Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MWANGA UNAVYOKUUA USIKU🔆💡❌

Madhara ya Taa Usiku, screen za simu, TV, na Cinema, ni makubwa kuliko madhara ya Vyakula vya kisasa na sukari

KISA KIDOGO CHA KUSHINDA NA MIANGA USIKU NA VITAMBI

Sayansi ya mionzi ya vifaa vya umeme, na kuchelewa kuamka

Summary

Mwanga wa taa, tv, simu wakati wa usiku huzuia homoni ya melatonin. Homoni hii huchuja sumu za mwili zote, na kusaidia mitochondria ijizalishe, izalishe nishati na kutozalisha sumu ‘’ROS’’. Unapokuwa sana katika mianga hii usiku, sumu hujaa, na mwili huchochea zaidi mafuta ili kujilinda. Kwa hiyo mafuta kwanza kabisa huwa ni namna ya mwili kujilinda. Pili, mitochondria zinapoathirika, sukari nyingi hubadilishwa kuelekea zaidi kuunda mafuta. Ukitaka kujua tatu mpaka kumi, soma chini.

Hii ni miongoni mwa biolojia ambayo watu wachache sana wanaweza kuielewa, natoa shukurani zangu kubwa sana kwa mtaalamu mkongwe wa Ubongo Dr. Jack kruse, kwa ufupi sana, viumbe ni matokeo ya asili yao, viumbe wametoka katika udongo na maji, na wanaishi kwa sababu ya hewa na mwanga. Ni muhimu sana kujali mfumo wako wa asili unaokushikilia. Watu wengi hupuuzia sana biolojia hii, sehemu ya mbele tutaangalia kiundani zaidi sayansi hii.

Kuhusiana na Mafuta ya miili ya viumbe, ni muhimu kutambua kuwa, mafuta ni tabaka pekee la kulinda kila kilicho hai. Unapoelekea katika ubongo, seli za ubongo huitaji kufunikwa na tabaka hili la mafuta, ambayo huitwa ‘’myelin’’, hata kila seli, huwa na ukuta ambao huwa umejaa mafuta. Mwili hutengeneza kiwango cha mafuta kulingana na sumu zinazouzunguka, popote pale panapokuwa na changamoto nyingi zaidi za kuudhuru mwili, mwili huongeza kiwango cha mafuta.

Kutanuka marazote hutokana na kuisha, kila kitu kinapokuwa kikiisha huwa kinatanuka, Kuanzia katika mifumo ya galaxy, nguo za watu, moyo tuliona unapoisha hutanuka, moyo unapozeeka hutanuka pia, hii ni sheria kubwa sana ya sayansi inayosema vitu huelekea marazote katika kuchoka. na katika kuchoka kani zinazoshikilia vitu hivi huishiwa nguvu na hivyo vitu huanza kutanuka vikijiachia. Kama ukiona maiti ya siku moja tu iliyoachwa huru utagundua maana ya kauli hii ya kutanuka, kadri vitu vinapokuwa na saizi ya wastani, maana yake huwa vinakuwa na nguvu kubwa zaidi. Kuna sheria nyingi sana za fizikia zinazofuata uhusiano huu, ikiwemo kani ya gravitation, kani ya chaji za umeme, kani ya usumaku, kani ya mvuto wa vitu elastic,n.k. 

Lengo ni hili, hata seli za mwili nazo hufuata sheria hizi, kadri ambavyo seli huwa zikiisha huwa zinazalisha mafuta mengi zaidi. Watu wengi wanene huwa na wastani wa matatizo mengi zaidi ya watu wa saizi ya wastani, penginepo hata zaidi ya watu wembamba. Huu unene huanzia katika seli zao, na katika seli zao stori huanzia katika kiwango cha mafuta. Na kiwango cha mafuta huanzia katika kiwango cha sumu.  kiwango kikubwa sana cha sumu kinatokana na watu kutozingatia utaratibu wao wa asili yao waliyotokana nayo.

Kiumbe yeyote aliyemzima amelala anapaswa kuamshwa asubuhi na mfumo wake wa homoni na ubongo, na anapoamka anapaswa Kwenda kufanya kazi, na hapa anahitaji kuwa na nishati ya kutosha ya kusukuma misuli yake. Matendo haya huitaji sana mfumo unaoitwa ‘’Hypothalamo-pituitary-adrenal axis’’, ambapo huwa unaenda sambamba na utendaji wa tezi ya pineal ‘’pineal gland’’, hii huusiana na mzunguko wa siku. Kitu pekee ambacho huratibu mzunguko wote huu, ni mipishano ya mianga ya asili katika namna za frequency, kutoka kubwa sana ya mwanga, mpaka hafifu sana ya giza, na kuendelea huku ikipishana kidogo kidogo kama ambavyo tezi na mifumo hii hufanya kazi.

Kazi kubwa sana za ubongo kipindi kiumbe anapolala huwa ni kuchuja sumu zote, figo pia hukusanya uchafu wote, kila kiungo wakati wa usiku huwa ni wakati wa usafi. Misuli yote huwa ime paralaizi ili kurekebisha vidonda, michubuko, kutoa sumu, na kujenga kinga ya mwili. Viumbe wanapolala miili yao huwa haina stress hata kidogo, maana mfumo wa stress wa ubongo wa ‘’sympathetic nervous system ‘’ huwa umezima kabisa, na homoni za stress kama adrenaline, na cortisol huwa chini kabisa. Na hapa ndipo hata kumbukumbu huboreshwa kipindi watu wanapokuwa wanalala katika hatua ya usingizi ya ‘’rapid eye movement’’, ambapo mtu huwa akiota. Usiku huambatana na giza kwa kuwa asili imeutengeneza ubongo usipate taarifa wakati wa usiku mfano kwa kuona, ili usizingatie, utulie sasa uweze kurelax, na hata hali ya hewa ya usiku huwa ni ya baridi, kutengeneza mazingira ya ‘’hibernation’’, yaani, mwili uweze kupooza mpaka utendaji wa seli, au metaboliki za mwili. 

Wakati wa usiku giza linapoingia husisimka mfumo wa protini wa tryptophan ambao huambatana na uzalishwaji wa homoni ya ‘’melatonin’’, ambayo hii ndiyo kama sabuni kuu ya ubongo ‘’major antioxidants’’, husafisha sana ubongo. pia huzalishwa sana serotonins, ambazo hizi hutuliza mood za akili, watu wengi wakati wa usiku akili zao huwa zimetulia sana, na hata viumbe wengi wakati huu huweza kufanya mapenzi kwa kuwa stress huwa chache sana zinazozuia mfumo wa parasympathetic nervous system, ambao ndiyo unahusiana na kujaa kwa damu katika via vya uzazi, na mara nyingi nyakati hizi, tryptophans huzalisha pia homoni za endorphins, ambazo hutengeneza hisia za raha kabla ya kulala. Asili ipo vizuri sana katika kusapoti maisha, sifa hizi zote ziende kwa Mungu muumbaji wa mbingu na nchi.

Chanzo cha Tatizo

Usasa mwingi sana ulioanza karne ya kumi na tisa, ambapo kazi kubwa ya engineer Nicola Tesla ya taa za AC, au umeme wa kisasa ulipofikia jamii za watu, ijapokuwa awali hakukuwa na shida sana kutokana na matumizi ya taa za mwanga hafifu-mwekundu, baadaye matumizi ya taa zenye nguvu za mwanga mkali, wa frequency hizi za kawaida, kama za mchana za -Blue zilishamiri sana. 

Mianga unayotumia katika simu yako, katika gari lako, nyumbani mwako, na maeneo kadha wa kadha hata hospitalini, kipindi cha upasuaji, na mashine nyingi za kuonea, ndiyo mwanga ninaouzungumzia kuwa ni hatari sana.

Mwanga huu kwanza kabisa ni tofauti na wengi wanavyouhisia, wengi wanahisi mwanga huu hauwezi kupenya katika vichwa, na pili, wengi wanahisi mwanga huu hauna madhara ya kuendelea zaidi ukiachana na tu na kutua katika jicho. Lakini ajabu ni kuwa, mianga hii kama ambavyo unapokuwa ukiangalia mpira, au filamu wakati wa usiku, au ukisoma kompyuta wakati wa usiku. Mianga hii huingia moja kwa moja mpaka kwenye jicho, mingine hupenya katika Ngozi, na hii mianga husisimua maelfu ya sensa za mwanga mfano zinazoitwa ‘’melanopsin’’, ambazo zimetapakaa kutoka kwenye ubongo, mpaka kwenye utumbo, na huko huuambia mwili kuwa upo katika mazingira sawa kabisa na mazingira ya mchana. Yaani, mazingira ya stress, mazingira ya kuzingatia, mazingira ya kutohitaji biolojia yote ile niliyoielezea ya umuhimu wa usiku. Watumiaji wa taa hizi, Biolojia yao yote hubadilika.

Watu wengi hawaelewi kwanini madaktari wengi hasa wa shift za usiku wanazidi kuwa vibonge, kama ilivyo kwa manesi, kama ilivyo kwa madereva pia. Usipolielewa hili unaweza kuhisi kuwa watu hawa hawazingatii afya, lakini ukweli ni kuwa. Kama ambavyo wakati wa usiku watu wanapolala huwa hawahisi tena hamu ya kula. Hii ni kutokana na kuwa, mfumo wao wa hisia ya kula huwa chini sana. Lakini mianga hii ya blue huathiri mifumo hii, hasa mfumo unaoitwa ‘’leptin melanocortical pathway’’, ambapo mfumo huu huongoza mfumo wa homoni wa kuridhika, na kubalansi kiwango cha chakula mwilini. Madhara yake watu huwa walaji sana, lakini pia hata kiwango cha mafuta ambayo huwa yanaundwa huwa ni kikubwa sana, sababu zikiwa zifuatazo.

Mwanga na Mitochondria

Mwanga wa giza ndiyo swichi kuu ya kuwasha mfumo wa ubongo wa kusafisha uchafu na sumu zote, kwa kuchochea uzalishaji wa homoni ya melatonin. Homoni ya melatonin ndiyo huusika moja kwa moja na kurekebisha makosa yote yanayofanyika katika chembechembe za nishati za mwili, yaani Mitochondria. Melatonin unaweza iita kama ‘’major brain anti-oxidant’’. Inapotokea mwili, au ubongo upo katika mwanga wa mchana, hasa kwa matumizi ya balbu za taa za mwanga mkali mpaka usiku, mfano, watu wanapokuwa wanaangalia mpira, au wanapokuwa wakichati kwenye simu zao, au wanapokuwa wanaangalia filamu, au wanapokuwa wakisoma usiku. Frequency za mianga ya blue wanayoitumia hupelekea ubongo kutozalisha homoni hii ya melatonin.

Na sababu ya kutozalisha ni kuwa, mwanga wa blue, au huu wa kawaida wa hivi vifaa na taa, huwa ukichochea stress wakati wote. Yaani, unachochea uzalishwaji wa homoni ya ‘adrenaline’’, na kwa wakati wa usiku unapowashwa, huchochea uzalishwaji wa homoni ya stress ‘’cortisol’’. Na kumbuka watu hupenda kuutumia sana wakati wa usiku kwa kuwa huwa unachochea sana uzalishwaji wa homoni za ‘’dopamine’’, ambapo hizi hutengeneza hisia za uzingatiaji na motisha. Na sasa basi, homoni zote zinazochochea stress huathiri utendaji wa mfumo wa protini wa tryptophan, ambayo ndiyo huusika pia na uzalishwaji wa homoni ya melatonin zaidi kwa usiku, na serotonin kwa mchana (serotonin ndiyo hubadilishwa kuunda melatonin), homoni ya melatonin moja ya kazi yake kubwa kabisa huwa ni kusafisha sumu za ubongo, na kurekebisha makosa ya Mitochondria, ambayo ndiyo kiungo kinachozalisha kemikali sumu nyingi sana, ‘’ free radicalss’’. 

Mitochondria huzalisha sumu nyingi za free radicals kwa kuwa yenyewe ndiyo huusiana na uzalishaji wa chembechembe za elekroni, na sasa inapopata changamoto, hupelekea hizi elektroni kuzalisha kemikali sumu nyingi sana. Ni jukumu kubwa la melatonin kuhakikisha inarekebisha makosa ya mitochondria yenyewe, na pili inafuta uchafu wote uliotokana na kemikali hizi sumu. Melatonin pia huchochea kuzalisha kemikali zingine kama (superoxide dismutase, glutathione peroxidase, catalase) za kusafisha chembechembe hatari za free radicals kama (hydroxyl radicals, superoxide anions, n.k). mtu anapokuwa macho usiku katika mazingira ya mianga ya kisasa, huchochea stress kama ilivyo kawaida, na stress hizo husisimua chembechembe zinazoitwa IDO ‘’indoleamine 2,3-dioxygenase’’ ambazo hizi huzuia uzalishaji wa melatonin, na kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyingine inayoitwa ‘’kynurenine’’. Hii hupelekea kuzalishwa kwa chembechembe za ‘’NAD’’, na chembechembe inayoitwa ‘’Quinolinic acid’’. Chembechembe ya NAD inafahamika kutumika katika kuzalisha chembechembe za kubeba nishati, na Quinolinic acid inahusiana na matatizo mengi sana ya ubongo. hizi zote ni lugha ya kuwa ubongo upo katika mazingira ya hatari.

Ajabu zaidi ni kuwa, kiwango kikubwa cha chembechembe zilezile za awali za ‘’IL-1, IL-6, na TNF-α”” humchochea sana chembechembe IDO ili kuzuia uzalishwaji wa melatonin, na kuchochea uzalishwaji wa kynurenine. Hii inaweza kukwambia nini? Giza na maji ni vitu vyenye umuhimu sana katika kuondokana na madhara ya uvimbe, na shida za ubongo. unapokosa wakati wa giza wa kutosha, unaongeza kiwango cha stress, unaongeza kiwango cha sumu taka za mwili, na mwili unaanza kusisimka kwa kujihami kwa kulinda kuta zake kwa uvimbe. Na hapo ndipo tunapopata chembechembe hizo za kinga za uvimbe, na mwili kujirekebisha. 

Tryptophan kutokana na stress za kukosa mwanga hubadilishwa kupitia chaneli hiyo ya kynurenine, na kuzalisha kemikali mbili, picolinic acid, na quinolinic acid. Kemikali ya pili huchochea uvimbe, na ni sumu kwa namna husisimua sana mageti ya ubongo yanayoitwa ‘’NMDA’’ yanayohusiana na kumbukumbu, kujifunza, na kukua kwa ubongo kimaarifa. Na huu ndiyo mwanzo wa magonjwa mengi kama ya kupoteza kumbukumbu, kuishiwa uwezo wa kutawala misuli, kukosa balansi ya homoni za kuongoza utendaji wa ubongo, yaani magonjwa kama ‘’Parkison disease, Alzheimer’s disease, Schizophrenia, Huntington’s, na amyotrophic lateral sclerosis, na hata cancer’’. Upande wa picolinic acid, yenyewe huwa na kazi ya kuulinda ubongo usivimbe. 

Kama unaweza kuelewa ubongo unachosema pale unapokuwa na mwanga wa kisasa wakati wa usiku kutokana na tryptophan metabolism ni kwamba, ‘’mfumo wa utoaji taka umezuiwa, mfumo wa uzalishaji nishati umezuiwa, na sasa hebu tuongeze vizalisha nishati, tutengeneze mazingira ya kutoshambuliwa na sumu zitakazoanza kujaa, na mwisho tujilinde tusidhulike sana’’. Kutokana na hili tatizo, basi ndipo ubongo husisimka hata kuepelekea matatizo mengine kama ilivyokuwa kwa mifumo mingine.

Mwanga na Kujaa Mafuta

Katika Mitochondria huwa kuna protini zinaitwa ‘’UCP, au Uncoupling Proteins’’. Hizi huwa na kazi moja kubwa sana, zenyewe wakati wa usiku huwa zinapunguza kiwango cha chembechembe za Proton zinazoingia ndani ya mitochondria, na kwa kufanya hivi huzuia uzalishaji wa chembechembe za nishati za ATP, na madhara yake nishati yote hubadilishwa na kutengeneza Joto. Kiwango hiki cha Joto husaidia sana katika kuvunja vunja mafuta yaliyo katika seli, na hata kuzalisha nishati katika mazingira ya baridi ‘’cold thermiogenesis’’. Miongoni mwa makosa makubwa ya kukaa usiku na mianga ya taa za kisasa ni kuwa, huwa inaathiri protini hawa wa ‘’UCP. Madhara ya kuwaathiri hawa protini huwa ni kupelekea kujaa sana kwa mafuta katika mwili, hii ni kwa kuwa, mfumo wa kuvunja haya mafuta umeshaathiriwa.

Na sababu ya kwanini hizi protini zinaathiriwa huanzia kulekule ya kuwa, mwanga wa blue huathiri utendaji wa homoni ya kuridhika, ya Leptin. Unapokula mafuta siku zote katika chakula, huwa mafuta yakisisimua homoni hii ya leptin na kukufanya usijisikie hamu ya kula zaidi. Mwanga wa blue huathiri kabisa uwezo huu wa leptin wa kutuliza hamu ya kula, na madhara yake mtu hula na hula zaidi, hii ni sababu ambayo hupelekea watu kuwa wanene sana, au kuwa na cholesterols sana. Lakini pia, leptin huchochea mfumo wa ubongo unaoitwa ‘’Leptin melanocortical pathway’’, ambao mfumo huu ndiyo husisimua sasa wale ‘’UCP’’, na kwa mantiki hii, chaneli moja, huchochea chaneli nyingine, lakini zote huishia kujaa kwa mafuta.