LUSIFA DHIDI YA STRESS #5
LUSIDA DHIDI YA STRESS
Kama Nyoka
Lusifa anatambua kama kuna jambo mwanadamu
linamtesa sana ni stress. Mwanadamu kama ilivyokuwa kwenye kazi, ndivyo
hivyohivyo ilivyo kwa stress. Mwanadamu hapendi stress, stress zinamaliza afya,
zinaondoa amani, na zinakaribisha hata magonjwa kwa watu. Mungu pia hapendi
kumwona mwanadamu akiwa na stress, na hii ndiyo sababu Mungu huwasisitiza sana
watu wake, Usiogope, kuwa na Imani, Pia Yesu anasema, Duniani mnayo Dhiki,
lakini jipeni moyo, ni ya kitambo kidogo tu, vumilieni.
Lusifa hana hiyo ajenda, yeye husema
ninayo namna bora kabisa ya kupambana na stress, nayo sio ya kuvumilia.
Utavumilia hata lini wakati unaweza kuishinda. Lusifa ameshawishi maelfu ya
wanadamu kutafuta namna kadha wa kadha za kupambana na stress, ambazo zote
zinakinzana na uvumilivu.
Kumeshamiri maelfu ya burudani kama za
miziki ya midundo, vinywaji kama Pombe, Sigara na Shisha, Madawa ya Kulevya,
Casino za pombe na Malaya, Cinema za filamu za visa vya Uongo na kubuni, Ulaji
wa vyakula vya misisimko mkubwa mdomoni, kumbi za mipira, michezo ya ngumi ya
kila aina, filamu za ngono, sherehe za ajabu ajabu, n.k. Lusifa anawaita watu
toka kona zote za babeli kuwa huku ndiko kuna suluhisho la stress zao, na
watapata furaha.
Lusifa hupata watu wengi sana kwa mbinu yake hii. na hii ni kwa kuwa hizi triki zote ni za uleweshaji kama tulivyoona katika sehemu zilizopita. Lusifa anatambua sayansi ndogo ya ubongo ya kutriki hisia za misisimko ya furaha na raha kwa watu, lakini anajua mbinu hii hufanya kazi kwa muda mfupi sana, na kuchochea msongo mkubwa zaidi ya uliyokuwepo awali. Na hivyo huwafanya watumiaji wote kuwa wategemezi zaidi na waraibu zaidi wa mbinu hizi, ambazo sasa huwafanya kuwa watumwa zaidi, lakini pia hukuza soko la vibaraka wa lusifa zaidi.
Kumbuka msingi wa mbinu hizi zote za uleweshaji ambao Lusifa huutumia, unaweza kujifunza zaidi katika injili ya sayansi Q4, lakini kwa ufupi sana, msomaji anapaswa kutambua, Lusifa hujikita katika kuuzimisha Ubongo kifikra, hata usiweze kufikiria zaidi stress. Na hii huwa kupitia sanaa za kurudiarudia kama inavyofanywa katika miziki ya kisasa, lakini pia, Lusifa anatumia mbinu ya kusisimua sana sehemu za hisia ‘’limbic system’’ katika ubongo. kwa uzalishaji sana wa homoni za dopamine katika sehemu zinazoitwa ‘’ventral striatum’’, mfano, ‘’nucleus accumbens’’, ambayo huusiana na uzalishaji mkubwa sana wa Dopamine, katika chaneli ya ubongo inayoitwa ‘’mesolimbic dopaminergic pathway’’, hii sehemu husisimuliwa sana na madawa karibia yote ya kulevya kama ‘’heroin, cocaine’’ hata sigara ‘’nicotine’’, Bahati mbaya hata sukari za juisi na soda nyingi hutumia ‘’fructose’’ ambayo nayo husisimua sana hii sehemu.
Nimeelezea sana Lusifa anavyoweza
kusisimua haya maeneo hata katika magemu, mipira, starehe kadha wa kadha, kwa
kurejelea tu uhusiano wa seli za ubongo kama ‘’mirror neurons’’, sehemu za
ubongo kama ‘’orbitalfrontal cortex’’ ambazo hupendelea vitu visivyougharimu
sana ubongo, mfumo wa hisia ambao huenda kinyume na sehemu zinazohusiana na
kufikiria. Unaweza kurejea kusoma injili ya sayansi Q1 kupata msingi mpana
zaidi.
Kama Joka
Lusifa kama joka amewakamata maelfu ya
watu na kuwafanya kuwa na msongo mkubwa wa Mawazo ‘’depression and major
depression syndromes’’. Hii ni kwa kuwa wengi wametafuta namna za kupambana na
stress, badala ya kukubaliana nazo na kuvumilia. Stress sio kitu cha
kukishikilia na kupambana nacho. Stress ni kitu cha kupambana nacho na kukiacha
unapomaliza tu sababu yake. Ni kama usivyokumbuka maumivu ya uchungu tena baada
ya kuzaa, hayana mantiki. Watu kwa kushindwa kufikiria namna ya kupambana na
stress zao, hasa kutokana na uvivu wa kutumia ubongo wao, na kukubali
kujishusha. Wamekuwa wahanga wa stress, na Lusifa huwaendesha kama gari bovu.
Dunia imejaa watu wanaopenda sifa toka kwa
watu, kuliko kutoa sifa kwa watu. Dunia imejaa watu wakorofi, na wakatili. Watu
wasio na upendo wa kweli, wanafiki, tena hata wanaoonekana wapo katika nafasi
zenye nguvu, ndiyo huongoza kwa kujinyonga kwa stress, na misongo mikuu ya Mawazo. Hii ni kwa kukataa msalaba
wa dhiki za kibinadamu, na kukimbilia mbinu za kisasa. Sasa mbinu hizo ndizo
zimezidi kuwatesa kuliko stress walizokuwa nazo awali.
Mafanikio ya Lusifa, ameweza kuwafanya
watu kuwa wabinafsi kama biblia ilivyotabiri kuhusiana na nyakati za mwisho.
Watu wamekuwa wadhaifu sana ndani ya nafsi zao, wamejawa na stress juu ya
maisha yasiyo na uhakika kabisa, hasa kwa kukosa Imani juu ya uwepo wa Mungu
anayeweza kujali hisia zao. Na kwa hisia hizi za stress, dunia imekuwa sehemu
hatari kabisa ya kuishi, imekuwa kama jangwa lililopana lakini lisilo na mimea
kabisa.


Join the conversation