LUSIFA DHIDI YA NGOZI #3
LUSIFA DHIDI YA NGOZI
Kama Nyoka
Ngozi ni mlango wa fahamu ambao lusifa huutumia
sana, pengine kuliko wengi wa wasomaji wanavyoweza kufikiria. Lusifa kama
alivyokuwa msanii, hakuwa wakukaa katika viti vya nyuma, alikaa juu kwenye
steji. Wasanii wote hukaa mbele na juu wakionekana na wote. Wengine husema
wasanii ni vioo vya jamii. Ukisoma Biblia katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana,
Kila Babeli au uovu unapozungumziwa, huzungumzwa ukipambwa kwa mavazi ya
dhahabu, na vito vya thamani za kuvutia. Hoja ni kutambua kuwa, Lusifa kama
alivyo kahaba, hujali sana mwonekano wa nje, kuliko hata uhalisia mzima wa
ndani. Kama kuna kiungo ambacho kimebeba tamaa za mwonekano wa mwanadamu, basi
ni Ngozi yake.
Lusifa anatambua kuwa mwanadamu huonekana kwa
afya ya Ngozi yake. Lusifa anatambua Uzuri ni tamaa ya mwanadamu aliyeanguka.
Lusifa anatambua uzuri kwa asili sio mbaya, lakini anajua kama wanadamu watajua
namna za asili na bora kiafya za kutunza afya zao za Ngozi na mionekano ya
uzuri, hatakuwa na nafasi ya kuwachochea wengi zaidi katika uharibifu wake.
Lusifa anajua kwa namna ameshachochea uharibifu katika mitindo ya ulaji,
mizunguko ya kuamka na kulala, fiziolojia za mwili, n.k. binadamu hatakuwa na
mwonekano mzuri. Na sasa Lusifa anakuja na njia mbadala ya kutatua tatizo hili.
Cosmetics kama Mafuta ya kisasa, make-ups za uzuri, serums, creams, ointments, lipstics, sunscreens, nail dyes, eye lashes, tattoos, skin plastic implants, mawigi, perfumes, hair dyes, cleansers, n.k. hii sasa ni sample ya saloon ya uzuri ambayo Lusifa anaiweka kutatua matatizo ya shida za kutokulala, kutumia mianga hatarishi kwenye simu na vifaa vya elektoniki, kula vyakula vilivyoshamiri sukari na viongezwa kwenye vyakula, vyakula vya kukaanga na nyama nyekundu, pombe, kupungukiwa maji, n.k.
Lusifa anatambua kuwa mitindo hiyo yote inachofanya ni sawa na kuziba nyufa juu ya ukuta wa nyumba iliyopasuka katika msingi. Afya ya Ngozi hauwezi itatua kwa kutumia Cosmetics, ila unaweza kuiharibu kwa kuzitumia. Ngozi inaundwa asilimia zaidi ya 90% kwa vitu vinavyotoka ndani ya mwili, na sio juu ya Ngozi. Afya ya Ngozi inahitaji vitamini C, inahitaji vitamini A, inahitaji protini kamili iliyosheheni Amino acids zote. Inahitaji chembechembe za Collagen, elastin, inahitaji melanin, inahitaji maji, inahitaji vitamini E na selenium, inahitaji mwanga wa jua wa miale ya asubuhi yenye mionzi ya UV-A, infrared rays, na inahitaji kidogo sana Blue-lights, inahitaji kidogo sana stress zinazotokana na homoni ya Cortisol, n.k.
Lusifa ameificha taaluma hii kwa wasomi wengi,
Lusifa anawadanganya mataifa kuchanganya Uzuri ‘’beuty’’ na Umahaba ‘’sexuality’’. Lusifa anatambua
kuwa, mwonekano wa kila binadamu unaweza kuwa aidha mzuri kama Yusufu,
Absalomu, Raheli, Sara, au Esta. Lakini pia unaweza kuwa wa kimitego kama
makahaba wengi sana. Uzuri ni mpana sana kuweza kuuelezea, maana ni matokeo ya
mwonekano na tabia. Lakini Lusifa hufeki mwonekano wa nje kwa mbinu za
kisaikolojia, na kutengeneza mwonekano ambao huchochea Ubongo kusisimka
kimapenzi. Na kisha kudanganya watu kanakama mwonekano huo ni Uzuri ambao Mungu
ameuumba.
Lusifa huwa kitaalamu anachochea ‘’Estrogen look’’ ambayo mimi napenda kuiita. Wanadamu kisaikolojia huvutiwa kuelekea mwonekano unaoelekea uzazi wanapokuwa katika hatua ya kuhitaji uzalianaji. Wanaume hupenda wanawake wenye maumbile mazuri ya uzazi kama matiti na nyonga zilizoachana kwa wastani wa 1:3 kati ya kiuno na hips kwa urahisi wa kuzaa Watoto. Wanaume huvutiwa kwa wanawake wenye afya nzuri ya Ngozi kama ishara ya afya bora. Wanaume huvutiwa kwa wanawake wenye mwonekano wa kuvutia wa sura, unaoashiria kiwango kidogo cha stress cha kukomaza miili yao, yaani kama timu zinavyopenda kusajili wachezaji wadogo, ndivyo wanaume hupenda mabinti wadogo ili kuwazalia sana. Wanaume hupenda wanawake wenye sura zenye tabasamu kuashiria amani, macho makubwa na meupe kuashiria uwezo mkubwa wa kuhisi huruma au kuzingatia, nywele nyingi kuashiria estrogen nyingi, au sifa nyingi za umama. Wanaume huvutwa katika vigezo hivi kisaikolojia bila wao kujijua.
Vivyo hivyo kwa wanawake ambao huvutiwa kwa
wanaume wenye mionekano ya uimara kimisuli na urefu kama ishara ya usalama na
ulinzi. Wanawake hupenda wanaume wenye nguvu kiuchumi kama ishara ya usalama
wao na uzao wao. Wanawake hupenda wanaume wenye sauti nzito na ndevu kama
ishara ya mamlaka na uwezo wa kufukuza maadui. Wanyama majike hukimbia
wanapopandwa na madume ili kutopandwa na madume yasiyo na ulemavu, au wasio
wadhaifu. Wanawake pia huvutiwa na wanaume wenye mionekano mizuri ya sura kama
ishara ya amani, ukarimu, na mifumo imara ya kinga kama tulivyoona katika
injili ya sayansi Q5.
Hii mivuto hakuna mwanadamu ambayo anayo
kwa asilimia zote 100% zaidi ya Adamu na Eva tu, shida nyingi na makosa katika
jenetikia imepelekea wengi tumeathirika katika mionekano yetu. Lusifa
analitambua hili, na sasa kwa kuusoma ubongo wa binadamu kwa karne nyingi,
anachochea sanaa za uongo, sanaa za kufeki mionekano kuelekea katika vigezo
vikuu vya uzazi kimionekano bila uhalisia.
Lusifa anachochea mavazi ya nusu uchi ili
kusisimua ubongo wa wanaume kuelekea hitaji la uzazi katika mazingira
yasiyohitajika, na anajua kwa kuwazoelesha mionekano ya nusu uchi, baada ya
muda wengi wa wanaume hawa hawataweza kusisimka tena kwa kuwa wameshazoelea
mionekano hii. na hii ndiyo sababu tafiti kadhaa zinaonyesha vijana wengi wa
miaka 15 wamepungua sana hamu ya kufanya mapenzi, sio kama ilivyokuwa awali.
Hii ni kama mtoto unavyompiga sana, baada ya muda huota sugu. Lengo la lusifa
ni kuwafanya wanaume kutokuwa na nguvu za kiume, huku akiwaondolea wanawake
kabisa thamani za miili yao.
Lusifa anajua matumizi ya Cosmetics kama
make ups, lipsticks huchochea mionekano ya mafuta mafuta kuashiria estrogens,
ambazo huwafanya wanaume kusisimka sana kimapenzi. Eye brows na lashes,
hutengeneza kona ‘’margins’’ kwenye macho, na kuyafanya macho kuonekana na weupe
kipekee sana, nguo za kubana vifua zikiyaonyesha matiti kwa theluthi walahu,
huyafanya matiti kuonekana madogo ishara ya ubichi kiuzazi, na kuwasisimua sana
wanaume, make ups huzifanya sura za wanawake kuficha mikunjo yote ya Ngozi, na
kuchochea mionekano ya afya ya Ngozi ishara ya estrogens nyingi kwa mwanamke,
na wanaume wengi husisimka zaidi. Wanawake wengi huvaa nguo zenye kuwabana ili
kuonyesha tofauti za maungo yao kati ya hips na nyonga, hii huwasisimua zaidi
wanaume.
Wanaume wengi huwa hawaelewi nini
huwasukuma zaidi katika uzinzi wanapokutana na wanawake wa mitindo hii, ambao
wamejawa na mionekano ya kimahaba, ambayo hawakupaswa kuwa nayo katika
mazingira ya jumuiya.
Lusifa amesheheni mionekano hii feki
katika filamu, miziki, n.k. katika injili ya sayansi Q4 nimeelezea namna sanaa
hizi zinavyochangamanishwa na mianga ya kisasa, na Camera za kisasa, na
programs za kisasa katika kutengeneza filamu, music-videos, social media arts
na matangazo, ambapo matokeo yake ni kuwachochea vijana wadogo kabisa kuingia
katika kuangalia filamu za ngono, wanawake kuumwa matatizo ya kisakolojia,
kuwazia sana mionekano yao ya uhalisia kwa kutamani mionekano feki
‘’fake-obsessions’’, wengi huishia kutokujikubali, hushindwa kuelewa tatizo lao
haswa ni lipi, na hata hivyo huwa hawapo hao wanao wa tamani kimionekano.
Picha zimeshamiri za watu wenye mionekano
mizuri, wakiwa katika mazingira ya kitajiri, na vijana wengi huvutiwa. Maelfu
ya vijana wa kiume hushinda kwenye majimu wakikuza misuli yao, na kusahau kuwa
afya za miili yao zinategemea zaidi afya ya moyo na ubongo, na sio misuli. Wala
hakuna wanaokufa kwa shida za misuli bali moyo na ubongo. takwimu zinaonyesha
watu wanaoishi miaka mingi, na kuwa na afya sana ni wale ambao huwa na wastani
wa mionekano ya kawaida kama wayahudi, wachina, n.k. wanyakua vyuma na wajenga
misuli wengi hufa mapema, na huzeeka vibaya. Hii ni kwa kuwa mwili unahitaji
‘’Mitochondria nyingi zaidi katika moyo na ubongo’’’, na sio misuli kama watu
hawa wanavyofanya. Hii ni tofauti ya binadamu na sokwe. Sokwe wanamisuli mingi
na huishi miaka mifupi ukilinganisha na binadamu, maana huwa na mitochondria
chache sana katika ubongo na moyo, Lakini Lusifa huwachochea wanadamu hawa
kutaka kuwa kama sokwe kwa kutamani sifa za uzazi, na kukosoa fiziolojia zao
kwa kuwapatia mionekano ya wastani, kwa kutamani mionekano feki.
Kama Joka
Lusifa masikini baada ya kuwateka vijana
wengi sana katika furushi lake la tamaa ya mionekano, huwaua wote kwa namna
mbalimbali. Lusifa anatambua katika kila mbinu aliyoitengeneza katika sifa feki
za uzuri, ana maelfu ya madhara kuliko faida.
Cosmetics zote ni hatari kuliko wengi
wanavyohisi, kwanza, kama ilivyokuwa awali, kuanzia miaka ya 1970’s na
kuendelea ndipo kiwango kikubwa sana cha cosmetics za kisasa kilianza
kutumika. Na kuanzia hapo ndipo matatizo
makubwa zaidi ya Ngozi yalipoanza kushamiri. Na msingi wa Lusifa katika kuwaua
watu kwa ufupi ni kama ifuatavyo.
Lusifa na Biolojia ya Hatari za Vichochea Urembo
Wengi wa warembo hukimbia sana mwanga wa
jua. Kwa kuwa huamini mwanga wa jua huwazeesha, au wakakamaza Ngozi. Wengi wao
hutumia Cosmetics ambazo huwa na chembechembe za kuzuia mwanga wa jua kupenya
katika Ngozi. Hizi huitwa
‘’sunscreens’’. Kati ya hizi, zote huwa na madhara. Lakini madhara makubwa
zaidi huwepo kwa zinazoitwa ‘’chemical sunscreens’’, mfano, Oxybenzone. Hizi
kwa asili zinapokuwa katika mafuta, hufanana sana na chembechembe za estrogens,
na madhara yake ni kuwa, kadri mtu anavyozitumia, hasa anapokuwa mwanaume,
humchochea sana kuwa kama mwanamke ‘’feminizes’’, hii ni kwa kuwa, husisimua
sensa ‘’receptors za estrogens’’ ambazo zisingehitajika ndani ya mwanaume. Na
pia, bado zimeonekana kuwa na madhara mengi sana zinapokuwa ndani ya mtu.
Chembechembe nyingi katika mafuta, kama
‘’Parabens, hydroquionones, n.k.’’ zimejikita kumpunguza nguvu enzyme anayeitwa
‘’tyrosinase’’, ambaye huyu hubadili phenylene kuwa tyrosine katika uundwaji wa
melanin. Kutokana na wanawake kutotamani kuonekana Weusi unaochochewa na
melanin, wengi wao hupendelea mafuta yenye tabia hizi, lakini matokeo yake ni
mwili kuishiwa melanin. Kumbuka melanin ni ya msingi sana katika kufyonza
mionzi ya muhimu sana ya mwanga wa jua kama UVA, na infrared rays, na kuzalisha
electrons ambazo huenda kusaidia mwili kuzalisha maji katika mitochondria, na
kuchochea afya ya mwili mzima. Madhara yake ni kuwa mwili huishiwa nguvu
kabisa, na kadri melanin inapopungua, ndipo mionzi hatari ya jua ya UV na
Blue-rays inapopenya zaidi kuingia ndani ya Ngozi, na kuathiri kila kitu katika
afya ya mwili. Lusifa anajua kadri anavyoua kinga, kila mfumo wa afya
utaathirika, na watu watazidi kuwa watumwa wake kwa kutegemea mifumo yake kwa
madawa na matibabu tegemezi.
Cosmetics nyingi kama ambavyo huwa zikiwa
na harufu nzuri sana, zimejawa na maelfu ya chembechembe zenye mamia ya
Fluorides, mfano ‘’PFA’s’’, hizi zimejaa fluorides ambazo huvuta karibia
electrons zote toka kwa Oxygen, na kufanya mitochondria kushindwa kuzalisha
maji, wala kuzalisha nishati. Hii kitaalamu pia unaweza iita kama ‘’reduction
in redox potential’’.
Cosmetics huwa zinajazwa chembechembe
ambazo hata mashirika ya afya huwa wanashindwa kuzinyumbua na kujua hatari
zake, ijapokuwa huwa zimejazwa kwenye ingredients. Mfano ni ‘’Fragnances’’,
hizi ni hatari sana kwa afya ya Ngozi, lakini hakuna namna watumiaji wanaweza
kukimbiana nayo kwa kadri maisha yamekuwa hayawezekani bila bidhaa hizi.
Watengeneza mafuta wengi wanatambua shida
kubwa za watumiaji wao ni matatizo ya vimelea kama fangasi, bakteria, na shida
za mwili kujishambulia ‘’autoimmune disorders’’, ambazo huchochea uvimbe na
vipele, na wakati kadhaa shida hizi huchochewa sana na allergy. Watengeneza
mafuta wengi huweka chembechembe kama ‘’steroids’’ ili kupunguza uvimbe, lakini
madhara yake ni kuwa, chembechembe hizi sasa ndizo hushusha kabisa afya ya
kinga ya Ngozi, na huifanya Ngozi kuathirika zaidi na vimelea na fangasi, hata
na virusi. Matumizi pia ya viua vimelea kama kwenye ‘’cleansers’’ nyingi, ili
kuua bakteria kama staphylococcus, au streptococcus, huua mpaka vimelea wazuri
katika Ngozi, na hivyo kuathiri balansi ya Ngozi, na kuchochea kushuka kabisa
kwa kinga za warembo hawa.
Lusifa hufurahia sana anapoona sasa
warembo feki, hawana kinga kabisa katika miili yao. Kadri wanavyojiwekea
mawigi, ndivyo wanavyopunguza mianga mizuri kuingia katika ubongo wao, na hivyo
kupunguza afya bora ya ubongo. serums nyingi, huingia katika damu na kujaza
chembechembe ngeni na hatari kwa mifumo ya afya. Mafuta mengi yamejaa
chembechembe nzuri kama Retinol au Vitamin A, lakini hazina uhalisia, wala
vitamin C zisizo na faida. Maana viwango vyake huwa vidogo sana. Creams nyingi
huzuia matundu ya Ngozi kupumua, na kuchochea chunusi kwa baadhi ya watu wenye
Ngozi laini za mafuta.
Tattoos zina madhara makubwa sana katika
Ngozi, huongeza kiwango kikubwa sana cha ‘’plastics nanoparticles’’ katika
damu, ambazo madhara yake ni hatari, na hayatabiriki, lakini huchafua afya ya
damu, huchochea uvimbe mdogo chini ya rangi hizi. Na ndivyo zilivyo rangi
nyingi pia za kisasa ambazo hupenya aidha toka katika dyes za nywele na kuingia
katika kichwa, au toka lipsticks na kuingia katika mdomo, haya yote hushusha
sana kinga ya binadamu, na kuwafanya maiti zinazotembea.
rejea nukuu kadhaa kuhusu madhara zaidi ya cosmetics ingredients kadhaa,
pia rejea,,



.png)

Join the conversation