Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

UNAZIELEWA RANGI ZA MIMEA?

Siri ya rangi za Mimea

Rangi ya Kijani

Mimea huwa na rangi ya kijani kutokana na uwepo wa chembechembe zinazoitwa ‘’Chrolophyl’’. Hizi chembechembe huwa zina kazi moja kubwa zaidi ya kufyonza miale ya mwanga, hasa mwanga mwekundu ‘’red light-620-750nm’’, na mwanga wa blue ‘’blue light-430-450nm’’, kutoka katika jua. Chrolophyl kupitia madini ya magnesium yaliyo ndani yake hufyonza miale hii na kutengeneza sukari, au wanga, kupitia kitendo kinachoitwa ‘’photosynthesis’’. Chrolophyl inafanana kabisa kiumbile na chembechembe inayobeba Oksijeni katika damu inayoitwa ‘’Hemoglobin ‘’Hb’’, tofauti pekee ni kuwa; Hb huwa na madini chuma ‘’Fe’’ Katikati, na hivyo hufyonza miale ya mwanga wa blue, lakini hutoa nje mwanga mwekundu ‘’Red light’’, kuifanya damu kuonekana nyekundu. kipindi ‘’Chrolophyl’’ hutoa nje mwanga wa Kijani 500-550nm. Hii ndiyo sababu Mimea huwa inaonekana zaidi kwa rangi ya kijani, huku Wanyama wakionekana zaidi kwa rangi nyekundu.

Kadri Mmea unavyoonekana zaidi wa kijani, ndivyo unavyokuwa na chrolophyl nyingi zaidi. Na mimea ambayo huwa ya kijani sana, ina maana pia huwa na magnesium nyingi sana. Na hii ndiyo sababu, Mimea kama Spinach na Parachichi huwa na kiwango kikubwa sana cha madini ya Magnesium. Sababu kubwa ni kuwa huwa na ukijani sana kutokana na chrolophyl nyingi. Kiwango cha Vitamin B zote nane, huwa ni kikubwa sana kwa Parachichi ukilinganisha na matunda mengine yote, na hata kwa spinach, sababu kubwa ni kuwa; kwa kuwa mimea hii huwa na matendo makubwa sana ya ‘’Photosynthesis’’, basi huitaji kuwa na vichakati ‘’enzymes’’ nyingi sana. Na mimea hutumia hizi Vitamin B kwake kama mashine zake za kuwezesha metabolikia za kujitengenezea chakula chake, sio kwa ajili yako, mbeleni tutaliona zaidi hili.

Mmea au jani linapokauka huwa lina rangi ya njano au kahawia kwa kuwa, kiwango cha maji kinapopungua ndani ya seli ya mmea matendo ya ‘’Photosynthesis’’ hufeli, na hivyo, chrolophyl huvunjwa, na hii huweza kutokea pia madini ya Nitrogen yanapopungua katika ardhi, maana haya ndiyo huwa yakizingira ile magnesium katika chrolophyl. Haya yanapotokea, mmea sasa kwa kuishiwa hizi chrolophyl zenye rangi ya ukijani, huanza kung’ara kwa kuonyesha mwonekano wake wa ndani ambao huwa ni wa rangi ya njano, au kahawia, ambao huwa ni rangi za chembechembe zinazoitwa ‘’Carotenoids’’, hizi huwa ni kama vizuia madhara ya UV, au mwanga wa blue kuleta madhara ‘’sunscreens’’. Na zinapoonekana huashiria mmea umezidiwa, unajilinda, au umeshakamilisha kazi yake ya kuunda chakula. Wataalamu wa kilimo huipatia mimea yenye rangi za unjano mbolea za ‘’NPK’’ zenye wastani mkubwa wa N-Nitrogen ili kuirejeshea Chrolophyll uwezo wake. 

Kipindi unapoamini kuwa Rangi ya kijani ni bora sana katika mlo wako, ‘’Eat greeny’’, kumbuka mmea huweka rangi hiyo, na chembechembe zingine zote zinazoambatana nayo kwa ajli yake wenyewe.

Rangi za Wekundu-njano


Nani asiyependa rangi za Matunda karibia asilimia 75% yanapoiva? Wengi wanaposikia mchanganyiko mzuri wa mbogamboga hushindwa kujizuia kufikiria rangi za unjano kama za Karoti, wekundu wa Nyanya, na hata rangi za machungwa ‘’orange’’, na ukahawia wa njano kama uliopo kwa viazi vitamu. Lakini swali kubwa bado hurudi kuwa, je rangi hizi zina maana gani? Je ni kwamba maembe hukuita ukayachume kuwa yameiva ili uyaue?

Mimea hutumia rangi za njano, ambazo huzionyesha kupitia chembechembe zake za ‘’Carotenoid’’. Chembechembe hizi huwa pia zikifahamika kwa jina la ‘’Retinol’’, ambazo ndizo huzifanya kuwa chanzo kikubwa sana cha Vitamin A. sifa kubwa ya chembechembe hizi za njano ni kuwa, rangi za njano za mawimbi kati ya 550-580nm hufyonza mawimbi ya blue ya 430-450nm na kuzuia madhara ya mawimbi ya blue kusababisha kifo cha seli. Siku zote kitu kinachoua huwa ni kitendo kinachoitwa ‘’oxidation’’. 

Kitendo hiki ndicho hufanya ukiweka tunda juani, au chakula usipokifunika kikapigwa na mwanga kuharibika haraka zaidi. Mwanga wa jua uliosheheni mawimbi ya blue husisimua chembechembe za elektroni katika chrolophyl na mmea unapozidiwa uwezo, chembechembe hizi hupelekea kushamiri kwa kemikali sumu ‘’free radicas’’, ambazo huitwa pia ‘’Reactive oxygen species’’, na madhara yake, hupelekea mitambo ya nishati ya seli kufa ‘’mitochondria’’. Hivyo rangi za njano kazi yake kubwa huwa ni kuzuia miale hii. Unaweza kugundua siri zifuatazo;

..To be continued