UTAVUKAJE MIAKA 90 NA AFYA❓
Siri ya 08-03 (Part 2)
MAELEZO RAHISI
DOZI 01
Kwa Picha ni David Sinclair, hapo ana Miaka 50. Ni kiongozi katika kitengo Cha Kutozeeka "Anti-aging". Kwake UZEE ni Ugonjwa. Kwa awali nalenga hoja yake Moja tu....lakini kabla ni muhimu sana kutambua Nitamkosea sana Prof au Dr Sinclair kama sitamtaja kama miongoni mwa wagunduzi wa vinasaba vya kuishi MIAKA mingi "Sirtuins",...
Upi ni mfumo imara zaidi Kwa Uhai mrefu?
- kula kidogo sana/ mara mbili, au kuwa na vipindi virefu Walahu masaa 14 Kila siku kati ya Milo. Hii ni sawa na mtazamo wa Dr Jason Fung ambaye ni Muasisi mkubwa wa Sayansi za Kufunga.
- Ni hatari sana kula katikati ya Milo "snacking".
- Kula zaidi mbogamboga za majani, nyama kula Kwa kiasi kidogo usiache, Wanga na matunda ya sukari sana kula kidogo sana.
- Madini chuma yakizidi hupelekea ngozi kulegea kizee "zombie/senescent cells", kuonyesha unahitaji kiasi ktk protini za wanyama unazokula. (Lakini Mimi naumia kaua panya wengi sana Kwa experiment zake).
# Utafiti unaonyesha Mbwa wa Mtaani wanaokula mlo mmoja-mmoja wanaishi miaka asilimia 30% zaidi ya Mbwa wa ndani wanaolishwa Kila mlo.
DOZI 02
Kadri mwili wako unavyoingia, au unavyobakia katika hali ya kuwaza mapenzi, au Sex! Ndivyo unavyowahi zaidi kuzeeka & kufa.
Asili imekaa hivi; "Ukishazaa, ushamaliza mwendo na unapaswa kufa"
Viumbe wengi sana hufa baada ya kuzaa, Sio tu vinyonga, bali hata samaki; mfano Pacific salmon hufa katika kuzaa, na ndivyo ilivyo Kwa jamii ya Samaki pweza wengi sana.
KUZAA SIO HATARI, NI JUKUMU LETU KUZAA, NINI MAANA YA SOMO❓
MOJA(1)
Matumizi ya sukari na kuwa ktk Hali ya kushiba Kwa Wakati wote huzifanya insulin kuwa juu muda wote. Insulin huufanya mwili kusema; umeshiba Sasa zaa!! Na hii hupelekea kushushwa Kwa protini SHBG, na kupanda Kwa homoni ya Testosterone. Hii Sasa hupelekea yafuatayo;
i. kuongezeka Kwa hisia za Mapenzi baada TU ya ulaji wa Vyakula vya sukari vya kusisimua.
ii.kuongezeka Kwa chunusi Kwa ulaji sana wa sukari, maana Testosterone huzisisimua sebaceous glands chini ya ngozi kuzalisha mafuta. Kumbuka lengo lilikuwa kuifanya ngozi iwe na mafuta ivutie kimapenzi, ila Kwa kuwa imezidi, hupelekea Chunusi. Na nyakati nyingine hubadilishwa kuunda DHT ambayo hupelekea nywele kuisha.
PILI(2)
Hii nawalenga sana vijana, "kushinda sana ktk Screen za simu"..Blue frequencies zinachochea kupanda Kwa Insulin, & Social content zimejaa sana Semi-Nudity & sexual contents. Hizi huwasisimua sana kihisia' za Mapenzi.
HATARI ZAIDI❌❌❌❌❌❌
kuanza kufanya mapenzi mapema ni hatari sana!!!! Sokwe tuliofanana nao Kwa 99% wanaanza kufanya mapenzi wakiwa na Umri wa miaka 12, na Wanaishi miaka 30 TU. Binadamu wanapaswa kuanza wakiwa na miaka Walahu 19 mpaka 25 ili kubalansi miaka 70.
Hiyo hoja unaweza kumuelewa vizuri zaidi Professor Nick Lane Kwa Picha... Nimempenda sana ktk kitabu chake Cha "The Oxygen"
Milioni 30 kati ya 50 ya wanawake wanaozaa kabla ya miaka 19 ni Waafrika. Na ndivyo ilivyo chini pia miaka yao ya kuishi ukilinganisha na Wazungu Kwa nyakati hizi. Ni kweli Waafrika wapo vizuri zaidi kiuzazi, lkn Sio ktk Ulimbukeni wa usasa unaowamaliza zaidi. Usione Wazungu wanazaa watoto wawili ukahisi ni Viazi😶, wanajua Siri ifuatayo👇
Nishati ya mwili Ina makundi mawili, Moja ni kuendeleza Uhai wa mwili, na pili ni kuwezesha uzazi wako ili unapokufa uzao wako uendelee. Hizi nishati zimeunganishwa ktk mifumo ya homoni na matabolikia.
Unapaswa kuwa imara sana kabla ya kuamua kuzaa ili udumu zaidi. Kufanya maamuzi ya kuzaa ili Hali hutaweza kuhudumia uzao wako kutakufanya kutumia ziada yako yote ya kimwili kuendeleza uzao wako na wewe kuishia mapema.
Wanaume KUfa Mapema❓
Kitendo Cha wanawake kuingia Menopause hasa baada ya miaka 51, huwa-Fanya kutunza nishati yao yote Kwa ajili yao. Kitendo Cha wanaume kuendelea kuwa sexual active bila Stop, huwa Fanya kuishiwa fuel mapema.Kisayansi Kuna msem0✓✓✓ unasema "Biolojia inamjali ANAYEWEZA kuzaa. (Mti usiozaa wakatwa). Ila maajabu huyu Sio lzm yule anayenyonyesha...huyu ni yeyote mwenye nishati ya kuweza kumzaa na kumlea Mtoto. Wazazi wenye watoto wengi ni kweli wanaishi miaka mingi, lkni ni wale hasa wenye watoto waliowalea vizuri ht wakafanikiwa#
Fikiri kabla ya kufanya Sex, mwili unatambua sex ni Kwa ajili ya kuzaa# kuzaa pasipo mpango, kuwaza kuzaa (sex) pasipo mpango, matokeo yake ni watoto watakaokulaumu.
DOZI 03
Baridi, ukiachana na njaa, na Kupuuzia mambo yanayokuudhi ni Siri za Maisha Marefu.
Huyo Mzee usione kazeeka, ktk Sayansi za Afya (Biochemistry &Genetics) usipomjua Rudi shule❌
Anaitwa Professor Denham Harman, ndo mtu aliyegundua kadri unavyozeeka kemikali Sumu (Free radicals) huongezeka zaidi. Baada ya kugundua watu wakakimbilia Vitamin C (Antioxidant kutoa free radicals) ili waishi milele, Looh!!! Hakuna kitu. Kumbe mwili nao unahitaji Sumu bwana ili uishi. Hata hivyo! Bado Kuna uhusiano yakinifu wa kushindwa kuratibu kemikali hizi sumu na kuzeeka hata kufa.
Kila mwili wako unapokuwa na metabolikia kubwa zaidi (high metabolic rate), ndivyo unavyozalisha kemikali Sumu (free radicals) nyingi zaidi, na unakufa mapema, na unakula sana, ili kuwezesha metabolikia zako kuwa juu.
Panya, metabolikia zake ziko fasta na juu mara 50 zaidi ya tembo...na anaishi miaka 2~4 ila paka wasiwepo!!, tembo anaenda miaka 60~70. Ndivyo ilivyo, panya anakula muda wote, metabolikia kuwa juu zinawafanya wanazalisha sana Sumu(free radicals) na wanakufa mapema.
SOMO KWAKO♨️❓❓❓
Moja(1)
Baridi inakufanya metabolikia yako iwe chini, utazalisha kemikali Sumu "free radicals" chache..na hii Ndiyo sababu Wajapani, au hapa Bongo maeneo ya Baridi kama kaskazini na kusini nyanda za juu wanaishi miaka mingi zaidi.
1.Hii itakuambia kwanini kama ukiweza- OGA MAJI YA BARIDI.
2.Lala na kaa zaidi kwenye sehemu yenye ubaridi, madirisha makubwa.. Kama Daktari najua wanyama wote wanaolala nje mbugani kama Serengeti au Ndege wanaolala kwenye Miti, wanaishi miaka mingi zaidi ya Kuku wako unaowafugia Kwa Joto la Mkaa, au Ng'ombe anayelala ndani kasoro tu Hana shuka.
Pili (2)
(Hili najua huwezi❌❌❌)
•••Centanarians ni watu wanaoishi miaka zaidi ya 100+, wengi wapo Japani.
Hawa jamaa hawaishi miaka mingi sababu ya Mazoezi, au Mbogamboga za majani zenye antioxidants kama Vitamin E, au selenium. Siri yao kubwa ni Moja👇👇
1.HAWANA STRESS/ HAWAJALI
2.HAWANA MALENGO MENGI, KWANZA WENGI HAWAOI HAWATAKI SHIDA.
3 HAWANA TAMAA ZA MAFANIKIO YA MAISHA, KWAO WANAAMINI ZAIDI KTK UTAWA WAO.
lkn Walahu unaweza jifunza kitu hapo kuhusu umuhimu wa falsafa ya "Stoic". Sio Kila kitu lzm ufanikiwe, wewe sio wa muhimu sana❌❌..hii kijenetikia tunasema..Think slow~Die slow#
Ukiwaza sana, unakufa why?👇
UKIWAZA SANA~UTAKUFA MAPEMA
(Una bahati kujua hili👇)
-kila unapowaza, Ubongo huwa unaelekeza Nishati katika mawazo yako, Sio katika kuondoa kemikali Sumu"free radicals". Kwa hiyo mwili unajawa na Sumu nyingi sana zinazochochea shida sugu za kimetabolikia (oxidative Stress).
-Watoto hawawazi sana, huwa na kemikali Sumu chache sana, maana nishati yote hutumika kuondoa kemikali Sumu. Shida inaanza hapa kati (No job, No family, No Love, No God, No Peace, No Money,.....)
Mwili unatumia ATPs zote ku unfold Neuronal connections, Sio kuboost Catalase, Glutathione, SOD, n.k...
KITU WANAJENETIKIA WANAJUA ILA HAWATAKUAMBIA❌❌❌
1.watu wakubwa zaidi kimaumbile wanawahi kufa zaidi ya wadogo kimaumbile. Sababu ni hii! Homoni ya Ukuaji (GH ni pro-oxidant) inachochea zaidi Metabolikia kuwa kubwa, kuwahi kupevuka, na hatimaye; utawahi kuzeeka.. ( somo hapa!! Kamwe usichukue Supplements za Growth hormones au Testosterone kukuza Misuli)
Na ukiwa mkubwa kimaumbile, jaribu kutulia zaidi.
2 . Wanaume wanawahi kufa kutokana na metabolikia zao kuwa juu kutokana na kazi zao, na hii Ndiyo sababu Watoto hawatumii DNA za kwenye Mitochondria kutoka ktk Sperms za Baba zao, maana huwa na makosa mengi sana yanayotokana na kemikali zao Sumu kubwa.
Wanawake nao metabolikia zao huwa juu, lkn kutokana na maumbile yao madogo..maana ukiwa mdogo metabolikia zako pia zinakuwa juu ili uzalishe Joto, na hii Ndiyo sababu;
Wanawake Wana Joto zaidi. Lkn hawaathiriki sana Kwa kuwa, huwa watulivu, wapole, wanazungumza shida zao, na Wana watu wa kuwabembeleza#
Nilipokuwa nazungumza na rafiki yangu @Steve.. nilimwambia akae mbali na GYM, labda afanye-Millitary workouts)
Wengi hawavukagi miaka 50+...sababu ni hizo story hapo juu☝️..mfano angalia chini Hawa baadhi ya walio maarufu👇
Mazoezi Bora ni;
1. KUOGELEA
2. KUTEMBEA
3. KUKIMBIA & KURUKA KAMBA
4. KUCHEZA
5. KUFANYA KAZI ZA SHAMBA
6. KUBEBA UZITO MDOGO..



















Join the conversation