifa, maana yeye tayari alikuwa ni kiumbe. Lakini kupitia mbinu ya Uhuru, alitengeneza hoja yake ionekane kuwa na mashiko. Sura zilizopita tuliangalia kiundani zaidi hoja hii.

Lusifa ameweza kuchochea mabilioni ya watu kutotii sheria na maagizo ya Mungu, kwa hoja tu ya kuwa, tuna uhuru wa asilimia 100% kutengeneza matokeo ya matendo na maamuzi yetu. Hakuna nafasi ya Muumbaji juu ya uhuru wetu. Huu ndiyo msingi uliotapakaa katika kila vyanzo vya burudani na usanii katika zama hizi giza za kisasa. Lusifa ameyafanya maarifa kuonekana kana kama ni kitu ambacho kila mtu anaweza kuamini cha kwake, na sio kwamba maarifa na kweli zatoka kwa Mungu. Na kwa kufanya hivi ameua kabisa sayansi ya kweli, na dunia imefikia kiwango ambacho taaluma zote zimefikia kikomo katika namna sayansi ilipaswa, au taaluma ilipaswa kuwa.