SIRI YA WEKUNDU WA NYANYA
Kwanini Nyanya huwa nyekundu zikiiva?
Nyanya huwa za kijani zinapokuwa mbichi kumaanisha huwa zinahitaji chrolophyl nyingi kutengeneza chakula kwa ajili ya mtoto wake, au mbegu zake, kutoka kwenye jua. Badala ya kuiona nyanya ni sawa na ungekuwa ukiiona Mimba tumboni mwa mama. Mbegu au mtoto anapokuwa amekamilika, huwa hakuna uhitaji zaidi wa kutengeneza chakula zaidi, huwa kuna uhitaji wa kumzaa, au kuzisambaza hizi mbegu.
Nyanya maranyingi unapofikia wakati huu wa kuzisambaza hizi mbegu pia huwa zimeshachoka sana, ni kama vile viumbe wengi wanapozeeka baada ya kuzaa na kulea. Kiwango hiki cha stress, na uhitaji wa kuzisambaza hizi mbegu, na upungufu wa chrolophyl za kijani zilizokuwa zikitengeneza chakula cha mbegu (nyama ya nyanya), hufanya mmea kuchochea kuonekana kwa chembechembe zinazoitwa ‘’Anthocyanins’’. Hizi huwa na rangi ya wekundu zikiwa kwanza ni ‘’Antioxidants’’, au vizuia mwanga wa blue usidhuru mbegu au Watoto wake. Pia huwa nyekundu kwa kuwa mawimbi ya wekundu ni marefu sana kati ya 630-750nm, hivyo kuonekana hata kwa kitu kilicho mbali zaidi, hii ndiyo sababu jua la asubuhi huonekana jekundu, sababu ni kuwa huwa linakuwa mbali sana. Mimea hutumia hii rangi kuwaita wadudu na Wanyama walio mbali waje kuila nyanya na kusambaza mbegu zake.
Kwa hiyo kipindi wataalamu walishe huamasisha kuwa ni vizuri sana kula rangi hizi, kwa kuwa huwa na chembechembe hizi za afya ambazo huziita ‘’Polyphenols’’, ni kweli kuwa huwa zinasaidia sana mwili kupambana dhidi ya kemikali sumu ‘’free radicals’’, lakini ni kweli kuwa mmea uliziweka kama ‘’antioxidants’’ kwa ajili yake wenyewe ambao ndiyo hushinda juani siku nzima.
Utamu wa NYANYA hutokana na kiwango chake kikubwa Cha protini "amino acid" inayoitwa "Glutamate', sifa yake kubwa ya kiafya hutokana na kiwango chake kikubwa Cha Vitamin C, Vitamin K, vitamin B, na uwepo wa anti oxidants 'Lycopene'



Join the conversation