Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

WEWE UNAKULA PILIPILI?🌶️🌶️🍲🥗

Pilipili inakataa kuliwa, Capsaicin yake inautriki Ubongo kuwasha Moto. Swali ni je, faida za ulaji wa Pilipili zinazidi hatari ya ulaji wake?

PILIPILI ‘’SPICY"

Yawezekana hakuna mtu ambaye hajawahi kula pilipili. Lakini pia yawezekana hakuna atakaye acha kula pilipili. Lakini hizi zote haziwezi kubadili lolote kuhusiana na namna pilipili inahusiana na mwili. Yawezekana madhara ya pilipili yakawa ni madogo sana katika kiwango cha kusemwa ni madhara, lakini hiyo pia sio sababu kwa maana hoja ni madhara, na sio kiwango cha madhara. Watu wengi hawajui kuwa bado kiwango cha maarifa yetu hakijajafikia mwisho wa kutambua madhara ya vitu ambavyo yawezekana hatuoni madhara yake Kwa sasa. Ilitumia miaka mingi sana kuja kugundua kuwa mionzi ya madini ya uranium na mengineyo huathiri mwili kijenetikia.

Vivyo hivyo Pilipili ambayo imekuwa miongoni mwa vichochea Ladha maarufu sana, nayo imeingia kwenye mgogoro mkubwa sana. Hii ni kutokana na kuwa na faida nyingi, na kupendwa na wengi, lakini pia kuonekana kabisa kuwa haipendwi na ubongo, wala mwili mpaka mtu atakapokuwa mlevi wa pilipili. Hebu tuangalie kiundani swala hili.

SAYANSI YA UTENDAJI WA PILIPI

Pilipili ina kemikali zinazoitwa ‘’Capsaicin’’, Ambazo huamsha au huisiwa na receptors ambazo huwa zinashughulika na kuhisi Moto, au vitu vyenye joto. Na pia, tuliona kuwa receptors hizo maarufu zinaitwa ‘’TRPV1’’. Unapokula kitu chenye pilipili, ubongo wako huwa unatambua kuwa umekula kitu cha moto. Sasa hata kwa kutumia uelewa wa kawaida, je huu sio udanganyifu wa mfumo wa fahamu?

Mtu mmoja angeweza kuhisi labda pilipili ilipaswa kuufanya mwili utende kama unavyotenda kwa vitu vya moto, na kwa mantiki hiyo, sio udanganyifu. Hoja hiyo sio kweli kwa maana, matendo ambayo mwili huyatenda baada ya mtu kula pilipili yana manufaa tu kama mtu angekula chakula cha moto, na wala hayana maana kama namna ya kujikinga na pilipili. Huu ni udanganyifu wa mlango wa fahamu.

MATOKEO YA ULAJI WA PILIPILI

MAUMIVU MAKALI

Kwanini Watoto hulia unapowawekea pilipili kwenye chakula? Ni kwa kuwa hushindwa kuvumilia maumivu kama wakubwa wao wanavyovumilia. Na hata wakubwa wao pia macho huonesha dalili za machozi, na hata hulia kama pilipili hizi zitakuwa nyingi sana. au zitaingia katika sehemu zingine za mwili kama vile machoni au kwenye vidonda.

Nini maana ya maumivu?

Maumivu ni utambuzi wa hatari. Mwili unapoumia ni kama unakwambia hebu acha utakufa. Acha ondoka. hii ni lugha ya mfumo wa ubongo, na ndiyo maana unapokanyaga mwiba haraka sana huondoa mguu wako.

NINI HASA HUTOKEA KAMA UTAKULA SANA PILIPILI?

Pilipili haijawai rekodiwa kuweza kuleta madhara makubwa yoyote yale kwa watumiaji, ijapokuwa pilipili huweza sababisha changamoto za kuongezeka kwa mafuta, na kuvimba kwa kuta za utumbo ‘’inflammation’’. Pilipili huweza kupelekea kutapika, kuharisha, na matatizo hasa ya utendaji wa mfumo wa chakula. 

Changamoto kubwa bado ipo katika kuelewa zaidi matokeo ya ulaji wa pilipili kwa ubongo, tafiti zaidi zinahitajika hapa kama tafiti nyingi zilizofanyika katika kuangalia faida za ulaji wa pilipili.

Faida kadhaa za ulaji wa pilipili

huongeza hali ya kuridhika na chakula ‘’satiety’’ na pia hupunguza hamu ya kula ‘’appetite’’. Hupunguza ukinzani dhidi ya homoni ya leptin ambayo hutawala mfumo wa hamu za kula na matendo baadhi ya mfumo wa homoni zinazoshughulika na mfumo wa ulaji. huongeza adiponectin, na kupunguza uzito wa mwili na BMI. Pia huongeza UCP1 na PGC-1α zinazosaidia kuzuia uzito mkubwa. Na Huongeza joto na nishati

Huvunja mafuta ya mwili, Hupunguza kujaa au kujiunda kwa mafuta meupe ‘’WAT’’ au white adipose tissues na pia Huchochea mafuta ya njano ambayo yanafanana na misuli, ‘’BAT’’ au brown adipose tissues. huyabadili mafuta meupe ‘’WAT’’ kuwa njano ‘’BAT’’

Pilipili ni ‘’Antioxidants’’ hupambana na kemikali sumu free radicals kama ‘’reactive oxygen species’’, na kwa mantiki hii, inaweza tumika kutunza chakula, na kusaidia tishu za mwili.

Pilipili humfanya mtumiaji ajiisikie raha’euphoria’’. Na Pilipili huchochea au ‘’boost’’ hali ya mwili ya matendo ya kibiolojia ‘’metabolism’’. Pia Pilipili huua vimelea vilivyopo kwenye chakula.

MASWALI YA MASHAKA YA KUJIULIZA?

Kwanini mwili mfano ulimi huzamisha zaidi receptors za TRPV1 kwenye ulimi ili zisikutane na pilipili? Hiki kitendo hupelekea mtu kula zaidi pilipili bila kuhisi. Na hali hii inaitwa desensitization . hii ni kama mpaka jenetikia imehusika kupambana na swala la ulaji wa pilipili baada ya kuona changamoto katika ubongo, je swala hili lina nini cha kusema kuhusu tusichokijua?

Pilipili hupelekea hali ya kuhisi raha sana ‘’Euphoria’’ Ambayo mara nyingi hufikiwa na watu waliofanya aidha mazoezi makubwa sana yaliyopelekea joto kubwa sana na sasa wamemaliza. Mfano, baada ya kumaliza mechi ya mpira au kukimbia, mwili hujisikia raha sana? Au watu wanaofanya vitu vinavyotumia nishati kubwa sana. Hali hii inahusianaje na pilipili kama sio tu kwa kuutriki ubongo?

Pilipili husababisha uraibu ‘’addiction’’. Iweje pilipili isababishe uraibu na iwe tu kemikali isiyo na madhara ya uchochezi hatari kwenye ubongo?

Kwanini asili iumbe kitu chenye faida katika namna ya kutesa? Tofauti na uumbaji wake mwingine wa vitu muhimu kuvutia.

KWANINI SISHAURI PILIPILI 

Biolojia

Kadri unavyokaribia maeneo ya Tropiki ndivyo Pilipili zinavyozidi kuwa Kali zaidi. Sababu ni kuwa Tropiki Kuna wanyama Wala nyasi na Mammalia wengi sana. Pilipili ni aina ya Mimea ambayo inaonyesha kuwa ni maalumu Kwa ndege. Ndege hata wakila Pilipili hawahisi ukali kama ambao huisiwa na Mammalia kama Binadamu, au mbuzi, na Ng'ombe. Pilipili ni Mimea ambayo ina kemikali za ukali"Capsaicin" ili isiliwe na viumbe wengine tofauti na ndege, inalenga iliwe na ndege TU ambao watazisambaza Mbegu zake.

Pilipili ni Mimea maalumu isiyohitajika kuliwa na Mammalia kama Binadamu. Na hii ni sababu Mammalia wote hawali Pilipili ukiachana na Binadamu wabishi. Pilipili ni kama walivyo Kunguru, au Nguruwe, au fisi, au Simba, n.k. wanyama hawa hawaliwi Kwa kuwa wanatambulika kuwa na kusudi maalumu katika ikolojia ya ulimwengu, mfano; kubalansi uwiano wa wanyama mwituni, au usafi katika asili. 

Simba anabalansi idadi ya wanyama Wala nyasi wasizimalize, Nguruwe anasafisha mazingira Kwa ulaji wake, Samaki kambare anakula samaki wengine kubalansi ukuaji wa samaki wengine majini, fisi anakula mizoga kusafisha mabaki, hii stori ndiyo ipo Kwa Pilipili pia, zipo kahamasisha ushamiri zaidi wa ndege ambao hubalansi ukuaji wa wadudu Kwa kuwala, Pilipili inasababu za kukataa kuliwa na Mammalia.

Kiafya

Pilipili inapoliwa inasababisha mfumo wote wa Chakula kuwa mithili ya unakula moto, hii Ndiyo sababu huitwa "Irritant'. Pilipili hupelekea mwili kuingia katika Hali ya kupambana na moto Kwa kuongeza uzalishaji wa vimiminika au maji katika tumbo na utumbo, jambo hili Kwa mara chache sana watu huisi ni hatari kama litapelekea kuharisha, lakini wanasahau hupelekea Hali ya uvimbe mdogo, na huathiri ufyonzwaji wa madini muhimu katika utumbo.

Sensa za kuhisi Joto "TRPV1" huzidi kujididimiza ndani, hii huanza kuathiri mfumo mzima wa mwili kuweza kujua Hali Joto ya Chakula, na mwishowe; mfumo wa umeng'enyaji huathiriwa Kwa kuwa Kuna uhusiano wa utambuzi wa Hali Joto ya Chakula na katika utumbo, na umeng'enyaji Kwa uzalishaji wa vimeng'enya au enzymes. Kwa kula Pilipili, watu huanza kuathiri umeng'enyaji na ufyonzwaji wa virutubisho.

Kwa ulaji wa Pilipili watu hupoteza maji mengi sana, hii ni Kwa kuwa mwili huisi mtu yupo katika Hali ya Joto sana, kama katika zoezi, au kazi nzito, na jambo hili hupelekea mwili kupoteza maji mengi sana kama namna ya kujipooza. Na hii Ndiyo sababu utaona Wala Pilipili wakitokwa sana na jasho. Hili ni tatizo kubwa sana, Wakati wa kula Sio Wakati sahihi wakupoteza maji, Kwa kuwa mwili huitaji zaidi maji Wakati wakula. Upotezaji wa maji huathiri metabolikia za mwili. Faida zote za Pilipili za kupunguza mafuta msingi wake ni hisia ya mwili kuwa ipo katika Joto na zoezi, hivyo unapaswa kuvunja mafuta, lakini hasara yake ni kuwa; mwili haupo katika zoezi na hivyo kazi yote ni Bure,  na ndiyo maana hakuna mbinu ya kushusha uzito Kwa kula Pilipili.

Watu wanaokula Pilipili hujikuta wakila sana Chakula, sababu kubwa ni ongezeko la msisimko wa Ladha Kwa kuchochea hisia za Joto. Kiasi ni jambo la msingi sana linalozidi kupotea Kwa mapenzi makubwa sana ya utumiaji wa bidhaa za kusisimua kama Pilipili. Kadri utumiaji na kiasi vinavyozidi ndiyo madhara yanavyozidi.


Kama utapuuzia asili, fiziolojia, na Saikolojia ktk Uchaguzi wako wa Chakula, Kwa kuangalia virutubisho tu vilivyomo mfano vitamins, au madini, ipo siku utakula nyama ya mtu kisa ina protini nyingi na omega fats#