Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

LUSIFA DHIDI YA KILIMO #8

 SAYANSI YA KUBADILISHA DUNIA KWA KUPITIA KILIMO

                  ‘’Modern Agricultural Modifications’’

Nimeeleza sana katika  kitabu cha Q8, Historia na Kiini Cha Magonjwa, historia nzima ya kilimo, na hatimaye changamoto kubwa sana zilizoikabili dunia kutokana na kilimo. Katika sehemu hii nitaeleza ufupi tu wa namna Lusifa anatambua kiini cha kazi zote za mwanadamu, zinahusiana na uhusiano wake na asili, hasa mimea, ambacho ndicho chakula chake. Na Lusifa hataki kabisa uhusiano wa mwanadamu na mimea, na anajua kwa kuangamiza mimea, mwanadamu hataweza kuwa salama tena.

Kama Nyoka

Kutokana na mabadiliko ya hali ya nchi, kutokana na kilimo kilichoshamiri cha aina moja tu ya mazao ‘’monoculture’’, kutokana na kukata sana miti na kufyeka mapori ilikuandaa mashamba makubwa, kutokana na kufuga Wanyama wengi jambo litakalo wajaza maelfu ya Wanyama katika eneo moja tofauti na mbugani, kutokana na kuwa na watu wengi katika eneo dogo wasiofanya kazi za kujitafutia chakula, haya na mengineyo yalipelekea ardhi ya dunia kuishiwa kabisa rutuba.

Mpaka dunia inapomaliza vita ya pili ya dunia, maeneo mengi ambayo yalikuwa na watu wengi, au miji mikubwa, ardhi zake hazikuwa zikisapoti kabisa kilimo. Na uharibifu huu ulianzia zamani sana maeneo ya Asia, na Ulaya, ambako walianza na kilimo, na kisha kusambaa na Amerika, na Afrika, hasa kipindi cha Ukoloni. Ambako tamaa kubwa ilikuwa ni kugombania maeneo yaliyokuwa bado yana Rutuba nzuri.

Tatizo la kuishiwa Rutuba halikuwa na dawa bora yenye mashiko zaidi ya dawa za kuichochea ‘’boost’’ ardhi walahu kuweza kujimudu kivirutubisho walahu kusaidia mimea ikue. Hivyo matumizi ya mbolea yalikuwa ni mapinduzi makubwa sana, toka kwa wanasayansi wa awali sana kama ‘’Harber process’’ ambayo Mr. Harber aligundua namna ya kutengeneza mbolea za kwanza kabisa. Mbolea nyingi huwa ni madini ya Nitrogen, Phosphorus, na Potassium. Hii ni kwa kuwa, mimea hutumia sana madini haya kutengeneza chembechembe za seli zake za kutengenezea chakula zinazoitwa ‘’Chrolophyll’’,  na hizi huipa mimea rangi ya ukijani, zinapopungua mimea huonekana ya njano. lakini pia mimea huitaji madini ya ‘’Phosphorus kwa ajili ya kutengeneza sana chembechembe zake za Nyuklia, kama DNA. pia huitajika sana phosphorus katika kutengeneza chembechembe za nishati kama ATP, n.k. zinapopungua hizi, mmea hujawa na chembechembe zinazoitwa ‘’anthocyanins’’ ambazo hizo ndo huufanya mmea kuwa na rangi ya damu ya mzee, au ‘’pink’’. mmea pia huitaji sana madini ya Potassium kwa kazi za kuongoza kufunga na kufunguka kwa stomata, mawasiliano ya seli, n.k. kiufupi, madini haya huitajika sana katika mmea, na upungufu wake huwa haraka sana katika udongo, pale mimea inapooteshwa mingi sana.

Hoja kubwa ni kuwa, wakulima walipokuwa wakilima sana, mashamba makubwa sana, tena mazao ya chakula ambayo hufyonza madini mengi sana toka kwenye ardhi, ili kutengeneza chakula chake, baada ya muda ardhi hizi ziliishiwa kabisa madini. Na huku kulipelekea sasa mazao yasikue tena. Magugu tu ndo hukua, hii ni kwa kuwa huwa hayatunzi sana chakula yenyewe, na hivyo hata katika ardhi yenye madini kidogo yenyewe hustawi, pia magugu huwa na protini ngumu kama ‘’lignin’’, ambazo vimelea hushindwa kuzimeng’enya, na hivyo hubakia ikikua tu.

Ugunduzi wa mbolea za kisasa ambazo zenyewe zinaongeza madini kwenye ardhi moja kwa moja ilikuwa ni faida sana kwa wakulima wote. Sasa wangeweza kulipia deni la upungufu wa madini yale makuu matatu ‘’N-P-K’’, lakini pia wakaongeza na madini mengine mengi, kwa urahisi sana.

Upande wa pili ulimaji wa mashamba makubwa hupelekea kufyekwa sana kwa mapori, huku hupelekea wadudu wadogo wengi sana kukosa kabisa chakula kutoka mimea midogo. Na hivyo wanapoona mashamba ya wakulima, basi wote hujazana katika mimea hii mizuri, na hapo wakulima huteseka sana kwa uharibifu mwingine mpya wa wadudu. pia vimelea wengi wa ardhi hutegemea sana mabaki yaliyooza ya mimea na kuila, huku wakiibadilisha kuwa udongo. sasa ardhi huwa na misimu mirefu ya ukame mpaka msimu wa kilimo, ikiwa na mabaki machache sana. Na hivyo maelfu ya vimelea hawa hufa, na balansi ya madini kama mzunguko wa Nitrogeni kupitia bakteria kama ‘’Pseudomonas, Thiobacillus denitrificans, Nitrobacter, nirtomonas, etc’’ hushindikana kabisa. Hawa hubadilisha ammonia kuwa chumvichumvi za nitrite, kuwa nitrate, au nitrogen kwa ajili ya mimea. Hawa bakteria wengi hufa. na baadhi ya vimelea kama bakteria kadhaa na fangasi huwa hatari sasa hata kwa mimea, kwa kuwa huitaji kula hata mimea, na hivyo kuitengenezea magonjwa mengi sana shambulizi.

Ugunduzi wa dawa za kuulia wadudu na vimelea katika kilimo, ulileta Faraja kubwa sana. Kwa kuwa sasa wakulima wanaweza kutatua matatizo yao kiurahisi sana. Na ndivyo dunia nzima ilivyoingia katika namna bora kabisa za kilimo.

Lakini ukweli ni kuwa, Pamoja na kuwa mimea inakua, lakini bado ukuaji wake ni dhaifu. Hii ni kwa kuwa, kuna wastani wa madini kidogo sana katika ardhi, lakini pia mimea haiwezi kuzalisha mazao makubwa kutokana na mabadiliko ya chemistry hizi za udongo na hali za mvua. Pia hata kutokana na athari katika mifumo ya homoni  ya ukuaji wa mimea.

Habari njema tena kwa wakulima ikaja kwa ugunduzi wa namna za kuboresha moja kwa moja biolojia za mimea, ili kuweza kumudu mazingira haya magumu ya ardhi. Hapo ndipo kulikuwa na namna mbili, ya kwanza ilikuwa ni uboreshaji wa mifumo ya homoni za mimea, mfano, ‘’Plant growth regulators’’, kama vile boosters, n.k. hizi zimelenga zaidi kusaidia ukuaji kwa kubalansi homoni za ukuaji kama vile ‘’Auxin, Abscisic acid, Gibberellins, ethylene  n.k.’’ lakini wakulima waligundua njia hii Bado haina ufanisi sana.

Namna ya pili waligundua mabadiliko ya kijenetikia moja kwa moja ya mimea, mfano, waligundua taaluma ya kuchanganya jamii mbalimbali za mimea, kwa kuchagua ile inayoweza kukabiliana na hali za ukame, au upungufu wa madini Fulani. mimea ya namna hii huwa na mafanikio makubwa sana, hii inaitwa ‘’selective breeding’’, maana yake, kama mmea ungehitaji kutumia miezi minne kukomaa, na hali za mvua zimebadilika zimekuwa miezi isiyozidi mitatu. Basi ukichagua mbegu zinazokuwa haraka ndani ya miezi miwili tu, basi utafanikiwa sana. Lakini pia, kama mmea unatumia madini mengi sana mpaka kukomaa, basi ukiupata ambao unatumia madini kidogo tu, utakukomboa. Hii ni kama tu ilivyo katika kuku wa kisasa wa Broiler, unaoweza wala ndani ya week 4 hadi 6 tu. kwa wakulima wengi utasikia kauli kama ‘’Mbegu fupi’’ au mbegu zinazostahimili ukame, n.k. hii nayo ni taarifa njema sana kwa wakulima, na hata kwa wafugaji, ambao nao ni sehemu ya wakulima.

Kuhusu Mifugo

Kuhusu mifugo msingi ni uleule, Wanyama hawana kinga imara sana tena. kutokana na mazingira magumu ya ufugaji, upungufu wa virutubisho toka katika ardhi, selective breeding ambayo hushusha kinga za Wanyama kama tulivyoona katika Q8, lakini Wanyama wanafugwa kibiashara hivyo hawawezi kuishi maisha yao ya asili, na upungufu wa kinga utakaozaliwa suluhisho ni madawa. na pili ni kutumia Wanyama watakaokomaa mapema sana ili kuvunwa kibiashara.

Kama Joka

Lusifa baada ya kuwaingiza katika furushi lake wakazi wote wa dunia, furushi la mifumo yao mama ya chakula, yaani Kilimo. Sasa anajua hawataweza pambana na changamoto zifuatazo.

Kwanza kitendo cha kilimo cha mashamba makubwa kilimaliza madini katika ardhi, halafu matumizi ya mbolea za kisasa ziliharibu balansi ya madini moja kwa moja katika ardhi. Hii ni kwa kuwa ardhi inahitaji balansi kubwa sana ya madini, unapojaza madini ya N-P-K unafanya ardhi Kujawa na chembechembe za uasidi kama ‘’nitrates’’ ambazo kadri mvua inaponyeshea, ndivyo zinavyoingia mpaka katika vyanzo vya maji. Madini kama ya Phosphorus yanafahamika kwa asili yake ya kuunda chembechembe za uasidi ‘’phosphoric acids’’, potassium zinafahamika kwa kuathiri balansi za madini mengi ya calcium katika complexes ambazo huundwa katika udongo, au huungana na nitrates na kuchochea kujaa kwa hydrogen ambazo huchochea uasidi wa udongo.

chemistry ya udongo huathirika moja kwa moja kwa matumizi ya mbolea. Maji ambayo yalipaswa kuwa safi sasa hujazwa na aidha kemikali hizi toka mashambani, au toka mvua zenye makemikali ya asidi. Vyanzo vya maji hupoteza viumbe wengi sana ambao wanapokufa huzalisha sumu, mfano, tatizo la ‘’Algae blooms’’, ambao huzalisha sumu kama ‘’Mycystins, brevicystins, n.k.’’ hizi huua Samaki wengi, na magonjwa mengi ya vyanzo vya maji hutokana na madawa ya wakulima.

Wakulima hutumia sana kemikali kama ‘’Roundup’’, ambazo huwa na chembechembe zinazoitwa ‘’Glyphosate’’, hizi huua mimea mingi sana, kwa kuzuia uundwaji wa chembechembe za protini ‘’amino acids’’ kupitia chaneli inayoitwa ‘’shikimate pathways’’, na sasa basi, hii chaneli hutumika pia na kwa bakteria. Na kwa hivyo, hizi dawa huleta matokeo hasi sio tu kwa mimea, bali hata kwa vimelea, na hivyo kuua kabisa balansi ya mimea. Kibaya zaidi, hizi dawa huwa na matokeo hata zinapoingia katika mwili wa mtu, pale mtu anapokula chakula chenye mabaki ya madawa haya, humuathiri moja kwa moja mfumo wake wa homoni. Na hii imekuwa hata na kwa madawa mengine kama 2,4-D,  atrazine, na zingine nyingi, ambazo zote maranyingi zaidi zimeonekana kufanania zaidi chembechembe za estrogens, na kupelekea shida za uzazi, kwa wanaume kupungukiwa nguvu za kiume, kuzalisha seli za uzazi zilizoharibika, na vivyo hivyo kwa wanawake kuwa na shida kama viuvimbe kwenye mayai ‘’polycystic ovarian syndrome’’.

Matumizi ya mbegu fupi au za kustahimili hali ngumu ni kama matumizi ya vimalizia madini yaliyobakia kidogo katika ardhi. Yaani, ni kama baada ya kuula mnofu, sasa ukaacha sehemu zilizobakia kwa mafisi. Wakulima wengi na wasomi wengi hawalelewi umuhimu wa mzunguko wa nishati, sheria kuu ya sayansi inasema ‘’nishati huwezi iunda, au poteza, unaweza tu ibadilisha’’. Unapotoa madini katika ardhi, jua hakuna namna ya kuyarudisha pale bila kurejelea katika asili ya mzunguko wa awali wa ardhi ile, ambayo mpaka sasa hivi Lusifa ameshaubadilisha.

Hii inamaanisha kuwa, uzalishaji wa vyakula duniani unazidi kudorora. Na hata vyakula vinavyopatikana, vinazidi kuwa vilivyo dhaifu. Na uwezo wa kutatua matatizo haya, unazidi kudhoofika. Lusifa anatambua sasa hivi anaenda kuwafanya wote wakazi wa dunia kusujudia tena mamlaka yake kwa ajili ya kupata vyakula. Na hili analifanikisha kwa kuwa, kadri siku zinavyozidi kusonga, wakulima wadogo wanazidi kushindwa kumudu mashamba yao kutokana na ugumu wa kilimo na hasara za hatari za mabadiliko ya hali ya hewa, wakulima wachache sana wanaomudu hili, na hawa wengi wao ni matajiri wakubwa. Hawa hulima lakini huwa hawajali mzunguko wa vyakula kusambaza chakula, wao hujali tu kupata faida kubwa. Na kitendo cha watu wengi kukimbilia mijini, na kuondoka vijijini, kunawafanya wengi zaidi kutegemea mfumo mdogo kwa lengo la kujipatia vyakula, hili tayari linawaandaa kuwa watumwa, na wanyang’anyi ndani ya muda mfupi sana uliombeleni kama Biblia ilivyotabiri.