LUSIFA DHIDI YA UHURU #6
LUSIFA DHIDI YA UHURU
Kama Nyoka
Sehemu kubwa kuhusiana na uhuru nimekwisha
ielezea katika sura iliyopita. Binadamu kwa asili anatamani sana uhuru. Na kwa
kutamani sana uhuru binadamu amekuwa hatarini sana hata kutamani kutopatiwa
mwongozo wa nini anapaswa na nini hapaswi kufanya. Lusifa amewachochea watu
kuhisi kuwa sheria za Mungu ni za kikatili sana, na kuwa, kadri watu
wanavyoweza Kwenda mbali na sheria hizi, basi hisia zao za uhuru, na ubora wa
maisha yao unaweza kuongezeka.
Uhuru tangia historia ya binadamu umekuwa
ni kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio ya binadamu. Hakuna uhuru duniani, wala
popote pale. Hakuna uhuru kama umezaliwa. Kila kitu kinafata utaratibu na ndiyo
maana kilikwepo na kitaendelea kuwepo. Hakuna uhuru wa kuamua utakunywa maji au
petroli, unapojaribu kutafuta uhuru unatafuta kifo. Lusifa amejawa na sera za
kuchanganya watu, ati uhuru ni bora kuliko maarifa! Na kwa mantiki hiyo watu
wanaangamia kwa kukosa maarifa, na sio maarifa.
Lusifa amewavuta watu kufanya mapenzi
kabla ya ndoa, wengine jinsia moja, wengine kwa mdomo, wengine kinyume na
maumbile, wengine kaka na dada, wengine na Wanyama au hata roboti za mapenzi,
wengine mme mmoja na wake wengi, n.k. Lusifa amewachochea watu kuwa huru kuua
kwa mabomu ya nyuklia, kusema uongo kisa watanufaika, kutukana hovyo hovyo,
kutokuwa na kiasi, kutoheshimu, kuvaa nusu uchi, kuchora tatoos na kula vyakula
hatarishi kwa afya zao, n.k. Lusifa anajua kwa kuwa kila mwanadamu mpumbavu
ndani yake kuna chembechembe ya ukaidi, anaojidanganya ni Uhuru.
Lusifa amefanikiwa kuwapata wengi sana,
kutokana na msingi wa ubongo. Ubongo haupendi kufikiria, au kufuata maelekezo,
hasa unapokuwa tayari una stress, au umechoshwa na maisha. haya ni mahesabu ya
lusifa. lusifa hutumia tamaa ambazo huwa amewatriki watu wake kuwa wanaweza
zifikia kwa mafanikio sana kama watakuwa na uhuru.
Kama Joka
Nilishaelezea awali kuwa, Lusifa awali
kabisa alikuwa na shida za kisaikolojia za kutamani sana kuwa kama Mungu.
Lusifa alikuwa na tamaa sana. Na hakukuwa na namna ya kuzifikia tamaa zake kwa
kutumia Logic, au maarifa, maana yeye tayari alikuwa ni kiumbe. Lakini kupitia
mbinu ya Uhuru, alitengeneza hoja yake ionekane kuwa na mashiko. Sura
zilizopita tuliangalia kiundani zaidi hoja hii.
Lusifa ameweza kuchochea mabilioni ya watu
kutotii sheria na maagizo ya Mungu, kwa hoja tu ya kuwa, tuna uhuru wa asilimia
100% kutengeneza matokeo ya matendo na maamuzi yetu. Hakuna nafasi ya Muumbaji
juu ya uhuru wetu. Huu ndiyo msingi uliotapakaa katika kila vyanzo vya burudani
na usanii katika zama hizi giza za kisasa. Lusifa ameyafanya maarifa kuonekana
kana kama ni kitu ambacho kila mtu anaweza kuamini cha kwake, na sio kwamba
maarifa na kweli zatoka kwa Mungu. Na kwa kufanya hivi ameua kabisa sayansi ya
kweli, na dunia imefikia kiwango ambacho taaluma zote zimefikia kikomo katika
namna sayansi ilipaswa, au taaluma ilipaswa kuwa.

Join the conversation