LUSIFA DHIDI YA MACHO #1
MACHO NA LUSIFA
Utangulizi
Kama nilivyoeleza awali
kabisa, watu wengi wanahisi ulimi ndicho kitu ambacho kinawaathiri zaidi,
lakini ukweli ni kuwa Lusifa hutumia macho zaidi kuathiri na kuwateka watu.
Lusifa hujua udhaifu wa macho, na ameiva katika taaluma ya kucheza na ubongo
kupitia macho. Kiukweli macho ndiyo mlango mkuu wa kuufikia ubongo kama Biblia
ilivyosema, na ajabu ni kuwa Macho yenyewe ni sehemu ya ubongo ‘’Diencephalon
in origin’’. Na hata hutumia seli za kujikinga za ‘’Oligodendrocytes’’ kama
tishu zingine za ubongo, na sio za sehemu zingine za mwili.
Kama ilivyosemwa na Biblia,
hata katika Upasuaji kuuelekea Ubongo, Fuvu eneo la Macho ndiyo njia nyepesi
zaidi ya kuufikia ubongo. Ubongo wa mbele unaotengeneza tafakari na maana za
taarifa zote za ubongo kimantiki, huamini moja kwa moja taarifa zinazotoka
katika macho, kama msemo unaosema, unapoona unaamini.
Kwa kuona unaweza kuridhika,
kufurahia, kusisimka, kushiba, kukinai, kuumia, kutambua Ladha, na hata matendo
magumu kabisa kuweza kueleweka kisayansi, kama kutabiri. Hii inaweza kukupatia
msingi wa kutambua kuwa tabia za watu zinaelemea zaidi katika taswira
wanazoziona, na wanazoziunda, maana Ubongo marazote hutenda kwa namna ya kutengeneza
taswira, hata pale mtu anapokuwa amefumba macho.
Mzee Lusifa hutriki macho kama
nilivyoelezea katika kitabu cha Q4 injili ya sayansi, kwa urahisi sana. Hii ni
kwa kuwa msingi wa tabia yake ya Tamaa huwa rahisi sana kuuambukiza kwa watu
kupitia macho. Hebu tafakari mfano, Vitu vikubwa viwili ambavyo vina msisimko
mkubwa zaidi kwa asili ‘’greatest natural rewards’’, ni ‘’Mapenzi na Chakula’’.
Ili mtu aweze kuwaka hisia za tamaa ya mapenzi, anapaswa kwanza kuona,
ijapokuwa kwa Wanyama huwa kinyume, wao husisimka zaidi kwa Harufu, lakini
sehemu ya ubongo inayohusiana na harufu ‘’olfactory lobe’’ haijaendelea sana
kwa binadamu kama ilivyo kwa Wanyama. Lakini hata hivyo mifumo hii miwili
hufanya kazi kwa kushirikiana sana, na yote huwa haihusishi sana tafakari baada
ya taarifa, yaani, watu baada ya kuhisi harufu huwa hawafikirii sana na kuamua
kusisimka au laa!! Kiufupi mfumo wa harufu ni sehemu moja kwa moja katika mfumo
wa hisia wa ubongo ‘’limbic system’’, na ndivyo zilivyo nguvu pia za taarifa za
macho, mwanaume anapoona sehemu za maungo ya uzazi wa binti katika mionekano ya
kimivuto ya kimapenzi, husisimka moja kwa moja bila kupata nafasi ya kufikiria.
Lusifa na Jopo lake
wamechochea kwa kiwango kikubwa sana kujazwa kwa taarifa zisizo za muhimu
katika mitandao ya kijamii, zaidi ya taarifa zenye umuhimu. Lengo lake ni
kuwafanya watu kuingia katika ulimwengu wa giza la kimaarifa. Katika Q4 tuliona
namna ambavyo taarifa hizi huathiri uundwaji wa ubongo, kwa kupunguza kiwango
cha seli za ubongo ‘’gray matter’’’, tukaona taarifa hizi zinavyoathiri
uzalishwaji wa homoni za motisha ‘’dopamine’’, tukaona zinavyoathiri falsafa na
mitazamo ya watazamaji kisaikolojia kwa kuwazoelesha taarifa zisizo na
uhalisia.
Lusifa amefanikiwa kuwarudisha
binadamu wa karne ya 21 Babeli katika mitandao hii, au ulimwengu wa kimitandao
kwa ujumla. Watu wamekuwa ni wapweke kwa nje, watu wapo ndani maranyingi zaidi.
Watu wana marafiki wasiowahi kukutana nao, watu wanawawaza zaidi watu
wasiowajua kuliko walio majirani yao. Watu wanakesha kufurahia shughuli
zisizofanywa katika jamii zao. Watu wanavutiwa na mionekano ya watu wasio wa
jamii zao. Watu wanajifunza vitu visivyo na uhalisia wala umuhimu katika jamii
zao. Watu wamekuwa si wa kuwajali wakwao kama Biblia ilivyotabiri, huku wengi
wao wakiwa wabinafsi ‘’narcissistic’’, hasa kutokana na mitandao hii ya
kijamii.
Kama Joka
Kama kuna jambo ambalo wenda
madaktari wote, na wasomi wote wangepaswa kufundishwa walahu hata kwa kiwango
kidogo sana, basi ni hili. Tangia mtoto anapoundwa akiwa tumboni, huwa anatumia
mwanga kama chanzo kikuu cha taarifa kuhusiana na kila ratiba, na mwongozo wa
matendo yote yanayofanyika hata katika kiini cha seli zake za uhai. Ni kweli ni
ngumu sana kuweza kuelewa kiwango kidogo kabisa cha
utendaji wa seli za uhai, maana hugharimu taaluma pana zaidi inayoitwa
‘’Quantum Biology’’. Lakini katika taaluma hii, ndipo huwezekana kuelewa kuwa,
kiini cha maisha ambayo yanatokana na Nguvu za uhai ambazo huonekana toka
katika chembechembe za nishati za seli, au ‘’Mitochondria’’, hutegemea zaidi
Maji, na Mwanga.
Kumbuka, Huwa naishiwa Nguvu
kabisa ninapoona Yesu naye alijiita, ‘’Maji ya Uzima, au Nuru ya Ulimwengu’’.
Lakini ajabu sana, Mungu alipokuwa akiumba siku ya kwanza, yalioonekana zaidi
ni Maji na Nuru aliyoiumba, au Mwanga kama nilivyoelezea katika Q3. Hiyo ndiyo
misingi mikuu ya uhai ukiongezea na Usumaku ambao ndiyo Nguvu ya mawasiliano
katika viwango vya Quantum Biology.
BIOLOJIA YA MWANGA KWA UFUPI
Sasa basi, unapaswa kutambua walahu kidogo kuwa, mwanga wa jua unapoyafikia maji yaliyo ndani ya seli, kwa kufyonzwa kupitia chembechembe za melanin ambazo huwa kama mashine zinazounda kompyuta zinazoitwa ‘’semiconductors’’, maana mwanga wa jua mwekundu hupenya tabaka la Ngozi kwa 10cm mpaka 30cm, na hivyo huu mwanga sasa unapoingia katika chembechembe zile za Mitochondria, huyasisimua maji ambayo huwemo mule, kumbuka maji ndani ya Mitochondria huundwa mulemule, kwa kupitia chembechembe inayoitwa ‘’Cytochrome C oxidase’’, hii huusiana na utendaji kazi wa mashine ya nishati ya Mitochondria, au ‘’enzyme ATPase’’, maji yanapokuwa yakimulikwa na mwanga ambao hautoki kwa jua, ila unatengenezwa moja kwa moja ndani ya seli kupitia chembechembe za melanin, hubadilika maumbo mbalimbali na kutengeneza maumbile ambayo huchochea tofauti za uchaji ‘’polarities’’, hizi tofauti huchochea tabia tofauti tofauti za usumaku ambao ndiyo msingi wa uendeshaji wa mitambo ya ufanyaji kazi wa seli. Seli huitaji sana maji, na ndiyo maana sababu ya vifo vyote ni upungufu wa maji ‘’dehydration’’. Utendaji wa seli huitaji sana chembechembe kuu tatu, yaani, Hydrogen Proton, Electron, na Oxygen.
LUSIFA NA BIOLOJIA YA MWANGA
Lusifa kwa kuchochea mwanga wa
Taa za Kisasa ‘’Blue lights’’ wakati
ambao watu walipaswa kulala, amefanikiwa sana kuharibu kizazi cha binadamu.
Lusifa kwa kuwafanya watu wasilale usiku, wakikesha kwenye masinema, wakichati,
wakiwa katika starehe, n.k. amewaharibia kabisa binadamu mfumo wao wa kalenda
ya Biolojia ya mwili ‘’circadian rhythm’’, binadamu hukaa kwenye mimba kwa
miezi tisa, huzaliwa na kuota meno kwa wakati maalumu, huanza kutembea na
kuzungumza kwa wakati maalumu, huanza kupevuka katika wakati maalumu, na
nyakati hizi zote hufanana kwa jamii yote ya binadamu kwa wastani. Hii ni kwa
kuwa binadamu wote huwa na aina moja ya maelekezo ya kifiziolojia na jenetikia.
Kama mtu angekuuliza mwili unajuaje kalenda hizi? Mfano, Ubongo wa binadamu
hukomaa kabisa miaka kuanzia 25, je ubongo unawezaje Kwenda na kalenda hizi za
nyakati kwa ufanisi mkubwa kiasi hiki. Basi jibu pekee ni kuwa, mwili wa kiumbe
yeyote ule hufuata kalenda ya mwanga unaotoka kwenye jua. Na hii ndiyo sababu
uharibifu wa kalenda hii unapelekea Watoto wanaanza kupevuka kabla ya wakati.
Mitochondria hizi katika seli
ili zifanye kazi ya kuunda maji ambayo ndiyo yanaongoza utendaji wake huitaji
mionzi ya mwanga wa jua tu ‘’visible light spectrum’’. Na sio mionzi mingine
yeyote ile kama ya simu na vifaa vya kisasa ambavyo watu hushinda navyo. Lusifa
na Jopo lake alihakikisha kuwa anachochea watu kutumia screen za LED za Blue,
na ndiyo maana watu wengi huwa hawajui kwanini Taa za awali za Mwanga mwekundu
zilipotezwa. Baadhi huisi wenda shida ilikuwa ni matumizi yake makubwa ya
nishati, lakini La hasha! Lusifa alishagundua ili aweze kutawala akili za
binadamu, hoja ya kutumia Nyaya au Vipandikizwa katika Ubongo itakuwa ni ngumu
sana, lakini kwa kutumia mfumo huu ‘’Wireless’’ unaotumia tu Mwanga wa Blue, au
mwanga wa taa hizi za kisasa, atafanikiwa sana. Na amefanikiwa sana kwa kuwa,
kila watu wanapotumia taa hizi za kisasa, hupelekea mageti yanayoitwa ‘’UCP’’
katika ubongo Kufunguka, na mageti haya yanapofunguka, hupelekea kupotea kwa
kiwango kikubwa sana cha electrons. Kwanza kumbuka, mwanga wa asili
unapomulikia mwili wa kiumbe, huchochea mwili kuzalisha electrons kwa
kuzisisimua melanin.
Sasa basi, watu hawa
wanapokesha na mianga isiyo ya asili, au wanapoamka nayo asubuhi kwa kuzisoma
emails, au meseji katika simu zao, au mfano katika mazingira yenye kiwango
kikubwa cha chembechembe za Fluorides, kumbuka Fluorides huvuta sana electrons
‘’more electronegative than oxygen’’, mitochondria hushindwa kuunda maji, na
hupunguza hata uhitaji wake wa Hydrogen toka katika mzunguko wa TCA cycle,
mitochondria sasa huingia katika mzunguko mwingine unaoitwa ‘’serine oxidation glycine
cleavage system’ ilikutatua tatizo hili, lakini mwishowe Mitochondria hujawa na kiwango
cha Deuterium, ambazo hizi huwa ni kama mbadala wa hydrogen nyepesi ambazo
zimekosekana kutokana na kukosekana kwa electron. Na hizi zinapokuwepo katika
mitochondria hupelekea ishindwe kufanya kazi vizuri, DNA huwa nzito
isiyojifungua kirahisi, seli huitaji mwanga mwingi na huwa wazi sana ‘’switch
ON’’, huu ndiyo mwanzo wa magonjwa yote.
Kukosekana kwa mwanga wa asili
mwekundu katika Ubongo, kutokana na watu kuchelewa kuamka, na kukesha wakiwa na
masimu au makompyuta, au kwenye taasisi zinazofanya kazi usiku zikiwa na
matumizi ya taa za mianga hii ya kawaida, au blue. Huathiri mfumo wa ubongo
unaoongoza matendo makubwa sana ya mwili, unaoitwa ‘’leptin-melanocortical
pathway’’, huu ni mfumo ambao ungeambatana na hisia za kutulia kwa hamu za kula
kwa kuzalishwa kwa homoni ya kuridhika kwa hamu za kula inayoitwa ‘’leptin’’.
Lakini pia huu mfumo huongoza uzalishaji wa homoni ya ‘’Melatonin’’ ambayo
huusiana na afya ya ubongo, huchuja sumu chafu katika ubongo, maana ni
‘’antioxidant’’, pia melatonin inapozalishwa huchochea Kimiminika kinachoitwa
‘’CSF’’ kusafisha Ubongo, maana hii homoni huchochea hisia za kulala, melatonin
pia huchochea tezi za Ubongo kama ‘’Pituitary’’ kuzalisha homoni za ukuaji, na
homoni za uzazi kama ‘’Testosterone, au kuchochea uzalishaji wa homoni kama
Luteinizing hormone, n.k.’’ mwanga wa
jua wa asili huchochea afya ya mfumo wa ubongo toka katika macho unaoitwa
‘’Retinal-cortical pathway’’, na watu wanaokesha sana na vifaa hivi vya usasa
hujikuta wakiwa na shida za macho ‘’Myopia’’, ambapo hutokana na miale hii
mikali ya mwanga, hupelekea tabaka la ndani la jicho ‘’retina’’ kujiachia toka
katika ukuta wa jicho ‘’macular degeneration’’, na matokeo yake ni taswira
kuundwa kwa mbele ya retina, na watu hujikuta wakiwa na shida za kuona ‘’Near
sightedness’’.
popote pale mwanga wa Blue
unapogonga katika tabaka la jicho hasa wakati wa usiku, huchochea mfumo wa
Ubongo unaoitwa ‘’Sympathetic nervous system’’ ambao huu huchochea Stress, na
huzalisha ‘’Stress hormone’’ au ‘’Cortisol’’, hii huenda katika tishu zote za
mwili, na huvunjavunja mafuta, sukari, na hata protini, na hii ndiyo sababu ya
mionekano ya kuzeeka kwa watumiaji wengi, hii ni kwa kuwa tabaka la Collagen
linaloshikilia zaidi Ngozi nalo huathiriwa. Pia cortisol huathiri uzalishwaji
wa melanin ‘’melanogenesis’’, na hivo kuathiri biolojia yote ya utendaji
tuliouzungumzia.
Vijana wengi huishiwa Nguvu za
Kiume kutokana na shida za mianga hii inapofika katika sehemu ya ubongo
inayoitwa ‘’Hypothalamus’’, na kuifanya itanuke. Kumbuka kila kitu kitu
kinapoelekea kuangamia hutanuka, iwe ulimwengu ‘’Universe expansion’’, iwe Nguo
inayoisha, liwe Jicho, uwe Ubongo, hata mwili. Hii ni kwa kuwa, Seli inahitaji
nishati kubwa sana kuendelea kushikilia umbile lake, na inapoishiwa Nguvu,
hujiachia na kutanuka inapoelekea kufa. Sasa basi, kushinda na mianga hii,
huathiri Ubongo ‘’hypothalamus’’ na kupelekea shida katika tezi ya Pituitary,
na kisha tezi za uzazi ‘’Gonads’’, ambapo matokeo yake ni kuzalishwa hafifu kwa
homoni hizi. Kiwango kikubwa cha stress
za Cortisol huathiri uotaji wa nywele kwa vijana wengi kama tafiti kadhaa
zinavyoonyesha.
Mafanikio ya Lusifa
Watu washaingia katika kumi na nane za kutumia taa hizi za kisasa, kuamka na simu zao wakiangalia ‘’Updates’’, kuchati kwa masimu haya, n.k. na kadri watu wanavyokuwa watumiaji wa bidhaa hizi, ndivyo wanavyokuwa waraibu zaidi. Hii ni kwa kuwa mianga hii au ‘’blue lights’’ huchochea ‘’dopamine, na hata adrenaline’’, na hii ndiyo sababu kila viwanda vya teknolojia hutumia mianga hii katika bidhaa zao. Hii ni kwa kuwa zinamatokeo makubwa kiuchumi au kibiashara. Mafanikio makubwa zaidi hata hivyo ya lusifa ni kuwa, bado watu wachache sana ambao wameweza kugundua siri na sayansi hii ya uharibifu. Hii ni kwa kuwa, taaluma hii haipatikani katika mitaala ya kielimu kirahisi.


Join the conversation