Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

KATAA SIGARA & SHISHA🚫🚭❓

Shisha, sigara, na Moshi wa wavutaji wa bidhaa hizi una hatari kubwa sana Kwa wavutaji kiafya.

UVUTAJI WA SIGARA NA SHISHA


Sigara ‘’cigarrete’’ ambayo hutokana na mmea wa tobacco, Ni miongoni mwa vitu ambavyo pengine watu wote hujua kuwa vina madhara. Kwenye makasha ya sigara kuna onyo kuwa sigara ni hatari. Lakini cha ajabu siku hizi kuna aina mpya za uvutaji wa mfano wa bidhaa hizi unaoitwa '’shisha’’. Wengi hawajui namna vitu hivi vilivyo vya raha na kusisimua mpaka watakapo jaribu. Lakini sifa kubwa ni zile zile, kemikali hizi haziishii tu kuusisimua ubongo, huanza na kuua ubongo,mwili, na akili. 

SAYANSI YA UTENDAJI WA SIGARA

Sigara ina kemikali inayoitwa ‘’Nicotine’’. Kemikali hii mtumiaji anapoivuta huingia mwilini na kisha kwenye damu. Madhara ya uvutaji wa sigara yametofautiana kulingana na sehemu ambapo moshi na kemikali za sigara hufika. 

SIGARA KWENYE UBONGO

Baada ya sigara kuvutwa na kemikali za sumu za nicotine kuingia kwenye damu ambayo inaelekea kwenye ubongo. Ikishafika kwenye ubongo, mambo yafuatayo hutokea; 

Kemikali ya Nicotine ikishafika kwenye ubongo hukutana na receptors za ubongo maalumu kabisa, ambazo huitwa ‘’Alpha-4-Beta2’’. Receptors hizi kwa kawaida hushughulika na maswala ya kutawala utambuzi, hisia za maumivu, motivation, mood, na kusisimua seli za ubongo. Sasa basi, ukivuta sigara, nicotine ikishafika kwenye ubongo , tena hasa ubongo wa shina la kati ‘’midbrain’’, huyashikilia mageti na kuyang’ang’ania yawe wazi, na madhara yake ni kuwa, chaji nyingi za sodium,calcium, na potassium huingia ndani ya receptors za (α2β4 nicotinic receptors), na kufanya ndani kuwe na chaji Chanya zaidi, na seli ya ubongo husisimka sana. Na huyu mvutaji hujisikia raha sana, kulingana na kazi za hii receptor nilizozisema pale juu.

Mageti haya huambatana na uzalishaji wa homoni za dopamine, ambazo huongeza zaidi msisimko wa mvutaji.

Lakini nicotine huwa haikai kwa muda mrefu sana katika ubongo, huondolewa. Na swala hili hufanya kushuke kwa kiwango cha homoni ya Dopamine, na hiki hasa ndicho ambacho humfanya mvutaji ajisikie karaha sana. Na hizi karaha humsukuma kupiga pafu zaidi, au kutafuta sigara zaidi.

SIGARA NDANI YA MWILI KWA UJUMLA

Moshi wa sigara una zaidi ya kemikali elfu tano. Na ndani ya hizi kemikali, kumejawa na sumu nyingi sana. Mfano, kuna kemikali ambazo huitwa TAR au ‘’total aerosol residues’’. hizi husababisha kukakamaa kwa fizi za midomo ya wavutaji, na huunda tabaka jeusi ‘’resins’’,pia huathiri meno kwa nje na ndani.

Zinapopita katika tishu za mwili, husababisha madhara katika mishipa ya fahamu. Huua zile terminals za neva zinazotumika kuhisi ambazo huitwa ‘’nerve endings’’. Huathiri mapafu kwa kuua kabisa seli katika kuta za mapafu, na huua vinywele nywele vya muhimu sana katika mapafu vinavyoitwa ‘’cilia’’. hewa sumu ya ‘’carbon monoxide’’ kwenye mapafu huathiri seli za kubeba oksijeni ‘’hemoglobin’’ kwa kujaa gesi ya sumu badala ya oksijeni.

Nicotine husababisha mishipa ya damu kusinyaa zaidi ndani ya mwili ‘’vasoconstriction’’ kwa lengo la kuzuia isijazwe na kemikali hizi sumu, hii husababisha kujiminya kwa mishipa ya damu hata kuathiri seli za kuganda ‘’blood platelets’’.

Husababisha mshtuko wa moyo ‘’heart attack’’ na stroke. Kemikali nyingi sana huathiri matendo ya kijenetikia kupitia kuchochea uharibifu katika DNA, au  ‘’mutations’’. hii hutokea kwa kuwa siku zote Nicotine huathiri uwezo wa kujirekebisha wa DNA, na huu ndiyo mwanzo wa utokeaji wa saratani, na matatizo ya nguvu za kiume.

Maisha ni Uchaguzi...