Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

ULE AU USILE NYAMA❓VEGAN VS CARNIVORE PART 1

Ule nyama au usile ni matokeo ya Maarifa ya kina kuliko hisia ktk kutambua msingi wa afya, lishe, na magonjwa.hata hivyo, bado adui mkuu siyo chakula#

KABLA YA KUANZA TAMBUA HAYA

Watu wengi hawaathiriwi Kwa ulaji wa nyama, idadi ya watu wanaokidhi upatikanaji wa nyama katika Milo yao ni ndogo sana. sababu kubwa zaidi ya shida za wengi zinazowamaliza zinatokana na ulaji wa Wanga, mafuta ya Mbegu, na kubwa zaidi mfumo wa Maisha unaowaweka kwenye Mwanga Wakati wa Usiku; na kuuwawa Kwa sumu za mionzi, na Sumu za kemikali za bidhaa za kisasa.

Asilimia kubwa ya watu wanaokidhi upatikanaji wa nyama bado wengi hula kiasi kidogo sana kama kinachoshauriwa, kisichozidi Nusu kilo Kwa wiki, lakini ajabu ni kuwa; wengi wao bado hawapati nyama zenye ubora. Wengi hupata nyama zinazowasisimua tu, lkn zilizojaa kemikali Sumu za madawa, wanyama waliofugwa ndani wakilishwa Wanga, na hula nyama zilizoandaliwa Kwa mafuta mengi ya Mbegu 'PUFA's" ambayo huwa na madhara makubwa sana mwilini.

Tabaka la juu la watu wanaokidhi kula nyama Kila siku, wengi wao hawanufaiki na nyama Kwa kuwa; wengi wao hula nyama za makopo zilizojaa kemikali Sumu kama Nitrites zenye matatizo maelfu ktk mfumo wa damu, hula pia wanyama wa kisasa hasa Kuku kama Broiler ambao hufugwa Kwa pumba na madawa, hivyo hawafaidiki ila hudhurika zaidi, na mwisho; wengi wao hupenda nyama za kukaanga zilizojaa mafuta Sumu ya Mbegu yakikaangwa, na hula sana nyama wakichanganya na Vyakula vingine visivyo na faida kiafya kama viazi vya kukaangwa, pombe, vinywaji baridi sana, na Wanga zilizokobolewa.

Ni ngumu Kwa mtu anayeishi mijini kupata nyama yenye ubora. Ni ngumu Kwa mtu aliye mijini kupata wanyama wanaofugwa kienyeji. Wanaokula nyama mijini wanakula madawa "Antimicrobials", na mafuta hatari mengi ya omega 6 yanayotokana na Pumba wanazolishwa wanyama wanaofugwa mijini, au wanaonenepeshwa.


KIFALSAFA KUHUSU NYAMA

Ulaji wa nyama ni ishara ya Neema ya Mungu juu ya Mwanadamu ambaye hajiwezi Tena kujimudu kivirutubisho na kimazingira. Wanyama hawakuwa chaguo la awali ki Vyakula, Wala Nyama Sio Chakula. Wanyama ni Kafara kimavazi kama Nguo Kwa ngozi zao na tabia zao. Ni Kafara Kivirutubisho ambavyo Mimea haiwezi kamilisha vyote Tena kirahisi kama kupitia misuli yao. Kiroho kama Damu zao ambayo ni ishara ya Ukombozi kupitia damu ya Kristo Yesu. 

Ulaji wa nyama Sio kiburudisho, na ndiyo maana Tutaona hata nyama Sio tamu isipobadilishwa au pikwa. Uraibu katika ulaji wa nyama ni ishara ya kutoelewa Siri nyuma ya nyama. Kuhisi ulaji wa nyama ni Dhambi ni matokeo ya kutoelewa biolojia ya umuhimu wa nyama, na hata Kwanini Baada ya kufufuka Yesu alikula samaki, na Sio wanyama waliobadilishwa kijenetikia na kufugwa kisasa toka zamani kama Nguruwe.

Msingi wote wa ubora wa nyama kivirutubisho ni uwezo mkubwa wa Wanyama kula Mimea mingi sana ambayo Binadamu hawawezi kuila kutokana na kupungukiwa vimeng'enyaji, hasa vya Cellulose. Wanyama hula aina nyingi sana za Mimea na madini, Binadamu wanapokula wanyama hunufaika Kwa kupata virutubisho vya Mimea ambavyo wasingeweza vipata wenyewe, ila Kwa Neema mithili ya damu ya mwanakondoo, Kwa kula nyama watu hupata hata madini ya Cobalt ktk Vitamin B12 ambayo wasingeweza yapata, au mafuta ya Algae na DHA ambayo bila samaki wasingeyapata..Kwa wengine Kila uuaji ni ukatili, hoja ambayo ni sawa na kusema Simba wote hata wa Yuda ni washetani ilihali bila wao hakuna nyasi, Wala Oksijeni isingesalia Kwa uhai wa Dunia! 

Msingi wa somo hili ni kujifunza kiasi ndiyo nguzo ya Maarifa, Sio hisia zilizopelekea hata shida ya wazazi baadhi kuwapa watoto wao maziwa ya soya badala ya maziwa ya Wanyama na kupelekea shida za Ubongo haijawahi onekana.

NYAMA


Nyama ni tishu laini aidha msuli au mafuta ya mnyama inayotumika kama chakula. Mtu akisema nyama ni misuli ya Wanyama wenzetu waliohalalishwa kuuwawa na kuliwa ni sahihi pia. Wapo Wanyama ambao huchinjwa, na pia wapo ambao huwa hawaliwi. Wanyama wote wasioliwa, huwa hawaliwi sio kwa sababu kuwa nyama yao haiwezi kulika, bali kwasababu za mitazamo ya kijamii, au miiko ya kijamii kadha wa kadha. 

HISTORIA YA ULAJI WA NYAMA

Hakuna chanzo maalumu kabisa cha kupata historia ya ulaji wa nyama, ila inaonekana kuwa ulaji wa nyama kwa historia kutoka katika biblia ulianza hata kabla ya gharika ya Nuhu, yaani ‘’antedeluvian’’. Historia hii haijaweka wazi kabisa kuwa nini hasa kilikuwa chanzo cha ulaji, lakini maagizo ya kwanza kabisa ya Mungu yanaonekana kuwa yaliwaagiza Wanyama wote kula majani, hata wale wanaokula nyama leo ‘’carnivores’’.  

Upande wa "secular mainstream"huamini kuwa ulaji wa nyama kwa binadamu ulikuwa toka maendeleo yake ya awali kabisa kutoka katika jamii za nyani. Hawa husema binadamu ‘’Homo erectus’’kikubwa alichokifanya ni kuja na ugunduzi wa moto katika zama za mwanzo za mawe ‘’early stone age’’ karibia miaka milioni mbili iliyopita. Hakuna sababu ya kuwaamini hawa watu ambao hawana hata Ushahidi wa aidha muda, wala mabadiliko ya mtu nyani wao.

Mungu hakuumba kiumbe asiye na akili hata ya kugundua moto na ndiyo maana sadaka za Watoto wa kwanza wa Adamu zilikuwa za kuteketeza. Hii inamaanisha tayari walikuwa na akili na moto walikuwa nao wakuteketezea.

Nyama ziliendelea kuliwa hata baada ya gharika ya nuhu, au baada ya miaka elfu mbili. Kipindi Mungu anamuagiza Nuhu kuchukua Wanyama na kuwaingiza kwenye Safina, alimwambia kuwa achukue Wanyama safi saba, na wasio safi Wanyama wawili. Hii inamaanisha tayari walikuwa wana maarifa ya kujua Wanyama wapi wa kuliwa, na wapi sio wa kuliwa. hii namna ya maarifa ya awali inashangaza kwa namna Fulani, na ndiyo maana utakuta kaini akiulizwa kwanini amemuua ndugu yake Ijapokuwa amri kumi za Mungu zilikuwa bado hazijatolewa! 

Sheria zote zilikuwa tayari zikifahamika na wana Israeli wanapotoka Misri ndipo unapoona kwa mara ya kwanza Musa akitoa sheria za ulaji wa nyama kwa mara nyingine, kwa staili ya uandishi kupitia maandishi. Sheria hizi za ulaji wa Wanyama zimeendelea hata katika kipindi cha Yesu na mitume, na pengine mtazamo wa mwisho kabisa wa namna ya ulaji wa nyama unaweza kuuona kwa Petro katika kitabu cha matendo ya mitume, ambapo anapewa kila kitu ale, na yeye anasema ‘’sijawahi kamwe kula kiumbe kilicho najisi au kichafu’’. Na huo ndiyo utaratibu wa ulaji wa nyama katika historia nzima ya biblia.

Upande wa pili unaweza kula chochote, hakuna mipaka ya ulaji. Mipaka ni mitazamo yako tu. Hakuna mnyama mchafu au najisi, wala hakuna sababu za kuacha kula chochote. 

Biblia imeandika nyakati za mwisho kutakuwa na ongezeko la maarifa, na hebu tutumie maarifa haya sasa kuona je nini maana ya nyama hasa na ulaji wake.

KWANINI TUNAKULA NYAMA?

Tunakula nyama kwa sababu ni chakula!!! Huo ni uongo mkubwa kabisa, chakula sio msuli wa mnyama wa mwenzako. Sifa kubwa kabisa za chakula ni hizi

kinatakiwa kiwe kinahakikisha uhai au kusaidia kuishi. Hii inaweza kuwa aidha kupitia kutoa nishati, au kusaidia matendo ya kibiolojia ya mwili . Nyama inaua Maisha. ili ule nyama maana yake mnyama anapaswa kufa, kwa hiyo nyama sio chakula, nyama ni uuaji. Kauli sahihi ya wanyama Wala Nyama ni Wauaji "Predators"

Kinapaswa kuhusisha uhusiano mzuri miongoni mwa viumbe hai na visivyo hai. Ukila embe utapata nishati lakini hautakula kokwa. Ambalo litakuwa msaada kwa embe kusambaza mbegu zake. Embe lililoiva hufurahia kuchumwa na ndiyo maana huanguka lenyewe, au kukuvutia tokea mbali, lakini nyama sivyo hivyo. Hakuna wakati unaotia huruma kama dakika za mwisho za mnyama anavyoona kuwa anaenda kuchinjwa, Wanyama hulia sana na hujuta kwa kuwepo duniani.

Chakula kinapaswa kuwa na muunganiko wa tofauti na wa kiumbe mlaji. Hii mimi nimeiita ‘’complimentary relationship’’, mfano, unapokula mhogo una virutubisho ambavyo vina chembechembe ambazo zinameng’enywa vizuri kabisa na vimeng’enyaji vilivyo ndani ya viumbe walaji. Lakini unapokula msuli wa mguu wa ng’ombe, ule msuli na msuli wako unafanana kabisa, yaani tofauti ni chache sana. tena kama tu tofauti zilizopo kati ya msuli wa huyohuyo mnyama kama ng’ombe na msuli wa mbuzi, au farasi. 

kinapaswa kuwa kitamu kwa asili. Nyama sio tamu kwa asili, inahitaji kubadilishwa kikemikali kwa kupikwa , na ndani ya nyama tutaona mbele kidogo namna matendo ya kikemikali ‘’mailard reaction’’ yanavyoibadilisha hata kuwa na ladha ya mvuto. Unaweza kula boga, au maharagwe, kwa kuyachemsha ili kuyalainisha, unaweza kula mchicha vizuri kwa kuulainisha , unaweza kula pera au tikiti maji bichi. Lakini nyama mbichi haiwezi kabisa kukaa mdomoni kama ambavyo njegele mbichi ingekaa. Unaweza vumilia kuweka maharagwe mabichi mdomoni, ila huwezi vumilia damu mbichi au utumbo mbichi wa nguruwe.

Chakula huwa na usisimuaji wa kawaida. kama ukila mhogo basi umekula chakula. lakini kama ukila ‘’aspartame iliyo kwenye sukari za kisasa’’ haujala chakula. Kama ukila ugali basi umekula chakula, lakini kama ukipewa ‘’Drip ya Glucose’’ hospitalini hujala chakula. Chakula kwa asili huwa ni standard ya nishati na matter. Chakula hakisisimui sana kama nyama, na ndiyo maana ulaji wa nyama unavutia sana. hii ni kutokana na tabia zake kadhaa ambazo tutaziangalia hapo mbele.

WANYAMA WALA NYAMA ‘’carnivores’’

Mtu mmoja anaweza kujiuliza kama nyama sio tamu, kwanini simba, chui ,mamba na wanyama wengine wala nyama wanaiona tamu?

Mpaka sasa tunafahamu kuwa Wanyama wala nyama wana seli chache sana za kuhisi Ladha, wapo wenye ‘’tastebuds’’ kati ya 450-500’’ tu Ukilinganisha na wasio walaji nyama wenye kuvuka elfu. Hiyo inaweza kuanza kukupa picha ya kuwa, ulaji wa nyama kwa Wanyama wala nyama hauendeshwi sana na hamu ya utamu kama ilivyo kwa binadamu. Na Wanyama hawa hula mara moja moja sana, sio walaji sana. 

Takwimu zinaonesha pia Wanyama wengi wala nyama wa mwitu, kama utawapa nyama za kupika, hawavutiwi na hawazitaki mara nyingi. Pia kama utawapa Wanyama wa kufuga nyama mbichi na ya kupika, kuna uwezekano mkubwa sana wa Wanyama hao kupenda zaidi nyama za kupika. Na hii yote ni kwasababu, nyama za kupika zina msisimko zaidi kama tutakavyoenda kuangalia huko mbele.

Wanyama wala nyama ‘’carnivores’’ wapo hasa kwa ajili ya kuokoa mimea. Kama Wanyama hawa wasingekuwepo basi uzalianaji mkubwa sana wa Wanyama wala mimea ungepelekea kuisha kabisa kwa mimea. Na hii ingeathiri kabisa hali ya dunia. Hawapo hasa kwa kutaka kula nyama kwa sababu ya utamu wa nyama, na ndiyo maana wanapomla mnyama mmoja hutaona wakiweuka kwa kutaka kula nyama zaidi.

Pia Wanyama hawa huwa wana sifa ya ajabu sana. Huwa hawali kila mnyama, wao hawalengi tu kupata virutubisho. Mara nyingi sana hawa Wanyama hutaona wakila Wanyama wala nyama wenzao. Hutaona kirahisi simba akimla chui au kinyume chake. Wanajitambua kiasili zao.

WATU WANAOKULA NYAMA MBICHI

Kuna makabila baadhi hula nyama mbichi na pia husema kuwa zina Ladha nzuri. Sio kitu cha kawaida lakini pia sio cha kushangaza. Uwepo wa kitu kisicho cha kawaida haubadili mtazamo wa uhalisia. Uwepo wa mtu anayesema nyama mbichi ni tamu hauathiri kuwa nyama mbichi sio tamu. Usipolitambua hilo utakutana na la ajabu kabisa, kuna watu wanaokula hata watu wenzao ‘’cannibalism’’. Kuna Ushahidi mkubwa sana wa vikundi vya watu wa aina hizo. 

Wapo wanaokamatwa katika kufukua makaburi au hata kuvamia wenzao, na hata katika historia za dunia kama vita kali na dhiki, matukio hayo yameshawai rekodiwa au hata katika Biblia katika zama za kuzingirwa na jeshi la washami, kuna visa vya wamama waliokuwa wakila Watoto wao. Matukio haya hayamaanishi kuwa nyama za watu nazo zaweza kuliwa, ila yanaweza kukupa taswira ya kuwa, nyama sio chakula, nyama ni chanzo Cha nishati ya maisha ambacho ni alternative au mbadala baada ya kufeli kivirutubisho kwa Vyakula vilivyokwepo.

KWANINI WATU HUCHAGUA AINA ZA NYAMA?


Mara nyingi watu huwa wakipiga mahesabu ya umuhimu na mvuto wa kijamii wa mnyama wakuliwa, upatikanaji wake kiurahisi, na utamu wake. Watu hula kila mnyama kwa kweli. Na kila nyama huwekwa kwenye makundi Fulani ya Ladha. Watu humla nyoka, watu hula sungura,ng’ombe, farasi, Samaki, ndege, paka, mbwa, punda, nguruwe, kondoo,kobe, kenge,tembo,nyani n.k 

Wanyama hawa wote huliwa aidha kwa kuhalalishwa kijamii, au kwa kujiamlia tu. Hii ni kwasababu binadamu tuna uhuru kamili juu ya wanyama. Ukitaka kuamini hebu fikiria hili, ijapokuwa zipo mamlaka zinazopinga utesaji wa Wanyama, Lakini kama ukimnunua mnyama  ukawa unamtesa kila siku, je iko siku ataenda kukushtaki, au kukusemea? hata umtesaje atakaa kimya tu.

SAYANSI YA UTAMU WA NYAMA

Nyama sio tamu kama nilivyoelezea awali. Sisi huwa tukiibadili nyama ili iwe tamu. Na sisi tunauwezo wa kuibadili nyama ikawa tamu kwa kuipika katika namna mbalimbali, kama vile kuichoma, kuichemsha, kuikaanga, au kuikausha.

Nyama ni tamu kwa sababu unapoipika nyama. Huwa unafanya yafuatayo

Huondoa maji mengi sana na hivyo huwa ukisababisha chembechembe nyingi sana za Ladha zikusanyike kwa Pamoja. Na hii ndio sababu kubwa ya mtu kuhisi Ladha ya utamu. Hii ni sawa na kusema, una ‘’concentrate’’ madini yaliyomo katika nyama.

Mabadiliko ya kikemikali ‘’Mailard reaction’’

MAILARD REACTION

Unapopika nyama huwa unasabisha miunganiko ya kikemikali baina ya Glucose na Amino acids. Hii huwa sawa na kuandika: Glucose + Amino acids→Amadori compounds. Mabadiliko huendelea kwa kuanza kwa mabadiliko ya miunganiko ya kekimikali ‘’rearangement’’ na pia maji mengi hupotea ‘’dehydration’’, hii ni kama nilivyoelezea awali. Hii hupelekea kuundwa Kwa kemikali zingine zinazoitwa ‘’dicarbonyl compound’’ baada ya maji kupotea.

Uundwaji wa chembechembe kadhaa ‘’mailard reaction intermediates’’, hizi huundwa kutokana na mabadiliko kati ya α-dicarbonyl + amino acids. Na mabadiliko huendelea na kuunda kemikali zifuatazo: heterocyclic rings, pyrazines, na furans. Kemikali hizi heterocyclic rings, pyrazines, na furans ndizo ambazo hupelekea harufu na Ladha ya upekee ya nyama.

Uundwaji wa kemikali zingine zinazoitwa ‘’Melanoids’’. Hizi kemikali huundwa pale ambapo zile tulizoziita ‘’mailard reaction intermediates yaani: pyrazines, furans, na heterocyclic compunds’’ zinapoendelea na mabadiliko zaidi, mabadiliko haya huusisha ‘’polymerization na cross linking processes’’, na haya hupelekea kuunda chembechembe za rangi za kahawia ‘’brown’’ ambazo ndiyo rangi ya nyama, ambayo huwa inaonekana ikiiva. Kwa hiyo ukiona mshikaki au nyama imeiva, inaka rangi ka kahawia ‘’ujue sasa melanoids’’ zimeshaundwa. Nyama ni tamu pia kutokana na mabadiliko haya kupelekea kuundwa kwa kemikali nyingi sana za harufu ‘’volatile aromatic compounds’’.

HARUFU NZURI ZA UTAMU ‘’aromatic flavors’’

Mtu mmoja anaweza sema kuwa nyama ni chakula kwa kuwa kinanukia vizuri. Nyama hainukii ikiwa mbichi, Ukiipika nyama ndiyo hunukia. Vyakula kwa asili hunukia kwa uwepo wa hizi harufu za gesi za Ladha ili kuvutia viumbe waje kuila. Na ndiyo maana, machungwa au ndizi zikishaiva tu huanza kunukia, lakini nyama ya mnyama kamwe haitanukia. Ila ukiipika itanukia kwa sababu utakuwa ume ‘’concentrate’’ kemikali hizi kidogo kwenye sehemu ndogo na hivyo lazima zitanukia. 

Unapokula nyama, unapoitafuna unakuwa ukikandamiza na kusababisha harufu hizi nzuri ‘’aroma’’ kutoka kwenye nyama na kuja kwenye ukuta wako wa kuhisi harufu ‘’olfactory epithelium’’. Na hapa husisimua mfumo mzima wa kuhisi Ladha kupitia harufu kama nilivyoelezea awali kwenye sehemu ya fiziolojia ya kuhisi harufu na Ladha.

Nyama ni tamu kutokana na uwepo wa chembechembe za protini au amino acids zinazoitwa ‘’Glutamate na Inosinate’’. Amino acids hizi huenda kusisimua seli za kuhisi za ulimi, katika kundi la ‘’seli za kuhisi protini/ umami/ savory taste’’. Na hizi tuliziona zikiitwa T1R1/T1R3 receptors.

Seli hizi husisimuliwa sana na utumiaji wa nyama. Nyama yenye Glutamate nyingi sana husisimua zaidi ya nyama yenye glutamate chache. Hebu tuangalie takwimu juu ya viwango mbalimbali vya protini hii ya glutamate katika aina mbalimbali za nyama.


Kutokana na hili jedwali unaweza kuanza kupata picha kadhaa kama vile, Glutamate inavyoongezeka zaidi ndivyo watu wanavyokipenda zaidi kitu. Mfano, kama mtu atakuuliza kwanini watu hupenda sana kula nyama ya kuku kuliko nyama ya ng’ombe. Pamoja na sababu zingine tutakazo ziona huko mbele, lakini kiwango cha Glutamate na inosinate kinaweza kusema sana kuhusu jawabu. Na hii ni kwasababu, hawa ndiyo wasisimuaji wakuu wa hizo Ladha za nyama.

Unaweza pia kuona namna Nyanya ni miongoni mwa vyanzo vikubwa zaidi vya protini hizi za glutamate. Nyanya ina Ladha ya utamu wa asili kwa kiwango kikubwa sana, na ndiyo maana, hata mapishi yetu mengi huwa tukiipa kipaumbele aidha kupitia kutengeneza roast za vyakula, au kachumbari, au kuboreshea Ladha ya michanganyiko mbalimbali. Glutamate ndiyo sababu yake kuu. Na hata nyama haifikii kiwango cha glutamate cha nyanya, ila nyama inapopikwa huwa inakuwa na combinations nyingi zaidi za Ladha ukilinganisha na za nyanya.

Supu ya pweza hupendwa sana na wengi, msisimko wa Ladha yake pia una msingi kutoka katika kiwango kikubwa cha glutamate, kama kinavyoonekana katika jedwali juu. Hata Samaki unaweza ona walivyo na kiwango kikubwa cha glutamate na ndivyo ulivyo upekee wa Ladha yake.

Unaweza ona pia viwango mbalimbali vya glutamate kwa vyakula kama mahindi ,lotus roots n.k, havina msisimko mkubwa sana kama utalinganisha na msisimko uliopo kwa nyama . 

KWANINI NYAMA ZIMETOFAUTIANA UTAMU?

Nyama zimetofautiana utamu kutokana na sababu kuu zifuatazo.

Kiwango cha chembechembe za protini/ amino acids za Glutamate na Inosinate. Hii ni Kama tulivyoona katika jedwali juu, viwango tofauti tofauti vya amino acids hizi hupelekea ladha tofauti tofauti. Hii ni kutokana na combination tofauti tofauti za misisimko. Hapa utaona mfano Kuku wana kiwango kikubwa sana cha Glutamic acids kuliko wenzake.

Kiwango cha chembechembe za Mafuta/ fatty acids composition

Kuna aina mbili za mafuta, yapo mafuta yenye asili ya kuganda ‘’saturated fatty acids’’ na pia kuna yasiyo ya asili ya kuganda ‘’non saturated fatty acids’’, sehemu za nyuma nilionyesha, namna tofauti hizi zimesababishwa na uwepo wa ‘’double bond’’.

Kuna nyama ambazo huwa na kiwango kikubwa sana cha mafuta yenye asili ya kuganda au ‘’saturated fatty acids’’. Na mfano wa nyama hizi ni nyama ya ‘’Ng’ombe’’. Ukija kwa nyama ya Kuku na nyama ya Nguruwe, utaona zina kiwango kidogo sana cha mafuta ya kuganda, au zina kiwango kikubwa sana cha mafuta yasiyo na asili ya kuganda ‘’unsaturated fatty acids’’. na ndiyo maana utaona supu ya ng’ombe huharakisha kuganda na wala sio ya kuku katika mazingira tu ya kawaida.

Watu huona Ladha zaidi pale kiwango cha mafuta haya ya kuganda kinapopungua, na hii ni kwasababu, Mafuta haya yanapokuwa mdomoni huzuia au ‘’insulate’’ seli za kuhisi zisikutane kwa upana zaidi na chembechembe za chakula.

Kiwango cha chembechembe za tishu za kambakamba ‘’Collagen’’ na uvunjikaji wake.

Kuku na Nguruwe wana kiwango kidogo cha tishu za kambakamba za ‘’collagen’’. Na hii ndiyo sababu huifanya nyama yao iwe na ulaini ukilinganisha na nyama ya ng’ombe ambayo ina kiwango kikubwa cha kambakamba za collagen. Hizi chembechembe za collagen ndizo msingi wa ugumu wa tishu za nyama. 

Kiwango kikubwa cha kambakamba katika tishu hupelekea upikaji wake kuhitaji kiwango kikubwa cha joto, ambacho mpaka kukifikia, kitapelekea kuharibika kabisa kwa composition nzima ya madini na chembechembe za Ladha. Siku zote Joto huaribu miundo ya protini, na kwa hivyo, upikaji wa nyama ya ng’ombe huitaji joto kubwa zaidi ukilinganisha na upikaji wa nyama ya kuku au kitimoto, na hivi vyote huepelekea Ladha tofauti tofauti. 

Kiwango Cha Damu katika nyama ‘’Heme content’’

Nyama kama ya ng’ombe ina wekundu mkubwa sana ukilinganisha na nyama kama ya kuku au Samaki. Wengine huiita ‘’red meat’’ na zingine nyeupe huziita ‘’white meat’’. Huu wekundu unasababishwa na kiwango kikubwa sana cha chembechembe nyekundu za damu zinazoitwa ‘’hemoglobin’’. Hizi chembechembe ndani yake huwa na chembechembe ndogo zaidi zinazoitwa ‘’heme’’. Chembechembe hizi ndani yake huwa na madini ya chuma ‘’Iron’’. Haya ndiyo humsaidia mnyama katika kubeba hewa ya oksijeni katika mapafu. 

Nyama ya mnyama mwenye kiwango kikubwa cha huu wekundu, huwa na Ladha ya upekee sana inayoitwa ‘’metallic taste’’. Ladha hii ya chuma au metallic taste inasababishwa na madini chuma ya ‘’iron’’ na husababisha nyama ya ng’ombe ‘’beef’’ kuwa na ladha ya upekee kutokana na kiwango kikubwa sana cha wekundu, au madini chuma.

Kiwango kikubwa cha wekundu unaochangamana na damu huambatana Pamoja na uwingi wa ‘’Glucose’’, na hivyo basi, hii huchangia kwa zile ‘’mailard reaction’’ ambazo hupelekea Ladha ya upekee wa utamu wa nyama hasa ya ng’ombe, au ya viungo kama Maini yenye damu nyingi.

Natumia sana mifano ya ng’ombe, kuku, na nguruwe; Kwa kuwa hawa Wanyama ndiyo wanaoliwa sana katika jamii zinazonizunguka. Na pia, kielelezo cha Wanyama hawa kinaweza kumpa mtu msingi wa kuelewa na kwa Wanyama wengine wote.

Mabadiliko ya kikemikali ‘’Mailard reaction na Caramelization’’

Haya matendo ambayo huusisha uundwaji wa unjano katika vyakula kadha wa kadha. Tofauti ya matendo haya ni kuwa, mailard huusisha ‘’reactions’’ za amino acids na glucose kwa kutumia moto. Lakini caramelization huusisha matokeo ya moto moja kwa moja kwenye sukari. Mfano mzuri kabisa wa caramelization ni pale unapochoma muogo, utakuta unaanza kuwa na unjano, au ukiwa unatengeneza mkate utakuta kwa nje unaanza kupata rangi ya njano. Lakini matendo haya kuna wakati yote huchangamana. Mfano ni kama hivi, kama utakuwa ukiipika nyama, kutakuwa na ‘’mailard reactions’’ lakini bado kutakuwa na baadhi ya chembechembe za glucose ambazo zitaungua moja kwa moja kupitia ‘’caramelization reactions’’. 

Matendo haya hutengeneza tofauti za Ladha kwa kupitia namna moja kubwa ambayo ni hii; Nyama zenye viwango tofauti tofauti vya glucose, amino acids, na chembechembe zingine kwenye nyama ‘’ingredients’’, hupelekea Ladha tofauti tofauti. Ni kama juisi yenye vijiko viwili vya sukari, na nyingine ikawa na vijiko vine vya sukari, hazitakuwa na Ladha sawa.

Maisha na Mazingira ya Mnyama.

Unaweza jiuliza kwanini kuna tofauti ya Ladha ya nyama ya ng’ombe wa kufugwa na Nyati. Au kwanini kuna tofauti ya nyama za Wanyama wa kufugwa na Wanyama pori. Sababu kubwa huwa ni hii. Wanyama wa mwitu huwa wanakula aina mbalimbali za mimea, wale wana kiwango kikubwa sana cha utofauti wa malisho au ‘’diverse feed types’’ ukilinganisha na wanyama wa kufugwa, ambao huwa na aina chache tu ya vyakula. Hii hubadili nini?

Hii hufanya misuli ya Wanyama wa mwitu kuwa na kiwango kikubwa sana cha chembechembe za Ladha, ambazo hufikia kiwango cha kuwapa upekee wake, huwa zinaitwa ‘’Gamey flavor’’. Ladha hizi utahisi kama utakula nyama ya ‘’nyati, tembo, swala, nyoka,sungura, farasi na hata kwa wale wanaokula paka.

Wanyama wanaofugwa zaidi ndani Kwa kulishwa Pumba, huwa na kiwango kikubwa sana Cha mafuta "SFAs" ambayo huzifanya nyama zao kutokuwa tamu sana ukilinganisha na wanaokula zaidi nyasi.

Nyama ya Broiler haichemshwi!

Sababu kubwa ni uwezo wake mdogo wa kufyonza maji na kubakia imara "intact". Nyama ya Broiler ina kiwango kidogo cha protini na hivyo uwezo wake wa kufyonza maji huwa ni mdogo Sana. Broiler hulishwa Pumba na hivyo huwa na kiwango kikubwa sana Cha Mafuta "SFA's" na Triglycerides ambazo hufanya saizi yake iwe kubwa lakini ikiwa laini sana. Ladha yake huwa si tamu kama ya Kuku wa kienyeji ambao hula sana nyasi na wadudu, hivyo kuwa na protini nyingi sana. Kuku wa Broiler huwa na stress sana zinazoambatana na kiwango kikubwa cha uasidi, huu huathiri zaidi protini na uwezo wake wa kufyonza maji. Kumbuka, Ladha zinahitaji sana ufyonzwaji wa maji kuzunguka protini, na maji ndiyo hushikamanisha kemikali za Ladha.

Msongo wa Maisha au ‘’stress’’ huathiri sana Ladha za nyama za Wanyama. Wanyama ambao hufugwa muda mwingi huwa na stress za kutokuwa huru, hawa si sawa na wale ambao huwa huru machungani. hii ni kwa sababu stress huamasisha uzalishaji wa homoni kutoka katika tezi ya adrenali inayoitwa ‘’cortisol’’, na homoni hii huamasisha sana uvunjikaji wa chembechembe za ‘’Glucose’’ kupitia kitendo kinachoitwa ‘’glycolysis’’, na hii tayari huathiri viwango vya ‘’glucose’’. stress huwa hata ikishusha kiwango cha ‘’protini’’ katika mazingira Fulani.

Mitazamo ya kijamii na saikojia za watu;Kama utaishi katika jamii ambazo wanakula sana nyani, Basi nyani kwako anaweza kuwa mtamu sana. Hii ni kutokana na kuwa kipindi ubongo wa kila binadamu unapoanza kutengeneza taarifa kuhusu mazingira yanayouzunguka, hutengeneza msingi kutokana na taarifa za kwanza kabisa ambazo ulizipata. 

Na hii ndiyo sababu ya kusema kuwa mpaka mtoto anapofikia miaka minne ya kwanza, vyakula alivyokuwa akivila ndivyo atakuwa akiviona vitamu kwa Maisha yake yote. Hata asili au ‘’nature’’ ya maziwa ya mama yake aliyokuwa akiyanyosha yana mchango katika utambuzi wake wa Ladha mpaka atakapokuwa mkubwa.

Lakini pia Kama ilivyo katika mazingira ya kawaida, nyama inaweza kuwa ni ileile ila ikapikwa kwa aina tofauti tofauti na kuleta Ladha tofauti tofauti. Hivyo mapishi hupelekea mabadiliko mbalimbali ya kikemikali. Pia zipo sababu za mtu binafsi; Kuna watu wao wataona nyama Fulani ni tamu kuliko nyingine Kulingana na upekee wa fiziolojia zao au mazingira na Maisha yao. Muhimu kutambua ni kuwa; Ladha haipo kwenye ulimi!! Ladha ni matokeo ya kinachoenda katika sehemu yako ya ubongo inayohusiana na ladha. 

SABABU MAARUFU ZAIDI ZA KULA NYAMA

Chanzo cha Protini Bora kabisa kwa mwili.

Nyama ndiyo chanzo pekee cha protini zilizo kamilika. Nyama hutoa protini zote muhimu kwa afya, tena kwa kiwango maalumu na muhimu kwa mwili ‘’right proportions’’. Hizi protini huwa zikiitwa ‘’essential na non-essential amino acids’’. Wanyama tunahitaji aina zote za protini. Lakini Kwa upande wa Essential amino acids (EAA) mwili wa mnyama hauwezi jitengenezea, na kwa hivyo, huzipata kwa mimea tu. Kama utakula mnyama mwenzako maana yake utazipata zote maana na yeye anazihitaji kama wewe. Na ndiyo maana sasa husemwa kuwa nyama ni chanzo bora kabisa cha protini kwa kuwa kimekamilika kwa kuwa na protini zote. Wanyama huwa na EAA Kwa kuwa hula sana manyasi na Mimea ambayo Binadamu hushindwa kula Kwa wingi na Kwa aina zake nyingi kama wanyama, na hivyo kupungukiwa EAA. 

Hoja hii ni kweli kabisa Kwa kuwa kupata EAA zote Kwa kula Mimea kunahitaji Maarifa mengi sana ya kuielewa mimea, kupata Mimea aina mbalimbali jambo lisilo rahisi, na gharama za kupata mbogamboga za jamii mbalimbali na matunda ya kutoka maeneo mbalimbali, na hata supplements za Mimea Kwa nyakati kadhaa, jambo ambalo ni la gharama ndogo sana ukilinganisha na gharama ya kutumia robo kilo TU ya nyama kama ya Maini au msuli wa mnyama pori.

Chanzo cha Virutubisho vya muhimu kabisa katika mwili. Hapa nyama inaonekana kuwa bora katika kutoa au ‘’supply’’ virutubisho kama vifuatavyo.

Madini ya Chuma au Iron.

-madini haya huonekana kuwa kwa uwingi sana kutoka kwa Wanyama wenye nyama zenye wekundu sana au ‘’red meat’’. Madini haya ya chuma ‘’iron’’ huwa katika namna kuu mbili, ambapo moja huitwa ‘’haem iron’’ ambayo haya ni madini chuma yanayopatikana kwa ulaji wa nyama, na pili ni ‘’non-haem iron’’, haya ni madini chuma yanayopatikana kwa kula vyakula tofauti na nyama kama mimea. Nyama nyekundu huwa na kiwango kikubwa sana cha ‘’haem iron’’; na madini haya kutokana na tafiti nyingi sana yameonekana kusaidia sana walaji wa nyama kutoteseka kwa kupata tatizo la damu linaloitwa ‘’Iron Deficiency Anemia’’.

Pia tafiti zimeonesha kuwa, madini kutoka kwenye nyama ‘’haem iron’’ husaidia sana hata katika kuchochea ufyonzwaji wa madini ya chuma yasiyotokana na ulaji wa nyama ‘’non-haem iron’’. Na sababu hii imetumiwa baadhi ya muda kuhamasisha baadhi ya watu wasiokula nyama "vegetarian" kuanza kufikiria ulaji wa nyama kutokana na kujiondoa katika hatari ya kuathiriwa kwa tatizo la upungufu wa madini chuma ‘’IDA’’. Hii imetokana na tafiti kadhaa kuona kuna ongezeko la tatizo la ‘’IDA’’ kwa wala mimea tu ‘’vegetarians’’.

Madini chuma yana faida nyingi sana katika miili ya Wanyama. Madini haya husaidia sana katika kubeba hewa ya Oksijeni na kuisambaza mwilini, yanasaidia sana katika kuwezesha matendo ya kibiolojia ya uzalishaji wa nishati, hii ni kutokana na kuwa, madini chuma hutumika moja kwa moja katika hatua ya tatu ya uzalishaji wa nishati wa mwili ‘’kama Cytochromes katika electron transport chain’’. Pia madini chuma ni muhimu sana kama madini yenye kazi mbalimbali katika afya ya ubongo.

Madini ya Zinc.

Madini haya pia hupatikana kwa kiwango kikubwa sana kutokana na ulaji wa nyama. Na madini haya yana umuhimu mkubwa sana katika utendaji wa Kinga za mwili, husaidia katika uponaji wa vidonda, na pia madini haya ni ya muhimu sana katika uundwaji wa protini za mwili ‘’protein synthesis’’.

Vitamini B12

Nyama ni chanzo muhimu sana cha vitamini B12. Vitamini B12 ina umuhimu mkubwa sana kama vile hutumika sana katika afya ya ubongo, husaidia katika matendo ya kijenetikia ‘’DNA synthesis’’. Na pia ni muhimu kwa seli nyekundu za damu ‘’RBCs’’.

Chanzo kikubwa cha Omega-3-Fatty Acids.

Na hasa nyama za Samaki, huwa ni chanzo kizuri na kikubwa sana cha virutubisho hivyo vya mafuta ‘’omega-3-fatty acids’’. Mafuta haya huwa na faida nyingi sana katika afya, huboresha mfumo wa moyo, na mzunguko wa damu ‘’cardiovascular system’’, huboresha afya ya ubongo, hii ni kwa kuwa ubongo huwa na kiwango kikubwa sana cha mafuta. Ambayo hutumika kuunda njia zake ‘’white matter’’ . lakini pia husaidia katika ku control uvimbe ‘’inflammation’’ katika miili.

Chanzo kikubwa cha Selenium

Nyama huwa na selenium. Ambazo ni za muhimu sana hasa katika kuzuia matatizo ya uharibifu wa mwili dhidi ya sumu. Selenium huitwa ‘’antioxidant’’, hii ni kama tulivyoona kwa sehemu zilizopita, namna ambavyo hizi huwa zikizuia madhara ya kemikali sumu kama ‘’reactive oxygen species’’. Hizi husaidia moja kwa moja utendaji wa tezi ya Thyroid, huboresha utendaji wa kinga ya mwili, na pia husaidia katika utendaji wa matendo ya kijenetikia ‘’DNA synthesis’’ , hii ni kwasababu ya kuondoa sumu. Ambazo husababisha madhara kwenye DNA na kupelekea makosa ‘’mutations’’ ambayo huweza kuishia katika utengenezwaji wa saratani.

Nyama ina kiwango kikubwa cha virutubisho vikuu vya mwili.

Nyama ina kiwango kikubwa sana cha protini. lakini wakati huo huo, nyama ina kiwango kikubwa cha mafuta. Virutubisho hivi huridhisha kabisa hamu ya kula ya mtu, na pia huboresha kiwango cha sukari ya mwili. Pia hutoa kiwango cha nishati cha kutosha kabisa kwa mwili

Nyama ina kiwango kidogo cha kemikali zisizohitajika mwilini ‘’anti nutrients’’. Ukilinganisha na vyakula vya mimea, ambavyo huwa na kemikali nyingi ambazo huwa kwenye Maganda, mbegu, nyuzi nyuzi n.k ambazo huwa hasa hazina faida kwa mwili. kama vile ‘’phytates, oxalates, au lectins’’, na zinginezo.  Nyama huwa haina hizi kemikali na hivyo ulaji wa nyama huwa na usalama mkubwa dhidi ya hizi kemikali.

Ladha za Nyama huwa zakuvutia na huridhisha.

Kama mtu akipewa ale mchicha na ugali, na mwingie akapewa ugali na kuku aliyerostiwa. Baada ya muda mfupi utagundua kuwa huyu anaekula ugali na mchicha; Aidha akipungukiwa hamu ya kula kama aliyo naye anayekula nyama. Au pia unaweza ona anayekula nyama akiwa na msisimko sana wa utamu ukilinganisha na anayekula mchicha. Sababu hizi hazifichiki na ndiyo maana hata wapanga bei huweka vyakula hivi katika bei tofauti tofauti. Uandaaji wa nyama huwa rahisi kwa baadhi ya nyama ukilinganisha na vyakula vingine, unaweza ichoma, chemsha, kausha n.k, lakini maharagwe mfano huwezi yakaanga au yachoma.

HITIMISHO

Hoja hizi ni za kweli kabisa kuhusu faida za kula nyama. Lakini hebu tuhame upande ili tuje kufanya maamuzi baada ya kuangalia pande zote. Kumbuka hizi ndizo sababu kubwa zaidi za kula nyama zilizo maarufu.

MADHARA MAARUFU YA ULAJI WA NYAMA

TAMBUA?

Madhara makubwa zaidi ya ulaji wa nyama yaliyowahi rekodiwa ni Aidha matokeo ya ulaji wa nyama za makopo "processed meats", nyama za wanyama wanaofugwa kisasa hasa Kwa Madawa na kulishwa Pumba, na mwisho ulaji wa nyama uliopita kiasi#


Chanzo Cha Saratani ‘’carcinogenesis’’

Ipo mijadala mingi sana iliyotapakaa kuhusu utokeaji wa aina mbali mbali za cancer zinazochangiwa na ulaji wa nyama. Cancer hizi mara nyingi huonesha kutokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na ulaji wa nyama. Na mara nyingi cancer ambayo huwa maarufu sana ni cancer ya utumbo wa colon. Hii pia huitwa ‘’colorectal cancer’’. Cancer hii haipingiki kuwa hutokana na madhara ya ulaji wa nyama, na jamii wanaokula zaidi nyama hasa za makopo tafiti nyingi zimeonesha kuwa na kiwango kikubwa cha cancer hii ya colon.

A: CANCER YA COLON

B:SABABU YA CANCER YA COLON

Hiyo ndiyo namna nzuri ya msomaji ili uweze kujua chanzo cha matatizo mengi. Mwili sio kama injini ambayo ukiharibu sehemu Fulani, lazima sehemu Fulani iathiriwe. Mwili una muunganiko mpana ‘’coordination’’, na hivyo; madhara katika sehemu moja yanaweza kupelekea matatizo katika sehemu tofauti na ulivyotegemea.

Nadharia za nyama inawezaje kuleta haya madhara 

Nyama Huwa na madini Chuma mengi sana, hasa nyama nyekundu ‘’high heme content’’. Madini haya ya chuma huchochea uundwaji wa kemikali sumu zinazoitwa ‘’N-nitroso compounds’’. Hizi kemikali ni sumu kwa kuwa, huwa zina uwezo wa kuathiri vinasaba vya jenetikia. na kupelekea ukoseaji wa maelekezo au ukoseaji katika uumbaji. na mwisho wake ni kuzaliwa seli zisizo za kawaida ambazo ndizo cancer, na huweza kumuua mtu kwa hatari kubwa sana. Kwa hiyo hizi N-nitroso compounds huenda na kuathiri DNA katika seli zilizo katika ukuta wa utumbo wa Colon, na wa Rectum. Hizi ni sehemu za utumbo wa chini kabisa kufuatana tu na sehemu ya kutolea haja kubwa.

Nyama nyingi zilizokuwa ‘’processed’’ kama nyama za makopo, kama sausages n.k, hutunzwa kwa vitunza chakula kama vile ‘’nitrates, nitrites n.k’’, vitunza chakula hivi, kipindi cha umeng’enyaji wa chakula, hubadilishwa kuunda hizi sumu tena za ‘’N-nitroso compounds’’, na hapo huchochea tena makosa katika utendaji wa kijenetikia.

Nyama nyingi hupelekea uundwaji wa kemikali sumu zinazoitwa ‘’Polycyclic Aromatic Hydrocarbons’’ au kifupi ‘’PAHs’’, pia uundwaji wa Heterocyclic Amines ‘’HCAs’’ , kutokana na Joto Kali sana katika uundwaji wake. Ambazo Kama unaweza kukumbuka utagundua kuwa hizi kemikali tuliona kuwa huwa zikiundwa kile kipindi cha mabadiliko ya kikemikali ‘’mailard reaction’’. Hizi kemikali ambazo tuliziona zikichangia katika hisia ya Ladha ya utamu wa nyama, ikiwa mdomoni, ndizo sasa huwa zikisababisha ‘’DNA adducts’’, hii ni kama niseme kuwa huenda kuzisonga DNA. na kupelekea madhara ya michubuko, na uharibikaji wa seli za mwili ‘’oxidative stress’’. na pia husababisha Uvimbe, ambao huchangia katika kutokea kwa saratani, au huchangia kwa makosa katika utendaji wa kijenetikia.

Nyama husababisha kiwango kikubwa sana cha Mafuta Hatarishi kwa mwili. Ambayo huwa yanaitwa ‘’Saturated Fatty Acids’’ au kifupi ‘’SFA’’.

Unapokula nyama huwa unakula mafuta mengi sana, huwezi linganisha na unapokula maboga au kisamvu. Haya mafuta yakifika mwilini yanahitaji kuvunjwa vunjwa. Ili uyavunje haya mafuta unahitaji mwili wako uweze kuzalisha kiwango kikubwa cha Nyongo ‘’Bile’’, hii ni kwasababu, nyongo ndiyo huwa inatumika kuvunja mafuta unayokula siku zote, kupitia kitendo kinachoitwa ‘’emulsification’’. Sasa basi, kwa kuwa nyama ina mafuta mengi, basi nyongo nyingi sana itazalishwa. Na hizi nyongo huzalishwa kutoka kwenye aina za mafuta yaitwayo ‘’cholesterol’’ katika ini. Lakini uundwaji wa nyongo haukamiliki katika ini, huwa unaenda kukamilika katika utumbo wa colon na rectum.

Katika utumbo wako wa colon na rectum, huwa kuna kiwango kikubwa sana cha Bakteria Ambao huwa wanasaidia kumeng’enya chakula. Hawa bakteria hukamilisha uundaji wa nyongo ambayo pia inaitwa ‘’bile acids’’. sasa basi, kiwango kikubwa cha hizi ‘’bile acids’’ katika maeneo ya Colon, kama ilivyo sifa ya asidi yoyote, huwa ikichubua na hivyo kutengeneza njia kwa sumu zote nilizozitaja hapo juu ambazo zimekuja Pamoja na nyama kuingia katika seli kiurahisi sana, na kupelekea madhara hayo ya saratani katika utumbo wa colon na rectum.

Michubuko hii pia hupelekea kuzalishwa kwa chembechembe za kusisimua uvimbe, ‘’pro-inflammatory mediators’’. na hawa, hupelekea mazingira ya viuvimbe. Ambavyo, ndivyo huichochea sasa cancer kukua vizuri.

Uvimbe ‘’inflammation’’.

Ni rahisi sana mtu kulalamika mkono wake wote ukiwa umevimba hata kama ni uvimbe mdogo kwa kuwa, ni rahisi kuona, hata kama hakuna maumivu. Utumbo huonesha dalili za uvimbe wa mtindo huu kwa ulaji sana hasa wa nyama nyekundu ‘’red meat’’. Hii inatokana na kuwa, ulaji wa nyama husisimua sana chembechembe za usisimkaji wa uvimbe ‘’pro inflammatory cytokines’’. Na uvimbe huu, huwa sio wa ghafla kama tatizo la kukanyagwa uwanjani, huwa ni kidogo kidogo kwa ulaji wa muda mrefu huitwa ‘’chronic inflammation’’, na hali hii hutengeneza mazingira ya kuibuka kwa cancer.

Nyama huathiri balansi ya Bakteria na vimelea wa tumboni, Ambao huwa na manufaa kwa mwili, hawa huitwa ‘’gut microbiota’’. Hapa pia ni kwa kuwa makini sana, kuna uhusiano mkubwa sana wa vimelea hawa kwa afya nzima ya kiumbe. Sehemu za mwanzo tuliona kuwa, viumbe hawa huwa na umuhimu hata katika afya ya ubongo, na mfumo wa kinga ya mwili. Tuliona katika ule mfumo wa ‘’Microbiome-gut-brain axis’’. Na sasa basi, nyama siku zote huathiri hawa viumbe. 

Huwezaje kuwaathiri? Ni kupitia kiwango kikubwa cha mafuta ya aina ya ‘’Saturated fatty acids’’. ambapo haya mafuta yanapokaa katika ukuta wa seli wa kiumbe ‘’cell membrane’’ huiruhusu kudhurika kiurahisi sana. Haya mafuta huwa sawa na mtu anaejikinga na maji kwa kujifunika na makaratasi, huwa yakishalowana kidogo tu yanajiachia. Na ndivyo haya yanapokaa kwenye ukuta wa seli.

Kitendo cha nyama kuathiri balansi hii hupelekea kuongezeka sana kwa kiwango kikubwa cha chembechembe ambazo huchochea makosa katika matendo ya kijenetikia, au ‘’carcinogens’’.

Madhara ya Mfumo wa Moyo "cardiovascular diseases’’

Kwanza ni muhimu kutambua kuwa hapa:

A: Ugonjwa wa Moyo

B: Shida za Moyo

Yale Madini Chuma yanayotokana na nyama ‘’Haem Iron’’. Ijapokuwa kule tuliona yana umuhimu sana, lakini kumbe yale madini huchochea uundwaji wa zile sumu tulizokuwa tunaziita ‘’reactive oxygen species’’. Hii tabia ya haya madini kuunda hizi sumu huitwa ‘’pro-oxidant effect’’.

Hizi sumu za reactive oxygen species kama tulivyoona kwenye sura zilizopita. huenda moja kwa moja na kuathiri DNA, na Protini mbalimbali katika mishipa ya damu. Changamoto hizi hupelekeaa uharibifu wa tabaka la ndani la mishipa ya damu ‘’endothelial damage’’. Na hii husababisha mshipa wa damu kupoteza chembechembe muhimu sana katika utendaji wake zinazoitwa ‘’NO’’ au nitrous oxide. Chembechembe hizi zinapopotea hupelekea mishipa ya damu kushindwa kujitanua, na kuwa imekakamaa. na pia huwa na presha kubwa katika kutembea kwa damu ‘’hypertension’’.

Madhara haya ni mabaya kuliko msomaji ambavyo ungeweza kuhisi, hapo mbele tutaona kwanini!

Kuundwa kwa kemikali sumu zinazoitwa ‘’Trimethylamine N-Oxide’’.

Kemikali hizi uundwaji wake kutokana na ulaji nyama huwa kama ifuatavyo, Nyama nyingi huwa na kemikali zinazoitwa ‘’ Carnitine na Choline’’. Hizi kemikali zinapoingia katika utumbo baada ya kuliwa, hukutana na wale vimelea wasaidizi wa tumboni ‘’gut microbiota’’. Hawa hufanya jambo moja kubwa la kubadilisha hizi kemikali na kuunda kemikali zinazoitwa ‘’Trimethylamine’’ au TMA. Hizi kemikali za TMA huwa zinapenya na kuingia katika mishipa ya damu na kusafirishwa mpaka zinapofika katika Ini, kule kwenye ini huwa zikibadilishwa na kuunda kemikali zingine zinazoitwa ‘’TMAO’’.

Hizi TMAO ndizo kemikali zenye changamoto zaidi, maana zenyewe huamasisha uundwaji wa chembechembe zile za mafuta zinazoitwa ‘’Cholesterol’’ ndani kabisa katika mishipa ya damu, Lakini huzuia mafuta haya ya cholesterol kutoka katika mishipa ya damu. Huchochea uvimbe ‘’inflammation’’ na kujikusanya kwa seli za kuganda za damu ‘’platelet aggregation’’, na mshipa wa damu huvimba na kupekelea mabonge ya damu zilizoganda kuzuia kabisa damu kupita katika mshipa wake. Na pia huchochea na lile tatizo la mabonge kujikusanya kwenye ukuta wa mshipa wa damu wa artery au ‘’atherosclerosis’’.

Nyama na Vitunza/viongezwa kwenye nyama huchochea yafuatayo katika kuleta shida katika mfumo wa damu.

Kujaa kwa sumu za ‘’N-nitroso compounds’’ ambazo hizi kama tulivyoona katika sehemu zilizopita, huwa na asili ya kuchochea cancer. Tuliona kuwa hizi husababisha ‘’oxidative stress’’, na pia tuliona hizi huwa zinachochea uvimbe katika matabaka ya seli zilizo katika kuta za viungo. Na hapa changamoto hasa huwa pale zinapokuwa zinaathiri kuta za seli za damu, basi hupekekea moja kwa moja shida katika mfumo wa moyo na mzunguko wa damu.

Vitunza vyakula vya ‘’nitrites na nitrates’’ tulishaona namna ambavyo vinachangia katika uundaji wa hizi N-nitroso compounds.

Pia chumvi nyingi zilizo katika bidhaa hizi, hasa nyama za makopo; huchochea katika kutokea kwa shida ya ‘’hypertension’’, hii hutokana na kuwa chumvi nyingi huchochea kuongezeka kwa presha ya damu, na hii hupelekea stress katika mishipa ya damu, na kuathiri moja kwa moja kuta za artery.

Uvimbe ‘’inflammations’’

Hii ni kama tulivyoona kule juu, ila kwa hapa ile changamoto inatokea katika mishipa ya damu. Na kama nilivyosema awali uvimbe wa aina hii, huwa ni uvimbe wa muda mrefu au ‘’chronic inflammation’’ ambapo tuliona madhara haya yalikuwa yanatokana na uwepo wa zile chembechembe za uvimbe, ‘’inflammatory cytokines’’ kama vile TNF-α, IL-6 na CRP.

Madhara ya upishi wa nyama kupitia kuunda ‘’Advanced Glycation End Products’’ au ‘’AGEs.

Hizi ni zile kemikali ambazo huwa zinatokea kutokana na yale matendo ya kikemikali ya kuunda Ladha. Hizi kemikali mara zote hupelekea uundwaji wa chembechembe za awali ya uvimbaji. lakini pia, hupelekea uundwaji wa kemikali sumu za mwili ‘’oxidative compounds’’. Hizi ndizo hupelekea kuundwa kwa zile ‘’reactive oxygen species’’.

Hizi ‘’AGEs’’ huwa na madhara makubwa sana, maana hizi kemikali zikiingia katika seli zako, au tishu zako, huwa zinasababisha mabadiliko ya maumbile ya tishu. Hizi huwa zina kunja kunja protini, hiki kitendo kinaitwa ‘’cross linking’’. Na hiki kitendo cha kukunja kunja protini, hupelekea tishu kukamaa na hata kusababisha viungo kutofanya kazi vizuri. Mfano, hupelekea kiungo kushindwa kurejea umbo lake baada ya kutingishwa kidogo ‘’impaired elasticity’’. 

Kemikali za utunzaji nyama zinapoliwa huathiri wale vimelea wazuri ‘’gut microbiota’’, na hiki kitendo huathiri balansi ya hawa viumbe ambao, hatma yake huwa ni kuzalishwa kwa sumu zao. Kivipi? hawa bakteria huwa wanakufa, wanapokufa huzalisha sumu zinazoitwa ‘’Endotoxins’’. Hizi sumu huwa zinaitwa pia ‘’lipopolysaccharides’’ au ‘’LPS. Na hizi huingia katika damu ya mlaji. Na hii hali ya kuwepo kwa hizi sumu kwenye damu huitwa ‘’endotoxaemia’’. Na huwa na madhara mbali mbali ikiwepo uvimbe katika sehemu tofauti tofauti na kushindwa kwa kufanya kazi kwa insulin.

Hizi sumu kwa Pamoja na zile zilizopita huwa na tabia ya kuamsha mifumo ya kinga za mwili. hii ni kama ilivyo kawaida siku zote, sumu au kitu hatarishi mwilini lazima kitaamsha mifumo ya kujikinga. Na hii huwa hivi, hizi sumu huenda kuamsha sensa au receptors zinazoitwa RAGE. Hizi huamsha mifumo ya uzalishaji wa zile chembe chembe za uvimbe ‘’cytokines’’. hizi huita seli kwa ajili ya kujikinga. Hizi huitwa kupitia network mbalimbali za seli Mfano, kupitia (NF-kB, MAPK na JAK/STAT.)

Nyama za Makopo Huathiri Nguvu za kiume 

Kuna uhusiano wa moja kwa moja wa ulaji wa nyama, na nguvu za kiume. tena ni rahisi sana kujua uhusiano huu ambao umekwisha fanyiwa tafiti nyingi. Hebu tuangalie sababu za msingi za utokeaji wa hili tatizo, lakini kabla, hebu tatambue kuwa;

Sababu zifuatazo zinatokana na ulaji wa nyama za makopo

Kuathiriwa kwa mfumo wa ujaaji wa damu ‘’Vasodilation’’. Hii hutokana na madhara katika kemikali ya kutanua mishipa ya damu inayoitwa ‘’Nitric Oxide au NO’’. tuliona kuwa sababu kubwa ni kuwa, unapopika nyama, huwa unasababisha uwepo wa kemikali zinazoitwa ‘’AGEs’’ au unaweza ziita ‘’amino glycation end products’’. Hizi tuliona huwa zinazalishwa katika yale matendo ya kikemikali yanayoitwa ‘’Mailard reaction na Caramelization’’.  hizi AGEs huwa siku zote zinaenda kwenye ukuta wa ndani wa mshipa wa damu na kuathiri enzyme mmoja anayehusika na hizi ‘’NO’’ ambae anaitwa pia ‘’nitric oxide synthase’’, na pia AGEs huathiri uzalishaji wa ‘’NO’’; hizi hupelekea kufeli kwa utendaji wa ule ukuta wa ndani wa mshipa wa damu. Hii hali huwa inaitwa ‘’endothelium dysfunction’’. Na madhara yake ni kuwa mshipa wa damu hushindwa kutanuka , lakini hayaishii hapo tu madhara , pia hupelekea kupungua kwa kiwango ‘’nitric oxide’’, kemikali ambayo pia ingepaswa kuufanya mshipa wa damu kutanuka.

Kilichohitajika hasa ni mshipa wa damu uweze kutanuka , na ili utanuke ulihitaji hizo’’ nitric oxide signaling’’. ambazo kama zitatanua mshipa wa damu, basi uume utaruhusu damu nyingi kujaa katika mishipa yake, lakini pia katika tishu ambayo huitwa ‘’corpora cavernosa’’ ambayo kama ikijaa basi mtu atakuwa na nguvu za kusimamisha uume wake. 

Nyama hudhoofisha uwezo wa Mifupa

Ongezeko kubwa sana la madini ya Phosphorus. Nyama huongeza kiwango kikubwa sana cha madini ya phosphorus. Unaweza kutaka kujua kwanini? kwanza kabisa lazima utambue aina za upikaji wa nyama huusisha ku ‘’concentrate’’ madini mengi katika sehemu ndogo. na ndiyo maana, utakuta unaikaanga au ichoma. Lakini phosphorus siku zote ipo kwa wingi sana katika misuli, ipo katika protini na ipo mpaka kwenye vinasaba, mfano DNA ina kiwango kikubwa sana cha phosphorus. Haya madini hufanyaje mpaka calcium nyingi kupotea?

Haya madini siku zote huwa yakikinzana na kiwango cha madini ya calcium mwilini. Hii ni kwasababu ifuatayo, siku zote madini ya phosphorus na calcium huwa mwilini kwa wastani maalumu kuanzia 2:1 mpaka 3:1. Hii inamaanisha kuwa, mfano kama phosphorus yapo 30 basi calcium yanapaswa kuwa kumi. Na sasa basi, chukulia hiyo standard ndio ipo mwilini, sasa ikitokea mtu amekula nyama hasa za makopo na soda, basi huyu mtu ameongeza kiwango kikubwa sana cha phosphorus, kitakachotokea ni kuwa;

Phosphorus ya ziada kuanza kuungana na calcium kutengeneza Calcium phosphate complexes. Hizi Sasa hupelekea calcium kuanza kupungua mwilini. Kumbuka shida ni kuwa huyu mtu hajaongeza calcium, yeye kaongeza tu phosphorus. Hivyo matokeo yake ni kuwa. kiwango cha ‘’calcium’’ mwilini hupungua sana kwa sababu tu ya ulaji wa nyama.

Mwili hauwezi kuvumilia upungufu wa madini ya calcium maana yana kazi nyingi sana, hasa katika mfumo wa fahamu. Ambapo neva zote hutumia calcium katika utendaji wake katika synapse au makutano au maungano yake; ubongo huunda kumbukumbu kwa msaada wa madini ya calcium, calcium ina umuhimu mkubwa sana hata katika mfumo wa kinga za mwili, pia katika fiziolojia za kazi za viungo mbalimbali ikiwemo na moyo. Na sasa basi, kitendo cha calcium kupotea, mwili hupanga mbinu. na mbinu kuu ni hii.

Kuvunja calcium zote zilizojaa kwenye mifupa ili zije kusaidia kulipia hili deni la calcium zilizopotea. kwa mwili ni bora mifupa ipungukiwe nguvu kuliko ubongo na fiziolojia za mwili ziathiriwe. Hiki kitendo kinapojirudia siku kwa siku humsababisha mla nyama za makopo azidi kupungua nguvu za mifupa siku kwa siku. Na huyu mtu huzidi kuwa mdogo mdogo kila siku zinavyoenda. Anakuwa hakui kwa kuwa ukuaji wote wa mifupa anaulipia kwa kula nyama. Ni kama vile laana ya kula nyama za makopo huwa inajilipa kisayansi. Mlaji wa nyama anaejiona bado ana mifupa imara na ili hali anakula sana nyama hizi basi anaweza kutambua kuwa angeweza kuwa na nguvu zaidi ya hizo, lakini pia madhara haya huusiana na sababu zingine katika kuchochea sana au kupooza matokeo.

Mazingira ya asidi ‘’acidic environment’’. 

Nyama zozote zile zinapoliwa huwa zinasababisha kuwepo na kiwango kiwango kikubwa sana cha asidi, au hii pia huitwa ‘’low pH’’. Hii ni kwasababu siku zote nyama hupelekea uzalishaji wa madini ya sufur, phosphorus, Nitrites, hasa processed meats au kiwango kikubwa sana Cha nyama. Haya madini yametapakaa kwenye misuli ya nyama. 

Pia kutokana na Nyama kuwa na protini nyingi sana ambazo amino acids zake zina sulfur. Hizi sulfur sifa yake kubwa ni kuwa, kipindi cha matendo ya kibiolojia ya umeng’enyaji wake, huzalisha asidi inayoitwa ‘’sulfuric acids’’. Hizi zikiambatana na chembechembe nyingi za asidi ‘’acidic metabolites’’ husababisha kuwa na mazingira hatari sana ya asidi kwenye mfumo wa chakula ‘’low pH’’, na suluhisho pekee la mwili kutatua hili tatizo huwa ni kuzalisha madini ya calcium ili yaje kubalansi hizi chaji kupunguza haya madhara ya asidi. 

 Calcium zinatoka wapi? Zinatolewa kutoka kwenye mifupa. Mwili unatatua tatizo kubwa kabisa la uasidi kwa kuendelea kumeng’enya mifupa. na hiki kitendo kinaitwa ‘’osteoporosis’’. Kumbuka unaposema hii nyama ina protini nyingi sana, ndivyo unavyosema hii nyama ina amino acids nyingi zaidi, na ndivyo unavyosema hii nyama itafyonza calcium zangu nyingi zaidi kutoka kwenye mifupa.

Unapokula nyama tulishaona kuwa unaongeza kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma yanayotoka kwenye damu yaani ‘’haem iron’’. Sasa basi, haya madini yanapofika kwenye utumbo. Ile sehemu ambayo ilipaswa madini ya calcium yaweze kupita, huwa hawa jamaa wa chuma wanang’ang’ania. Na huu ushindani hupelekea madini mengi sana ya calcium kushindwa kupita kutokana na uwingi wa madini chuma ‘’haem iron’’. Hii moja kwa moja humfanya mla nyama kuwa na upungufu wa madini ya calcium, hata kama atakuwa anakula vyakula vyenye calcium.

MWANAMKE NA NYAMA

Mwanamke siku zote huwa hana mifupa mikubwa kama ilivyo kwa mwanaume, na kitendo cha kuwa na mifupa midogo humhitaji kuwa makini sana na bidhaa zinazoweza muathiri kiwango chake cha ‘’calcium’’. wanawake hupoteza kiwango kikubwa sana cha ‘’calcium’’ kwa ajili ya Watoto wanapokuwa tumboni, mifupa yote ya mtoto inatokana na calcium kutoka kwa mama, na hupoteza pia calcium kupitia kunyonyesha maziwa. Wanawake wanahitaji kiasi sana katika ulaji wa nyama.

Rejea part 2 kuelewa zaidi asili ya mgogoro huu wa ulaji wa Nyama dhidi ya ulaji wa Mimea#