Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SIRI KUU YA KUJIOKOA AFYA ❤️‍🩹

Siri za ndani za mifumo ya afya

 Siri Ya 08-01

Hakuna daktari asiyejua kuwa hakuna kitu kinachoitwa tiba wala kinga, hizi zote ni sifa, na uwezo wa mwili wenyewe. Madaktari huikutanisha tu mifupa, lakini ni mifupa ambayo hujiunga yenyewe. Madaktari hukuwekea tu drip za maji, lakini ni mwili ambao huwa unajisaidia wenyewe. Kama tulivyoona katika sehemu zilizopita tulivyoona mfumo wa mwili unavyojiongoza, siku zote ugonjwa hutokea pale ambapo mwili huathiriwa katika mfumo wake wa mawasiliano. 

Na mwili huweza kuathiriwa katika mfumo wake wa mawasiliano kwa kuathiri mfumo wake wa maji, mwanga, na umeme ambao huwa unaongoza nishati zote za uhai. Mwili wa binadamu zaidi ya asilimia 75% ni maji, damu yake zaidi ya asilimia 93% ni maji, Vimiminika vyote vya tumboni asilimia 99.5% ni maji, hata ubongo wake zaidi ya asilimia 85% ni maji. Watu wengi huisi wanakula mimea, lakini asilimia zaidi ya 95% ya mmea ni mwanga. Na hii ni kutokana na kuwa mmea hubadilisha nishati yote ya mwanga kuunda chakula, kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Photosynthesis’’. 

Mwisho wa siku binadamu huishi kutokana na nishati ambayo huipata kupitia kitendo kinachoitwa ‘’Electron Transport Chain’’. Huu ni mfumo wa umeme wa seli ambao ndiyo huzalisha nishati ya mwili. Wasomi wadogo huisi kuwa nishati ya mwili huwa kupitia ATP, lakini kiuhalisia nishati ya mwili huwa kupitia balansi ya matendo ya ‘’Redox’’ ambayo huwa na nishati ya kujenga ‘’Reduction’’ kupitia chembechembe za NADPH, NADH, na Glutathione. Lakini huwa na nishati za kuvunja ‘’oxidation’’ za ‘’ATP’’ ambayo ndiyo wengi huijua.

Mfumo wa maelekezo ya mwili ndiyo huongoza afya ya kiumbe yeyote yule. na mfumo huu huathiriwa katika mazingira ambayo huwa na ongezeko kubwa zaidi la kemikali zisizohitajika, au Upungufu sana wa kemikali zinazohitajika. Kama mtu atapata chakula kinachohitajika kwa kulingana na asili yake au mazingira yake, sio chakula feki. Kama mtu atakunywa maji kwa kiwango kinachohitajika, kwa mfano lita hata 3 kwa watu waliozidi kilo 50, kama mtu atalala kwa wastani wa masaa 8 katika giza, kama mtu atahusisha vipindi vya kutumia misuli yake kama kutembea au kazi yoyote ile walahu kati ya masaa yake ya siku, hakuna mtu atakayepata ugonjwa hata kidogo. 

Vimelea wengi ambao watu huwa wanaumwa, huwa tunauwezo wa kuishi nao, lakini kinga inaposhuka watu huzidiwa na kuumwa. Kila mtu huwa na seli za saratani, lakini kinga inaposhuka saratani huzaliwa. Kila mtu huwa hatiani kupata magonjwa ya umri, lakini afya inapokuwa mgogoro ndivyo hutokeza zaidi. Katika 10 bora ya magonjwwa yanayoua zaidi kuanzia mwaka 2021, Magonjwa ya moyo yanaongoza, yakiwemo ‘’IHD, HTN, Stroke’’, yapo magonjwa ya Kisukari ‘’DM-2’’, kuna magonjwa ya TB, kuna mashambulizi ya Mapafu, na COVID-19. Magonjwa haya yote unaweza yaelezea kama magonjwa yakutengenezwa na binadamu wenyewe. 

Ukianza na shida za moyo zote hutokana na mfumo wa maisha ya kutokunywa maji ya kutosha, kushamiri kwa vinywaji vya sukari za kisasa, kuwa na stress sana za maisha ya kisasa. Ukija mashambulizi ya mapafu, sababu kubwa ni Uvutaji wa sigara, kuishi katika maeneo yenye Hewa chafu, na Kuishiwa Kinga sana kama ambavyo TB imeonyesha. kila mtu huwa ana vimelea vya TB (Mycobacterium), kitendo cha ugonjwa huu kushamiri ni dalili kubwa kuwa, watu hawana kinga kabisa. Magonjwa ya Kisukari yanatokana na ulaji sana wa vyakula vya wanga, Pombe, na Shida zote za kihomoni. Ugonjwa wa COVID-19 ukifuatilia asilimia kubwa zaidi waliokufa ni watu wa Magharibi, ambao wao waliwekwa Quarantine wasipate Hewa ya kutosha na kukosa Mwanga, jambo ambalo lilichochea zaidi Kushamiri kwa kemikali sumu, huku wakipungukiwa Vitamin D ambayo huwa mstari wa mbele kuzisisimua seli za kinga ‘’T-Helper Cells’’.

Watu hawajui mengi sana kuhusiana na mashirika ya dawa, na hata dawa zenyewe. Kwanza hii Dunia haina Dawa nyingi kama wengi wanavyohisi, makundi ya madawa ni machache sana kuanzia Antibiotics kama Sulphonamides mpaka Penicillin ambazo ndizo zilikuwa dawa za kwanza kabisa. Madawa mengi zaidi huwa ni Uboreshwaji au ‘’Modifications’’ za dawa zilezile za miaka yote. Zama hizi asilimia kubwa ya madawa hutengenezwa sio katika dawa za antibiotics za kuua bakteria. Bali hutengenezwa toka dawa zinazoweza kuathiri chaneli kadhaa, na kemikali kadhaa katika mifumo ya seli ya mwili. Dawa hizi hutengenezwa zaidi na wataalamu wa Biolojia za Molekuli na Biokemia. Watu hawa wanaposikia ugonjwa wowote ule huwa na swali la kwanza kuwa, umepelekea nini Kupungua? Na unapowaambia mfano Collagen, basi wao kesho huja na Dawa na Dose yake ya kuongeza Collagen. Watu hawa sio wepesi wa kujiuliza kwanini Collagen ipungue? Na kwa mantiki hii, Dawa nyingi zimekuwa zikitibu Dalili sio chanzo. Kama nilivyosema awali, Mwili wote hufanya kazi kama kitu kimoja, unapoenda kuathiri chaneli yoyote ile, haitaathiriwa peke yake, lazima itaathiri na sehemu zingine, na hii ndiyo sababu dawa nyingi huwa na matokeo hasi ‘’Adverse Effects’’. Na nyingi huwa zinaathiri sana Ubongo. 

Hii ni kwa kuwa, Ubongo ndiyo huwa unaathiriwa zaidi balansi ya utendaji wa mwili inapoathiriwa. Haimaanishi Dawa hizi huwa hazisaidii, ila inamaanisha Dawa hizi huwa hazitibu tatizo kuu. Na kwa falsafa hii, watu wengi huwa wanaendelea kuwa wategemezi wa dawa hizi milele mpaka wanapokufa. Ni vigumu hata kupima kuwa kwa kiwango gani dawa hizi husaidia, hii ni kwa kuwa magonjwa mengi Sugu hutokea mwili unapokuwa umeshapoteza wenyewe uwezo wa kujisaidia kwa miaka yote mtu alipokuwa akiuathiri. Wagonjwa wengi wanaopelekwa hospitalini hupata nafuu kutokana na imani yao ‘’Placebo Effect’’, lakini sio Dawa wanazopewa, na hii ndiyo maana Toka Madawa haya yaanze kutumika hakujawahi kuwa na Ongezeko lolote lile katika Afya dhidi ya magonjwa haya yote Sugu. Msingi wa kuelewa afya na Kinga, huwa rahisi sana unapoelewa kwanini Binadamu Huzeeka hata Kufa. Stori ya Maji na mwanga ndiyo inaweza kulielezea hili vizuri zaidi. Katika sehemu nimetengeneza stori nzuri ya kuelewa kwanini watu wanazeeka.