Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

LUSIFA DHIDI ULIMI #2

LUSIFA DHIDI YA ULIMI

Kama Nyoka

Lusifa anatambua kwa kuchochea sana sensa za hisia za utamu wa protini kama nyama, na za Sukari  yaani ‘’T1R3/ T2R3’’, mtu huzalisha homoni za hamu nyingi sana ‘’dopamine’’. Lusifa akitaka kutengeneza uraibu, huchochea sanaa za upishi, uzalishaji, na matumizi ya bidhaa ambazo huwa na kiwango kikubwa sana cha chembechembe za kusisimua za bidhaa hizi. mfano, bidhaa za sukari, juisi na soda. Kuna maelfu ya aina za vyakula vya kisasa vyenye maelfu ya nguvu za msisimko, zingine zina protini zenye chembechembe kama glutamate za kutosha, za kusisimua Ladha. Zingine zina namna mbalimbali za michanganyo ya sukari hasa za ‘’fructose’’, zikiwa na chembechembe kadha wa kadha za makundi ya sukari. Michanganyo baadhi huongezwa visisimuaji vingine vya ubongo kama Caffeine, wengine huweka ‘’Monosodium glutamate’’ kwenye Supu, wengine huweka Ladha za kutengeneza kama za ‘’strawberries, vanilla, n.k.’’ wengine hutumia visisimuaji Ladha vya kisasa vyenye nguvu mara mia ya sukari kama ‘’Aspartame, neotame, saccharins, n.k.’’

Kuna maelfu ya aina za upishi, na aina za nyama na Ladha zake. Watu hupika katika namna mbalimbali za kisasa zilizolenga zaidi kuchochea Ladha za bidhaa hizi. Jambo ambalo wengi hawajui ni kuwa watu wamezidi kuwa waraibu wa bidhaa hizi, na kadri wanavyozitumia zaidi, ndivyo wanavyoongeza zaidi kiwango cha dopamine kinachotokana na utamu wa bidhaa hizi hata kutovutiwa na vyakula vingine vyenye wastani mdogo wa utamu ukilinganisha na bidhaa hizi.

Mafanikio ya Lusifa

Lusifa amefanikiwa kwa asilimia 100% kuchochea matumizi ya bidhaa hizi za utamu. Asilimia kubwa zaidi ya watu ni watumiaji wa bidhaa aidha za sukari, au za nyama, au za kukaanga. Pili, asilimia kubwa zaidi ya wanataaluma wa afya, hawaelewi msingi wa hatari za bidhaa hizi kwa afya za watu, wengi wao huegemea zaidi kupambana na matatizo yasiyo kiini cha shida za watu, na kibaya zaidi, hata wao wenyewe wengi wao ni wahanga wa matatizo ya afya. Msingi wa mifumo ya utabibu umebadilika kabisa, wataalamu wamekuwa wakifanyia kazi taasisi zao, na sio wagonjwa wao. Dawa zimekuwa ni Kinga, badala ya kinga kama dawa.

Kumbuka kwa taswira ya nje inaonekana viwanda vya madawa na vyakula ‘’Food and Drugs Industry’’ ndivyo chanzo kikubwa zaidi cha matatizo haya, kwa kupuuzia matatizo halisi yanayoikumba jamii, ambayo yanatoka mikononi mwao. Na huonekana kana kama kutokana na nguvu kubwa ya Uchumi wao, huwa na ushirika mkubwa sana na serikali za dunia hata kupuuzia uhalisia wa madhara makubwa wanayoyasababisha. Lakini ukweli ni kuwa, hiyo siyo hoja ya kweli kwa asilimia zote mia. Ukweli ni kuwa, Madawa na vyakula hivi ni sehemu ndogo tu ya taasisi ambazo Lusifa ameweka mkono wake, na sio kuwa Lusifa hutenda mwenyewe, Lusifa hutumia watu wenye akili nyingi sana kama alivyofanya enzi za Marekani kipindi cha ‘’Operation PaperClip’’ au Manhattan project, ambapo jopo dogo tu la wanasayansi waliweza kutengeneza Bomu la Nyuklia, au ‘’Atomic Bomb’’. Lusifa anayo timu yake ya siri ya watu wenye akili nyingi sana, ambao hutembea katika ramani hii ambayo Mungu ameamua kumfunulia msomaji anayesoma kitabu hiki. Hoja ni kuwa, sio matatizo yote yanasababishwa kupitia ulaji, ila ulaji ni sehemu kubwa sana katika uharibifu ambao walahu, watu wachache baadhi wameweza kuugundua, lakini kuna mengi bado wasomi wengi hawajui, lakini mwisho wa sura hii, kila msomaji atakuwa amekwisha Jifunza.

Kama Joka

Kitabu chote cha Injili ya sayansi Q4 kimejaa Uharibifu unaofanywa na bidhaa hizi za tamutamu. Kama utaweza kuweka sumu kidogo isiyoweza kugundulika kirahisi, katika kitu ambacho kitakuwa kikitumika sana, basi sumu ileile kidogo inaweza kufikia kiwango kikubwa kutokana tu na matumizi yake kuwa makubwa. Hii huwa napenda kuiita ‘’Dilemma’’, yaani, sumu ni kitu kinachoathiri afya, au maadili ya kitu’’. Sasa basi, vitu vingi vilivyo sumu katika bidhaa hizi za utamu utamu, huwa sio sumu katika utengenezaji wa bidhaa hizi zenyewe. Yaani, mfano chembechembe za ‘’Emulsifiers’’ ambazo huongezwa kuvunja vunja mafuta katika michanganyo ya bidhaa za juisi, au vinywaji, au vimiminika vingi vya kisasa, huwa vinasaidia kuboresha mkorogo wa vinywaji hivi, lakini ukweli ni kuwa mwilini mwa mtumiaji huwa havihitajiki. Na ndivyo ilivyo kwa chembechembe zote zinazoongezwa kama vile ‘’stabilizers, food dyes, flavors, colors, enhancers, n.k. ‘’ hizi zote huwa hazihitajiki mwilini, na huchaguliwa kwa viwango vyake vidogo vya madhara kwa afya.

Ndivyo ilivyo pia kwa nyama, ambazo mwili huitaji gramu 250 mpaka 500 tu mwilini kwa wiki nzima, lakini walaji wa nyama hula mara kumi na kuendelea zaidi ya inavyohitajika, hupelekea kujaa kwa chembechembe hatarishi zinapozidi kama mafuta ‘’SFA’s, viwango vya uasidi ‘’acidic amino acids’’, madini chuma mengi, madhara ya upungufu wa madini ya Calcium, shida za madawa, upungufu wa kambakamba ‘’fibers’’, shida za chembechembe zinazochochea saratani hasa kwa nyama za kusindikwa, mfano, chembechembe za saratani kama ‘’Heterocyclic amines, Polycyclic aromatic hydrocarbons’’, n.k. kiufupi ulaji wa nyama sio hatari sana, lakini ulaji wa nyama za Wanyama wa kufuga hasa katika zama hizi, ni hatari sana kwa afya kuliko wengi wanavyohisi.

Takwimu na uhalisia ni kuwa, idadi kubwa kabisa ya watu saivi huumwa matatizo yasiyo ya kuambukiza. Matatizo mengi zaidi watu wanayoumwa hutokana na shida za moyo, shida za kupungukiwa kinga za mwili, shida za kiakili na ubongo, magonjwa ya virusi, kupungukiwa nguvu za kimwili, uwezo wa kufanya maamuzi, na kibaya zaidi, ni utegemezi wa madawa na mahospitali kutatua changamoto zinazowatesa watu.

Mafanikio ya Lusifa

Ameweza kuwadhoodisha maelfu ya wanaume kuwa dhaifu kiakili, kwa kuwaathiri mifumo yao ya kihomoni za kiume, na afya zao za uzazi. Ukiua mifumo ya homoni za wanaume, umeshawaua hata wao wenyewe. Lusifa hakuishia tu kuwaua wanaume katika mifumo yao ya kihomoni, au kiakili. Pia amewaathiri sana katika mifumo yao ya kimwili kwa matumizi ya bidhaa hizi, maana hizi bidhaa huwafanya kuwa wasisimkaji wa juu juu tofauti na asili ya wanaume, ambayo ni ya utululivu na ufatiliaji. Wanaume kwa bidhaa hizi hupunguza nguvu za mifupa yao kwa kupungukiwa madini ya muhimu sana katika miili yao kwa bidhaa hizi, wanaume huchochewa kupata shida za insulin ‘’insulin resistance’’, wanaume hupata mafuta mengi sana katika miili yao ambayo ni matokeo ya mitindo mibaya zaidi ya kiafya, na huwaathiri.

Lusifa amefanikiwa kuwafanya maelfu ya wanawake kuteseka kwa shida za migongo, matatizo ya presha, maumivu ya viungo, matatizo ya uzazi, uraibu uliokithiri, na magonjwa sugu ambayo huwafanya kuwa watumwa wa mifumo yao ya kitabibu, ya kiserikali.

Lusifa amefanikiwa kuwafanya watu kuendelea kuwa wahanga wa matatizo sugu, ambayo kwayo hawawezi kuacha kutegemea madawa, wala pia hawawezi kuachana na vyanzo vyake kutokana na uraibu. Hii ni namna ya kisasa sana ya utumwa, ni kama ilivyo kwa kahaba ambaye kadri anavyofanya uchafu wake, ndivyo anavyojipatia fedha lakini pia anajisikia raha zaidi. Ukimwambia kahaba aache tabia yake hawezi, sio kwasababu tu ya uozo wa afya yake ya kimwili ambayo hawezi tena kufanya kazi zingine, pia kutokana na uozo wa afya yake ya kiakili ambayo hawezi tena kuachana na uraibu, na hivi ndivyo mauti humfikia pale ambapo huwa hana familia, huweza kupata magonjwa, hawezi tena kufanya ukahaba kutokana na umri, au hata huweza kufia katika aibu yake. Watu hawawezi tena kuachana na uraibu wa bidhaa hizi, hata kama watapitia madhara yake, wengi wapo ambao huishi kwa kutegemea tu bidhaa hizi kiuchumi, na hivi ndivyo ilivyokuwa malengo ya Lusifa tangia awali kabisa.