Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

IMANI YA KULA MIMEA TU SI SAYANSI❌

Nyuma ya vegetarianism vs carnivorism Sio Afya, Wala Sayansi, ni Msukumo wa BigPharma

Siri ya 08-03 (Part 4)

Janga la mwisho ambalo pia limeiathiri sana dunia linalotokana na falsafa za watu wa mashirika ya vyakula na madawa, ni uchochewaji wa nadharia kuwa vyakula bora zaidi vya kuliwa ni vya mimea tu, na watu wengi kwa kuwa na mitazamo ya ubora wa mbogamboga kuliko nyama. Wamekimbilia nadharia hizo. Lakini kwa ndani sana, nadharia hizi hazijalenga mbogamboga kama watu hawa wanavyochochea. 

Ni kweli kuwa ulaji wa nyama sio bora sana kutokana na msukumo wake mkubwa sana wa hamu unaopelekea ulaji uliokithiri. pia nyama huwa na mabaki mengi sana ya madawa, na hivyo kuchochea sana usugu wa madawa, na hata sababu za ubinadamu, si vyema kuua wanyama wenzetu. Sababu hizi zote huchochewa sana lakini uhalisia wake ni mdogo sana katika afya za watu. Kwanza idadi ndogo sana ya watu huwa wanamudu kula nyama katika familia za leo, hasa kwa nchi zinazoendelea. Nakumbuka wengi wetu tulikuwa tukila nyama X-mass mpaka Eid inapofika, na ulaji sana huwa ni wa Vipande vitatu. Lakini wasomi wasioelewa Vita nyuma ya sakata hili, huwafundisha watu kuwa shida zote za Moyo zinatokana na ulaji wa nyama.

Ukweli ni kuwa, Mashirika ya Madawa yalichochea nadharia ya mwaka 1823 ya kuwa Mafuta yaliyopo katika wanyama ndiyo huchochea shida zote za moyo. Vitabu vyote vya afya huandikwa kuwa mafuta ya wanyama ‘’SFAs’’ ndiyo hupelekea kushamiri kwa Cholesterols. Na hivyo kufanya Cholesterols kuonekana kama Lusifa katika Vyakula vya watu. Ukweli ni kuwa, Asilimia karibia 90% ya Cholesterols zote zinazoshamiri katika mishipa ya damu ‘’Atherosclerosis’’, huwekwa na mwili wenyewe katika tishu za mwili. Kwa lengo la kujilinda kutokana na stress zilizoshamiri za kujaa kwa kemikali sumu, vyakula vya kisasa, vya wanga, mafuta ya mbegu, na hasa upungufu wa maji. 

Na hii ndiyo sababu mafuta haya hushamiri zaidi katika mishipa ya artery ambayo huwa na presha kubwa zaidi ya stress. Kiwango cha Protini kinachobeba mafuta haya kinachoitwa ‘’LDL’’ huwa kinamaanisha, Mwili unaenda kuziba michubuko inayotokana na damu kuwa nzito sana na kujaa kemikali sumu zinazochubua tishu na mwili. LDL hutengeneza kuta ili kulinda tishu za mwili zisiathiriwe. Mtu anaporejea Afya yake nzuri mfano kwa kunywa maji vizuri, HDL huongezeka ambazo hurudisha cholesterols zote kwenye Ini na kuzichoma. Kama mtu hatabadilisha mtindo wake wa maisha, LDL ambazo huwa nyepesi na kubwa, hujaa katika mishipa ya damu, na kufanya tundu la mshipa wa damu kuwa dogo, na kama mtu atavuta sigara, atatumia mafuta ya mbegu, atashinda kwenye mianga ya kisasa, hizi zote zitachochea kemikali sumu ‘’Free radicals’’, ambazo zitatengeneza Vibonge ‘’Plaques’’, ambazo ndizo huenda ku block mishipa ya damu na kupelekea Stroke.

Stori hii ina lengo moja kubwa, Mfumo wote wa Madawa umejikita kuuza Dawa zinazoitwa ‘’Statins’’, ambazo zimelenga kushusha Cholesterols. Na kwa kufanya hivyo maelfu ya watu wenye shida za Presha hawajawahi kupata ahueni. Na Mashirika ya dawa yamezidi kuuza falsafa hasi kuwa mafuta ya wanyama, na Nyama ni chanzo kikubwa cha shida za watu. Huku ukweli ukiwa ni Wanga zinazosisimua sana wanazoziuza, Mafuta ya mbegu wanayoyachochea, Madawa wanayoyauza, na Ulaji wanaouchochea ambao hauna kambakamba kama katika Mikate, Soda, Sembe, Biskuti, n.k. hivi ndivyo vyanzo vikuu vya magonjwa. 

Mafuta ya mbegu yana mageti ‘’Unsaturated Bonds’’ ambayo hupokea elektroni toka katika Mitochondria na kuunda kemikali sumu, lakini hakuna atakayekufundisha hilo. Ila utaambiwa mafuta ya wanyama ndiyo huganda katika mishipa ya damu, jambo ambalo halina mantiki kwa kuwa mafuta haya huvunjika kirahisi sana, na jambo la msingi sana ni kuwa, Cholesterols ndiyo msingi wa kutengeneza homoni zingine zote za mwili kama tulivyoona kwa namna huungana na Vitamin A, na kutengeneza Pregnenolone, inayounda homoni za uzazi kama Testosterone, Estrogens, Progesterone, DHEA, na mpaka Vitamin D. watu wengi wanaupungufu wa mafuta haya kutokana na mifumo ya stress ambayo hubadili Cholesterol yote na kuunda homoni ya stress Cortisol, katika kitendo kinachoitwa Pregnenolone steal syndrome. Mwili unahitaji sana chembechembe za DHA ambazo ndizo huunda asilimia kubwa zaidi ya Ubongo, chembechembe hizi hakuna namna ya kuzipata zaidi ya Kula samaki.

Mashirika ya madawa na Vyakula hayapati faida kwa ulaji wa nyama, kwa kuwa wafugaji wengi huwa watu wa kawaida, tofauti na viwanda kama vya mikate, soda, biskuti, juisi, n.k. ukweli ni kuwa, maisha ya kuishi kwa kula mimea tu ‘’Vegetarianism’’ ni mzuri zaidi ya ulaji wa nyama, lakini una gharama kubwa sana, na unahitaji maarifa makubwa sana. Na ndiyo maana hata Yesu anapopaa alikula Samaki. Wenda ni kwa kuwa alijua ulaji wa nyama nyingine utakuwa hatari zaidi, maana wanyama wengi siku hizi hufugwa kwa kulishwa Pumba, kama ilivyo kwa kuku wa kisasa ‘’Broiler’’, hata pia Wanyama wengi hunenepeshwa kwa pumba hizi.

Pumba zote huwapelekea wanyama hawa kujawa na mafuta yasiyohitajika mwilini kwa kiwango kikubwa ya ‘’Omega-6’’, lakini mbaya zaidi, Kuku wengi wa siku hizi huwa wameboreshwa kijenetikia kwa ‘’Selective breeding’’, na hivyo huwa hawana kinga kabisa. Madhara yake ni kuwa, huishi kwa kutegemea madawa ya Vets. Madawa haya kwa kuku wa wiki 4-6, au Maziwa ya Ng’ombe wa kisasa huua Mfumo mzima wa Bakteria zaidi ya Trilioni 37+ waliomo tumboni, huua mfumo wa kinga, na binafsi nahisi ni Laana kula kifaranga wa Wiki 4. Tafiti zinaonyesha kuku wa kisasa wapo katika maumivu muda wote, wanateseka na ndiyo maana ukiwapa dawa za maumivu kama ‘’Aspirin’’ utawaona wakichangamka. Kuku hawa misuli yao huwa mikubwa kuliko mifupa yao, na wanapokimbia au ruka huchanika, na ndiyo maana huwa chini muda wote wakitulia kwa maumivu. 

Jambo pekee ninaloshauri ni watu wale wanyama wa kienyeji, waliofugwa bila madawa, lakini falsafa za kula mbogamboga tu, kama uchumi wako hauwezi mudu supplements za upungufu wa Omega-3 Fatty acids ambazo huwezi zipata zote tatu zaidi ya kula samaki tu, hata na protini zingine kama B12, au huwezi kula mboga za majani za aina mbalimbali kila siku bila kuwa na uraibu wa wanga, nahisi kama huwezi, usitumie uzoefu wa kuacha kula tayari ukiwa mtu mzima ukalazimisha na kwa watoto wadogo, hata ukapelekea mtoto akawa na shida za ajabu za ubongo unaohitaji zaidi mafuta ya samaki. 

Historia zote za hamasa ya ulaji wa mimea tu katika sayansi zilianzia kwa John Harvey Kellog, ambaye alikuzwa katika falsafa za Waadventista wasabato, na alikuwa mgunduzi wa mbinu kadhaa za ulaji wa wanga zaidi, katika miongoni mwa ‘’Sanitarium zake’’, lakini ni kosa kuamini kuwa Mr Harvey alikuwa sahihi kwa asilimia 100%, hasa ukilinganisha na kuwa sayansi ya afya ilikuwa chini kidogo kwa wakati ule, na pia alikuwa na mitazamo iliyopitiliza ‘’Extremism’’ kama kutumia ‘’weak acids’’ kuwakeketa mabinti wasiwe na mihemko sana, au watu wawe wanatafuna mara nyingi sana ilikuzuia magonjwa, kiufupi alikuja kuwa kinyume hata na Nabii Ellen G White aliyemuongoza hata akawa Daktari.

Kwanini unapaswa kutopuuza nyama?

Rejea sehemu ya kwanza# https://drbrightonshoo.blogspot.com/2026/01/ule-au-usile-nyamavegan-vs-carnivore.html