SUKARI YA MATUNDA INA KAZI GANI?
Je Matunda kama Matikiti, Maboga, au Maembe hunufaikaje na sukari yake?
Ni kame vile matunda hutengeneza chakula ambacho huwa hayakihitaji, hata watu baadhi wakahisi hutengeneza kwa ajili ya Wanyama, si kweli. Mmea hutengeneza chakula katika hatua ya kwanza kama Wanga kutoka kwenye mwanga wa jua, maji, na hewa ya kaboni dioksaidi katika majani. Maeneo mbalimbali ya mimea hasa mizizi, na mashina, huwa hayana ukijani hivyo hutegemea moja kwa moja chakula hiki cha wanga kilichokwisha tengenezwa katika majani. Mimea hutengeneza chakula chake toka kwenye mwanga wakati wa siku, na hutumia mwanga moja kwa moja kupata nishati wakati wa siku. Unapofika usiku, mimea hutegemea chakula kilichokwisha tengenezwa mchana, na hukivunja kwa kutumia Oksijeni ambayo huivuta wakati wa usiku kama ambavyo seli za Wanyama hufanya kupitia matendo kama ‘’TCA, na ECT’’, katika seli ‘’Mitochondria’’.
Mmea hujaza chakula cha sukari kuzunguka mbegu ili tunda litakapoiva au komaa hata likaanguka, sukari hiyo ndiyo iwe chakula cha mbegu ambazo huwa haziwezi kujitengenezea chakula zenyewe toka kwenye mwanga wa jua, kwa kuwa huwa hazina majani. Sukari au nyama za matunda kuzunguka mbegu huwa ni kama maziwa kwa mtoto. Matunda yanapooza pia hutengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya mbegu kukua, unyevunyevu, na uvundo ambao hutoa kaboni dioksaidi nyingi sana kwa ajili ya majani madogo.
Hivyo kipindi watu hujihalalishia sukari za mimea, ambazo ndizo msingi wa vyakula vyote vikuu vya wanga vinavyoliwa zaidi, yaani Mpunga, Mahindi, Ngano, uwele, n.k. kwa upande mwingine hizi zote ni mbegu, ni Watoto wa mimea, na mimea haipo radhi kupoteza Watoto hawa, na huu ndiyo msingi wa siri ifuatayo ya uharibifu.
..To be continued
Kumbuka kutokana na asili ya sukari ya matunda kuwa katikati ya kambakamba "fibers" nyingi, huwa Haina madhara Kwa mlaji, walakini tu isifanaywe juisi. Kwa kufanywa juisi kambakamba "fibers" zote huondolewa na kupelekea changamoto za "insulin".
Ni muhimu kula matunda Kwa Msimu na mazingira yake ya asilia ili kutokuwa mhanga wa viwango vya sukari kupita wastani.


Join the conversation