Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

MAJI NA DAWA, TIBA KUU ZA MAGONJWA SUGU

 


UTANGULIZI

Tiba ya Maji, Mwanga na Usumaku ni kitabu cha upekee sana katika vitabu vya mfululizo wa injili ya sayansi. Kitabu hiki kinaangazia namna ambavyo matatizo mengi zaidi yanaweza tatuliwa kwa kutumia nguzo kuu za asili, yaani maji, mwanga, na usumaku. Kitabu hiki kinaelezea pia namna magonjwa mengi sana yanavyoibuka kama madhara katika uhusiano wa nguzo hizi kuu tatu, na miili ya viumbe, aidha kutokana na ujinga, au kutokana na mifumo hatarishi ya maisha.

Kitabu hiki hakina malengo yoyote ya utabibu kwa wasomaji wake, kitabu hiki hakiwezi chukua nafasi ya daktari. Kitabu hiki kimejikita katika kutoa msingi mpana zaidi wa elimu ya kujikinga na magonjwa, kuelewa sababu za magonjwa zilizojificha kwa mtazamo wa kawaida wa taaluma za afya, kutambua maana za dalili za magonjwa mengi hasa sugu na ya akili, kutambua namna ya kurekebisha changamoto za afya kulingana na elimu ya kujua namna ya kuhusianisha vyema mwili, na nguzo kuu tatu za afya, na mwisho, kujikinga, na hata kutatua moja kwa moja matatizo kadhaa yaliyo katika hatua za awali, au yasiyo katika hatua hatarishi zaidi za magonjwa.

Uandishi wa kitabu hiki umetokana zaidi na hamu ya mwandishi kutamani kuona idadi kubwa ya watu wakielewa lugha ya asili ya utendaji wa mwili, yaani fiziolojia, inavyozungumza na nguzo kuu tatu za uhai, yaani maji, mwanga na usumaku. Viumbe wote walianzia toka katika maji, awali Dunia ilianza tokea katika maji, na vivyo hivyo viumbe wote huzaliwa tokea tumboni kwenye Bahari ya maji ya plasenta. Maji na mwanga marazote vimekuwa sambamba, aidha katika uumbaji wa Mungu wa siku sita, au katika mabadiliko ya awali sana ya Big-bang. Mimea ambayo ndiyo chanzo kikuu cha nishati, hutengeneza chakula moja kwa moja kutoka katika mwanga, maji, na hewa. Viumbe wote wamedisainiwa kufuata nguzo hizi kuu tatu kama tutakavyoona.
Mwishoni mwa kitabu hiki, matarajio ya mwandishi ni kuona wasomaji wakiwa na uelewa mpana sana, hasa dhidi ya matumizi hatarishi ya madawa, na njia zote hafifu dhidi ya kupambana na magonjwa. Magonjwa ni matokeo ya mahesabu mabaya ya kiafya, kutopona magonjwa ni aidha kuendelea kushikilia sumu kama dawa, au kutokuwa na maarifa juu ya changamoto zinazoleta dhiki husika. Kitabu hiki hakiwezi toa majibu ya changamoto zote, na wala hakijalenga hilo, ila kimelenga kutoa msingi mpana sana wa kiafya unaoweza kusaidia kupambana na magonjwa mengi sana yanayofanana tabia, na kujenga kesho iliyobora zaidi kwa kizazi kijacho cha Watoto waliopo, na wanaoendelea kuzaliwa.

Matumizi ya Lugha katika kitabu hiki yanahusisha lugha zote, yaani, Kiswahili, na kiingereza kwa misamiati ya kisayansi. Kitabu hiki kinahusisha uchambuzi wa sayansi wa kina katika baadhi ya sehemu, lakini kwa sehemu kubwa zaidi kimejikita katika kutumia lugha nyepesi kueleweka kwa watu wote. Sehemu ambazo kimehusisha uchambuzi wa kina kisayansi, lengo kubwa ni kutoa mwangaza kwa wasomi wengi wa taaluma za afya, na sayansi, kuweza kuelewa undani wa taarifa ambazo wanaweza kuwa wamefichwa, au wametengenezewa falsafa ya kuzipuuzia, hili limelenga sana kugundua msukumo wa kiviwanda, biashara, na hata siasa katika kupuuzia kwa mara nyingi afya za watu, hasa kutokana na kutamani zaidi nguvu za kiutawala, kutokuwa na upendo, na kutumia ujinga, ukatili, na ujanja kama silaha.

Imani ya mwandishi ni kuwa Mungu yupo, na anawapenda sana watu wake. tena kiasi hata cha kumtumia yeye kuweza kumsaidia kila msomaji wa kitabu hiki. Mwandishi anapokea maoni ya namna zote juu ya maboresho ya kitabu hiki, tamaa kubwa ya mwandishi ni kuona mabadiliko kwa kila msomaji baada ya kujifunza kazi hii, na kusapoti usambazaji wa maarifa haya. Mwandishi hana upande wowote kimtazamo juu ya chanzo cha changamoto zitakazo jadiliwa katika kitabu
hiki, ila anaamini yupo Shetani anayewatumia watu, na pia anaamini Sayansi ni injili ya pekee ya mwisho ya kuikomboa jamii kama Mungu alivyoibariki kazi hii.


SHUKURANI

Namshukuru sana Mungu wangu kwa kazi hii, maarifa ya kazi hii hayakuwa rahisi hata kidogo kuyaelewa. Shukurani kubwa sana ziende kwa familia yangu, Mama yangu Dementina Fransis Mkote, na Baba yangu Godwin Efraim Shoo. Sapoti kubwa sana kwa familia yangu, shangazi yangu Lilian Shoo, rafiki zangu Dr. Mihambo Masasila, Dr. Magesa Matiku, Sir. Wyclife Tuarira, Hort. Ernest B Jonass, Dr.Kim Mkufi, Dr. Ntemi Joseph, na wengineo wengi.

Shukurani kubwa sana pia iende kwa wataalamu wengi sana wa afya ambao nimeweza kupitia kazi zao nyingi sana, na hasa wanasayansi wengi sana. Dr. Doug Wallace, Dr. Jack kruse, Dr. Batmanghelidj, Dr. Zack Bush, Dr. Jason Fung, Dr. Zach Murphy, Dr. Paul Mason, Dr. Gerald Pollack, Dr. Thomas Seyfried, Dr. Stephanie sereff, Dr. Allessio Fasano, Dr. Bruce Lipton, Dr. Nasha Winters, Dr. Pall, Dr. Warburg, Dr. Walter Veith, Barbara O.neil, Dr.berg, Dr. Robert Lustig, Dr. Wambura, Dr. Malago, Dr. Barnaba, Dr. Gaymarry.


YALIYOMO

UTANGULIZI............................................................................................. 3

SHUKURANI ............................................................................................. 5

SURA YA KWANZA ................................................................................. 12

LUGHA ZA MAGONJWA..................................................................... 12

Utangulizi ...................................................................................... 12

Siri ya mawasiliano........................................................................ 13

SURA YA PILI .......................................................................................... 15

HOMA ‘’FEVER’’................................................................................. 15

Lengo la Lugha ya Homa ............................................................... 15

Sayansi ya Homa ........................................................................... 15

Homa na Kutohisi Hamu ya Kula ................................................... 16

Madawa yanayotibu Homa ........................................................... 17

LUGHA ISIYOELEWEKA YA HOMA.................................................. 18

Hatari Za Kushindana na Homa kwa Madawa .............................. 20

Ushauri Unapopata Homa ............................................................ 21

SURA YA TATU........................................................................................ 23

MAUMIVU YA VIUNGO ‘’JOINT PAIN’’ ............................................... 23

Utangulizi ...................................................................................... 23

Inayojulikana katika Maumivu Mengi ya Viungo .......................... 24

LUGHA ISIYOJULIKANA YA MAUMIVU YA VIUNGO ....................... 25

BADALA YA KUSEMA GOUTS ......................................................... 27

Madawa ya Kutibu Shida za Maungio’’Joint’’ ............................... 28

KUJAA KWA MAJI MIGUUNI NA MWILINI ‘’EDEMA’’ .................... 30
Sayansi ya Kujaa Maji Miguuni...................................................... 30

Usilojua Kuhusu Chumvi na Kujaa Maji......................................... 32

USHAURI KWA SHIDA ZA MAUNGIO NA KUJAA MAJI MIGUUNI .. 33

SURA YA NNE......................................................................................... 38

SHIDA ZA MOYO NA PRESHA............................................................. 38

Utangulizi ...................................................................................... 38

UNAPOSEMA NINA PRESHA ‘’B.P’’- HYPERTENSION .................... 39

Sayansi ya Presha kubwa ‘’Hypertension’’.................................... 40

Wanavyotibu Hypertension .......................................................... 42

LUGHA ILIYOJIFICHA YA MAANA YA PRESHA JUU – HYPERTENSION
....................................................................................................... 43

Ushauri Juu ya Matibabu ya Presha-Hypertension....................... 45

SHIDA YA KUTANUKA KWA MOYO ‘’CONGESTIVE HEART FAILURE’’
....................................................................................................... 46

Wanavyotibiwa watu wenye tatizo la Kutanuka Moyo ................. 48

Ushauri juu ya Matibabu............................................................... 48

TATIZO LA MISHIPA YA MOYO ‘’CORONARY HEART DISEASE’’ ...... 49

Maumivu ya Kifua ‘’Angina Pectoris’’............................................ 49

Mshtuko wa Moyo ‘’Myocardial infarction-Heart Attack’’............ 50

Kujaa kwa Mafuta katika Mishipa ya Artery ‘’Atherosclerosis’’ .... 50

Mshtuko ‘’Stroke’’ ......................................................................... 51

Wanavyotibu Shida hii ya Moyo.................................................... 52

LUGHA ISIYOFAHAMIKA YA SHIDA ZA MAFUTA NA MOYO ........... 53

Usilojua kuhusu mafuta ................................................................ 53
Ushauri wa ulaji wa mafuta ya Wanyama na mimea.................... 54

Shida za Mafuta na Moyo ............................................................. 54

SEHEMU YA KWANZA YA MAFUTA ................................................ 55

Vinywaji na Vyakula vya sukari na pombe .................................... 55

Kwanini usilaumu cholesterols na ulaumu mafuta yako ya kula .. 58

Mafuta ya mishipani ni mpango wa mwili .................................... 58

Insulini inavyotambua shida ya maji ............................................. 59

Nini Maana ya Mwili Kibonge ....................................................... 60

Kuhusu pombe .............................................................................. 61

SEHEMU YA PILI YA MAFUTA ........................................................ 62

Kushinda na mionzi ya vifaa vya Kielektroniki usiku, na kuchelewa kuamka.......................................................................................... 62

Chanzo cha Shida za Mianga Kielektroniki.................................... 65

Mwanga na Mitochondria............................................................. 67

Mwanga na Kujaa Mafuta ............................................................. 69

USHAURI KUHUSU SHIDA ZA MAFUTA NA MOYO......................... 71

Maji kama tiba ya Shida za mafuta na Moyo ................................ 72

Kuamka asubuhi kama tiba ya Mafuta mengi na shida za moyo .. 73

Baridi ya asubuhi kama Tiba ya Moyo .......................................... 73

Kutotumia mianga ya kisasa usiku kama tiba ya moyo na mafuta 74

Kutotumia chumvi ya mezani, kupunguza mafuta ya mimea, na kupunguza sukari .......................................................................... 74

SURA YA TANO....................................................................................... 76
SHIDA ZA MAUMIVU YA TUMBO NA VIDONDA VYA TUMBO
‘’ULCERS’’ .......................................................................................... 76

Utangulizi ...................................................................................... 76

Sio Ugonjwa ni Vidonda ................................................................ 76

Kwanini Haviponi na unatumia dawa?.......................................... 80

Shida za dawa za Kuua Helicobacter pylori................................... 81

Vidonda vinapokomaa .................................................................. 81

Dawa sahihi ya Vidonda vya tumbo .............................................. 82

Ushauri wa Kinga katika Mfumo wa Chakula................................ 84

SURA YA SITA ......................................................................................... 86

SHIDA ZA ALLERGY NA MWILI KUJISHAMBULIA ‘’AUTOIMMUNE DISEASES’’ ......................................................................................... 86

Utangulizi ...................................................................................... 86

Sayansi Fupi................................................................................... 86

LUGHA YA MAGONJWA YA ALLERGY NA MWILI KUJISHAMBULIA
‘’AUTOIMMUNE’’........................................................................... 89

Ushauri wa Matibabu ya Shida hizi ............................................... 92

SURA YA SITA ......................................................................................... 93

SHIDA ZA MAGONJWA YA NGOZI NA MWONEKANO WA KUZEEKA
‘’AGING’’ ............................................................................................ 93

Utangulizi ...................................................................................... 93

Sayansi ya Shida za Ngozi .............................................................. 94

LUGHA YA SHIDA ZA NGOZI ISIYOFAHAMIKA NA WENGI.............. 96

Matumizi ya Sabuni, ‘’Cleansers, antimicrobial lotions, n.k’’ ....... 96
Ulaji Uliopitiliza wa Protini za Wanyama, Mboga zenye mabaki ya
RoundUp na Ngozi mbaya............................................................. 98

Ulaji wa Bidhaa za Sukari na Kushamiri kwa Chunusi ................... 99

Unywaji wa Maji na Afya ya Ngozi .............................................. 100

Epuka Maji yenye Chlorine.......................................................... 101

Sabuni na Maji ya Kuoga na Ngozi yako ...................................... 102

Mafuta ya Kujichubua na Ngozi yako .......................................... 103

Ukweli kuhusu Supplements za Mafuta na Vyakula juu ya Ngozi
..................................................................................................... 104

Stress, Collagen, na Afya ya Ngozi............................................... 105

Amka mapema, vaa nguo rahisi, ungana na asili kuboresha Ngozi yako ............................................................................................. 105

Wahi kulala, zima Taa, Simu, au Tv yako, Shusha Insulin, Boresha
Ngozi............................................................................................ 106

Ushauri kwa wagonjwa wa Ngozi................................................ 107

Vyakula bora kwa Shida za Ngozi ................................................ 107

Kuhusu Maziwa ........................................................................... 108

SURA YA SABA ..................................................................................... 110

SHIDA ZA UVIMBE ‘’INFLAMMATION’’ NA SARATANI ‘’CANCER’’ ... 110

Utangulizi .................................................................................... 110

Sayansi Fupi ya Saratani na Uvimbe............................................ 110

LUGHA YA SARATANI NA UVIMBE SUGU ISIYOELEWEKA ............ 113

Protini nyingi za Wanyama na saratani na uvimbe ..................... 114

Bidhaa za Viwandani, Pombe na Vyakula vya makopo ............... 115

Vifaa vya Kielektroniki na Mionzi ya Mitandao na saratani ........ 117
Madawa ya Kuulia Magugu, Wadudu, ‘’Pesticides’’ na Mazao za
GMO na Saratani ......................................................................... 118

Ushauri wa kuepukana na Saratani na Uvimbe Sugu ................. 120

SURA YA NANE .................................................................................... 122

SHIDA NA MAGONJWA YA UBONGO, KISAIKOLOJIA NA KIHOMONI
......................................................................................................... 122

Utangulizi .................................................................................... 122

LUGHA ISIYOELEWEKA YA SHIDA HIZI ZA UBONGO .................... 125

Ushauri kwa wagonjwa wa Magonjwa Sugu ya Ubongo ............ 127

SHIDA ZA KIHOMONI NA KISAIKOLOJIA ZA UBONGO ................. 128

LUGHA ISIYOELEWEKA YA SHIDA HIZI ZA KIHOMONI NA KISAIKOLOJIA ............................................................................... 129

USHAURI WA KUSHINDA MATATIZO YA KISAIKOLOJIA NA HOMONI
..................................................................................................... 133

Kunywa maji mengi ..................................................................... 133

Lala Mapema, Amka mapema .................................................... 135

Kula wanga halisi, kula kijani, protini na mafuta kidogo ya
wanyama na mafuta kidogo ya mbegu ....................................... 137

FALSAFA YA SHOO YA MAGONJWA YOTE ............................................ 138

Kuhusu References.............................................................................. 139
SURA YA KWANZA

LUGHA ZA MAGONJWA

Utangulizi

Asilimia ndogo sana ya watu wanatambua kuwa hisia zote unazozihisi unapokuwa unaumwa, huwa zinatengenezwa na mwili. Mwili hutengeneza hisia hizi ili ubongo wa mbele utambue kuwa upo katika hali mbaya na uweze kuchukua hatua. Hii ni namna ya kwanza kabisa ya maana ya lugha za magonjwa.

Pili, hisia na dalili nyingi sana za magonjwa hutengenezwa na mwili, ili kupambana na hali za magonjwa. Yaani, mwili ndiyo hutengeneza dalili nyingi sana za magonjwa, kuliko magonjwa yenyewe yanavyoweza kutengeneza dalili nyingi sana za magonjwa. Hivyo sasa, ni jukumu la ubongo kuelewa namna mwili wake unavyopambana na hali hizi za magonjwa, na sio kushindana nao.

tatu, dalili nyingi za magonjwa yanapokuwa yamekwisha shindikana, baada ya mapambano ya muda mrefu, hutokana sasa na magonjwa yenyewe kuuongoza mwili sawa na matakwa yake. katika hatua hii, mwili huwa unazungumza kidogo sana, au kuzungumza kupita inavyopaswa, au hata kutozungumza kabisa.

Vita kuu kati ya mwili na ugonjwa huwa katika kuongoza mfumo wa mawasiliano wa mwili. Mfumo wa mawasiliano wa mwili ndiyo huongoza kila tendo katika mwili wa kiumbe, kuanzia usambazaji wa virutubisho, misisimko ya utendaji, na uboreshwaji wa kiungo husika kwa kadri ya ukuaji na changamoto za kifiziolojia na kimazingira. Kunapokuwa na changamoto ndani ya mwili, kama vile sumu, vimelea, au shida yoyote ile, changamoto hizi huanza kuingilia utendaji wa kawaida wa mwili, kwa kuathiri mfumo mzima wa mawasiliano. na mwili sasa huanza kutoa taarifa maeneo mbalimbali ya mwili kuja kusaidia
kuondokana na shida hizi. Na taarifa hizi hutafsiriwa na ubongo, na hutafsiriwa na seli na mifumo mingine pia ya kinga za mwili.

Siri ya mawasiliano

Vita yoyote ile hulenga kushambulia mfumo wa mawasiliano wa wapinzani kwanza kabla ya kushambulia ngome husika. Maharamia hutamani sana kuwaangusha vichwa vya mawasaliano wa wapinzani wao, mfano, viongozi wakubwa zaidi wanaoongoza mawasiliano yote ya ngazi husika hushambuliwa sana. Raisi Donald Trump wa marekani mwaka 2024 alikoswa na shambulio la Risasi lililolenga kumuua, kama alivyouawa Raisi wao wa zamani JF-Kennedy. Tanzania kiongozi wa Upinzani Tundu Lissu aliponyeka kifo kwa shambulizi kubwa sana la risasi, Hayati Raisi wa Tanzania John Magufuli aliwahi lalamika kushambuliwa kwa sumu. Wenda Imani kubwa za kikristo na Uislamu zingeisha kwa shambulio la awali kabisa la waasisi kama Musa walipokuwa wadogo kabisa, au Yusufu. Yesu Kristo pia alishambuliwa kutakwa kuuwawa kama ilivyokuwa kwa musa tangia akiwa mdogo kabisa kwa agizo la herode la kuua Watoto wote wadogo wa kiume lililofanania na la farao. hata baada ya kusulubiwa msalabani, Warumi walifunga kaburi la Yesu, ku block mawasilano.

Vita ya pili ya dunia ilichochea sana ukuaji wa sayansi za anga, matumizi ya satalaiti yalishamiri baada tu ya vita kwa msaada wa wanasayansi kama Werner von Braun, mashirika makubwa ya nchi kama NASA na majeshi ya Anga kama US-Airforce, n.k. yalijimilikisha anga kama sehemu yao kuu ya kiulinzi, lengo likiwa utawala, hata leo, wanaotawala mawasiliano, sio tu matajiri wakubwa zaidi kama Elon Musk, au Mark Zuckerberg, au Bill Gates, pia ndiyo hutawala dunia.

Dawa nyingi za kuua vimelea, hata kwa mimea, hulenga zaidi kuathiri mifumo mikuu ya mwasailiano, kuanzia mifumo ya fahamu, mpaka mifumo ya jenetikia. Mfano, dawa zote zinazosaidia upasuaji
‘’anaesthesia’’, hukatisha ‘’block’’, mfumo wa fahamu aidha kwa kuzuia kusisimka kwa sensa za neva ‘’