Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

Usahihi wa Ellen G White Kuhusu Ulaji wa Mimea zaidi Kisayansi

Kwanini Ellen G White alikuwa sahihi kuhusu afya kupitia mbogamboga?

Kwanini Ellen G White alikuwa sahihi kuhusu afya kupitia mbogamboga?


Part 1

Katika kitabu changu cha historia ya magonjwa, nilieleza kwa kina sana kuwa historia za magonjwa zote zinaonyesha magonjwa kuanza kushamiri hasa baada ya Kilimo. Nilieleza kuwa Kilimo cha Mimea kiliharibu sana ardhi kwa kuharibu balansi ya madini kwa kufanya iwepo aina moja tu ya mazao, jambo ambalo lilipelekea maelfu ya bakteria, fangasi, na wadudu wengine wa ardhi kufa sana, na hasa pia kutokana na ardhi kusafishwa msimu wa kilimo kwa kufyekwa, au kuchomwa moto, na kufanya jua kuwa kali hata wengi wa vimelea kufa. Hii ilianza kupelekea aina ya vimelea sugu tu kuanza kuishi na kuanza kushamiri.

Kwa kuwa Kilimo kilihitaji sana msaada wa Wanyama, kwa lengo la kupata nguvu ya kulimia na mbolea, huu ulikuwa mwanzo wa kufuga Wanyama wengi kwenye eneo dogo. Hapa yalijitokeza matatizo yafuatayo: kwa kuwa marazote vimelea huishi kwenye kinyesi, matumizi ya mbolea kwenye mimea yalianza kufanya bakteria wengi zaidi kuanza kuwa karibu na chakula cha viumbe, sio chini ya ardhi, bali juu ya ardhi (vimelea wengi hupenda kinyesi na hufa kwenye oksijeni, na ndiyo maana usafi huwaua, lakini uvundo wenye ammonia, au methane huwashamirisha). Sasa basi, matumizi ya mbolea yaliwafanya wale vimelea sugu kuanza kuwa karibu zaidi na wanyama. (kwa kufuga Wanyama kinyesi kingi sana chenye vimelea huwa Pamoja, tofauti na mwituni ambapo huwezi kuta vinyesi vimekusanyika eneo moja)

Tatizo la pili, Wanyama wengi kufugwa kwenye eneo moja kuliwaongezea stress, kuliwafanya wazaliane wao kwa wao ‘’inbreeding’’, jambo lililowapunguzia zaidi kinga, na huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa vimelea sugu kuingia katika miili ya viumbe, na kuanza kushambulia tishu zilizoathirika mpaka zilizo hai tofauti na asili yao ya kushamiri katika vitu vilivyooza tu. Huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa magonjwa kuanza kwa Wanyama.

Stori haikuishia hapo tu, kwa kuendelea kusafisha mapori na kuandaa mashamba, uoto ulizidi kuathirika na Wanyama wadogo wengi, Pamoja na wadudu wengi walizidi kupoteza mimea, minyoo, na vyakula kwa ujumla. Hii iliwafanya na wao kutegemea zaidi mazao ya binadamu, jambo ambalo binadamu baadae alilipambania kwa kutumia dawa za wadudu, lakini hata hivyo, idadi ya viumbe wapori ilizidi kuvutwa kuwa karibu zaidi na binadamu ili kujipatia vyakula. Na huu ukawa mwanzo wa pili wa magonjwa ya mbali kuvutwa karibu na mwanadamu.

Vyanzo vikubwa vyote huonyesha kuwa magonjwa mengi sana yalianzia kwa kilimo, na Wanyama. Hata leo magonjwa mengi ya kuambukiza huwa na uhusiano wa moja kwa moja kati ya binadamu na Wanyama ‘’Zoonosis’’. Tafiti zinaonyesha Uhai wa watu karne mbili nyuma ulikuwa mfupi sana, sababu kubwa zaidi ilikuwa ni magonjwa ya kuambukiza. Kitendo cha kukosekana kwa madawa ya ‘’Antibiotics’’ kabla ya Vita ya pili ya dunia, kilipelekea watu wengi kuishi wastani wa miaka 30 mpaka 40 kutokana na kufa kwa mashambulizi ya vimelea hawa. Ushauri wa Ellen G White kisayansi ulikuwa sahihi sana, na inafahamika hata leo kuwa hata tamaduni za kale za Wayahudi kunawa hata kutawaza miguu, utaratibu uliokuwa hata kwa Waislamu, ulilenga sana kujisafisha kujikinga dhidi ya mashambulizi ya magonjwa haya ya kuambukiza. Tazama picha chini kuhusu magonjwa na uhusiano wao na Wanyama.

Unaweza gundua namna magonjwa yote yaliyotesa zaidi binadamu yalihusiana zaidi na uhusiano wa vimelea, Wanyama na binadamu, na ulaji wa nyama ulikuwa ndiyo njia pekee kubwa zaidi ya kuwaingiza mwilini. Kwa karne ya 19, na karne ya 20, ambapo Ellen G White alizaliwa hata kufa, Takwimu zinaonyesha magonjwa yaliyoua zaidi yalikuwa ni : 

  1. Tuberculosis (vifo zaidi ya Bilioni 1)
  2. Smallpox (Vifo zaidi ya milioni 500) 
  3. Spanish Influenza (Vifo zaidi ya milioni 100)
  4. Kipindupindu ‘’cholera’’ 
  5. UKIMWI uliohusiana sana na nyani 
  6. Malaria 
  7. Typhus 
  8. Yellow fever 
  9. Diptheria 
  10. Polio 
  11. Measles, na Whooping cough

Hata leo magonjwa mengi ya bakteria kama Salmonella, E. Coli, Campylobacter, n.k. yote yanahusiana sana na Wanyama. Kuna kila sababu ya Ellen G White kuhamasisha mtazamo wa afya bora kupitia ulaji zaidi wa mimea, hasa kwa karne zake.

Part 2

Teknolojia za kilimo ambazo zilihamasisha zaidi kuchanganya aina Fulani za mimea zaidi ‘’selective breeding’’, ili kutengeneza mazao ambao yatakuwa na wanga nyingi zaidi, malaini sana kuliko yasiyo na kambakamba nyingi sana, yalipelekea kushamiri kwa vyakula vingi sana vya wanga na laini. Teknolojia ilipelekea kushamiri kwa mashamba ya ngano, mahindi, mpunga, mihogo mikubwa, soya, matunda mbalimbali hasa yanayozaa mapema, na yenye mbegu kidogo. Mazao haya kwa kuwa yalikuwa matamu sana na laini, wadudu na magugu waliyashambulia sana, hapo ndipo ilipoibuka teknolojia ya kutengeneza dawa za kuulia wadudu, au magugu ‘’pesticides’’. Lakini pia kwa kuwa ardhi haikuwa na rutuba tena, basi zilizaliwa teknolojia tatu, ya kwanza ilikuwa ya kutengeneza mbolea za kisasa zenye madini maalumu tu, mfano ‘’NPK’’, pili iliibuka teknolojia ya kutengeneza homoni za mimea kuiboost, na tatu iliibuka teknolojia ya kubadilisha mimea kijenetikia ili ikue haraka, isihitaji madini mengi, na iwe na kemikali za moja kwa moja za kuua wadudu bila kutegemea madawa ya wadudu, mfano mazao ya GMO.

Dunia sasa haina shida tena ya magonjwa ya vimelea ambavyo vilikuwa ni Mzimu mkubwa katika ulimwengu wa karne ya kina Ellen G White. Sasa Dunia inaingia katika zama ambazo sumu kubwa zaidi ni bidhaa za mimea kama Soda, mikate, juisi, biskuti, mafuta ya mbegu, n.k. vitu ambavyo awali vilikuwa ndiyo Dawa. Madini sumu mfano yaliyo katika Round Up ‘’Glyphosate’’ huchubua madini chuma mwilini ‘’metal chelation’’ na kuharibu mfumo mzima wa afya. Sukari nyingi za kwenye vyakula vya Wanga ambavyo zamani vilikuwa asilia vyenye kambakamba, sasa hivi vimekuwa laini kama Biskuti, na watu wanaweza kula mpaka zaidi ya gramu 500g za ugali kwa siku. Mafuta ya Wanyama ambayo yameshaitwa shetani hayapo tena, na sasa watu wanatumia zaidi mafuta ya mbegu ‘’corn oil, sunflower, etc’’. Dunia sasa imebadilika, Magonjwa yanayoua zaidi ni;

  1. Moyo ‘’ischemic heart disease’’
  2. COVID-19
  3. Moyo ‘’Stroke’’
  4. Mapafu ‘’Chronic Obstructive Pulmonary Disease’’
  5. Mapafu ‘’Lower Respiratory infections’’
  6. Ubongo ‘’Alzheimer’s na Dementia’’
  7. Kisukari ‘’Diabetes Mellitus’’
  8. UKIMWI
  9. Shida za Kuharisha ‘’Kipindupindu, Rotavurus’’
  10. Shida za Figo

Unaweza ona tofauti kubwa iliyopo kati ya karne hizi mbili. Magonjwa yote yanayoua zaidi zama hizi ni matokeo ya mifumo iliyonyuma ya ulaji, madawa, mtindo wa maisha, na mazingira ya kisasa. Katika magonjwa haya kama ukipangilia visababishi vikuu zaidi vitakuwa kama ifuatavyo;

  • Ulaji sana wa vyakula vya sukari na wanga
  • Kushinda sana na mianga wakati wa usiku
  • Shughuli za kukaa sana chini bila kutumia misuli
  • Kushuka kwa kinga kutokana na kutopata vyakula vya asili, utulivu wa mwili, na akili 
  • Viburudisho hatarishi kwa afya kama pombe, sigara, na mazingira yenye mionzi ‘’nnemf’’
  • Ongezeko kubwa la sumu za madawa, chanjo, dawa za kilimo, na vitunzaji vya bidhaa za kisasa
  • Mfumo wa afya ulioegemea matibabu kuliko kinga

Katika sababu hizi zote hakuna hata moja ambayo inahusiana na ulaji wa nyama, lakini zipo nyingi zaidi zilizoegemea utumiaji wa bidhaa za mimea ambazo zimechochewa kuwa na misisimko mikubwa ya Ladha na kuwa na hatari kwa afya.