MUZIKI WA KISASA UNAVYOUA UBONGO
Miongoni mwa taalumu ambazo zimekuwa
na utafiti mkubwa sana, ni juu ya sayansi ya muziki katika Ubongo. Hii taaluma
ni pana sana, hii ni kutokana na kuwa na sehemu kubwa mbili. ambazo zote,
zinahitaji utafiti mkubwa. Sehemu ya kwanza ni madhara ya muziki na sauti moja
kwa moja katika ubongo. lakini pili, ni namna ambavyo muziki unavyochakatwa, na
kuleta matokeo mbalimbali katika ubongo. Tukianza na sehemu ya kwanza,
tutaangalia nini hasa hutokea katika ubongo pale mtu anaposikiliza muziki.
Kabla hatujaendelea ni muhimu kwanza kutambua sehemu ya muziki katika ubongo.
Sehemu ya Muziki katika Ubongo.
Kama utafungua Ubongo kama inavyoonekana picha chini, basi kinachoonekana ndicho ‘’Auditory cortex’’, ambayo, imejipanga kwa frequency kama nota, ambazo ni mfano pia wa namna ambavyo huwa zikijipanga katika ‘’cochlea’’. Kwa Binadamu kwa kufatilia majina maalumu ya kila sehemu ya Ubongo, sehemu inayohusiana na Muziki, inapatikana upande wa pembeni wa Heschl’s gyrus na sehemu ya mbele pembeni ya A1 au ‘’primary auditory cortex’’. Kwa hiyo Muziki una eneo maalumu na sio tu kwa binadamu, bali kwa mammalia wengi kama vile nyani, mbwa, paka na wengineo
.
ENEO LA KUCHAMBUA LUGHA NA KUZALISHA SAUTI, YOTE YANACHANGAMANA NA UBONGO WA SAUTI
Haishangazi kuona eneo linalohusiana
na kutambua maana ya maneno ‘’language comprehenssion’’ ambalo huitwa
‘’wernicles area’’ liponyuma tu ya ‘’auditory cortex’’, lakini pia eneo
linalohusiana na kutoa sauti ‘’speech production’’ linaloitwa ‘’Broca’s area’’,
nalo lipo mbele tu ya ‘’Auditory cortex’’ .
Na kwa kutumia neurons zinazoitwa ‘’arcuate fibers’’, inawezekana kwa sehemu hizi za ubongo kuwasiliana moja na nyingine
PREDICTIVE CODING MODEL
Hii ni nadharia maarufu zaidi katika
sayansi za Ubongo, iliyoletwa na miongoni mwa wanasayansi wakubwa sana wa
Ubongo, ‘’Neuroscientist mwanamuziki Peter Vuust’’ na wenginewe ikiwemo ‘’Maria
A.G. Witek’’. Wanasayansi hawa waligundua kuwa, Ubongo una asili ya kukadiria
matukio yanayofuata kwa kila tendo linalofanyika. Nadharia hii siyo mpya katika
namna ya kimtazamo, maana tayari yalishakwepo masomo ya mfanano wake. Nadharia
hii imechochea namna bora zaidi ya kuelewa namna ubongo unavyochakata ‘’matendo
na mtazamo’’ kwa mfuatano au ‘’action-perception’’.
Nadharia hii rahisi sana kueleweka ina
maanisha hivi, mfano ukiwa unamwangalia mchezaji wa mpira anakimbia na mpira
huku akimwangalia kipa, ubongo hukadiria tayari matokeo ya kuwa atapiga
atakapofika sehemu Fulani. Ubongo siku zote hukadiria matokeo yatakayo fuata
hata kabla hayajatokea, kwa kutengeneza kielelezo cha matendo kipindi
yanatendeka. Hii ni sawa na ukiwa unaandika kwa kutumia smartphone yako maneno
kama haya ‘’I will come brother’’, kama utaandikia watu kadhaa sms hii, baada
ya muda, utakapoanza tu kuandika ‘’I…’’ basi yatakuja maneno chini ya ‘’will,
come, brother’’. Hizi ni algorithms za computer, namna zinavyojifunza, na
kuunda kumbukumbu au memory. Na ndivyo ilivyo pia kwa ubongo. Unapokuwa
unasikiliza muziki wa msanii Fulani ukiimba, ubongo huwa unatengeneza
kumbukumbu katika namna ya kielelezo au ‘’Model’’. Model hii hutengeneza namna
mabiti ya muziki yanavyoenda, yaani namna yanavyopiga na kuachiana muda, lakini
pia hutengeneza kielelezo cha namna ambavyo frequency za muziki zinavyopiga, hutengeneza
namna viwango vya sauti vinavyopishana ‘’Intensity’’ na hata nguvu ya midundo
ya sauti ‘’music tone’’. Kwa hiyo hebu chukulia taswira ukiwa unaimba huu
wimbo.
‘’TanzaniaTanzania ,Nakupenda kwa Moyo wote’’ ‘’Nchi yangu Tanzania ,????………………………………... ‘’
Hata kama mtu atakuwa hajui mstari au ‘’verse’’ ya mwisho katika mstari wa chini wa huu wimbo, tayari atakuwa ana uwezo wa kukadiria namna ya mabiti yatakavyokuwa katika mstari huo. Hiko kinacho muwezesha mtu kuweza kukadiria namna ambavyo muziki utakuwa katika verse hii, ndiyo ‘’Model’’ ambayo Ubongo huwa unaitengeneza popote pale unapokuwa ukiusikiliza muziki. Kila muziki unapokuwa ukiusikiliza, huwa unatengeneza model ya aina yake, na kutokana na hii model, ndipo tunapopata majibu yote ya msingi kuhusu tabia ya muziki na fiziolojia za utendaji wa ubongo.
Picha hii ni kielelezo kikubwa zaidi cha hii ‘’predictive coding’’. Katika hiki kielelezo, miongoni mwa vitu ambavyo ni vya muhimu ni hisabati zinazoitwa ‘’Bayesian inference’’. Hizi ni hesabu ambazo, kwa huku hutumika kama kielelezo cha namna ambavyo, Ubongo kuchukua wastani wa mapigo ya muziki ambayo, yana msukumo mkubwa zaidi katika kujenga kielelezo chake. hii ni sawa na kusema, sio kila biti hutumika kama kielelezo. Lakini pia katika usikivu huu. huwa kuna upendeleo au ‘’bias’’ ambayo, hutokana na asili ya nje ya mtu, kama vile jamii, tamaduni, nini mtu husikiliza mara nyingi zaidi n.k, hii ndiyo ile huitwa hamasa ya chini kuelekea juu ‘’down-top effect’’, lakini pia kuna ile namna mtu huvutiwa zaidi kusikiliza kutokana na biolojia yake mwenyewe, au mapenzi binafsi ya mtu na huitwa ‘’top-down’’. Kwa upande mwingine kielelezo hiki ni sawa na uangalie picha zifuatazo chini.
Picha hizi mbili ni sawa kabisa,
lakini mtu atakapo angalia picha ya kushoto, ataona kana kama ni vyakula
vilivyomo ndani ya beseni ‘’hii ni kutokana na uwepo wa model nyingi za
mwonekano huu katika ubongo zikifanania beseni na vyakula’’ lakini picha ya kulia
wengi wataona mwonekano wa mtu aliyejifunika kofia inayofanania na beseni, na
tena akiwa na madevu mengi’’ hii nayo haitokani na uhalisia wa picha hii,
inatokana tu na model za mionekano ya watu wenye taswira hizo, waliowahi
kuonekana na kutunzwa kumbukumbu kwa mionekano yao.
Hii ndiyo namna pia Ubongo siku zote unapokuwa ukisikiliza muziki, huutengeneza model ambayo ndiyo huwa kielelezo cha kukadiria namna ambavyo muziki utakuwa ukipiga.
SYNCOPATION
Hii ni namna ambavyo, kunatokea makosa katika Ubongo katika namna ambavyo ulikadiria mabiti au muziki utakavyokuwa, na ulivyokuwa baada ya kuifikia sehemu ya muziki kipindi cha usikilizaji. Mfano, hebu tafakari muziki Fulani ukiwa unapiga kwa namna Fulani ya mabiti, na kisha baada ya muda Fulani ukabadilika kwa namna Fulani, na ukawa unapiga kwa namna ya utofauti na awali. Au chukulia mfano kipindi ukiwa unasikiliza nyimbo iliyokuwa ikipiga kwa muundo Fulani, na wasanii wakifatiana na mabiti Fulani, halafu ghafla msanii mwingine akaingia kwa biti la aina ya kipekee, au verse za aina ya kitofauti na awali. Hapa kinachotokea ndicho kinachoitwa ‘’syncopation’’. Haya makosa huwa yanaitwa ‘’prediction error’’. Yaani hapa kinachotokea ni badiliko la muziki tofauti na ubongo ulivyotegemea.
SYNCOPATION KATIKA MUZIKI
Hili ndilo wazo la muziki ambalo utalipata kwa kusikiliza tu ‘’verse’’ ya kwanza. Kwa mfano, katika shairi la wimbo wa Tanzania
‘’Tanzania Tanzania ,Nakupenda kwa moyo wote’’ ‘’Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana’’
katika verse ya kwanza kabisa, huo mtiririko wa sauti ndiyo ‘’melody’’ nzima ya wimbo huu. Mtu anaposikiliza muziki wowote ule, huwa anatafuta kwanza kiini cha sauti za muziki, na hiko ndicho melody, hiko ndiko huunda msingi au ‘’framework’’ ya muziki wote mpaka unapoisha. Hili ni eneo la kwanza kabisa, ambapo mtu anaweza kulibadilisha kwa kiwango Fulani, na kupelekea ‘’prediction errors’’ au syncopation. ambazo kwa kiasi cha kawaida sana, zinaweza kuleta msisimko, lakini mara nyingi sehemu hii, huwa haibadilishwi sana na hivyo kutokuwa msingi sana wa usisimuaji.
Hivi ni vichocheo vya Ladha ya muziki.
Hivi huongezwa katika melody ya muziki. Katika muziki unaweza pata mamia ya
vichombwezo. hasa katika miziki ya kizazi kipya. Harmony katika muziki zinaweza
kuwa katika namna ya mabiti sindikizi ya muziki, au zinaweza kuwa sauti za
mapigo yanayopiga kama ‘’background beats’’, sauti za vinanda, midundo ya ngoma
n.k.
Harmony sio msingo wa melody ya
muziki. lakini huiongezea Ladha, na kwa mantiki hii sasa, mtu angeweza kuweka
harmony katika hatua yeyote ile ya muziki. na kwasababu hiyo, akapelekea kuwepo
kwa ‘’prediction errors’’, au syncopation, ambazo, miongoni mwa matokeo yake ni
msisimko na kuhisi Ladha ya muziki
Hii ni namna ambayo vina vya muziki,
vinakuwa na sauti zinazofanania kimapigo, kwa kila baada ya vituo. Hizi rhythms
unaweza ziona kupitia maneno katika muziki, au kupitia mabiti ya muziki. Hapa
unaweza tengeneza ‘’syncopation’’ kwa kubadilisha mfuatano huu kwa kiwango
Fulani.
Rhythms katika Ubongo, zina matokeo
makubwa sana. kwa sababu, mwili wa binadamu pia una utendaji ulio katika muundo
wa ‘’rhythms’’ mfano, mapigo ya moyo huwa yana rhythms, uhemaji una mapigo
katika kutoa hewa nje na kuingiza ndani, mapigo ya mfumo wa umeng’enyaji (
tumbo, utumbo na mfumo wote huwa una mfululizo wa mapigo ambayo ni matokeo ya
kujikunja na kujilegeza ili kukisogeza chakula mbele zaidi), pia Ubongo una
mawimbi ya aina mbalimbali. Kwa ujumla mawimbi yaliyo katika mfanano wa sauti
za muziki ‘’rhythms’’ yana ambatana sana na utendaji mzima wa fiziolojia ya
mwili.
Makosa haya huwa katika ngazi
mbalimbali. kuanzia katika makosa makubwa sana ‘’high prediction error’’ kama
pale ambapo biti lina badilika kabisa au halieleweki, kuna makosa ya kati
‘’moderate prediction error’’ kama pale
ambapo Producer anaongezea mbwembwe,
kwenye melody za muziki. au DJ au MC au msanii anaweka vichochea, na kubadilika
badilika katika staili za uimbaji. pia kuna makosa ya chini kabisa ‘’low
prediction error’’ kama pale ambapo wimbo unakuwa hauna mabadiliko badiliko
mengi katika uimbwaji wake, au muziki wake.
Ubongo hufurahia sana syncopation.
huwa ukiongeza msisimko wake wa furaha kuanzia makosa kidogo, na kuwa na
msisimko mkubwa sana kwa makosa ya kati ‘’moderate prediction error’’. msisimko
wa Ubongo huwa mdogo mpaka kuisha kabisa kwa makosa makubwa kabisa ‘’high
prediction error’’.wanasayansi wengi wa Ubongo wamejaribu kutafuta sababu za
msingi zinazopelekea Ubongo kusisimka zaidi, kwa makosa haya ‘’prediction
errors’’. lakini mtazamo pekee unaotambulika mpaka sasa kwa wanasayansi wa
Ubongo, ni kuwa ‘’Ubongo huongeza msisimko wake siku zote kunapokuwa na makosa,
kwa sababu ya kujifunza zaidi’’
Hii ni sawa na kusema ‘’unapokosea,
ubongo huongeza msisimko wake kwa lengo kuu moja la kukuhamasisha, ili uwe
makini na ujifunze zaidi’’, Ubongo siku zote hupenda kujifunza vitu vipya.
Ubongo haupendelei kurudia rudia taarifa zinazofahamika, na hii ndiyo sababu
yake ya kutovutiwa sana na mapigo ya muziki yasiyobadilika badilika ‘’very low
prediction error’’. Jibu hili ijapokuwa linatokana na mtazamo unaoaminika zaidi
wa kisaikolojia, lakini unaungana na nadharia yangu kubwa zaidi niliyoielezea
katika kitabu changu cha injili ya sayansi sehemu ya pili, ambapo nilielezea
kuwa, Ulimwengu huwa na asili ya kuvutwa kuelekea kwenye utofauti, ambako ndiko
kwenye msingi wa thamani za upendo’’.
Ubongo huzalisha homoni za Dopamine za msisimko kwa wingi sana, pale kunapokuwa na ‘’syncopation’’, na misimko hii huanzia ndani kabisa ya ubongo, katika mfumo unaoitwa ‘’mesolimbic dopaminergic system’’ mfumo huu ndio msingi wa hisia za msisimko kwa muziki, lakini hasa kwa kusisimua kwa mfumo mwingine unaozalisha hisia za raha katika ubongo ‘’endogenous opioid system’’, ambao, huzalisha kemikali za raha pale mtu anaposikiliza muziki. kinachotokea ni namna ambavyo, mtu anapokuwa akitegemea biti liende kwa namna Fulani, kama litabadilika kiaina Fulani hivi, basi mtu huyo ubongo wake utasisimka kwa kuzalisha kiwango kikubwa cha homoni ya dopamine. Mfumo huu wa dopamine unahusiana na mfumo mzima wa hisia ‘’limbic system’’, na hii ndiyo sababu ya mtu kusisimka kwa kusikiliza mabiti haya.
Haya ni maneno yanayofahamika sana kwa
kila muimbaji, kama yatatafsiriwa kwa Kiswahili kama ‘’rhythm’’ kumaanisha
‘’kujirudia rudia kwa sauti za kumuziki’’, nyimbo isipokuwa na ‘’rhythm’’ maana
yake haina vituo vinavyofanana kwa mtiririko wa sauti ‘’vocal sounds’’ na kwa
upande wa ‘’meter’’, hapa tunazungumzia mgawanyo wa kipindi cha muda kwa kila
mfuatano wa ‘’rhythms’’ Fulani.
Hivi ni vitu vya msingi kabisa,
ambavyo, Ubongo huvizingatia pale unapokuwa ukisikiliza muziki. Inapotokea kuna
badiliko katika mifuatano hii, hiyo ndiyo hasa sababu ya ‘’syncopation’’ .
Hii ndiyo Ladha ya muziki ambayo mtu
anaihisi anapokuwa akisikiliza muziki. Groove inahusisha mfano matokeo ya
kisaikolojia yanayotokana na usikilizaji wa miziki kama ya hip hop au funk na
mingineyo ambayo huwa na ‘’rhythm’’ ngumu sana ‘’complex’’ ambazo hupelekea
hisia za misisimko ‘’pleasurable drives’’ ya miondoko. kama kucheza, au
kurukaruka, au kukimbia ‘’Urge to Move’’
ambapo hisia hizi huwa ni matokeo ya mapigo yake.
Matokeo haya huwa yanahitaji midundo
ya kiufundi sana katika kutengeneza rhythms, au Ladha za vina vya muziki.
‘’rhythmical complexity’’. Ladha hizi katika miziki mingi ya namna hii
husababishwa pia na kubadilika kabisa kwa midundo ya kivina ‘’cross rhythms’’
mfano ni namna ambavyo unaweza kuta ‘’Msanii akirap au akiimba kwa spidi kubwa
sana, na kisha biti likabadilika kwa muda,
na baada ya muda biti linajirudia lile kama la awali, na msanii
anabadilisha staili tena’’, hizi ndizo ‘’cross rhythms’’ ambazo ukichanganya na kitu kitu kingine, katika
ubongo kinachoitwa ‘’Microtiming’’, ambayo ina maanisha tofauti ndogo ndogo,
zilizojaa katika mapigo ya kimuziki, ambayo muda wote yanakuwa yakipelekea
‘’prediction errors’’ ambazo kwa ujumla wake wote, basi hupelekea kiwango
kikubwa sana cha msisimko.
POLYRHYTHMS
Kwa miziki kama ya Jazz, na mingineyo unaweza ona sifa ya uwepo wa ‘’Rhythms’’ nyingi sana, kiasi kwamba ikawa ni vigumu hata kwa msikilizaji kugundua ule mfuatano wa vina, kwa kila baada ya muda ambao unaitwa ‘’meter’’. Polyrhythms hufanya Ubongo wa msikilizaji muda wote kutabiri lipi linaweza kuwa biti la muziki baada ya muda Fulani, maana hakuna ‘’meter’’. Hapa pia huusisha zile ‘’cross- rhythms’’ ambapo, kuna kuwa na ‘’rhythms’’ mbalimbali ambazo, zinakuwa zikipigwa kwa Pamoja au kwa vituo na kuacha Ubongo ukiwa unasikilizia kuwa nini inaweza kuwa ‘’rhythm’’ ya muziki baada ya kipindi Fulani.
Zipo meter mbili za kutambua hizi ‘’polyrhythms’’.
katika namna hii kuna kuwa na mapigo yanayoenda na midundo inayoachana (time signatures) kwa ¾, ambapo Hapa ni sawa na upige ubao mara tatu katika mkono wako mmoja, kwa wakati huo huo uwe unapiga ubao mwingine mara nne, kwa mkono mwingine. Na mapigo haya kipindi yanapigwa, yawepo mengine yanayoenda na mtindo (time signature) ya 4/4, haya yawe yanapiga kama muitikio wa yale ya ¾, haya ya 4/4 kwa hapa yanaitwa ‘’counter metric pattern’’
Duple meter. Hapa inakuwa ni kunyume na kwenye ‘’triple meter’’, hapa mapigo ya 4/4 yanakuwa yakipiga kama sauti kuu, na yakiitikiwa na yale ya ¾ ambapo hapa, ndiyo yenyewe yanaitwa ‘’counter metric pattern’’. Inafahamika kuwa duple ndiyo mtindo wa muziki unaopigwa sana, na wasanii wa aina nyingi sana. Wengine huisi ni kutokana na kuwa, ni mapigo pendwa zaidi kwa miziki ya magharibi za ulaya na marekani.
Upigaji wa mabiti haya kwa Pamoja, hupelekea pia muda mwingine mtu kuhama katika ile namna anavyouhisi muziki, kutokana na Ubongo kuhama katika midundo hii, kipindi cha kusikiliza.
MUZIKI NA HISIA ZA KUSOGEA, TEMBEA AU CHEZA
‘’URGE TO MOVE’’
Miziki mingi huamsha hisia hizi za
kutaka kutumia misuli, unaweza ona namna baadhi ya mabiti yanavyosisimua
kucheza, na huku mengine yakitoa morali ya kukimbia. lakini pia kuna mabiti
ambayo husisimua hata kutingisha kichwa, au mikono. au miguu, au vidole. Yote
hii huitwa kama ‘’urge to move’’. Hali
hizi zote zinatokana na sababu moja kubwa ya kuwa, sehemu zinazochakata muziki
katika ubongo, zinahusiana na sehemu zinazochakata miondoko. Tuliona kuwa
sehemu zinazochakata sauti, zipo kwa wingi sana katika ubongo, na katika uwingi
ule, kwa sehemu kubwa sana, huusiana na sehemu ya miondoko ‘’motor cortex’’.
Kuna channel ya msisimko wa miondoko
katika Ubongo, inayoitwa ‘’Nigrostriatal dopaminergic pathway’’, hii channel
inafahamika kwa kuchakata taarifa za midundo ‘’meter’’ Pamoja na vipindi vya
midundo ‘’timing’’. Na hii huwa na Ushahidi mkubwa sana kwa wagonjwa wa
‘’Parkison’s disease’’, watu hawa huwa na shida katika channel hii ya
‘’dopamine nigrostriate pathway’’. na hatimaye, huwa na shida ya kutembea,
lakini pia, hushindwa kutofautisha ‘’rhythms’’ mbalimbali za miziki.
Yapo maswali mengi sana yanayohusiana
na nini hasa, ni sababu ya kufanya muziki, uweze kuhamasisha hizi hisia za
kutembea, au kurukaruka, au hata kucheza, na kukimbia. Lakini yote yana logic
kadhaa zinazofanana kama vile,
Hii ni ile hali ya vitu
kujirudiarudia, hapa utaona kwa mfano, mtu anapoimba nyimbo au anapokuwa
akisikiliza nyimbo. nyimbo inavipengele vya kujirudia rudia kama ‘’rhythms’’
lakini pia matendo ya kutembea au kukimbia pia yanasifa ya kujirudia rudia,
hebu chukulia mfano, unapotembea unarudia rudia hatua zako, na hata mikono yako
inarudia rudia miondoko yake, kwa hivyo, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya
muziki na miondoko. kwa kuwa, yote ina tabia ya kujirudia rudia. Ukiangalia mtu
anayecheza pia hurudia rudia steps zake, kama ilivyo pia kwa mabiti
yanavyojirudia. Kwa hapa hakuna jibu la moja kumpelekea mwingine, lakini
unaweza ona namna ambavyo moja, linaweza kumhamasisha mwingine kwa namna
wanafanana.
KUCHEZA ILI KUONGEZA ATTENTION
Nyimbo nyingi zinazosisimua sana
kucheza. ni nyimbo zenye mabiti mengi ‘’polyrithms’’, huku kwetu Tanzania kwa
kusikiliza nyimbo kama ya Singeli, mtu anaweza akaanza kucheza.
Sababu kubwa huwa ni uwingi wa mabiti
yake, ambayo huufanya Ubongo kutafuta ni nini hasa ndilo biti kuu ‘’accent
meter’’. na katika namna hii, Ubongo hutumia viungo vyake ili kulifatisha biti
Fulani kwa umakini sana, bila kulipoteza, kwa kulifuata kimapigo. Ambapo,
huonekana mithili ya mtu akitikisa kichwa au mguu (hii ni kulifuatisha biti
kuu), hapa Ubongo hutumia viungo ili kuongeza ‘’attention’’ yake kwa biti kuu,
usilipoteze kwa uwepo wa mabiti mengi. Na hii ni sababu ya moja kwa moja ya
namna ambavyo, muziki ungeweza kusababisha muondoko Fulani wa kiungo, kwa lengo
la kulitambua kiundani kabisa. Zipo sababu nyingi za kucheza hii ni mojawapo
tu.
Huwa kuna tabia ya Ubongo ya
kujiungamanisha na kufuatisha mapigo ya sauti Fulani, na mapigo yake binafsi.
Hili hudhihirishwa zaidi kwa namna ambavyo mtu anayekimbia, angependezwa na
mabiti ya namna Fulani tu. Kiufupi mtu anaposikiliza mabiti, na namna Fulani,
hupelekea Ubongo wake kuanza kuendana na mabiti hayo, kitu ambacho huitwa
‘’entrainment’’. Sababu hii hutumika kuelezea kuwa, mapigo haya ndiyo mwanzo wa
kuhamasisha miondoko. Ambayo, huchangiwa na mawimbi ya mapigo haya.
Lakini kwa upande wa ‘’embodiement’’, hufahamika kuwa, kadri mtu anavyosikiliza muziki, basi yale mawimbi hupelekea mabadiliko ya kifiziolojia, ya kuendana na ule muziki, kwa lengo moja. Ambalo, ni kuufanya ubongo uweze kuuelewa muziki kwa kina kabisa, kumbuka kuwa, lengo la ubongo tokea awali, lilikuwa ni kuelewa na kutabiri kila kitu katika muziki.
JE WAJUA SABABU YA KUKINAI MUZIKI!!
Baada ya kusikiliza sana muziki
Fulani, ubongo hupunguza kuvutiwa sana na huo muziki. Na sababu kubwa hasa
huwa ni kuwa, umeshatambua kwa kina
model ya muziki husika, na hivyo basi kuwa na kiwango kidogo sana cha ‘’prediction
errors’’, na hata kwa wale wanaosikiliza nyimbo za zamani au zenye hisia,
huvutiwa zaidi na kumbukumbu za hisia zilizohusiana na hizo nyimbo, kuliko hata
‘’prediction errors’’ zinazotokana na hizo nyimbo.
DYNAMIC ATTENDING THEORY ‘’DAT’’
Hii huelezea kuwa, kwa namna ambavyo Ubongo huchakata kazi zake katika namna ambayo huwa ya kimabadadiliko badiliko kwa kila muda, basi huendana sana na muziki ambao, nao huwa ukibadilika badilika kwa kila baada ya muda Fulani. Nadharia hii huusiana pia na utendaji mzima wa mfumo wa ‘’prediction coding’’.
JE WAJUA!!
Ubongo
hupunguza nishati, ndiyo maana watu hawapendi kazi, na wanapenda kula. Nishati
hupunguza Ubongo, ndiyo maana Pesa nyingi huleta maamuzi dhaifu. Nishati
hupunguza muda, ndiyo maana Nguvu nyingi, humaliza kazi ndani ya muda mfupi
sana. Muda mwingi, hupunguza nishati, ndiyo maana, ukiongeza muda sana, nguvu
chache tu yaweza kutumika. Muda hupunguza Ubongo, ndiyo maana, watu hawapendi
kusubiria sana, au kuchelewa. Na mwisho, Ubongo hupunguza muda, ndiyo maana,
watu hupenda kutumia mashine kufanya kazi kwa muda mfupi. Muziki, marazote
Hublock uchakataji wa muda katika ubongo, na hivyo nishati kubwa sana huweza
kutumika bila mtu kutambua. Hii humpatia faida mtendaji kufanya kazi kubwa
zaidi kwa kutumia muziki bila kuchoka.
Kutokana na
uhusiano mkubwa wa channel za miondoko ‘’motor pathways, prefrontal cortex,
Orbitalfrontal cortex, basal ganglia, nigrostriatal dopaminergic tracts na
channel za kusikia na miziki’’. Sehemu hizi huusiana na utambuzi wa muda
.unaweza rejea tafiti za (DANIELSEN,A.,HAUGEN,M.R.,&JENSENIUS, A. R.2015.
Timing and Time Perception, 3, 133–154).
Utambuzi wa
muda hutawala ‘’regulate’’ matumizi ya
nishati katika ubongo (ubongo huwa ukipunguza matumizi ya nishati yake kwa
kutengeneza hisia ya kuwa muda umeenda sana)
Ubongo
hupima muda kama kipimo cha kazi (ukiwa unafanya kazi ngumu, ni rahisi kuhisi
umetumia muda mwingi sana, ubongo hufanya hivyo kwa lengo la kuzuia matumizi
makubwa ya nishati). Mtu anaposikiliza muziki akiwa anafanya shughuli,
uchakataji wa muziki huusiana na misisimko mikubwa sana ambayo hufunika
‘’mask’’ hisia za muda kutokana na namna channel za shughuli za miondoko ya
misuli huchangamana na channel za
misisimko ya miziki. (muziki hupeleka uwezo
mdogo wa ubongo kutambua muda kwa kipindi cha kuusikiliza).
Ubongo
ungetumia kemikali zake ‘’inhibitory neurotransmitters’’ kwa lengo la
kudidimiza hisia za kazi kwa kutengeneza hisia za uchovu ili kutunza nishati,
lakini muziki huchangamsha mfumo mzima wa miondoko mpaka na kuzalisha
‘’norepinephrines’’ kemikali zinazohusiana na kuchangamka. Na matokeo yake huwa
ni mtu kufanya kazi kubwa bila kuchoka. Ijapokuwa wapo wanasayansi baadhi
waliokwisha husianisha uchakataji huu wa muda, lakini nadharia ya shoo imeweza
kuelezea kwa uhusiano rahisi zaidi na wa moja kwa moja.
Mfano,
unapomsubiria mtu halafu huyo mtu anachelewa. Ni rahisi kuhisi kuwa umetumia
muda mwingi sana katika kumsubiria huyo mtu, Hata kama itakuwa ni tofauti ya
muda mdogo sana. Hii ni kwa kuwa, unapomsubiria mtu, unapunguza matumizi ya
misuli iliyokwisha chochewa kwa kazi ‘’hii ni kama kupiga breki kwa gari
linalotembea’’, unapunguza nguvu ya motisha katika ubongo ‘’nigrostriatal
dopaminergic system’’, matendo haya yanatumia nishati kubwa sana ya ubongo, na
hivyo ubongo unachochea hisia ya kuhisi umetumia muda mwingi sana, ili
kupambana na upotezaji wa nishati na motisha zaidi katika ubongo.
UTAFITI WA
SHOO: BONDE LA AFRIKA LA KATI KUELEKEA KUSINI NA KUSTAWI KWA MIZIKI YA KUCHEZA
NADHARIA Katika historia ya muziki inatambulika kuwa muziki wa kucheza wa kizazi kipya ulianza sehemu mbalimbali lakini hasa ilikuwa ni marekani. kwa kuchochewa na waafrika waliokwenda marekani kipindi cha biashara ya Utumwa. Hakuna msomi wa historia za muziki asiyetambua muziki wa ‘VOODOO’’ kama ndiyo chanzo cha miziki yote ya kisasa iliyoanzia marekani, kwa kupitia hatua mbalimbali kama kipindi cha zama za ‘’The Blues’’ , Rock n’ Roll ‘’The Beetles’’ na wengine wengi wanaoweza rejewa kwenye historia’’. Muziki wa Afrika wa Voodoo ambao ndio msingi wa miziki ya ‘’Polyrythms’’ ya kucheza ambayo ilianza Afrika na sehemu baadhi kwenye ibada za kipagani, ulipitia zama mbalimbali za mabadilisho mpaka ukawa bora kwa masikio kama mziki wa leo wa kizazi kipya wa Marekani na sehemu nyingine nyingi duniani. Ukweli huu unarejea tena kwenye udhihirisho wake kwa namna muziki wa Afrika upo juu sana kwa midundo ya kucheza. Hii ni kusema tu kuwa Muziki wa kucheza umeshamiri sana Afrika ukilinganisha na sehemu zingine. Afrika ni kitovu cha ‘’Polyrhthmic musics’’.
KISIO LA SHOO ‘’HYPOTHESIS’'
Kadri mtu anavyosikiliza zaidi muziki ndivyo ubongo wake unavyoendelea zaidi katika uwezo wa kuuchakata huo muziki ‘’neuroplasticity from continuous musical hearing’’.(Eric kandel, Principles of neural science, Pg 669). Kadri mtu anavyotembea sana na kutumia sana misuli, ndivyo sehemu za Ubongo wake za miondoko zinavyoendelea sana, hii nayo ni kwa msingi uleule wa ‘’cortical plasticity’’. kila jamii hutumia zaidi miziki katika miondoko yake ili kupunguza gharama ya matumizi ya nishati kama nilivyoeleza katika ‘’shoo masking theory’’. watembeaji wa umbali mrefu huwa bora zaidi katika mifumo hii miwili. Hii ni kama ilivyo ile hoja ya ‘’mimesis’’, matumizi makubwa ya ‘’rhythms’’, huambatana na ufanisi mkubwa zaidi wa utembeaji, Pamoja na uwezo mkubwa wa uimbaji wa miziki ya miondoko.
USHAHIDI1.
Kitabu kikubwa zaidi cha sayansi ‘’Biblia’’ kinaonesha asili ya Waafrika ni Watoto wa Ham, au ‘’Hamites’’ ambao walitoka maeneo ya kati ya Dunia ‘’Middle east’’ na kushuka katika bonde la bara la Afrika, hivyo maeneo yote ya kusini yanahusisha watu waliotembea umbali mrefu zaidi katika historia ya dunia, na hivyo tutegemee wakiwa na sifa nyingi za kimiondoko na muziki.
USHAHIDI2.
Maeneo mengi ya Afrika ya kati kuelekea kusini, yanahusisha watu wenye sifa kubwa za miondoko. Mfano, uwezo wa kukimbia na namna za kufanania za kutumia misuli ‘’Athletic characters’’ ukilinganisha na sehemu zingine. Sifa hizi zinatabiri uwezo wao wa kimuziki wa mtindo wa miondoko na kucheza kutokana na uhusiano wa moja kwa moja kati ya mifumo hii miwili.
USHAHIDI’’3
Watu wengi
wenye miili mikubwa zaidi duniani kwa historia ya kipindi Fulani cha hapo
awali, walikuwepo maeneo ya Afrika. Nikirejelea ripoti maarufu ya wanasayansi
‘’Bergmann na Allen’’ hawa walionyesha ukubwa huu wa Afrika ulitokana na faida
za kibiolojia za kuwawezesha kupoteza joto kirahisi mwilini, kutokana na uwepo
wao katika nyanda za Equator zenye Joto kubwa sana. tazama mfano ukubwa wa
makabila kama ya wabantu, Nilotics kama Maasai, wanubi, n.k. Pia Afrika
ilihusisha makabila mengi sana ya wawindaji, kulikuwa na vyakula vingi sana Afrika,
na hata maendeleo ya magonjwa mengi, na madhara ya usasa mwingi, yalichelewa
sana kuwadhoofisha watu wa Afrika.
Hoja ni
kuwa, kadri Mwili unavyokuwa mkubwa, mapafu makubwa, uwezo mkubwa wa misuli ya kupumua, haya yote
huongeza uwezo mkubwa sana wa Uimbaji. Tazama mfano, Sololist wakubwa zaidi
huwa ni watu wanene, au wenye miili mikubwa kwa wastani. Hii ni hoja
inayochangia ubora wa Afrika katika muziki ulikuwa na sababu nyingi sana.
USHAHIDI’’4
Utazamaji
wa filamu za kutisha, huambatana na matumizi ya mabiti ya muziki ya kutisha.
Mabiti haya, huwa na msingi mmoja mkubwa ambao msikilizaji anapoyasikiliza tu,
hujua kuna tatizo linaenda kutokea, mfano, Jini, zombie, n.k. mabiti haya huwa
yanaongeza Frequency zake mpaka kufikia ya juu sana ndani ya muda mfupi sana,
tena huongeza kwa kasi na yakishafika juu kabisa, huwa kama yakistop kwa
ghafla, kutengeneza ‘’big prediction error’’, na tena, hii ambayo unaweza iita
‘’exponential frequency increase’’, hufanana na mabadiliko ya asili ya
frequency kitu kinapoenda kupasuka. Vuta taswira, mti unavyoanguka mpaka
unapopiga chini kwa kishindo, huanza na sauti kwa ghafla inayoongezeka, na
kisha hufikia juu kabisa ‘’maximum’’, na hustop. Mtu anapokimbilia kitu ili
akikamate, anapoelekea kukikamata, Huongeza matumizi ya misuli mpaka mwisho, na
anapokishika, hushuka ghafla. Anayekimbia ili apige mpira, au arushe jiwe wote
hufata hizi namna. Hii inathibitisha, Muziki katika kiini chake, una utendaji
sawa na mahesabu ya makadirio ya nishati, na muda katika ubongo.
TEGEMEO‘’PREDICTION’’1
Ikipimwa
watu wa maeneo ya mabonde ya kati kuelekea mpaka kusini mwa Afrika , watakutwa
kwa wastani wakiwa na sehemu za ubongo za kuchakata muziki zilizoendeleaa zaidi
(kama eneo la ubongo linaloitwa Broadman
area ‘’BA’’47 na “BA’’40 na mengineyo). Na wakipimwa watu wa maeneo
mengine wataonekana na maendeleo kidogo chini.
TEGEMEO‘’PREDICTION’’2
Ikipimwa uwezo wa utambuzi wa muda katika ubongo
kwa watu wanao kimbia wakiwa wanasikiliza muziki na wanaokimbia bila kusikiliza
muziki, itaonekana kwa kadri mtu atakavyokuwa akivutiwa na muziki, basi uwezo
wake wa utambuzi wa muda ukipingua na ukiongezeka kwa yule asiyesikiliza
muziki.
LENGO LA NADHARIA
Ni kuonesha kuwa Muziki una sifa ya kuathiri uwezo wa utambuzi wa muda na nishati kama ambavyo pia wanasayansi wakubwa zaidi wa ubongo na muziki ‘’Katarina Jerotic, Peter Vuust na Mortem L. kringlbach’’ walivyoonesha katika jarida lao lililokuwa likielezea namna ambavyo muziki huwa na matokeo sawa na ya dawa za kulevya ‘’interplay of music and psychedelics’’. nadharia ya shoo, inatengeneza njia ya kuelewa zaidi uhusiano wa muziki,muda, nishati na kucheza. Inatoa sababu ya Ubongo kupenda kucheza kama namna ya kujilevya kutokana na sifa yake ya kuchukia matumizi ya nishati.
Hakuna mfumo wa mlango wa fahamu
uliojitawanya Sana katika Ubongo Kama mfumo wa kusikia. Channel za mfumo wa
kusikia zimejichimbia zaidi ya mifumo yote mingine ya fahamu, katika ubongo.
(Tumeona channel hizi katika Fiziolojia ya kusikia, tokea katika Ubongo wa
medulla oblangata, pons, midbrain, cerebellum, basal ganglia, limbic system,
auditory cortex na cerebral cortex). sehemu ya kusikia ina uhusiano na mfumo
mzima wa lugha, ambao unachakata pia taarifa kutoka sehemu zote za ubongo. Pia
sehemu ya Ubongo wa kusikia, ina uhusiano wa moja kwa moja na kuona, mtu
anaposikia, hugeuka Mara moja, ukimsimulia mtu kwa mfano." Kuna jumba
kubwa kwekikweli!! , Atakapo sikia tu, atatengeneza taswira. Yaani masikio Yana
uhusiano mkubwa Sana na mfumo mzima wa fahamu, lakini pia mfumo wa kusikia,
unahusiana moja kwa moja na mfumo wa hisia, mfano unaposikia mtu akikutukana,
Hasira huja Mara moja. Mtu anaposifiwa, husikia na Mara moja hujisikia Raha.
Lakini hata hivyo Mfumo wa kusikia unasifa moja kubwa sana.
SIFA KUU YA MFUMO WA KUSIKIA
Huu Ni mfumo ambao huruhusu zaidi
Kufikiria. Msingi mkubwa zaidi wa kufikiria umejikita katika kusikia. Mara
nyingi watu huwa hawafikirii vitu wanavyoviona. Ukimwona rafiki yako akipigwa
risasi, utaamini na kuumia Mara moja. Ukiambiwa rafiki yako amepigwa risasi,
utafikiria!! Je Ni kweli? kwanini? wapi? n.k, lakini hata Kama rafiki yako
angepigwa risasi kipindi unamuona, Kama ungetaka kujua zaidi, ungepaswa kuuliza
na kusikiliza!! Ili ujue sababu. Watu wengi hawajui kuwa mtu akiwa anasoma
vitabu, huwa anasikiliza!! Unaposoma mfano, "hapo mwanzo kulikuwepo na
neno!!, Hapo mtu anasoma kwa macho, lakini hasa anasikiliza simulizi
iliyoandikwa. na hata namna ambavyo mtu anachakata taarifa hizi, huwa Kama mtu
anayesimuliwa na sio anayeona. Hii ndiyo sababu pia sikuhizi Kuna "audio
books", vitabu unavyosoma kwa kusikiliza, havina tofauti na unavyosoma kwa
kuangalia. Sasa Basi, kwanini vitabu na masimulizi? Huwezi kufikiria Kama hauna
vya kuvifikiria!! Kufikiria Ni kukusanya taarifa zilizopo, na kujenga maana au
hoja. Watu wanaofikiria Sana, huonekana kuwa na akili Sana
"intelligent", Einstein anafahamika kwa kufikiria Sana, je angeweza
kufikiria Sana bila kusoma Sana, " au kusikiliza zaidi", ndiyo maana huwa Wana msemo unaosema toka
enzi ya Newton, "reaching far, by standing on shoulders of Giants",
yaani Kama unataka kufika mbali, Basi Ni kwa kusimama juu ya mabega ya wakubwa,
ambayo hiyo Ina maana, unahitaji kuwasoma zaidi waliopita. Biblia pia
inathibitisha hoja hii, Danieli anasema "nimejua mengi kwa kusoma Sana", neno akili au "intelligence"
linahusisha maneno mawili "inter - na legal", yaani akili Ni
kulinganisha, taarifa zilizokwisha kuwepo, maana yake uwe umekwisha zisikia au
zisoma", msingi wa maarifa na akili sio kuona, Ni kusikiliza. Leo hii
tunajua kilichotokea miaka 3000B.C na hatukuwepo, lakini kwa kusikiliza. Biblia
pia inasema "Imani huja baada ya kusikia neno la Mungu", neno Imani
Ni kuwa na uhakika, katika Sayansi huwa tunarudia rudia majaribio ili tuwe na
uhakika, tunafanya experiments kuthibitisha tuwe na Imani na study fulani.
Msingi wa kufikiria Ni kusikiliza, unaposema kitu chochote katika sayansi,
utaulizwa " kitu chako kinahusiana vipi na kinachofahamika tayari".
Maana yake kila kitu kinachohusiana na kufikiria kinahusiana na kusikia.
KWANINI KUNA UHUSIANO WA KUSIKIA NA
KUFIKIRIA
Mtu anapofikiria huwa hata akifumba
macho, au akiangalia lakini asiwe anaona anavyoviangalia, mpaka atakapo maliza
kufikiria. Siri kubwa iliyojificha hapa ni hii.
Maarifa= Jumla ya taarifa( To-Tt)
+Jumla ya taarifa(ESo-ESt)
Hapa katika hii hesabu. kwanza tunaona
Maarifa Ni kujua maana zote za vitu toka siku ya kwanza ya uumbaji wa Ulimwengu
mpaka kufikia Duniani leo hii(To-Tt), Leo hii watu Kama "Michio kaku,
Richard Dawkins" wanasikilizwa Sana kwa kuonekana Wana akili Sana. hasa
kwa kuelezea historia za ulimwengu kwa kutumia Bigbang na kwa msaada wa uwezo
wao wa kutumia sayansi za kifizikia au jenetikia. lakini pia hata watumishi
wengi wa Imani husikilizwa Sana, hii ni kwa kuweza pia kuzungumzia matukio ya
awali kabisa katika uumbaji, na kutabiri yatakayotokea baadae katika Dunia kwa
ujumla. Hoja ya msingi hapa ni hii, kwa
wote wanaoamini dunia aidha Ina miaka bilioni 13.8 au wanaoamini Ina miaka
6000. Je kwa miaka 70 ya Ubongo wa binadamu, Nani anaweza kujua Siri za
ulimwengu kwa huu muda mfupi kiasi hiki? Hakuna namna. lazima mtu asikilize
waliotangulia, ili japo aongeze kujua taarifa za wakati uliopita, na makisio ya
wakati ujao. na Kisha akishasikiliza, Basi Sasa anaweza kufikiria! Kwa hiyo,
lazima mtu asikilize na sio aone. utaona nini miaka 70?
Pili, Maarifa Ni kujua Siri za
ulimwengu kwa sehemu zote za ulimwengu(Eso-Est), kuanzia ndani kabisa katika
atomu za DNA za seli za mwili, Kama ubongo, mpaka kila sehemu katika dunia, na
ulimwengu kwa ujumla. Sasa, Ni Nani anayeweza kuwa kila sehemu katika
ulimwengu. Unapaswa usikilize!! je unaweza kuona kinachotendeka kwa Sasa
marekani, au Sweden, au China?? Au hata tu kwa jirani yako? Ndiyo maana
inahitaji kusikiliza taarifa za habari au kusoma , ili uwe na akili, au
Maarifa, au ili iweze kufikiria.
JE WAJUA SIFA ZA UVIVU WA KUSIKILIZA!
watu walio wavivu wa kusikiliza, wakitumia muda mwingi kutazama vitu vilivyo mbele ya macho yao, mfano, mtu anatumia muda mwingi kazini kwake tu, kwenye burudani Kama michezo, kuangalia vinavyotendeka tu kwa muda huo!! Watu hawa huwa Wana uwezo mdogo Sana wa kufikiria. kwa maana, hawana taarifa nyingi. Utaona mtu mmoja akisema kuwa "haiwezekani kwenda na spidi ya sauti!!, Huyu mtu hawezi kufikiria vizuri katika maswala ya spidi za vitu, na ndiyo maana hata ameweza kusema hoja hii, hii ni kwasababu ana taarifa chache. huyu hasikilizi Mambo yaliyokwisha fanyika, au yanayofanyika katika maeneo mengine ya dunia. Biblia inasema " enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima". wenye hekima, Wana Maarifa ya kusimulia, jamii nyingi huamini wazee ni watu wenye Maarifa zaidi, hoja Ni kwa kuwa wameona mengi " wana taarifa nyingi' na kwahivyo "husimulia zaidi" na msikilizaji "Masikio yake hupokea zaidi".
Msikilizaji mzuri huwa na Maarifa Mara
nyingi zaidi ya mtazamaji mzuri. Masikio husikiliza hata mtu anapolala, masikio hayafumbwi!! Watu huweza kuona
taarifa zilezile, lakini kila siku husikiliza taarifa mpya, huoni unachokisia
Kama ambavyo usivyoona mawazo. Ni rahisi kutazama, lakini sio rahisi
kusikiliza, na kufikiria kwa pamoja.
UBONGO KIPINDI CHA KUFIKIRIA NA KUVUTA
TASWIRA.
Ubongo unapokuwa unatafakari Jambo
lolote Lile, iwe utatuzi wa changamoto fulani au ujio wa mbinu fulani, huwa
unafanya baadhi ya hatua. Katika ubongo, Kuna network zinazohusiana na Hali za
kufikiria. Zipo kuu mbili na moja ambayo Ina control badiliko la kutoka moja
kwenda nyingine inaitwa "salience network". Ya kwanza inaitwa
"Central executive network" au CEN", hii hutawala fikra zozote
zile zinazohusiana, au zinazotokana na shughuli za nje, mfano, Nina njaa,
ninawezaje kupata chakula. Au unapokuwa unafanya maamuzi, unapokuwa
unatafakari, unapokuwa unawaza Jambo lolote Lile. Na Mara nyingi CEN huambatana
na mawimbi makuu mawili ya Beta "Beta waves" ambayo huwa na frequency
kuanzia 13-30Hz na Gamma waves zinazoanzia 30-100Hz. hii network pia huitwa
"frontoparietal network kwa namna huusisha zaidi ya maeneo ya Ubongo wa
mbele juu, na pia Ubongo wa kati. Lakini pia huwa Kuna network nyingine
inayoitwa "Default mode network", hii huusiana na fikra zote mtu
anazozifanya akiwa anatengeneza taswira "imagine" na meditations,
ndoto za mchana "day dreaming", Hali za kutulia Sana kipindi mtu
anasinzia, na Mara nyingi huusiana na mawimbi ya alpha waves, ambayo huwa
yanaanzia frequency za 8-12Hz, na pia theta waves yanayoanzia 4-7Hz. Na hii
hupatikana Sana maeneo ya Ubongo wa mbele ndani, na pembeni chini. Lakini pia
Kuna network za hisia ambazo hizo huitwa "limbic system" ambazo
huusiana Sana, na sehemu za ndani za ubongo. na huusiana pia na sehemu zingine
za
ubongo Kama sehemu za ladha na harufu,
na hata sehemu za
Namna zote hizi za kutafakari au
kuvuta taswira zinachangiwa na sehemu zingine, vijedwali vya chini vina maneno
kama ‘’Top-down control’’-hii inamaanisha Mawazo huathiri matendo mengine,
sensory input-hii inamaana hisia za mazingira kama unachoona, sikia, mguso na
ladha huathiri Mawazo. limbic input-humaanisha hisia ‘’emotions’’ huathiri
Mawazo. self referential processing humaanisha tathmini binafsi.
Mtu anapofikiria, mfumo wa mawimbi ya
umeme ambayo yanajibadilisha badilisha, kulingana na Jambo au Mambo
anayoyafikiria, huonekana ukitamalaki katika Ubongo. Mfumo wa mawimbi na
umeme, Ni wa msingi Sana katika utendaji
wa ubongo, ukisikia mtu ana kifafa, Basi Ni huu mfumo unaoathiriwa hata
kupelekea kuripuka kwa msisimko wa umeme wa ubongo, na kusababisha baadhi ya
sehemu za mwili kuanza kuhemka tofauti na matakwa ya mtu. Lakini pia, hata
matumizi ya madawa yanayopooza mihemko ya ubongo, huusiana na kuzuiwa kwa
baadhi ya kemikali za ubongo "neurotransmitters" zinazohamasisha
mihemko ya ubongo. Kadri tutakavyokuwa tukiangalia sehemu hii, ni muhimu
kutambua kuwa, Miziki na taarifa za sauti zote tutakazokuwa tukizizungumzia,
Zina madhara katika makundi mawili.
1.madhara ya kifiziolojia yanayotokana
na Sauti zinazosikilizwa
2.madhara ya kisaikolojia yanayotokana na taarifa zinazosikilizwa.
Na katika kila kundi kuna sababu za msingi Sana, zinazoleta madhara
makubwa Sana katika mifumo ya fahamu ya watu. Hebu tuangalie Sayansi za
udanganyifu nyuma ya triki hizi.
TRIKI NA MADHARA YA KUSIKILIZA MIZIKI YA MIDUNDO HASA YA MISISIMKO
SAUTI INAVYOATHIRI MAUMBO YA MAJI
Mawimbi ya sauti huathiri kila sehemu ya vitu inavyovipitia, sauti husafiri kwenye chembechembe za hewa, maji au vyuma. Ukipiga kelele kwenye maji, utaona maji yakitikisika, lakini kubwa zaidi ni kuwa, sauti siku zote huathiri mpangilio mzima wa maji. Neno huathiri linamaanisha sauti, hubadili muundo wa maji, maji yanaundwa na molekuli za oksijeni na hydrogen. Molekuli hizi huwa na umbile lake la kawaida. Unapopitisha mawimbi ya sauti kwenye molekuli hizi, basi unapelekea umbile au maumbile yale ya awali ya maji kubadilika. Mabadiliko haya ya maumbile ya maji hutegemea na kiwango au nguvu au frequency za sauti zitakazokuwa zikipita katika hayo maji. Mfano picha chini inaonesha namna maumbo ya maji yanavyobadilika kulingana na frequency mbalimbali za sauti za muziki
Ukichukua maji na kisha ukayaweka kwenye chombo kama cha bati, yakiwa yametulia kabisa, halafu ukaanza kupiga hiyo miziki hapo juu, basi maji yataonekana kwa maumbo hayo juu. Miongoni mwa watafiti ambao wanatambulika kama ‘’Pseudoscientists’’ masaru emoto wa Japan, aliandika kitabu kinachoitwa ‘’taarifa zilizofichwa katika maji’’ au ‘’hidden messages in water’’ mwaka 2004, katika kitabu chake hicho ambacho kiliuza sana katika ‘’Newyork bestseller’’, alionesha kuwa, mapigo ya sauti hatari au mabaya, huusiana na maumbile mabaya ya maji ‘’ugly’’. na pia mapigo ya kutulia ya sauti, huusiana na maumbile mazuri ya maji. Ijapokuwa awali ilionekana kana kama ni nadharia za kufikirika zinazochochewa na wanasayansi wa nadharia za kufikirika ‘’pseudoscience’’, lakini ikaja kugundulika kuwa ni jambo la kweli na mpaka sasa tutaenda kuangalia athari za mabadiliko haya ya maumbile ya maji, kutoka katika sayansi na vyanzo vinavyoaminika zaidi duniani kwa tafiti.
Anasema muziki mzuri na maneno, hupelekea kuundwa kwa maumbo mazuri katika maji, kama hayo yanayooneekana katika picha upande wake wa kulia.
hapa pia akawa anaonesha kuwa, sauti zisizo na mipangilio mizuri Pamoja na miziki isiyomizuri, hupelekea maumbile yasiyo mazuri kwa maji. masaru emoto amenukuliwa kwa tafiti yake ya maji tu. ambayo pia imefanywa na wengine wengi, na sio mitazamo yake mingine kama inavyofanywa pia kwa wengine wanaonukuliwa!!
MSINGI WA KWANZA WA UHARIBIFU KATIKA MIZIKI YA MIDUNDO!!
Miziki mingi inayopigwa huwa ikipigwa
katika frequency za 440Hz na miziki michache sana ile inayopigwa katika sauti
za utulivu sana, hupigwa katika frequency za 432Hz. Sauti hizi nyingi za
frequency za miziki inayopigwa sana yaani wastani wa 440Hz, huambatana na
mabadiliko makubwa sana ya maumbile ya maji. Maji yanachukua asilimia zaidi ya
60% ya mwili wa mtu, tena kulingana na jinsia, umri au hata hali ya kiafya na
kifiziolojia ya mtu.
Mjadala mkubwa sana
ulioletwa na sayansi za mabadiliko, ya maumbile ya maji, kutokana na sauti
‘’cyamatics’’. Ni je, mabadiliko haya ya maumbile ya maji, hayawezi kuleta
madhara katika miili ya binadamu? Watu wanaosikiliza sauti mbalimbali hata hizi
zenye kuleta mabadiliko makubwa sana, je hawawezi kuathiriwa kwa frequency
kubwa za sauti? Kibaya zaidi ni kuwa, miziki mingi huwa na frequency kubwa
sana, tena zaidi ya hata hizo kubwa zinazofahamika yaani 440Hz. wasanii wengi
maarufu huwa wakikubalika sana kwa nyimbo zao zenye frequency kubwa sana za
sauti. kwa mfano (Mariah
Carey, Ariana Grande, Beyoncé, Whitney Houston, Celine Dion, Adele, Sam Smith,
Sia, Christina Aguilera, Bruno Mars, Demi Lovato, Justin Timberlake, Kelly
Clarkson, Ed Sheeran, P!nk, Lady Gaga, Rihanna, Taylor Swift, John Legend, Katy
Perry na wengine wengi kama baadhi ya nyimbo za Drake) wasanii hawa, pia huwa
na nyimbo baadhi zilizotulia. lakini
mara nyingi nyimbo zao, wakati mwingine hufika mpaka 10,000Hz na hata
14,000Hz.
Kadri ambavyo ilivyokuwa bado haitambuliki hasa je! ni kwa
kiwango gani, sayansi inakubaliana na madhara makubwa yanayoweza pelekewa, na
usikilizaji wa nyimbo za muundo huu, ambazo zinaweza pelekea mabadiliko makubwa
ya maumbile ya maji, katika afya za watu, na kuleta madhara. ndipo utafiti mpya
uliofanywa mwaka 2022 na kuchapishwa na ‘’Pubmed’’ ulidhihirisha haswa, madhara
makubwa yanayoweza pelekewa au chochewa kwa hata badiliko dogo tu la frequency
la 8Hz. tena katika frequency za miziki ya kawaida kabisa ya 440Hz, iliyojaa
katika staili za miziki ya kisasa.
UTAFITI WA MADHARA YA SAUTI KUBWA KATIKA AFYA
MATOKEO YA UTAFITI
Sauti ina uwezo wa kusababisha matokeo
ya kimekaniki ya kitu inachokutana nacho, kama ilivyo kwa kani zingine za
mekaniki. Nguvu ya sauti katika fizikia inafahamika sana, japokuwa katika
biolojia bado inafanyiwa utafiti zaidi.
Zipo tafiti nyingi zinazooonesha namna
sauti inavyoweza kuathiri mifumo ya kibiolojia ya viumbe mbalimbali. Viumbe
vidogo sana vinapowekwa kwenye maji, mawimbi kutokana na sauti inayopita katika
maji, yameonesha kuathiri sana matendo ya biolojia ya viumbe, pia madhara ya
sauti yameonekana kwa vimelea vya seli moja, kama bakteria, protozoa na
wengine, pia madhara yameonekana kwa mimea.
Kuna tafiti imenukuliwa inayoonesha
sauti za frequency kuanzia (38-689Hz) zilipopigwa, zilionesha kuathiri moja kwa
moja Ukuaji wa viumbe, matendo yao ya kibiolojia au metaboliki za mwili. na
pia, kwa viumbe hawa ambao wana seli za muundo wa bakteria ‘’prokaryotes’’ na
seli kama za binadamu ‘’eukaryotes’’, ilionekana hata uwezo wa dawa kuwaathiri
uliathiriwa.( Sarvaiya, N.; Kothari, V. Effect of audible sound in form of
music on microbial growth and production of certain important metabolites.
Microbiology 2015, 84, 227–235. [CrossRef] 9. Kothari, V.; Sarvaiya, N. Audible
Sound in Form of Music Can Influence Microbial Growth, Metabolism and
Antibiotic Susceptibility. J. Appl. Biotechnol. Bioeng. 2017)
Sauti na madhara ya DNA
tafiti iliyofanywa kwa mimea inayoitwa
(chrysanthemum) ilionesha kuwa, mawimbi ya sauti yalichochea au huweza
kuchochea uundwaji wa vinasaba vya jenetikia, vinavyoitwa RNA na protini. Hii
inaonesha kuwa, Sauti ina uwezo wa kuwasha hata mifumo ya jenetikia. Ambayo,
haipaswi kuwa ON. Au unaweza sema sauti zinaweza kuziwasha ‘’genes’’ za mwili,
ambazo zimezuiwa na mwili zisilete madhara.
Zaidi tena ilionekana kuwa, Sauti
iliifanya mimea inayoitwa (Arabidopsis), iweze kukaa kwa muda mrefu zaidi
katika upungufu wa maji, ukilinganisha na mimea mingine ambayo ilikaa penye
ukimya.
Uwepo wa genes mbili za mekaniki.
Mfano, ya (sauti) tu!
Tafiti hii ilionesha uwezo wa
kusisimua vinasaba ‘’genes’’ 87. Ambapo katika genes hizi, nyingi zake huusiana
na stress zisizotokana na matokeo ya kibiolojia, madhara ya kujikinga ya
vimelea hatarishi, na mabadiliko ya kikemikali ya mabadiliko ya ‘’oxidation na
reduction’’, na ajabu ni kuwa, ilionekana zipo genes 2 zinazohusiana moja kwa
moja na mabadiliko ya kimekaniki.(Hii ina maanisha kuwa, unaweza kufanya
mabadiliko ya kiumbe kwa kutumia tu sauti)
Sauti na mabadiliko ya maumbo ya
protini
Madhara ya sauti kwenye biolojia za
viumbe yalichunguzwa kiundani, na kuonesha kuwa, sauti husababisha mabadiliko
ya maumbo ya protini, zilizo ndani ya mwili ‘’protein crystallization’’ na
mabadiliko haya ya kimaumbo, hutegemeana na frequency. Kwa hiyo sauti kubwa
sana, yaweza pelekea madhara makubwa zaidi.( Zhang, C.-Y.; Liu, J.; Wang, M.-Y.;
Liu, W.-J.; Jia, N.; Yang, C.-Q.; Hu, M.-L.; Liu, Y.; Ye, X.-Y.; Zhou, R.-B.;
et al. Protein Crystallization Irradiated by Audible Sound: The Effect of
Varying Sound Frequency. Cryst. Growth Des. 2019, 19, 258–267).
Sauti ilionekana pia kuleta madhara,
kwa kuathiri uwezo wa seli za mwili, kuwasiliana ‘’signal pathways’’. tena
uwezo huu, ulionekana kuathiriwa kwa mimea, na kwenye mfumo wa fahamu wa
Wanyama.
Muziki Na Kula Sana Na Ongezeko La
Uzito
Katika kujifunza matokeo mbalimbali ya
muziki wa frequency kuanzia 432Hz mpaka 440Hz. katika tabia za kula, na uzito,
kwa panya. Iligundulika kuwa, mawimbi mbalimbali au frequency mbalimbali za
muziki, huathiri chembechembe za protini zinazoitwa ‘’peptide’’ za aina mbili.
zilizopo katika seli za fahamu. Muziki ulionesha kuathiri uwezo wa chembechembe
hizi, kujiunda, katika hatua ya kijenetikia ‘’expression’’. protini hizi zinazopatikana katika sehemu ya ubongo,
inayoitwa ‘’hypothalamus’’, ni za muhimu sana katika uwezo wa ku control hamu
ya kula, na hivyo, madhara ya kushindwa kujionesha yalipelekea kuongezeka kwa
hamu za kula kwa panya, hata kupelekea ‘’kuzidi kwa uzito’’. Na hii ni kwa panya waliosikilizishwa muziki wa
frequency za muziki wa kisasa, wa 440Hz. maana walikula sana, na kuongezeka
sana uzito, ukilinganisha na wasiokuwa wakipigiwa frequency hizo za muziki,
wale ambao waliosikilizishwa frequency za 432Hz.( Russo, C.; Russo, A.; Gulino,
R.; Pellitteri, R.; Stanzani, S. Effects of different musical frequencies on
NPY and Ghrelin secretion in the rat hypothalamus. Brain Res. Bull. 2017, 132,
204–212.)
Muziki Wa Pole Hushusha
Presha Kwa Wenye Presha
Ilionekana katika tafiti kuwa,
kusikiliza sauti zenye frequency za 432Hz, kulipelekea kushuka kwa mapigo ya
moyo kwa viumbe wenye presha kubwa ya damu ‘’high blood pressure’’. (Halbert, J.D.; van Tuyll, D.R.;
Purdy, C.; Hao, G.; Cauthron, S.; Crookall, C.; Babak, B.; Topolski, R.;
Al-Hendy, A.; Kapuku, G.K. Low Frequency Music Slows Heart Rate and Decreases
Sympathetic Activity. Music Med. 2018, 10, 180–185)
Mabadiliko Ya Muziki Toka 440-432hz Hupelekea Kushuka Kwa
Presha Na Hali Ya Kutulia Ya Mwili
Ijapokuwa ukipigiwa muziki wa 432Hz na
440Hz unaotumika zaidi, ni kama inafanana. lakini tofauti ipo. Na badiliko la
kuelekea katika frequency za 432Hz ,hupelekea kushuka kwa presha ya damu na
mfumo wa upumuaji. Hii humfanya mtu kuhisi ku relax, ukilinganisha na muziki wa
frequency za 440Hz. Muziki wa 432Hz pia hupelekea usingizi mzuri, hata kwa
wagonjwa wa uti wa mgongo, na huongeza uwezo wa kujitambua ‘’perceived
arousal’’ (. Calamassi, D.; Pomponi, G.P. Music Tuned to 440 Hz Versus 432 Hz
and the Health Effects: A Double-blind Cross-over Pilot Study. Explore 2019,
15, 283–290.)
Muziki Wa 440hz Na Hisia Mbaya Kama Hasira
Tafiti ilionesha pia kusikiliza muziki
wenye frequency za 440Hz. (muziki wa mtindo wa kisasa zaidi) huambatana na
hisia za Anxiety ( hali ya kutotulia kiakili, mithili ya hisia ya kukandamizwa
maeneo ya juu ya tumbo kuelekea kifuani, wakati mgumu, kutokuhisi wepesi,
kutoelewa elewa, kuwaza mbali kinamna ya msongo, kuchanganywa ), nervousness na
aggression( hali ya kuwaka kwa hasira, kukakamaa kwa ghadhabu, udhaifu,
kuongezeka kwa hisia za tempa, kuwa mkali), hali hizi zote zilionekana
kuambatana na aina hii ya muziki. waweza pia kurejea (Calamassi, D.; Pomponi, G.P. Music
Tuned to 440 Hz Versus 432 Hz and the Health Effects: A Double-blind Cross-over
Pilot Study. Explore 2019, 15, 283–290)
Mabadiliko Ya Mawimbi Ya
Muziki Na Madhara Katika Dna
Tafiti iliyofanywa juu ya madhara ya
sauti, katika vinasaba vya ndani kabisa vya jenetikia ya viumbe yaani DNA.
Yalionesha kuwa, DNA ya binadamu inahisi au sense sana Muziki. ‘’DNA is
sensitive to music’’. Na ikaonekana kuwa, kwa kupiga muziki wa frequency
mbalimbali katika seli mama za viungo ‘’stem cells’’( hizi ndizo hupelekea
kukua kwa seli zingine zote, zenyewe huwa na utendaji mkubwa sana wa DNA,
katika kuumba seli zote za mwili), huweza kupelekea kubadilishwa kwa utendaji
wa asili wa seli, na viungo hatimaye. Hii ni sawa na kusema, kwa kupitia
miziki, unaweza kubadilisha kabisa fiziolojia ya kiumbe kuanzia ngazi ya
jenetikia ya ndani kabisa. Unaweza rejea ( Muehsam, D.; Ventura, C. Life rhythm
as a symphony of oscillatory patterns: Electromagnetic energy and sound
vibration modulates gene expression for biological signaling and healing. Glob.
Adv. Health Med. 2014, 3, 40–55. )
Bado Sehemu Kubwa
Haifahamiki Kuhusu Utendaji Wa Muziki
Pamoja na tafiti hizi kujitahidi sana
katika kuchambua, undani wa madhara ya muziki katika biolojia za viumbe, lakini
bado, sehemu kubwa haifahamiki. Lakini kitu pekee kinachotishia sana ni kuwa,
kuna uwezo wa kutumia mawimbi ya sauti, katika kuathiri matendo mbalimbali ya
kibiolojia ya viumbe. Tena, katika kiwango cha chini kabisa. Sayansi inaendelea
kupambana ili iweze kufikia kiwango cha kutambua, namna sauti inavyoweza
kuathiri chembe moja moja katika mwili wa kiumbe, kitu kinacho fahamika mpaka
sasa, ni namna ambavyo sauti, inaweza kuathiri matendo ya kibiolojia kwa ujumla
kwa viumbe. (Stoilov A, Muncan J,
Tsuchimoto K, Teruyaki N, Shigeoka S, Tsenkova R. Pilot Aquaphotomic Study of
the Effects of Audible Sound on Water Molecular Structure. Molecules. 2022 Sep
26;27(19):6332. doi: 10.3390/molecules27196332. PMID: 36234868; PMCID: PMC9573228.)
MADHARA YA
MUZIKI KATIKA SAIKOLOJIA YA WASIKILIZAJI
Jedwali La Maeneo Ya Ubongo
Yanayosisimuliwa Na Muziki
Maeneo ya ubongo yanayosisimuliwa mtu anapokuwa akisikiliza
muziki. Maeneo haya yanaeleza namna muziki, ulivyo wa msingi sana. hii ni kwa
kuwa, ni maeneo ambayo yanashughulika na sifa mbalimbali za msingi za tabia za
watu.
|
Region (Brodmann Area) |
|
|
Temporal cortex (YANAHUSIANA NA SAUTI, MUZIKI,
LUGHA,KUMBUKUMBU, TAARIFA ZA VITU ) |
|
|
Right |
Primary auditory cortex (41) |
|
Secondary auditory cortex (22 and 42) |
|
|
Superior temporal sulcus (21 or 22) |
|
|
Temporal pole (22 or 38) |
|
|
Middle temporal gyrus (21) |
|
|
Left |
Primary auditory cortex (41) |
|
Superior temporal sulcus (21 or 22) |
|
|
Limbic areas ( YANAHUSIANA NA HISIA NA
KUMBUKUMBU) |
|
|
Right |
Anterior insula |
|
Hippocampus |
|
|
Left |
Retrosplenial cortex (29 or 30) |
|
Anterior cingulate cortex (32) |
|
|
Anterior insula |
|
|
Subcallosal cingulate gyrus (11 or 25) |
|
|
Others brain areas (YANAHUSIANA NA TABIA ZA KUIGA) |
|
|
Lingual gyrus (18 and 19) |
|
|
Inferior parietal lobule (39) |
Maana Ya Msingi Ya Jedwali
Muziki husisimua moja kwa moja sehemu
zinazohusiana na hisia, kumbukumbu na sehemu za lugha, tabia na kujifunza. Kama ukimuambia mtu akumbuke maneno yaliyo
katika wimbo, na maneno yaliyo katika kitabu, basi itakuwa ni rahisi sana kwa
kukumbuka maneno yaliyo katika wimbo. Hii ni kwasababu, muziki unapendwa sana
na kupewa sana kipaumbele na ubongo. hii ni kwasababu, muziki umeungana sana na
hisia. na pia, una husiana sana na misisimko ya kujisikia raha, kama
tulivyoangalia katika sayansi ya muziki katika ubongo.
Katika sehemu hii tutaangalia ni kwa
namna gani, mtu anaweza kutumia uhusiano huu wa muziki, katika kuleta madhara
makubwa sana, katika saikolojia ya msikilizaji.
MISINGI
YA UHARIBIFU WA SAIKOLOJIA ZA WATU KUPITIA MUZIKI
Kutumia Mabiti Ya Nyimbo Zenye Midundo Kuondoa
Uwezo Wa Kutafakari
Tumeshaona kupitia tafiti mbalimbali,
namna ambavyo nyimbo zenye mabiti mengi sana (polyrhythms) hupelekea msisimko
mkubwa sana wa ubongo. kama yalivyo madawa ya kulevya. (unaweza rejea nukuu ya
Peter vuust: interplay of music and psychedelics). Na kwa mantiki hiyo,
misisimko hiyo ambayo huchochea miondoko ambayo inaweza kupelekea kucheza, au
hisia za raha sana (fananisha, watu wanapokuwa wameshinda kombe hushangilia
sana, muda mwingine hata kutokujali kama wanaweza kujidhalilisha), hizi zote
zinaelezwa kwa nadharia hii hii moja ya tabia za muziki, kudhoofisha uwezo wa
kutafakari.
KWANINI WATU WANACHEZA
Kucheza kuna maanisha, mabiti ya muziki yameingia hata ndani kabisa ya Ubongo, na kushabiiana na mawimbi ya mwili mzima. (rejea :entrainment na embodiement) na kitendo hiki cha kushabiiana, humfanya mtu Kwenda na mabiti haya, kwa kuyacheza, kwa lengo la kuongeza msisimko mzima wa mapigo haya (rejea: freeing attention with dancing), sasa basi, nyimbo zote zenye mabiti ya kuchezeka, huondoa utaratibu na uwezo wa ubongo wa kutafakari (rejea:disturbance in beta waves), na hii ndiyo sababu, mtu hawezi kutafakari mipango yake kwa ufasaha, akiwa anakimbia, au anafanya kazi ya kuchosha misuli. kwasababu kubwa moja, kufikiria, kuna husisha kusitisha kupokea taarifa toka viungo vya fahamu. (ukiwa unawaza, unaweza fumba macho kumaanisha ‘’hupokei taarifa za kuona’’, unaweza acha kusikiliza kelele, na mazungumzo ya watu. ‘’kumaanisha, hupokei taarifa za masikio’’, unaweza acha kuhisi maumivu madogo madogo ya viungo na uzito ‘’kumaanisha hupokei taarifa za ngozi’’, unaweza pia usisikie hata Ladha ya chakula kilicho mdomoni ‘’kumaanisha hupokei taarifa za ulimi’’ na mwisho unaweza usihisi harufu nzuri au mbaya zinazokuzunguka ‘’kumaanisha hupokei taarifa za harufu za puani’’). na sasa basi, sifa hizi zote haziambatani na kucheza, au kufanya kazi, ambako, kunahitaji sana kuangalia, ili uwe makini usiumie au anguke. Hivyo ukitaka watu wasifikirie, wewe wapigie nyimbo za midundo ya kucheza.
Mlevi aliyelewa kisawasawa, hata
nyimbo yenye mapigo ya kawaida kabisa, yeye hujisikia kucheza. Huwezi elewa
hili mpaka utakapojua kuwa, siku zote Ubongo wa kufikiria (prefrontal cortex
una matabaka sita) umejaa channel zinazozuia mihemko ya hisia. (rejea: mtu
mwenye akili hata akiwa na hasira, au mhemko, huwa hazioneshi hisia zake
kirahisi ) sasa basi, Pombe hufanya prefrontal cortex ishindwe kabisa kufanya
kazi yake (rejea sehemu ya pombe:kutokana na mgandamizo unaosababishwa na
uharibifu wa kazi za kemikali za GABA, na Glutamate), kitendo hiki hupelekea
mabiti ya muziki, yanapochakatwa kwenye sehemu za ubongo hasa wa hisia,
kusababisha ‘’entrainment’’ au ubongo kuendana moja kwa moja na mapigo haya, na
kuanza kusisimua misuli kucheza, ukiongeza na kujaa kwa mhemko wa kemikali za
mhemko ‘’dopamine’’ basi mlevi lazima acheze hata kama kwa udhaifu sana.
Je wajua
Mara nyingi nyimbo za midundo ya
kucheza, hupigwa maeneo ambayo watu huwa hawafikirii sana. Mfano kwenye ‘’Night
clubs, vilabuni, Casino, Sherehe za kushangilia aidha ushindi, au kitu
fulani’’, sehemu hizi pia huchangamana na unywaji wa pombe, maana muziki na
pombe, ni kama pete na kidole, kila mmoja ana lengo moja la kuulevya ubongo
mpaka mwisho.
Huwezi piga nyimbo zenye midundo ya
kucheza, katika sehemu ambayo watu wanahitaji kuwa makini watafakari.
Usikilizaji uliokithiri wa nyimbo zenye midundo, huanza kupelekea matatizo ya
kudumu ya udhaifu katika uwezo wa kufikiria. Tafiti nyingi zinaonesha,
usikilizaji wa nyimbo za midundo, hupelekea tabia za kuzoelea mihemko. kitu
ambacho, huchochea uraibu wa kutaka kusikiliza nyimbo zenye midundo zaidi na
zaidi, na hata baadae kuwa watu wenye maamuzi ya juu juu, na ya hatari, kwa
kutokuwa na busara.
Sayansi Ya Muziki Iliyofichika Ya Utofauti Wa Nyimbo
Za Midundo Ya Kucheza Na Nyimbo Za Utulivu.
Watu wengi huchanganyikiwa katika uchaguzi wa muziki, maana kuna wengi ambao waliamini kuwa, nyimbo za dini ni nyimbo zilizotulia sana. Na nyimbo zisizo za dini, ni nyimbo zenye shida sana ya midundo. Lakini cha ajabu hata nyimbo za dini nazo, siku hizi zimeshamiri staili ya midundo, hebu tuangalie nini hasa ni sababu ya kushamiri kwa midundo.
|
|
‘’Honey…Honey…’’(limeshatengeneza‘’melody’’),
kama atalirudia mara nne, tayari limeshaunda ‘’verse’’, kama ataongezea na mabiti au ‘’Harmony’’, tayari umeshakuwa wimbo. Nyimbo nyingi sana zisizo za dini, hutumia tekniki ya kurudia rudia au ‘’polyrhythms’’ kutengeneza nyimbo zenye mihemko. Japokuwa zipo hata za dini siku hizi hutumia mbinu hii.
Siri Ya Ubongo Wasiyoijua Wasanii Na Wapenzi Wa Nyimbo Za
Kizazi Kipya
Ubongo hasa wa kufikiria ‘’prefrontal cortex, orbitalfrontal cortex, cingulate cortex, n.k.’’ haupendi kurudia rudia vitu. Na ndiyo maana, ukishaiangalia filamu, haitakuvutia sana tena. au hata nyimbo ukiisikiliza sana, hautavutiwa nayo sana. Au hata kitu ukikizoea sana, hautavutiwa nacho sana. Sasa basi, Nyimbo hizi za kujirudia rudia mara nyingi, ili zimvutie mtu, inapaswa ziende kwa haraka haraka. Hii ni kwa lengo la kwanza kabisa, la kuudanganya ubongo kuwa, kuna verse mpya inakuja baada ya muda mfupi sana (fananisha na umakini wa mtu unapoongezeka, unapomwambia, hebu subiria mara moja!!!). sasa basi, baada ya kipindi kifupi panapokosekana mabadiliko, ubongo wa mbele ‘’PFC’’ huachana kabisa na kutafakari huu mziki. Na hii huwa inatokea hata kipindi cha Jogging, baada ya muda, Ubongo huwa unapoteza kabisa mvuto wa nyimbo na kiongozi hupaswa kubadilisha. Sasa basi, kwa wasanii wa nyimbo za kizazi kipya, mara nyingi ili kuendelea kuchukua umakini au ‘’attention’’ ya ubongo, basi hutumia mabiti yaliyopangiliwa kwa ufundi sana ‘’polyrhytmic sound beats’’, na kwa haya mabiti, ubongo hupagawa ukiendelea kutafakari, lipi hasa ndilo biti mama ‘’accent meter’’ kwa namna yalivyo mabiti mengi. Haya yote yakiambatana, hupelekea hali ya Ubongo kupumbazwa, na ilihali umechangamshwa. Hii ni sawa na mgonjwa wa kifafa, anakuwa anasisimka huku hajitambui. Na ndiyo maana, utakuta mtu anacheza lakini hasa haelewi nini kinachomsukuma acheze, mcheza mpira hukimbia akiwa na lengo maalumu la kuukimbilia mpira, au kipa huruka kwa lengo la kuutafuta mpira hewani, mcheza mziki hata hawezi kuelewa hasa kwanini anacheza. Ila anachohisi ni kuwa, amesisimka kwa raha, na zinamsukuma kucheza ili kukazia hisia zake za raha.
Hapana, Watoto hucheza
sana maana Ubongo wao bado hauna uwezo wa kujizuia, na hisia kwao zina nguvu
sana. na ndiyo maana, mtoto ni rahisi kulia na akacheka ghafla, bado ubongo
wake ‘’cerebrum’’ haijakomaa na hisia zina nguvu sana. Lakini pia mtoto hucheza
cheza sana ili kutumia sana misuli yake. kuongeza ukuaji wa sehemu za Ubongo.
kupitia kucheza cheza huongeza uwezo wa kuelewa namna viungo vinavyopaswa kuwa,
na balansi katika pande kuu tatu za dunia. mtoto mdogo hujifunza kila muda, kwa
kuwa bado, hajui vitu vingi, na hii ndiyo sababu pia, Ubongo wake huwa
hautulii, ili aende kila sehemu, akijifunza mazingira yake. Watoto hufundishwa
kwa namna ya kutumia viungo, wakicheza na nyimbo. Mfano, sote tulianza kukarii
irabu kwa kuimba ‘’a,e,i,o,u’’. na hivyo hivyo kwa silabu zote. Hii
inadhihirisha namna ‘’kucheza kunavyokazia umakini na kumbukumbu, mtu
anayecheza muziki, pia anakazia tafakari za mabiti bila yeye kujua!
Mtoto kadri anavyokuwa tabia hizi
huisha, huwa hapendi kucheza cheza mbele za watu (maana huwa sio hisia rahisi
kufurahisha kwa wengi, wengine huisi kama ni udhaifu kuanza kucheza mbele za
watu, kama ukiwaambia ghafla watu 10 unaofahamiana nao, waanze kucheza mbele za
watu, hata kwa nyimbo wanazozipenda, ni asilimia ndogo sana watakuwa na
ujasiri!) kucheza ni matokeo ya udhaifu wa kushindwa kujizuia, na ndiyo maana,
kuna mabiti yanapopigwa tu, watu hata bila kutaka, hujikuta wanaanza kucheza au
kuhisi hali za kutokuwa na utulivu. Pia hisia za kucheza, huwa na nguvu mtu
anapokuwa peke yake, au na watu anaowaamini sana, ni rahisi kwa mtu kucheza na
mpenzi wake, au rafiki zake, hii inarejea kulekule kwa nadharia ya kucheza na
udhaifu. Kwa hivyo, Watoto huacha kucheza cheza kadri umri unavyosonga mbele.
Ingawa, matumizi ya mabiti ya ‘’polyrythms humrudisha mtu katika umri wake wa
utoto kwa kucheza’’.
Narudia kucheza sio vibaya hata kwa
watu wazima, ni hisia ya asili ya ubongo. ila, kucheza hakuambatani na utendaji
kazi wa kifikra pana, kama kutafakari, kuwa na kiasi, n.k. ‘’Central executive
network’’ haifanyi kazi unapocheza kiuhalisia. ubongo kwa muda wote mtu
anapocheza, huwa bize kufatisha mawimbi ya mabiti, kuwa makini na balansi ya
mwili, sehemu za hisia huwa juu sana, na motisha ya matumizi ya misuli huwa juu
kadri ubongo unavyohangaika kufatisha mabiti yaliyo complex.
Pia, ni raha na rahisi kumwangalia mtu
akicheza, lakini sio rahisi kwa mchezaji hata atakapokuwa mzoefu. Kisaikolojia,
hapa huwa sawa na mtu anayepiga chabo mtihani wa mwenzake. Ubongo hupenda kuona
namna kazi yake iliyopaswa kuifanya, ikifanywa na mwingine vizuri zaidi. Wengi
tunapenda starling anavyopigana katika filamu ya kivita, kwa kuwa kupitia
‘’mirror neurons’’ tunajiona sisi ni kama yeye. Watazamaji wa ‘’Pornograph’’,
hutamani sana wanayoyaona, ingawa wanajua ni matendo ya udhaifu, na hakuna
mtazamaji ambaye angetamani aanikwe yeye vile katika udhaifu. Hivyo basi,
Ijapokuwa wengi hupenda kutazama udhaifu kwa wengine, wao wenyewe
wasingeukubali, au wangeukubali katika siri tu, na ndiyo maana, wengi wetu
hucheza sana miziki tunapokuwa sirini, au na wale tunaowaamini sana, au labda
kama tayari mtu ashapata saikolojia mpya ya kupuuzia udhaifu wake!!
Baadhi huchanganya kauli hizi mbili,
kushangilia ni mihemko ya kusheherekea. kwa kuongeza hatua za misuli, na hata
kuruka ruka, hii ni hisia ya kila mtu mzima atakaye shinda. Na mtu hushangilia
akiwa na sababu maalumu, zilizotangulia. Lakini kucheza, kuna maanisha tendo
linaloanzia katika msisimko unaotengenezwa na Muziki. (kushangilia kunaanzia na
ushindi, labda vitani, mtihani au chochote kile). Utagundua pia kushangilia,
hakuna steps maalumu. lakini kucheza, kuna steps maalumu.
Sio Nyimbo Zote Zisizo Za Dini Zina
Madhara Na Sio Kila Nyimbo Ya Dini Haina Madhara.
Nyimbo zisizo na madhara ya hapo juu, huwa na sifa ya kuwa na kiwango kikubwa cha ubora wake katika ‘’Melody’’. Melody ni kama vile kusema, nyimbo inakuwa imejikita zaidi katika ubora wa mashairi huku ikiwa haijaegemea katika mabiti. Mfano mzuri wa hizi nyimbo, hebu tafakari nyimbo ya taifa ya Tanzania
’Mungu Ibariki Afrika, Wabariki viongozi wake, Heshima uhuru na umoja, hizi ni ngao zetu, Afrika na watu wake, Ibariki Afrika, Ibariki Afrika, Wabariki Watoto wa Afrika.’’
Katika hii nyimbo, kuna Rhythm. Lakini sehemu kubwa imejikita katika melody ya nyimbo. Na ndivyo ilivyo pia kwa nyimbo nyingi za vitabu vya zaburi. Msanii wa singeli angeweza kuchukua tu neno ‘’Mungu ibariki Afrika’’ na akatengeneza nyimbo kwa kujaza ‘’Rhythms’’ na harmony (mabiti na vionjo)
Wapo wasanii wanaoimba nyimbo zisizo za dini na wakiimba agenda za msingi tu katika Maisha, na huimba kwa kuzingatia melody ‘’ambapo ndipo uwezo wa msanii hupimwa’’. Kumbuka dini ni Imani ambayo kila mtu anayo, kukosa dini ni kukosa Imani ya uwepo wa chanzo cha maadili, kwa kigezo cha nadharia ya ‘’evolution’’ kitu ambacho ni hatari sana kwa maendeleo ya sayansi. mtu asiye na dini na haamini ‘’evolution’’ huyo bado haijui ‘’evolution’’ ila ndiyo anaiishi, ni sawa na kuchukua uraia wa marekani na kuikana Tanzania, hiyo wala haiathiri Utanzania wa Mtu kama alizaliwa Tanzania.
Je Wajua Kuna Nyimbo Za Dini Zilizojaa Rhythms!!
Unaweza kuta nyimbo moja ina dakika
kuanzia 9 mpaka 14 hata 20 muda mwingine. Na inarudia maneno yaleyale, na
mabiti ya frequency ndogo ndogo. Nyimbo hizi nazo huua uwezo wa ubongo wa mbele
‘’Prefrontal cortex’’, kwa kuwa ubongo usingependa kurudia rudia, ni kama tu
ambavyo, ungekasirika kama mtoto wako
angekuwa anakuita ita kila baada ya muda, kwa kitu kilekile. Baadhi ya watu
huwa wanaenda kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu, na kupiga nyimbo za mtindo
huu wakupooza, huku wakirudia rudia maneno.
na walivyo wajanja wasimamizi wa haya
matamasha ‘’pia hutumia taa za mianga dhaifu’’ ili kudhoofisha zaidi na zaidi
uwezo wa ‘’prefrontal cortex’’, madhara yake ni watu kupoteza kabisa uwezo wa
ku focus, na hapo pia tutaangalia katika sehemu inayofuata madhara yake ni
nini.
Pia zipo nyimbo za dini zenye mabiti
ya midundo mikubwa sana ya kucheza, mara zote midundo ya nyimbo hizi huwa na
misingi ile ile ya usisimuaji kwenye Ubongo, kama zile nyimbo za midundo zisizo
za dini.
Je Wajua: Msifu Mungu Kwa Kucheza!!! Neno Kucheza Sio ‘’Dance’’ Ni Kifaa
Kuna baadhi ya watu walihisi labda Biblia ilipoandika msifuni Mungu kwa kucheza, ilimaanisha kucheza kama ‘’kitenzi’. Neno kucheza lilitafsiriwa kutoka neno ‘’Dance’’ ambalo katika Lugha yake ya asili, lilikuwa likitumiwa kama kifaa hiko hapo juu. Na katika fungu la zaburi 150 lilipotajwa neno ‘’dance’’ ulikuwa ni mfuatano uliokuwa unaorodhesha vifaa tu. Lakini pia katika vifaa vyote vilivyoorodheshwa, hakukuwepo na Ngoma au ‘’Drums’’, ambazo ndizo msingi wa mabiti ya kucheza.
Hii ina maana gani?
Iwe kwenye sayansi za jamii, iwe
kwenye evolutionary science , iwe kwenye neuroscience na mwisho iwe katika
Biblia. Kote kutaleta jibu lile lile kuwa,
kucheza ni dalili ya moja kwa moja ya madhara ya kisaikolojia
‘’Psychopathognomic sign’’.
Kuna baadhi huuliza, kama ni hisia
mbaya, kwanini ipo katika Ubongo? kucheza sio hisia mbaya, ni hisia za ndani za
udhaifu, kama tu zilivyo hisia za kutaka kufanya mapenzi. kucheza kunahitaji
upweke, uwe na mpenzi wako, familia, na marafiki. Kitaalamu lazima kuwepo
‘’Privacy’’, hakuhitaji kufanywa kwa umma, mfano, Kanisani, taasisi za elimu,
vyombo vya serikali, au kiufupi ‘’Public’’.
URAIBU
WA MIDUNDO SEHEMU YA KWANZA
Mtu anaposikiliza sana midundo ya
nyimbo zenye kuhamasisha kucheza, katika ubongo wake anakuwa akimwaga homoni
nyingi sana za ‘’Dopamine’’. Ambazo, huambatana na homoni za raha
‘’endorphins’’, hizi humfanya ajisikie raha. Na sasa basi, anapoisikiliza
nyimbo kwa muda Fulani, na ubongo ukawa umeshauelewa wimbo vizuri, hakuna tena
‘’syncopation’’ na Ubongo hausisimki zaidi, basi huyu mtu hushuka ghafla sana,
toka kwenye msisimko mkubwa, mpaka kwenye msisimko mdogo kabisa, kitu ambacho
humfanya asijisikie raha kabisa.
Na hii shida sasa humfanya atafute
nyimbo nyingine. hasa mpya, kwa ubongo, ili aweze kuuchanganya tena, Ubongo
usisimke. mpaka utakapouelewa wimbo vizuri, ubongo usisimke zaidi, basi atakuwa
na mwingine mpya tayari. Hii ndiyo siri ya waraibu wa hii miziki, kuwa na
nyimbo nyingi sana katika ‘’playlists’’ zao. Na ukiwa msomi mzuri mchunguzi,
sifa hii pia wanayo ‘’watazamaji wa filamu, waangaliaji wa video za ngono,
waraibu wa mitandao ya kijamii n.k’’ hawa wote wapo katika kundi la uraibu,
ambalo madhara yake huwa ni ‘’anxiety’’, ambayo huwafanya wawe na hisia kama za
upweke, au kutoona wepesi, mpaka watakapopata vitu vya kuwasisimua zaidi.
Mpenzi wa nyimbo zilizojaa ‘’Rhythms’’
na harmony nyingi sana, hupenda sana kucheza ‘’kama ambavyo mlevi hupenda
kucheza akishalewa’’. Madhara yake ni kuwa huyu mtu huwa inakuwa ngumu sana
kuja kupenda nyimbo zisizo za aina hii.
Sifa Ya
Nyimbo Zenye Melody Nyingi Zaidi Ya Rhythms
Mara nyingi hizi huwa hazileti uraibu.
Lakini pia mara nyingi nyimbo hizi, huambatana na ujumbe ambao msanii
huuwasilisha, na mtu anaweza kuzisikiliza nyimbi hizi, huku akitafakari lengo
kuu la mtunzi. Hii inawezekana tu kwasababu, msikilizaji huwa huru katika
Ubongo wake kutafakari ujumbe wa nyimbo, msikilizaji hashambuliwi na midundo ya
‘’rhythms’’ ambayo inamtengenezea misisimko ambayo, atake asitake atakumbana
nayo tu.
Je Wajua Mabiti Yote Ya Kucheza Hufanana??
Ingawa ni ngumu mtu kugundua kirahisi,
lakini mabiti yote ya kucheza katika kiini chake hufanana, na hata ukivuta
asili yake kabisa, utarejea kwenye ‘’polyrhythmic patterns za tangia miziki ya
enzi za voodoo’’. Mara nyingi mabiti haya huwa ya asili ya Polyrhythms za
Druple (4/4 kwa 3/4). Hizi druple ndizo biti pekee zenye connection au zenye
channel zinazoenda kwenye sehemu ya Ubongo inayoitwa ‘’Basal Ganglia’’ ambayo
huusiana na uchakataji wa miondoko. Na ndiyo huko huchangamana na channel
zingine za mihemko, hata kuishia na kucheza.
Ushahidi Wa Nje Wa Watu Kukosa Uwezo Wa Kutafakari Kupitia
Mapigo Ya Mabiti
i.Kuwepo kwa kesi za watu wanaovua
Nguo Majukwaani. Hakuna mtu ambaye angeweza kufanya hivyo kirahisi, ijapokuwa
wapo ambao wangeweza kwa sababu zao binafsi, lakini uwingi wa kesi hizi
unathibitisha kuwa, watu hawa wamelevya na mabiti haya ya mihemko
ii.Kuongezeka kwa hisia za mapenzi
katika clubs au vilabu vyenye namna hizi za miziki. Watu wengi wanaojaa katika
viwanja vya mapigo ya mabiti haya, hujawa na mihemko ya kimapenzi. na ndiyo
maana, utakuta mara nyingi wakicheza kwa kushikiliana katika staili za
mapenzi.
Hii moja kwa moja inathibitisha
kupungukiwa nguvu katika sehemu ya ubongo wa kutafakari ‘’PFC au prefrontal
cortex’’. PFC ilipaswa kuzuia mihemko ya kimapenzi, mpaka watu wawe sehemu
iliyo ya siri.( PFC huruhusu hisia za mapenzi sehemu yenye usiri tu, au giza,
na ndiyo maana, katika sayansi ya uzazi, husemwa kuwa kwa viumbe wengi, kushuka
kwa yai la uzazi kwa wanawake au ‘’ovulation’’ hufanyika gizani, lakini katika
Ubongo inatambulika kirahisi kuwa, wakati wa usiku, jua linapozama ‘’kiwango
cha homoni ya Norepinephrine’’ inayokinzana na utulivu unaopelekea mihemko ya
kimapenzi , hushuka. Na hivyo kuruhusu mhemko mkubwa wa hisia za mapenzi, wapo
viumbe wengi sana wasiozaliana hata kuwe na giza, au sirini) lakini uwezo wa
kuonesha hisia za kutaka kufanya mapenzi hadharani, ni tatizo kubwa kabisa la
Ubongo ‘’psychopathology’’ ambalo, linatokana na kuisha kabisa kwa uwezo wa
kuhisi aibu. Aibu ndiyo msingi wa utu, watu hawa hawana kabisa ubinadamu. ni
kama Wanyama, maana Wanyama baadhi kama mbuzi au kuku huweza hata kuzaliana
mbele ya Watoto wao, au na Watoto wao. wakati Wanyama walio na akili kama nyani
tu, au sokwe, hujikinga pia na hadhara kwa ajili ya mapenzi, hii inathibitisha
mabiti ya muziki ni hatari kwa ubongo.
iii.kuweza kutamka na kusikiliza
maneno machafu bila kushtuka. Wengi wa wasanii kama ungewaambia wayaseme maneno
yao, kipindi cha ‘’interview’’ wanayoyaimba kwenye majukwaa, wasingeweza
kirahisi. Lakini huyaimba kirahisi jukwaani. Katika mabiti haya watu huweza
hata kutukana wazazi wao, na wasiwaze. Hii inathibitisha madhara ya
kisaikolojia yamekithiri katika ubongo wa wasikilizaji
iv.Kushuka kwa nguvu ya elimu na uwezo
wa kufikiria.
jamii zote duniani kwa zama hizi
zimejaa vijana, na Watoto wapenda shari, wasio na huruma, na wasio na kujizuia.
Hizi sifa ni kinyume kabisa na maarifa. na mwisho wake mkubwa, ni kuongezeka
kwa changamoto zisizo na mwisho
v.Kuporomoka kwa maadili.
vi.kushuka kwa uwezo binafsi wa
wasanii.
vii.Kushuka kwa mvuto na nguvu kwa
nyimbo za maadili, na za dini. Watu wengi hawajui kwanini miziki ya dini haina
nguvu tena kama ilivyokuwa zamani. Sababu kubwa ni kuwa, wasikilizaji wengi
wameshaleweshwa na ‘’rhythms’’. hawawezi tena kuzielewa ‘’melody’’. Wasanii wa
nyimbo za dini pia, wengi wameshaathiriwa pia, maana sanaa ya mabiti ina nguvu
sana hasa kwa mtu asiye elewa siri zilizo nyuma ya mabiti na ubongo.
Kutumia Kuchanganyikiwa Kwa Watu Kuingiza Tabia
Mbaya Hasa Za Uhuru Wa Tabia Za Kichafu
Falsafa Tatu Katika Zama Za Muziki Na Sayansi Katika Zama Za Usasa
Watu wengi wasiojua
sayansi kiundani kabisa, hawatambui kuwa sayansi na muziki vyote vimepitia zama
kuu tatu.
PRE-MODERN
ERA ( tokea zamani za kale mpaka 1789)
hizi zama ndizo zama
zilizoanzia toka uumbaji wa dunia. kwa wanaoamini Biblia miaka 6000 iilyopita,
ambayo kwa miaka ya 1789, basi ingekuwa toka uumbaji mpaka miaka 5789. Na kwa
wasioamini uumbaji wa Mungu, basi kuanzia miaka ya Bilioni 13.8 mpaka miaka ya
1789. Katika zama hizi sifa kubwa kabisa ilikuwa ni ‘’Upo Ukweli Ambao
Unatoka Kwa Mungu’’ au wengine huuita ‘’Absolute truth’’.
Katika zama hizi, kila msingi wa maarifa ulitengenezwa. Na waasisi wa kila elimu au taaluma walianzia katika zama hizi.
Mfano
Falsafa zote za kina
Socrates, Plato, Aristotle, Hippocrates, Pythagoras, Democratius. kusambaa kwa
taaluma za kigiriki kwa nguvu ya utawala wa Alexander the great. Ukija kwenye
Taaluma za matibabu au medicine za awali kabisa, tokea enzi za Galen mpaka zama
za kuinuka kwa dola ya uislamu na kina Al Ibn issa, kuinuka kwa Imani ya
Kikristo kuanzia miaka ya 30 AD, kuja kuinuka kwa dola ya kiislamu miaka ya
600AD, kuinuka falme za ulaya baada ya kuanguka kwa dola ya rumi ya magharibi
miaka ya 395AD, kukua kwa taaluma za uinjinia tokea dola za china mpaka
maendeleo makubwa ya taaluma za ujenzi za Rumi,
kukua kwa uprostestanti miaka ya 1500’s kulikochochewa na kina Martin
Luther, maendeleo ya sayansi za Fizikia kuanzia kwa kina Copernicus, Galilei,
Newton ,Leibniz, Descartes, na wengine wengi, kukua kwa sayansi za kemia
kutokea ‘’alchemy’’ mpaka kwa kina ‘’Antoine Lavoisier’’. Falsafa nyingi sana
na misingi mingi sana ya elimu ilianzia katika karne za hawa watu.
Zama hizi hakukuwa na
mjadala kuwa kipi ni sahihi na kipi sio sahihi, ukweli ulikuwa unafahamika. Na
ndiyo maana, utakuta mwanafizikia mkubwa kabisa kuwahi kutokea sir Isaac Newton
akitengeneza nadharia ambazo ndizo msingi wa sayansi yote ya fizikia ya leo,
lakini bado akisema Mungu ndiye aliyeshikilia ulimwengu, na bado akatumia miaka
mingi sana kusoma Biblia. Ijapokuwa inafunirahisha leo hii ukijitambulisha
mwanasayansi, na kisha ukaonesha unamwamini Mungu, watu wanakushangaa, kiufupi
sayansi ilianzia kwenye imani hii.
Muziki katika zama
hizi ulikuwa ni muziki wa ibada tu. Kipindi hiki muziki ulikuwa ni sehemu ya
ibada. na sio muziki wa matumizi mengine kama katika zama hizi. Pia muziki
ulitumika kwa heshima sana katika nyumba za kifalme, na matibabu kwa baadhi ya
nukuu. Hakukuwa na miziki ya kucheza wala polyrhythms, katika sehemu kubwa za
jamii za watu. hasa ambapo rekodi za historia zilizonukuliwa kwa jamii kubwa za
watu wa Eurasia ‘’Ulaya na sehemu za Asia’’ sehemu zilizoendelea zaidi za
awali, na kaskazini mwa Afrika. ijapokuwa maeneo yaliyokithiri upagani yakisiwa
kuwepo tayari kwa mtindo huu wa midundo.
MODERN ERA
(tokea zama za 1789 mpaka 1970)
Hizi zama katika
historia ya Dunia, ndizo zama zilizojenga misingi ya kuua kabisa kizazi
kilichofuata baada yake, kizazi hiki ndicho kizazi kilichoua dunia kabisa. Katika kizazi hiki kulitokea
mapinduzi makubwa sana ya sayansi, baada ya watu kuweza kufanyia kazi maarifa
ambayo walikuwa tayari wameyasoma sana. Na hapa kulitokea mapinduzi makubwa
katika nyanja zote. Katika upande wa sayansi ya Fizikia, kulitokea mapinduzi
makubwa ya fizikia ya nadharia kwa kuamka kwa nadharia za fizikia ya kisasa,
kama nadharia za Albert Einstein, ambazo, zilionekana kana kama zimekuja na
majibu pale Isaac Newton aliposema kuna
mkono wa Mungu, na ikaonekana kana kama imani kwa Mungu ni kukosa majibu
ya maswali ‘’God of Gaps’’, nadharia za albert einstein ambazo ziliitwa
‘’General na Special Relativity’’ zilikuwa zinakataa uhalisia mmoja wa kitu,
bali zilikuwa zinasema kitu hubadilika kulingana na mazingira yake, katika
namna bora zaidi ya kifiziikia, lakini pia zilikuja na namna ya kuelezea zaidi
‘’Gravitation’’ kama hali na sio kani au Force, watu walifurahia sana na hata
Albert mwenyewe hakuamini Mungu ambaye Newton alimwamini. ( kumbuka Einstein
mwenyewe kuna ushahidi mkubwa sana kuwa, nadharia zake nyingi alikopi kwa
wenzake, poincare, na Lorentz, na wengine wengi, hakuna kubwa jipya alilofanya
zaidi ya kuja na fasiri zake mwenyewe zenye kuathiri kabisa uelekeo wa fizikia
bora ya utendaji) Pia nadharia za Quantum Physics, ambazo zilitengeneza hoja za
kifalsafa, kana kama, katika viwango vya chini kabisa vya chembechembe, hakutabiriki!
Hivyo, hakuna sheria za utendaji za kudumu, ni kama vile, asili ya vitu ni
uhuru, usio na mipaka! Lakini hata hivyo, katika zama hizi tokea kabla ya hawa
jamaa, alikwepo mwanasayansi kama Laplace ambaye naye alionesha kutoona sababu
ya kuamini Mungu, kumbuka fizikia ndiyo sayansi iliyokuwa ina nguvu zaidi. na
hivyo, comment kutoka kwa wanasayansi hawa zilikuwa na nguvu ya kubadili hata
jamii. Zama hizi pia ziliibuka na mapinduzi makubwa ya sayansi za uinjinia, kwa
kuja na sayansi za mionzi iliyopelekea mabomu, sayansi za uinjinia wa umeme,
sayansi za uinjinia wa magari na vyanzo vya usafiri, sayansi za uinjinia wa
vifaa vya muziki na kurekodia, kamera na video, mwanzo wa kukua kwa teknolojia
za satalaiti na uinjinia mkubwa sana wa teknolojia za leo. Zama hizi zilikuja
na mapinduzi ya kibiolojia ambapo anatokea Charles Darwin. ambaye nae,
anapingana na misingi yote ya kuamini kuna muumbaji Mungu. kama ilivyokuwa
tokea zama za kina Aristotle. Darwin akiwa na sapoti kubwa kuliko hata hoja
zake baadhi, anapokelewa kama Einstein wa sayansi za uhai, hata kwenye
Jiografia wanaibuka kina Charles Lyell. ambao wanachochea uumbaji wa dunia bila
Mungu. tofauti na sayansi za waliokuwa tu nyuma yao tena kwa kufuatana ‘’George
curvier’’ ambae alithibitisha uumbaji wa Mungu, katika masomo ya mabaki ya vitu
katika ardhi, wapo waliokuja na nadharia za kila aina za kutokuwepo kwa Mungu
na kuwa, Sayansi pekee inaweza toa majibu ikichanganywa na uwezo wa binadamu wa
kufikiria. na hapa pia, wanasayansi wakwanza kabisa wa Ubongo, kina Sigmund
Freud, walianza na nadharia za kukataa uwepo wa Roho kwa kuchukua kila kitu
katika ufahamu kama matokeo ya ubongo. na mengineyo mengi.
Muziki katika zama
hizi rasmi ulianza kubadilika katikla muundo wake. Wengine huziita hizi zama
kama ‘’Romantic era’’ na muziki ulitumika sana katika namna ya kuwasilisha
mawazo ya watu. Na dunia ilionekana sio sehemu bora ya utukufu kama awali, bali
ilionekana kama sehemu ambayo haina Mungu, na mtu anaweza kufanya chochote
kile. Matumizi ya Piano yalianza. Baadhi ya historia hunukuu pia kuwa, waafrika
waliokuwa maeneo ya Marekani katika kuchangamana katika ibada na wazungu,
waliokuwa na asili ya muziki ule wa awali uliokuwa hauna midundo ya aina
nyingi. basi walianza kuunganisha vipengele mbalimbali ambavyo viliendelea kuwa
na chembechembe za polyrhythms. Hizi ziliendelea kuboresheka kwa kadri muda
ulivyokuwa ukienda mbele, na hata kupelekea muziki wa kwanza wa muundo wa
muziki wa kisasa wa leo, kutoka kwa wasanii kama ‘’Robert Johnson’’’ au unaweza
mwita ‘’first bluesman’’.
MWANAMAPINDUZI HASI
ASIYESEMWA!!!
Kuna
mtu mmoja aliyekuwa anaitwa ‘’Aleister Crowley’’, huyu aliandika kitabu maarufu sana kwa zama
hizo za marekani kilichoitwa ‘’Kitabu cha sheria’’ au ‘’Book of the Law’’.
Katika kitabu hiki aliandika sheria moja kubwa ilikyokuwa inasema ‘’FANYA
UNACHOJISIKIA’’ au ‘’Do what thou wilt’’. Pichani ni Jay Z akiwa na
tishati iliyoandikwa, fanya unachojisikia. Falsafa hii na dini hii imesambaa
kwa kila sehemu.
kwa kipindi hiki marekani ilikuwa na idadi kubwa
sana ya wakristo, hasa kutokana wengi kukimbia toka ulaya. kukimbia
ugandamizaji wa Papa kwa zama zile, na
tokea zama za giza ‘’dark ages’’. Na sasa basi, kutokana uwingi wa
wakristo. na ukristo kuwepo kwenye mifumo mingi ya kiutawala. Shida ilianzia
pale ambapo, bado kulikuwa kuna namna mbalimbali za kiukandamizaji, kwa watu wa
matabaka ya chini. na hasa waliotoka hali za kitumwa. Watu hawa walichukia sana
watawala wanaojitangaza kwa sera za kikristo lakini wana mitindo ya
ukandamizaji, kwa hiyo sera za ukinzani kama Hii, ilichochea ujumbe huu wa
fanya unachojisikia’’ ilikubalika sana. ilikuwa ni habari njema sana. Ulikuwa
ni mithili ya wito wa amani, na hata ukisikiliza wasanii wengi wa Hip Hop wa
marekani, waliotoka katika familia za kimasikini, utagundua ni kana kama aidha
walikuwa wanalaani ugandamizaji, au wanalaani wagandamizaji wanaomtumia Mungu
kuficha ugandamizaji wao, au walikuwa wanalaani mifumo na hata kutoamini Mungu
wao. Bwana Alister Crowley anatambulika kwa kuanzisha kanisa la shetani
‘’Satanic Church’’, lakini wikipedia na vyanzo vingi pia humtambua kama
muanzilishi wa siasa za ‘’Humanism’’ au imani za mtu kujiamini yeye mwenyewe,
na kutotishiwa na mitazamo ya imani za kikristo.
Siogopi kusema kuwa
yupo shetani, lakini kinachojulikana ni kuwa, wasanii wote wakubwa wa kizazi
kipya cha muziki ambao nao ulikuwa katika mapinduzi makubwa hata kuzaliwa kwa
‘’Rock n Roll’’, Pop, Jazz na mingineyo. Wote walikuwa katika falsafa hii ya huyu
bwana. Picha zote walikuwa wakiwa na nembo za jamii hii mpya. na wengi walikuwa
wakiimba moja kwa moja kuwa ‘’hawaamini kabisa uwepo wa Mungu’’ au kuonesha
wana mdhihaki. Na hata alipokufa Crowley, bado falsafa zake ziliendelea kwa
uwepo wa wanaharakati wa aina yake wakubwa tena kama ‘’Anton Lavey’’ na hawa
watu walikuwa na mafanikio makubwa sana, kwa kuibadilisha jamii kubwa sana ya
watu. hii ni kwa kuwa, walikuwa wanatumia muziki, na pili walikuwa wanafanya
mambo yao huku asiwepo mtu wakuwazingatia. Maana, ni taasisi za siri. Ni kama
hivi leo msanii akionesha ishara za kishetani hakuna anayejali kwa kuwa haina
msingi katika maana ya kawaida. Lakini kwa msomi mzuri wa sayansi, lazima ajue
kila kinachoendelea na ndiyo maana, utamkuta ‘’Isaac Newton’’ akiwepo kwenye
‘’Alchemy’’ na hata Albert Eintsein akionesha imani yake, kwa Mungu wa Spinoza
(anaamini asili ndiyo Mungu, huitwa pia Pantheism). kiufupi Swala la imani
linahusiana moja kwa moja na uwezo au IQ ya mtu, kujitathmini yeye ni nani.
Ajenda kuu za muziki mpya zilikuwa ni uhuru, wa kufanya
vitu ambavyo jamii ingevizuia, kwa kutishia hofu za imani. Na watu wengi
hawajui kwanini jamii kubwa za watu wa marekani, na Ulaya, hawana kabisa
maadili. Unaweza kuta mtoto mdogo kabisa tayari anajihusisha na mapenzi, na
hakuna anayejali, unaweza kuta watu wanafanya ushoga hadharani kabisa, unaweza
kuta watu wanatembea uchi barabarani, unaweza kuta mauaji hayashangazi watu,
unaweza kuta wanaume wanavaa milegezo mpaka chini kabisa ya suruali, unaweza kuta
watu wanatukana mbele ya wazazi wao, unaweza kuta watu wanajichorachora,
unaweza kuta watu wanalipua mabomu kama hiroshima na nagasaki vita ya pili ya
dunia, unaweza kuta watu wanafanya tafiti za sayansi za kubadilisha jenetikia
za watu, unaweza kuta watu wanafanya biashara ya vidole vya watu, kama wakoloni
walivyofanya Congo, unaweza kuta nchi ina asilimia 85% ya watu hawana dini na
waliobakia bado sio wadini, kama Netherland. Yote hayo yalianzia katika muziki na yalianzia katika falsafa hizi
katika kizazi hiki cha ajabu zaidi.
1960-1980: kuliongezeka asilimia 400% kwa ndoa
za watu wasioona. Sababu:muziki!!
Toka Uumbaji wa dunia- 1960:kulikuwa na magonjwa mawili tu yakuambukiza kwa njia ya ngono, leo hii kuna magonjwa 25. Mauaji ya kimashambulizi yameongezeka kwa asilimia 995%.
Falsafa za Humanism na Satanism ambazo zimejikita katika hakuna muumbaji ‘’Atheism’’ , imani ya ‘’Evolution’’ na fanya unachojisikia, ilipata nguvu mpaka Serikalini rasmi. Na kwa mara ya kwanza miaka ya 1920’s. Shule zote zikaanza kufundisha hakuna Mungu, bali tumetokana na mabadiliko tokea ujiuji wa miamba, seli za vimelea, samaki, jamii za manyani mpaka watu. Na hivi ndivyo kila mtu amefundishwa, haikuwa hivi miaka michache tu nyuma.
Sababu Za Kutumia Taarifa Za Mihemko Ya
Uchafu
Imani hizi hasa
zilipata nguvu kutokana na kutumia sana mapenzi, katika kitovu cha kuondoa
uwepo wa Mungu. Watu wengi hawajui Biblia iliposema Mpende Bwana Mungu wako,
kwa Moyo wako wote, kwa Akili zako zote, na kwa Nguvu zako zote. Ili maanisha
kuwa, Upendo ni mjumuisho wa moyo+hisia+nguvu. Hakuna kitu cha kufanania
kupokea hizo sifa zaidi ya hisia za mapenzi. kupitia kuweka mapenzi, mtu
angeweza kuigiza ibada hapo. Na ndiyo maana, imani hizi huambatana na sanaa za
kusisimua hisia za ngono, na hata picha zao nyingi huwasilishwa katika muundo
wa picha za uchi. Mwanaume anaweza kutumia nguvu zake zote ili amridhishe
mwanamke, akatumia moyo wake wote na akili zake zote. Tayari mwanamke amekuwa
kama Mungu. Na vivyo hivyo kwa mwanamke, na ndiyo maana, utakuta nyimbo nyingi
za watu hawa wakisifia sana wapenzi wao. tena husema wewe ni ‘’Nyota ya maisha
yangu, au kila kitu kwangu, au hata husema wewe ni Pumzi ya uhai wangu,
ukiniacha napoteza uhai wangu”, kwa mtu asiyeelewa kuwa hiyo tayari ni ibada,
ni rahisi kuupenda huu wimbo, bila kujua siri iliyo nyuma yake. Hakuna hata
sehemu moja Suleiman alipomsifia mpenzi wake kwa sifa za muundo huo. Nyimbo
zote zimejaa ajenda za mapenzi na ngono, au hasira na migogoro au ulevi na
visasi. Wanasayansi wa kweli hutambua sababu hii.
Msingi wa pili wa
imani hizi, ni kutumia sana Nguvu za sehemu za mamlaka ya umma na vyanzo
vikubwa vya fedha. Jambo hili hulificha kwa siri sana ili lisionekane, na ndiyo
maana, utakuta hata katika sayansi, pamoja na kitabu kama hiki kuwa kizuri
sana, utaambiwa hakikidhi vigezo tu kwa sababu kinamtaja Mungu (rejea sababu ya
Prof Damadian kunyimwa Nobel prize baada ya kugundua MRI, kwasababu tu ni
Mkristo). Ukirejea Crowley angewezaje kupata nguvu kwa kiasi kile?, na kwanini
zama hizo hizo?, na falsafa hiyo hiyo, iwe inakuwa maeneo yote ya dunia kama
Russia?, ambako ilibidi hata kutokee mapinduzi makubwa, ambayo chanzo kabisa
alikuwa ni Karl Marx, ambaye naye alikuwa na imani za kisatanist. Ambazo
alizirithi Vladmir Lennin, ambaye nae alimpindua hata Tsar kwasababu alikuwa na
imani ya Mungu. na wao sasa walianza rasmi kuingiza falsafa za Humanism Russia.
Pia kwanini China? Kwanini Cuba? n.k. Mpaka hapa unaweza kujua kuwa, hata wale
wasanii wengi walipata Nguvu kubwa kutokana na kuwa, walikuwa wanatumia sanaa ya
kuteka akili za watu, lakini walikuwa wakifadhiliwa sana na mamlaka za siri
zenye ajenda ya kuingiza falsafa za ki humanism. Huu ni muziki uliokuwa ibada,
katika kubatiza zaidi vijana.
POST-MODERN ERA (kuanzia 1970 mpaka leo)
Zama zilizopita za modern era za
kuanzia miaka ya 1789-1970. Iliaminiwa kuwa Sayansi, falsafa na logic zina
uwezo wa kumuelekeza mtu katika ukweli au "absolute truth". Na hivyo
Sayansi iliheshimiwa Sana, Kama chombo ambacho kina uwezo wa kumuelekeza mtu
katika kuujua ukweli. Akili ya mwanadamu ilionekana ndiyo inamtengeneza Mungu,
na sio Mungu anaitengeneza akili. Lakini Cha muhimu zaidi hapo nikuwa, bado
kulikuwa na msingi wa ukweli, Ila haukutoka kwa Mungu, ulitoka kwa akili za
wenye Maarifa.
Kilichofelisha Zama Za Modern Era
Zama zile zilizotegemea akili za watu,
katika kuamua ukweli. ziliishia na migogoro mikubwa zaidi kuwahi kutokea katika
historia ya dunia. Vita vya kwanza vya dunia, Vita vya pili vya dunia,
mapinduzi ya damu katika sehemu mbalimbali za dunia, milipuko ya magonjwa ya
kutengeneza, milipuko ya migogoro ya kijamii, kisiasa na kifalsafa. Maporomoko
makubwa zaidi ya maadili.
Haya yote yalipelekea jamii zote za
watu, kuishiwa kabisa Imani juu ya maarifa, Tena juu ya watu walioaminiwa
kuweza kuwa na maarifa. Hii Ni kwa kuwa, maarifa ambayo walitegemewa kuwa nayo,
ndiyo yameishia kutengeneza matatizo makubwa zaidi. Mfano mzuri, Ni namna
taaluma za masomo Kama ya fizikia, yalivyo chochea uundwaji wa mabomu hatari
zaidi duniani, masomo ya kemikali yakiishia uundwaji wa sumu hatarishi zaidi,
na hata masomo ya maisha yakiishia na uundwaji wa magonjwa mengi zaidi ya
awali. Zama zote hizi hakukuwepo na Biblia ya kurejea, kipi Ni kweli! na kipi
si kweli! maana tayari kilionekana Ni kitabu Cha masimulizi ya kusadikika, na
kisicho na hadhi ya kitaalamu. Na Hili ndilo lilikuwa hasa lengo na mwanzo tu
wa dini mpya ya "Humanism''. ambayo ili Hali duniani haikutambulika kwa
wazi, lakini ndiyo ilikuwa inachochea Kasi hasa kupitia Miziki pamoja na Nguvu
za umma.
Kuzaliwa Kwa Zama Za Post-Modern Era
hizi ndizo Zama kuanzia miaka ya 1970. Katika Zama hizi Sasa, Dunia Haina wa kumsikiliza. Hakuna Sayansi, Wala falsafa, Wala logic na Wala Biblia. Zama hizi ndizo ile misingi ya dini mpya "Humanism''" imetawala kwa falsafa zake za fanya unachojisikia. "Do what thou want". Zama hizi Ni mfanano halisi wa kipindi Kama kile, baada ya falme ya Rumi ilipoupokea Ukristo. na kupelekea karibia dunia yote kuambukizwa ukristo. au Zama zile baada ya kuanguka kwa Alexander the great, ambapo karibia dunia yote iliambukizwa tamaduni za kigiriki. Na hivyo Basi Zama hizi, Ni kana kwamba sehemu kubwa ya dunia iliambukizwa tamaduni za "fanya unachojisikia". Matokeo ya Zama hizi Ni kuwa na jamii ya watu wenye mafundisho mengi zaidi, ambayo ndani yake hushindwa kabisa kuchambua kipi Ni sahihi, na kipi si sahihi. kila mtu Ni Mwalimu, kwa kuwa Hakuna standard au kipimo maalumu Cha kupima maarifa Kama awali. Zama za nyuma ingetumika Biblia, Zama za Kati ingetumika Sayansi na falsafa, lakini Zama za mwisho Hakuna kipimo!! Hizi ndizo Zama ambazo, zinamaliza kabisa uwezo wa binadamu wa kimaarifa, maana kila taaluma Haina thamani Tena.
Siri Nyuma Ya Msukumo Wa Vipaumbele
Vya Elimu
Mfumo wa elimu hubadilika kwa kila
zama, kulingana na uhitaji wa hizo Zama. Mfano, Zama za dhiki za migogoro ya
kivita, elimu iliongozwa zaidi katika masomo ya ufundi, na fizikia, kwa lengo
la kujenga silaha nzito, pamoja na ujenzi wa miundombinu mikubwa ya kiuchumi,
na ulinzi. Kwa Zama baada ya migogoro, elimu huelekezwa zaidi katika taaluma za
kutatua changamoto za matokeo ya migogoro, Kama vile, taaluma za kuboresha
kilimo, matibabu, utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa uchumi. Katika Zama hizi
za post modern era, hakuna elimu Tena za muundo huu, maana hata watu hawajui
matatizo yao. Elimu za uinjinia za maroboti, na akili za kisasa, zinapamba Moto
zaidi! huku tatizo likiwa ni kukosekana kwa kazi, kwa watu, kwa kila sehemu.
Hii Ni sawa na kusema, elimu inachochea Moto zaidi kuwachoma iliyopaswa
kuwaokoa. jamii bado halilijui tatizo. Idadi ya matatizo ya akili, na
kisaikolojia, yameongezeka Mara elfu zaidi ya Zama zote zilizopita. Dini
inatumika Kama falsafa, falsafa Kama Sayansi, Sayansi Kama dini, kila mtu na
mitazamo wake.
Sifa Za Zama Za Post-Modern Era
Kuongezeka kwa ubinafsi kwa Hali ya
juu zaidi. Zama zote watu wangetoa maarifa yao kusaidia jamii zao, lakini Zama
za PME, watu wenye maarifa hutumia maarifa yao, kujiweka juu zaidi, au
kukandamiza zaidi wa chini. Hii ndiyo sababu ya matumizi makubwa ya maarifa,
katika kubadilisha jenetikia za watu. ili kuwaathiri, kutengeneza vyakula
vyenye madhara, kutumia teknolojia kushusha uwezo wa watu, kutengeneza Rocket
za kwenda sayari za mbali, lakini kushindwa kutatua matatizo ya ajira. Asilimia
karibia tisini ya Mali za duniani, zipo kwa asilimia kumi tu ya watu wote.
Serikali zimejaa ubepari na migogoro. sio Tena nchi na nchi tu, Bali hata ndani
ya wananchi.
Kupungua Sana kwa wasomi wakubwa, na
watu wenye maarifa, Kama Zama zilizopita. Kila Zama zilizopita ungekutana na
watu wenye maarifa, na kupendwa Sana na jamii zao. Lakini Zama hizi za PME bila
hata aibu, unaweza kuta hata wasanii walio mfano mbaya kabisa, wakipewa tuzo za
watu wenye hamasa zaidi. Sasa Watu watajifunza wapi? Leo hii Huwezi kumuelewa
mwanafizikia Kama Michio kaku, au Brian green, au Penrose Roger, kama mtu
mwenye maarifa zaidi, Kama hawezi hata kuelewa kuwa Hakuna ushahidi kabisa wa
uumbaji usio wa akili, kupitia taaluma za Sayansi za biolojia. Matatizo yote
yameanza baada ya watu kufundishwa nusu nusu tu.
Kuzidi kwa matatizo katika kila
nyanja. kuanzia kijamii, kwa kuisha kabisa kwa maadili, kuongezeka kwa matatizo
ya kiafya, matatizo ya kiuchumi, matatizo ya kisiasa, matatizo ya kiakili kwa
kuongezeka Sana hofu. zinazotokana na changamoto za Maisha, zisizo na mwisho.
kuzidi kwa uongo katika kila sekta, sio elimu , sio siasa, sio dini kumejawa na
unafiki. hizi ndizo Zama ngumu zaidi kuwahi kutokea na zinaleta hofu Sana,
katika kutabiri mwisho wake.
Kazi Ya Muziki Kama Msingi Katika Zama
Mpya
Miziki ndiyo silaha kubwa ya dini ya
"Humanism''. Inasikitisha namna ambavyo wasanii wengi wa Miziki ya kisasa,
wasivyotambua suala hili. na hujikuta wakiendeleza utume wa dini hii, bila wao
kujua. Wasanii hutumia mbinu kadhaa katika kusogeza falsafa hii.
Mbinu za Kisaikolojia za Wasanii,
wasizozijua hata wenyewe.
Kufanya Vitu
Kitofauti."kisanii"
Neno Usanii, kutumiwa Kama
"utofauti" huanza kuharibu saikolojia za msanii mwenyewe, kabla ya
watakaomsikiliza. Binadamu wote ni sawa katika kila hatua na hata tabia. Msanii
hapaswi kujiona Ni mtu wa tofauti. Usanii Ni kujiongeza kitaaluma, kutokana na
kipaji, sio kujibadilisha kitaaluma kutokana na kipaji. Sasa Basi, falsafa hii
hatari huwafanya wasanii muda wote kujihisi wapo sahihi kwa kuenenda Kitofauti
na jamii zao. Unaweza rejea interview nyingi za Beyonce ambae kwasasa Ni Kama
"Malkia wa mziki wa kizazi kipya kwa dunia mzima", huwa anasema
"nikiwa kwenye stage, huwa nakua sio Mimi Tena, Kuna mithili ya kitu
huniingia na kunifanya niwe mtu mwingine kabisa, na Hali hiyo hunifanya nifanye
Mambo yote ninayoyafanya pale,ambayo kwa akili zangu nisingeweza
kuyafanya". Mfanano wa stori hizi huwa kwa Wasanii wote, kuaminisha zaidi
umma kwa ajenda za kweli, au Wenda sio za kweli, lakini zote Ni kumtambulisha
msanii Kama mtu wa tofauti na mtu wa Kawaida. Hivyo msanii atafanya vitu vyote
ambavyo mtu wa Kawaida "aliyeumbwa na Mungu" asingeweza kuvifanya.
Hii maana ya msanii Ni Kama inamtambulisha msanii, Ni mtu mwenye matatizo ya
akili, au mtu mwenye pepo. Kitu pekee ambacho huwashangaza hata Wasanii
wenyewe, Ni namna ambayo Mara zote, utofauti wao hukubalika!!, Wasanii baadhi
hufanya vitu viovu kabisa! hata wao wasingetamani kuvifanya kisanii, lakini
bado hushangaa kuona wanawafuasi wengi. Hii Sasa huwafanya wawe watumwa wa
akili zao wenyewe. Hebu angalia kwa mfano, sifa zifuatazo za msanii Kama mtu wa
tofauti.
Msanii Ni mtu ambae anaeweza kuvaa
nusu uchi, na jamii bado ikamkubali
Msanii Ni mtu ambae hapaswi kuvaa
nguo, Kama ilivyo kawaida ya watazamaji wake
Msanii Ni mtu ambae anaruhusiwa
kutukana, na kuzungumzia lugha chafu, bila kushangawa
Msanii Ni mtu ambae kila anachofanya,
anapaswa kukidhihirisha kwa umma
Hii Ni mifano tu ya matatizo ya awali
kabisa ya kisaikolojia, yanayojengwa kwa Wasanii. Na matatizo haya huwafanya
wengi Wa Wasanii, wawe Ni watu ambao
muda wote huwa wanahangaika kufanya Vitu Kitofauti na maadili, tofauti na
mitazamo, tofauti na mategemeo, na hata tofauti na mamlaka zozote zile
zilizopo. Wenda Ni dini, serikali, familia , taasisi na zinginezo nyingi Kama
familia.
Kutegwa kutamani umaarufu Kama
mafanikio toka kwa mashabiki
Hapa Kuna saikolojia kubwa Sana kwa
Wasanii wengi. Ndoto zao huwa Ni kuwa na wasikilizaji wengi Sana, na hasa kwa
kufatiliwa Sana, na kuwa maarufu. Lakini tatizo kubwa Sana ambalo huwa
hawalijui Ni kuwa, mafanikio hayatokani na umaarufu, na mafanikio hayatoki
mbali. Kupitia kuwa na wafuasi wengi, kwenye mitandao ya kijamii, hakumfanyi
mtu kuwa na mafanikio yoyote hata ya kiuchumi. maana mitandao yote inayotawala
biashara za internet na Aina zake mfano "Spotify" au apple" yote
huwa chini ya taasisi za watu wenye ajenda zilezile za kutawala watu. Matokeo
yake huishia tu wasanii wakijiona Ni maarufu, lakini bado wanachangamoto kubwa
za kiuchumi, na kijamii. na kibaya zaidi, jamii haiwategemei kuwa katika Hali
hizo, maana sivyo wanavyojionesha katika nyimbo zao. Na kwa mantiki hiyo,
Wasanii wengi wakubwa hujikuta wanaingia katika hatari ya kuingia katika
mkataba wowote ule, ambao utatumia umaarufu wake, kuwasilisha ajenda. na ili
Hali itawaachia namna walau Bora ya kuishi, kwa viwango vya umaarufu wao.
Biashara zote za wireless
technologies, au teknolojia za Mitandao, hazifanyiki kama utendaji wa biashara
za moja kwa moja. Mitandao ipo chini ya uongozi wa moja kwa moja wa vituo
vikubwa kabisa vya mawasiliano. Ambavyo, hutawala mawasiliano kulingana na ajenda
zao. Mitandao Ni ya kuwa nayo Makini Sana. Hata kwa wasomi wazuri wa Sayansi za
kompyuta, hushauri hivyo. utendaji wake Ni Dhahiri, lakini, unapaswa kutazamwa
kwa umakini, hata Kama mtu ataona ametazamwa na watu bilioni moja. Je yeye ana
uhakika gani? Amewaona? Waliomtazama wamevutiwa naye? Walikuwa na lengo la
kumtazama? Hayo yote yanaweza kumaanisha kuwa, umaarufu hutengenezwa, au huweza
kuharibiwa.
Hali Za Wasanii Maarufu Zisizosemwa!
Wasanii wengi walio maarufu, wengi
hujutia hali zao baada ya muda tu, aidha hadharani au sirini. Lakini wote
hujutia Hali zao. Wasanii wengi Kama Michael Jackson, wamewahi kuonesha kabisa
hadharani kuwa wanateseka, au wapo kifungoni. Wengine hawana kabisa amani, na
hukiri kuwa hawafurahii, Ila hawana namna. Unaweza tazama namna Wasanii wengi
hawana familia za kudumu, ili Hali katika nyimbo zao, huonesha hufurahia
mahusiano yao ya ndoa!!
Kuaminishwa kuwa Mapenzi Ni mazuri
Kuliko ndoa.
Wasanii wengi huaminishwa kuwa,
kupitia kutembea na mabinti wazuri wa mionekano ya sura, na maumbile. au
wanaume wazuri wamionekano, na utajiri. basi wanaweza pata faraja kubwa sana.
nyimbo nyingi huyatukuza Mapenzi, Kama faraja yenye hisia za kiungu "divinity
na eternity". Falsafa hii unaweza iona kwa namna nyimbo nyingi zina ajenda
za Mapenzi, na hufanyiwa video kwa kushirikisha ma videovixens. na hivyo hivyo
kwa wanaume. Hii mitazamo dhaifu kabisa ya kisaikolojia, huanza kuisha baada tu
ya mtu kuanza kuvuka Zama za ujana, na kuanza kuingia hatua za utu uzima. hisia
Kali za Mapenzi huwepo ujanani, kwa lengo la kutafuta mwenzi na kuzaa. Ila
baada ya hapo, hupoa au kushuka kwa lengo la kulea na kuishi na familia
(haimaanishi huisha, ila hushuka!) Na tabia za kutembea na wanawake wengi,
huondoa kabisa uwezo wa ustahimilivu kifamilia. maisha huwa mabaya asilimia
zote. Kwa kukosa familia, kwa kuhisi hatia na kwa kudhalilika nafsi.
Namna Jamii Inavyoharibiwa Saikolojia
Kwa Kusikiliza Nyimbo Hizi
Kwanza kabisa nyimbo hizi huambatana
na mapigo ya nyimbo za mabiti, au polyrhythmic beats, ambazo, tulishaona katika
sehemu iliyopita namna zinavyoharibu ubongo. Nukuu mbalimbali huonesha namna
ambavyo usikilizaji wa mabiti yanayojirudia walahu Mara tatu au nne tu,
huifanya sehemu ya ubongo wa mbele kupoteza kabisa hamasa na kuuacha ubongo
ukiwa huru, kwa mihemko ya moja kwa moja ya mabiti, kutoka katika sehemu ya
hisia kupitia kitendo kinachoitwa "Entrainment". Sasa Basi, baada ya
ubongo kupoteza kabisa uwezo wake wa kushikilia umakini, Nini hufuata ambacho
huua ubongo.
Taaluma Ya Kuingiza Mitazamo Katika Ubongo Wa Msikilizaji
Bila Msikilizaji Kujitambua
Kuingizwa kwa falsafa za msanii katika
ubongo wa msikilizaji moja kwa moja, katika sehemu za hisia ambazo kitaalamu
huitwa "subconscious mind". Wachache Sana wanaoweza kujua hii mbinu
Makini Sana ya kisaikolojia, ya Hali ya juu. Sehemu za ubongo za hisia,
zinachangamana moja kwa moja na sehemu za kumbukumbu. Ndiyo maana, unapokumbuka
tu kitu, huja na hisia zake. Au watu hukumbuka Sana vitu vinavyowaumiza Sana,
au wafurahisha Sana, Kuliko wanavyokumbuka vitu vyenye mhemko mdogo wa hisia.
Mfano mwalimu aliyekuwa anachapa sana, utamkumbuka zaidi ya yule wa kawaida.
Sasa basi, kitendo Cha watu hawa kuleweshwa na mabiti, hata kuondoa uchujaji wa
kinachotakiwa kukumbukwa. ambayo ndiyo kazi ya prefrontal cortex, basi ubongo
wa kumbukumbu na hisia hupokea moja kwa moja mitazamo ya msanii. hata bila ya
msikilizaji kujua, Kama anawekewa kumbukumbu bila yeye mwenyewe kujua.
Madhara yake hujikuta msikilizaji
akiwa tayari ameshaambukizwa tabia, na falsafa za msanii wake, hata bila yeye
mwenyewe kuamua. Tuliona katika sehemu ya juu namna ambavyo wimbo wa matukano,
mtu angeogopa kusikiliza, lakini baada ya kusikiliza Mara mbili au tatu.
Hujikuta tayari ameweza hata yeye kuyatamka matukano yaleyale bila shida!!
Msanii anaweza kufundisha namna kadha wa kadha ya tabia za uchafu, na
msikilizaji ambaye hujidanganya kuwa anasikiliza tu Wala hatafuata, hujikuta
tayari na yeye akitenda yaleyale. Sheria Ni ile ile ya utendaji wa Miziki,
ambao, hufukuza kwanza mlinzi wa Ubongo. ambaye, Ni prefrontal cortex. na
kusisimua mifumo ya kumbukumbu ya fahamu, na kuingiza moja kwa moja falsafa
zake.
Ushahidi mkubwa unaweza kuangalia tu,
namna tabia za watu zinavyofanana, na Aina ya nyimbo zao wanazozisikiliza.
msikilizaji wa nyimbo zenye mabiti ya hip hop, ambayo hufahamika kwa sifa ya ku
"drain off" au kupumbaza kabisa mawimbi ya Beta waves ya kwenye
ubongo. na hatimaye kupelekea mtu kuingizwa falsafa za msanii, ambae Mara
nyingi huwa mtukanaji au mpinzani mwenye Hasira.
Kutumia Mabiti Ya Mawimbi Ya Mihemko
Ya Kingono Na Sauti Za Mivuto Ya Hisia
Mbinu hii huwasaidia Sana Wasanii
kuwalevya zaidi wasikilizaji wao. Kama msanii atatumia mabiti yanayoendana sawa
na frequency za matendo ya kimapenzi. kipindi Cha entrainment, Ubongo utahemka
zaidi kimsisimko huo huo wa mabiti, na msanii atakapoongezea na maneno yake.
Basi atapelekea kuwepo kwa mtu ambaye tayari Ni mlevi wa Mapenzi. Hii ndiyo
sababu Mara nyingi wasikilizaji wa nyimbo hizi, huwa wanamisisimko mikubwa Sana
ya kingono. ukilinganisha na wasio wasikilizaji, ni kwasababu huwa mifumo yao
ipo juu juu Sana.
Video Za Miziki Ya Midundo, Taa Za Mianga Hafifu Na
Maonesho Ya Taswira Za Kimivuto Ya Mapenzi
Nyimbo nyingi zimejaa video za mtindo huu. Utaona Wasanii wakiwa wamevaa kimivuto ya kimapenzi, wakiwa maeneo ya kuvutia, na mianga hafifu wanayoitengeneza kwa teknolojia nilizozielezea sehemu ya udanganyifu wa macho. Sasa hebu changanya vitu hivi vitatu kwa Pamoja, halafu uone Nini kinatokea katika Ubongo!!
Ubongo unakorogwa kabisa maana mfumo
mzima wa Fiziolojia ya kuona, inayohusiana na Imani pia, unakuwa umeshambuliwa
Kama tulivyoona kule juu. Lakini pia mfumo mzima wa Fiziolojia ya kusikia,
unaoambatana na kufikiria, unauwawa. Na
zaidi mfumo wa hisia, unasisimuliwa moja kwa moja, hii Ni hatari kubwa ambayo
madhara yake kwa kuangalia tu Mara moja, yanaweza mfanya mtu aathiriwe kwa
kiwango kikubwa Kama hatakuwa mraibu.
Watu wengi hudharau madhara haya, ili
Hali wao wakiwa ndiyo wahanga wakubwa zaidi wa kitabia, na wakipitia matatizo
makubwa wanayoshindwa kuyatatua, kwa kukosa kabisa uwezo wa kufikiria. Zama
hizi zenye changamoto zote, Kama tulivyoona katika sehemu iliyopita, changamoto
zote zimetokana na video hizi ambazo, ndizo ibada mpya katika kizazi Hiki Cha
hatari kabisa kuwahi kutokea.
INJILI YA SAYANSI TUNAKUPENDA SANA MSOMAJI WETU.
MAWASILIANO ZAIDI
DR. BRIGHTON GODWIN SHOO
+255 6139 069 30
brightonshoo7@gmail.com
Kupata full soft copy link👇👇👇
















Join the conversation