UBONGO WA MTU MWEUSI
KISA KIFUPI
CHA MTAA MMOJA WA JIJI LA PENTAGON
Mara moja nilikuwa nikipita
katika mtaa mmojawapo ulioshonana sana katika Jiji la Pentagon. Kulikuwa na
watu wengi sana wanaosongamana katika njia na eneo dogo sana. msongamano huu
ulitokana na wengi wa watu hawa kuwa wakifanya biashara, na wengine wakipita,
na hata wengine wakifanya makazi katika eneo dogo. Idadi ya watu ilizidi idadi
ya makazi, na kutokana na kiwango kikubwa cha joto katika eneo lile, kulikuwa
na kiwango kikubwa sana cha hewa nzito. Ikiwemo kaboni dioksaidi.
Uchafu mwingi uliokusanywa
maeneo kadhaa na kuvunda, ukaribu wa vimitaa vidogo ambavyo watu hawa baadhi
huwa wakijificha kujisaidia, kutokana na uchache wa vyoo, na gharama za vyoo
vya kulipia. ulichochea hewa nzito ambayo, watu wengi wa maeneo haya hawakuwa
wakiihisi! Kwa kuwa, wameizoea.
Bado eneo hili halikuwa na
utulivu wa sauti. Kulikuwa na sauti endelevu ya aidha viwanda, vyombo vya
usafiri, makelele ya watu, miziki toka kwa watu na clubs, na matangazo ya
wafanyabiashara. Watu kwa wastani walikuwa wakiongea kwa sauti kubwa ukilinganisha
na maeneo mengine, na wao walikuwa wakiona kawaida. awali nilifika eneo hili
nikiwa nasikiliza muziki kwa kutumia ‘’earphones’’, na sasa, nilikuwa siusikii
tena kwa kuwa, sauti ya mazingira ni kubwa sana. Lakini watu wa eneo hili wao
wanaona kawaida kabisa, na tena, bado wanapiga na miziki kwa sauti ya juu
zaidi.
Kipindi naendelea na safari
yangu, nilikuwa nikijikuta mhanga wa kusisimuliwa sana kihisia na wadada wengi
sana wa maeneo haya ambao, wengi wao walikuwa wakiwa wamevaa nguo fupi sana
zinazoonyesha maungo yao ya karibia na sehemu za uzazi, mapaja, matiti, na
wengi wao walikuwa wamejiremba sana sura zao. lakini kwa utafiti wangu mfupi
niligundua kuwa, vijana wengi wa maeneo haya, kwao haikuwa hivyo. wao waliona
kawaida sana. Wala hawakuwa wakiwasindikiza mabinti hawa kwa macho!
Taswira nyingi sana katika
eneo hili zilikuwa zinazoonyesha matangazo yenye rangi kali sana za mng’ao,
rangi nyekundu, bluu, nyeupe, na nyeusi. Na matangazo mengi yalikuwa katika
muundo wa kushangaza, yaani, Kuna bidhaa nzuri ajabu sana iliyopo pale! Au
labda kuna huduma bora sana eneo hilo. Wengi walikuwa wakionyesha taswira
zinazokazia utofauti, na upekee wao.
Baada ya muda kadhaa nilipatwa
na njaa. Nikawa nikitafuta sehemu ya kula. Nilikutana na sehemu nyingi sana
ambazo watu walikuwa wakiuza juisi za sukari sana. Juisi za muwa, ambazo huwa
wanachanganya na ndimu. Juisi za matunda mchanganyiko baadhi, zenye sukari kali
sana. Wengi walikuwa wakiuza Supu ya pweza, na supu za aina nyingine nyingi.
Walikuwa wengi wakiuza vyakula vya kukaanga, na baadhi ya watu pia walikuwa wakienda
kununua kwenye ma ‘’supermarket’’ vyakula vya kupaki moja kwa moja.
Nilifanikiwa kupata mgahawa mmoja ndani ndani sana ambao, niliona wengi
wakinunua vyakula hapo. Na walikuwa wakila huku wengine wakiwa wamekosa kabisa
hata sehemu ya kukaa, na walikuwa wakila huku wamesimama. Nikaagiza ugali wa
dona na mboga za majani, nikakosa, wakasema upo wa sembe. Nikasema nipatie wali
na maharagwe kama upo, wakanipatia. Watu wengi hapa walikuwa wakila wali na
Samaki wakurostiwa, wali na nyama za ng’ombe, chipsi na mayai ya kisasa, au na
kuku wa kisasa kama broiler.
Joto ni kali sana, lakini watu
bado wanakunywa maji kidogo sana. Kipindi najiuliza kwanini, nikagunda huwa
wanakunywa maji ya baridi sana. Maana, hayo hukata kiu mapema. na hivyo kwa
kunywa maji kidogo, unaweza okoa gharama ya kunywa maji mengi sana. Maana huku,
maji ni ya kununua. Lakini kipindi naendelea kutembea, niligundua mtaa huu kwa
chini, ulijawa na chupa nyingi sana za juisi za ‘’energy drink’’, soda za kopo,
na chupa za maji ambazo zote, zilikuwa zimekusanywa sana karibu na sehemu za
wauzaji wa vyakula, na mabarabarani. Hii ilikazia hitimisho la utumiaji
uliokithiri wa bidhaa za sukari, katika maeneo haya, na bidhaa za baridi kali.
Mitaa mingi niliyokuwa
nikipita niligundua kuwa walikuwa wakisikiliza miziki ya wasanii kadhaa, ambao
wote walikuwa wa ‘’Bongo flavour’’, na miziki waliyoipenda sana, ilikuwa ya
msanii mmoja mwanadada aliyekuwa akiimba miziki ya kucheza sana, na mabiti ya
kujirudia. Na pia, wapo wasanii wa kiume ambao nyimbo zao zote zilikuwa ni aina
ya ‘’dance music’’, miziki ya ki ‘’Nigeria’’ ilisikilizwa sana pia. Kuna aina
ya muziki ambayo ilikuwa inafikisha mpaka mabiti 250 kwa dakika, ni kama
‘’electronic music’’, ila inaitwa ‘’Singeli’’, nayo ilikuwa ikipigwa sana.
Na miongoni mwa vitu
vilivyonishangaza sana ni kuwa, aina zao za muziki zina aina moja ya ujumbe,
yote ilikuwa imejikita kuzungumzia mapenzi, kufanya mapenzi au migogoro ya
mapenzi, hasa kutokana na pesa. Na muziki mwingine niliousikia kwa baadhi sana
ya maduka, ulikuwa wa dini, ambao nao, ulifanania sana na ule wa wenzao, na
pia, kuna uliokuwa ukirudiarudia sana maneno machache yaleyale, lakini ulikuwa
wa muda mrefu sana.
Kwa muda mfupi sana nilikwisha
kuwaonea huruma hawa watu kwakuwa, mfano. idadi kubwa ya watu hawa na Maisha
yao yalivyo, lazima watakuwa na stress sana. Hilo nililithibitisha hata kabla
ya kuendelea mbele zaidi, maana, niligundua wengi wao wakiwa ni watu wenye
kupenda sana vitu vya kuwaliwaza, kuwaburudisha, kuwasahaulisha! Niliona
wakibishania sana mipira, wengine walikuwa wakiwafuatilia sana manabii baadhi.
Pia walikuwepo wasanii wengi sana karibu na maeneo haya, na wote! Walikuwa muda
mwingi sana wakizurura katika mitandao ya kijamii.
Nikamuuliza kijana mmoja
aliyekuwa akiuza madafu eneo nililoamua kupumzika kidogo, nikamuambia ‘’ukipata
nafasi ya kufanya kazi nyingine nzuri kama unayoifanya, au yakuifanania kwa
maeneo mbali na maeneo haya unaweza kuikubali? ‘’ akaniambia ‘’hapa nilipo
nimetoka huko mbali, na Maisha huko yalikuwa magumu zaidi, kwangu hapa ndipo
kama bustani ya edeni!!’’
HISTORIA FUPI YA HILI ENEO
Hili eneo ambalo linakaribiana
na mji wa Dar es Salaam. Kwa ujumla maeneo haya yote huwekwa katika kundi la
miji ya nyanda za chini Pwani ‘’sio nyanda za juu pwani’’. Maeneo haya huwa
hayana ardhi kubwa sana yenye Rutuba ya kufanya kilimo (Kilimo Kikubwa
kinachozungumziwa), na pia, huwa hayana mabonde mengi na maji ya mito mengi
kama kwa maeneo mengine ya pwani za juu, ya kuyawezesha kwa kilimo kikubwa.
Watu wengi maeneo haya huwa wakifanya shughuli za Biashara na uvuvi. Wengine
huiita hii miji kuwa, miji ya biashara.
Hapo zamani kipindi cha Jamii
nyingi za Bantu zilipokuwa zikiteremka toka kaskazini, kupitia bonde la ukanda
wa Kongo, na kuanza kutengeneza Jumuia kubwa ‘’small empires’’, au unaweza ita
‘’Chiefdoms’’, ambazo ndizo kama jumuiya za makabila baadhi, mfano
‘’Wanyamwezi’’, n.k.
basi kipindi jamii hizi
zilipokuwa zikizidi kukua na kupata nguvu, zilipelekea wakazi wengi ambao
hawakuwa na jamii zenye nguvu, kama ilivyokuwa kwa jamii za ‘’Khoisan’’
walivyosukumwa mbali, ndivyo ilivyo pia hapa, wenyeji wengi wa pwani walikuwa
pia ni wabantu, wa jamii kama za wa kwere, zaramo, ndengereko, wadoe na
makabila ya kuzunguka mto Rufiji. Lakini makabila haya yalifika pwani katika
zama tofauti tofauti, na historia kadhaa mbele tutaona zinaonesha wengi wa
makabila haya walikuwa ni wahamiaji, waliotoka katika jamii kubwa zaidi za
awali. Na walijikita zaidi katika uwindaji na ukusanyaji, na kisha uvuvi na
biashara. Hivyo awali hawakuwa na jamii zenye nguvu sana, tofauti na makundi
yenye ustadi zaidi wa kilimo ya kibantu yaliyozidi kushuka katika bonde la
Tanzania, na hivyo walisukumwa mbali zaidi. Hawakuwa na nguvu za kushindana na
wabantu hawa waliozidi kuwa na nguvu. Hawa wabantu wengi walikuwa ni wakulima,
na kwa hivyo, walichukua maeneo mengi sana yenye Rutuba.
Maeneo ya pwani yalianza
kujawa na watu waliokuwa na jamii zisizokuwa na nguvu sana, ni kama ilivyokuwa
kwa maeneo ya milimani walivyokuwa wakisukumwa makabila ya waliokuwa na jamii
ambazo hazikuwa kubwa sana, pale makabila yenye nguvu yanapochukua ardhi zenye
rutuba.
Huku pwani jamii nyingi za
awali kabisa zilianza kushughulika na shughuli za uvuvi wa Samaki. Na kisha,
zilikuwa zikifanya biashara na makabila ya maeneo ya kati. Nitaelezea historia
ya lugha ya Kiswahili, lakini kwa awali kabisa ni muhimu kujua kuwa, kutokuwa
na makazi ya kudumu kwa jamii hizi za awali kabisa, kulizifanya kupokea lugha
ya kibantu moja kwa moja, ambayo ni lugha matokeo ya koo kadhaa kuu za bantu,
ambazo zote zilikuwa zikifanana.
Sasa basi, kuanzia mwaka 100AD
inanukuliwa na baadhi kuwa, miji hii ya pwani ilishakwisha anza kufanya
biashara na maeneo ya India, China na Misri. Na biashara hizi zilizidi
kuendelea na hata dhidi ya jamii nyingi sana za nchi za kiarabu.
KUKUA KWA MAENEO HAYA YA PWANI
Unaposafiri, mara zote
unajiandaa sana. Wasafiri wengi huwa wakijiandaa sana kiuchumi. Wasafiri wengi
wa awali kabisa kufika katika pwani hizi, walihitaji msaada mkubwa sana wa
wenyeji wao. Walihitaji wafasiri wa kuwawezesha kuingia ndani zaidi ya miji ya
nchi kwa ujumla. Walihitaji wenyeji wakuwapatia mahitaji ya msingi katika
maeneo mapya.
Hii iliwapatia fursa wenyeji
wa maeneo haya ya pwani, kuweza kutengeneza thamani kubwa sana, kwa kuwa, wao
ndiyo walikuwa waamuzi wa kwanza wa thamani za mabadilishano ya huduma na vitu,
au huduma na fedha. Thamani kubwa ya nchi yeyote ile haijawahi kuwepo miji ya
Pwani. Lakini, pwani ndiyo kituo kikuu cha mabadilishano.
Hii inamaanisha kuwa,
wafanyabiashara wakubwa zaidi, walikuwa ni wageni wenyewe waliofika pwani hizi.
Wao waliangalia thamani ya vitu katika nchi zao wanazotoka, na upatikanaji wake
katika makazi mapya. Namna nyepesi kabisa ilikuwa ni hii, kutengeneza makazi ya
kudumu katika maeneo haya, na kuwatumia wenyeji hawa wa pwani kurahisisha
ubebaji wa vitu vya thamani, na kisha wao kuvisafirisha kuelekea katika nchi
zao. Wenyeji wengi wa pwani ndiyo walioshiriki katika usambazaji wa bidhaa na
huduma katika ya jumuiya za ndani, na za wageni. Walibeba wakati mwingine kama
watumwa, au wakati mwingine kama wasaidizi.
Vituo vingi vya huduma
vilianza kufunguliwa maeneo haya na wageni. idadi kubwa ya watu ilianza kujaa
katika maeneo haya kwa ajili ya kufanya kazi za wageni. Wanawake wengi walianza
kuzaa na wageni hawa, wengi wao wakiwa waarabu. Hakukuwa na lugha zaidi ya
Kiswahili, lakini misimu, rahaja na hata lafudhi nyingi zilianza kushepiwa kwa
mchangamano na waarabu.
Wageni wengi walihitaji
burudani katika maeneo haya, na wasanii walinufaika kwa huduma hizi. Wenyeji
wengi wa maeneo haya walinufaika pia kwa kuuza maeneo yao mengi kwa wageni,
wakati huu sasa, waliuza kwa wabantu waliosukumwa kibiashara zaidi kuja pwani,
na kwa wageni. Wenyeji hawa wengi waliendelea kusambaa hata kufika maeneo ya
visiwani, ambako awali, hakukuwa na makazi ya wengi zaidi ya wavuvi, lakini
ugunduzi wa waarabu kuhusu upekee wa visiwani, ulihamasisha zaidi mchangamano
kama uliokuwa upande wa pili wa bara.
ASILI YA MWAFRIKA MASHARIKI
Hakuna ubishi kuwa jamii
nyingi za maeneo ya Afrika Mashariki zilianza kushuka kutokea maeneo ya
kaskazini. Zingine zilishuka mpaka kufika kabisa kusini, ila baadae, zikaanza
kupanda tena juu kama ‘’Wangoni’’. Rangi za Waafrika kuanzia Rangi za weupe kabisa,
mpaka Weusi kabisa, zinathibitisha kabisa uhusiano wa kiwango cha mionzi ya Jua
kwa kadri unavyokaribia Equator, na ongezeko la mwonekano wa Weusi unaotokana
na ‘’melanin’’ inayozalishwa kujikinga na upenyaji zaidi wa mionzi katika
ngozi.
Na hata ongezeko la ukubwa wa
mwili (makabila kama wanubi, wajaluo, wakamba, wamaasai, wajaluo, wasukuma,
wabantu karibia wote, n.k.) ‘’ingawa sio kwa siku hizi za madhara ya afya’’.
Ilikuwa ni kwa lengo la kurahisisha zaidi upotevu wa joto kali katika maeneo
haya ya equator, kutokana na kiwango kikubwa cha miale mikali ya jua. Pia hata
nywele laini, zilizonyooka kwa watu wa asili ya Afrika, kunathibitisha kiwango
kikubwa cha joto ambalo liliwachochea kuwa na matundu yaliyojiminya kutengeneza
umbile la ‘’C’’ ili kutoruhusu mionzi mingi kuathiri Ubongo, na pia nywele za
Waafrika hunyooka ili kuruhusu kupotea kwa joto kirahisi, tofauti na nywele za
ulalo ambazo hulenga zaidi kuzuia kutopotea sana kwa joto kutokana na baridi
kali. Nywele za Waafrika hutambulika kwa Weusi wake, ambao maranyingi ni
kutokana na kiwango kikubwa sana cha ‘’eumelanin’’ na Jua linapokuwa kali sana,
nywele hupoteza ‘’Pigments’’ hizi na kuwa za rangi ya wekundu.
Uwezo mkubwa wa Waafrika
kimifupa, na misuli ‘’athletic characters’’, ni matokeo ya safari yao ndefu
zaidi kutoka Kaskazini kabisa mwa dunia, mpaka kuelekea kusini, pia mitindo ya
Maisha ya waafrika hawa ya uwindaji, na ukusanyaji iliwahitaji sana kuwa bora
katika matumizi ya misuli, jambo lililowachochea sana kimaumbile yao. katika
Q42 nimeelezea hata sifa za uimbaji sana wa miziki, hasa ya kucheza, namna
kunavyohusiana na safari ndefu katika ubongo.
Kiwango kikubwa cha
Testosterone kwa Waafrika, kama inavyooneshwa na baadhi ya Report, kinaweza
kuzungumza kutokukua sana kwa nywele kwa Waafrika wengi wakiume. Hii ni kwa
kuwa, testosterone inapokuwa nyingi, huchochea kukua sana kwa nywele za
mwilini, kama vinyweleo, ndevu, n.k, lakini pia hubadilika na kuzalisha
‘’Dihydrotestosterone’’ au DHT ambayo huenda kwenye kichwa ‘’scalp’’, na kuzuia
kukua kwa nywele zaidi. Wanawake wengi wa Kiafrika pia huwa na ‘’Estrogens’’
nyingi sana, ambazo ndizo huwapa maumbile makubwa, kama ya ‘’Hips, makalio,
n.k.’’.
Kumbuka, hoja hizi usipokuwa
msomi mzuri unaweza ziunganisha katika fikra za kiubaguzi ‘’racism’’, lakini si
kweli, mbeleni tutaona namna jamii zote zilikuwa sawa kabisa awali, lakini
mitindo ya kimaisha, baadhi iliwafanya kubadilika na kuathirika kiakili kabisa
‘’kama jamii baadhi za Afrika waliokuwa wakila mpaka nyama za watu’’, na
wengine walibadilika sana kiafya ya mwili, kama homoni, na kupelekea vizazi vya
watu wenye magonjwa mengi, wengine huko ulaya mpaka wakazamia kwenye
‘’Ushoga’’, wengine wakawa na taaluma sana na elimu, falsafa, vita, n.k.
KWANINI MAENEO YA KATI YALIKUWA NA WATU WACHACHE?
Kabla ya kukimbilia kuangalia
makabila kama ya Wagogo, waliopo sana Dodoma na sehemu baadhi za Singida, ni
wengi sana hawa watu, kwa takwimu za zamani sana, walizidi hadi milioni moja na
laki tano, inajulikana waliathiriwa sana na utumwa. Na hata bado baadhi huamini
hakukuwepo kabila la Wagogo, bali ni jumuiya tu iliyoundwa kwa jamii za
wamanghala, wabambali, wayenzele, na wanghulimba, ambao walikuja kuitwa kama
Wagogo, na huisiwa kuwa watu hawa walikuwa ni wakulima, baadhi wawindaji, wengine
wafugaji, na wengi wao walikuwa waoga hasa dhidi ya jamii za wanyamwezi,
wahehe, na wambugwe. Lakini hizi sio sababu kubwa.
Zipo sababu nyingi, kwanza
kabisa, kama nilivyoelezea katika Q3 kuwa, maeneo haya ya bonde la kati,
kipindi cha awali kabisa kipindi baada ya Bara la Afrika kumeguka, kujitenga
toka ‘’Mid-Atlantic Ridge’’, Bara la Afrika katika maeneo ya Bonde la Afrika Mashariki,
kulitokea mithili ya mikunjo iliyopelekea mabonde kama maeneo mengi ya Congo,
na Miinuko ambayo ilipopasuka, ilipelekea Bonde la Ufa, ambalo, lilipoinuka
lilikusanya maji mengi sana kutoka katika maji ya kutoka gharika kuu, na maji
mengine yote yalisukumwa kushuka katika mteremko kuelekea katika Bahari ya India,
upande wa Mashariki. Kadri maji yale yalipokuwa yakishuka, yalipelekea maeneo
yote ya nyanda za kaskazini kuwa na kiwango kikubwa cha mmomonyoko wa udongo,
uliopelekea udongo mwekundu, miamba ya magma, na viwango vikubwa vya madini
karibia tu na usawa wa ardhi.
Lakini maji haya yalianza
kuishiwa nguvu yalipoanza kufika katika ukanda wa kati, na hapo yakapelekea
kiwango kikubwa sana cha Mchanga uliojaa katika maeneo mengi ya kati mwa
Tanzania, hii ilichochea hali ya ujangwa katika maeneo baadhi kama ‘’Dodoma’’, manyara,
n.k. na tokea maeneo haya, maji mengi yakaanza kutengeneza chaneli maalumu
zilizopelekea mito mingi katika maeneo ya nyanda za juu pwani, na miji ya kati
kama Morogoro.
Hivyo basi, kutokuwepo kwa
mimea mingi na rutuba katika maeneo ya kati, kulipelekea wakazi wengi kutafuta
makazi katika maeneo ya mbali na miji hii, maana hata Wanyama wa kuwindwa
hawakuwa kwa wingi.
Lakini pia zipo sababu za
karibuni za miji hii kutokuwa na watu wengi, mojawapo ni kuwa, miji hii
ilitumika kama Njia, au ‘’Routes’’ za wafanyabiashara wengi sana, ikiwemo wa
‘’Watumwa’’. Na wengi wa wakazi wa maeneo haya, walisukumwa kuenda mbali zaidi.
Na pia hata wengine huisi kuwa, miji hii ilijazwa na makabila ya watumwa ambao
baadae walikuwa hawana tena hata makazi maalumu.
UFUPI KUHUSU MAKABILA YA TANZANIA
Pamoja na kuwa makabila mengi
ya Wabantu (ambao ni karibia asilimia 95% ya Tanzania yote). kuwa ni watu walioshuka
toka kaskazini kupitia mabonde ya Congo, makabila mengi ya nyanda za juu kusini
ni matokeo pia ya jumuiya nyingi zilizotokea kanda za kusini, au Afrika ya
kusini. Afrika Mashariki ina makabila mengi sana ambayo yaliundwa kupitia jamii
za watu waliotokea ‘’Ethiopia’’, sudani, misri, n.k. na jamii hizi nyingi ni jamii za maeneo ya
Kaskazini.
Kwa upande wa Kaskazini, Hawa
ni mchanganyiko wa jumuiya mbalimbali, baadhi zikiwa za wabantu na makabila
mengine, mfano ‘’Batrezi’’, banyankole, banyoro, Bahaya, kuna makabila kama ya
‘Chagga’’ kupitia jina lao, wengine huthibitisha kuwa hawa ni matokeo ya
‘’Kuchanganya’’ jamii mbalimbali za bantu, pia kuna jamii za ‘’Nilotics’’
mfano, Maasai, hawa na jamii baadhi za kenya kama Wajaluo walifuata tu mkondo
wa mto nile, hata kufika na kutawala eneo kubwa sana la Afrika mashariki.
Wanyaturu pia ni wenyeji wa
Ethiopia wanaoaminika kushuka chini wakitafuta nzige kutokana na njaa kubwa,
wanyiramba wakitokea sudani, wakatua kanda Jirani na wakurya kwa kitambo kabla
ya kushuka zaidi hata kanda za singida, na wengine wakielekea pande zingine,
wabarbaig au wamang’ati ambao ni nilotics pia, walioshuka kupitia kenya hata
kufika manyara, singida, n.k.
Hoja ni kuwa, wengi huwa
hawajui kuwa, Jamii za Waethiopia, huwa wanaonekana kuzaa sana. Hii huwapelekea
kuwa na idadi kubwa sana ya watu. Na muda mwingine huisiwa wenda, mifumo hafifu
ya kuweza kuwamudu watu wao, hupelekea jamii hizi nyingi, kuendelea kushuka kutafuta
maeneo yenye uhafadhali zaidi wa kujikimu. Haimaanishi hatuna jibu la kwanini,
wenda watu hawa wanazaliana sana? La hasha, ila sio mada katika sehemu hii.
watu wa asili ya ethiopia wengi wanaonekana kuzunguka Mashariki, na magharibi,
mwa bonde la Ufa, hata na kwa upande wa kenya. Miongoni mwa wanaozungumziwa
sana kwa ukanda wa Tanzania, ni makabila kama ya wairaqw (wamburu).
Ukanda wa Kalahari
‘’Namibia’’, maeneo ya manyara, Dodoma, n.k. yanahisiwa kuhusisha sana jamii za
jumuiya za ‘’Khoisan’’ ambao wengi wao, ndio waliokuwa wenyeji wa awali kabisa
wa mabonde mengi ya Tanzania kabla ya kusukumwa na Wabantu, waliotokea Afrika
ya kati, na kasakazini. kwa sasa, wapo maeneo ya kusini mwa Afrika, lakini hata
hivyo kuna makisio mengi sana juu ya uwepo wa makabila ya jamii zao, katika
maeneo baadhi katika miji baadhi kati kusini.
Wabantu wengi, mfano, Wahehe
chimbuko lao ni mtu aliyeitwa ‘’Mufwimi’’, alikuwa mwindaji, aliyetokea
Ethiopia ‘’Kwa Mujibu wa Wikipedia’’. lakini hoja ni alitokea ‘’Kaskazini’’,
akipita Kenya, kabla ya kufika Tanganyika. Wengi walimfananisha na ‘’Wakamba’’
kabila la kenya kutokana na Ukubwa wake wa mwili. Hata tu kwa Makabila makubwa
zaidi matatu, yaani, Wasukuma, Wanyamwezi na Wachagga. Na kisha ukaja kuangalia
na makabila mengine yote, bado utaona wote asili yao walishuka toka maeneo ya
kaskazini. Tanzania ina makabila zaidi ya 125, katika haya yapo ambayo
yamesogea toka nchi Jirani, kama Wamakonde wa Msumbiji, au wangoni wa Kusini
mwa Afrika, lakini wote bado asili kabisa ilikuwa ni kaskazini.
Wanyakyusa walitoka kaskazini,
wakipita bonde la mto nile, na inaaminika na baadhi kuwa, hata kabla ya kufika
Rungwe, mpaka Malawi, waliishi pia Morogoro. Waha ni wabantu pia waliotoka
Congo. Wazaramo hata neno lenyewe humaanisha, ‘’Wahamiaji’’. Inaaminika
wazaramo walikuwa ni matokeo ya koo mbalimbali ambazo zilifika pwani, hata
kabla ya miaka ya 1600. Na wakazi hawa wanaonekana kuweka makazi yao ya asili
kabisa katika eneo la sasa, la wilaya ya kisarawe, mkoani Pwani. Mahali
panapoitwa leo ‘’Mwanarumango.
Wakurya nao inaaminika
walitokea maeneo ya kaskazini, ‘’Misri’’, na wabantu hawa walishuka kupitia
Kenya hata kutengeneza jamii zao zilizo kenya na zilizo Tanzania, kama ilivyo
kwa wajaluo, amba oni nilotics. Wakurya walikuwa na migogoro sana ya ardhi na
wamaasai, ambayo inaaminika ilichochea vita zilizowasukuma zaidi wamaasai mbali
na bonde la Serengeti.
KUKUA KWA THAMANI YA PESA PWANI ZA KUSINI
Kuendesha Maisha kwa kazi
ngumu za kilimo, na ufugaji. kuliambatana na changamoto kubwa sana katika
maeneo mengi ya miji, ya Katikati mwa nchi. Lakini stori haikuwa hivyo katika
miji hii. mtu angeweza kuchukua kitu kwa thamani ndogo eneo moja, na kisha
akaenda kukiuza kwa thamani kubwa sana kwa wageni katika maeneo haya. Na
akapata faida kubwa sana ya kuweza
kukidhi mahitaji yake, kutokana na thamani ndogo sana ya Maisha kwa
wenyeji mpaka wakati huo.
Watu wa maeneo haya wakaanza
kuwa ni watu wajanja sana wa lugha, kama tu ilivyo kwa miji mingine kama hii.
kwa kuwa hiyo iliwawezesha kuunganisha pande zote mbili za mabadilishano. Watu
hawa toka zamani walikuwa ni waokotaji na wawindaji, na pia, wengi wao walikuwa
bado ni wavuvi. Hawakuwa ni watu wakuzoelea matumizi ya misuli sana. Lakini
kwao lugha na ujanja wa kutengeneza faida bila kazi kubwa, ulikuwa mpaka
mwisho. Miji hii ilikuwa na thamani kubwa sana ya pesa.
Nguvu Ya Wanawake
Tofauti na kanda zingine zote,
miji hii ilikuwa na nguvu kubwa sana ya wanawake. Hii ilitokana na kuwa, awali
kabisa kulipokuwa kukitokea migogoro ya kushindania maeneo, wanaume wengi wa
jamii hizi waliuwawa. Na mara nyingi wanawake hawakuwa wakiuwawa, na hivyo,
wengi wao walikimbilia maeneo haya ya pwani wakiwa na Watoto wao, na wanaume
kadhaa. Lakini pili, Jamii nyingi za huku hawakuwa wakikumbana na changamoto
nyingi za vita kupambania maeneo yenye rutuba. na hivyo, hakukuwa na kipaumbele
sana cha kupata mtoto wa kiume, au mjeshi ‘’warrior’’ hii ilichochea sana
kuinuka kwa nguvu kubwa ya jamii za wanawake.
Tatu, wageni wengi walikuwa ni
wanaume, na mara nyingi huwa ni wanaume wanaosafiri sana kutafuta maeneo mapya,
hivyo, wageni hawa walihitaji sana wanawake. Na wanawake wengi wa maeneo haya
walianza kupata nguvu kwa kuweza kuchangamana na wageni waliokuwa na nguvu sana
za kiuchumi, na kijamii. Nne, shughuli nyingi za pwani zilikuwa sio za kutumia
misuli, zilikuwa ni biashara ambazo, wanawake wengi walizimudu vizuri zaidi, na
hata shughuli za uvuvi, bado wanawake walihitajika sana katika kuwatengeneza na
kuwaweka sawa Samaki kibiashara.
Mwisho, uchache wa wanaume,
kukosekana kwa nguvu dume za kiutawala, na uwingi wa nguvu za wanawake
kulipelekea wanawake wengi kutumia akili sana kuwapata wanaume. Wanawake
walikuwa wakiwalinda zaidi wanaume zao. Na huu ndiyo mwanzo wa sanaa nyingi za
miziki ya kuwateka wanaume kwa kuwaliwaza, na taaluma za kuwateka wanaume, kwa
wanawake wengi wa pwani.
Saikolojia ya Usaliti na Ukoloni
Wakoloni wengi kabla ya
kushambulia ngome kubwa za maeneo ya ndani ya nchi. Walihitaji sana wapelelezi.
Wapelelezi walihitaji sana wafanyabiashara wenyeji wa awali kabisa ambao, nao
walikuwa chini ya jumuiya zao kadhaa. Hawa waliwasaidia sana kuelewa ramani
nzima ya ngome kadha wa kadha. Maana walikuwa tayari na uzoefu na miji yao.
Kwao hii ilikuwa bado ni namna
ya biashara. Kumbuka, tabia hii
ilifanywa na karibia jamii zote zilizokuwa dhaifu, waliungana na
wakoloni ‘’allies’’. kwa lengo la maslahi baada ya kushinda. Falsafa hii
iliendelea kwa maeneo kadha wa kadha hata baada ya uhuru, bado wengine
waliendelea kupendelea maslahi kwa ujanja ujanja wa kibiashara.
UCHAMBUZI KWA UFUPI JUU YA TABIA ZA WATU WA ENEO
HILI
Watu hawa kwa kipindi kirefu
sana wamekuwa sio watu wa kufanya kazi ngumu. Ni watu wa kufanya kazi
zisizotumia sana nguvu za misuli kwa wastani. Mfano, kufanya biashara aidha kwa
kukaa, kutembeza, kutumia usafiri mfano, kutumia wanyama, n.k. bado walikuwepo wavuvi, wasanii, wafasiri,
wapishi, n.k.
kiwango kidogo cha matumizi ya
misuli kilienda sambamba sana na kiwango kidogo sana cha hamu ya kula vyakula
vya nishati, na hata pia vyakula vingi vya wanga vilikuwa havilimwi katika
maeneo haya, vilitoka mbali sana na vilipatikana zaidi kwa gharama. Hizi sababu zote kwa Pamoja
zilichochea utumiaji wa vyakula vyenye sukari sana, na vyenye msisimko sana.
Ili ku ‘’boost’’ hamu ya kula zaidi.
Inafahamika pia kuwa, wasafiri
wengi sana huwa si wapenzi wa ubebajii wa vyakula vizito, ambavyo vinaongeza mizigo,
na viwango vyake vikubwa vya maji, huongeza uharaka wa kuharibika. Na sasa
basi, wasafiri wengi hupenda vyakula vyenye sukari nyingi, ili kutumia kiwango
cha chakula kidogo, na kupata nishati nyingi ‘’calories’’. Pia, vyakula vya
asili ya kukaanga, na kukausha, huweza kukaa kwa muda mrefu sana bila
kuharibika. Na taaluma hizi zote zilizidi kushamiri maeneo ya pwani, wapishi
wengi iliwapasa kuiga kwa dhumuni la biashara.
Vyakula hivi kwa ujumla vina
kiwango kidogo sana cha maji, vipo ‘’concentrated’’, na hivyo, vina kiwango
kikubwa sana cha ‘’msisimko’’ au ‘’stimulant effect’’. Matumizi ya chumvi
kuzuia kuharibika kwa chakula, nyama za kuchoma, vyakula vya kukaushwa, vichochea
Ladha vingi, n.k. yalishamiri sana.
Kumbuka kabla ya kuendelea
tumeshaona katika Q4 kuwa, matumizi ya vyakula vyenye tabia za kusisimua sana
ulimi na ubongo kama hivi vya kukaanga, sukari, viungo vya vyakula, ambavyo
vingi huku vilikuwa vikitokea nchi za India, na uarabuni. n.k. huwa vina
virutubisho vichache sana. Kwa kuwa, uandaaji wake huaribu virutubisho vingi
sana.
Pia, kiwango kikubwa cha
sukari tamu, ambayo huwa ni chembechembe za ‘’fructose’’ kwenye vyakula hivi,
huathiri kabisa mwili, kwa kujaza sana mafuta katika maini, huathiri
chembechembe za seli za kuzalisha nishati zinazoitwa ‘’mitochondria’’, kwa kuua
watenda kazi wake ‘’enzymes’’, kama ‘’AMP Kinase1, CTP, n.k. na pia, matumizi
sana ya bidhaa ya nyama za kukaanga, na bidhaa zingine za kukaanga, huathiri
ukuta wa utumbo, ufyonzwaji wa virutubisho tumboni, viungo vya vyakula huua
sana bakteria wazuri wa tumboni, huathiri utendaji wa kijenetikia. Na katika
ubongo, vyakula hivi huchochea sana uraibu.
Hii ni kwa kuwa, chembechembe
zile za utamu ‘’fructose’’ huenda kusisimua sana sehemu ya ubongo ya uraibu,
ambapo hata madawa ya kulevya kama ‘’heroine, cocaine, na nicotine’’ huenda kuisisimua,
sehemu inayoitwa ‘’Nucleus accumbens’. Sasa basi, uraibu wa vitu hivi vya tamu
tamu, kwa watumiaji wa bidhaa hizi, huwa ni ngumu sana kuviacha, na huzidi
kuvitamani hata wanaposhindwa kuvimudu. Hii tayari huwazidishia kutumia kila
mbinu ya ujanja aidha wa lugha, au biashara, ili kupata faida waweze kurejelea
katika maeneo yaleyale ya uraibu.
Maeneo mengi sana katika miji
hii huwa tayari yakimilikiwa, na gharama za kuyanunua huwa ni kubwa sana.
Tatizo hili huwafanya watu wengi wa maeneo haya, kushindwa kumudu kupata
makazi, na njia pekee, huwa ni kutafuta maeneo duni yasiyo na gharama, na kuweka
makazi yao dhaifu, na maeneo haya huwa na watu wengi sana, na huwa na
miundombinu dhaifu sana.
Hali hii huwafanya kuwa ni
wahanga wa virutubisho vya muhimu kabisa katika afya. Hii ndiyo sababu, kama
ilivyo kwa miji mingine duniani ya kuifanania miji hii, milipuko ya magonjwa
inapotokea, huwaathiri watu wengi sana. Kutokana na hali duni tayari za afya za
wengi wa watu hawa.
Ulaji mbaya, makazi mabaya, na
kushindwa kupata hali bora za Maisha kama za watu wengi ambao tayari wanamiliki
hali za juu kabisa za Maisha, hutengeneza msongo wa Mawazo, hali za kutamani
bila kuweza kumudu, na zinginezo. huamasisha sana matumizi ya madawa ya
kulevya, au bidhaa za kulevya kwa watu hawa. Kijana ambaye asingeweza kumudu
kuendesha familia yake, na asiwe na uwezo wa kuondoka maeneo haya, hujikuta
hata familia yake tu ikimshinda.
Suluhisho pekee la kutatua
tatizo hili, ni kujisahaulisha. Hapo ndipo kukaibuka matumizi sana ya pombe,
sigara, kupenda starehe za gharama ndogo, miziki ya kupumbaza ubongo kama bendi
mbalimbali za zamani kabisa, na wakati mwingine, hata baadhi walianzisha
vikundi vya awali kabisa vya ugaidi na ujambazi, na wengine wakaanzisha biashara za kikahaba kama za
kujiuza.
KUSHAMIRI KWA URAIBU WA NGONO NA MAPENZI
Zipo sababu nyingi sana.
Kwanza, matumizi hafifu sana ya misuli, kutumia sana vyakula visivyo na nishati
bora kwa mwili, vyakula vyenye mafuta mengi hasa vyakukaanga, kuishi sana
katika jamii zenye mchangamano wa wakati wote na wanawake wenye malengo ya
kuwatega wanaume, haya na mengine mengi yalipelekea idadi kubwa sana ya wanaume
kupungukiwa nguvu za kiume.
Kadri matatizo haya
yalivyozidi kushamiri, taaluma mbalimbali na vyakula vya kutatua tatizo hili
vikazidi kushamiri. Matatizo haya yalichochea falsafa mpya ya kuwa, heshima za
wanaume wengi zinazidi kupungua kutokana na kupoteza uwezo wao wa asili.
Tatizo!! Wasomi wengi
wanachanganya kwakuhisi mara nyingi shida huwa ni nguvu za kiume, lakini ukweli
ni kuwa, shida huwa ni kuathirika kwa tabia za kiume. Hii ni kwa kuwa, madhara
yote yanayopelekea kuathiriwa kwa nishati ambazo mwanaume anazihitaji, huaribu
utaratibu wa kudumu wa wastani wa homoni za kiume. kwa kushamiri kwa mafuta na
‘’estrogens’’. kutokana na mitindo mibaya ya chakula na maisha.
Huwaondoa wanaume kutoka hali
yao ya kupuuzia vitu na shida kwa asili ‘’stoic philosophy’’, na kuwafanya kuwa
ni watu wa kujali na kuumia hata kwa vitu vya kijamii, sifa ambazo sio za kiume
kwa asili. Wanaume wa maeneo haya kwa mara ya kwanza wakaanza kufanya ngono kwa
lengo la kijamii sasa!! Afanye ngono kuzidi wenzake, au mpaka amridhishe mke
wake, au kuzidi alivyokuwa awali!! Sababu hizi na nyinginezo zikaanza
kuchanganya saikolojia ya ngono, na maisha kwa ujumla.
Malezi dhoofu marazote
hupelekea Watoto na vijana wadogo kuanza kushiriki katika tendo la ndoa kabla
ya utu uzima. Hili kama tulivyoliona katika Q5, hupelekea mvurugano wa mfumo
mzima wa hisia na kujitawala katika ubongo. madhara yake ni kuwa, vijana hawa
wanapofikia wakati wa ndoa, huwa tayari wana uwezo mdogo sana wakuwa waaminifu
katika ndoa zao, hii ni kutokana na athari zilioathiri utendaji wa ‘’Oxytocin-
katika social bonding’’ katika mahusiano ya awali kabisa.
Na sasa basi, ugumu wa Maisha
na idadi kubwa ya watu, viliwapelekea wanandoa hawa kusalitiana pale
zinapotokea changamoto kubwa za kiuchumi, au kijamii, katika ndoa zao. Hii ni
kwa kuwa, tayari uwezo wao wa awali wa uvumilivu katika mapenzi wengi wao walishauathiri.
Hii inaletaje shida? Vijana hawa huwa na shida nyingi sana za mahusiano,
mapenzi, na usaliti. Na pale inapotokea nafasi ya kuwasilisha hisia zao kama
kupitia miziki, basi huwasilisha sana machungu yao, hiki ni kielelezo cha
kutumika sio tu katika miji ya pwani hasa za kusini zenye idadi kubwa sana ya
watu kwenye eneo dogo, bali hata na maeneo mengi yenye tabia hizi.
Msingi wa Tabia Za Uchafu Katika Ngono
Ijapokuwa wengi hawatambui
msingi wa sababu za tabia kama za ushoga ‘’homesexuality’’, na mapenzi hata kwa
kutumia kinywa ‘’oral sex’’. Katika miji mikubwa kabisa ya awali, kama miji ya
Sodoma, Ugiriki, Fransisko, Miami, New York, Paris, n.k. miji hii ilikuwa ina
asilimia 100% ya mitindo yote ambayo kwa maeneo haya ninayoyaelezea bado sana
kuyafikia, japo inaelekea. Mitindo mibaya ya namna niliyoielezea, yote ilianza
katika namna ileile ya wageni, biashara, ugumu wa Maisha, uraibu, na utumwa.
Hawa watu waliishiwa kabisa
nguvu na tabia za kiume. Na suluhisho la kuendelea kupata msisimko kupitia uke,
haikuwezekana. Hii ni kwa kuwa, msisimko endelevu wa kihisia, hasa kupitia
kutazama taswira za mihemko ya kihisia, huufanya ubongo kupunguza mhemko wake
kwa hisia. Hii ni ili kuzuia, kushtushwa shtushwa na hisia.
Idadi kubwa ya wanawake
wanaojirahisisha kwa ngono, huongeza idadi ya wanaume wanaofanya zinaa, wanaume
hawa wakati huo huo wapo katika mazingira wanayopata lishe dhaifu, na makazi
hatarifu. Hii huufanya Ubongo kupunguza msisimko wake katika mapenzi ‘’brain
receptors desensitization’’, ambapo, kwa matendo yaleyale sasa mtu hasisimki
tena kwa kiwango kikubwa.
Sasa ili mtu asisimke tena,
suluhisho ni kutumia sensa chache zilizobakia
‘’sensory receptors’’, kuzisisimua sana, mpaka mwisho, ili ubongo uweze
kupata msisimko sawa na ule wa zamani ulipokuwa mzima. Na hapa sasa, hutumia
sehemu za nyuma ya maumbile ambazo huwa ni ngumu sana, na hivyo, huweza kusisimua sana uume. Lakini pia kutumia
mdomo ambao nao una uwezo wa kujishepu kutengeneza msisimko mkubwa, huweza
kusisimua. Kwa kufanya hivi, watu hawa wasio na nguvu za kiume, hujihisi
kusisimka tena.
Kwa upande wa wanawake ambao
wao fiziolojia yao ya ubongo mara zote, hukinzana na kusisimka mpaka mwisho,
pale wanapokuwa hawako na wanaume wanaowaamini, kutokana na sehemu yao ya
ubongo inayoitwa ‘’Anterior cingulate cortex’’ kutojizima ‘’shut-off’’, kwao
pia namna ya kujiridhisha huwa kupitia, matumizi ya madawa, usisimuwaji wa
Clitoris kwa kutumia viungo vingine kama vidole, na haya yote ni matokeo
yanayotokana na ubongo wa watu baadhi walioathiriwa sana, wa miji ya namna hii
kama Miami au Paris, kutokuwa sawa.
MSHAMBA AKIFIKA MJINI
Kama ilivyo kwa dawa za kuzuia
maumivu kwa wagonjwa wa saratani, ‘’opioids’’ zinapotumika kwa watu wasioumwa,
huwa ni madawa ya kulevya yenye mhemko mkubwa sana. Ndivyo ambavyo huwa kwa
watu wote ambao hawakuwa waathirika, na kisha wanapofika katika maeneo haya kwa
mara ya kwanza. Kukutana na misisimko mikubwa sana katika kila tendo, katika
kila hisia. huwafanya kuwa ni waraibu wa ghafla, na tena, kwa kiwango kikubwa
zaidi.
KUKUA KWA USANII
Miji yote mikubwa hushamiri
sana kwa usanii. Ugumu wa Maisha ya jamii, na uchache wa fursa za nje, husukuma
sana matumizi ya vipawa vya ndani katika kutengeneza fursa. Msingi wa usanii
mara nyingi huwa ni upekee. wasanii hupata nguvu sana katika jamii kubwa za
watu, kwa kuwa, mara nyingi miziki huwa na uwezo wa kuzungumza na kufariji watu
kwa lugha zote mbili, lugha ya maneno, na lugha ya hisia. Uchakataji wa muziki
katika ubongo huusiana na uzalishwaji wa homoni za msisimko, hasa dopamine.
Lakini ili muziki ukue
unahitaji usikilizaji uliolengwa kibiashara zaidi, na sio kutuliza tu hisia za
watu. Na kwa namna hiyo, utumiaji wa midundo ‘’drums’’, na ala zinginezo, tena
kwa mapigo ya haraka haraka, na mengi kwa wakati mmoja ‘’polyrhytms’’, huchochea sana uzalishaji wa dopamine kwa
kiwango cha kupelekea uraibu. Unaweza rejea Q4, sehemu ya sayansi ya ubongo ya
muziki.
Muziki wa mtindo huu ambao
huchochea sana kupumbazwa kwa ubongo kama tulivyoona namna urudiaji rudiaji wa
mabiti kwa kiwango kikubwa sana, huathiri utendaji wa sehemu ya mbele ya
ubongo, matokeo yake huwafanya watu kuwehuka kihisia. Hupelekea hisia za
kucheza, huchochea kupungua kwa stress, na huu ndiyo msingi wa watu kununua na
kununua zaidi muziki.
Kadri muziki unavyohusisha
zaidi visa vya kijamii, ndivyo unavyopata mashabiki wengi zaidi. Miji hii mingi
kutokana na urahisi wa usafirishaji, mawasiliano, na biashara, ilishamiri kwa
haraka sana kuweza kupata vifaa vya awali kabisa vya uundwaji bora zaidi wa
muziki wa kisasa.
UGENI NA UVUNJIFU WA MAADILI
Miji mingi tokea awali sana
ndiyo iliyohusisha sana matumizi ya usiku kwa shughuli za siku. Tokea matumizi
ya taa za mafuta, mpaka taa za umeme kwa kila mji, miji yote ilihusisha sana
matumizi ya usiku. Wakati wa jioni miji mingi sana ya pwani ilihusisha watu
toka maeneo mbalimbali kuelekea maeneo ya kingo za Bahari, kubarizi.
Kadri watu walivyokuwa
hawafahamiani, ndivyo pia watu walivyokuwa huru zaidi kujiachia bila kubanwa na
sheria za maadili, ambayo, kadri unavyokuwa mzawa, ndivyo unavyofatiliwa sana
utovu wako wa kimaadili. Hivyo wageni wengi, wa mbali na karibu, walijikuta
wakiwa huru sana katika Kutenda matendo yasiyo ya staha kabisa katika miji hii.
jambo hili liliwaathiri sana Watoto wa maeneo haya. Ambao kwao, hapa ndipo
palikuwa nyumbani.
Kadri siku zilivyoendelea kusonga, vijana hawa wengi wakakua wakiwa wamezoelea matendo haya ya uvunjifu wa maadili. Hii ilihusisha matumizi ya lugha chafu, matendo machafu, mionekano mibaya, na kuiga matendo ya nje yasiyo mazuri kimaadili. Unaweza kurejea Q4 kuelewa zaidi msingi wa mmomonyoko huu kisaikolojia.
UTANGULIZI
Hakukuwa na namna ya kuelezea ufupisho wa kitabu hiki
bila kutumia kisa juu. Kisa hicho ni sehemu ndogo sana inayoweza kukuonesha
kuwa, misingi ya tabia nyingi sana katika jamii yoyote ile. Uharibifu wa
kitabia katika jamii yoyote ile. Unaweza kuwa na historia yenye sababu pana
sana. Hii ni kusema, kwa mtafiti au msomi wa kawaida, ni ngumu kuelewa! Na ni
rahisi kusema kuwa, watu Fulani huonesha sana tabia Fulani, kutokana na jambo
moja Fulani. huu huwa ni udhaifu sana wa kujifunza misingi ya tabia Fulani, kwa
lengo la kuwasaidia watu. Tabia hazitabiriki, hii ni kwa kuwa, utokeaji wake huwa una mnyororo
mrefu sana.
Kama ungekutana na mtu
anayeonekana yupo timamu kabisa
barabarani, aidha kwa namna anavyoonekana na hata kimavazi, lakini anaonesha
kuchanganyikiwa huku akilia! Sio busara kusema mtu huyu ni kichaa kwa kuwa
anaonyesha tabia isiyozoeleka, busara ni kufuatilia historia yake kwa ufupi
mpaka alipofikia hatua hiyo. Na huo ndiyo msingi wa matibabu yote ya kidaktari,
huanza na ukusanyaji wa historia.
Natambua ni vigumu sana kwa
mtu mmoja kuweza kuzoelea taarifa nyingi sana kuhusiana na watu, Historia na
mazingira yao, na fiziolojia zao, hata akafikia kiwango cha kukaribia kuelewa
kabisa sababu za misingi ya matatizo
mengi ya kitabia , na hata hali zao. Lakini hata hivyo, inawezekana kwa neema
za Mungu, kwa kuwa, Mungu hataki yeyote apotee.
Kitabu hiki ni matunda ya
Upendo wa Mungu. Katika kitabu hiki tutajifunza kiundani kwanza kabisa, sababu
za msingi za awali kabisa za hali za kijamii kwa kila eneo, kisiasa,
kiutamaduni, kimazingira, kiimani, na kiuchumi.
Baada ya msomaji kuelewa
sababu za msingi kabisa za msukumo wa hali na tabia yake, na ya jumuiya yake.
Lengo sasa la mwandishi litatimia la kuweza kueleza ni kwa namna gani
inawezekana sasa, kucheza na jamii yeyote ile kama inavyochochewa na wataalamu
wachache, ambao hata na wao kwa wakati mwingi hawajielewi. Lakini wanashiriki
katika kukamilisha haya, ambayo yamelenga zaidi katika uharibifu wa hali na
tabia za binadamu wenzao. Kisa cha Pentagon mwanzoni kabisa kilihusisha
ubainifu wa hali kadhaa zisizo za kawaida, uchambuzi zaidi tutauangalia kwa
sehemu za mbele.
Kumbuka pia kuwa, Kama kuna
jambo limekuwa likileta changamoto kubwa sana kwa wasomi wengi, ni maamuzi
binafsi ya watu ‘’free will’’. Watu hawatabiriki. Maamuzi ni siri ya mtu
isiyotabirika. Kama kuna jambo linaloibua hisia za maumivu sana, ni pale watu
baadhi wanaposemwa kuwa wana uwezo mdogo wa kuzaliwa, katika kufanya maamuzi
yao. Ubora wa maamuzi ya mtu, hupimwa kwa matokeo ya anachoamua. Matokeo
hafifu, duni, na ya kudharaulika kwa baadhi ya vikundi vya watu, mara zote
huwasukuma baadhi kuwadhania watu hao ni dhaifu kwa asili. Na huu ndiyo mgogoro
mkubwa sana wa hisia za ubaguzi ‘’racism’’.
Siri ya nguvu kubwa
iliyojificha nyuma ya kila tabia, na inayosababisha kila tabia ya mtu, na jamii
yake, imekwisha elezwa na wataalamu wengi sana wa sayansi za tabia. Kitabu hiki
kina ajenda kuu moja, Tabia nyingi za ajabu za watu huwa zikihamasishwa, na
hata kutengenezwa. Tabia hizi hazitengenezwi na sababu moja, zinatengenezwa na
vitu vingi sana. Ambavyo, Pamoja na uwingi wake, bado kuna sababu zilizo na
nguvu zaidi. ambazo kwa hizo, baadhi ya watu huzitumia kwa faida yao kuwaathiri
wengine. Idadi kubwa ya watu hudharau kutawaliwa kimwili na kifikra, lakini muitikio
wao huthibitisha zaidi kuwa wao ni mateka mahututi kabisa.
Hakuna uwezo mkubwa wa watu
baadhi katika kufanya lolote lile zaidi ya wenzao kwa kila wakati. mara zote
uwepo wa sababu za kina huwa ndiyo msingi wa tabia Fulani. matokeo yanapokuwa
yakionekana mara zote, huwa pia kuna sababu. Uharibifu pia, huwa una sababu.
kitabu hiki kinarejelea historia nzima ya dunia mpaka ilipofikia kwa mtazamo
mpya kabisa ambao haujawahi zingatiwa.
Historia ndiyo nguzo pana
zaidi ya kujifunza sayansi tena zaidi hata ya fiziolojia, Jiografia ndiyo
maabara pana zaidi ya kujifunza sayansi zaidi mara elfu ya maabara, inahitaji
uwezo mpana sana wa kujifunza katika mazingira yasiyotabirika, kuliko mazingira
yaliyotabirika, kama mazingira ya katika utafiti wa kawaida wa kisayansi.
Kupitia kitabu hiki msomaji
ataelewa kwanini kila bara duniani lina watu wenye hali na tabia hizo
walizonazo, msomaji ataelewa kwanini wengine wanaonekana kuwa na mafanikio
zaidi ya wengine, msomaji ataelewa kwanini wengine wanaonekana kuwa wadhaifu au
tabia Fulani kuliko wengine, lengo hapa halitakuwa kujifunza historia. Lengo ni
kuanza kujifunza kusoma sababu za hali mbalimbali za watu, ili iwe rahisi sasa
kuelewa lengo kuu la mwandishi la kwa namna gani, kwa kuiga utaalamu huo
kushepu hali na tabia, sasa unaweza kutengeneza tabia za hovyo kabisa, na hali
ngumu zaidi kwa watu, tena kuwatawala kabisa kifikra kama inavyoendelea hali
hiyo sasa hivi.
kupitia mlinganyo kielelezo
uliotengenezwa kwa logic pana zaidi kutokana na elimu za tabia. B(p) = Eqm ±
UPEKEE WA KITABU
Kipa hajawahi kuwa sehemu kubwa ya mchezo
uwanjani, lakini amekuwa ni mwamuzi mkubwa sana wa matokeo ya mechi. Kipa huwa
na mpira kwa wakati mchache zaidi ya mchezaji yeyote yule. Kipa anapokuwa na
muda mwingi zaidi na mpira zaidi ya wachezaji, basi ujue mpira umekwisha, na ni
matuta ya penati sasa. Mpira ni Maarifa, wachezaji ni sehemu yenye watu wengi
zaidi duniani, ambazo ni sehemu za Bara la Ulaya, na Asia. Makipa ni sehemu za
watu wachache sana duniani, ambao ni Marekani, na Afrika. Kipa wa marekani ameshapoteza mpira katika nafasi
yake. Kipa pekee aliyebakia kutegemewa kwa ushindi, au Nuru ya Maarifa, ni Afrika. Kama Waafrika tutaipoteza nasi
nafasi hii, basi hakutakuwa na nafasi zaidi ya ushindi kwa maarifa.
Kumbuka, hakuna nafasi ya kucheza zaidi
ya Matuta ya penati. Hakuna nafasi ya kuelewa zaidi maarifa, zaidi ya namna hii
inayotumika katika uandishi huu. Msomaji yeyote hata aliyesoma soshiolojia,
fiziolojia, ethnobiolojia, na anthropolojia za watu wote duniani, bado hajui
vingi tutakavyoviangalia humu. lengo ni kushinda hisia za uovu, na kuinuka, na
kuokoka kutoka katika madhara yote ya kutuangamiza.
Kwa miaka maarifa yamekuwa yakitegemewa kutoka kwa watu wenye sifa na nafasi kubwa sana za kuheshimika, lakini sasa ni wakati wa makipa, wachezaji wote wamekwisha shindwa. Sitatumia muda mwingi kuelezea wasifu wa mwandishi, maana makipa wote huvaa namba dhaifu au ndogo zaidi katika timu. lakini ndiyo huwa na muda mwingi zaidi wa kuiangalia mechi toka inaanza, kumbuka! hakuna kipa aliyewahi kushinda ‘’ballon D’or’’ au tuzo ya mchezaji bora.
SHUKURANI
Mungu alituamua tuwe Waafrika tutakaotumika
katika dakika za jioni kabisa kusaidia jamii zetu, maana mimi kwa mfano, sikuwahi
chagua kuzaliwa nilipozaliwa, wala katika familia niliyozaliwa. Kwa kazi zote
ntaendelea kumshukuru kwanza Yeye Mungu wetu. Uandishi wa kitabu hiki
ulichochewa tokea nikiwa mdogo sana na Baba yangu, Marehemu Godwin Efraim Shoo.
Alikuwa na Vitabu vingi sana, ambavyo
Pamoja na kutengeneza Library ‘’maktaba’’ yangu binafsi chumbani kwangu, nikiwa
darasa la Tano, bado vingi sana vilishamiri katika kila kabati nyumbani,
nilivisoma vitabu karibia vyote. Vitabu vilishamiri aina nyingi sana za
taaluma, na historia, na stori. Vingi nilizidi kuvielewa zaidi kadri muda
ulivyosonga. Lakini kikubwa zaidi, nilipokuwa mdogo nikijifunza kusoma vizuri,
Baba yangu alinizoelesha kutumia Biblia kama kitabu cha kujifunzia kusoma,
siwezi kusema niliisoma Biblia yote, ila ninachokumbuka stori zake zilinifanya
niisome sehemu kubwa sana, popote palipo na stori, kasoro Ufunuo wa Yohana, na
pale vinapozungumziwa vizazi vya watu.
Nilipopata tu Nafasi ya Kwenda kusoma
Shule ya Sekondari, nikapewa nafasi ya kuwa ‘’Librarian’’ au ‘’Mtunza maktaba’’
wa kwanza kabisa, kwa maktaba ambayo haikuwahi tumika kwa miaka mingi sana,
maktaba ilikuwa nzuri sana, japokuwa vitabu vyake vingi havikuwa vya kiwango
cha ‘’ordinary level’’, lakini kumaliza kwangu syllabus kabla ya wakati,
kulinipa muda mwingi sana wa kupitia vitabu hivi vizuri.
Waadventista wasabato japo ni watu
wakawaida sana, ila wana maarifa makubwa sana. Nilipokuwa kidato cha Pili,
nilipata nafasi ya kujifunza zaidi nao, nilisoma vitabu vyao vingi sana, hasa
vya Ellen G. White, nilipendezwa sana nao hasa kutokana na uwezo wao mkubwa wa
kuelewa vitabu vyote vya Biblia ikiwemo na Ufunuo wa Yohana, na Danieli, tena
bila kukinzana kimaarifa popote pale katika Biblia yenyewe na ukweli wa kila
Nyanza, kama sayansi, historia, na falsafa. Tofauti kidogo na wengine, ambao
kuna wakati huacha baadhi ya maswali kwakuwa na majibu ya mitazamo binafsi,
Nyumbani kwa asili Baba alikuwa ni Mlutheri, na mama alikuwa ni Mkatoliki.
Walinizoelesha kujifunza Biblia, na walinipa Uhuru wa kuamua Imani yangu kwa
uhuru.
Unapokuwa mwanafunzi na unapenda sana
sayansi, lugha, Jiografia, na Historia. Watu huisi utabadilika tu uendeleavyo
kuchagua fani mojawapo. Lakini stori huwa haipo hivyo marazote, hata Pamoja na
kuendelea na PCB kwa ‘’A-level’’, lakini bado nilitumia muda sawa pia na kwa
Jiografia, Historia, Siasa, Jamii za Siri, na Biblia. Changamoto kubwa
niliyoipata ilikuwa tu ni kuweza kujifunza sana ‘’Advanced Mathematics’’ kwa
kuwa, Baada ya kupata nafasi ya Kuendelea na masomo ya Chuo Kikuu katika fani
ya ‘’Veterinary Medicine’’, bado ilinibidi nijifunze zaidi ‘’Modern Theoretical
Physics’’, jambo lililonigharimu sana, lakini hata hivyo nilifanikiwa kwa
kiwango cha msingi wa kimaarifa.
Veterinary Medicine ni fani ambayo kwa
haraka naweza sema, inampatia mwanafunzi wake upana zaidi wa kuelewa sayansi za
afya na maisha. Hii ni kutokana na namna masomo yake yanahusisha uchambuzi wa
kina sana wa kila kiumbe, kuanzia wadogo kama minyoo, virusi, fangasi, protista
na bakteria, kisha Wadudu kama viroboto, kupe, nzi, mbu, n.k. kisha Wanyama
wadogo wa porini kama Nyoka, panya, sungura, konokono, n.k. kisha makundi kwa
makundi ya Wanyama, utajifunza paka, mbwa, nguruwe, punda, farasi, ngamia,
kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe, Samaki. utasoma wanyamapori kama simba, tembo,
twiga, viboko, faru, swala, nyumbu, pundamilia, na tena kwa aina zao, Wanyama
hao unapokuwa unajifunza, utajifunza kwa wastani wao na Binadamu. Kuna masomo
ambayo utajifunza moja kwa moja kumhusu binadamu, kama ‘’afya ya jamii’’.
Taaluma hii bila kuficha, hutoa msingi
mpana zaidi wa kuelewa sayansi zote za misingi ya afya na maisha, kuanzia
viungo ‘’anatomy’’, fiziolojia, Utendaji wa magonjwa ‘’patholojia’’, madawa,
vyakula, vimelea vyote, jenetikia, teknolojia za kisasa, upasuaji, mionzi, n.k.
kitu pekee ambacho hautakipata, ni ubora mkubwa wa kitabibu! Hii ni kwa kuwa,
hautakuwa na muda wa kutosha na kiumbe mmoja mmoja, au uamue kuwekeza
‘’specialize’’ kwa Wanyama baadhi tu. hii nimeisema ili kuonesha ni kwa namna gani,
asili ina malengo yake katika machaguo yake.
Mfumo wa elimu husaidia sana kuwatembeza
watu maeneo mbalimbali nchini, na hata nje ya nchi. Lakini hauwezi jua maeneo
yote kwa kuyafika, ila kwa kuongeza uwezo wa kuzingatia. Namshukuru sana awali
kabisa Baba yangu mkubwa ‘’Frank Mmary’’ huyu ni mtaalamu wa ‘’Anthropolojia
kwa kuijua nchi nzima ya Tanzania, na Afrika’’. Ametembea vyakutosha, na anajua
vya kutosha, alinipatia Courses kadhaa katika kujifunza ‘’soshiolojia’’.
Namweka sambamba kabisa na ‘’Prof-Jared Diamond’’, huyu kwangu ni wa muhimu
sana. Siwezi kuficha kutumia sehemu yake kubwa sana ya tafiti zake, lakini
nasikitika kuwa hata na yeye bado kuna vitu alichanganywa pia, lakini kupitia
kitabu hiki, sehemu kubwa itafahamika kwa vizazi vijavyo.
Kila msomi anapokuwa hajui, huwa
anatengeneza Imani ‘’Hypothesis’’, ambayo atakuwa akitenda kuitegemea. Na huo
ndiyo msingi wa Ubongo, hata kama unajenga jengo ambalo hujawahi lijenga au
liona, huwa unatengeneza kwanza taswira yake kichwani, kupitia network za
ubongo zinazoitwa ‘’Default mode network’’. Wanasayansi wengi hutengeneza Imani
kwanza katika nadharia ya ‘’Evolutionary science, na Big Bang’’, hasa pale
wanapokuwa hawajui. Na hapo ndipo panapowafanya ‘’average minded’’, Kitabu hiki
kinatumia sayansi kujifunza. historia na falsafa zote, zimejikita toka kwa
Biblia, na Rekodi za uhakika, sio mamilioni ya miaka ya Radio-Carbon datings,
nilishaeleza katika Q1 na Q3, hazina uhalisia katika vipindi virefu hizi mbinu .
Labda wengi hawaelewi kuwa, Baba wa
Sayansi mara zote huitwa ‘’Isaac Newton’’ na ‘’Galilei Gallileo’’, hawa wote
nao waliweka Biblia kama mimi ninavyofanya, siyo hivyo tu, sidhani kama kuna
majitu yaliyokuwa ‘’technical’’ kama ‘’Nikola Tesla, Leonard Da Vinci, na John
Von Neumann, wenda na wengine wasiopo katika rekodi, lakini wote walisema
nilichosema.
kinachowashangaza wengi juu yangu leo, ni
kwanini niiweke Sayansi mikononi mwa Mungu! Na mshangao huu ndiyo ulioifanya
sayansi ianguke mpaka leo hii hakuna jipya, hata zaidi ya 80% ya tafiti zote ni
matokeo ya kukopi na kupesti kazi zilizokwisha fanyika, hakuna nadharia mpya
iliyo bora, tuzo za sayansi mwaka 2024 mfano zote ni matokeo ya Chat GPT au
Roboti, Ubongo wa wengi umeishiwa kabisa Nguvu. hakuna kitabu unachoweza
linganisha na Biblia linapofika swala la Maarifa, na ndiyo maana, hata kwa
mwanasayansi kipenzi wa wengi ‘’Albert Einstein’’ ambaye ilionekana kana kama
hana Imani kwa ‘’Mungu na Biblia’’ kutokana na Uyahudi wake, falsafa za kutoka
katika nadharia yake ndiyo imechochea kuiua sayansi, haina matumizi makubwa
maishani, ni ngumu kwa wasioielewa, na hata hivyo, ni sahihi kabisa kwa maelezo
ya walioifanyia kazi kabla yake, wakina ‘’Poincare, na Lorentz’’, kabla ya yeye
kuikopi ‘’plagiarize’’ na kuipa tafsiri zake, na kufanywa ‘’hero’’ kwasababu za
siri sana.
Kumbuka, wanasayansi wasio makini huisi
ni Imani za kufikirika kupaa kwa Yesu kinyume na matokeo ya ‘’gravity’’, lakini
wanasayansi makini wanatambua fizikia bado ina miujiza mikubwa zaidi ya kupaa
kwa yesu, kama asili ya kani ya gravitation ‘’unawezaje kutengeneza
gravitation’, bado kuna ‘’three body problem’’,wanabiolojia wanatambua hakuna
muujiza mkubwa duniani zaidi ya chembechembe zinazounda ubongo
‘’molecules’’ kutengeneza utambuzi
‘’consciousness’’, wanakemia wanatambua hakuna muujiza kama namna maelfu ya
chembechembe, na kani zilivyo katika balansi yenye usawa wa asilimia 100%, bila
kosa hata la 0.01 unit ambalo lingepelekea kusiwepo uhai, wanajiografia
wanatambua hakuna muujiza kama namna ilivyo sayari ya Dunia tu, kati ya
matrilioni ya sayari na nyota, yenye sababu matrilioni kusapoti Maisha. na
wanahistoria wanaoana ni muujiza sana kila taarifa inayotokea, ilishanukuliwa
na Biblia, na Biblia ndiyo msingi wa Maarifa ya kweli na uhai.
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA KUSOMA
Kitabu hiki hakina msingi wowote wa kuonyesha
kuwa kuna kundi Fulani, ni dhaifu kuliko kundi lingine. Hayo yanaweza kuwa ni
madhara ya kusoma juu juu. Mfano, kwa kisa pale juu, kwanini kulikuwepo na
makabila dhaifu? Utakaposoma zaidi huko chini, utaelewa kuwa, hawakuwa dhaifu,
ila mfumo wao uliwafanya, na sasa kujua mfumo wao, unapaswa kujifunza zaidi.
Kitabu hiki kitatoa ufupisho sana wa mada
za historia za mazingira, na tabia za jamii Fulani. hii imelenga katika
kupunguza ukubwa, na kumchosha msomaji, historia tu ya Kijiji kimoja ingeweza
kuhitaji kitabu kizima, vipi kuhusu dunia? Na sasa basi, tutazingatia zaidi
hoja za msingi, ili tuweze sasa kuingia katika mada za muhimu kabisa na lengo
la mwandishi.
UPATIKANAJI WA KITABU
Utangulizi na ufupisho wote wa kitabu, unaweza upata bure kabisa, kupitia blog, ya injili ya sayansi. Lakini kupata kitabu kizima itahitaji gharama za kukinunua. Sababu kubwa ni kuwa, ‘’Ilipo hazina ya mtu, ndipo ulipo moyo wake’’, kitu ukikigharamia, utajua thamani yake. Lakini kuonyesha kuwa hatujali zaidi maslahi ya kibiashara, bali tunajali kusaidia jamii. Kitabu hiki kitauzwa kwa thamani ndogo sana, si sawa na vitabu vingi katika shelves za Amazon.
YALIYOMO
KISA
KIFUPI CHA MTAA MMOJA WA JIJI LA PENTAGON
KUKUA KWA MAENEO HAYA YA
PWANI
KWANINI MAENEO YA KATI
YALIKUWA NA WATU WACHACHE?
UFUPI KUHUSU MAKABILA YA
TANZANIA
KUKUA KWA THAMANI YA
PESA PWANI ZA KUSINI
Saikolojia ya Usaliti na
Ukoloni
UCHAMBUZI KWA UFUPI JUU YA
TABIA ZA WATU WA ENEO HILI
KUSHAMIRI KWA URAIBU WA
NGONO NA MAPENZI
Msingi wa Tabia Za Uchafu
Katika Ngono
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA
KUSOMA
MABADILIKO YA AWALI KABISA
YA MWANADAMU NA VIUMBE HAI
KUZALIWA KWA FALSAFA KUU
MBILI ZA DUNIA MPAKA MWISHO WAKE
KAINI MKULIMA ‘’FOOD
PRODUCTION SYSTEM’’
HABILI-MFUGAJI/MWINDAJI/MKUSANYAJI-
‘’HUNTERS AND GATHERERS’’
VIPINDI VYA UKUAJI WA
JAMII ZOTE DUNIANI
KUELEKEA MWISHO WA ZAMA ZA
AWALI
Mnara Wa Babeli Na Mwisho
Wa Zama Za Kwanza
TOKA BABELI MPAKA MIAKA YA
2000
Kwanini Kilimo Kilishamiri
Ulaya-Asia + Afrika Kaskazini, Na Hasa Bonde La Rutuba?
Kilimo Na Kukua Kwa Kasi
Kwa Ulaya-Asia Na Afrika Kaskazini
Kwa Hiyo Wa-Afrika,
Marekani & Australia Walikuwa Na Bahati Mbaya!
Kukua Kwa Biashara,
Usafirishaji Na Afrika
Kielelezo Cha Mduara Wa
Maarifa, Ugunduzi Na Nguvu Cha Shoo
Kosa Kubwa Lililo
Wagharimu Waafrika Na Wamarekani?
Nini Maana Ya
Environmental Brain Sensory Potentials ‘’EBSP’s’’
Nini maana ya Tropiki, na
Sub-tropiki?
Kwanini Iringa na Mbeya
Zinaongoza Uzalishaji wa kilimo Tanzania?
BIOLOJIA ZA WATU KWA ASILI
KWA MAZINGIRA YA KUSINI JUU.
Kufanya Sana Kazi na Kuwa
na Nguvu.
Kuwa na Mapafu imara na
Mwonekano wa wastani wa Ufupi
SAIKOLOJIA ZA WATU KWA
ASILI KWA MAZINGIRA YA KUSINI JUU
Asili Ya Upole Na
Kutowehuka Kirahisi
Msukumo Mdogo Wa
Utandawazi na Teknolojia
Uwezo Mkubwa Wa Kitaalamu
Na Kitaaluma.
CHANGAMOTO ZA KISAIKOLOJIA
ZA WATU WA NYANDA ZA JUU KUSINI
Upweke Hasa Kwa Wanawake
(Huwasukuma Zaidi Kwa Manabii Na Makanisa)
Changamoto Za Kifamilia Na
Maamuzi Magumu
KASKAZINI ‘’NYANDA ZA
BARIDI’’
Historia Inavyojenga
Msingi Wa Tabia Za Watu Wa Kaskazini
BIOLOJIA ZA WATU WA NYANDA
ZA KASKAZINI
SAIKOLOJIA ZA WATU WA
NYANDA ZA KASKAZINI
Msukumo Wa Unywaji Wa
Pombe Na Matumizi Ya Madawa Na Bangi
Ujanja, Usomi, Udini, Na
Uchumi
Historia Fupi Yenye
Kujenga Msingi Wa Tabia Za Watu Hawa
BIOLOJIA ZA WATU WA MAENEO
YA KANDA YA ZIWA
SAIKOLOJIA ZA JAMII
MBALIMBALI ZA WATU WA KANDA YA ZIWA
Kupenda Sana Sifa ‘’Baadhi
Ya Wahaya’’
Kuchelewa Kustaarabika
‘’Baadhi Ya Wasukuma’’
Kutunza Jadi Zao, Na
Kupenda Utawala
UWANDA WA KATI, MAGHARIBI
NA KUSINI
BIOLOJIA ZA WATU WENGI WA
KANDA HIZI
Kwanini Kanda Hizi
Zinaongoza Kwa Afya Dhaifu Zaidi?
SAIKOLOJIA ZA WAKAZI WENGI
WA MAENEO HAYA
Imani Za Uchawi
‘’Sumbawanga’’
NYANDA ZA MASHARIKI KATI,
PWANI MPAKA VISIWANI
Uwanda wa Kati Mashariki
na Sehemu Za Pwani
BIOLOJIA NA
SAIKOLOJIA ZA WATU WA MASHARIKI, PWANI,
MPAKA VISIWANI.
SAYANSI YA KUKOLONI WATU
KWA KUWATEGENEZEA TABIA BILA WAO KUJIJUA
Upekee Wa Tanzania Zaidi
Ya Afrika Nzima?
Matokeo Ya Awali Ya
Saikolojia Ya Watanzania
Vita Iliyofichika Kuhusu
Tanzania
SAYANSI YA KUHARIBU TABIA
ZA WATU NDANI YA WAKATI MFUPI
Mlinganyo Wa Hisabati ya
Tabia
Kuua Uwezo Wa Watu Kuujua
Ukweli ‘’Abstractive Destruction’’
Kuua Mifumo ya Kusapoti
Elimu ya Kweli
Kuua Uwezo Wa Watu Kuuishi
Ukweli ‘’Integrative Destruction’’
SAYANSI YA KUUA UWEZO WA
WATU KUUISHI UKWELI.
KUTUMIA VIWANDA VYA
VYAKULA ‘’Food Industry’’
Chochea matumizi ya Bidhaa
za sukari, kama soda, Biscuits, Energy drinks, Fruit Juices, n.k
Chochea Matumizi ya Nyama
na Protini za Wanyama
Chochea Matumizi ya Bidhaa
Zote Hatarishi, kama Pombe
Chochea Matumizi ya Madawa
katika Kilimo na Ufugaji
KUTUMIA VIWANDA VYA DAWA
‘’Drug Industry’’
Kutumia Sanaa Za Michezo,
Burudani Na Usanii
KUIBUA NAMNA BORA MBADALA
WA UKWELI ‘’Creative Destruction’’
Hakuna namna ya kufuga
Wanyama wa kisasa bila madawa
Unawezaje Kuuza Duka bila
kuhusisha Bidhaa za Kisasa zenye Madhara
Unawezaje Kuwa
Mwanasayansi ilihali unamwamini Mungu
Mifumo yote ya Mali ipo
mikononi mwao
Binti anawezaje kupendeza
kwa kuvaa mavazi yakujifunika sana
Tutakula nini sasa, maana
hivyo ndivyo vyakula vyetu
KUTAWALA WATU WASIO NA
UPINZANI ‘’Mental Colonialism’’
SURA YA KWANZA
MABADILIKO YA AWALI KABISA YA MWANADAMU
NA VIUMBE HAI
Historia ya Mwanadamu
Sitarudia asili ya mwanadamu, na
ulimwengu mzima kama tulivyoona katika Q3.(unaweza soma kitabu kizima Bure
kabisa katika blog ya Injili ya sayansi) Hapa tunaenda kuangalia mabadiliko
makubwa kabisa ya viumbe toka hatua yao ya kwanza, mpaka kufikia hatua yao ya
mwisho, yaani hali zetu sisi.
Ni kinyume kabisa na mtazamo wa
wanamabadiliko wa ‘’evolution’’. Binadamu wa kwanza, na viumbe wote wa kwanza
walikuwa bora kabisa, tena katika ufanisi wao wa asilimia 100%, na kadri siku
zilivyokuwa zikizidi kusonga, basi na hali zao zikazidi kuwa dhoofu. Sio kwamba
viumbe wa kwanza walikuwa mambumbumbu kabisa tena zaidi hata ya nyani, na kisha
wakaanza kuwa bora mpaka hali zetu tulizonazo leo.
Binadamu alikuwa katika hali ya ubora
sana, kisha akaathiriwa hata kuwa katika hali ya udhaifu kabisa, na kisha
akapanda na kuanza kurejea hali ya ubora angalau tena, na kisha akashuka katika
ubora, akawa dhaifu kama hali zetu tulizonazo hivi leo.
Rejea kielelezo cha ramani fupi ya
kielelezo hiki ninachokisema.
|
|
|
|
|
|
|
|
Ukiangalia mabaki ya viumbe wengi wa
zamani ‘’fossils’’, walikuwa wakubwa sana. Wanahistoria huona vichwa vya
Wanyama wazamani kuwa vilikuwa vikubwa sana ukilinganisha na vichwa vya Wanyama
wa sasa hivi. Ukiangalia migodi ya mafuta, na makaa ya mawe, unapata taswira ya
uwingi na ubora sana wa vyakula, na mazingira katika jamii ya zamani sana.
Lakini pia, jamii za zamani hazina mabaki mengi sana ya maandishi, vifaa vya
teknolojia, n.k. hii ni kuonyesha kuwa walikuwa na uhitaji mdogo sana wa vifaa
hivi kwa kazi zao, ni kama ndege asingehitaji drone ya kurukia hewani. Uwezo
mkubwa wa kumbukumbu hupunguza sana uhitaji wa makablasha kama vitabu vya kutunza
kumbukumbu pale unaposahau.
Adamu aliweza kuwaita majina viumbe wote,
kumaanisha, alijua Biolojia ya viumbe wote, maana, huwezi mwita mnyama jina
bila kumjua ‘’ sheria za Taxonomy’’, kumbukumbu ya viumbe vyote isingekaa kwa
kichwa cha kiumbe wa kawaida, alikuwa na uwezo asilimia 100%, hakuwa mla nyama,
wala mtumiiaji wa bidhaa za kisasa, hakuwa na madhara yoyote katika Ubongo.
Aliweza kuzungumza na Mungu aliyemuumba, alijua sheria nyingi sana za uumbaji
wake, au fiziolojia yake, hakufanya vitu kwa msukumo wa dhiki, bali kwa msukumo
wa utajiri, alikuwa na uwezo mkubwa zaidi.
Kiwango cha oksijeni kilikuwa bora sana,
na hivyo, alikuwa na uwezo bora zaidi wa uzingatiaji. Hakuwa na changamoto
zozote zile za kiafya. Na hali ilikuwa hivyo kwa viumbe wote, mimea, Wanyama,
wadudu, mpaka bakteria, virusi na wengineo.
Badiliko La Ghafla
Adamu alipotenda Dhambi kwa makusudi yake
kwa mara ya kwanza. Alidhihirisha kuwa Mungu sio mkamilifu, kiuwezo, na Upendo.
Kosa hili ni sawa na Gari kumkataa Injinia wake. Hivyo, Adamu kila
alichokifanya, kilipoharibika, hakikupata Fundi. Mungu alishalijua hili maana
alimwambia, Ukitenda Dhambi, Hakika Utakufa. Na sio, Ukitenda Dhambi, Hakika
Nitakuua! Mungu hakumuua Adamu, bali Uzee ulimuua, magonjwa, vita, dhiki, n.k. Haya
Yote ni matokeo ya mfumo kujiendesha
bila muumbaji wake.
Mungu aliviumba viumbe vyenye Uhuru wa
Kifikra ‘’free will’’ katika hali ya ubora kwa asilimia zote 100%. Lakini
alikuwa bado akiviwezesha kuendeleza hali hiyo ya ubora kupitia uwepo wake.
Mungu alilenga viumbe hivi vitakapoweza kutumia uhuru wao wa kifikra katika
kuelekea wema tu, bila uasi, basi angevikamilishia hali ya umilele katika
ubora. Lakini pia, alilenga kama havitatumia uhuru wao wa kifikra katika wema,
basi atavipatia mpango wa kuviokoa lakini si kupitia uhai tena, bali kupitia
kifo ambacho watakuwa wamekielekea.
Adamu alipoonesha kutokubaliana na Mungu,
yeye mwenyewe ndiye aliyejitenga na Mungu, akaenda mbali naye. Uwezo wa Mungu
ambao ulikuwa ukisimamia ufanisi wa matendo yote ya kimwili ya binadamu, ukawa
mbali naye, mwili wake ukaanza kukosa uwezo, ukaanza kufanya makosa, ukawa
unaelekea katika kuharibika, na kifo kwa ujumla. Wote tunafahamu, kila
unapozeeka, ndipo makosa yanapoongezeka ya mifumo yako ya jenetikia, na kifo
kinakukaribisha.
Wanasayansi huwa tukishuhudia tu namna
ambavyo mwili hurekebisha makosa yake panapotokea changamoto, huwa tunaona tu
namna ambavyo mwili huwa ukifuata maelekezo yake ya asili katika Kutenda
biolojia zake. Lakini mtu anapokufa, Pamoja na kuwa kila kitu tunaweza kuwa
nacho, ila hatuwezi kumfufua! Hii ni kwa kuwa, uhai sio umeme, wala sio
usumaku, wala sio nguvu za ATP, Uhai ni Nguvu isiyoonekana iwezayo kusukuma
matendo yote ya kiumbe hai.
Kifo kitaalamu huwa kinatokana na sababu
moja kubwa zaidi, inayoitwa ‘’Multiple organ failures or dysfunction’’. Yaani,
viungo vyote kwa Pamoja vinapofeli, au poteza wastani wake wa utendaji bora,
basi kifo utokea. Hii inamaanisha, uhai pia ni matokeo ya usahihi na ufanisi,
wa hisabati ya utendaji wa viungo na mifumo yote ya mwili.
Wanabiolojia wengi huwa hawajui kwanini
mwanadamu hawezi kufa ghafla kirahisi, ijapokuwa marazote huwa anazingirwa na
changamoto nyingi sana zinazotaka kumuua. Mfumo wa kinga wa kila kiumbe
haujawahi kutulia, kila wakati huwa unapambana kuzuia kifo, tena kwa akili
nyingi sana kuliko jambo lolote lile ulilowahi kuliona. Mfumo wa kijenetikia,
wakati wote huwa unapambana kupunguza makosa katika namna unaumba viungo
mbalimbali, makosa muda wote huwa yakitokea katika biolojia za mwili.
Hakuna jambo linalomzunguka mwanadamu
ambalo halina hatari kwake, kuanzia mwanga wa jua, hewa anayovuta, maji
anayokunywa, chakula anachokula, sauti anazosikia, Mawazo anayoyafikiria, na
hata dawa anazotumia. Hivyo Maisha ni kama kondoo anayezungukwa na dubu ambao
ndiyo wanamlisha, hayana usalama. Lakini bado tunaishi. Hii inamaanisha kuwa,
kuna Neema kubwa sana ya Mungu hata pale ambapo mwanadamu alipoamua kujitenga
naye, bado Mungu hakuruhusu ujinga wa mwanadamu umuangamize moja kwa moja.
Uwepo wa mipaka ya uhai, inamaanisha kuwa
kifo ndicho chenye mamlaka zaidi. Chukulia mfano, maji ambayo binadamu
anakunywa, bado akitumbukia ndani yake, lazima atakufa! Binadamu aliyeishi
miaka 70, na kisha akafa mwaka 10 AD, mpaka leo amekufa. Kifo kimemchukua kwa
miaka 2000, wakati uhai ulimchukua kwa miaka 70 tu. Kifo ndicho kina nguvu
zaidi. Wastani wa kufa marazote ni 99%, wakati wa kuishi ni 1%. Unaweza kumuua
mtu kwa vitu vingi sana, mfano, moto, maji, jiwe, sumu, ajali, n.k. lakini vipi
kuhusu kumfufua mtu?
Badiliko la Ghafla lilikuwa ni Kifo
kutawala juu ya Uhai. Ambapo kutawala huku kwa kifo, kulihusiana na kufeli kwa
mifumo yote ya muhimu ya Maisha. lakini neema ya Mungu, ilihusisha kutumia
kifo, kuleta tena wokovu, yaani, kwa Kufa kwake Muumbaji, kulilipa Deni la haki
yake mwenyewe, lakini kwa sharti la mwanadamu kutumia tena Uhuru wake uleule wa
dhamira, katika kuchagua uhai.
Kifo kina maana gani? Kifo kinamaanisha,
Mungu mtoaji wa uhai, ataendelea kuishi milele. Wote wanaomuasi, itawapasa
kupotea milele. Kifo kinamaanisha aibu, fedheha, ujinga, udhaifu, uovu, n.k. na
ndiyo maana hakuna anayependa kufa! Kama ukimvua mtu nguo hadharani,
hatakubali! Lakini kiburi chake kikowapi akishakufa? Ukimpiga mtu hatakubali,
ukimtukana hatakubali, lakini akishakufa! Itampasa kukubaliana na kila hali.
Swali La Kifalsafa : Vimelea Na Parasites
Kama Virusi Na Wanyama Walanyama Walitoka Wapi, Kama Uumbaji Haukulenga Kifo?
Magonjwa ya Vimelea ‘’microbial
infections and diseases’’, huwa yanatoa maswali mengi sana kwa wasomi, Kwanini
yawepo? Au Wanyama wala wenzao ‘’carnivores’’, huwachanganya sana wasomi juu ya
maswali ya nini maana ya Uumbaji uliolenga uhai tu? Maswali ya kwanini kuna
viumbe hawawezi kuishi bila kuwadhuru wenzao, yaani ‘’Parasites’’, pia huchanganya sana watu.
Lakini swali hili jibu lake ni rahisi
sana. Unapomfunga Baba kwa kosa alilofanya, unategemea familia yake itaishi
vizuri? Hivi ukimuuzi Mungu kwa Kufuru, unategemea familia yake ya Malaika
italifurahia hilo? Wanyama ni familia ya mwanadamu. Na ndiyo maana, Wanyama
marazote huwa wanamuogopa mwanadamu, au wanajilinda dhidi yake. Wanadamu na
Wanyama wote ni familia ya viumbe hai wenye mwili, hata tu mtoto mdogo anajua
Sokwe kafanana na Baba yake. na ndiyo maana, Salmonella anayemuathiri Kuku,
ndiye anayemuathiri mwanadamu. Na dawa inayomuua salmonella huyu, ikizidishwa
inaweza muua hata kuku na mwanadamu. Hivi unajua Samaki anaumwa pia TB ambayo
hata binadamu anaweza ipata, kitaalamu inaitwa ‘’Atypical mycobacteriosis’’.
Mwanadamu ndiye mtawala wa viumbe vyote,
na Wanyama ni familia yake. Kosa lake liliathiri mpaka Wanyama wadogo zaidi.
Mfumo mzima wa viumbe ukaelekezwa katika mteremko wa kifo. Tafiti nyingi sana
bila kukuchosha kwa kuziorodhesha, zinadhihirisha inavyowezekana sana hata kwa
kuangalia baadhi ya viumbe ambao walikuwa wala nyasi, walivyoanza kula nyama.
Hata Binadamu alikuwa mla mimea tu, ila akaanza kula na nyama. Na sio tu
alikula nyama za Wanyama, historia inaonyesha hata visa vya kula binadamu
wenzao, hata Biblia inasapoti hili katika zama Fulani za dhiki za kuzingirwa na
jeshi la washami, wamama kadhaa walikula Watoto wao, lakini historia inathibitisha
pia hilo kupitia vikabila baadhi ambavyo sitavitaja, lakini vilikutwa na
mitindo hii.
Wachache hutishwa na meno marefu ya
Wanyama wala nyama ‘’canine teeth’’, lakini meno haya yapo hata kwa ‘’Kulungu
maji wa China’’ au ‘’chinese water deer’’ unaweza muita, na wanyama hawa hula
nyasi tu. kama isingekuwa neema ya Mungu kwa mabadiliko ya Wanyama kama simba
kuanza kula nyama tu, basi idadi kubwa ya Wanyama wala nyasi wangeikausha dunia
kwa mwezi tu, na stori nzima ya Uhai isingetokea.
Wengi wa Wanyama wala nyama, huwa
hawahisi Ladha ya utamu sana wa nyama. Hata idadi ya seli zao za kuhisi Ladha
kwao ‘’tastebuds’’ ni chache sana, wastani wa 200 mpaka 500. Huwa wanamotisha
tu na nyama kwa kuwa Maisha yao huwa ni magumu na ya kutumia akili sana mpaka
kupata chakula, na hasa anapoelekea kuzeeka. Tofauti na wala nyasi, ambao huwa
na maelfu ya tastebuds, na huwa na urahisi wa kupata chakula, na ndiyo maana
huzaliana sana hawa Wanyama.
Bakteria, Virusi, Protista, Minyoo, n.k.
hawa wote huwa na kazi nyingi sana katika ulimwengu. Hawa ni kama mashine za
kubalansi hali za chembechembe zisizo hai ‘’inorganic’’ za dunia. Hawa
hubalansi chembechembe za madini, hewa mbalimbali katika anga, ufyonzwaji wa
virutubisho aidha katika mimea, au katika miili ya viumbe. Unaweza vuta picha
ingekuwaje tumbo la ng’ombe lingekosa hawa vimelea? Au Unaweza vuta picha
ingekuwaje utumbo mkubwa wa binadamu ungekosa hawa viumbe? Maana wao ndiyo
husaidia sana kuzalisha hata chembechembe za muhimu sana katika hali ya kutulia
ya Ubongo, kama ‘’dopa, GABA, Serotonin, n.k.’’ bado husaidia uchakataji wa
madini mbalimbali, hivyo ni muhimu sana kutambua kuwa, hawa viumbe walilenga
ubora zaidi wa mifumo ya Maisha.
Baba yao mkubwa Adamu alipoasi, nao
walitenganishwa na uwezo wa ukamilifu wa Uhai, wakaanza kuathiriwa. Wakawa
wadhaifu hata kutegemea tu baadhi ya viumbe wengine. Wengi wao hata wanapokuwa
virusi hatari kabisa, sio kuwa huwa wamelenga hivyo!! La hasha, hujikuta tu
wakisukumwa na wimbi la makosa katika mifumo yao ya kijenetikia ‘’mutations’’.
Watu wengi hawajui kuwa, binadamu ndiye muuaji mkubwa zaidi hata ya virusi,
minyoo na bakteria. Maelfu ya masumu ya viwandani, milipuko ya mabomu, madawa
makali, n.k. huwaua hawa viumbe, huwadhoofisha hata hujikuta wanabadilika na
kuwa viumbe wa ajabu kabisa, kumbuka wana akili hawa!! Kadri wanavyojilinda, na
umewaathiri sana, wanakuwa hatari sasa sio tena rafiki. Ila hitimisho ni lile
lile yote haya huonesha uasi, umepeleka kila aina ya makosa katika ulimwengu.
‘’unaweza kusoma kitabu cha injili ya sayansi cha historia na kiini cha
magonjwa, kuweza kuelewa vimelea hawa walibadilikaje na kuanza kusababisha
magonjwa.
Maisha Baada Ya Badiliko
Mwanadamu kwa mara ya kwanza sasa akaanza
kuzoelea kuishi Maisha katika Udhaifu wake. Dunia bado ilikuwa na utajiri
mkubwa sana wa maliasili, malighafi, hali bora ya hewa, n.k. lakini hata hivyo,
Uharibifu katika kila mfumo wa ulimwengu ulikuwa ukizidi kuendelea. Mabadiliko
kidogokidogo ya tabia ya nchi yalisonga mbele, viumbe siku kwa siku walizidi
kudhoofika kutokana na kushindania sana maliasili, na stress zikaanza kutawala
katika vichwa vya viumbe katika ulimwengu.
Kwa mara ya kwanza Wanyama katika dunia
ikawapasa kujisambaza katika uso wa nchi. Hii ilitokana na kuwa, baada ya
dhambi kuliibuka migogoro tofauti tofauti kati ya viumbe. Na hivyo kukabiliana
na hizi tofauti, iliwapasa viumbe mbalimbali waanze kutafuta kanda zao watakazo
kuwa na amani zaidi.
Fiziolojia mbalimbali zilibadilika na
kuwa sehemu mpya ya Maisha ya viumbe. Mfano mzuri kabisa, ni kupungua kwa uwezo
wa Ubongo hata kuanza kwa uzoefu mpya wa Kusahau. Binadamu awali kabisa alikuwa
hawezi kusahau, lakini sasa akaanza kusahau. Kusahau kulilenga kumsahaulisha
kumbukumbu za maumivu, kama vile, kifo cha mtoto habeli, n.k. lakini pia
binadamu na viumbe wakaanza kuzoelea kuchoka, na kuzeeka, na hata kufa.
Binadamu akapoteza uwezo wa ku control
hisia zake za kiuzazi, na pia akawa na uwezo dhaifu katika mfumo wake wa
umeng’enyaji. Hii ndiyo mifumo injini kuu ya kuishi, hata binadamu akiwa
kichaa, akaumwa shida yoyote ile ila akawa tu hajafariki. Ili aweze kuishi yeye
na kizazi chake, anahitaji kula, na kuzalisha. Udhaifu wa mifumo hii ndiyo
mwanzo wa kuzaliwa hisia za Uchi, au Aibu ya uchi. Kama Adamu alivyohisi yu
uchi baada ya Kutenda dhambi, ndivyo kila binadamu baada tu ya kujitambua, hujihisi
hatia anapoonekana uchi, hii ni kumaanisha kuwa, sasa hivi mtu huyu mfumo wake
‘’subconscious mind’’, unatambua kuwa ana udhaifu wa asili wa kushindwa
kujizuia, na kujitawala, na hii hali ya kudumu inatengeneza msingi wa aibu,
binadamu anaanza kuhisi kuwa yeye ni sehemu ya kifo, ni mdhaifu, anatamani
kujificha.
Familia ni sehemu kubwa sana katika historia ya mwanadamu. Wanadamu wakaanza kuoana na kujitenga na familia zao. Kadri walivyokuwa wakijitenga na familia zao, ndivyo walivyozidi kusambaa katika uso wa nchi. Ijapokuwa dunia ilikuwa na bara moja, lakini bado ilikuwa ni sehemu kubwa sana ya ardhi ya kutosheleza mtawanyiko mkubwa wa viumbe. Hata katika mtawanyiko huu wa familia kadhaa, bado kulikuwa kuna familia ambazo walikuwa waaminifu kwa Mungu wao, na kulikuwa pia na familia ambazo hawakuwa waaminifu kwa Mungu wao. Kulikuwa na familia za mitala, yaani mume mmoja dhidi ya wake wengi, na kulikuwa na familia za mume mmoja na mke mmoja.
SURA YA PILI
KUZALIWA KWA FALSAFA KUU MBILI ZA DUNIA
MPAKA MWISHO WAKE
Natamani Prof. Jared Diamond angekisoma
hiki kitabu. Falsafa kuu mbili zilizozaliwa katika Dunia hii. na kusababisha
migawanyiko yote ya mitindo ya Maisha tunayoiona leo. Ilianzia mwanzoni kabisa
kwa Watoto wa Adamu. Kulikuwa na Watoto wawili wa Adamu, yaani Kaini, na
Habili.
|
Kaini alikuwa
-MKULIMA/ MFUGAJI ‘’Food Production
system’’. Habili alikuwa-MFUGAJI / MWINDAJI/ MKUSANYAJI ‘’Hunters, Nomads and Gatherers’’. |
KAINI MKULIMA ‘’FOOD PRODUCTION SYSTEM’’
Ni kweli kabisa kuwa, falsafa ya Kulima
ilianza baada ya baadhi ya watu kuamua kuwa na makazi ya kudumu, katika sehemu
Fulani. na kisha, kuanza kutunza vyakula vyao hata kwa vipindi ambavyo
hawatakuwa wakilima.
Falsafa ya kilimo ndiyo msingi wa
maendeleo makubwa ya jamii zote kubwa duniani. Kunapokuwepo na wakulima, Jamii
hukua haraka sana. Hii ni kwasababu.
-Huwepo chakula cha kutosha hata katika
kipindi ambacho watu hawalimi, na kwa hivyo, watu hazaliana sana kwasababu,
huwa wana uhakika wa chakula.
-Huwepo na wataalamu wengi wa fani
mbalimbali. Hii ni kwakuwa, huwa kuna uwepo wa chakula chakuwatosha wakulima,
na wanataaluma wengine.
-Huwa na Nguvu zaidi ya jamii za wasio
wakulima. Wakulima huwa na uwezo wa kuwawezesha wanajeshi, wanateknolojia, wana
Uchumi, wasanii, n.k.
Jamii zote kubwa kabisa za awali
ziliendelea sana kutokana na uwepo wa wakulima katika maeneo yao. Hawa
waliwezesha jamii kujikusanya kwa Pamoja, na hata kuanza kuelekea katika
uundaji wa falme ambazo zililenga usimamiaji wa idadi kubwa ya watu, ambayo ilianza
kuibua migogoro ya kijamii.
Ni makosa kutengeneza mtazamo wa kuwa
mfumo wa kilimo uliibukia Katikati ya maendeleo ya binadamu kama Prof Jared
anavyohisi. Maendeleo ya kilimo yalikuwa ni falsafa iliyokuwa inafahamika ya
muda mrefu, na wanadamu walichokuwa wakikifanya ilikuwa tu ni kutumia mazingira
yao kufanya linalowezekana zaidi kwa wakati huo.
Falsafa ya Kilimo hata baada ya miaka
2000 ya kwanza kupita na kuangamia kwa dunia kupitia gharika ya Nuhu, ‘’unaweza
rejea sayansi nzima katika Q3’’, bado
ilibakia katika vichwa vya binadamu wote kwa asili. Wanadamu walisukumwa
kuchagua kati ya falsafa hizi aidha kutokana na mazingira yao, au kutokana na
maamuzi yao. Yakobo ni kielelezo kizuri sana cha mfumo huu wa kazi za kudumu
katika mazingira Fulani. Esau ni kielelezo cha makazi ya kuhamahama, au
uwindaji. Falsafa hizi mara zote zimekuwa zikishindana huku ya makazi ya kudumu
ikishinda.
HABILI-MFUGAJI/MWINDAJI/MKUSANYAJI-
‘’HUNTERS AND GATHERERS’’
Hii ni falsafa ya kutumia mazingira moja
kwa moja kila siku, katika kujitafutia mahitaji. Wawindaji na wakusanyaji na
wafugaji, huwa na makazi ya kuhamahama kulingana na malisho, huhama kulingana
na upatikanaji wa vyakula. Huwa hawaundi jamii kubwa za watu, hii ni kwa kuwa,
huwa hawatulii eneo moja.
Jamii za watu hawa huwa na idadi ndogo
sana ya watu. Hii ni kwa kuwa, hulenga msimu wa kuzaliana ambao hauhusiani na
shughuli za safari za masafa ambayo Watoto hawataweza kusafiri. Hivyo huzaa kwa
mpango. Pia, huwa hawakusanyikani kwa wingi kwa kuwa, huwa hawapendelei
ushindani wa malighafi chache zilizo katika mazingira.
Jamii hizi mara nyingi huwa hawana
utunzaji wa chakula kwa muda mrefu. Na hii ni kwa kuwa huwa hawalimi. Hivyo
basi, jamii hizi huwa hawana chakula cha ziada cha kuwalisha wataalamu wengine
tofauti na wao wenyewe wakusanyaji au wawindaji. Kwake muwindaji hata aone
swala mia, bado atamuua mmoja au wawili tu. Hata waua wote na kisha awatunze!
Sasa basi, hii hudhoofisha kuzaliwa kwa taaluma zingine ukiachana na taaluma
kuu.
VIPINDI VYA UKUAJI WA JAMII ZOTE DUNIANI
Jamii za binadamu zilianza kupitia
vipindi mbalimbali vya ukuaji vikiongozwa na falsafa hizi kuu mbili. Falsafa
hizi zilikuwa zikipingana katika kila zama za dunia, hebu tuangalie vizuri.
Toka Uumbaji Mpaka Babeli.
Zama hizi zilianza tokea familia ya
Adamu, mpaka Mnara wa Babeli. Katika kipindi hiki chote kulikuwa na falsafa
hizi kuu, yaani, upande wa kaini ambao ulijikita katika kujenga jumuiya
mbalimbali kubwa. Ambazo zilihusisha maendeleo makubwa sana ya jamii kadha wa
kadha. Historia ya kaini inaonyesha kuhusisha kushamiri kwa sanaa kama za
miziki, usanii, kilimo. Pia familia za kaini zinaonyesha kuhusisha sana ndoa za
mitala, ambazo zinaonyesha kiwango kikubwa sana cha uzalianaji katika hizi
jamii.
Jamii za kaini pia zilihusisha ufugaji
sana. Hii ni kwa kuwa mifugo walikuwa wakichangamana na kilimo moja kwa moja.
Mifugo ilisaidia katika kutoa mbolea za kulimia, lakini pia nguvu kazi. Mifugo
ilikuwa sehemu ya mgawanyo wa taaluma mbalimbali katika jumuiya.
Biblia inaonyesha kuwa jamii za kaini,
ndizo zilizoanzisha msingi mkubwa sana wa kukua kwa miji. Miji na watu wengi
sana walishamiri katika upande huu, na falsafa hizi.
Je Wajua
Jamii hizi ndizo walizoanzisha teknolojia
za ‘’Breeding’’. Yaani, kuchanganya viumbe Fulani, ili kupata viumbe wenye sifa
za utofauti. Kulenga kupata viumbe bora zaidi. Hizi teknolojia zilihusisha
kuchanganya mimea kadha wa kadha ili kupata mimea ambayo, itakuwa na mazao bora
zaidi. Pia kuchanganya Wanyama mbalimbali kwa kuwazalisha, ili kupata Wanyama
watakao kuwa bora zaidi.
Kuzaliwa Kwa Demokrasia
Jamii hizi zilikuwa na watu wengi sana.
Na hivyo, kuepuka changamoto za migogoro ya watu kutokana na kupishana
kifalsafa. Iliwapasa kutengeneza mfumo wa kuvumiliana, wa demokrasia ya wengi,
kwa kila tofauti walizo nazo. Na hivyo basi, jamii hizi zilihusisha kundi kubwa
sana la watu ambao walikuwa waasi sana kutokana na demokrasia. Hii ni kwa kuwa,
walikuwa huru.
Jamii hizi zilihusisha kuibuka kwa maovu
makubwa ya mvunjiko wa maadili. Hii ni kwa kuwa, binadamu kwa asili wanapokuwa
wakijiona kuwa wamejitosheleza, huwa na asilimia kubwa sana ya kuelekea katika
uovu. Wanawake wa jamii hizi walikuwa na mitindo ya ukahaba hata kuvutia
wanaume toka jamii zingine za sethi, ambapo walikuwemo vijana wengi wacha
Mungu, na hii ilipelekea kuzaliwa kwa wanefili ‘’majitu’’.
Japokuwa huwa kuna midahalo kadhaa juu ya
wanefili ni nani? Lakini hiyo ni hoja rahisi sana. Wanefili walikuwa ni Watoto
matokeo ya watu toka familia ya seti waliokuwa ni wachaji sana, na kuitwa
‘’Wana wa Mungu’’, dhidi ya ‘’Wana wa Binadamu’’ au ‘’familia za uovu, ambazo
zilitapakaa sana katika falme hizi za kaini’’. Ndoa hizi zilipelekea Watoto
ambao walikuwa na Uwezo mkubwa sana, hii ni kwa kuwa, ‘’wana wa Mungu’’ huwa na
uwezo mkubwa sana, rejelea watu kama Suleimani, Danieli, Yusufu, Daudi,
Samsoni, Ayubu, Paulo, n.k. mara nyingi watu hawa waliobarikiwa wanapoelekea
katika uovu, huwa wanapelekea Uovu mkubwa sana kuliko hata kawaida. Na matokeo
yao ni kuwa, hata familia tu za seti nazo wote waliangamizwa katika gharika
hata akabaki Nuhu peke yake na familia yake.
Jamii nyingi za seti walikuwa ni kinyume
na jamii za kaini. Jamii hizi hazikuwa za kuchangamana sana kama zilivyokuwa za
kaini. Jamii hizi hazikuwa na mfumo mkubwa sana wa kilimo, na sanaa kama jamii
za kaini. Jamii hizi zilihusisha sana kiwango cha kawaida tu cha ufugaji,
kilimo, na uwindaji, na hata ukusanyaji.
Jamii hizi hazikuhusisha mikusanyiko ya
mithili ya falme katika maeneo kadhaa. Hawakuwa na familia za mitala. Hawakuwa
na mifumo ya demokrasia, wao walitii moja kwa moja sheria za Mungu. Jamii hizi
walijitenga mbali na miji mikubwa ya uovu wa jamii za kaini, kabla ya kuja
kuangamia kwa kuruhusu kuchangamana tena Pamoja kupitia wanefili.
Falsafa Iliyofichika
Wengi hawajui kuwa Mungu hupingana na
falsafa zote za kujikusanya wengi katika eneo moja, kujilimbikizia mali kwa
uhakika wa Maisha ya nyakati zote, na kujipa uhuru kwa kila tendo. Falsafa hizi
ni kinyume na ndiyo maana, Biblia huamasisha kutojilimbikizia mali. Mfano, husema katika Mathayo 6:34 ‘’ Basi
msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe’’ au hutoa kisa cha
Tajiri mpumbavu aliyekuwa mkulima, na kisha baada ya kulima na kuvuna sana,
akajisemea sasa ntakaa na kufurahia Maisha yangu yote! Na Mungu akamwita ‘’leo
wewe mpumbavu naihitaji roho yako’’.
Mfumo
wa viumbe wote duniani unahitaji Imani kwa Mungu juu ya kesho. Yaani, hakuna
kiumbe asiyefanya kazi, lakini hakuna kiumbe anayejitaabisha ili ajaze ghala
yake. (umewahi ona ghala ya vyakula mbuga za Wanyama? ) Hii ni kumaanisha
viumbe wote, mara zote, hukabidhi hatma yao ya kesho kwa Mungu. Falsafa hizi za
wana wa sethi za kutojiegemeza sana katika kilimo, au shughuli zingine
zinazolenga uzalishaji wa kuzidi, ziliwafanya kuwa waaminifu sana kwa Mungu
wao. Na kamwe hawakuwa na siku ya kutulia maana, iliwapasa kufanya kazi ili
wale.
Kumbuka; Haimaanishi binadamu hapaswi kuweka akiba! La
hasha, hata Biblia inasisitiza busara za wadudu ‘’Chungu’’ katika kujiwekea
akiba (Mithali 6:8), na mithali 6
ilikuwa ikionya tabia za Uvivu, kutofanya kazi. Na hata pia haimaanishi
‘’Wakusanyaji na wawindaji, hawakuwa wakiweka akiba kabisa’’. Ila tatizo huanzia katika Falsafa zinazolengwa
na Kuibuka katika uwekaji huu wa akiba.
Kwanini
Falsafa Ya Kaini Hushinda?
Hawa marazote hushinda kwa kuwa,
hujikusanya na kuwa na jamii kubwa sana ya watu wenye ujasiri wa kufanya sana
maovu, kama vile vita, n.k. hawa hushinda pia kwasababu huaribu sana mazingira,
kiasi cha kupelekea kupungua kwa Wanyama wa kuwinda, mimea ya vyakula vya asili
ya kuokoteza, na malisho ya mifugo. Je wajua ulimaji wa kilimo chochote kile,
kwa kurudia rudia zao moja hilohilo, kwa kiwango kikubwa huua kabisa ardhi? Na
ndiyo mwanzo wa uhitaji wa mbolea.
Sababu hizi hupelekea jamii za falsafa ya
wana wa sethi kujikuta tu aidha, wakizidi kujitawanya zaidi mbali nao, au,
wakijikuta tu nao inawapasa kuiga mifumo ya watu hawa. Mbeleni tutaliangalia
hili katika mtazamo wa tofauti kabisa.
KUELEKEA MWISHO WA ZAMA ZA AWALI
Falsafa ya kaini ilishamiri sana, hata
kuibadilisha kabisa falsafa ya sethi. Jamii yote ya wanadamu katika zama hizi
walijikuta wakiingia katika uovu mkubwa sana, mpaka kumfanya Mungu kuamua
kuangamiza kabisa kizazi chote.
Nuhu kutoka falsafa ya seti, anapatiwa
neema, na kisha anaanza kuwahubiria watu kuacha uovu. Lakini watu hawawezi
kumsikiliza kwa kuwa wameshaathiriwa na uovu, na Mungu anaangamiza kizazi chote
hiki cha wakulima Hodari, na wasanii maarufu zaidi, na wajenzi wakubwa zaidi wa
awali, na unakuwa ni mwanzo wa mwisho wa zama za kwanza.
Kuna Ushahidi wa kutosha wa kisayansi wa
gharika hii ya Nuhu. Unaweza rejea kusoma Q3 kuona namna ambavyo, mabaki
mbalimbali ‘’fossils’’ yanadhihirisha gharika hii. lakini pia masomo mbalimbali
ya miamba ‘’geology’’, yanadhihirisha gharika hii. lakini pia elimu za
ulimwengu, nyota, sayari na mwezi, nazo zinadhihirisha sana gharika hii ya
nuhu. Hakuna ukinzani juu ya upana wa sayansi inayothibitisha ukweli huu.
Mnara Wa Babeli Na Mwisho Wa Zama Za
Kwanza
Baada ya kutoka kwenye gharika. Binadamu
wanaanza kuishi katika dunia iliyojaa mimea, na Wanyama, tena yenye Rutuba ya
kutosha. Lakini idadi yao bado inakuwa ni ndogo sana kuweza kuijaza dunia.
Dunia sasa imebadilika, dunia ina mabara sio tena eneo moja kama ilivyokuwa
mwanzoni. Na kwa mantiki hii sasa binadamu wanaweza kutengana hata kujikuta
wapo katika maeneo tofauti kabisa.
Kujengwa kwa Mnara wa Babeli ambako
kulilenga kuwakusanya tena watu katika eneo moja, kulifanyika katika maeneo ya
Mesopotamia, miji ya kuzunguka Iraq ya leo. Chini tutaangalia maeneo haya
kiundani zaidi ili tuweze kuyaelewa kiundani, lakini hata hivyo, bado
kunakubaliana na falsafa ileile ya kaini. ya kilimo, na uwepo wa watu wa sanaa
za ujenzi ‘’craftsmen’’, na wafalme.
Mungu anatenganisha yeye mwenyewe ufalme
huu wa falsafa ya awali ya kaini. Na matokeo yake, mabadiliko yafuatayo
yanatokea, lakini huu ndiyo mwisho wa zama za kwanza za awali.
TOKA BABELI MPAKA MIAKA YA 2000
Baada ya kutawanyika toka mnara wa
Babeli, kulikuwa na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wakielekea katika
kanda tofauti tofauti za dunia. Kulikuwa na makundi makubwa makuu matatu,
yaliyotokana na Watoto wa Nuhu, yaani, Hamu, Yafeti, na Shemu. Watoto hawa
walianza kuelekea maeneo mbalimbali kulingana na kanda zao, ambazo wanaonekana
kuelekea kutokana na mtazamo wa historia.
hoja kuu ni zifuatazo.
Rejea picha zifuatazo katika ramani ya
Dunia.
Bonde zima la Ulaya na Asia, na kaskazini
mwa Afrika, lilishamiri sana kwa kilimo. Hii ilitokana na sababu tutakazoziona.
Tambua pia kuwa, ukanda huu wa Asia, Ulaya na Kaskazini mwa Afrika, sifa zake
pia zinapatikana katika maeneo kadhaa duniani, japokuwa ni kidogo ukilinganisha
na eneo hili. Mfano ni maeneo ya bonde
hilo la California, Chile, Cape town South Africa, n.k. lakini hata hivyo,
ukanda wa Ulaya-Asia + Afrika ya kaskazini ndiyo ulikuwa bora zaidi, na hii ni
kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa zaidi cha sifa za kusapoti kilimo.
Kulikuwa na Bonde Moja kubwa sana ambalo
kwa Kiingereza huwa likiitwa ‘’Fertile Crescent’’, au ‘’Bonde la Rutuba’’
ambalo, linapatikana maeneo ya Mesopotamia. Msomaji ni vema kutambua kuwa falme
zote kubwa zilizowahi kutawala dunia, ziliegemea zaidi katika bonde hili.
Kuanzia Babeli, Wamedi na Uajemi ‘’Medo-Persians’’, Wagiriki, na hata Warumi.
Bonde hili huwa napenda kuliita ‘’Mjini
Duniani’’. Huku ndiko idadi kubwa sana ya watu ilikuwepo, lakini hebu tuvute
taswira hatuelewi chochote, na tuanze kutazama tena kuanzia awali kabisa katika
maendeleo ya binadamu baada tu ya mgawanyiko toka mnara wa babeli.
TOKA MNARA WA BABELI
Idadi kubwa sana ya watu ikaanza kushuka toka maeneo ya Babeli,
ambayo nayo yalikuwa mazingira ya miji hii hii ya Persia. Na sasa basi, wapo
walioshuka kuelekea chini kabisa mwa Bara la Afrika, wapo walioishia kaskazini,
wapo walioelekea mashariki kabisa ya Asia, kama China, wapo walioelekea magharibi
kabisa mwa Ulaya, na hawa ndiyo walioendeleza safari hata kuifikia marekani,
hii ni kutokana na uwepo wa kina kidogo cha maji zama za barafu ‘’ice ages’’,
unaweza kurejea Q3 kulielewa zaidi hili.
Kwanini
Kilimo Kilishamiri Ulaya-Asia + Afrika Kaskazini, Na Hasa Bonde La Rutuba?
Tazama
ukanda huu ulioshamiri sana kwa kilimo, na picha hii ambayo nimeitoa katika
kitabu cha ‘’germs, steel and guns’’, inaonyesha rangi nyeusi ambayo ndiyo
bonde hili la rutuba.
sababu
za kushamiri kilimo katika ukanda huu
Ukanda
huu una tabia ya nchi ya ‘’Mediterranean’’. Sifa za kanda hizi ni kuwa, huwa na
mvua chache sana, na huwa na vipindi virefu sana vya jua. Hii hupelekea kukauka
kwa mimea mingi sana kutokana na kiwango kidogo cha maji. Mimea ambayo huweza
kustawi katika ukanda huu, huitaji kuwa na uwezo mkubwa sana wa kustahimili
ukame. Ambapo, huitaji kuwa na mizizi mikubwa sana, au mipana sana. Na huitaji
kuwa na matunda makubwa sana. Hii mizizi kama ya miogo, au viazi Maana yake ni
kuwa, huifadhi kiwango kikubwa sana cha maji na virutubisho, kwa ajili ya
kujipatia chakula chake kwa wakati wa ukame.
Hii
tayari ni faida kwa mkulima. Kwa watu walio katika maeneo haya, walichoweza
kukifanya ilikuwa tu ni kukusanya kiwango kikubwa cha mimea ya namna hii. na
kuipanda katika eneo moja ikiwa peke yake, ikizaliana sana. Na kwa hivyo,
wakaweza kuzalisha kiwango kikubwa sana cha mazao.
Maeneo
mengi ya marekani, na Afrika. Yalikuwa katika kanda tofauti tofauti, hasa kanda
za ‘’Tropical, na Equatorial’’. Huku kulikuwa na kiwango kikubwa sana cha mvua.
Hizi zilisababisha kuwepo na kiwango kidogo sana cha mimea yenye namna hii ya
kutunza mizizi. Maana mimea haikuhitaji kutunza sana chakula, maana mvua
zilikuwa za uhakika. Mfano, tazama jedwali chini linaloonyesha sehemu, na idadi
hii ya mizizi mikubwa.
Unaweza
ona namna ambavyo bonde letu lote la nchi zetu za chini ya jangwa la Sahara,
Jiografia haihusishi uwepo wa aina hata moja ya mimea yenye aina hizi za
mizizi. Na unaweza ona namna ule ukanda wa bonde la rutuba ulivyo na mimea
mingi ya namna hizi za mizizi. Na hiyo tayari ilikuwa ni sababu kubwa sana ya
kuendelea sana kwa kilimo katika ukanda ule.
Mimea
ya mizizi hii mikubwa katika mabonde haya ya rutuba, pia ilikuwa na sifa moja
kubwa, ilikuwa na uwezo wa kujichavusha yenyewe ‘’self -pollination’’. Hii
iliiwezesha kuzaliana sana hata bila kutegemea kuwepo kwake mingi katika eneo
moja. Hii tayari ilikuwa sifa kubwa sana kwa wakulima. Wakulima sasa waliweza
kuizalisha hii mimea, na hata kwa kuichanganya ‘’breeding’’, ili kuweza
kuzalisha aina mbalimbali za mimea bora kabisa.
Pili,
ukanda huu wa ‘’Ulaya-Asia-Afrika kaskazini. Upo katika mstari mmoja tambarare,
‘’horizontal axis’’. Yaani, ukanda wote huu unapitia mara nyingi zaidi, tabia
za nchi, na majira yanayofanana. Hii inasaidia sana kusambaa sana kwa taaluma
za kilimo, mbegu, uhitaji, na maarifa yoyote yale katika ukanda huu wote,
kuhusiana na kilimo. kwa namna yanafanana . Hebu tazama picha chini.
Hii
picha inaweza kukuonesha namna ambavyo hata aina moja ya mbegu, au taaluma, au
hata wafanyakazi wangeweza kutoka sehemu moja, na kuelekea sehemu nyingine
katika ukanda mmoja.
Wanyama
wa kufuga ni miongoni mwa sababu kubwa sana iliyochochea kushamiri kwa kilimo
katika mabonde haya. Afrika inatambulika kwa kuwa na Wanyama wengi sana
wakubwa, kama tembo, n.k. lakini Afrika haikuwa na Wanyama wapole wa kufugika.
Afrika ilishamiri sana Wanyama mwitu, wakali, ambao ni vigumu sana kufugika.
Lakini hata kwa aina zingine za Wanyama kama Swala, Pundamilia, uwoga wao
kupindukia haufai kwa kufugika. Mnyama wa kufugika anahitaji kuwa na upole wa
kiasi, na asiwe na ukali wa kuhatarisha kama Wanyama mwitu wengi waliomo Afrika.
Tazama
jedwali chini na kisha utaona namna ambavyo Wanyama wapole wakufugika wala
majani wote wakubwa, kwa asili hawakuwa wenyeji wa Afrika bonde la chini ya
sahara. Walikuwa wenyeji wa bonde la ‘’Ulaya-Asia, na Afrika kaskazini’’. Sasa
hivi tunatambua Wanyama wa kufugika kwa wastani wana Ubongo kidogo mdogo kuliko
jamii zao waliomwitu.
Wanyama
hawa wakufugwa waliendelea kuzalishwa kwa kuchanganywa wao kwa wao, na kuzidi
kutengeneza jamii za Wanyama ambao ndiyo wakawa wapole, na bora zaidi kwa
kufugwa.
Kilimo
Na Kukua Kwa Kasi Kwa Ulaya-Asia Na Afrika Kaskazini
Kama
tulivyoona awali kilimo kilipelekea ulaya na Asia, na kaskazini mwa Afrika,
kuanza kukua kwa kasi kubwa sana ukilinganisha na maeneo mengine yote ya Dunia.
Hii ilitokana na kuwa, kilipatikana chakula cha kutosha kwa wakulima, na
wanataaluma wengine wote. Ikiwemo, wanasanaa ‘’craftsmen’’, wasanii,
wanafalsafa, wanasiasa, wanateknolojia, n.k.
Biblia
hurejelea stori ya Yusufu aliyechochea ulimaji mkubwa Misri kwa miaka saba, na
kisha Utunzaji mkubwa wa chakula kwa miaka saba, na uundwaji wa dola kubwa
zaidi ya Misri. Hii ni kama ambavyo historia inavyothibitisha maendeleo ya
awali kabisa makubwa zaidi ya Misri, kutokana na Kilimo, kilichochochea sana
hata sanaa za Ujenzi wa Pyramides, na maandishi.
Kukua
kwa jamii tena kwa mara nyingine katika ukanda wa mediterranean. Ukianzia na
miji ya Mesopotamia, ambapo falme kubwa nyingi au zote ziliegemea sana. jamii
kubwa kabisa za kwanza zilianza kukua katika maeneo haya. Watu walizaliana sana
kutokana na uwingi wa vyakula, watu walikaribiana sana na hata kupelekea
migogoro iliyopelekea maendeleo makubwa ya mifumo ya uongozi, au falme za awali
kabisa.
Kuzaliwa
Kwa Maandishi
Maandishi
mengi yanaonekana kuanza katika miji ya Misri, na miji ya Sumaritan, ukanda huo
huo tunaouzungumzia. Wanasayansi wengi hutafakari nini hasa kilikuwa chanzo cha
kuanza kwa uandishi. Ila inafahamika mpaka leo kuwa, uwepo wa Wanyama wengi,
mazao mengi, watu wengi, kulipelekea binadamu kuhangaika sana kuweka kumbukumbu
ya idadi yao. Kuna wakati waliweka aina mbalimbali za vitu kuwakilisha idadi
Fulani ya vitu, baadae wakaanza kutumia alama, na baadae wakaanza kutumia alama
mbalimbali kwa sauti maalumu za kutamkwa.
Uwepo wa watu ambao wangekuwa wakihangaika na kutatua maswala haya, kwa kuwa na muda mwingi nje na shughuli za kuwinda zinazokutaka kuwa kazini kila wakati. Basi kuliwawezesha kuweza kufanikiwa kuchochea maandishi yaliyowasilisha ala mbalimbali za sauti, au alama mbalimbali za vitu. Zipo namna mbalimbali za uandishi wa lugha, lakini nyingi zinafanana kiasili. Mchangamano mkubwa wa watu ulichochea kusambaa kwa haraka sana kwa taarifa hizi au maandishi kutoka eneo moja kuelekea eneo lingine.
Kukua
Kwa Teknolojia
Watu
wengi sana hata mimi kwa wakati kadhaa nyuma, tulikuwa na mtazamo mmoja tu kuwa
‘’Uhitaji huchochea Ubunifu’’. Ni kweli, lakini sio mara zote. Mara nyingi,
‘’Ubunifu huchochea Uhitaji’’. Hakuna aliyekuwa na stress za kutamani kupaa,
kabla Ndege haijagunduliwa. Vitu vingi ambavyo huwa tukivifanya, hatukujua
awali kama tungepaswa kuvifanya, lakini kadri unavyokuwa na kubadilika, ndivyo
unavyochochea uhitaji mpya.
Inafurahisha
hata vitu maarufu kabisa kama Umeme vilipogunduliwa awali kabisa, bado watu
wengi sana walivipinga. Injini ya Carl Benz ya gari la kwanza kabisa, hakuna
aliyekuwa na muda nayo. Watu hawakuwa na muda na magari. Waliamini zaidi
farasi. Lakini muda ulivyosonga, kila mtu hakuamini alipojikuta akihitaji gari.
Nadharia nyingi sana za sayansi, mfano ‘’Lamarckism ambayo haina miaka mingi
toka ikubalike, hata Relativity ya Poincare, Lorentz na Einstein’’ zimewahi
kutupwa lakini baadae wakazipa tuzo. muda mwingine hata waliozifanyia kazi huwa
wamekwisha kufa. Nakumbuka simu za ‘’Smartphones’’ zilipoingia nchini Tanzania
kwa mara ya kwanza kabisa, bado wengi walizikimbia wakiamini ni mbaya sana,
mara zinanyonya damu! Lakini leo hii kila mtu anaziamini na kuzihitaji.
Hii
ina maana gani? Wagunduzi wengi wa teknolojia walikuwa ni watu waliokuwa huru
kufanya mambo yao, bila dhiki yoyote ile. Walikuwa katika jamii hizi za
‘’mediterranean’’. ambapo, chakula kilikuwa cha kutosha. Unaweza kumbuka hata
maendeleo ya wagiriki, kukua kwa falsafa au sayansi katika miji ya Athens.
Ambapo kulikuwa na chakula kingi, hasa kutokana na ushindi wa majeshi ya
Ugiriki ‘’spartans’’ ambao waliteka malighafi na vyakula kila waliposhinda
vita, na kuzijazia nchi zao vyakula. Hivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa na kukua kwa
elimu zama za Dola ya Uislamu, Kukua kwa Ujenzi ‘’Engineering’’ katika zama za
dola ya Rumi, hata China mpaka mwaka 1400 ilikuwa inaongoza kwa teknolojia
kwasababu ya Kilimo.
Ukoloni
japo tutauangalia kiufupi lakini nao unadhihirisha ni kwa namna gani, kushamiri
kwa malighafi kwa nchi za ulaya, kulichochea sana maendeleo ya teknolojia.
Ijapokuwa, teknolojia yenyewe haihitaji ukoloni. Na hata ukoloni kiuhalisia una
mchango mdogo sana katika kukandamiza eneo moja, au kuliinua sana eneo jingine.
Kwa mantiki ya dola moja kuitawala dola nyingine, karibia kila nchi imewahi
kutawaliwa na dola nyingine.
Maendeleo
ya teknolojia, sayansi, falsafa, na maarifa kwa ujumla. Hayajawahi kutokana na
jitihada za mtu mmoja, au upekee wa mtu mmoja. Hata kauli hii, haijawahi semwa
na mtu mmoja. Prof. Jared ameisema, lakini hata mimi katika Q2 niliisema. Mara
zote huwa teknolojia ni ngazi kutoka kwa waliotangulia, na sio aliyetangulia.
Hakuna zama katika dunia hii ambapo kilianza kitu kipya, ila kuna zama ambapo
kitu fulani kilishamiri zaidi.
Hata
kwangu neno, ‘’wakati wa mwisho, Maarifa yataongezeka’’, huwa naelewa kama
‘’Maarifa yatasambaa zaidi, yatakusanywa yote, yataboreshwa zaidi, na
yatafanyiwa kazi zaidi’’. Na sio kuwa kuna jambo jipya. Mara nyingi tumekuwa
tukivifikiria vitu na kutovifanyia kazi, na ghafla huwa tukiona vikifanyiwa
kazi na wengine, wenda kutokana na nafasi zao, au urahisi zaidi kutokana na
misaada na kuchangamana na wataalamu mbalimbali katika jumuiya zao, wagunduzi
wajinga huisi walianzisha wao. Je wajua, Newton hakuwai iona Rocket, lakini
alijua ukienda na spidi ya 11.2km/s, utaivuka kani ya mvuto wa gravity, na
miaka mia tatu mbele yake, ikawazekana! Da vinci, hakuwai iona ndege wala
parachuti, lakini alijua na kuchora, mfano wa kielelezo cha Parachuti ambalo
lilipoboreshwa, liliwezesha kupaa! Tena miaka mia nne mbele yake!
Kwa
Hiyo Wa-Afrika, Marekani & Australia Walikuwa Na Bahati Mbaya!
Tukirejea
katika falsafa yetu ya awali kabisa. Waafrika wengi sana walishuka katika Bonde
la Sahara na kuendelea na safari kuelekea kusini mwa Afrika, na maeneo mengine
mengi ya kati. Watu wote toka mnara wa babeli walikuwa wakishuka kama vikundi
vidogo vidogo vya watu. Watu hawa waliendelea na falsafa ileile ya zamani ya
‘’Kuwinda, na Kukusanya’’. Wengi wa watu hawa walikuwa wakiishi katika mabonde
ambayo yalikuwa na Wanyama wengi, na mimea mingi sana ya asili, ya vyakula.
Kwa
kuwa Afrika haikusapoti sana Kilimo, jamii nyingi sana za wakazi, mfano kwa
Afrika, jamii kama ‘’Bantu, Khoisan’’, Pygmies, na wengine. Walikuwa ni
wawindaji sana wa Wanyama, na wakusanyaji. Hawakuwa na makazi ya kudumu,
walikuwa wanahamahama, hawakuwa wakiunda jamii kubwa za jamii za watu. Na hii
ilikuwa hivyo hivyo na kwa wakazi wa marekani, kama ‘’Maya’’ au ‘’Indians’’, pia
ilikuwa hivyo hivyo kwa jamii za Australia.
Nikisema
wakusanyaji namaanisha watu waliotimamu kama tu wale waliopo ‘’ulaya-Asia na
Afrika Kaskazini’’, na tena mara nyingi walikuwa hata wakifanya biashara
Pamoja. Ng’ombe wengi sana wa wabantu walinunuliwa toka ukanda wa Afrika
magharibi na kaskazini. Maana hata hivyo, wabantu wengi sana tunaamini walikuwa
ni wenyeji toka Maeneo ya Nigeria, na Cameroon. Wanyama kama Ng’ombe hawakuwepo
kwa asili ukanda huu wa Afrika. Na hata baadhi ya makabila walishuka na mazao
kadhaa, maana Afrika ilikuwa kwa asili na mazao ya aina mbalimbali za Mtama zaidi, na Magimbi. Mazao kama Ndizi
yalitoka Asia, Mahindi marekani, Ngano ilitoka zaidi Ulaya.
katika
vyakula vyote vilivyoshuka hakuna hata kimoja kinachofikia jamii za mtama kwa
virutubisho. Mfano tu kiwango cha madini ya Calcium kwenye mtama gramu 100,
unapata milligram 350. Hii ni zaidi ya vyakula vyote vilivyoshuka. Na jamii
hizi za mtama mfano, uwele, ulezi, mtama wa kawaida ‘’kodo-millet’’ huondoa
kabisa mafuta mabaya mwilini ‘’triglycerides’’. Pia kwenye Maganda yake kuna
‘’peroxidase’’ ambazo huzuia seli za saratani zisisambae. Kiufupi mtama ni mara
nyingi sana bora zaidi ya mahindi, na ngano, na mchele. Afrika magharibi pia
ilikuwa na aina ya mchele ambao ulishuka, ukiachana na uliotoka China.
Waafrika
walikuwa watu wenye afya sana. Walikuwa ni watu ambao wakati mwingi zaidi walikuwa
katika miondoko, aidha uwindaji, au ukusanyaji wa vyakula. Walikuwa ni watu
wenye misuli yenye nguvu sana, lakini changamoto yao kubwa ilitokana na mitindo
ya Maisha yao kama ifuatayo.
Kutokuwa
na Mifumo ya kilimo. Kutokana na uwingi wa aina za Vyakula, mifumo ya uwindaji
ambayo mara nyingi zaidi watu huwa hawana makazi ya kudumu sana. Haya Yaliwapelekea kuibuka kwa vikundi mbalimbali,
au makabila. Ambayo, walikuwa wakishindana mara kwa mara katika vita za wao kwa
wao. Hii ni kutokana na kushindania maeneo, au Sifa za jamii ipi ni bora sana,
hii mara nyingi hushamiri kwa jamii ambazo hutumia sana misuli.
Migogoro
ilishamiri zaidi kwa kuwa, hakukuwa na kilimo ambacho kingewafanya watu hawa
watengeneza jumuiya kubwa ambazo zingewahitaji kuwa na Uongozi wa kutawala
maadili ya jumuiya nzima. Vita za makabila zilishamiri sana. Hakukuwa na
wataalamu wa fani mbali na fani za uwindaji na ukusanyaji. Teknolojia kwa
maeneo mengi sana ilikuwa ndogo.
Maadili Afrika
Jamii za Afrika hazikuwa na watu wengi
sana, kama zilivyokuwa jamii katika kanda za mediterranean. Huku wanaume
walikuwa ndiyo watafutaji wa chakula kila siku kunapokucha, na wanawake
walikuwa ni walezi na wazazi wa nyumbani. Wanaume Afrika walikuwa ni walinzi na
wapambanaji wa vita. Mwanaume alipaswa kuwa na maadili ya ukakamavu wa kiume
kila wakati. Afrika ilishamiri Falsafa ya Mwanaume anayezoelea tabia za mapenzi
huwa ni mdhaifu, na si mpambanaji mzuri vitani.
Pia Afrika iliaminika mwanamke
anayemchochea sana mwanaume kwenye mapenzi anamfanya mwanaume huyo kuwa
mdhaifu. Sio kana kama hii falsafa ilikuwa ya pekee sana Afrika, hata maeneo
mbalimbali kama miji ya Ugiriki falsafa hii ilisambaa, na Uarabuni. Jambo hili
lilichochea sana uwepo wa gepu kubwa sana kati ya wanaume na wanawake.
Ijapokuwa Afrika ilishamiri sana kwa mila
potofu sana kwa baadhi ya zama katika historia. Kama vile ukeketaji wa
wanawake, ndoa za mitala, Imani za ushirikina, ibada za miungu n.k. mara nyingi
huwa ni hoja zisizo na nguvu maana tabia za zama za ujinga penginepo kitovu
chake kilikuwa ‘’Mediterannean’’ yaani ‘’Ulaya-Asia’’ ambako hata Ushoga
ulizaliwa.
Tatizo pekee lililoiathiri Afrika ni
mfumo wa Uongozi wa makabila mengi, ambao kitaalamu huitwa ‘’Kleptocracy’’ hili
ni janga la Afrika. Hii ina maanisha, Afrika imekuwa sana na Viongozi
wanaopenda Kujilimbikizia Mali za umma, kwa tamaa zao. Hii ilikuwa ni hali
ambayo Afrika haikuanza nayo jamii nyingi ziliposhuka toka mnara wa babeli.
Waafrika zamani walikuwa wanapenda sana usawa, kitaalamu waliitwa
‘’Egalitarians’’. Lakini hebu vuta picha
Raisi kama ‘’Mobutu’’ wa Congo!!! Mtu anaweka Mabilioni ya mapesa ya
nchi kwa akaunti yake tu, na nchi yake anashindwa hata kuisambaza japo tu mfumo
wa Simu.
Hili janga la mifumo mibovu kabisa ya
Uongozi ilianzia pale ambapo Viongozi wengi wa makabila tokea awali hawakuwa
wakichaguliwa kwa sababu za sifa za uongozi, bali aidha za uwindaji, au Nguvu
za vitani. Viongozi hawa hawakuwa na tume za ushauri, maana mifumo ya uwindaji
haina nafasi sana juu ya taaluma zingine. Tabia hizi ziliwajengea viongozi hawa
tamaa ya kupenda kujilimbikizia sana jambo ambalo liliendelea kurithishwa hata
kwa jamii za baadae. Karibia Afrika yote tatizo hili limesambaa, Nchini Tanzania
tuliwahi pata bahati ya kupata Raisi mzuri sana ‘’John Pombe Magufuli’’ ambaye
alipigana sana dhidi ya mifumo hii ya ‘’Kleptocracy’’ iliyosambaa nchini,
lakini hata yeye hakufanikiwa, maana hii mifumo inasababu za kisaikolojia
ambazo kitabu hiki kinazichambua kwa kiwango kikubwa sana.
Kukua Kwa Biashara, Usafirishaji Na
Afrika
Kuanzia miaka ya 1400, Dunia ilikuwa
imeshamiri sana kwa maendeleo ya teknolojia za usafiri na biashara. Hii
ilitokana na maendeleo ya kasi sana ambayo yalikuwa yamekwisha tokea katika
kanda nyingi sana za Ulaya-Asia, na Afrika ya Kaskazini. Jamii hizi zilikuwa na
migogoro mingi sana ya vita, na kutawaliana. Kumbuka kanda hizi hazikuwa na
vita za kila siku kama vita za makabila ya Afrika. Jamii hizi zilikuwa
zikipigana na kisha Ufalme mmoja unatawala, na kadri unavyoishiwa nguvu,
unaibuka mwingine kwa vita kali hata kuupindua. Vita zilihusisha umwagaji
mkubwa zaidi wa damu, lakini ulihusisha kushabiiana sana kwa maarifa kila jamii
zinapokuwa Pamoja. Na maarifa haya ndiyo yalikuwa msingi wa hitaji la malighafi
zaidi, na ugunduzi zaidi.
Miaka ya 1400 na kuendelea kulikuwa na
safari nyingi sana za majini kwa wafanyabiashara wengi sana kama, Christopher
Columbus, Vasco Da Gama, Bartholomeu Dias, Vasco Nunez de Balboax, Nyuma kidogo
walikwepo kina Marco Polo, wengi wao hapa walitoka Spain, Portugal, na pia
kulikwepo wafanyabiashara toka China, India, Uarabuni, n.k. wengi walizunguka
dunia nzima hata na Afrika. Na kupitia hawa Afrika ilifahamika sana, Utajiri
wake, Uhitaji wake, Udhaifu wake, na huu ndiyo ulikuwa mlango wa Afrika
Kibiashara, kukua kijamii, na hata Ukoloni.
Kwanini Ulaya-Asia Na Afrika Kaskazini
Zilikuwa Na Nguvu Na Teknolojia Zaidi Ya Afrika, Australia Na Marekani, Na Sio
Kinyume?
Ni kweli tumeshaona kuwa ukanda wao
ulikuwa wa mstari wa ulalo uliochukua eneo kubwa na kuwezesha zaidi kujamiiana
kimaarifa, kivita, kilimo, n.k. kuliko Afrika iliyo kwa wima, na bado ina
majangwa kama Sahara ambayo kuvuka ni shughuli, bado Afrika kuna mito mizito
yenye maporomoko isiyosapoti safari za majini hata kuweza kuchochea maendeleo
ya meli, na mashua kubwa. Tumeshaona pia kuwa ukanda wa mediterranean tu ndiyo
uliokuwa na mimea yenye mizizi na matunda ya kusapoti sana kilimo kutokana na
hali za hewa za kiangazi, na mvua chache. Ila bado haya sio majibu, kwanini
isiwe kinyume?
Ndiyo, Tumeshaona kilimo kilivyosapoti
wanataaluma wa teknolojia zingine n.k. tena wengine husema hata na hali za
baridi huwafanya watu kuhitaji joto muda wote, hivyo huitaji ujenzi mara zote
wa kulitunza joto, ingawa huwa hawawezi kutetea kwanini maeneo mengi tu yenye
baridi zaidi, ndiyo hayana maendeleo kabisa. Ndiyo unaweza sema Afrika ilikuwa
na falsafa za uwindaji sana na ukusanyaji, hivyo walikuwa hatarini zaidi
kutoendelea kwa jamii kubwa, na ndiyo maana hata waliweza kutawaliwa kipindi
cha ukoloni. Lakini Bado Hujajibu swali. Kwanini isiwe kinyume?
Hili linaitwa swali Gumu la Kifalsafa la
kwanini? ili kuweza kujibu maswali kama haya, hauhitaji kufikiria kwa kiwango
cha kawaida tu cha Sayansi. Ambayo inakwambia tu sababu za imewezaje kutokea,
au ‘’How’’. Maswali kama haya wanasayansi ambao hujaribu kutumia sababu za
‘’Evolution theory’’ kuyajibu. huaribu kabisa maana. kwa kuwa, huwa wanapelekea
hata kuibuka kwa falsafa za ubaguzi na ukandamizaji, au ‘’Racial segregation’’’.
mfano kusema, mtu wa kwanza alifanania
aina za Sokwe, halafu alitokea Olduvai Gorge, Tanzania. Halafu akaanza kusambaa
na sehemu zingine za dunia, hata akafika Ulaya n.k. mitazamo hii ni kama
inakuonyesha kuwa mtu atakayebaki Afrika maana yake atakuwa bado ana
Usokwesokwe, na ndiyo maana utakuta ‘’Adolf Hitler’’ akikitumia kitabu cha
‘’Charles Darwin’’, yaani ‘’Origin of Species, and Descendants of Superior
man’’ kumaanisha Waafrika, wayahudi, na wengine kuwa bado wana asili za usokwe,
huku wao wakiwa watu wa kisasa zaidi ‘’Superior Race’’. Hii kitaalamu inaitwa
‘’ Eugenics’’. Kumbuka, vipo vitabu maarufu kama ‘’Anatomy of Restlessness’’
ambavyo vinaonyesha, kadri unavyotembea zaidi, ndivyo unavyoendelea zaidi, kwa
hiyo, kama mtu alitokea Afrika, basi aliyefika Ulaya-Asia, ametembea sana? Ameendelea
sana, na vipi kuhusu aliyebaki? Maana yake hajatembea sana, bado ana
usokwesokwe, hana akili sana!! ( hoja hizi ili uzipinge, inabidi ung’ang’anie
kuwa zimetafsiriwa vibaya, au msomaji hana akili za kutosha kuweza kuzielewa)
kumbuka pia, Afrika ndiyo ina aina
mbalimbali za jamii za watu ‘’high genetic diversity’’, ukitafsiri kinyume kama
wanavyofanya hawa watu, unaweza pata jawabu hasi kuwa watu walitoka Afrika na
kuelekea Kaskazini, na utafeli kama wanavyofeli hawa watu. Watu walitoka Babeli
kuja Afrika, na kwa kuwa Afrika ipo Wima, ina mazingira na majira tofauti
tofauti, basi Jenetikia ya kisasa zaidi ya ‘’Epigenetics’’ mfano,
‘’Lamarckism’’, inatuthibitishia kuwa, watu lazima watabadilishwa badilishwa
sana katika jenetikia. Na ndiyo uhalisia wa Afrika kuwa na ‘’diverse
genetics’’.
Unaweza danganya Watoto wadogo kuhusu
fuvu la mtu wa kwanza, na mabaki yake kwa kuunganisha vipisi vya mifupa isiyo
hata na uhusiano, kama wana nadharia hawa wanachofanya, lakini msomi mzuri
anatambua tabia hizi za wanasayansi wa sanaa za kufikirika, wanaochochea tu
kuua sayansi, na familia zao. (rejea Q3
unaweza elewa mbinu za upotoshaji mkuu wa wanasayansi hawa, hasa kwa vifaa vyao
vya kupima muda-Radiocarbon datings, K-Ar datings, na matabaka ya dunia
‘’geologic layers)
Wanasayansi husema kuwa nadharia hii wala
haimaanishi hivyo, ila tu ni makosa ya kuitafsiri. Hata wanasayansi wasioamini
huu ukandamizaji, ila wanaitumia hii nadharia. huwa wanahangaika sana mithili
ya watu ambao hawajawahi Kwenda shule, wanapojaribu kutaka kuitumia kujibu
maswali kama haya ya kifalsafa. Tatizo kubwa ni kuwa, nadharia hii imepinduliwa
juu chini, na chini juu. Mtu alifika Afrika kutoka Babeli, na siyo alitoka
Afrika Kwenda Babeli.
Siku zote anayechelewa kufika, huwa
anachelewa Kuanza.
Kuelewa msingi wa sababu, ambazo ndizo
zinakupa Jibu la swali la kwanini? haikuwa kinyume kwa Afrika kupiga hatua kabla
ya Ulaya-Asia. Rejea kwanza kielelezo kifuatacho, na kisha nitatoa maelekezo
yatakayojibu swali hili kiundani zaidi. Zaidi ya hapa hakuna jibu lingine
lolote ambalo linaweza maliza utata wa swali hili la kifalsafa, na likatunza
ukweli wa sayansi.
Kielelezo
Cha Mduara Wa Maarifa, Ugunduzi Na Nguvu Cha Shoo
|
|
|
B,
t=T |
|
|
|
NGUVU |
|
A
t=0 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
A, t=0-X’s |
Tafsiri
Ya Kielelezo Cha Mduara Wa Maarifa Na Nguvu
A ni Mnara wa Babeli. t=0-X, ni Muda ambao
watu wote toka walipotoka mnara wa Babeli walikuwa sawa kwa kiwango Fulani katika
maarifa, teknolojia, afya, falsafa, na hata idadi.
B ni mwisho wa Milenia ya 7, yaani t=2031±. Ambapo jamii za binadamu wote wamekwisha changamana hata kufikia mfanano kabisa. Kama watu wa maarifa wanaongea lugha moja kila nchi. Kama wanadini wana kiongozi mmoja. Kama wajinga wapo kote, na wanasababu wote za kuwa wajinga, na wanaongea lugha moja. Kama wachawi, mashoga, kama wasanii, kama wanasayansi, n.k.
Mstari Mwekundu Waliopita
Ulaya-Asia Na Afrika Ya Kaskazini
Huu mstari una maana ifuatayo. Japokuwa
ukipima umbali wake, na mstari wa kijani, yote inalingana kabisa kiumbali. Lakini
mstari mwekundu unawakilisha jamii za Ulaya-Asia. Ambazo, Upande wa Ugunduzi,
kwa sehemu ya kwanza mpaka kufikia wakati Fulani. Ugunduzi ulikuwa juu sana.
Ugunduzi ulikuwa juu sana, ukilinganisha na Kiwango cha Ugunduzi kwa Mstari wa
Kijani, hii ni kwa kuwa, Njia waliyoipita ilikuwa ni mithili ya Kupanda Mlima,
Ijapokuwa mpanda Mlima atatumia Nguvu nyingi sana, ila atakapofika juu, ataona
umbali mrefu sana.
Nini maana ya Kupanda Mlima?
Kuishi katika Ukanda wa Mediterranean,
ambao ulipelekea kukua kwa kilimo. Haikuwa kazi rahisi. Historia ya Kilimo
haikuwahi kuwa Nyepesi. Na Ugumu wa Kilimo pia Ulichochea kukua zaidi kwa
falsafa za uwindaji, na Ukusanyaji. Bado hata kilimo kilipofanikiwa, kulikuwa
na changamoto kubwa sana za Milipuko ya Magonjwa.
Kwanini Kilimo Kilipelekea Milipuko ya
Magonjwa?
Kilimo kilichochea kuchanganya aina
mbalimbali za Mimea na Wanyama wanaofanana, kwa lengo la kuongeza uzalishaji.
Kadri unavyowachanganya Wanyama hawa, unawapelekea kuwa na Kinga dhaifu sana.
Matokeo ya kuwa na kinga dhaifu, ni kupelekea Kuanza kwa mashambulizi ya
vimelea. Lakini pia, Wanyama hawa unapowafuga kwa Pamoja katika sehemu ndogo,
unasababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa sana cha mbolea, (kazi kubwa ya vimelea
ni kuvunja vunja uchafu kama kinyesi, ili kurejesha virutubisho katika ardhi,
unapobeba mbolea, unabeba nyumba yao vimelea) ambayo itakuwa ikitumika hata
katika kilimo cha mimea. Mara zote hizi mbolea huwa ndizo nyumba za vimelea. Na
kwa mantiki hiyo, ufugaji na kilimo kilipekea kuibuka kwa kiwango kikubwa sana
cha Magonjwa.
Inafahamika kuwa idadi kubwa sana ya
magonjwa ya binadamu, yanatokana na Wanyama. Penginepo, hata magonjwa makubwa
yote yanaonekana kuhusiana na Wanyama. Mfano, Measles imetoka kwa N’gombe
(Rinderpest), Tuberculosis imetoka kwa Ng’ombe, Small pox imetoka kwa Ng’ombe
na Wanyama wengine, Flu kwa Nguruwe na Ndege, Pertussis kwa Nguruwe na Mbwa,
Falciparum Malaria kwa ndege, Salmonella kwa ndege, Leptospirosis toka kwa
mbwa, Brucellosis kwa ng’ombe, Psittacosis kwa Ndege, kuna UKIMWI toka kwa
nyani, kuna Tauni ‘’Black Plaque’’ hii iliua zaidi ya Robo ya watu wote wa
Ulaya kuanzia mwaka 1346. Kuna Influenza, Cholera, n.k. vimelea vingi
humwathiri binadamu moja kwa moja, au, hubadilika toka kwa Wanyama, na kuanza
kumuathiri binadamu moja kwa moja. Je wajua!! Hata magonjwa yasiyo ya
kuambukiza, bado yametokana kwa ulaji wa nyama, bidhaa za kisasa, na uharibifu
wa mazingira rejea Q4 (utaona uhusiano mkubwa wa Saratani na shida za mfumo wa
moyo na nyama, n.k.)
Changamoto za uwepo wa idadi kubwa ya watu, zilipelekea migogoro
mingi sana ya kisiasa. Ambayo watu wengi walipingana kwa hoja, kutetea misimamo
yao. Kushindana kwa dola, huku kote kulichochea sana kuongezeka kwa Ugunduzi
juu ya namna bora ya kutatua changamoto.
Ulaya-Asia pia imewahi kupitia vipindi
vingi sana vya ukame mkubwa. Kukosekana kwa chakula kwa maeneo na maeneo, na
haya yote yalichochea sana kuongezeka kwa Ugunduzi. Hasa katika kutafuta namna
ya kujiokoa.
Yesu Kristo alizaliwa katika miji hii. tena katika nchi iliyo maeneo ya
Katikati kabisa mwa dunia. Hii ni kumaanisha kuwa maarifa yatapaswa kusambazwa
kwa dunia nzima. Ujumbe wa ukristo haujawahi kuwa rahisi hata leo. Watu
hujifunza katika mazingira magumu sana, hasa enzi hizo za Rumi ya Ubepari. Haya
yote yanaonyesha ni kwa kiwango gani maeneo haya yalipitia changamoto kubwa
sana hata kabla ya kufikia Ugunduzi mkubwa sana.
Nini maana ya Kupungua kwa Nguvu katika
hatua ya kwanza?
Kipindi jamii nyingi za Afrika, na
Marekani. Zikizidi kuwa na watu wengi kulingana na maeneo yao. Na zikizidi kuwa
na vyakula na malighafi za kutosha, ambazo jamii hizi nyingi, hata thamani ya
mali zao kuna wakati hawakuziona. Mara nyingi ukiwa na nyingi sana, huwezi
kuona thamani sana. Mambo yalikuwa kinyume katika jamii za kaskazini.
Vita zilikuwa ni nyingi sana. Ufalme
uliondolewa kwa ufalme. Zama za Giza kwa mfano, kuna maelfu ya watu waliokufa.
Kuna vita zilipiganwa mfano kati ya Ufaransa na Uingereza, hadi miaka mia. Toka
ufalme wa Persians, mpaka Ugiriki, mpaka Roma, mpaka roma inagawanyika, mpaka
vinaibuka vikundi hatari kama ‘’Vandals, Huns’’, kuibuka na Kutawala kwa dola
ya Uislamu, kuibuka kwa dola ya Ottoman, Ugandamizaji wa Papa ulaya zama za
giza, milipuko ya magonjwa kama ‘’Black Plaque, Influenza, small pox’’, kuibuka
kwa dola ya Mongolian, zama za mapinduzi, ya ufaransa, vita za Napoleon,
Mapinduzi ya nchi nyingi za ulaya, Russia, Vita za Makabila ya Ujerumani ‘’Vita
za Balkan’’, vita ya kwanza ya dunia, vita ya pili ya dunia, n.k. haya yote ni
sehemu ndogo tu ya migogoro ambayo iliwafanya watu wa Ulaya-Asia kuwa sio watu
wakutulia kiakili. Inatambulika hata leo, Bara la Asia ndilo limemwaga damu
nyingi zaidi. Kila ufalme ulipotawala, watu wote waliotawaliwa walikuwa
watumwa. Nchi kama Russia zilipitia vita nyingi sana.
Kuelekea katika Ugunduzi mkubwa zaidi.
Watu walipitia maumivu makubwa zaidi. Walitumia nguvu kubwa zaidi. Upande wa
pili, jamii nyingi zimeanza kushuhudia mauaji makubwa sana baada ya Ukoloni
kutoka miaka ya 1880’s, mpaka uhuru miaka ya 1960’s kwa wastani. Lakini hata
hivyo tayari kulishakuwepo unyanyasaji wa Utumwa. Lakini utumwa haukuwa sehemu
za Afrika tu, sema tu Watumwa toka Afrika walikuja kupendelewa zaidi kwa
kuelekezwa marekani kuanzia miaka ya 1500’s mpaka 1900’s. Ukoloni haukuwa na malengo zaidi ya ujinga na
tamaa, na ndiyo maana hata nchi nyingi za Asia kama China bado zilikoloniwa na
Wamagharibi. Na hata wao wenyewe wakoloni, walipopigana vita ya kwanza, bado
walielekea kukoloniana.
Hivyo hitimisho hapa ni kuwa, watu hawa
walipitia kipindi kigumu sana. Ni rahisi kusema walipiga hatua kwa ugunduzi wa
unga wa risasi ‘’Gun-powder’’ huko china, lakini huo sio ugunduzi wenye kuleta
amani. Ni rahisi kusema waligundua Chanjo, lakini hautaambiwa hali zao za
kiakili mpaka wanaigundua hiyo chanjo. Ulaya imeshuhudia katika historia miji
mingi sana ikiisha watu karibia wote kabisa kwa vifo vya milipuko ya magonjwa.
Hatua Ya Pili ya Kushuka Ugunduzi
Hatua hii inahusisha sasa Baada ya
kugundua Mambo makubwa sana, hata kufikia kiwango Mr. Isaac Newton, Leibniz,
Georges Curvier, na wengine wengi mpaka Ellen G White, wanaweza kuelezea
Maarifa katika Lugha moja, yaani, Sayansi, Uumbaji wa Mungu, na Unabii wa Hatma
ya miisho ya Dunia. Watu hawa baada ya
kufika kilele chao cha Ugunduzi, wanaanza kushuka na kuingia katika Hali ya
Udhaifu sasa.
Jambo linalotokea ni la watu hawa kuanza
kupeleleza sehemu mbalimbali zingine za
dunia. Kwa lengo la kuweza kupata ahueni. Wakiwa na hofu kubwa, lakini wamejawa
na ujasiri wa kuzoea shida yeyote. Wanafika maeneo ya ndani kabisa ya Dunia. Na
cha Kustaajabisha!! Wanagundua kuwa, kuna sehemu ambazo wapo nyuma kabisa yao.
Na hicho ndicho kielelezo cha Nguvu zao kuanza kuongezeka tena. Hii ni kwa
namna wanavyoweza kuwatawala wenzao na kujimilikia nguvu nyingi sana.
Kielelezo cha Kushuka Kiugunduzi
kinamaanisha, kadri wanavyoanza kufanya utawala kwa wenzao, huku wakijiona wao
ni wapekee kiuwezo. Akili zao zinadhoofika. Kwa kuwa, Ugunduzi waliokuwa nao haukuwahitaji
Kutenda hivyo, wakazidi kusahau misingi hii. Wakasahau nidhamu, na upole wa
Baba zao kabla ya kuwa na ugunduzi huo na kuwarithisha. Kushuka kiugunduzi
kunahusiana na kutoruhusu kujichosha kimawazo, kufanya vitu kulingana na
mihemko ya kihisia isiyo na muelekeo wa nidhamu. Huu ndiyo mwanzo wa kushamiri
ulaya kwa elimu za kijinga kabisa, kama Nadharia za mabadiliko ‘’evolution’’,
Big-Bang, Uwepo wa jinsia ya Mashoga, Uharibifu wa Afya za watu kutaka
kuwatawala kiakili wenzao, n.k.
Kadri Ugunduzi unavyowashuka, ndivyo
wanavyozidi kupata Nguvu. Hii ni kutokana na kuzidi kutumia mbinu zao za
uharibifu katika nafasi ya uwezo waliokuwa nao awali. Mwisho wa milenia ya saba, hakuna nchi ambayo
itaweza kuwa na Nguvu ya Jumla juu ya nchi nyingine zote, ila itazipasa zote
kuungana na kutengeneza mfumo mmoja wenye Nguvu, ili kuweza Kutenda ajenda
zitakazopitishwa ikidhaniwa na wote, lakini kumbe bado tu ni za wachache.
Mambo Ya Kustaajabisha
Asilimia kubwa sana ya vita ambavyo watu
toka bara la ‘’Ulaya-Asia’’ walishinda, havikutokana na uwezo wao au bunduki
zao. Vilitokana sana na Magonjwa ambayo walikuwa nayo, lakini kwa kuwa wao
walikuwa na kinga nayo, hayakuwaathiri. Lakini kwa wageni waliowafikia, wengi
wao walikufa sana. Mfano, inakadiriwa asilimia 90% ya Wamarekani wa kwanza
kabisa ‘’Red Indians’’, ambao wanakadiriwa kufikia Milioni 20. Walikufa mpaka
wakabakia Milioni Moja tu, kutokana na Magonjwa waliyokuwa nayo Wazungu
waliofika marekani.
Lakini pia, idadi kubwa sana ya Waafrika, wamarekani, n.k. walioshindwa na wazungu. Wengi wao walikuwa ni wajinga sana. Wengine waliwapokea na mabunduki yao wakiamini yale ni mafimbo tu. Wengine waliwapokea wakiamini wale ni watu wema sana. Wengine waliwashinda baadhi, ila hawakuweza kutumia silaha zao. Wengine walisalitiana wao kwa wao. Kiufupi wengi waliangamia kwa kukosa Maarifa ambayo sasa hivi wanayo.
Kwanini Nimesema Ugunduzi Na Sio Maarifa?
Maarifa ni kila taarifa inayolenga kuokoa
uhai wa jamii kiakili, na kimwili, huku ikilenga kujenga jamii bora zaidi
kiufahamu wa Maisha bora kwa kila kiumbe hai. (Tambua: watu wanaangamia kwa
kukosa maarifa, sio ugunduzi, Danieli hakuangamia kwa kuwa alikuwa na maarifa,
ila enzi hizo bado ndege, wala umeme haukwepo). Ugunduzi ni taarifa yeyote mpya
yenye uwezo wa kipekee kiutendaji. Ugunduzi unaweza kuwa kinyume kabisa na
Maarifa. mfano, kuna mtu aligundua kuwa mwanaume anaweza mwingilia mwanaume
mwenzake na akasisimka.
Ugunduzi wa Unga wa risasi na
rocket-ranger, ulilenga kuua, na ugunduzi wa Printa ya kwanza kabisa ya umeme,
ulilenga kusaidia uandishi, na usasa. Hii mifano yote sio ya maarifa, ni ya
ugunduzi. Maarifa ni namna jamii itaweza kuishi kwa amani, wakiwa na chakula
bora, na afya njema ya kiakili, bila kufurahia maumivu ya wengine, wala uharibifu
wa mazingira kwa ujumla. Afrika ambayo ilikaribia sana sifa hizi, ilikuwa
karibu na Maarifa zaidi hata ya Ulaya-Asia. Ambao walikuwa na ugunduzi mkubwa,
lakini walikuwa mbali na maarifa, maana walimwaga sana damu (vifo vikizidi,
rejea: watu wanaangamia kwa kukosa maarifa)
Unaweza thibitisha hili kwa namna
ambavyo, ili wawe na maarifa iliwapasa nao waweke bunduki, na vikundi vya siri
vya kisasi pembeni, na kisha waanze kuishi kama Waafrika. Damu kubwa
waliyoimwaga na maumivu waliyoyapata, na afya za ubongo na mwili walizoziharibu,
zinalingana sawa sawa na ugunduzi walio nao, ili kuwasaidia walau wasiangamie
kabisa. mfano, kama wasingegundua Chanjo, ni nani leo hii angeandika historia
yao dhidi ya milipuko ya magonjwa ya virusi?
Kumbuka haimaanishi Maisha ya Afrika
yalikuwa ni kielelezo cha Maarifa moja kwa moja, bado waafrika walikuwa na
upumbavu mwingi sana kama tutakavyouona, na ndiyo maana walikuwa na Maarifa
kadhaa, lakini hawakubadilika kabisa Kiungunduzi ambao haukutegemea sana uwepo
wa dhiki.
Mstari
Wa Kijani Uliopita Afrika Na Marekani Ya Kale
Mstari huu unamaanisha kuwa, watu hawa Kinguvu
hawakubadilika sana mpaka katika hatua ya mwisho, wamekuwa wakiongezeka kwa
kiwango kidogo sana. Na mwishoni kabisa, wanaelekea kuwa kama wale wa mstari
mwekundu. msingi wa Maarifa ya Msingi
kabisa ambayo walipaswa kuwa nayo, nao waliyaacha kwa Kwenda mbali na mstari
mnyoofu, na tofauti na mstari mwekundu, hawa hawakuenda mbali na maarifa kwa
namna ya ugunduzi, na changamoto nyingi, wao walienda mbali na maarifa kwa
namna ya kupuuzia maarifa wakifanya vitu kwa kawaida sana, hata kutokujua
thamani zake, na mwishowe kuwa mbali na maarifa.
Hawa watu hawajawahi kutengeneza soda za
chupa za cocacola. Kiwango cha nguvu ambacho watu wanapaswa kuwa nacho, ndicho
hicho hicho walichokuwa nacho toka awali. Hapaswi mtu mmoja kumtawala mwenzake.
Hii ni kuonyesha si watu ambao walijilimbikizia sana nguvu dhidi ya wenzao kama
ilivyo kwa wenzao. Lakini dakika za mwisho kabisa, nao wanaungana na mstari
mwekundu, na kuwa sawa na mstari mwekundu kifalsafa za mamlaka za kutengeneza
matabaka.
Shida zote zilizotokea hapo Katikati kama
namna inavyoonekana wanavyozunguka, ni matokeo pale walipoacha kufuata mtindo
wao wa asili ambao walipaswa kuuishi. Hata hivyo, bado hatujafikia mwisho wa
miaka 7000, ambapo ndicho kitakuwa kipimo kizuri zaidi cha kupima hatma ya
ulimwengu kwa mzunguko mrefu zaidi.
Kosa Kubwa Lililo Wagharimu Waafrika Na
Wamarekani?
Hawa napenda kuwaita ‘’watu wa kuchukulia
vitu kawaida’’. Afrika hawana kitu chenye thamani kwao, ili mradi wanaishi, na
wanapata vitu kirahisi, basi kwao hawana muda wa kujishughulisha kutafakari.
Utajiri wa malighafi, na mazingira yasiyo na ushindani mkubwa, viliwapumbaza
kuwaza mahitaji makubwa mawili tu, yaani kula na kuzaliana. Ujinga hutawala
popote watu wanaporidhika, ndoa za mitala, ukeketaji wa wanawake, ukandamizaji
wa kijinsia, ibada za miungu na miti, ushirikina, na kuua walemavu na albino.
Afrika haikuwa na jumuiya kubwa za
kifalme, ilikuwa tu na vikabila vidogo vidogo tena vingi sana. Watu walikuwa na
ubaguzi sana, hasa wao kwa wao. Hawakuwa wepesi kushirikiana, na kukuza
Ugunduzi wao. Wageni waliochanganyikiwa walipowakuta watu hawa ghafla wakiwa na
Afya, malighafi na mazingira bora, huku wakiwa wajinga. Ilibidi Damu na maumivu
mengi yaweze kuwaamsha watu hawa, na ndiyo maana leo hii, hakuna vikabila tena
vya kubaguana, ila kuna Tanzania moja, au leo hii, wanawake na ma albino wapo
serikalini.
Lengo ni kuweza kutofautisha maarifa, na
ugunduzi. Lengo ni kungundua kuwa Afrika ilikuwa na Maarifa kama vyakula bora,
ndoa ni ya mume na mke, watu wanapaswa kuishi kwa kuridhika na uwezo wao, Mungu
anapaswa kuabudiwa, lakini, hawakuwa na maarifa yote, na hawakuwa na Ugunduzi,
kwa kuwa walijihisi hawahitaji ugunduzi.
Jibu Kwa Ufupi
Waandishi wa Habari hupenda uwape hata
hoja za kitabu kizima kwa neno moja. Swali la kwanini sio Afrika, au Marekani.
Ni ‘’Asia-Ulaya’’. Jibu lake ni kuwa, Ukipima Nguvu waliyotumia, Ugunduzi
uliofanyika, Maarifa waliyotumia, na Muda waliyotumia. Yote ni sawa
kabisa. Ni uelewa hafifu tu ndiyo
unaweza sema mtu anayekunywa soda ya Chungwa ya Kopo amefanikiwa kuliko
anayekula Chungwa toka kwenye mti.
Kielelezo Cha Jibu
Una watu wawili wanaoenda sehemu moja na
wanatakiwa wafike kwa wakati mmoja. Mmoja anapita njia ndefu sana, na anatumia
nguvu nyingi sana. ili afike kwa wakati kutokana na urefu wa njia yake,
inambidi akimbie au abuni mbinu ya kisasa ya kumrahisishia sana safari yake. Na
pia, anagundua maeneo mengi sana. Kwa upande wa mtu mwingine, yeye anapita njia
fupi sana, tena moja kwa moja. Yeye anaona vitu vichache sana, na anaonekana
hana ubunifu mkubwa sana.
Kwa Wajinga wote, huyu wa kwanza
anaonekana ana mafanikio makubwa zaidi ya huyu wa pili. Lakini katika fizikia,
nishati huwa haipotei, au haiwezi tengenezwa. hawa watu wote wana nishati
ileile. Na katika Ubongo, huyu wa kwanza uwingi wa taarifa alizoziongeza ambazo
ni nje ya lengo kuu, hazimpi faida yoyote, maana tayari zimeshapunguza uzito wa
taarifa kuu, kwa kujaza taarifa zisizo hitajika. Kujifunza kwa makosa,
hakumfanyi mkosaji kuwa mwanafunzi bora zaidi ya mwanafunzi asiye mkosaji.
Ipi Ni Jamii Bora Zaidi
Jamii pekee ambayo ilikuwa bora zaidi. Ilikuwa ni ‘’Israeli’’ kabla ya 70AD. Au kabla ya kuanguka kwa Jerusalemu na kuchukuliwa mateka. Jamii hii ilikuwa na misingi yote ya maarifa, kuanzia ulaji, mavazi, elimu, ibada, mtazamo wa kijinsia, n.k. lakini hata hivyo, bado ilianguka kwa kuendeleza misingi ya ubaguzi kwa kujiona bora zaidi ya wengine, na kukataa mfumo wa usawa kwa wote kwa kumkataaYesu Kristo. Na matokeo yake, ikaanguka, kama jamii zote Duniani zilivyoanguka, na kwa hivyo, hakuna jamii iliyokuwa imekamilika zaidi ya jamii zingine zote. Ila tu zilitofautiana katika aina za madhara.
SURA YA TATU
RAMANI ZA TABIA
Tabia ni Matendo ‘’action’’ juu ya Muitikio ‘’Reaction’’ wa jambo Fulani, au ni ‘’Muitikio
‘’reaction’’ juu ya matendo Fulani ‘’action’’. Kula sana inaweza kuwa ni tabia
inayotokana na kuhisi sana njaa, au kuhisi sana njaa kunaweza kuwa ni tabia
inayotokana na kula sana. Mara nyingi tabia huchanganywa na mazoea kimaana,
watu wengi huzungumzia tabia pale hali hizi zinapotokea zaidi ya mara moja. Ni
rahisi mtu kusema ‘’hii siyo tabia yake!!’’ akimaanisha, tendo linalotendwa kwa
mara moja tu na mtu fulani, linaweza kuwa, siyo tabia yake, bali tu ni msukumo
wa kiakili au kihisia wa huyo mtu kwa wakati huo.
Ni kweli tabia ni matokeo yanayohitaji
muda hata kujidhihirisha. Tabia haijengwi kwa mara moja. Na pia huwa
haijidhirishi kwa mara moja.
Sehemu hii tutaangalia namna ambavyo,
tabia sio tu matokeo ya muda. Bali pia ni matokeo ya eneo ambalo mtendaji yupo.
Ramani ya Tabia inamaanisha kuwa, kama ilivyo miti Fulani huwa ikiota sana
maeneo Fulani, na miti mingine isiote maeneo hayo. Vivyo hivyo na tabia nazo
hutofautiana kulingana na maeneo husika. Miti inayoota jangwani, sio sawa na
miti inayoota kondeni, tabia za watu wengi wa kanda za Joto, sio sawa sana na
Tabia za watu wengi wa kanda za baridi. Japokuwa tabia ni ngumu kidogo kuziweka
katika makundi ya kiramani kama ilivyo
miti. Lakini bado ukichukua ramani na kuziangalia tabia za watu, bado utagundua
maeneo mbalimbali yanatofautiana kitabia, kulingana na mazingira yake.
Kwanini tunao ujasiri wa kuzipangilia
tabia katika ramani, ni kwasababu kwa kiwango kikubwa sana watu hutenda, au
huitikia mwito wa matendo Fulani, kama matokeo ya fiziolojia zao za ndani ya
miili yao kwa wakati huo. Au kama matokeo ya matendo yaliyochochewa na
jenetikia zao kwa wakati huo. Hebu chukulia mfano huu, Kungekuwa kuna mto
Fulani unaopitisha maji Fulani yenye madini sumu ambayo huathiri sana hatua
Fulani za maendeleo ya ubongo, kwa kiwango kidogo sana kuweza kugundulika
kirahisi. Na watu wa mji unaotumia maji haya wakawa hawalijui hili, wakawa
wakiyatumia maji haya kwa muda mrefu. Watu wengi wa mji huu watakuwa waathirika
wa afya ya akili kwa kiwango Fulani. watu wa miji Jirani itakuwa ni rahisi sana
kutengeneza hisia za kuwa watu toka mji huu ulioathirika kuwa hawapo sawa sana
kiakili. Kwao, watu hawa watawaona kama watu waliowadhaifu kwa asili, na
watawatengenezea ramani kuwa, ukanda Fulani! watu wake hawapo sawa.
Jamii nyingi sana zimekuwa zikiwa na
dhana kadha wa kadha, ambazo kwa nje ni kama za kibaguzi. Utakuta mfano kwa
Tanzania ikisemwa kwa baadhi ya watu, ‘’Wachagga wabahiri sana, au wachumi
sana’’, au ‘’wamasai wanakimbia sana’’, au ‘’wahehe wanaweza kujinyonga kwa
hasira’’, au ‘’watu wa tanga wanapenda sana mapenzi’’, au ‘’wahaya wanapenda
sana sifa’’, n.k. zipo sifa nzuri pia kwa watu hawa hawa, labda, upole,
ufanyaji kazi, utu wema, n.k. hoja ni kuwa, kwa akili za watu wengi sana, kila
anapotoka sehemu moja Kwenda sehemu nyingine, huwa anatengeneza taswira kamilifu
ya jamii ya watu anaoelekea kuonana nao. Watu wengi hutengeneza taswira
kulingana na historia walizonazo, na makisio yao. lakini katika sehemu hii,
tutaenda kuangalia sababu za msingi kabisa, zinazochochea tabia Fulani, katika
mazingira Fulani.
Kwanini Tujifunze Ramani za Tabia?
Kama mazingira yako yanaweza kuwa na
vichocheo vingi ambavyo vinakusukuma katika Kutenda tabia zisizo njema, basi
inaweza kuwa ni hatari kubwa sana. Yapo mazingira ambayo yanaweza kukuchochea
kufanya uasi, au yanaweza kukuchochea kuwa mdhaifu, na kibaya zaidi, ni
mazingira ambayo yanaweza kukuchochea katika Kutenda mambo ambayo yanaweza
kukuangamiza kwa haraka sana.
SAYANSI YA RAMANI ZA TABIA
Miongoni mwa vitu vikubwa sana ambavyo
ninamshukuru Mungu kwa kuvigundua, ni vitu nilivyoviita ‘’EBSP’’, au
‘’Environment Brain Sensory Potentials’’. Rejea kisa cha mtaa mmoja wa jijini
Pentagon. nilichokielezea mwanzoni kabisa mwa hiki kitabu.
Utangulizi
Kwa kawaida Ubongo huwa una hatua
mbalimbali katika ufanyaji kazi wake. Kuanzia hatua ya kutulia kabisa, mpaka
hatua ya shughuli kubwa sana. Katika ubongo, kila hatua huusiana na mawimbi
maalumu kwa wakati huo. Mfano, kuna Mawimbi ya Delta (0.5-4Hz) haya ni pale mtu
anapokuwa amelala fofofo, au amerelax vya kutosha. Kuna Mawimbi ya Theta
(4-8Hz), haya ni pale mtu anapokuwa amerelax kawaida tu, ndoto za mchana mfano
mtu anavuta taswira yupo sehemu Fulani, n.k. kuna mawimbi ya Alpha (8-13Hz),
haya huwepo mtu anapokuwa ametulia huku yupo macho, anaweza kuwa amefumba
macho. Kuna mawimbi ya Beta (13-30Hz), haya mtu anakuwa anatafakari kwa kina,
na mwisho ni mawimbi ya Gamma (zaidi ya 30Hz) hapa ni pale ambapo kuna shughuli
nzito za kiakili au tambuzi zinapoendelea kufanyiwa kazi.
Unapopima Chaji ya Ubongo kwa mazingira
ya kawaida kabisa, seli za Ubongo huwa zina chaji ya (-70mV) katika kuta zake
‘’neuranal membranes’’, hii ni kumaanisha, Ubongo sasa upo ‘’stand by’’ kuweza
kupokea taarifa mpya.
Ubongo mara zote upo katika mzani sawa
‘’equilibrium’’ na mazingira yake ya nje. Kunapotokea tu mabadiliko katika
mazingira ya nje, ubongo hugundua kuwa hapa kuna kitu kimeharibika. Na kwa
hivyo, huongeza umakini. Na umakini huu huusiana na kutafuta nini inaweza kuwa
sababu, na utatuzi wa tatizo lililokwisha kutokea.
Kwa mantiki hii, Mazingira ya nje nayo
yanapaswa kuwa katika hali ya Kutulia kama tu ulivyo Ubongo kwa wakati mwingi.
Hii ni kwa kuwa, kadri kama yatakuwa yanabadilika, basi yanaufanya ubongo
usiweze kutulia. Ili ubongo wa kiumbe yeyote yule uweze kutulia, sharti
mazingira yake kwanza yatulie. Mazingira hata hivyo, mara nyingi huwa
yametulia. Mazingira huwa na viwango vyake vya asili vya utulivu.
Mfano;-Hewa safi, Oksijeni (21%), Kaboni
dioksaidi (0.03%), Nitrogen (78%), Argon (1%), na Mvuke.
-Maji ya Joto la kawaida ‘’room
temperature’’, 25.5°c yenye madini
kidogo toka katika ardhi, kama Sodium, Calcium, Iodine.
-Sauti kwa asilia ya mazingira huwa kati
ya 500Hz mpaka 4000Hz. Inapaswa kuwa ya asilia, laini, na haipaswi kuwa
mfululizo ‘’not continous’’.
-Hewa haipaswi kuwa na Harufu yoyote
kali. Na inapokuwepo inapaswa kuwa kwa muda maalumu tu. Isiwe mfululizo. Harufu
za matunda mazuri, maua, perfumes, moshi, uozo, n.k. zinapaswa kuwa kwa kiwango
kidogo, na sio endelevu.
-Ubongo unapaswa kuzoelea taswira za
miundo ya asilia. Macho hayapaswi kuona taarifa za kushtukiza, usizozitegema
kuziona, na taswira zote za kihisia. Kadri tunavyoona, ndivyo tunavyoungana na
asili, taarifa zote ambazo tunaweza kuziona lakini sio za asilia, zinatuondoa
katika asili yetu.
- Joto la kawaida kati ya Nyuzi (22°c
mpaka 24°c) huuwezesha mwili kuwa timamu na bora zaidi. Joto chini ya nyuzi
20°c na juu ya nyuzi 27°c, huufanya mwili kuanza kuhangaika kuurejesha mwili
katika wastani wa kawaida.
- Hali ya Ukijani. Watu wengi hata wasomi
wasio wataalamu wa Ubongo huwa hawajui kwanini, Ubongo huvutiwa na mazingira
yenye Ukijani. Ubongo unapoona hali ya ukijani, huwa unaamini kuwa maeneo hayo
yana Vyakula vya Kutosha, Huamini mimea haiwezi kukua bila maji, na hivyo,
huamini pia kuna maji ya kutosha. Ubongo pia huamini kuwa mimea itatoa Oksijeni
ya Kutosha, Ubongo huenda mbali zaidi, huamini kuwa eneo hili lina amani,
halina viumbe wakatili wakukata miti. Haya yote huufanya Ubongo kuzalisha
homoni nyingi sana za Dopamine, Serotonins na Endorphins, ambazo huufanya
Kufurahia. Ni kama ngonjwa anapofurahia anapomwona daktari wake amefika.
-Sura zenye Tabasamu ‘’smiling faces’’,
na sura tulivu ‘’plain faces’’. Mazingira kwa asili huwa yana viumbe ambao muda
mwingi zaidi, sura zao huwa ‘’plain’’. Kwa miaka yangu mitano katika taaluma ya
Utabibu wa Wanyama, natambua ni vigumu kwa mtu wa kawaida kugundua kuwa mnyama
kama ng’ombe amekasirika, au paka, au ndege. Ijapokuwa mbwa atakubwekea, lakini
ndani ya muda mfupi utamwona sura yake ikiwa imetulia. Viumbe wote huvutia,
ukimtazama ngamia, punda, farasi, n.k. Ubongo huwa hausisimki kwa sura hizi, wala
huwa hauoni tashwishwi, ni kama ilivyo kwa namna viumbe wote Watoto hupendwa,
kwa namna sura nzao ndogo nzuri huonesha amani, Ubongo hupenda amani. Sura
zilizochoka, ubize, kufeli, ghadhabu, kwa asili sio sehemu ya mazingira ya
asili.
- Udongo wenye rangi ya Weusi kwa mbali,
chembechembe ndogondogo zisizo na mawe makubwa, mitelemko ya kawaida, mazingira
ya namna hii huchochea hisia za usalama. Huondoa hofu ya nguvu za mafuriko,
hatari za ajali, kukosekana kwa vyakula kwa kukosa rutuba, n.k.
-Upepo baridi wa kawaida, huu huashiria
uwezo mzuri wa eneo kudhibiti joto la jua kali. Uundwaji wa mawingu ya mvua,
n.k.
-Mwisho, Mazingira yenye viumbe wengi wa
jamii mbalimbali. Mfano, Ubongo wa binadamu unapokuwa katika mazingira yenye
Binadamu wengine, huwa unajisikia amani sana. Hii ni kwa kuwa, huamini ubora na
nguvu ya jumuiya katika mazingira hayo. Binadamu ni viumbe wa kijamii, huvutiwa
sana na jamii. Wanapofika eneo lisilo na watu, huwa na mashaka wenda kukawa na
hatari zilizowafanya wengine wahame au kulimbia eneo hilo.
Mazingira mara zote huzungumza na Ubongo
katika lugha ya kitaalamu sana ambayo, kwa kuangalia tu juu juu mtu anaweze
asielewe nini Ubongo unataka.
Katika mazingira ya mtindo huo
niliyoyazungumzia. Ubongo huwa na utulivu wa kiwango kikubwa sana. Hii ni kwa
kuwa, huwa kuna kiwango kidogo sana cha vichochezi vya kuusisimua sana.
Mazingira ya mtindo huu huufanya ubongo kuwa na ufanisi mkubwa zaidi, au
ufanisi bora sana.
Nini Maana Ya Environmental Brain Sensory
Potentials ‘’EBSP’s’’
Tuna watu wawili. Mmoja yupo ‘’Kariakoo’’
Jijini Dar es salaam, na mwingine yupo ‘’Lupembe’’ Mkoani Njombe. Tunaenda
kuwapima watu hawa Ubongo wao katika mashine ya ‘’ EEG’’ kuangalia viwango vyao
vya Shughuli za umeme wa Ubongo katika mizunguko yao ya siku nzima. Katika
mazingira yao hukohuko. Tunawapima na kisha, tunarejea jaribio hili kila siku kwa
kipindi cha miezi mitatu.
Na baada ya hapo, tunakuwa tumeshajua
wastani wa viwango vya shughuli za umeme wa ubongo wa watu hawa, ‘’brain
sensory potentials’’. hizo ndizo tunazoziita ‘’EBSP’s’’. baada ya kuzijua hizi,
hatuna tena haja ya kuhangaika kujua wastani wa tabia za watu hawa. kwa kuwa,
tayari tunajua nguvu ya matendo, na muitiko wa tabia za watu hawa. Kwa kuwa, ni
Ubongo wao ndiyo una Sukuma matokeo yote ya tabia za watu hawa kupitia utendaji
wa mfumo wake wa umeme wa ubongo.
Umuhimu wa EBSP’s
Inamsaidia mtu kujua ni kwa kiwango gani,
mazingira yake yanamuathiri. Watu wengi sana huwepo katika mazingira ambayo
kiuhalisia huathiri kila sekunde ubongo wao. Madhara haya huwa hayajioneshi kwa
mara moja, lakini kila siku yanazidi kuua Ubongo kama tutakavyoangalia kidogo
hapo chini.
EBSP’s hudhihirisha ni kwa namna gani,
kila eneo lenye viwango vinavyofanana vya sifa za kimazingira, hufanana hata
kitabia. Watu wengi sana huumwa, huwa wahanga wa shida mbalimbali, huangaika na
madawa. Lakini kiuhalisia msingi wa matatizo yao, hutokana na mazingira ambayo
huwa wanayaishi kila siku.
Msomaji anapaswa kutambua kuwa, ijapokuwa
mtu anaweza patwa na msongo wa Mawazo sana kutokana na kuachana na mpenzi wake.
Lakini ukweli ni kuwa, kiwango kikubwa zaidi cha msongo wa Mawazo aliyonayo
kimepandishwa zaidi na kiwango cha msongo ambacho alishakuwa akichochewa nacho
kila siku katika mazingira yake.
Sehemu hii hatutazungumzia kila tabia, lakini tutagusa miongoni mwa kanda mbalimbali na hatari ambazo wako hatarini zaidi kuwa nazo, kutokana na viwango vikubwa vya EBSP’s kama tutakavyoangalia.
NYANDA ZA JUU
Jiografia fupi
Maeneo haya yana baridi kali sana.
Kiwango chake cha baridi hubadilika kulingana na usawa wake kutoka pwani ya
Bahari. Kwanini maeneo haya yana baridi? Ni kwa kuwa, yapo usawa wa juu sana
toka usawa wa chini, au bahari. Hewa katika anga, ni kama maharagwe kwenye maji
katika sufuria, huwa mengi sana chini kwenye sufuria kuliko juu, sababu ni
‘’density’’ kubwa huyafanya yatuame sana chini, hewa pia huwa nzito sana usawa
wa chini, na huwa nyepesi sana usawa wa juu.
Na hiki kitendo cha kuwa nyepesi sana
usawa wa juu, hufanya maeneo ya juu sana kuwa na hewa nyepesi, au presha ya
anga ndogo, au huitwa ‘’low atmospheric pressure’’. Hii presha kuwa ndogo,
husababisha Joto nalo kuwa dogo sana.
Kwa sababu, hisia za Joto hazitokani na
mionzi ya moja kwa moja ya joto toka kwa jua, bali inatokana na mionzi ya jua
kuichoma dunia, na kisha dunia kuzalisha joto ambalo watu hulihisi kupitia hewa
inayochemka sasa kutoka katika dunia. Hewa ya joto inapokugonga ndipo
inakuchochea kuhisi joto. Hii hewa kadri inavyopanda kuelekea juu huzidi
kupoteza nishati au joto lake, na inapofika juu kabisa, huwa ya baridi sana
kama ilivyomiji mingi ya nyanda za juu.
Kuelewa hili, vuta picha unajipulizia
spray, utaona unahisi sana baridi, kwanini? ni kwasababu, ndani ya chupa ya
spray kuna presha kubwa maana imejazwa sana, na kadri inavyojaa sana ndivyo
molekuli zake zinapogongana sana, na kuwa za moto sana, ila nje unapoipulizia,
kuna presha ndogo sana, hivyo unavyoipuliza spray, zile molekuli za hewa
hutanuka sana kwa kuwa nje hakuna mgandamizo tena, na hapo inapojitanua, kama
wewe unapojitanua kitandani unapohisi sana joto, basi hupoteza joto lake haraka
sana, na huwa ya baridi sana kama unavyohisi inapokugusa. Hivyo ndivyo
ulivyopia upepo pale makambako unapokugusa, huo upepo ungekugusa ulipokuwa pale
chalinze au Bagamoyo, usingeuhisi wa baridi, lakini ulipopandisha mlima
kitonga, ulipoteza joto jingi sana.
Kwa maeneo kama ya milima kama
Kilimanjaro, unaweza ona Barafu kabisa. Hii ni kwasababu, kiwango kidogo cha
hewa husababisha presha kuwa ndogo sana, na joto kuwa dogo sana. Na hivyo basi,
mvuke wote unaoweza pita maeneo haya ukiwa umebebwa na upepo huganda kama vile
mvuke unavyoganda kuzunguka chupa ya soda ya baridi sana inayowekwa mezani.
Maeneo haya huwa hayana mvua nzito kama
maeneo ya nyanda za chini kusini. Hii ni kwakuwa, kwanza hupokea mvua kwa pande
zinazotazamana zaidi na upepo. Na pili, bado anga lake kuwa jepesi, tena lenye
baridi sana, husababisha mvuke mwingi wa maji kuwa katika namna ya kama vumbi
la barafu ‘’fog’’, (rejea namna maeneo haya yanavyoonekana yakiwa yamejawa na
mvuke, hata usione mbele wakati mwingi sana). Hii inamaanisha, anga lake halina
uwezo wa kubeba kiwango kikubwa cha hewa ya mvuke hata kuja kutengeneza mvua
nzito.
Na hivyo maeneo haya, huwa na mvua
nyepesi nyepesi. Na kitendo cha anga lake kuwa jepesi humaanisha pia kuwa, hata
kiwango cha hewa ya oksijeni huzidi kupungua kadri unavyopanda kuelekea juu
zaidi. Kwa pande ambazo huwa nyuma ya upepo ‘’leeward side’’, huku hupokea mvua
chache zaidi, na huwa kukame sana.
Maeneo haya huwa hayana misitu mizito
sana. Hii ni kutokana na kuwa na mvua na maji kidogo. Huwa hakuna mito mikubwa
sana maeneo haya, ila huwa kuna chemichemi na mito midogo. Huwa kuna viumbe
wachache sana katika mbuga ndogondogo katika maeneo haya. Na wengi wao huwepo
maeneo ya chini au bondeni mwa miinuko, au huitwa kwenye ‘’vinyungu’’.
Maeneo haya huwa yana vipindi vifupi sana
vya Jua. Huwa muda mwingi sana kukiwa na mawingu, au kukiwa na ‘’fog’’ yaani
anga likijaa mawingu. Hii ni kwa kuwa, kwanza hewa inapopaa tu huishia kuunda
mawingu kutokana na baridi kali. Pia, kipindi cha usiku, hewa nyingi ambayo
huwa ikipaa hewani, hutengeneza wingu la mvuke ‘condense’’, na maeneo haya,
anga la hewa la joto huwa juu na la baridi huwa chini, na hujitenga. hii
hupelekea mawingu kudumu kwa wakati mrefu sana. Pia jua linapokucha, hupelekea
hewa ya joto kupaa ambayo ndani ya muda mfupi tu kwa wakati wa mchana,
hupelekea tena kuundwa kwa mawingu.
Maeneo haya huwa na mvua za mara kwa mara
lakini zilizo nyepesi nyepesi. Ukijumlisha na hali ya baridi. Maeneo haya huwa
yakiwa na asili ya ukijani kwa wakati mwingi sana. Na hii huchochea sana kilimo
kwa maeneo ya mabondeni, na kando ya vimito vidogo. Maeneo haya huambatana na
kiwango kikubwa sana cha miti, aidha ya mwitu, au ya kupanda. Miti yake huwa
haiwi mikubwa sana, ila huwa ya wastani mpaka midogo, na hustawi sana. Kiwango
kikubwa cha miti na ukijani huchochea kiwango cha oksijeni, na mbogamboga nyingi
sana na matunda.
Maeneo haya huwa hayana nyasi nyingi za
pori. Ni mara chache sana kuona wafugaji wa Wanyama wakubwa kama ng’ombe maeneo
haya. Hii ni kwa kuwa, hali zake za ardhi hazisapoti uotaji wa nyasi nyingi
sana za kusapoti Wanyama wakubwa. Nyasi nyingi huitaji kina kirefu cha udongo
ulioshiba maji, lakini maeneo ya huku huwa na matabaka mafupi ya ardhi Kwenda
chini, na huwa na miinuko ambayo ni hatari kwa Wanyama wakubwa. Na pia,
mazingira ya wafugaji wengi huwa ni Maisha ya kuishi maporini wakiwa na mavazi
rahisi sana, mitindo hii ya Maisha si rahisi kuiishi katika maeneo ya baridi
kali.
Kiufupi maeneo haya huwa yana kiwango
kidogo sana cha Wanyama, hata na Samaki. Wakazi wengi huwa hawapati protini
nyingi za Wanyama kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa wakazi wa mabondeni.
Mazingira mengi ya nyanda hizi huwa yana
utulivu mkubwa sana. Huwa kuna kiwango kidogo sana cha misongamano ya watu, au
mikusanyiko ya watu wengi katika eneo dogo kama ilivyo kwa jamii nyingi za
kusini. Hii huchochewa pia na hali ya utulivu wa shughuli nyingi kulingana na
hali ya joto inavyozidi kuwa ndogo.
Maeneo haya huwa katika ukanda wa
Sub-tropiki.
Nini maana ya Tropiki, na Sub-tropiki?
Tropiki ni ukanda uliopo karibia sana na
mstari wa equator, yaani ni eneo linalotoka equator nyuzi sifuri, mpaka kufika
nyuzi 23.5° kaskazini, na kusini. Maeneo ya Tropiki mfano Morogoro, huku
tropiki ikikolea zaidi katika miji ya Dar es salaam, na Zanzibari. Huwa na
wastani wa jotoridi wa 25-30°c. maeneo haya huwa na kiwango kikubwa sana cha
mvua, na mvua zake huwa sio za vipindi vya kubadilika badilika. Ukipima kiwango
cha mvua katika maeneo haya, kinaweza kufika kuanzia 1200mm, mpaka 2500mm. ni
mvua nyingi sana.
Tropiki huwa ni maeneo yenye misitu
mizito. Na utaona mimea kama Minazi, Michikichi, miti ikishonana sana. Mazao
hukua sana kutokana na uhakika wa maji. Maeneo haya hushamiri sana kwa kilimo
kama cha Mpunga unaohitaji maji, mihogo, Cocoa, Kahawa, Miwa, michikichi, na
matunda kama maembe. Morogoro wanalima sana Mpunga, na hata mahindi, ijapokuwa
uzalishaji wake hauwezi shindana na wa shinyanga, au Mwanza.
Kwanini Iringa na Mbeya Zinaongoza
Uzalishaji wa kilimo Tanzania?
Ijapokuwa sub-tropiki ni maeneo
yanayoanzia nyuzi 23.5° mpaka 35° kusini na kaskazini mwa equator. Na tunategemea
maeneo haya kuwa na mvua za msimu, kuwa na wastani wa nyuzi joto za 20-30°c
kulingana na msimu. Maeneo haya huwa hayana sana mvua nyingi, huwa na maeneo
makubwa ya usavana kuliko tropiki.
Na maeneo haya ya Iringa, Njombe na
Mbeya, na Songwe, kulingana na hali zake za baridi na mvua za msimu, yanaweza
kuzalisha sana kilimo cha mazao yasiyohitaji mvua nyingi sana, matunda matunda
mengi kama machungwa, zabibu, ‘’citrus fruits’’, maparachichi, chai, mahindi,
ngano, na mbogamboga.
Kwanini sasa maeneo haya yanayazidi
maeneo ya tropiki kiuzalishaji?
Sababu ni kuwa, maeneo haya ya tropiki
huwa na mvua kubwa sana ambazo, hupelekea mmomonyoko wa udongo, na kupelekea
ardhi kupungukiwa sana virutubisho. Unaweza kuona namna ambavyo mikoa kama ya
Morogoro namna ambavyo hupatwa sana na majanga ya mafuriko, na hata udongo wake
ni mwekundu kwa maeneo kadhaa. Changamoto hizi zote hutokana na kiwango kikubwa
cha mvua.
Pia, maeneo haya huwa na joto, na mvuke
mwingi sana. Ambao, huchochea sana kushamiri kwa vimelea vya magonjwa ya mimea
‘’pests’’, na magonjwa ya mimea kwa ujumla. Hii ni tofauti kabisa na mikoa ya
sub-tropiki, ambayo, kiwango kikubwa cha baridi, huchochea sana kutoshamiri kwa
vimelea, na magonjwa. Na hii huyafanya kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi. Bado
maeneo ya sub-tropiki huwa na hali ya baridi ambayo, hupunguza kukauka kwa
mimea, na jamii nyingi hutumia namna za umwagiliaji katika kilimo.
Hii pia hufanyika nyanda za juu
kaskazini, na ndiyo sababu ya Kilimanjaro na Arusha bado kuwa juu kiuzalishaji
kuzidi Morogoro na Pwani. Kumbuka, ukame huathiri sana kilimo kwa maeneo ya
nyanda za juu, lakini madhara huwa makubwa zaidi kwa ukame katika maeneo ya
kusini ambao hulima sana mazao ya muda mrefu, na huwa hawatumii sana namna ya
umwagiliaji.
BIOLOJIA ZA WATU KWA ASILI KWA MAZINGIRA
YA KUSINI JUU.
Kufanya Sana Kazi na Kuwa na Nguvu.
Watu wa maeneo haya huwa wanafanya sana
kazi. Hii ni kwa kuwa, hali nzuri ya hewa isiyo na jua kali sana, huwapa muda
mwingi sana ndani ya siku wa kuweza kufanya kazi. Maeneo haya huwa na baridi
kali sana, ambayo, huwa haisapoti sana kulala sana, watu wengi wa maeneo haya
hata kufanania na ulaya, huwa na usingizi wa juujuu sana, ambapo inapofika
asubuhi, huwahi kuamka na kuingia kazini, wakifanya kazi hata muda wa jioni
sana.
Maeneo haya kutokana na mazingira yake
kijiografia, vituo vingi vya huduma huwa mbali sana na makazi ya watu. Unaweza
kuta makazi ya mtu mmoja mmoja mpaka kufika shuleni, au shambani, au hospitalini,
au popote pale, kunahusisha mabonde, au milima. Hii huwafanya watu hawa kuwahi
sana kuamka, na kutumia nguvu sana hata kufika katika maeneo husika.
Itamhitaji mtu kukusanya kuni za kutosha
kwa ajili ya kupata moto kipindi cha baridi, kulima mlimani ni kazi ngumu
kuliko bondeni, kutokana na ugumu wa ardhi. kutoka sehemu moja hata nyingine
katika jiografia hii huwa ni shughuli ndefu sana, watu wa maeneo haya huwa
wakiishi mbalimbali kwa wastani, hivyo watu hujitahidi sana kufanya kazi sana,
ili kupunguza utegemezi wa vitu vidogo vidogo kwa wengine kama ilivyo kwa watu
wa maeneo ya chini pwani.
Watu wa maeneo haya huwa ni watu wenye
nguvu sana. Hii hutokana na Maisha yao ya kimazoezi kila siku, lakini kutokana
na lishe zao. Watu wa maeneo haya huwa na lishe bora sana zinazotokana na
matunda mengi, mbogamboga nyingi sana, na protini toka kwa Wanyama na mimea.
Kwa Nchi kama ya Tanzania mara nyingi zaidi Ghala za Nchi nzima huwa zikijazwa
na watu wanaoishi toka katika kanda hizi za juu kusini. Kuna wakati watu wa
maeneo haya huwa hata wakiwa hawana muda sana na Watoto wao kwa namna wakiamka
tu, hudamkia mashambani, na hiyo hupelekea changamoto baadhi za afya kwa
Watoto.
Kuwa na Mapafu imara na Mwonekano wa wastani wa Ufupi.
Mara nyingi hata kwa takwimu za watu
wanaoishi miinuko ya Himalaya, Andes, na Ethiopia. Watu wa maeneo ya nyanda za
juu zenye baridi, huwa na maumbo ya ufupi kwa lengo la kupunguza saizi ya mwili
usipoteze joto sana kutokana na baridi kali. Maeneo ya miinuko huwa na oksijeni
chache kwa wastani ukilinganisha na maeneo ya mabondeni, hii huyafanya mapafu
ya watu hawa kuongezeka ukubwa ili kuweza kuchakata zaidi oksijeni iliyopo
katika anga lao.
Kuwa Na Mwonekano wa Weusi
Kutokana na anga la maeneo ya nyanda za
juu kuwa na kiwango kidogo sana cha hewa, au kuwa jepesi. Mionzi mingi sana ya
‘’UV-Rays’’ hulipita anga hata kuweza kuwakuta watu wa maeneo haya. UV-Rays
husababisha uzalishaji mkubwa sana wa Melanin, kwa lengo la kujikinga na mionzi
hii. Melanin mara zote hufyonza mionzi, na kupunguza madhara yake kutoathiri
moja kwa moja tishu za ndani ya Ngozi. Kadri melanin inapozalishwa, ndipo
mwonekano wa Weusi unapoongezeka.
Watu baadhi huchanganya kwa kuhisi kuwa
ni baridi inayochochea mwonekano wa Weusi. Si kweli! baridi hata Ulaya ipo kali
zaidi lakini watu wa kule ni weupe zaidi. Ni mionzi ambayo maeneo ya nyanda za
juu huwa kwa wingi zaidi, kutokana na kupita kiurahisi. Maeneo mengi ya Afrika
ya kaskazini, na Ulaya-Asia, huwa kwenye Latitude ambazo zipo mbali na equator,
na Jua huwa lipo mbali kidogo kutokana na kukunjika kwa umbile la dunia katika
maeneo kuelekea kaskazini. Hii hupelekea mionzi kutembea kwa umbali mrefu zaidi,
na kadri inavyotembea umbali mrefu, basi hupoteza sana nguvu, na hata
inapofika, watu wa maeneo haya kutokana na baridi kali, huwa wakivaa nguo za
kujifunika sana, hivyo hupata mionzi kidogo sana, na huzalisha melanin kidogo
sana, na huwa weupe sana.
Kuwa na Kinga sana ya Mwili
Kwanza kabisa baridi huupa mwili kiwango
kidogo cha stress ambayo, huuchochea mfumo wa kinga kuwa imara zaidi. Hiki
kitendo kitaalamu kinaitwa ‘’hormesis’’. Lakini matendo kama ya kutetemeka
huambatana na uzalishaji wa protini kama ‘’Irisin’’ ambayo ina umuhimu sana
katika afya ya matendo mengi sana ya kibiolojia, ambayo mtu angeyapata
angefanya mazoezi tu, lakini kutetemeka tu huizalisha kwa wingi sana. Mafuta
bora kabisa yanayoitwa ‘’Brown Fats’’ huzalishwa katika maeneo ya baridi, na
uzalishaji wa mafuta haya, huambatana na uzalishaji wa chembechembe za kinga
zinazoitwa ‘’cytokines’’, hizi huboost zaidi mfumo mzima wa kinga.
Bacteria wengi, virusi, fangasi, protista
na minyoo. Huwa kama wamehifadhiwa kwenye friji katika maeneo ya baridi kali.
Baridi huwapunguzia sana spidi ya kuzaliana, na pia spidi ya kuambukiza. Hii
huifanya mifumo ya kinga ya wakazi wa maeneo haya, kuwa imara sana.
Mara mtu ametetemeka na kupelekea mishipa
ya damu kuingia ndani zaidi ya Ngozi ikijikunyata ‘’vasoconstriction’’, au
ghafla baridi imepungua, mishipa ya damu sasa ime relax tena, sasa imefanya
‘’vasodilation’’ ikitokeza sana nje na ngozi. Mfululizo wa matendo haya, hupelekea
watu hawa kuwa na mfumo imara kabisa wa damu.
Na pia inatambulika kuwa, baridi kali huchochea uzalishaji wa seli
nyekundu za damu ‘’RBC’s’’, ambazo, husaidia kukusanya zaidi hewa ya oksijeni.
Mfumo wao wa upumuaji upo imara sana,
mapafu yao huwa makubwa sana yakiweza kutoa uchafu kirahisi sana. Na hii
hupunguza sana kusambaa kwa vimelea vya magonjwa ya mfumo wa upumuaji.
Inatambulika pia kuwa baridi huchochea
sana pia uzalishaji wa seli nyeupe za damu ‘’leucocytes’’. Na pia, baridi hupunguza uvimbe, kama tu
wachezaji wanapojiwekea barafu wanapovimba.
Hivyo baridi husaidia kupunguza uvimbe sugu.
Pia kutokana na uzoefu wa kawaida wa
maeneo haya, huwa kuna kiwango kidogo sana cha hewa chafu, hii ni kwa kuwa,
huwa kuna kiwango kidogo sana cha joto, lenye kuweza kupelekea molekuli nyingi
za hewa chafu kuunda gesi chafu ‘’evaporate’’ na kuchafua mazingira yote. Hii
husaidia sana kupunguza matatizo ya mfumo wa upumuaji.
Tabia za Ulaji
Watu wengi wa nyanda za juu kusini,
kutokana na hali ya hewa ya baridi, na jiografia za maeneo haya. Huwa ni watu ambao hula sana. Hii ni kwa kuwa, ili
kuzalisha nishati ya kutosha kupambana na joto linalopotea. Watu wa maeneo haya
hula kiwango kikubwa sana cha vyakula vya wanga, kwa wastani, ukilinganisha na
watu wa nyanda za chini.
Ulaji wa watu hawa hutofautiana kati ya
maeneo na maeneo. Baadhi ya watu wa maeneo haya hupata changamoto kubwa sana ya
kupata virutubisho vya kutosha katika mazingira yao, hasa pale wanapokuwa wapo
upande unaopokea kiwango kidogo cha mvua. Maeneo hayo huwa na kiwango kidogo
cha mimea yenye virutubisho vya kutosha, lakini pia huwa hata na Wanyama
wachache kuweza kutosheleza mahitaji ya protini kwa walaji wa nyama. Jamii
zenye sifa hizi kuna wakati zimewahi kuonekana kupendelea hata ulaji wa wadudu,
au Wanyama wadogo sana, kwa lengo la
kukidhi mahitaji ya upungufu wa virutubisho kadhaa.
Kwa jamii zote ambazo huwa na upungufu wa
lishe, au virutubisho, kwa mazingira ya baridi kali na kazi nyingi, yanayohitaji
nishati kubwa hasa kwa Maisha ya kila siku ambayo tayari huitaji nguvu nyingi
kwenye kanda hizi zenye milima na mabonde, basi watu wa maeneo hayo huishia
kuwa na miili midogo, kama namna ya ukuaji mdogo kulingana na deni kubwa la
nishati inayoingia ukilinganisha na nishati inayotoka.
SAIKOLOJIA ZA WATU KWA ASILI KWA MAZINGIRA YA KUSINI JUU.
Asili Ya Upole Na Kutowehuka Kirahisi
Wanasaikolojia wote ulimwenguni
wanatambua kuwa, kuna uhusiano kati ya Joto, na Hasira au hata Ukatili. Na wao,
hutumia kielelezo walichokigundua na kukiita ‘’CLASH’’ yaani, ‘’Climate,
Aggression, and Self Control in Humans’’. Sababu wanazotumia kuelezea uhusiano
wa joto na ukatili, au hasira, huwa wanauita ‘’Short time life strategy’’.
Kwamba, kwa kuwa maeneo ya joto huwa hakuna mabadiliko sana ya hali za nchi
‘’less seasonal variations’’. Basi, maeneo haya watu huwa hawawazi sana kuweka
au kuwekeza vitu kwa msimu wa baridi utakapofika, ambapo hawataweza kufanya
baadhi ya shughuli.
Kwa hiyo husema, asili hii ya kutowazia
sana siku za mbeleni kwa kuwa mara nyingi hali huwa zipo sawa tu kwa wakati
mwingi sana. Huwafanya kuwa ni watu wa kufanya vitu kulingana na hisia na
uhitaji wao tu kwa wakati huo. Na sio kwa ajili ya wakati wa baadae.
Wanasaikolojia hawa wanasema, hii huwasukuma kuwa na tabia kidogo sana ya
kujizuia ‘’self-control’’, mfano, anapohitaji kuzaa, atazaa hata Watoto wengi
sana, atakapojisikia hasira, atapambana.
Na husema kwa maeneo ya joto ambayo hata
viumbe wengi wenye sumu huwepo, tabia hii huwa na faida sana kwa watu, lakini
ndiyo huwachochea kuwa wenye tabia za kuripuka kwa kutenda.
Baadhi ya wanasaikolojia katika kielelezo
hikihiki wakaongezea tena kwa kusema, kiwango kikubwa cha joto huwafanya watu
wengi kuwa nje ya nyumba zao, au kuzurura nje kujikinga na joto kali la ndani.
Na kadri watu hawa wanavyokuwa nje mara nyingi, basi huwa na asilimia kubwa
sana ya kuwa na migogoro mingi kati ya wao, kwa wao.
Kielelezo hiki kinaelezea uhalisia wa
matokeo ya joto, na hisia za kulipuka hasira, au ukatili kwa usahihi kabisa.
Lakini kinafeli kwa asilimia kubwa sana kuweza kueleza sababu za msingi za
tabia hizi za hasira kwa watu wengi wa maeneo yenye joto kali. Na sababu hizo
nitazielezea kiusahihi zaidi katika wakati tutakapoangalia maeneo ya joto.
Kumbuka, kielelezo hiki hutumika kuwatenganisha au ‘’group’’, watu wa ukanda wa
equator, na watu wa ukanda wa mediterranean, na latitude za juu zote. Hapa
unazungumzia maeneo mengi ya Afrika kama watu wa kanda za joto, na watu wa
Ulaya-Asia kama watu wa kanda za baridi. Lakini bado kuna ukweli mwingi sana
wanaouzunguka, na kuukwepa, au hata kutougundua ambao tutauangalia.
Baridi huchochea hali ya upole, hali ya
kutulia, au hali ya kutolipuka kirahisi kwa mihemko ya hasira. Haimaanishi kuwa
watu hawa huwa hawalipuki kwa hasira, ila ina maanisha, huwa na uwezo mkubwa
sana wa kujizuia. Zipo sababu mbalimbali ambazo huwafanya watu hawa kuwa si
wepesi wa kuwehuka.
Kwanza kabisa, ni uwezo wao mkubwa wa
kustahimili presha ya damu, ambapo hasira huanza na mlipuko wa mfumo wa
‘’Sympathetic nervous system’’, ambapo mwili huzalisha chembechembe za
‘’adrenaline’’ za kutosha ambazo huchochea presha ya damu, na sehemu katika
ubongo ‘’amygdala’’ husisimka juu sana ikichochea motisha ya matumizi ya misuli
hasa ya mikono, na misuli mingine kama ya mapafu kubana hewa nyingi, kwa ajili
ya kupambana, na matendo haya, kwa watu wa maeneo ya baridi, huwa hayana
urahisi wa kusisimka kwa kuwa, nishati kubwa sana hutumika kuanzia katika
kuuchochea mwili upate joto la kutosha la hasira, mishipa ya damu ijitanue ili
hali kuna baridi, mfumo wa damu uongeze spidi kufika hata katika ubongo, au
adrenaline isambae vya kutosha katika mwili mzima, na watu hawa huwa na mifumo
mizuri sana ya damu, hivyo hata presha huwa haina nguvu sana ya kuwachochea.
Wengi wao pia sio wala nyama sana, hivyo kiwango kidogo cha ‘’SFA au
Triglycerides’’ huwafanya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kubalansi presha yao, hii
huwafanya kutolipuka kwa urahisi kama upande wa watu wa kwenye joto.
Chukulia mfano huu, una watu wawili. Mmoja ameshashuhudia ndugu yake akiuwawa kwa kupigwa risasi kwa bunduki, na mwingine hajawahi kushuhudia. Ikitokea watu hawa wakasikia risasi zikipigwa nje tu na eneo walilopo, yupi atakayesisimka sana? Jibu bila shaka ni yule aliye na historia na risasi. Hivyo hivyo, watu wa maeneo ya baridi kwa asili huwa na mihemko ya chini kutokana na usumbufu wa mazingira yao kuwa mdogo, hata anapokutana na usumbufu, huwa anatumia muda mrefu, na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuji control. Hii ndiyo ile niliyoiita ‘’low environmental-brain sensory potentials’’.
Msukumo Mdogo Wa Utandawazi na Teknolojia
Maeneo mengi sana ya nyanda za baridi
kusini, huwa na kiwango kidogo nyuma cha teknolojia na utandawazi ukilinganisha
na maeneo ya pwani chini. Sababu kubwa sio watu kuwa hawapendelei hatua hizi.
Bali ni wawekezaji wengi ambao huvutiwa zaidi na maeneo ya pwani, na miji ya
kati, ambayo, huwa na kiwango kikubwa sana cha watu, ambao kwa wao, huwa na
faida kubwa sana za kibiashara.
Tabia nyingi na mitindo mingi sana ya
usasa, haiendani na maeneo ya baridi kali sana. Hii ni sababu iliyojificha ya
sanaa na usanii ‘’Media’’’ nyingi sana kutawaliwa sana au zaidi, na watu wa
Marekani, na watu wa Afrika. Hii ni kwa kuwa, ni rahisi sana kwa binti kuvaa
nusu uchi katika mazingira ya joto, tena akiwa pwani ya Bahari, lakini sio
rahisi kwa binti huyu kufanya hivi akiwa njombe milimani. Mazingira ya baridi
huchochea sana matumizi ya misuli, na kujiandaa kujikinga na baridi, zaidi ya usanii wa kifua wazi
ukirekodi studio. Kumbuka pia, maeneo mengi ya baridi kali, huwa hayana
msongamano mkubwa wa watu, hii ni kwa kuwa, maeneo ya kujenga huwa yakitenganishwa
sana na mabonde na milima, hii hupunguza nguvu kubwa ya utandawazi kwa watu.
Uwezo Mkubwa Wa Kitaalamu Na Kitaaluma.
Hata baada ya wengi wa marafiki zangu
kutoka Denmark katika mafunzo yao ya ‘’Internship’’, wengi wao hukiri kuwa
mfumo wa Maisha katika miji ya baridi, huusisha watu walio serious sana na kazi
zao, kwa mara nyingi zaidi. Hivyo hivyo ndivyo ilivyopia hata katika miji yetu,
ni rahisi kukuta ‘’Vigoma vya Vigodoro vikipigwa hata kila siku kwa miji kama
ya Ifakara, Morogoro, pwani, Dar es salaam, n.k. miezi fulani’’ lakini sio
rahisi kukuta vigoma hivi kwa miji kama ya Mbeya, songwex, tunduma, Iringa, na
Njombe. Ni rahisi Ifakara kukuta wazee wakianza kucheza Draft saa 4 za asubuhi,
lakini huwezi kukuta jambo hilo Sumbawanga, au Iringa.
Miji mingi ya nyanda za juu zenye baridi,
huusisha watu ambao huwa wapo serious sana na kazi zao. Hii huwapa faida za
kuwa bora sana katika kazi zao, au taaluma zao. Ukifika nchi ya Tanzania na
ukawa ukipitia wanafunzi wa mikoa mingi sana ya nyanda za baridi, kuanzia
kaskazini, mpaka kusini. Na kisha ukaanza kupitia nyanda za chini kati, mpaka
pwani. Utagundua wanafunzi wengi wa nyanda za juu wakiwa serious sana na elimu,
huku wengi wa wanafunzi wa nyanda za kati mpaka pwani wakiwa ni vijana wa usasa
mwingi, na utandawazi.
Taaluma na Utaalamu huitaji sana
mazingira yaliyotulia sana. Huitaji usumbufu mdogo sana toka kwenye mazingira,
na toka kwenye jamii. Baridi huchochea uwezo mkubwa wa kukesha usiku kwa kazi,
na pia huchochea ufanyaji kazi kwa muda mrefu. Haya yote, huchochea katika
kuwafanya watu wengi wa maeneo ya baridi kuwa na ubora mkubwa sana. Lishe bora
ya mbogamboga na matunda ya asili, matumizi kidogo ya protini za Wanyama, na
uwezo mkubwa wa kimisuli na nishati, huchochea watu wengi wa maeneo ya baridi
kufanya vizuri zaidi katika taaluma, na kazi zao.
Maendeleo Makubwa
Miji mingi ya baridi hata leo, na hata
katika mabara ya mbali, huwa na maendeleo makubwa sana. Hii ni kwa kuwa, huwa
kuna maeneo makubwa bado yakiwa na nafasi ya watu kujenga, na kuwekeza. Miji
hii tokea zamani haikuwa na watu wengi, na hivyo bado huwa na maeneo makubwa
sana ya uwekezaji.
Miji ya pwani ambayo ilishajaa tokea
zamani, huwa na ushindani mkubwa sana wa kupata nafasi za uwekezaji. Vijana
wengi hukimbilia miji ya pwani kwa kuwa ni rahisi kupata kazi, na kupata fedha
za kukidhi mahitaji ya msingi. Lakini hata hivyo, miji ya pwani huwa haina
uwezo wa kumuwezesha kijana akakua kwa kiwango kikubwa sana kwa kuwa, huwa
haina nafasi, wala malighafi za kumtosheleza mtu mmoja tu hata akafika mbali
sana kiukuaji wa kiuchumi, na kijamii, tofauti na miji ya baridi, ambayo mingi
yake haina ushindani mkubwa, lakini changamoto yake kubwa katika uwekezaji ni
matumizi makubwa ya nguvu, na wakati
katika kuanza.

Join the conversation