Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

ASILI YA LUSIFA NA UTARATIBU WA AWALI WA ULIMWENGU #12

UTARATIBU WA AWALI WA ULIMWENGU NA KUIBUKA KWA LUSIFA



SEHEMU YA KWANZA

Kabla ya Kwenda kiundani kabisa kumtambua lusifa, ni vema tukamtambua kwanza Mungu. Ili ije kuwa rahisi kumtambua Lusifa.

MUNGU NI NANI?

Mungu ni nafsi ya uweza wa juu zaidi yenye kuwezesha kila kinachotambulika na kutendeka. Tofauti ya Mungu na nafsi zinginezo, ni sifa kuu tatu za Mungu.



Maswali kadhaa juu ya Mungu

1.Kama Mungu anaweza yote, je anaweza kujiua? Anaweza kuumba kitu kilichomzidi uweza? Kama Hapana, ina maana Mungu hawezi yote?

-Jibu; kama ataweza kujiua mwenyewe, maana yake hana akili au maarifa makubwa zaidi. Hii tayari itaua sifa yake ya uwezo wa kujua yote ‘’omniscience’’, na kwa hivyo swali hili linakosa mantiki, maana linavunja sifa yake nyingine ya Uungu.

-Kama ataumba kitu ambacho kitamzidi Nguvu, maana yake tayari ana mipaka ya uwezo. maana yake hatakuwa tena mwenye uweza wa juu zaidi wa kuweza yote. maana tayari kitakuwepo kitakachokuwa kimemzidi uwezo. Hii tayari inaua sifa yake ya ‘’omnipotency’’. Kuumba kitu kitakachokuwa kimemzidi uweza pia, kitamaanisha kuwa, yeye ana uweza mdogo hata kuzidiwa na matokeo yake, hii itaua uwezo wake mkubwa zaidi wa kimaarifa ‘’omniscience’’, hivyo swali hili nalo halina mantiki.

Unapomzungumzia  Mungu, unamzungumzia original wa kopi ambayo ni binadamu. Hakuna  namna ya kumuelewa  Mungu zaidi ya kuelewa mfano wake ambaye ni mwanadamu. Kwa maana hakuna mwanadamu aliyewahi kumuona Mungu katika utukufu wake. Kuna watu kadhaa hukataa Uungu wa Kristo, kwa hawa hawatawahi milele kumjua Mungu, kwa kuwa ni neno tu, ambaye ndiye Kristo tunaweza kumjua Mungu. Yesu mara nyingi alisema, mkiniona mimi, mmekwisha mwona Baba. hapo mwanzo alikuwepo neno, naye neno alikuwepo kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.   Biblia inamtambulisha Yesu kuwa ndiye neno.

2. Kama Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote, je yeye ameumbwa na nani?

Jibu: kwa kuwa kila kinachoishi kinatumia damu, haimaanishi visivyo na damu haviishi, mfano, mimea. Vivyo hivyo, kwa kuwa kila kiumbe kiliumbwa, haimaanishi mwanzo wa kila kitu ni matokeo ya kuumbwa. Mungu hakuumbwa, na ili aitwe Mungu lazima awe ni Muumbaji, sio muumbwaji, na ndiyo maana Mungu haabudii kiumbe chochote, yeye tu ndiye anayeabudiwa.

Wanafizikia kadhaa awali waliokuwa wakinga’ang’ania kuwa asili ya vyote vilivyomo ulimwenguni ni matokeo ya mlipuko wa awali sana, wa Big-bang, ulioanzia katika sifuri, na kuumba kila kitu, kama nilivyoelezea katika Q3. Nao sasa wanaamini sio kila kitu kiliumbwa, mfano, eneo la ulimwengu ‘’space’’, nishati ‘’energy’’, na hata taarifa ‘’information’’.

Kwa kuamini hivi, tayari wanarudi katika Upagani ambao ulikuwa nao ukiamini kuwa kuna vitu au viumbe visivyoumbika mfano wa miungu ‘’gods’’ katika asili. Na ndiyo maana walikuwa wakiabudu asili, mfano, miti, jua, milima, n.k. hii kitaalamu huitwa pia ‘’pantheism’’, ambayo tokea katika falsafa za kina ‘’Spinoza’’, mpaka wanafizikia ‘’Einstein’’, walikuwa wanaamini. Kiufupi asili na sayansi inaonyesha kuna Mungu aliyeumba, changamoto pekee ni watu kumtambua huyo Mungu, na kumcha.

TWAWEZAJE KUWA NA UHAKIKA NA MUNGU

Uhakika ni matokeo ya Uthibitisho wa ushahidi wa taarifa Fulani. Asili inaonyesha kuwa kuna Uumbaji wa Mungu ‘’intelligent design’’. katika Q1 tuliona huwezi kuona simu porini ukasema ilijiumba katika miaka mamilioni iliyopita, lazima tu utasema imeumbwa kwa akili za kiumbe mwenye akili sana, sio nyani, bali binadamu. Unapomwona huyo kiumbe mwenyewe binadamu, unaweza kupataje ujasiri wa kusema yeye alijitokea tu? Na ndiyo maana maelfu kwa maelfu ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu.

Katika Q1 tuliona ulimwengu wetu ni special kwa kiwango kikubwa sana. Kuna maelfu ya vigezo vya kusapoti uhai wa sayari , na viumbe wake, ambavyo kama vingebadilika hata kwa nyuzi 0.000000000001, basi kusingekuwa na uhai leo hii. lakini maelfu ya vigezo hivi vimewekwa kwa ustadi kabisa, kusapoti uhai, mpaka uwepo wa jua.

Wataalamu wa sayansi za nyota hata wasiomwamini Mungu kama Brian Cox husema, hakuna jambo la ajabu kama ulimwengu, kwa sehemu ndogo sana tunayoweza kuangalia angani, kuna uwepo wa Galaxies Trilioni mbili, ambapo Galaxy moja tu ina nyota zaidi ya Bilioni 400, kumbuka sisi duniani tunaizunguka nyota moja tu katika mfumo wetu wa jua. Na Galaxy yetu kwa mfano, ambayo tunaiita ‘’Milky way galaxy’’, ili utembee mpaka uimalize, unahitaji kutembea kwa spidi ya mwanga, na kisha utumie miaka 100,000, ili uimalize. Na hata hivyo galaxy yetu ni saizi ya kati tu, sio kubwa sana. Kiufupi, katika galaxy yetu hatujaweza kuona Ushahidi wa uwepo wa uhai katika sayari au sehemu nyingine yoyote ile, zaidi ya mabaki tu ya chembechembe za uhai zilizo angani ‘’organic molecules in universe’’, ambapo katika Q3 nilielezea kuwa ni mabaki ya gharika ya Nuhu yalitupwa angani kipindi cha mpasuko wa vilindi vya nchi.

Hiyo inadhihirisha namna uhai usivyoweza kuwa ni matokea ya bahati bahati tu. huwezi kutumia hisabati za bahati ‘’probability’’ kuelezea uwezekano wa kutokea uhai katika sayari ya dunia. Maana Pamoja na kuwa ulimwengu tu haiwezekani, hata uwepo tu wa maji katika hali bora kabisa ya kimiminika katika sayari ya dunia, tayari ni jambo usiloweza kulielezea pasipo kukubaliana na uumbaji. Wanabiolojia tunafahamu ya kuwa, yawezekana mahesabu ya nje ya dunia na sayari yakawa ya kawaida, lakini unapokuja katika swala la uhai, kuanzia katika DNA na seli, mpaka katika utambuzi ‘’consciousness’’, hakuna bahati bahati unayoweza kutumia kuelezea namna uhai unawezekana pasipo Muumbaji.

Mifumo ya utendaji kazi wa chembechembe za uhai na seli hutumia mawasiliano bora kabisa, kwa usahihi kabisa, tena katika namna za ajabu kiasi hata tu mwanadamu msomi kuelewa huwa ni changamoto, lakini mwili hufanya haya matendo katika namna ya kushirikiana kila sehemu, siyo sehemu moja kuwa chanzo cha nyingine. Wasomi dhaifu huisi wenda DNA ikaweza kuelezea kila kitu, lakini katika Q5 na Q4, tuliona kuwa DNA huongozwa na seli, protini huongozwa na enzymes, na enzymes hutegemea protini, kila kitu humtegemea mwenzake. Ni kama ilivyo kwa mammalia  baina ya jinsia, hakuna jinsia iliyo chanzo kwa mwingine, zote hutegemea uwepo wa mwingine, bila jike dume hatazaa na hivyo hivyo bila dume jike hatazaa, na inapotokea changamoto katika uundwaji wa jinsia, ndiyo huibuka changamoto kama za uwepo wa vilema wa kuzaliwa, watu wenye jinsia zisizo kamilika, n.k. wasomi wadogo huisi mfano, utokeaji wa Watoto walio na sifa za jinsia zote kuwa ni hatua za Katikati za uumbaji ‘’intermediates’’, na hawa wengi huwa ni wananadharia za mabadiliko ‘’evolution’’, kwao hawashindwi kutetea haki za mashoga, bila hata kujali namna fiziolojia na asili zinavyopingana na ukweli wao. Hawa sio wanasayansi bora.  

Hakuna sehemu katika fiziolojia kuwa kuna sehemu iliyo chanzo cha sehemu nyingine, maji huiua seli, lakini pia bila maji seli hufa, yote na zaidi hudhihirisha uwepo wa Mungu. Hivyo akili na asili vyote vyadhihirisha uwepo wa Mungu, lakini bado binadamu wanahitaji kuzungumza zaidi na huyo Mungu wao. Hii ni kama tunapokuwa kwenye Nchi kadhaa, au taasisi kama shule, au vyuo. Ijapokuwa tuna uhakika wa uwepo wa viongozi wakubwa katika maeneo yetu, lakini bado huwa tunahitaji kuzungumza nao, na kujua dhumuni lao la kutuhitaji sisi pale, hilo pia ndilo lengo kubwa la kuhitaji kumjua Mungu. Maana binadamu hakuchagua kuumbwa, ila alijikuta ameumbwa. Gari halikuchagua kuumbwa, ila lilijikuta tu lipo gereji likipatiwa haki yake ya matengenezo. Tunawaje kuzungumza na huyu Mungu.

MAWASILIANO YA VIUMBE NA MUNGU

Mungu hakumuumba binadamu tu, Mungu aliumba viumbe wengi sana ndani yake ikiwemo na Malaika Lusifa ambaye ndiye mhusika mkuu kabisa katika kitabu hiki. Lakini binadamu ni wa muhimu sana kwa kuwa, hawa ndiyo mfano mzuri kabisa wa Mungu mwenyewe. Mawasiliano tunayoyazungumzia hapa, ni mawasiliano baina ya Mungu na viumbe wake wote. Mungu huwa na namna ya kuwasiliana na viumbe wake, ambapo sisi tunazozijua kama inavyoelezwa katika Biblia, ni kwa kutumia neno.

‘’Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo Mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika’’ Yohana1:1-3

Yesu ndiye ‘’Neno’’,  ‘’Word’’. Kisayansi ni rahisi sana kuweza kuelewa maana ya hili fungu. Chukulia ungekutana na mtu na kisha akakaa kimya, na hujawahi onana nae. Bila shaka hutaweza kuelewa nini kilicho kichwani mwa mtu huyo. Utakuwa tu na makisio kadhaa kutokana na mwonekano wake, jambo ambalo lingekufanya tu uwe kama wanasaikolojia. Utaweza kuanza kumuelewa mtu atakapoanza kufungua mdomo, na kisha kuanza kutoa ‘’Maneno’’.  Mathayo 12:34 ‘’, Kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake’’. Sehemu inayohusiana na kuchambua lugha katika ubongo ‘’wernickle’s area’’, ipo katika makutano ya sehemu zote za utambuzi wa taarifa za ubongo kwa maeneo ya nyuma ‘’temporal parietal junction’’, na sehemu inayohusiana na kutamka maneno katika ubongo ‘’broca’s area’’, ipo sehemu ya ubongo wa mbele inayohusiana na kufikiria, na utendaji, maeneo yanayoitwa kitaalamu ‘’inferior frontal gyrus’’. Hii ni kusema, mtu anapozungumza, huwa anasema taarifa zilizosambaa katika ubongo wake wote, na ndiyo kweli yaujazayo moyo wake.

Yesu ambaye ni ‘’Neno’’, anaitwa ‘’neno’’, kwa kuwa yeye ndiye namna pekee ya kuelewa Nini kilicho katika akili na malengo ya Mungu juu ya mwanadamu, ambaye yeye mwenyewe alishiriki katika Kumuumba.

Mwanzo1:26 ‘ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;akatawale Samaki wa baharini, na ndege wa angani, na Wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.’’

Neno ni Yesu, na neno ni Mungu. Yeye anaitwa Neno kitaalamu kwa kuwa ndiye namna Mungu anajidhihirisha kwa viumbe wake kupitia yeye. Wataalamu wa jenetikia wanatambua, unapoona mtu ni mrefu, au mfupi, au mweupe au mweusi, haimaanishi kuwa huyo mtu sio mweupe kama anaonekana mweusi, au sio mfupi, kama anaonekana mrefu, bali ni sehemu tu za jenetikia zake ‘’genes’’ za ufupi, au urefu, au weupe, au Weusi, unakuta mojawapo tu ndizo zinazokuwa zimejidhihirisha ‘’gene expressed’’, na zingine zinakuwepo, ila zinakuwa tu hazijajidhihirisha  ‘’structural genes’’. Kwa hiyo hata mimi na Ngozi yangu angavu, ningeweza kuwa na Ngozi yenye weupe sana, au Weusi sana, ambapo hizi zote ni matokeo tu ya jenetikia zinazoongoza uzalishwaji wa chembechembe za Ngozi za melanin, unaweza kuelewa zaidi katika kitabu chetu cha ‘’Ubongo wa Mtu mweusi’’ tulipoangalia asili za tofauti za watu kati ya mabara na mabara, na sehemu na sehemu.

YESU NI NANI?

Watu baadhi huwa hawaelewi kwanini Yesu huwa ni serious ishu zaidi hata ya Mungu kwa ujumla. Watu wengi sana hawana shida sana na Mungu, lakini shida huwepo kwa Yesu. Na hata Mbinguni, Lusifa alishindana na Yesu ‘’Mikaeli’’. Kiufupi Yesu ni Mungu. na Yesu alikuja Duniani ili kudhihirisha dhumuni la Mungu kwa viumbe wake. Sasa basi, kuelewa hili, itabidi tujue yafuatayo.

Yesu sio mwana wa Mungu, ni kielelezo cha mwana wa Mungu.

Waebrania7:3 ‘’ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu);huyo adumu kuhani milele.’’

Kama fungu linavyojieleza, hakukuwa na namna ya wanadamu kuelewa namna ya Mungu zaidi ya kutumia kielelezo cha vitu walivyovizoelea kuviona. Inafahamika kitaalamu, huwezi kuota ndoto ya mfano wa kitu ambacho hujawahi kukitambua. Huwezi kuota upo na Mungu, lasivyo utatengeneza taswira ya kuwa Mungu anafanania kama Babu mwenye mvi nyingi, na mavazi meupe, hayo yote siyo kweli. na ndiyo maana filamu nyingi za Kristo, zimewafanya watu kuhisi Yesu ana mwonekano wa mwigizaji kama ‘’brian’’  na wengineo wa filamu ya Kristo.

Ilimbidi Yesu atumie kielelezo cha Mwana, na kuonyesha jinsi alivyo na utegemezi wote kwa Baba yake, jambo ambalo ni kweli. Yesu alipokuwa duniani alikuwa mwanadamu asilimia zote 100%, hakuwa na Uungu aliouficha sehemu, ila alikuwa bado na utambulisho wake wa asili wa kuwa yeye ni Mungu. Na ndiyo maana hakuna sehemu watu walimwona na kusema huyu ni Mungu, hata Shetani, hakulalamika mahala popote kwa kusema, wewe unashinda dhambi kwa kuwa una nguvu za Uungu. Ila alimwambia kuwa, utakufa na njaa, badili jiwe liwe mkate kama wewe ni mwana wa Mungu. Hii ni sawa na kusema, wewe sio mwana wa Mungu, wewe ni mtoto wa yusufu tu kama wengine wanavyokusema, na ndiyo maana unateseka, kama si kweli, thibitisha. Kitaalamu zaidi, shetani alikuwa anajua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, ila alikumbana na changamoto awali sana tokea mbinguni ambayo tutaiangalia tutakapoanza kumchimbua kiundani zaidi.

Kwanini kung’ang’ania Yesu ni mdogo kwa Mungu hakuna maana?

Katika hisabati huwa kuna msemo unasema, isiyo na mwisho ‘’infinity’’ ukijumlisha na moja bado itabakia isiyo na mwisho ‘’infinity’’,bado  ukitoa, au ukizidisha itabakia ileile, kiufupi, unaposema Mungu, una maanisha asiye na mwisho ‘’infinity’’. Unaposema asiye na mwisho ‘’infinity’’, ni mdogo, na kuna mkubwa, haina maana ‘’Nonsense’’.

Unaposema Mungu, unamaana moja kwa moja ya kuwa, ndiye kilele cha uweza. Kama Mungu atakuwa ni mdogo, maana yake huyo aliyemkubwa wake ndiye Mungu. Unaposema Mungu ana mwanzo, kuwa aliumbika wakati Fulani wa awali sana, tayari unamaanisha yeye sio ‘’asiye na mwanzo na mwisho’’ au ‘’infinity’’.

Wasomi baadhi husisitiza kuwa Yesu Kristo, ni mwana wa Mungu ‘’literaly’’, kwamba, alikuwa na mwanzo katika hatua Fulani za awali sana za Ulimwengu. Kuwa alizaliwa, wasomi hawa hutumia Ushahidi wa Mufungu kadhaa, kama yafuatayo

Mithali 8:23-24 ‘’Nalitukuka milele, tangu awali, kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa, wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.’’

Wasomi hawa hutumia neno ‘’nalizaliwa, kuonyesha kuwa Yesu anao mwanzo, na hivyo ni Mungu kwa asili ya umwana, lakini sio Mungu.

Pia hutumia fungu lifuatalo

Waebrania1:5 ‘’Kwa maana alimwambia Malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Wasomi hawa husema kuwa hoja hii humaanisha kuwa, Yesu alizaliwa kutoka kwa Mungu katika wakati Fulani wa awali sana, na hivyo kuwa na upekee sana wa uungu. Lakini hoja ya msingi hapa hubakia ileile ya kuwa, Yesu sio Mungu ‘’rejea sifa kuu tatu za Mungu’’.

Mathayo 24:36 ‘’Walakini Habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata Malaika walio mbinguni, wala mwana, ila Baba peke yake.

Wasomi hawa hutumia hili fungu pia kumaanisha kuwa, Yesu hajui yote. Na kwa mantiki hiyo sio Mungu, maana sifa moja wapo ya Mungu, ni kujua yote ‘’Omniscience’’.

Mathayo 27:46 ‘’Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

Mafungu ya namna zote ambazo Yesu alijionyesha moja kwa moja akijishusha, na kuonyesha utegemezi wote kwa Mungu wake. Wengi wa wasomi hawa huyatumia kumaanisha kuwa, Yesu mwenyewe anatambua kuwa kuna Mungu, na sio kuwa yeye ni Mungu.

Changamoto za fasiri mbaya zinazowafelisha wasomi hawa

1.Wasomi hawa wote kwanza hutumia makisio ‘’Assumptions’’ kwamba, namna za kiungu, ni asilimia 100% sawa na namna za kibinadamu.

Hili ni tatizo baya sana kuwahi kutokea kwa akili za binadamu mdhaifu kabisa. Binadamu ameumbwa kama kakitu kadogo sana. Sisi ni kama wadudu, soma Ayubu 25:6 ‘’siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!’’ ukisoma mafungu ya juu yake, utaona kuwa Mungu anaelezea namna ulivyo ukuu uwezo wake, uumbaji wake, awali nilisema, wengi wa wasomi hawa, hata hawajui kuwa wapo katika dunia ambayo ni kama ka uchafu tu, katika ulimwengu.

Ukisoma ‘’Astronomy, au Cosmology, au Modern Physics’’, utagundua wasomi hawa wanaohisi Mungu ni kama mwanadamu, au Njia za Mungu ni sawa na za mwanadamu, utagundua hawajui hata tu kani ya Gravitation, ni maajabu yanayoweza kujaza vitabu, na wataalamu kama kina Newton, au Einstein, wakipata umaarufu, na wanafizikia wakipata Nguvu za kutawala dunia, kwa kutumia tu sheria chache za maajabu ya Mungu. Unawezaje kuelezea mizunguko ya sayari zaidi ya tatu, huitwa ‘’Three-body problem’’, hakuna afahamuye mpaka leo, unaweza kutambua kipi kiusukumacho ulimwengu kadri unavyozidi kutembea, hakuna atambuaye? Matajiri wakubwa na wanasayansi wakuheshimika zaidi, kama Elon musk, taasisi za NASA, n.k. wanazidi kutawala dunia kwa namna wanavyojifunza zaidi sheria za ulimwengu ‘’sheria za Mungu’’ za utendaji wa ulimwengu, sayari , n.k.

Mtu mmoja mdogo sana kimaarifa ambaye hajui hata kuwa anatumia milango mitano tu ya fahamu, na kuwa taarifa zingine ambazo zinaweza kuwa nje ya milango hii hawezi kuzitambua, na sio kuwa hazipo. Kutokujua haimaanishi kuwa haipo, inamaanisha kuwa wewe ni mjinga. Kila unapoenda hospitali ukiwa na shida sana na hujui unasumbuliwa na nini, inamaanisha kuwa wewe ni mjinga, tena wa kimaarifa tu. Vipi kuhusu kuelewa taarifa nyingine zilizo nje ya utambuzi wako. Ndege wanaona mawimbi ya usumaku ‘’magnetic fields’’ wakati binadamu hatuwezi! Binadamu anataka kumjua ‘’Roho mtakatifu’’, na anasema ‘’Roho mtakatifu’’ ni kama uwepo, au uwezo, ilihali hata usumaku tu haujui huwa unakuwaje! Huu ni ujinga. Ni vyema ukatambua Mungu pekee ambaye tumeweza kumtambua kupitia milango yetu ya fahamu, ni Yesu Kristo.

Na ninapoandika hiki kitabu, haimaanishi kuwa mimi ni mwandishi tu, kitabu hiki ni sehemu moja tu ya mimi. Mungu anapomuumba binadamu, haimaanishi kuwa umilele wake wote umejikita kwa miaka 6000 tu ya binadamu, kuna mengi ambayo Mungu anajihusisha nayo milele na milele. Yesu amejidhihirisha zaidi kwetu, haimaanishi yupo pale akitutegemea, na kwa ajili yetu tu. Je, nani anayejua katika Ayubu2:1 kulipokuwa na kikao mbinguni, cha wana wa Mungu toka mbingu tofauti tofauti zilizoumbwa na Mungu, nani ajuaye kuwa ajenda zilikuwa ni zipi?

Suluhisho la tatizo hili

Mwana wa Mungu ni kielelezo na sio maana ya moja kwa moja ya uzazi kiungu. Ukisema Mungu amezaa, au amezaliwa, unaharibu maana, rejea.

Waebrania7:3 ‘’hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani wa milele.

Haihitaji tafsiri zingine za tofauti na maana hii, maana Mungu asingetaka maarifa yake yawe na maana za siri. Yesu ameitwa mwana kama kielelezo maana mwanadamu asingeweza kuelewa maana mbali na hii.

Tatizo la kifalsafa

Duniani baada ya dhambi, kila kitu kilianza kubadilika kuelekea kufeli na kufa. Na huo ndiyo mwanzo wa hisia za matabaka, na mashindano. Mungu alipomuumba Adamu na Eva awali, kwanza wote waliumbwa siku ya sita ‘’walikuwa sawa kiumri, ni kama mapacha mmoja atangulie kuzaliwa, afanye kazi kadhaa, na baadaye mwenzake azaliwe’’ pili wote waliumbwa katika namna ya usawa katika mantiki na thamani, walikuwa sawa katika namna ya utofauti wao kiutendaji, kitabia, na Walipendana sana, wala haikuwepo maana ya Adamu kuwa juu, au wathamani zaidi ya Eva.

Huu ndiyo ulikuwa mfano wa Mungu. Baba na Mwana, wanafanania ‘’Adamu na eva’’ kama wanavyosema na tuumbe mtu kwa mfano wetu. Na ndiyo maana Biblia katika Mwanzo5:1 inasema ‘’mwanaume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.’’

Mwanamke ni utukufu wa mwanaume ‘’1kor11:7’’, lakini pia ‘’Yesu ni mg’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi ya Mungu baba 1 ‘’Ebr1:3’’. Kitaalamu Nguvu na thamani ya mwanaume inaleta mantiki anapokuwa katika upendo na mwanamke wake. Vuta taswira mwanaume angelikuwa na kila kitu, ila yupo peke yake dunia nzima, bado kuna kitu kingekuwa kimekosekana. Na ndivyo ilivyo pia kwa Mungu baba. Mungu amejitolesheza katika upendo milele yote hata kabla ya uumbaji kwa uwepo wa nafsi hizi tatu.

Tatizo la kifalsafa ni kuhisi Mungu naye itampasa kuwa katika namna ya kimatabaka kama ilivyokwetu. Yaani, kwa kuwa Baba ni juu ya mama, basi Baba ni juu ya mwana. Haikuwa hivyo, soma Mwanzo3:16 ‘’Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa Watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala’’. Mwanamke alikumbana na laana ya kutawaliwa na kuwa chini ya mwanaume baada ya Kutenda dhambi ya kutamani kujiinua, na kuwa sawa na Mungu kwa kula tunda, na kumshawishi na mumewe ‘’adamu’’, ambaye naye alikula kwa kumpenda sana mkewe, kuliko hata kumtii Mungu, naye akapata laana ya kujikuta Upendo wake ukipungua kwa mkewe.

Mungu hutengeneza laana kwa kuruhusu madhara ya machaguo yetu kuturudia wenyewe. Mwanamke alianza kupatwa na hisia za kujiinua, soma Mwanzo3:6 ‘’Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti Wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala’’. Mwanamke alianza kula akiwa peke yake, na ndiyo maana ukisoma 1Tim2:14 inasema ‘’Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa’’. Kwa hiyo matabaka yaliyopo leo baina ya mwanamke na mwanaume, sio mfano wa Baba na Mwana tena, bali ni matokeo ya dhambi.

Kumbuka hata mwanaume naye siyo mfano mzuri sana wa Mungu, ijapokuwa Yesu alikuja kwa jinsia ya mwanaume. Kwakuwa, mwanaume baada ya dhambi, amekuwa na hasira kwa maamuzi yake aliyoyachukua kwa kufuata hisia, na sio neno la Mungu. Na madhara yake hata leo wanaume ndiyo viumbe wanaoteseka zaidi, iwe vitani, iwe magerezani, iwe kwa ajali za usafiri, n.k. kifiziolojia wanaume wanasehemu kubwa sana ya kuhisi hisia za maumivu, yaani ‘’amygdala’’, wanaume huteswa zaidi na stress, na hushindwa kuzionyesha hata tu kwa machozi, wanaume hawapendi kuonekana wakilia, au wakiwa wadhaifu, hata homoni za prolactin za machozi ni chache kwao, wanaume huvumilia zaidi maumivu, na hivyo kuumia zaidi, sehemu ya ubongo inayohusiana na kuvumilia maumivu ‘’Periaquaductal gray matter’’ kwa wanaume ni kubwa zaidi.

Biblia ilishaandika katika Mwanzo3:19 kuwa ‘’kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi’’. Hili ni agano la Mungu kwa mwanaume kuwa, atateseka mpaka atakapokufa, hapa anamfanya atambue matokeo ya hisia zake mwenyewe alizozichagua. Mwanaume sasa anakuwa mwenye ghadhabu, na mpambanaji wa kwenye mazingira yenye dhiki, hii inamuongezea utawala wa ukatili, kumbuka mwanaume anakiwango kikubwa sana cha homoni ya ‘’Testosterone’’, ambayo humfanya kuwa mkali ‘’aggressive’’, mkamiaji, mlazimishaji, mfuatiliaji wa kina, na ndiyo maana sayansi za vita na taaluma za kutafuta njia kwenye nyakati ngumu, wanaume huwa bora zaidi.

Usishangae tu namna kwa Wanaume ilivyorahisi sana kugundua hisabati au sheria mpya za fizikia, shangaa pia ilivyo rahisi kwao kugundua makombola mapya vitani, style mpya za kupigana, namna walivyo na ujasiri hata kufanya vitu hatarishi zaidi, mtoto wa kiume haogopi kupanda mti hata katika kilele kabisa, kipindi maendeleo mapana kabisa ya sehemu ya ubongo wa kutafakari ‘’prefrontak cortex’’  kwa wanawake, isingewaruhusu kukubaliana na hatari hizo. Kadri wanaume hawa wanavyoangamia zaidi na hatari za mitindo yao iliyo matokeo ya asili yao ya kukumbana na laana za dhiki ya dunia, vivyo hivyo wachache wanaofanikiwa huja na namna zingine bora zaidi za kutawala ambazo huwatawala wanawake ambao nao wana asili ya tamaa kama tulivyoona awali, tamaa ya kuwa juu, na kwa jinsi wanaume hawa walivyochanganywa kabisa kisaikolojioa, basi hapa ndipo linapotimia neno kuwa, ‘’naye atakutawala’’.

Lengo la haya yote ni kuonyesha kuwa, mwanaume na mwanamke walikuwa ni kielelezo cha Uungu, lakini kwa Maisha ya sasa hivi ya dhambi, inahitaji umakini sana kutumia kielelezo hiki. Na kadri watu wanavyotumia kielelezo hiki, ndivyo wanavyojikuta wanampatia Mungu baba sifa za mwanaume huyo tuliyemwona, na Yesu ‘’sifa za mwanamke huyo aliyechini ya mumewe, aliyetoka katika mbavu za mumewe’’.

Nini maana ya Mwana wa Mungu

Rejea Ebr1:5-10 ‘’Kwa maana alimwambia Malaika yupi wakati wo wote, ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana? Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu. Na kwa Habari za Malaika asema, afanyaye Malaika zake kwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.

8, Lakini kwa Habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 umependa haki, umechukia maasi;kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio. 10 Na tena, wewe, Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikoni yako;

Soma pia Ebr1:13 ‘’Je! Yuko Malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

Yohana14:8-9 ‘’ Filipo  akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo Pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?

Hapa tunaona Mungu baba akimwita, mwana pia ‘’Mungu’’. Ni kama tunapokuwa katika masomo katika timu ya upasuaji, huwa tukiitana ’‘Daktari’’ ijapokuwa wakati huo huwa tukifanya majukumu tofauti tofauti, na pia huwepo daktari mkuu, sio katika namna ya kimaarifa, bali katika namna ya uongozi, maana huwa kuna daktari anayeshughulika na dozi za nusu kaputi, usafi wa vifaa na mazingira ya upasuaji, daktari mpasuaji msaidizi, mpokea vifaa vya uchafu, na mwisho ni daktari mpasuaji mkuu. Wote huwa ni wataaluma moja, na tuna viwango sawa vya utaalamu, lakini huwa tukiwekwa katika makundi tofauti tofauti ya kitabibu. Mwamuzi mkuu hapa huwa ni daktari mpasuaji mkuu ‘’chief surgeon’’, lakini haimaanishi kuwa yeye ndiye daktari mkuu wa wote!

Ndivyo ilivyopia kwa nafsi za Uungu, zinatofautishwa katika namna ya kimajukumu zaidi ya namna za kiuwezo. Mtu mmoja anaweza kusema kuwa, kwanini daktari wa nusu kaputi asiwe kama daktari mpasuaji mkuu, kama timu ya udaktari huwa tunatambua, ni vyema kila daktari akakaa katika kitengo anachoweza Kutenda kwa ubora zaidi, kulingana na tofauti zetu, na sio matabaka? Kwa kuwa mwisho wa siku, sote tunalengo Moja, ambalo linatuhitaji wote tuwepo ili Kulikamilisha.

Yesu Kristo ni Mungu aliyefananishwa na Mwana wa Mungu. Na yeye katika Uungu huwepo katika sehemu ya kuwasilisha utukufu wake kwa viumbe wote walioumbwa. Ukisoma Mathayo11:29 inasema ‘’Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu;kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;’’ Yesu ni mnyenyekevu sana, hujiweka katika kiwango sawa na viumbe wake, hata baadhi huisi yeye hawezi kuwa Mungu. Yesu alijishusha hata viwango vya chini kabisa vya umauti, alitemewa mate na kudharauliwa na viumbe wake, inastaajabisha, hata Lusifa alimtega kuwa ‘’amsujudie’’ Yesu ni Mungu wa ajabu sana.

Yesu ni nafsi moja wapo kila unaposema ‘’Mungu’’. Yesu ni kielelezo kikubwa sana cha Upendo. kama ilivyo nafsi ya mwanaume, na nafsi ya mwanamke, haziweki kuwa sawa, ila zinamantiki yenye kuelekea usawa, na ubora. Hii ni kila mwanaume anapounganishwa na mwanamke wake katika pendo. Kwa kuwa tunasema Yesu ni nafsi ya Mungu, hatumaanishi kila alivyo Mungu baba, ndivyo alivyo Mwana, huku ni kuchanganya maana ya nafsi na maana ya Uungu. Hili linaweza kumsaidia sana mtu kutambua kuwa, kama zilivyopande mbili za sarafu, zote zinathamani sawa katika shilingi, ila zinautofauti, utoafuti wake haumaanishi moja ni kubwa au bora zaidi ya nyingine, ila inamaanisha ili nafsi ziwe na maana, lazima zihusishe upekee na utofauti, ambao ndiyo unaweza kupelekea Yesu kuacha majukumu baadhi kwa Baba tu, na hata Baba hivyo hivyo kuacha baadhi ya majukumu kwa Yesu tu.

Kama utasema Mungu ukitoa nafsi ya  Yesu ya Uungu, basi unazungumzia tu nafsi mbili za Uungu. Maana ya Mungu haitakamilika bila ya uwepo wa nafsi zote tatu za Uungu.

Kama unataka kusema kuwa, kama Mungu anajua yote kwanini Yesu hajui tarehe ya kurudi kwake? Inapasa kutambua kuwa, unaposema Mungu, unamaanisha Baba, Mwana na Roho mtakatifu, na siyo mmojawapo tu. Kuhusiana na tarehe ya kurudi kwa mwana wa Adamu, lazima tarehe hii ifahamike kwa nafsi hizi zote tatu za Uungu. Hoja pekee ambayo watu hawa huchanganya ni kuwa, je, Yesu anaposema kuwa hatambui tarehe ya ujio wake kwa mara ya pili, anazungumza akiwa katika namna ya ubinadamu kwa asilimia zote 100%. Tambua kuwa, fungu hili halimhusishi hata Roho mtakatifu, bali mwanadamu, mwana wa Mungu, Malaika, na Baba tu. Hii inamaanisha kuwa, hoja za ukombozi zinahusisha majadiliano yanayoegemea zaidi muktadha wa wakati huo.

Katika Yohana 16:12-15, inasema ‘’ Hata nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha Habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha Habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni Habari.

Hili fungu linaonyesha kuwa, Roho mtakatifu ni Mungu. Ni nafsi ya Mungu. Ana maamuzi yake, lakini kwa kuwa ni nafsi ya Mungu, marazote husema yaliyo malengo ya Uungu. Kama vile alivyo Baba marazote anavyosema yaliyo malengo ya Yesu. Yaani, ‘’na yote aliyonayo Baba, ni yangu’’.

Kwanini Roho mtakatifu hakufunuliwa sana, kama ilivyo kwa Baba, au kama ilivyokuwa katika hatua ya awali ya Ubatizo. Rejea Mathayo3:16-17 ‘’Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama mbingu zikamfunikia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.’’

Mafungu haya yanamaanisha kuwa, wanafunzi wa Yesu kuna vitu bado wasingeweza kuvielewa kumhusu Mungu, na ilihitaji wakati wa baadae sana atakaposhuka Roho wa Mungu, atawaelezea na kuwawezesha kuelewa alichokimaanisha. Na hiyo ndiyo sababu, awali hakuwa akionekana sana Roho huyu mtakatifu.

Kuna tafsiri dhaifu sana zinazomfanya Roho mtakatifu kuwa si nafsi ya Mungu, bali ni Roho ya Mungu. Tafsiri hizi humfanya Roho wa Mungu kuwa ni uwezo tu wa Mungu. Wengine husema ni Roho wa Kristo, wengine husema ni Roho wa Baba. Ubatizo wa Yesu hudhihirisha utofauti na upekee wa nafsi hizi zote tatu.

Ufunuo wa Yohana1:4-6 inadhihirisha nafsi hizi zote tatu zikishiriki katika kutoa neema kwa mwanadamu. Rejea mstari wa 4, Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti cha enzi; 5 tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliyemwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele Amina’’

Neema zinaonekana zikitoka kwa kujitegemea kutoka kwa kila nafsi. ‘’Roho saba za Mungu’’ neno ‘’saba’’ linamaanisha kuwa, ni Roho ya Mungu iliyopo milele, katika kila nyakati. Kiti cha enzi cha Mungu ni ishara ya mamlaka, na uweza, na utawala. Hakuna ajuaye Mungu angekaaje katika kiti, zaidi ya kutengeneza tafsiri za ajabu. Ukirejea tena Ufunuo wa Yohana 22:1 ‘’ kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo’’.

Mafungu haya yote yanadhihirisha Enzi Ipo mikononi mwa nafsi tatu za Mungu. Ambapo nafsi ya Roho mtakatifu, kama zilivyo nafsi zingine za Mungu, ina upekee wa ajabu sana, ambao kwa nje hatuwezi kuuona, lakini ndiyo inazungumza nasi moja kwa moja, tena ikizungumza nasi malengo na nia yote ya Mungu.

Nini maana ya Yesu kusema ‘’nalizaliwa’’

Neno nalizaliwa lina maana ndogo sana, wala siyo ya kutatiza. Waebrania inadhihirisha neno kuzaliwa, tofauti na Mithali inavyosema. Neno kuzaliwa lina maanisha Mwanzo. Mwanzo wa Yesu kuitwa ‘’Mwana’’ na kuacha Utukufu wake mbinguni, akiwa wa pekee zaidi ya kiumbe yeyote wa Mungu. Namna hii ya kujishusha na kuwa mwanadamu, kunamaanisha ‘’Kuzaliwa’’. Na ndiyo uhalisia, hata Mariamu anakubaliana na ukweli kuwa, alimzaa Yesu, sio ajabu, alizaliwa, na ilimpasa azaliwe, maana alikuwa ni Mwanadamu sasa kwa asilimia 100%. Yusufu hakumpa Mariamu mimba ya Yesu, na ndivyo inavyomaanisha kuwa, Ni Mungu aliyehusika kumzaa Yesu. Hebu tazama fungu lifuatalo.

Luka1:35 ‘’Malaika akajibu akamwambia, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu’’

Hapa tena unaweza kuona namna kuzaliwa kwa Yesu kunavyohusisha tena nafsi zote za Mungu. Roho mtakatifu akishuka. Mungu Baba akiwa juu na kutoa Nguvu zake kumfunika mariamu. Na kwa namna ya ajabu anazaliwa ‘’Mwana wa Mungu’’.

Sifa ya Mungu ni utendaji na mipango, na ndiyo maana utakuta wakitumwa Malaika. Mjinga mmoja anaweza kusema iweje kuwe na haja ya kutumwa Malaika kama Mungu yupo kila mahali. Huyu hatashindwa kusema, iweje ashuke Roho mtakatifu ikiwa Mungu Baba anaweza yote peke yake. Na ndiyo maana watu wenye Mawazo haya sio Mungu. Kwa kuwa Mungu Yu hai, na akitenda, sio Mvivu wa kukamilisha kila jambo na kutulia kama nafsi iliyokufa.  Na kama ingelikuwa hivyo, asingeumba, au angeumba kwa siku moja yote aliyoyaumba, lakini Mungu hutenda kwa utaratibu unaoleta mvuto, na umilele wa katika Kutenda.

Kwanini Mungu ampatie Utukufu na Mamlaka Yesu kama yesu tayari ni Mungu?

Mafungu kama Luka1:32 ‘’Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.’’

Au Waebrania1:13 ‘’Je! Yuko Malaika aliyemwambia wakati wo wote, uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?’’

Waebrania 2:8-9 ‘’Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake. Ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko Malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajli ya kila mtu.’’

Kwa Mafungu haya unaweza kupata maana ya kuwa, Mungu nikimaanisha wote, lengo kumaanisha Yesu kama walivyoshiriki katika kumuumba binadamu. Yesu kama ilivyokawaida yake, yeye hufunua Uungu na utukufu wa Mungu kwa kuwa sawa kabisa na viumbe wake, akiwa kiongozi wao mwema. Anapoteza nafasi hii kwa binadamu baada ya binadamu kuamua kuchagua njia ya Lusifa. na sasa basi, Mungu ‘’Yesu’’ anaamua kuchukua matokeo yote ya dhambi ya mwanadamu, ili kuilinda Haki ya Mungu. Anakubaliana na kupitia kila kilichompasa binadamu kuumia kwacho kwa madhara ya dhambi, ilihali yeye akiwa mwema kabisa.

Yesu anazaliwa akiwa kama kizazi cha Adamu, ibrahimu na daudi. Na kuishi kama kondoo akiitwa mwanakondoo, ambaye ni ishara ya unyenyekevu dhidi ya kuonewa ilihali hakustaili. Na mpaka dakika ya mwisho Yesu anakufa, Luka23:46 inasema ‘’Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi  mwako naiweka roho yangu.’ Yesu anakufa kama mwanadamu kwa asilimia 100%. Kumbuka, Yesu hakufa kama Mungu, alikufa akiwa mwanadamu. maana Mungu hafi. Yesu allithibitisha Uungu wake kwa kusema katika Yohana 10:18 ‘’Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu.’’ Hapa Yesu anazungumza kama Mwanadamu, lakini akiwaambia wanafunzi wake kuwa, Yeye ni Mungu, na namna yake ya Uungu ndiyo itahusika katika kumfufua tena ikiwa sawa na matakwa ya Mungu kwa ujumla.

Mungu-Baba anazungumza namna atakavyompatia mamlaka makubwa Yesu baada ya kushinda dhumuni lao kubwa la upendo la kumkomboa mwanadamu, ambao Yesu ndiye aliyejitoa kafara . kumbuka pia Lusifa na majeshi ya Malaika zake wote, hawaamini kuwa Yesu ni Mungu na mwenye mamlaka, na sasa Uungu wote unalenga kudhihirisha Uungu wa Kristo kwa jamii yote ya viumbe, hasa wale waliopinga na kudharau msingi wa namna ya chini kabisa ya Yesu ya kujishusha. Sehemu ijayo tutaangalia Habari hii ilivyo na mgogoro mkubwa sana kwa Lusifa, ambaye kwake yeye, Yesu hakuwahi, na hawezi kuwa Mungu, na hali akishindana na Yesu, na kuhisi anaweza kuwa bora hata zaidi yake, na kutamani kuwa sawa na Mungu, ambaye kwake alikuwa ni Baba, akajikuta akitazama sheria zote za Mbinguni zilizokuwa chini ya Yesu ni za kibepari, zisizo na uhuru, lakini kumbe hoja yake haikuwa uhuru, ilikuwa ni tamaa ya kujiinua, wivu na chuki dhidi ya Kristo, ambaye kwake hakuona sababu ya kuwa chini yake.

2.Wasomi hawa huamini Biblia ni kitabu cha Mungu, ambacho ni matokeo ya kazi, na maamuzi ya waandishi, ambao katika kukiandika, na kukichapisha, kumekuwamo na motisha zingine tofauti na nguvu ya Msukumo wa  Mungu.

Wasomi hawa huamini kuwa kuna sehemu kadhaa katika Biblia zimeandikwa au kuwekwa kimakosa. Hii ni kama ilivyo kwa mafungu ya 1Yohana5:8. Ambalo ni fungu linalodhihirisha utatu wa nafsi za Mungu, kwa kuziorodhesha moja kwa moja. Changamoto pekee iliyopo hapa ni kuwa, watu hawa huamini kabisa kuwa Biblia sio kitabu chenye kujitolesheleza chenyewe kimantiki kwa asilimia zote 100%.

Jambo hili halina mantiki kabisa, kwa kuwa, kama Mungu ni mkubwa na ndiye mwenye mamlaka ya kutawala kila kilichopo chini ya dunia. Hawezi kushindwa kulilinda neno lake. Mungu ambaye tunamwamini kuwa ana control DNA kuanzia ya kirusi mdogo kabisa mpaka panzi, anayejali njaa ya sisimizi, na kujua kesho ya kila mwanadamu, na kutawala galaxies zote za nyota mpaka na sayari na mifumo ya ulimwengu tusiyoijua, Mungu huyo hawezi kushindwa kuilinda Biblia yake.

Pengine changamoto pekee tunayoweza kuisema ni kuwa, watu wengi huchanganya njia za Mungu na za mwanadamu. Mfano, kama Mungu angemtumia masikini, na mtu wa chini kuhubiri Habari za ufalme, basi kwa wanadamu isingeleta mantiki. Au kwa mfano, kama mtu unayehisi ni mwovu kabisa Mungu angemtumia kupitisha ajenda yake mojawapo, kwa wanadamu bado isingeleta mantiki. Hizi ni namna mojawapo tunazoweza kuona namna njia za Mungu ni tofauti na mwanadamu. Mungu alimtumia kahaba Rahabu kukamilisha kazi yake ya kuwakomboa wana wa Israeli, na hakuna msomi wa Biblia anayepinga hoja hii kwa kusema Mungu hawezi kumtumia rahabu zaidi ya mafarisayo tu waliomkataa Yesu kwa kuwatumia watu dhaifu kama wavuvi kuhubiri Habari za wokovu. Kama Mungu angeruhusu watu ambao leo hii wanaonekana waovu kupitisha ajenda yake, je nini mtazamo wako? je hilo linawezaje kutupatia Imani juu ya nia njema ya Mungu hata kwa mafungu kama tuliyoyataja juu? Ni ujinga mkubwa sana kuhisi mwanadamu anaweza kumsaidia Mungu katika mantiki ya kuwa Mungu mwenyewe Aliona ila alishindwa kufanya lolote.

3. hawajui wanachokifanya, wala wanachokitaka, ni ujinga.

Watu wengi wanaochochea kuwa hakuna nafsi kuu tatu za Mungu, kama ukiwauliza, inamantiki gani ya msingi kwa mkristo kuamini uwepo wa Mungu mmoja, aliye na mwanae mwenye asili ya uungu Yesu Kristo, na akawa na uwezo kwa kiroho unaoitwa Roho mtakatifu, utagundua hawana mantiki yoyote ile? Wengine huisi wenda mbingu imejawa na ushindani na hisia za kimatabaka kama duniani. Wengine huisi wenda Mungu Baba angetamani mwanae Yesu Kristo asipewe heshima kama yake?

Na tena ukisoma Mathayo28:19, jukumu kubwa la Mungu kwetu limeandikwa kuwa ‘’ Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu’’. Hapa unapata lengo letu kuu wakristo likiwa ni kuwafundisha wamataifa waachane na njia zisizompendeza Mungu, na kuwabatiza kwa jina jipya la Mungu wao muumbaji, yaani ‘’Baba, Mwana, na Roho mtakatifu’’. Haileti mantiki kabisa kwa kusema kama watu hawa wanavyotaka, yaani, kwa jina la ‘’Mungu, mtoto wake, na roho yake’’.

Mpaka hapo unaweza kupata taswira ya kuwa, watu hawa wamepofushwa na Lusifa tunayeenda kumsoma, ili washindwe kumwelewa Mungu aliyejidhihirisha kirahisi kabisa, na kuanza kupotea huku wakijipoteza wenyewe. Mmoja wa marafiki zangu aliyehisi walau amejifunza teolojia vya kutosha aliwahi niambia, walioleta fundisho la utatu walikopi kwa ibada za kipagani za kimisri waliokuwa wakiabudu miungu watatu ‘’isis, Osiris, na horus’’. nakumbuka nilimwonea huruma kwa kuwa niligundua hajui hata historia vizuri kuwa, Lusifa aliyekuwa akijua kabisa asili ya Uungu kuwa una nafsi tatu, ndiye aliyeiga na kuiingiza Imani hii kwa wapagani, na ndiyo tabia ya lusifa marazote kukopi na kubadilisha mambo yaliyo Mbinguni. Lusifa kamwe hana jipya kama tutakavyomwona mbeleni.

Watu wenye maarifa ya kweli ya Mungu hawatumii muda wao mwingi kuhangaika kubishania hoja zisizo husiana na wokovu wa watu, mwanadamu hawezi kuhangaika kumuelewa Mungu kama hata shetani tu aliyenae wakati wote hawezi kumuelewa. Ni nani anayemjua Lusifa vya kutosha? Hapana! Lakini watu wanahisi wanaweza kumuelewa Mungu. Mungu anachotutaka ni nini kama si Kutenda wema na kumcha Bwana.

Watu hawa hawajui marazote Mungu amekuwa si wakupendezwa na wanadamu kutokana na ukamilifu wao, bali nia zao njema kwa yale wanayoyajua. Katika amri ya Mungu, mimi ni Bwana Mungu wako usiwe na miungu mingine ila mimi’’, hukumu kuhusu ile amri haitaweza kutengeneza mantiki, kama itahusisha hukumu kwa waliokuwa na miungu, ila ni mwana wa Mungu, au Roho wa Mungu, kwa mantiki hii, watu hawa huangaika katika kupoteza muda wao, na kufanya kazi za kuwapoteza watu hata wasimwelewe Mungu. Maana hakuna amri kumi za Baba, na Mwana, au za Roho mtakatifu. hawa wote wanaagizo moja, na kwa mantiki hiyo, Utiifu utapimwa kwa kiwango gani tulichokifahamu kuhusiana na haki ya Mungu tulitenda, zaidi ya hapo hakuna hukumu.

SEHEMU YA PILI

LUSIFA NI NANI?

Lusifa hakuwa tu Malaika wa kawaida, alikuwa Kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye,’’yaani Lusifa alikuwa akikaa meza moja na  Mungu Baba, Mikaeli, na Gabrieli’’. Mungu alimuweka katika ukuu wa falme zake, vito vyote vya thamani vya Mungu vilikuwa ni sehemu yake, alikuwa ndani kabisa katika ufalme wa Mungu. Lusifa aliumbwa akiwa ni mkamilifu kwa asilimia zote 100%.

Lusifa alijawa utajiri katika namna Mungu alivyomfanyia thamani nyingi kuwa chini yake, Lusifa alikuwa Mzuri sana, na tena alikuwa na mwangaza wa ajabu wa hekima, Lusifa alijawa na utakatifu, na inaonekana Lusifa Mbinguni alikuwa ni mkuu katika namna zinazojihusisha na Tamaduni zote za Mbinguni, kama vile Burudani, ibada, na alikuwa na wafuasi wengi sana waliokuwa chini yake.

Ukisoma Ezekieli 28:17 unapata sababu kubwa iliyomuangusha Lusifa ilikuwa ni Kujiinua Moyo wake, kwasababu ya uzuri wake, na utajiri wake, na maarifa yake. Na hicho ndicho unachokiona katika sura nzima hata kwa mstari wa pili, ambapo inaandikwa ‘’Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya Bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu. 4, kwa hekima yako na kwa fahamu zako umejipatia utajiri, nawe umepata dhahabu na fedha katika hazina zako; kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako;

Kwa hiyo Kujiinua na kujiona kama Mungu ndiko kulikomuangusha Lusifa. Lusifa kwa kujiona kama Mungu, hakuhisi anahitaji kufanya Ibada tena, alihisi anahitaji Kuabudiwa. Ukisoma tena Isaya14:13 inaandikwa ‘’Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini, 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.

LUSIFA NA KUJIINUA

Ijapokuwa Kujiinua kunaweza kukaonekana ni jambo la kawaida, lakini kila uasi unapotokea katika dunia hii, chanzo chake ni kujiinua. Lusifa alianza kujiinua baada ya Kugundua mambo yafuatayo.

Alipotazama Chini Lusifa

Yeye ni watofauti sana na wenzake, na kuwa yeye, ni mzuri, Tajiri, na ana hekima pana sana, kiasi cha kuona kuwa ni wapekee zaidi ya wenzake. Lusifa ni mgonjwa wa kwanza kabisa wa matatizo ya kisaikolojia, ya ‘’Narcissism’’, yaani, kujitazama sana kujiona kuwa ni wapekee, na kuhisi kila mmoja anapaswa kumzingatia. Na hili unaweza kulielewa zaidi katika Ezekieli 28:16 ‘’kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto’’.

Hawa waliomjaza udhalimu ni wale wenzake aliotupwa nao, maana hao walishiriki katika kumchochea Lusifa kujiona ni wa hadhi ya Kiungu kabisa kwa ufahari wake. Kumbuka kwa kitengo cha Lusifa mbinguni, alikuwa ni Malaika wa kusimama mbele za makutano makubwa ya utukufu wa Mungu, Uimbaji wake bora kabisa ulimfanya sifa nyingi sana zinazomwelekea Mungu kupitia Yeye, ahisi ni mali yake. Maisha ya wasanii maarufu sana katika namna ya utajiri, umaarufu, uzuri, n.k. ni kielelezo kidogo sana cha Maisha la lusifa mbinguni, alikuwa ni wa kipekee sana.

Kumbuka Lusifa hakushiriki katika uimbaji tu, alishiriki katika Nyanja zote za maswala ya ustawi wa Mbinguni, Lusifa alikuwa na vitengo vingi sana chini yake ‘’Sanctuaries’’ ambavyo unaweza kuona katika Ezekieli 28:18, kuwa kwa uovu wake, alivitia unajisi. Lusifa katika namna hizi alijikuta akihitajika kuikweza haki ya Mungu katika kila namna ya utumishi wake, jambo ambalo lilianza kumuwia ugumu kila alipoanza kupata hisia za wivu, na kujihisi hata yeye tu angeweza kukidhi kupatiwa sifa hizo.

Alipotazama Juu Lusifa

Kama kuna sehemu iliyomfanya lusifa ajiinue kwa haraka sana, ni pale alipotazama juu. Lusifa ambaye sasa ameshagundua kuwa yeye ni wa kipekee sana, anapotazama juu, hamuoni Mungu kuwa mbali naye, anamuona Mungu akiwa karibu na wakufanana naye kwa kiwango kikubwa sana.

Lusifa alikuwa ni kiumbe wa kwanza kabisa wa kuchanganywa na Uungu wa Mungu. Hii ni kwa kuwa, Lusifa hakuelewa sababu ya Mbingu kumheshimu Mikaeli, ambaye ndiye Yesu. Lusifa alijiona kabisa kuwa angehitaji heshima zaidi hata ya anayopatiwa Mikaeli. Kwa Lusifa, yeye alijiona akiwa sawa na Mungu-Baba kwa siku zake za usoni, na kwake aliamini sifa zote alizokuwa nazo Mwana, yaani, Mikaeli, hata yeye anazikidhi, tena kwa ubora zaidi.

Mbingu yote ilijawa na heshima na utukufu kwa Baba na Mikaeli, na Mikaeli ndiye aliyekuwa akishughulika katika nafasi zote ambazo alipaswa kusimama Mungu. Hapa Lusifa ndipo alipohisi kuwa hata yeye angeweza kuwa kama Mungu. Mikaeli alikuwa ni mnyenyekevu sana, mwenye kufanania sana na viumbe wake. Lusifa hakuligundua hili, kwake alimwona Mikaeli akiwa sawa tu na Malaika wengine, ni kama leo hii baadhi ya wafuasi wake wanaomwona Mikaeli akiwa sawa kabisa na wanadamu wengine. Na jambo hili kwa mara ya kwanza likamfanya Lusifa kuanza kuonyesha wivu kwa ndani, na kwa nje kuonyesha dalili za ukaidi, kwa kuonyesha ibada na heshima kwa Mikaeli.

Mgogoro wa kwanza wa Ulimwengu ‘’Great cosmic controversy’’ ulikuwa baina ya Lusifa na Mikaeli. Kwa kuwa Lusifa sasa alishakuwa amepata jawabu la kuwa hata yeye anaweza kupatiwa heshima ya Kiungu, sasa ilimbidi atafute njia ya kuifikia heshima hii. na njia pekee ilikuwa ni moja, kutengeneza ufalme wake, ambao utaenda kinyume na ufalme wa Mikaeli. Haikuwa kazi rahisi kwa kuwa Mbingu ilikuwa imejaa utukufu, haki, na upendo. kuweza kugundua uovu wa kuchafua haki hii ilimbidi lusifa awaze sana. na kumbuka, kadri haya yote yakiendelea, Mungu alishalitambua hili tokeo lilipoanza, na alimuonya Lusifa, lakini Lusifa ndipo lilipomchoma zaidi na kumuongezea hasira. moyo wake ulishainuka, na namna yoyote ile Mungu ambayo angeingilia kwa kumbadilisha hata Mawazo yake tu, basi angeonyesha udhaifu, na ndivyo ilivyo sheria ya Mungu, uhuru wote upo chini ya viumbe wake, na uhuru wote huelekea haki yake.

MBINU YA LUSIFA

Baada ya kuwaza sana namna gani anaweza kufikia ndoto yake ya kuabudiwa, kumbuka pia lusifa alipatwa na tatizo lingine la kiakili la ‘’Obsessive compulsive disorder’’, yaani alikuwa na hamaka na hamu iliyopitiliza ya kuabudiwa. Akapata mbinu kubwa moja, namna pekee ya kuwashika akili viumbe wengine wengi wa Mungu, na kuwatoa katika kufungwa na haki, na upendo wa Mungu, hata kutaka kumuasi, ni kuwachochea kutamani ‘’Uhuru’’. Lusifa ndiye mwanafalsafa wa kwanza Mbinguni, ambaye aligundua ‘’Demokrasia’’ haipo mbinguni.

Lusifa alianza kuchochea sera ya kuwa hakuna ‘’Uhuru’’ mbinguni. Aliwachochea Malaika kuwa mbinguni iliwapasa marazote kumwabudu Baba, na Mikaeli, na walipaswa kuwatii marazote hata bila ya matakwa yao. Kwa mara ya kwanza haikuweza kutengeneza mantiki sana kwa Malaika, ambao kumwabudu Mikaeli au Baba lilikuwa ni jambo la kawaida tu, kwa kuwa wao waliumbwa. Na Malaika wengi walishagundua mgogoro wake wa nafsi, lakini wapo Malaika wenzake ambao hao walikubaliana naye, na lusifa alifanikiwa sana kwa ajenda yake kuu moja, kuwa, Kumuasi au Kutokumuasi Mungu, hakuwezi kumfanya Mungu aweze kuwafanya Lolote, yaani, Mungu hana uwezo huo wakuwaua, wala hakuna Kifo.

Lusifa aliwashawishi wenzake Mawazo yake kuwa, inawapasa kutamani kuwa na Uhuru, na kama wataogopa madhara ya Kwenda kinyume na kanuni za Mungu, wasiogope hakuna Kifo, na tena yeye Lusifa, anaweza kuwa Kiongozi wao mwema sana zaidi ya Mikaeli. Katika haya mawili, Uhuru halikuwa kosa, na wala Mungu asingeweza kumhukumu kwa kutaka Uhuru, lakini kosa la kwanza la Lusifa lilikuwa ni Uongo, kwa kuwadanganya Malaika wenzake kuwa anatamani Uhuru, na kumbe ana wivu wenye chuki kwa Mikaeli, na anatamani kuchukua nafasi ya Mungu ya Kuabudiwa, pili, kosa lake  Lusifa lilikuwa ni kuchafua Haki ya Mungu, kwa kumsema Mungu ni Muongo hawezi Kuua, na tena ni katili, mwenye kulazimisha Ibada kwa vitisho vya kifo.

Utimilifu wa mashtaka ya Lusifa

Baada ya Tuhuma za Lusifa za muda mrefu sana juu ya kukosekana kwa Uhuru mbinguni, na kuwa kila kiumbe kina uwezo wa kuwa kama Mungu ‘’kwa kujiinua kwake’’, hatimaye Mikaeli ikampasa kuingilia kati. Katika sura ya Biblia chini, ni kielelezo cha malumbano ya hoja ya Mungu dhidi ya Lusifa kabla ya kumchukulia hatua. Mungu asingeweza Kumuua Lusifa hata matokeo ya kila hoja yake yatakapozaa matunda, na ulimmwengu wote ushuhudie Ukweli au Uongo wa hoja zake, na hatua ya kwanza ya Mungu ilikuwa ni Kumfukuza Mbinguni, na kumuweka katika mazingira huru ambayo hatafanya lolote. hii ilikuwa ili ikiwa yeye naye anaweza kuwa Mungu, aumbe ufalme wake, anaoweza kutawala.

Ufunuo wa Yohana 12:7 ‘’kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na Malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao Pamoja na Malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa nyoka za zamani, aitwaye ibilisi na shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na Malaika zake wakatupwa Pamoja naye. 10, Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.

Lusifa alipotupwa kutoka Mbinguni, akiwa na Malaika zake, lilikuwa jambo la kwanza la kuonyesha kuwa yeye ni mdhaifu, na hawezi kupaa zaidi ya nyota za mbinguni kama alivyohisi mwanzo. Maisha la lusifa na Malaika zake katika ulimwengu mpya usio na lolote la kufanya, uliwafanya wawe ni viumbe wa kujuta sana, huku wakiwa katika hali ya kulumbana sana wao kwa wao, na kumlaumu lusifa. na lusifa kama alivyoitwa kwa majina mapya matatu, yaani Shetani ‘’Devil’’, Ibilisi ‘’satan’’, na Mshitaki ‘’Adversary’’. majina haya ni sawa na uyaite ‘’Deceiver’’, Satan, na ‘’Adversary’’. Alikuja na mbinu nyingine.

‘’Shetani/Deceiver’’- inamaanisha mwongo anayetumia akili sana, huyu hutumia ukweli kwa asilimia kubwa sana huku akichanganya na uongo kidogo sana, ila hutumia uongo wenye kuweza kuharibu maana nzima ya ukweli kwa lengo la hila zake.

‘’Ibilisi/ Satan’’- inamaanisha mwongo ambaye yeye hubadilisha maana, kwa kuzifanya ziwe kinyume na uhalisia wake.

‘’Mshitaki/Adversary’’- inamaanisha tabia ya kushitakia popote pale panapoonekania wema.

Mungu hakumtupa Lusifa duniani kuwa Lusifa na Malaika zake waweze kuishi katika mahali ambapo wanadamu nao wangeishi, Hapana. Mungu alimtupa lusifa katika ulimwengu ambao lusifa asingeweza kufanya lolote lile, yaani, Dunia imeumbwa katika namna ambayo viumbe wenye mwili tu ndiyo wataweza Kutenda, kwa hiyo lusifa kwa dunia aliwekwa katika kifungo, na hiki ndicho kifungo pia ambacho atafungwa kwa miaka elfu moja 1000, ukisoma ufunuo wa Yohana 20:7.

Mbinu aliyoifikiria Lusifa ilikuwa ni moja, sio tena kuanzisha Ulimwengu wake kama alivyowashawishi Malaika baadhi huko awali, ilikuwa ni kuwadanganya viumbe wengine wa Mungu. Na hapa akatumia ajenda zake zilezile za uhuru na kuwahakikishia matokeo ya maamuzi yao ya ikiwa hawatamtii Mungu, na kufuata uhuru wao, hawatakufa.

Alijaribu mbinu hii kwa viumbe wengi sana wa Mungu, Mungu ameruhusu viumbe wake wote kuwa hatarini kwa maamuzi yeyote yale ya uhuru wao, lakini huwahakikishia matokeo ya machaguo yao. Mungu huruhusu hisia za uhuru kutoka ndani ya mtu, au kutoka kwa vishawishi kama vya Malaika huyu muasi, lusifa.

Katika kuhangaika kwake sana Lusifa, hatimaye alifikia kwa viumbe binadamu. Ambao hawa waliumbwa kwa mfano wa Mungu mwenyewe. Lusifa alitambua upekee wa viumbe hawa kwa Mungu, na hasa namna Mikaeli alivyokuwa amewekeza sana kwao, Mungu kwa ujumla alikuwa amewaumba binadamu kuwa kielelezo cha ufalme wake, na aliwapenda sana. Lusifa aligundua kuwa, kama atafanikiwa kuwaangusha binadamu, basi Mungu hatakubali kuwapoteza viumbe hawa, na kama itambidi kuwasamehe, basi itambidi kumsamehe hata na yeye mwenyewe Lusifa. kwa kufanya hivi Lusifa  alitaka kutumia tena hila kusamehewa, na sio kuhisi hatia ya dhambi kama ambavyo Mungu alilenga kwa kumuacha hai kwa kipindi chote hicho alichotupwa.

Hila za Lusifa zilimfanya awachunguze kwa muda mrefu sana Adamu, na Hawa. Alikuwa makini sana na njia zao, na maagizo waliyopatiwa na Mungu kwa kipindi chote ambacho Mungu alikuwa akiwapima Utiifu wao wa Uhuru, juu ya Haki ya Mungu, kabla ya kuwapatia hali ya kuishi milele. Lusifa aligundua matatizo kadhaa kwa binadamu hawa ambao nao waliumbwa kwa ukamilifu kabisa kwa asilimia 100%. Lusifa aligundua ana asilimia 0% ya kufanikiwa ikiwa binadamu hawa wawili watakuwa Pamoja, pia, Lusifa aligundua ana asilimia 0% ikiwa atamwendea Adamu, lakini Lusifa aligundua ana nafasi kidogo ikiwa atamwendea Hawa akiwa peke yake. Hii ni kwa kuwa, Hawa aliumbwa katika namna ya Utegemezi kwa Adamu, maana alitoka kwa mbavu za Adamu, na pia, Adamu itambidi tu kukubaliana na matokeo ya Hawa, kwa kuwa anampenda sana, na ndiyo anaweza onekana kuwa kampani yake ya pekee ya kufanana nae.

Adamu alikuwa na maarifa mapana zaidi ya Hawa, hii ni kutokana na muda wake mrefu zaidi katika dunia, ijapokuwa unaweza onekana ni muda kidogo, lakini ulikuwa ni mrefu sana kwa hali zao za awali. Adamu pia aliumbwa katika namna za utawala zaidi, na upande wa hawa ilikuwa tofauti kidogo kwa kuwa, yeye aliumbwa katika namna ya utukufu zaidi na uzuri kwa Adamu. Mungu aliwaagiza kuwa Pamoja kwa muda mwingi sana wazazi hawa wakwanza kabisa.

Hawa alianza kutengeneza uwezekano wa ‘’odds’’ au nafasi za ushindi kwa lusifa pale alipoanza kuonyesha hamaka ya kutaka kulijua sana tunda ambalo Mungu alikwisha kuwakataza. Hakuna namna ambayo kwa kawaida tunaweza kuelezea kipi kilichomchochea sana. Lakini tunaweza kuona mfanano uliopo katika namna hizi za uasi. Tuliona Lusifa alikuwa ndiye mzuri zaidi, na alitamani kujiinua zaidi. Tukaona pia Nyoka ambaye ndiye mnyama wa kwanza kumruhusu Lusifa autumie mwili wake, akisemwa kuwa, ndiye mnyama aliyekuwa mwerevu zaidi ya Wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Kwa Binadamu mpaka hatua hii Eva ndiye alikuwa binadamu mzuri zaidi, sina shaka hata Adamu hatapinga hoja hii. hata Tunda la mti wa kati ukisoma Mwanzo 3:6 inasema ‘’Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti Wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala’’ yaani, hata mti wa kati ulionekana kuwa ni mti mzuri zaidi na matunda yake yalipendeza zaidi macho.

Mpaka hapo tunaweza kuona katika sehemu ambazo huwa kunaonekana kuwa kuna ubora sana, au uzuri sana, au akili sana, ndipo uasi hutokea, na hata hatari za kuanguka, huwa kubwa sana. Hii inahusiana na hoja yetu ya awali ya kuwa, chimbuko la uasi ni kujiinua. Dhambi ya kujiinua huwa haipo hata mtu atakapohisi anayo nafasi kubwa sana ya kimwonekano, au kihisia za ndani za kujiinua kwa kiburi, au nguvu, au maarifa.

Mwanamke alihisi anaweza kufanya maamuzi bila kumhitaji mumewe, na hapo ndipo alipodanganywa. Mwanamke alihisi anaweza kufanya maamuzi kinyume na muumbaji wake. Na mwanaume alihisi ana haki zaidi ya Muumbaji wake, mwanaume anamlaumu Mungu kwa uasi wake yeye mwenyewe, akiamini Mungu hakuwa sawa awali kwa kumpatia mwanamke aliyemuangusha katika uasi, kwa kumpatia mwanamke aliyemletea changamoto za hisia zake. Mwanamke naye anakubali kudanganywa, lakini bado anaamini ni nyoka aliyemkosesha, na sio kuwa yeye mwenyewe alikuwa na hisia za uasi za kutamani kula tunda ili awe sawa na Mungu.

Lusifa kwa mara ya kwanza anafanikiwa katika Lengo lake la kuupata Ulimwengu wa kuutawala, ilihali sio kwa kuutawala kwa haki na uwezo, bali kwa uongo na hila. Mungu hujiunganisha na viumbe wake marazote akiwalinda, sasa Lusifa alikuwa na uhuru wa kuwatawala wanadamu vile anavyotaka ili kumuumiza mpinzani wake Mikaeli, ambaye aliwekeza sana kwa viumbe wake hawa. Hii ni kwa kuwa, kwa uasi binadamu anakuwa mbali na Mungu, na anakuwa chini ya Lusifa.

UDHAIFU NA UPUMBAVU WA LUSIFA

Lusifa ijapokuwa anaonekana ana akili sana, lakini anaingia moja kwa moja katika mahesabu ya haki ya Mungu. Na haya mahesabu ya haki ya Mungu kwa jinsi namna haki ya Mungu hubakia milele bila kujali Maamuzi ya Uhuru wa mtu, au kiumbe, ni jambo ambalo wasomi wengi hushindwa kuelewa. Namna ifuatayo ni namna nyepesi zaidi ya kulielewa hili.

‘’Mungu ameweka Nguvu ya motisha ya kufanikisha kila maamuzi ya Uhuru wa Kiumbe, nguvu hii husukuma uasi kuelekea kifo, na utiifu kuelekea uzima’’.

Lusifa alikuwa Mpumbavu pale ambapo kadri alipokuwa akifanikiwa katika uasi wake, alihisi wenda ni akili zake, na kumbe Mungu ameweka Nguvu za asili za kumchochea ili afanikiwe zaidi katika uasi wake, maana kwa kadri anavyofanikiwa katika uasi wake, ndipo anapokaribisha mwisho wake, na kwa mwisho huo, ndipo huonekana hatimaye kuwa Mungu ni wa haki na upendo, kwa kuwa uhuru wowote wa Kwenda kinyume naye hupelekea kiumbe huyo kuteseka zaidi, kuonyesha ujinga zaidi, na mwisho kuangamia kama namna pekee ya Mungu ya kumsaidia asiendelee kuteseka zaidi.

Hivyo Lusifa alipokuwa akikuza chuki yake dhidi ya Mikaeli, Mungu alishatengeneza Msukumo wa kumchochea zaidi katika uasi wake. Na kadri uasi huu ulipozidi kuongezeka, ndipo Lusifa alipojikuta tumaini lake likifa zaidi. lakini bado akiwa na msukumo mkubwa zaidi wa uasi. Watu wengi huwa hawajui kwanini Lusifa ana motisha kubwa sana ya kuchochea, na kufanya Uasi, ikiwa tayari anajua mwisho wake ni Kifo, kwanini asikate tamaa? Jibu pekee huwa ni kuwa, Lusifa hafanyi vile kwa maamuzi yake, ila tayari anao Msukumo unaomsukuma katika Kifo, na kadri anavyokaribia Kifo, ndivyo huvutwa zaidi katika Uasi.  Na hii ndiyo sababu Biblia inatuonya kuwa makini sana, kwa kuwa Ibilisi analitambua kuwa anao muda mchache, na utendaji wake unazidi kuwa mkubwa sana.

Katika kitabu cha ‘’Ubongo wa Mtu mweusi’’, nilieleza kuwa, tabia zozote zile hutengeneza mithili ya ‘’Momentum’’, yaani, namna ambayo ni Ngumu kuweza kuiacha. Ukiwa mnywaji wa pombe, au madawa ya kulevya, unaweza kuona matokeo haya kwa haraka zaidi, huitwa uraibu. Lakini hata kwa matendo ya kawaida kabisa, kama utaelekea uasi, au wema, bado matendo yako yatafuata muitikio huu wa asili. Kitaalamu tunasema fiziolojia hutenda katika namna za kujipongeza, au ‘’rewards’’, kadri unapokuwa mtukanaji, ndivyo unavyozidi kutukana kwa urahisi zaidi, kadri unavyompenda mbwa, ndivyo anazidi kukupenda zaidi, kadri unavyolitunza shamba lako, ndivyo huzaa zaidi. Hii ndivyo ilivyo pia kwa Uhuru wa Maamuzi yetu, unapochagua tu, Matokeo yako hukufuata. Kadri unavyochagua zaidi, ndivyo matokeo huwa makubwa zaidi.

Niliwahi kupenda kutumia neno Hamasa ‘’Influence’’ katika Fizikia katika namna utendaji wa sayari, na nyota unavyofuata sheria hii pia. Kadri kitu kinavyokuwa Kizito zaidi, ndivyo kinavyovuta zaidi vitu vingine kukizunguka, na kuzidi kuwa kikubwa. Hii huweza kuitwa pia kama ‘’Gravitational accretion’’, mfano, Jua limezivuta sayari zote za mfumo wa jua kulizunguka lenyewe, kwa kuwa lenyewe ndilo zito zaidi, kisayansi tunasema limekunja zaidi miale ya ‘’Space and time’’. Hoja ya msingi zaidi hapa ni kuwa, Mungu ameumba asili hiyo katika tabia za vitu kwa nje, na hata tabia za ndani kama maamuzi, ili mwisho wa siku, matokeo yake yaonekane. Kama Uasi usingepatiwa Nguvu ya msukumo hata utakapozaa, matokeo yake wangekuwepo waasi wengi sana ambao hawaonekani, ila tayari wana mashaka na haki ya Mungu.

JE LUSIFA NA MWANADAMU, NANI ANA AKILI ZAIDI?

Lusifa alikuwa na maarifa zaidi ya mwanadamu alipokuwa mbinguni. Alipoasi, alihitaji ujanja zaidi, na ndiyo maana hakutumia hoja za mahojiano dhidi ya Adamu na hawa, ila alitumia ujanja ujanja sana. Hivyo hakuwa na maarifa kuzidi Binadamu baada ya yeye kuasi. Baada ya binadamu kuasi, Lusifa alikuwa tena na maarifa kuliko mwanadamu, kwa kuwa alikuwa na faida ya uwezo wake wa asili wa kuwa maeneo mengi zaidi ndani ya wakati mfupi, kwa kuwa yeye ni Roho, lakini pia kutumia faida yake ya kuwa muda mrefu zaidi ya binadamu, lakini mwisho kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kumbukumbu, zaidi ya mwanadamu.

Lusifa alifeli baada ya Mategemeo yake makubwa kufeli, alitegemea atasamehewa kwa namna zake za Hila, lakini Mungu alitumia mbinu nyingine kabisa, tofauti na alivyotegemea. Lusifa hakuelewa kuwa Mungu hutoa msamaha lakini pia huruhusu kiumbe kutambua hatia ya matokeo ya uasi wake. Mungu alionyesha Upendo mkubwa zaidi ya Mawazo ya Lusifa, alishuka mwenyewe na kuwa kama Mwanadamu, Lusifa aligundua kuwa wokovu wa mtindo huu ulimlenga mwanadamu peke yake, tena, huku ukiendelea kumpatia uhuru wa kuamua kuchagua wokovu.

Lengo la Lusifa lilikuwa ni kumtawala milele binadamu ambaye alihisi atatengwa milele na Mungu kama ilivyokuwa kwake. Lakini Mungu sasa alikuja kwa namna ya ajabu kumuokoa mwanadamu. Lusifa sasa alikuwa na namna moja tu, kumfanya mwana wa Adamu, au Yesu Kristo asifaulu katika lengo lake. Alipanga hila zake tangia kuzaliwa kwa Yesu, mpaka kufa kwa Yesu, Lusifa baada ya kugundua ameshindwa kabisa katika mbinu zake, alibakiwa na njia moja tu, Kuhakikisha anawamaliza wote wenye Nuru ya Mungu, ili Ujio wa Yesu katika kuanzisha ufalme wake mpya usilete mantiki. Yaani, Arudi kufanya nini ikiwa dunia yote haina wachaji wa Mungu! Mbinu hii ya Lusifa ilionekana kuwa na mafanikio sana kwa Lusifa hata sasa, hii ni kwa kuwa, tangia awali sana watu wa Mungu huwa ni wachache sana, Lusifa hufanikiwa katika kuwafanya watu wa Mungu kuwa wachache kwa kutumia namna kadhaa ambazo nilikwisha zilelezea katika Injili ya Sayansi Q1, kitabu ambacho kinapatikana bure kabisa katika Blog ya Injili ya sayansi ambayo unaweza ipata Google, au mtandaoni.

Lusifa akawa na maadui kadhaa wapya sasa, watu wa maarifa. Na hasa watu wenye maarifa ya ukweli wa Neno la Mungu, wakimtambua Mungu katika kila Nyanja ya Maisha yao. Lusifa ambaye tangia awali alikuwa akitumia sana Mamlaka za Dunia, sera za Uhuru, na hisia za kiburi za Kutokufa, sasa alikuwa ana watu wengi sana wanaomfuata, kwanini watu wengi sana humfuata sana Lusifa, unaweza kurejea tena injili ya sayansi Q1, katika sehemu ifuatayo, tunaenda kuanza kumuangalia Lusifa katika namna ambayo, tutamchambua Yeye, Tabia yake, Udhaifu wake, Sifa zake, na Anachokitegemea kisayansi.