Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

SAYANSI YA KUBADILISHA HALI ZA HEWA

    SAYANSI YA KUBADILISHA HALI ZA HEWA 

           ‘’Geoecological engineering’’

Limeandaliwa na Brighton Godwin Shoo toka SUA mwaka 2025 Februari. sio sehemu ya masomo yake ya Udaktari Chuoni, ni sehemu ya masomo yake ya Injili ya Sayansi. Ni sehemu ya sura ya kitabu kinachoitwa Sayansi na Lusifa.

Taaluma ya kubadilisha hali za hewa na kutengeneza mvua imekuwa maarufu sana zama hizi. Pia taaluma za kupooza joto la dunia zimekuwa maarufu sana zama hizi. Kumbuka taaluma hizi ndizo kwa kiingereza huitwa ‘’Geoecological engineering’’.

Lusifa Kama Nyoka

Miongoni mwa vitu ambavyo vimefanywa kwa siri sana kwa nyakati nyingi sana ni sanaa za kubadilisha hali za hewa. Ugunduzi wa sanaa hii ulianza zaidi karne ya 19, hasa baada ya mapinduzi makubwa sana ya taaluma za umeme, na usambazaji wa mionzi kwa umbali mrefu, ambao ulichochewa sana na injinia, wengi humwita mwanasayansi mwenye akili zaidi bwana Nicola Tesla. Huyu bana aligundua au hata kuchochea gunduzi nyingi na kubwa zaidi ikiwemo usambazaji wa umeme wa AC tunaoutumia katika kila teknolojia na majumbani mwetu, alichochea sana taaluma za usambazaji wa mionzi kama ya redio na WIfI, lakini pia hata mionzi ya X-Rays, na zingine nyingi zaidi ya 300. Alipokufa huyu bwana Serikali ilituma wanajeshi na wanasayansi kadhaa Kwenda kuchukua kila kilichobaki katika tafiti na makablasha yake, na miongoni mwa vitu ambavyo huyu bwana alikuwa anafahamika kwa kuvielezea sana ni utumaji wa mawimbi au ufyonzwaji wa mawimbi ya umeme toka matabaka ya juu ya anga, ambayo alikuwa akisisitiza yakuwa yana uwingi wa umeme uliojaa huko.

Miaka kadhaa nyuma iligundulika kuwa inapolipuka Volkano, moshi mkubwa hutengeneza mawingu makubwa, ambayo hayo mawingu huzuia mionzi ya jua kufika duniani ikiwa na nishati kubwa ya kuchochea ongezeko kubwa la joto la dunia. na kwa hivyo, ilijulikana kuwa, tatizo la ongezeko la joto la dunia linaweza punguzwa kwa uwepo wa vitu ambavyo hata kama sio vya asili, ila vinaweza zuia mionzi ya jua kufika katika dunia moja kwa moja.  

Kulikuwepo gunduzi ‘’patents’’ nyingi sana Marekani ambazo zilifanywa na wanasayansi ambao walikuwa wanaonyesha, taaluma ya kutengeneza vitu kama injini za ndege inawezekana kabisa. vitu ambavyo vinaweza katika matabaka ya juu sana ya dunia ‘’Stratosphere’’ kumwaga chembechembe ndogondogo sana, ambazo hizo zitazuia mionzi ya mwanga wa jua kuifikia dunia na hivyo kuipooza dunia. Na unaweza lielewa hili kwa kutazama picha zifuatazo za taaluma hizi kama zinavyofanyika sana zama hizi, picha juu kulia ni kielelezo, picha juu kushoto na chini ni ndege zinapokuwa zikipuliza kemikali mawinguni. ‘’Cloud seedling, or ice nucleation, etc’’



Msingi wa chembechembe hizi ambazo humwagwa katika matabaka haya ya juu sana ni kuwa, hizi chembechembe ni ndogo sana, huwa zinaitwa ‘’Nanoparticles’’ ambazo huwa mara nyingi zaidi ni za madini ya Aluminium, zipo sulfates, n.k. Huwa zinaitwa ‘’alumina’’ kwa zile za aluminium. Na kwanini madini haya ya alumina hupendwa sana, ni kwa kuwa aluminium ni madini chuma ambayo yanahitaji zaidi elektroni, kwa kuwa huwa na chaji ya Chanya 3+, hivyo haya madini huwa na sifa nyingi sana za kiumeme, na huungana na oksijeni. Lengo ni kuwa chembechembe hizi zinapomwagwa hewani, zinapopigwa na mionzi ya mwanga wa jua, hufyonza mionzi ile ya mwanga, na baada ya kufyonza, hupunguza mionzi ya mwanga inayoifikia dunia.

Huwa sio alumina tu, huwepo pia madini mengine mengi kama silicones na hasa madini mazito kama Barium na strontium, ambayo huchaguliwa kwa kigezo chao cha uwezo wao mkubwa wa kufyonza sana joto au kusisimka yanapomulikwa na mwanga, pia mengine hata kutengeneza mawingu, ‘’high endothermic reactions’’, ni kama zile kemikali ambazo huweza kuunda barafu kwa kuzichanganya tu. Hoja ni kuwa, kwa kutumia kemikali hizi, wanaweza sasa kutengeneza mawingu ‘’condensation’’, na hivyo kuweza kutengeneza mvua.                                

Dr. David Keith ni miongoni mwa wanasayansi wakubwa sana ‘’Geoecological engineer’’ waliomstari wa mbele katika kuchochea ubadilishaji huu wa hali za hewa, na ameandika kitabu kinachoitwa ‘’Geoecological engineering of Climate’’. Hayupo peke yake, wapo wanasayansi wengi zaidi katika upande huu wa kubadilisha hali za hewa. Project hizi za kubadilisha hali za hewa tangia zamani sana zilikuwa chini ya Idara ya Jeshi la Marekani kama zilivyokuwa project nyingine nyingi za sayansi hasa za Anga, ambazo zilikuwa na maslahi makubwa sana ya kiulinzi na kivita, kama walivyowahi tumia zamani njia hii kwa kupulizia sumu anga la Wavietnamu walipokuwa wakipigana nao.

Lusifa Kama Joka

Natoa shukurani zangu kubwa sana kwa mwanasayansi Dane Wigington toka Marekani, na jopo lake lote la wanasayansi na wadau katika maandamano yao ya wakati wote ya kupambana na mabadiliko haya ya hali za hewa. Mr.Wigington amefumbua maelfu ya watu duniani juu ya hatari na hatua kubwa sana ya uharibifu huu wa hali za hewa, na unaweza jifunza zaidi katika chaneli yake ya ‘’Geoecological engineering watch.org’’

Kwa ndani ya Pazia nilishasema awali kuwa, misingi mikuu ya afya ni mwanga, maji, na usumaku. Lusifa na jopo lake la wanasayansi waovu wenye tamaa ya kutawala dunia, wanajua kwa kuathiri misingi hii, sasa wanaweza kuathiri dunia na kuwaingiza wakazi wote wa dunia katika dhiki kuu. Biblia inasema kabla ya ujio wa Yesu katika kitabu cha Mathayo kuwa, yatasikika mafuriko, matetemeko, na milipuko ya magonjwa. Na katika sehemu hii, ndiyo kuna namna nyepesi zaidi ya kuelewa siri ya hii sayansi.

Madini ya Aluminium ni sumu kubwa sana, wala hakuna kiumbe hai yeyote ambaye huwa akiyatumia. Na tena mbaya zaidi, madini haya ni yaliyoandaliwa Maabara kuwa madogo na hatari sana ‘’Nanoparticles’’, chembechembe zinapofikia hatua hii hata mwili huwa hauwezi kuzitambua, na mwili huwa hauwezi hata kujikinga. Hizi chembechembe huwa ni hatari sana. Kumbuka ijapokuwa chembechembe hizi hupulizwa angani, lakini baada ya muda chembechembe hizi hushuka mpaka chini kabisa, na hapo huingia katika miili ya viumbe, mimea, mpaka vimelea vya udongo.

Nilishasema awali, aluminium huwa na uhitaji sana wa elektroni, na kwa mantiki hiyo zinapoingia katika seli, huvuta sana elektroni, na unapoondoa elektroni iwe kwenye mimea au mnyama, zote ‘’Chrolophyll, Melanin, Mitochondria, Oksijeni, Haem, DHA, n.k. hushindwa kufanya kazi zake, maana yake hushindwa kujitengenezea chakula, au kuzalisha nguvu. seli hushuka kiwango chake cha kuchakata matendo yake ‘’low redox potential’’.

Kemikali hizi ndani ya mwili huathiri kabisa uzalishwaji wa maji ndani ya seli. Kumbuka Mitochondria huzalisha maji yake ndani ya seli kwa kutumia ‘’Cytochrome C oxidase’’ na kwa kuhitaji elektroni, na mwanga-hydrogen. Sasa basi, hizi kwanza zinaondoa elektroni, pili zinazuia mwanga, tatu hizi kemikali zina chaji sana, maana yake zinaharibu kabisa mfumo wa usumaku wa seli. Haya yote unaweza thibitisha kwa matatizo mengi ambayo marubani kwenye maanga haya wamekuwa wakikumbana nayo. 

Mamilioni ya mimea imekuwa ikikauka, tena toka juu kuelekea chini, kuashiria madhara ya sumu hizi inapokutana na majani ya miti au matawi zinapokuwa zikishuka. Na hii imechochea sana shida za kulipuka kwa mioto yenye nguvu sana. Hii ni kwa kuwa, mimea imekuwa ikikauka sana tena hata katika misimu isiyoyakupukutisha.

Unapozuia mwanga wa jua, unaathiri mizunguko ya asili ya fiziolojia za viumbe na mimea. Mimea mingi sana imeathiriwa mizunguko yao ya asili kila inapokutana na chembechembe hizi za sumu. Na kupoteza mizunguko hii ya asili kumeipelekea kushindwa kumuu, vipindi mbalimbali vya mwaka, na hivyo kukauka.

Kibaya zaidi, uwepo wa kemikali ngeni katika matabaka haya ya anga, huzuia mionzi yote ya mwanga mizuri kwa afya, isiyo na nguvu sana, yaani, UVA, UVB kidogo, na infrared rays. Na hivyo huchochea kushamiri kwa mionzi hatari kwa afya, UVC. Ambayo hiyo ndiyo msingi wa shida zote hatarishi za mwanga wa jua kwa mimea na wanyama.

Wadudu wengi sana wamekufa, na vimelea vya udongo. Hii ni kutokana na kwanza, kukosekana kwa mimea mingi midogo iliyochakula chao, kutokana na sumu. Pili, sumu nyingi zinaposhuka zinapoingia katika ardhi, huathiri balansi ya asili ya udongo, na kuufanya kuwa na asidi nyingi sana isiyosapoti uhai wa vimelea wa udongo ambao walipaswa kusapoti mzunguko wa urutubishaji wa udongo.

Kumekuwa na utumiaji wa kemikali ambazo zimekuwa zikiyeyusha mawingu ili kurahisisha utengenzaji wa mvua, kemikali hizi huitwa ‘’Surfactants’’, matumizi ya kemikali hizi yamepelekea madhara makubwa sana katika viwango vya maji yaliyo katika bahari. Kwanza, yamepelekea mabarafu makubwa sana kama yaliyopo katika bara la Arctic kuyeyuka. Mabarafu haya yanapoyeyuka hupelekea madhara makubwa sana katika hali ya hewa ‘’climate’’ ya dunia. Hii ni kwa kuwa, hupelekea kuongezeka sana kwa kina cha maji ya bahari. pili, hupelekea kuathiriwa kwa balansi ya maji ya chumvi, na maji yasiyo ya chumvi, ambayo hutoka katika mabarafu haya. madhara yake, ni kuathirika kwa mikondo ya maji ‘’water currents’’ ambayo ilikuwa inasaidia kubalansi hali za joto za maeneo mbalimbali, mfano, ‘’Atlanto-mediterranean overturning circulation’’, ambayo husaidia kubalansi hali za hewa za mabara ya kaskazini. Mkondo huu ‘’AMOC’’ umeathiriwa sana hata kupelekea joto la ulaya kuzidi kuongezeka.

Miongoni mwa vitu ambavyo vinawachanganya sana watu ni mitambo mikubwa ya marekani ya kutuma mawimbi makubwa kuelekea juu angani katika matabaka ya ‘’Ionosphere’’, mitambo inayoitwa ‘’HAARP’’, au ‘’high Frequency Active Auroral Research Program’’. Mitambo hii inatuma mamilioni ya MegaWatts angani, tofauti na frequency za mawimbi ya kawaida ya chaneli za mawasiliano ‘’Broadcasting frequency bands’’, wengi wa watu wamekuwa wakiuliza madhumuni ya mitambo hii. majibu ambayo yamekuwa yakipatikana sana ni kuwa, mitambo hii hutumika kwa shughuli za kuharibu makombola ambayo yangeweza kutumwa, pia, kujifunza sayansi za maeneo ya Ionospheres, au kutuma mawimbi makubwa angani kwa malengo ambayo bado wengi hawana ufahamu nayo sana.Tazama picha za mitambo hii kama zinavyoonekana kwa kamera.


HAARP kwa kutuma mawimbi makubwa katika matabaka yenye chaji nyingi sana kama Ionosphere, ambako huko ndiko Nguvu ya Usumaku wa Dunia umeegemea zaidi, inaweza kubadilisha hali mbalimbali za hewa, kama inavyosemwa na wengi kuwa miongoni mwa malengo ya mitambo hii, ni kubadili hali za hewa. 

Nguvu kubwa ya mawimbi ambayo HAARP huweza kuzalisha, huweza kupandisha kwa kulisisimua tabaka la Ionosphere kwa umbali kadhaa toka wastani wake, na hivyo kufanya matabaka ya chini yake kama ‘’stratosphere’’ kuzibia magepu hayo, na hivyo kuchochea moja kwa moja mabadiliko ya hali za hewa katika eneo husika. Kumbuka mitambo hii, na mingineyo baadhi imechukua maeneo makubwa sana ya ardhi, na husemekana kwa muda wa sekunde kadhaa tu kama ikiwashwa kwa dhumuni la kutengeneza nishati kubwa sana, inaweza lingana na mabomu kadhaa ya Atomu ‘’atomic boms’’ katika anga. Hii inatosha kuelezea ni kwa namna gani mitambo hii inauwezo wa kuathiri moja kwa moja hata frequency ambazo zingeweza yafanya maji kutengeneza mawingu.

Watu wachache sana wanaojua kuwa kwa kucheza na mawimbi mbalimbali, unaweza tengeneza maumbile mbalimbali ya maji. Hii ni kama tulivyoona awali, namna usumaku unavyoathiri ‘’Hydrogen bonds za maji’’, na hivyo sasa, kwa kuathiri haya maumbile ya maji, unaweza yafanya maji kuzunguka kama unavyoweza tazama mtandaoni majaribio mengi ya kubadilisha frequency na kisha kuyafanya maji yabadilike maumbile. Kama utafanya hivi kwa anga ambalo lilikuwa liingie katika msimu wa kuunda mawingu ya mvua, basi usitegemee mvua hapo.

Kumbuka bado watu hawa huweka madini mengi sana kama Barium, au Strontium, ambayo haya madini marazote huwa na sifa ya kufyonza sana mionzi ya Mwanga au UV-Rays, na kubadilika chaji zake, au huitwa pia ‘’Photoionization’’, hivyo sasa, uwepo wa haya madini, asili ya tabaka la Ozone, na mionzi mikubwa ya HAARP, wataalamu hawa huweza kuongoza matokeo mbalimbali ya usumaku ambayo hupelekea matokeo mbalimbali ya majanga kama ya Cyclones (kiswahili chake ni kama vimbunga vikubwa), pia huweza kutengeneza tufani mbalimbali baharini na nchi kavu, ukame, n.k.

Mafanikio ya Lusifa, maranyingi sana Lusifa amekuwa akitengeneza Vimbunga, mafuriko, ukame, milipuko ya mioto na matatizo mengi sana, kwa taaluma hizi, na kisha kuonyesha kana kama ni matokeo ya laana toka kwa Mungu. Mara nyingi imesikika ikisemwa kuwa mioto imetokana na Hollywood kumkufuru Mungu, au Tufani ya Brazili imetokana na wao kumkufuru Mungu. Lakini yote kwa yote ukifatilia, kabla ya tukio na hata nyuma ya tukio ni taaluma hizi za kubadilisha hali za hewa, na kisha kuwatengenezea watu fikra kana kama ni Mungu aliyenyuma ya majanga, ili watu wasifikirie ni nini hasa lililo tatizo. Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Dubai, ilivyokuwa kwa Ukame wa maeneo kadha wa kadha, na penginepo hata kwetu Tanzania. Maana ni maranyingi sana tumeshuhudia ndege zikipita au Jets huku zikiachia mithili ya Moshi nyuma, lakini sote tunajua injini za jets au ndege huwa hazitoi moshi au sprays nyuma kutokana na asili ya fuel yake, hizi zote ni kemikali ngeni zenye malengo husika.

Zifuatazo ni baadhi ya picha ambazo nimezitoa toka channel ya Dane Wigington kwenye Documentary yake ya ‘’The Dimming action’’, yaani, matokeo ya kulizima Jua kwa kutumia kemikali za kutengenezwa.

                   "Rejea kwenye kitabu" 

Unaweza gundua kuwa, madhara ya taaluma hizi yanaathiri kila kitu. Hii ndiyo mantiki ya kusema kuwa, viumbe wote walioumbwa na Mungu wanasifa zinazofanana.

Kujifunza zaidi kuhusu madhara ya teknolojia haya, unaweza rejea sura zilizopita. Lengo kuu la ufupisho wa sehemu hii, ni kuonyesha madhara haya yanatokana zaidi na mkono wa wanadamu wachache wenye nguvu katika kutawala chemistry za anga, na si mapenzi ya Mungu watu kuteseka. Lakini pia, bila upendeleo ‘’bias’’ watu wanapaswa kuelewa kuwa matokeo ya uharibifu huu yamechochewa zaidi pia na shughuli za kilimo, pitia somo lingine ‘’ short -article’’ kujifunza zaidi.