Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

UNAWEZA ISHI MIAKA 100+ ❓

Mitochondria zinaonyesha Binadamu ana uwezo wa kuishi miaka 150~170, kawaida Lifespan ni 70..lkn kwanini UZEE uwe ni Ugonjwa?

 Siri ya 08-02 (Part 1)

Je Wajua!!!!

Wastani wa watu wengi huisi wanakunywa maji, lakini kiuhalisia wengi wao huwa hawanywi maji ya kutosha. Wengi hutegemea hisia ya kiu ya maji kama alarm ya kuwashtua kunywa maji. Hii ni hatari. Wapo watu wanaosubiria kukauka Kwa Midomo, au mate kuwa mazito kama dalili ya kupungukiwa maji, hii nayo ni hatari. Wengi wa Hawa watu huwa katika hatua za mwisho kabisa za mwili kupungukiwa maji "dehydration".  Wengi hawatambui kuwa Ubongo hushindwa kutofautisha hamu ya maji ya kunywa, na hamu ya Chakula, au vinywaji. Wengi hunywa soda, Juisi, au hata hula Vyakula ilihali walikuwa tu wanahisi hamu ya maji. Hii inatokana na kuwa, Ubongo hushusha hisia ya kiu ya maji unapokunywa Juisi, au hata kula Vyakula kadhaa, si Kwa kuwa umetosheka na maji, La hasha. bali sababu umesitisha kuzalisha zaidi homoni za hamu ya maji, Kwa kuchanganywa na uwepo wa Juisi au Vyakula.

Wengi hawajui Sababu ya mwisho ya Vifo vyote ni upungufu wa maji "dehydration". Na ndiyo maana mgonjwa yoyote wa Nusu kaputi yule huanza kusaidiwa Kwa Drip za maji. Pia wengi hawajui Ukila sana usiku unaamka sana na Njaa, Si kweli. unaamka sana na kiu ya maji. Lakini unahisi ni hamu ya Chakula. matendo yote ya kibiolojia yanategemea sana maji. Bahati mbaya wengi hufundishwa umuhimu wa maji kama miongoni mwa sehemu za Chakula. Wengi huyaweka maji katika sehemu sawa na protini, Wanga, vitamini, mafuta na madini. 

Kwa Elimu ya muundo huu, hata wasomi hawawezi kuelezea umuhimu wa maji mwilini. Unaweza jaribu hili Kwa kuwauliza wawili watatu unaofahamiana nao. Wengi utagundua wakitumia lugha ya "maji yanasaidia jambo Fulani, " lugha hii Ndiyo wengi huielewa, yaani huyaweka maji kama nyuma ya vitu vya msingi zaidi mwilini, na kuwa maji yenyewe siyo ya muhimu Kwa kujitegemea. Sehemu hii haitaleza kirefu sana kuhusiana na umuhimu wa maji, namna yanaweza hata kutatua magonjwa na shida mbalimbali, Kwa kufanya hivyo nitakuwa kama naandika Tena kitabu nikichokwisha kiandika kuhusiana na namna maji yanatatua magonjwa Sugu. Sehemu hii inahusiana na namna maji yanavyohusiana na uzee.

Inafahamika kuwa kadri mtu anavyozeeka, au kuelekea uzeeni. Uwezo wake wa kutunza maji mwilini na katika seli zake unazidi kushuka. Kiwango Cha maji yaliyo ndani ya seli ukilinganisha na yaliyo nje ya seli hushuka kutoka wastani wa 1.1 mpaka 0.8. wengi hushindwa kuelewa kwanini uwezo huu wa kutunza maji hupungua, lakini yapo mengi yanayofahamika kuhusiana na swala hili. Kwanza kadri mtu anavyozeeka, ndivyo ngozi yake inavyozidi kushindwa kufyonza mionzi ya Mwanga wa Jua na kutengeneza Vitamin D. hapa ni kama unapata mantiki hii, kadri mtu anavyozidi kuzeeka, ndivyo anavyopungukiwa zaidi Mwanga na maji. Yaani huyu mtu Sasa anahitaji maji mengi sana, na vipindi virefu zaidi vya Mwanga. Watu wengi wanapoelekea uzeeni, hisia zao za kiu ya maji hushuka zaidi, hivyo Kwa wastani huisi kiu Kwa kiwango kidogo zaidi. 

Na kumbuka, hisia hizi hushuka Kwa kuwa wazee wengi huwa na utendaji mdogo Kwa wastani wa uzalishaji wa homoni zote, ziwe za uzazi, au za hamu za maji. Unapozaliwa unakuwa na maji mengi sana asilimia 80%, unapofika miaka 70, 80 mpaka 90, unabakia asilimia 50-55%, Tena mwili ukibakiwa na uwezo mdogo sana wa kufyonza Mwanga wa Jua wenye kuwezesha kuzalisha vitamin D, ambayo inahusiana Moja Kwa Moja na homoni zingine zote, na ndiyo husaidia Kinga ya mwili, na vitamin A ambayo inahusiana na afya ya ngozi na kuweza kuona.(Wazee wengi huwa na shida ya kuona, kutokana na upungufu wa vitamin A inayoathiriwa na vitamin D, pia kupungukiwa na ufanisi wa Neva za kuona, kutokana na shida za Kihomoni na cover za Neva za kuona)

Mionzi ya Mwanga wa Jua wa asubuhi na jioni huwa ya Infrared rays, na Red light, ambayo hii huingia katika ngozi na kusisimua kuzalisha vitamin D, lakini kubwa zaidi, Inapofika ndani ya seli za mwili, huingia hata ndani ya chembechembe za seli zinazozalisha nishati, kuamua seli ife au iishi, zinazoitwa "Mitochondria". Mwanga huu hukutana na maji yaliyo ndani ya chembechembe hizi. Na hapo Sasa, huyasisimua maji haya kutengeneza tabaka linaloitwa EZ, ambalo liligunduliwa na Gerald Pollack, ambalo hili Sasa huwezesha protini na chembechembe zote za Ndani ya seli kufanya kazi kama inavyopaswa. 

Mwanga huu wa asubuhi hauishii hapo tu, Kwa msaada wa maji ambayo mtu huyu huwa ameyanywa yakutosha, au amejizoesha kunywa, basi maji haya hulowanisha chembechembe zinazoitwa "melanin", na chembechembe hizi ambazo ndani ya seli huwa kama chip za Semiconductors za kwenye simu, hushusha Umeme wa unaozalishwa katika Kuta za chembechembe hizi za mitochondria mpaka umeme sawa na Moja ya Trillion ya unit Moja ya ampere. Huu umeme ndiyo huuwezesha mwili kuponyesha makovu, vidonda, tishu zilizokufa, kila kilichoharibika katika mwili wa Binadamu. 

Mpaka hapa unagundua mwanga na maji ndiyo dawa kuu za Uhai. Kadri wazee wengi wanapopungukiwa vitu hivi viwili, hupelekea chembechembe hizi za mitochondria kuvujisha Kuta zake, na kupelekea kupotea Kwa vipisi vinavyokaaga katika Kuta hizi vinavyoitwa "CC", hizi zikivuja tu zikaingia katika seli toka chembechembe za mitochondria, basi seli hufa Moja Kwa Moja.

Hufahamika kuwa kinachomfanya mtu kuzeeka ni kushamiri zaidi Kwa kemikali Sumu "free radicals". hizi Sumu zote huwa zinatoka kutoka chembechembe hizi za mitochondria. Na kemikali hizi huvuja kutokana na upungufu wa maji, ambao huwa hatari zaidi unapozeeka. Na upungufu huu ndo hupelekea Sasa mitochondria kuzalisha umeme mkali sana toka chembechembe za melanin, ambazo hupelekea kushamiri Kwa umeme hata kuvuja Kwa chembechembe za electrons zinazopelekea kushamiri Kwa kemikali Sumu. na mitochondria Sasa huamua tu kusisimua protini ambazo ndizo chinja chinja, zinazoitwa "Caspases". 

Hizi protini huua seli za mwili Moja Kwa Moja, hiki kitendo kinaitwa "apoptosis". Ni muhimu Kwa wasomaji kutambua kuwa, hutaona ongezeko la Moja Kwa Moja la kemikali Sumu "free radicals" Kwa wazee, hii ni Kwa kuwa namna seli zinavyokufa katika kipindi hiki cha "uzee " apoptosis", ni uuaji wa kimyakimya "silent death". Maana yake ni kuwa, kitu Pekee utakachokiona ni upungufu wa chembechembe hizi za mitochondria. Na kamwe usijaribu kuwapa sana wazee Hawa "antioxidants" kama Vitamin C ukihisi Kwa kufanya hivi utatatua shida ya uzee, si kweli. Kemikali hizi Sumu "Free radicals" pia zinafaida zake mwilini, maana huzipa seli taarifa kuhusiana na afya ya seli kwamba inapaswa kuisha, au Inapaswa kuendelea.

Jambo la mwisho la muhimu Kwa wasomaji kutambua ni kuwa, kadri mtu anavyoelekea uzeeni, huwa anashida sana ya stress, na hii ndiyo sababu wengi sana huwa na shida ya Misongo ya mawazo. Hii inatokana na kuwa, wazee wengi huwa na shida ya Upungufu wa maji, na hivyo damu zao huwa nzito na hivyo Ubongo husisimua sana uzalishaji wa homoni "vasopressin", ambayo hii kadri inavyozalishwa, huchochea sana stress zikiwa na logic ya kuongeza Presha ya damu. Vasopressin hii ambayo ndiyo homoni ya stress huwa na lengo la kuongeza kiwango Cha maji ndani ya chembechembe za mitochondria. kwanini zinaongeza maji? Nilishasema sababu ni kuongeza uponaji wa tishu za mwili "regeneration", na kuongeza uzalishaji wa seli za mwili "stem cells production". Na kitu cha ajabu ni kuwa, pia mwanga wa asubuhi na jioni huchochea kuzalishwa kwa kemikali za ‘’NO’’ ambazo, hizi huchochea kutanuka kwa mishipa ya damu kuruhusu damu ipite vizuri na afya ya moyo, lakini pia huchochea seli zizalishwe zaidi katika mifupa. 

Hii ina maana gani? Kumbe dawa kuu ya kutatua shida za kukosa Usingizi uzeeni, kuondoa msongo wa mawazo na usahaulifu, na shida zinginezo kama za Figo na moyo. Ni kunywa maji ya kutosha. Hii ni kwa kuwa maji ni dawa kuu ya kushusha Vasopressin "Anti-vasopressin", na hii Sio shida kuelewa. Maana kazi kuu ya vasopressin ni kutunza maji, na ndiyo maana pia huitwa ''kizuia upotevu wa maji" au "anti-diuretic hormone". Sasa ukinywa maji, tayari Ubongo wako hautakuwa na haja ya kuzalisha zaidi vasopressin, Kwa lugha nyingine, kumbe Kwa kunywa maji, unashusha stress Moja Kwa Moja. Kwanini? Kwa kuwa upungufu wa maji ndiyo stress zenyewe.

Jambo jingine la ajabu sana, Mwanga wa Jua ule wa kuanzia saa 11:30, hata wa mpaka saa Nne, usio na frequency za Blue hushusha stress. "Sunlight is Anti-vasopressin". Ndiyo maana, watu wanaoamka mapema sana na kunywa maji, na kutowasha taa za mianga ya Kisasa, huwa hawana stress, maana wameshatumia vitu vikubwa viwili vinavyoshusha vasopressin. Mwanga wa alfajiri na alasiri pia husisimua nyuklia Moja wapo katika Ubongo inayoitwa "POMC", ambayo inaposisimka huzalisha homoni kuu inayoitwa "Alpha -MSH". Hii ndo homoni inayoongoza utendaji na uzalishwaji wa homoni zingine zote, na ndiyo homoni ambayo hushusha hisia zote za Maumivu, na ndiyo homoni ambayo huongoza uzalishaji wa homoni kuu ya "Leptin".

Leptin ndiyo hutawala hisia za kuridhika, huuwezesha Ubongo kutawala utendaji wa seli zote za mwili. Watu wanapokuwa na leptin Kwa wastani mzuri, basi pia huwa na homoni za adiponectin za kutosha, ambazo hizo ndizo huupa mwili uwezo wa kupambana na changamoto zote za kujaa Kwa mafuta, na hushusha hatari za kujawa na mafuta kadri Umri unavyosonga. homoni zote ili ziundwe zinahitaji mwili tayari uwe na maji ya kutosha. Kwanini? Kwasababu mwili unapopungukiwa maji, husisimua mfumo wa stress " HPA-axis", huu unapowaka, huzimisha mfumo wa Ubongo wa kuzalisha homoni zingine ikiwemo mfumo wa homoni za uzazi "HPG-axis". Hii ni kama, mwili hauwezi kubali kuzalisha homoni za uzazi Wakati unatambua upo katika mazingira yenye hatari kubwa sana. Kitaalamu hii pia huitwa "pregnenolone steal syndrome", yaani, unapokuwa katika stress, mwili Hutumia cholesterol zote kuzalisha zaidi "cortisol" ambayo nayo ni "stress hormone".

Shida zote za uzeeni hutokea kutokana tu na upungufu wa maji, na upungufu wa Mwanga. Wazee pia huwa hawana Nguvu za mifupa, hii ni kutokana na upungufu wa vitamin D inayofyonza madini ya mifupa "calcium" toka katika Utumbo. Lakini pia upungufu wa maji huifanya mifupa kuwa kama zege lilipongukiwa maji, hulegea, katika blog zingine nimeelezea namna mianga ya Kisasa, upungufu wa ATP' au nishati, n.k. namna ambavyo huamasisha changamoto hizi. Wazee pia huwa na mvi nyingi kama ishara ya Upungufu wa chembechembe za melanin, na ndivyo huwa pia upungufu wa nywele, na kulegea Kwa ngozi, haya yote yanaweza punguzwa Kwa unywaji wa Maji, na kupata nyakati za kutosha katika mianga ya UV. Katika mtazamo huu unagundua kuwa Dawa nyingi huwa hazizingatii Biolojia ya Ndani kabisa ya mwili, na huwa zina malengo ya kuwafanya watu kuwa watumwa, na masoko ya madawa. Ushauri katika siri hii kwa wazee ni kunywa maji ya kutosha, kuanzia Lita mbili na nusu, mpaka Lita tatu, hata Lita tatu na nusu Kwa maeneo yenye Joto sana. 

Unywaji huu usiwe Kwa mara Moja, utawanyike ndani ya masaa kumi na mbili. Na usiwe nusu saa kabla na baada ya Chakula. unywaji wa maji uambatane na matumizi ya chumvi ya mawe si chini ya gramu Nne Kwa siku. ( Sio chumvi ya mezani, chumvi ya mawe ina madini zaidi ya 84, ikiwemo na ya magnesium, ambayo haya husaidia kubalansi kiwango Cha maji nje ya seli). Hii ni kwasababu maji yote yaliyo nje ya seli "ECF" hushikiliwa na chumvi hii, hivyo ukipungukiwa chumvi hii, utapungukiwa na Maji, ijapokuwa hospitalini utaambiwa umepungukiwa Chumvi " hyponatremia". lakini hoja ni kuwa, hata ukifia Mtoni, bado utakufa Kwa upungufu wa maji. Usishangae maana bado upungufu wa Oksijeni hupelekea upungufu wa maji ambayo ndiyo huundwa katika Mitochondria, na ndiyo ambayo hutawala Biolojia ya uhai. Kwa hiyo umekufa Mtoni, lakini umekufa Kwa upungufu wa maji, Kwa kupungukiwa Oksijeni.

Unywaji wa maji uambatane na kutembea tembea, hii ni Kusaidia maji yasukumwe Kila Kona ya mwili. Na unapotembea, unavunja mafuta yanayozuia mishipa ya damu isipitishe maji vizuri. Mzee Usinywe kahawa, wala soda, wala chai ya rangi, wala Pombe. Maana Kwa kufanya hivi, unapoteza zaidi maji ilihali tayari una upungufu wa maji. Vinywaji hivi vina Caffeine ambayo husisimua upotezaji wa maji zaidi, na hu boost stress Kwa kusisimua "adrenaline". Mzee usipende kutumia dawa za Maumivu, kama "NSAIDs" hii ni Kwa kuwa, dawa hizi hublock " Prostaglandins" na hublock pia "Histamines", kipindi ambacho kemikali hizi ndizo hujiusisha na kusambaza zaidi maji mwilini, na pia, Maumivu haya huwa ndiyo alarm ya mwili kusisimua Uponaji "Regeneration".

Wengi hawajui kuwa mwili ili uanze kujiponyesha, lazima uhisi kwanza Maumivu. Katika tafiti za mijusi (zilizofanywa na Robert O Becker na wengineo), mijusi ambao huweza jiunda hata mikia yao ikikatwa. utagundua kama utaua Neva zao za fahamu, hawataweza Tena jiponesha. Ndivyo ilivyo pia, badala ya kukimbilia paracetamol, unaweza tumia maji, na Mwanga, na hata Baridi. mzee inabidi uongeze sana kutumia matunda, kama maparachichi, ili kuongeza kiwango Cha madini, na maji mwilini. Maji yaliyo katika matunda ni bora sana Kwa mwili. mwisho, Mzee anapaswa kutumia sana Supu za nyama. Hasa wanyama wanaolishwa majani, na kuku wa kienyeji, au Samaki. Usitumie nyama zilizopikwa Kwa mafuta ya Mbegu. Wazee wengi wanaopatwa na stroke huogopa Cholesterol, lakini wengi wao hawajui Cholesterol inapoungana na vitamin A chini ya uwepo wa homoni za thyroid "T3 na T4", ndiyo hutengeneza homoni zingine zote za mwili ambazo wao huwa Wana upungufu. 

Mzee mwenye uwezo kiuchumi badala ya kutumia mkate na chai asubuhi, basi ili asizeeke haraka, angepaswa kutumia mayai ya kuchemsha na siagi "Sio ya Kisasa", angetumia kachumbari badala ya kutumia mchuzi uliojaa mafuta ya Mbegu.  Mwili unapopungukiwa stress, huacha kuvunjavunja Collagen zilizo katika ngozi, na kuiacha ngozi kuwa imara, uwepo wa vitamin C na madini ya Copper na Zinc yakutosha huwezesha nywele kuwa imara na kutopoteza rangi Kwa haraka sana, matunda kama Machungwa, mapera, n.k. husaidia sana kubalansi madini haya, na Kwa kufanya hivi ikiwa Mzee na mtu huyu ana maji, basi ngozi ya mtu huyu huwa imara, nzuri, na yakuvutia. Kunywa maji haijawahi kuwa kazi rahisi. Pia kunywa maji huleta kero ya kukojoa kojoa. Hii husaidia kusafisha Figo, kutoa sumu mwilini. Na pia humfanya mtu asikae sana chini Kwa kero za kwenda kukojoa. Watu wengi wanapofikia tu lita Moja ya maji hujisahau kabisa kuendelea kunywa maji. Hili huwafanya kufeli kuelewa umuhimu wa kuendelea kunywa maji, na kushindwa kutatua tatizo la kuwahi kuzeeka na kufa.

Mungu alimuumba mwanadamu toka katika maji. Yaani, Kila kilichoumbwa kuanzia siku ya pili, kilianzia katika maji yaliyokuwepo siku ya kwanza, ambayo Mungu alianza kuyaumba na Roho yake ikawa ikielea katika vilindi vya maji haya. Sayari ya Dunia ndiyo sayari Pekee yenye maji kama inavyoonekana toka katika Picha za satalaiti. Wanasayansi wa anga huiita Dunia "Water planet". Ina asilimia 75% maji.  Hakuna namna unaweza elezea asili ya maji katika Dunia. namna Pekee ni kupitia Kutambua "Uumbaji wa Mungu". Nimeandika kitabu kizima kinachoelezea tu Sayari ya Dunia, na asili ya maji yake, na chanzo Cha maji ya chumvi yaliyopo Duniani. Na hata kinaelezea kwanini ongezeko la madini ya Deuterium kwenye maji kipindi Cha Gharika ya Nuhu ndiyo chanzo kikuu Cha kushuka Kwa Umri wa kuishi toka miaka 900, mpaka miaka 600 na Kisha 120. Madini haya pamoja na Carbon-14. Ndiyo chanzo kikuu Cha kushuka Kwa Uhai wa wanadamu kutokana na kuathiri Moja Kwa Moja utendaji wa Mitochondria au chembechembe za Uhai.