INJIILI YA SAYANSI Q5
INJILI YA SAYANSI Q5
Injili ya sayansi Q5 ni kitabu kinachoangazia tofauti za
ubongo wa jinsia ya kiume na ubongo wa jinsia ya kike. Kwa karne nyingi sana,
tofauti juu ya namna ubongo wa kike na ubongo wa kiume unavyo tofautiana,
zimekuwa zikitafakariwa kwa changamoto kubwa sana. Hii ni kutokana na uwepo wa
teknolojia ndogo sana ya mbinu za kiutafiti, za sayansi ya ubongo kwa hapo
awali. Si rahisi na haiwezekani kwa mtu asiyemtaalamu au mzoefu wa taaluma za
ubongo kuweza kugundua tofauti za ubongo wa mwanamke na wa mwanaume kwa
kuuangalia kwa nje.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutambua sifa mbalimbali za
ubongo wa kike na wa kiume kisayansi zaidi. Utambuzi husaidia kwanza,
kuondokana na mitazamo hasi kama ya kuamini hakuna tofauti za kijinsia katika
ubongo. pili, husaidia kujua tofauti na sifa mbalimbali za Ubongo kulingana na
jinsia Fulani. pia husaidia kujua ubora zaidi wa mpangilio wa asili kimajukumu
na ufanisi zaidi, pale mtu wa jinsia Fulani, anapojijua zaidi sifa zake, na
kuutumia ubora wake.
Kitabu hiki hakina hoja zozote zinazoelekeza mitazamo juu ya
ubora wa jinsia moja zaidi ya nyingine kwa ujumla! Lakini kinatoa sababu bora
zaidi za kwanini jinsia moja huonekana bora zaidi ya jinsia nyingine katika
sifa Fulani, kutokana na tofauti za kijinsia.
Kitabu hiki kinamsaidia msomaji kujua msukumo wa sifa zake
nyingi sana, zinazotokana na msukumo wa jinsia yake, kutokana na mifumo ya mwili wake kijinsia, katika vipindi
vyote vya ukuaji. Na kinasaidia sana wazazi na walezi, kujua namna wanaweza
kuwasaidia Watoto na vijana wao, kutokana na shida za ukuaji, ambazo kama mtu
ataelewa msingi wake, basi atajua namna
ya kushughulika nazo.
Kitabu hiki kina malengo mengi sana, na miongoni ni kupambana
na matatizo mengi sana yanayotokana na kutoelewa tofauti za kijinsia. na
kupelekea kufeli kwa majukumu baadhi kiutendaji, kwa kuchanganywa
kimtazamo hata watu wakaamini wanawake
na wanaume ni matokeo tu ya mabadiliko kadhaa, na hata, wanaweza wakabadishwa
kuwa namna yeyote ile. Pia msomaji ataelewa ubora zaidi wa Ubongo wa wanawake,
na ubora zaidi wa Ubongo wa wanaume. hii
itamsaidia kujua thamani ya tofauti zetu za kijinsia, na namna bora zaidi ya
kunufaika nazo kama zawadi ya asili. na pia hata kuvumuliana panapotokea
udhaifu unaotokana na tofauti za kijinsia.
Changamoto kubwa zaidi katika kitabu hiki ni namna nyepesi ya
kuwasilisha ajenda baadhi kwa baadhi ya wasomaji walioathiriwa na mitazamo ya
kiugandamizaji ya kijinsia, kama wanaume wanaoamini kuwa wao, ni kichwa kwa
kila jambo, au wanawake ni wadhaifu kiuwezo kwa ujumla! lakini pia wanawake wanaoamini wao wanaweza
kila jambo, na wamekuwa wakikandamizwa kifikra. Pia kuna changamoto ya tabia za
Ubongo wa Mashoga ambao hutumiwa na baadhi ya wanasayansi kama ishara ya kutokuwepo
kwa uthabiti wa mipaka ya kijinsia, kitabu hiki kinatoa majibu mazuri zaidi ya
kuondokana na fikra hizo.
Ubora wa kitabu hiki ni namna ambavyo hakijaegemea katika mitazamo ya kifalsafa, lakini kimejikita katika matokeo ya tafiti ya kisayansi, hasa sayansi ya Utendaji wa Ubongo ‘’Neurology’’, saikolojia ‘’psychology’’, Sayansi za mifumo ya homoni ‘’Endocrinology’’, Tafiti za Sayansi ya Ubongo kwa Ujumla ‘’Neurosciences’’, Mitazamo ya kijamii ‘’Cultural Views’’ na mwisho zaidi ni Biblia ‘’Bible’’ ambayo hujenga msingi hasa panapobakia makisio katika Sayansi Za mabadiliko ‘’Evolutionary Sciences’’.
SHUKURANI
Kwanza kabisa Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kuelewa kiundani swali nililokuwa nikijiuliza
sana awali ‘’Kuna maana gani ya Mungu kuwa wa Haki na Usawa, kama aliamua
Kuumba Jinsia moja kuwa Bora zaidi ya nyingine? Na akawa anachagua mmoja
kuzaliwa mdhaifu na mwingine kuwa mwenye nguvu? hakuna anayechagua kuzaliwa
jinsia yeyote ile! mtazamo wowote ule uliojikita kuamini kuna Jinsia moja Bora
zaidi ya nyingine Kwa Ujumla, umejengwa katika msingi wa kuamini Mungu ni
mgandamizaji (hii ni hoja pendwa kwa wanasayansi wasioamini wakisema’’Vitabu
vya Imani vina ukandamizaji wa kijinsia’’), ni kweli wapo sahihi Kwa kuwa
hawaelewi kiundani.
Nilianza kuamua kuandika
baada ya kugundua hisia za maumivu ya ugandamizaji kijinsia kwa karne
nyingi nyuma, zimepelekea misukumo mingi hasi, ambayo inapelekea kila kukicha
kutokea kwa madhara makubwa katika ngazi za mifumo mikubwa mpaka kwa mtu mmoja
mmoja, kwa kutojua nini kipo nyuma ya Ubongo kwa kila jinsia. Na kibaya zaidi, wanataaluma wengi sana, na
wazazi, hawajui namna bora kabisa za kushughulika na changamoto za kijinsia, na
malezi yamekuwa ni shida kubwa mfano wake haujawahi tokea!
Natambua mchamgo mkubwa sana wa familia yangu, Mama yangu
Dementina F. Mkote, Baba yangu Godwin
E.Shoo, Ndugu zangu Neema, Catherine, Grayson, Eunice, Victor, Alen, Peter,
Stanley, Bruno, Beti, Daudi, Alestida, Judith na Gracious Shoo. Shangazi zangu
Lilian Shoo, Anith Mkote, Alfonsina Mkote na wenginewe, wajomba zangu Mario
mkote, Frank Mmary, Ernest Shoo, Ignas Mkote, Francis mkote na wenginewe. Bibi
yangu Betila Mkote. Familia yangu imechangia sana mtazamo wangu mpana wa
thamani na tofauti za kijinsia, bila kuathiriwa na falsafa hasi, na hii ni
kutokana na kutanguliza msingi wa Biblia, na Uzoefu wa kujifunza elimu za
sayansi, tamaduni na Jamii.
Natambua mchango mkubwa sana wa marafiki zangu, Dr. John ,
Dr. Emannuel, Dr.Mpogo Issa, Dr. Magessa, Dr. Mathew, Dr. Anatory, Dr.
Mwangosi, Dr. Alex, Dr. Eric, Dr. Pascal, Dr. Bernard, Dr.Mpoki, Dr.Salim, Dr.
Luckydube Mwaipape, Dr. Martina mgeni, Dr. Zephania bertha, Dr. Sweetbeth,
Dr.Winston, Dr.Adela, Dr. Ntemi, Dr.Masasila, Dr. Kajange, Dr. Kapinga,
Dr.Aidan, Dr. Daniel, Dr.Edison Kavenuke, Dr.Aweza james, Dr.Manyerere,
Dr.Gilbert Shayo, Dr. Juma, Dr. Joshua, Dr. masasila, Dr. Amos, Dr. Careem,
Dr.Chedela na wenginewe. Hawa wamekuwa Pamoja na mimi katika hatua mbalimbali
nilizokuwa nikijifunza kwa undani sifa mbalimbali za tofauti za kijinsia kwa
Wanyama, na kwa binadamu.
Natambua mchango mkubwa sana wa marafiki zangu, waliokuwa
wakinisapoti katika kipindi naendelea na uandishi wa kitabu hiki, Edward Singo,
Hagai, Samuel, Bright na Amara nyongole, Ernest B Jonass, Katemi, Miss Esta,
Mr.Kanolo, Mr. Alex, Mr. Nyange, na wenginewe.
Natambua mchango mkubwa sana wa mtaalamu wa Ubongo na afya ya
akili ‘’neuropsychiatrist’’ Mama Louann Brizendine, ambaye amekwisha Andika
kitabu kuhusiana pia na tofauti za kijinsia, Nimetumia nukuu zake baadhi, japo
si kwa baadhi zilizo na mashaka! kuna tafiti nyingi sana ambazo nitatoa nukuu
kwa heshima ya watafiti. Kumbuka yapo masomo mengi ambayo yanaunda upekee wa
kitabu hiki, ukiachana tu na nukuu zilizokwisha nukuliwa kwa vitabu na tafiti
mbalimbali.
USHAURI WA NAMNA YA KUSOMA NA MATUMIZI YA LUGHA
Kwa mtu ambaye hatakuwa na msingi mzuri kabisa wa masomo ya
sayansi, anaweza kuanza kusoma sura ya tatu na sura ya nne. Lakini pia anaweza
pitia sehemu kadha wa kadha katika sura ya kwanza na sura ya pili. Kitabu hiki
kinahusisha matumizi ya lugha ya Kiswahili, na matumizi ya lugha ya kiingereza
kwa maneno na vitendo visivyo na tafsiri za Kiswahili za moja kwa moja.
Uchambuzi kadhaa ambao unaweza onekana kuwa ni wa kina sana, una malengo mapana
zaidi ya kuziondoa hoja hatarishi za kifalsafa, na mitazamo hasi isiyo na
misingi ya ukweli.
pia kitabu kinahusisha matumizi ya visa vya wahusika kwa sehemu baadhi ya sura ya tatu, na sura ya nne. wahusika hawa na visa vyao ni vya kutungwa. msomaji anapaswa kutambua njia pekee bora zaidi ya kuileta sayansi ya kina katika jamii, ni kupitia kurejelea tabia zilizozoeleka.
YALIYOMO
MSINGI WA TOFAUTI ZA UBONGO KULINGANA NA JINSIA
KWANINI MSUKUMO WA KUSOMA TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA
NI MDOGO?
KWANINI INAPASWA KUJIFUNZA TENA SAYANSI YA UTOFAUTI WA
UBONGO KIJINSIA?
MAKUNDI MAKUBWA MATATU YA TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA.
AINA YA KWANZA YA TOFAUTI ZA KIJINSIA
AINA YA PILI YA TOFAUTI ZA KIJINSIA
AINA YA TATU YA TOFAUTI KIJINSIA
Jambo Moja laweza leta madhara tofauti kwa jinsia ya
kike na kiume!!
NAMNA JENETIKIA NA HOMONI ZINAVYOSABABISHA JINSIA YA
KIUME NA KIKE
NADHARIA ZA UTOKEAJI WA MASHOGA AU USHOGA
Sababu za maendeleo ya ukuaji tumboni
Sababu za Mama kuzaa Watoto wakiume wengi
Sababu za jenetikia za Kinasaba cha Ushoga ‘’Xq28’’
Kielelezo kwa Kondoo na ushoga
Kielelezo cha mapacha na ushoga
Ushoga na faida za ‘’natural selection’’
Sababu za Ushoga kwa tafiti za kisaikolojia
MAFANIKIO MAKUBWA YA NADHARIA ZA USHOGA KWA JAMII ZA
WASOMI
MAFANIKIO MAKUBWA YA NADHARIA ZA USHOGA KWA JAMII ZA
WANA DINI
JE UNAWEZA WAJIBU KUHUSU Xq28 (Gay gene-Kinasaba cha ushoga)?
Ushoga kwa namna nyingine ni Changamoto ya Kibiolojia
na sio Jinsia!!
Hakuna Hisia ya Asili ya Mwanaume kutamani Kuingiliwa!
Wanyama sio Kielelezo cha Ushoga!
NAMNA YA KUWASAIDIA MASHOGA KWA UPENDO
KINACHOUTOFAUTISHA
UBONGO WA KIUME NA WA KIKE
SEHEMU ZA UBONGO ZILIZOTOFAUTIANA KULINGANA NA JINSIA
Sehemu Za Ubongo Zilizoendelea Zaidi Kwa Wanawake
Anterior cingulate cortex (ACC)
Mfumo wa Hisia wa Kuiga na kuhisi Huruma ‘’Mirror
Neuron system’’ au MNS.
Mfumo wa kuchunguza na kuzisoma Sura za Vitu na
uzingatiaji.
Uwezo mkubwa wa kutumia Lugha na kutumia maneno
‘’Verbal skills’’
Upana wa Ubongo ‘’cortical thickness’’
HOMONI ZENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWA WANAWAKE
DHEA au ‘’Dihydroepiandrostedione’’
SEHEMU ZA UBONGO ZILIZOENDELEA ZAIDI KWA WANAUME
Temporal Parietal Junction (TPJ)
Tatizo vs mwanaume vs mwanamke!!
Dorsal Premammilary Nucleus ‘’DPN’’
Rostral Cingulate Zone ‘’RCZ’’
Ventral Tegmental Area ‘’VTA’’
Uwezo wa kuchakata taarifa kwa kuumba Maumbo ya
Taswira Kichwani. ‘’Spatial Skills’’
Ukubwa wa Ubongo kwa Ujumla ‘’brain Volume’’.
HOMONI ZENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWA WANAUME
Mullerian Inhibiting Substance ‘’MIS’’.
Baba ana dalili za ujauzito Kama mkewe!
NADHARIA ZA
UTOFAUTI WA UBONGO ZILIZOPITWA NA WAKATI
WATU WALIOENDELEA ZAIDI KATIKA UBONGO WA KUSHOTO AU
UBONGO WA KULIA
‘’left brained or right brained’’
WATU WALIOBORA UPANDE WA KUSHOTO ‘’left brained’’
WATU WALIOBORA UPANDE WA KULIA ‘’right brained’’
CHANGAMOTO KUBWA ZA HII NADHARIA
NADHARIA ZA KUWA UBONGO WA KIUME NA WA KIKE NI SAWA
KABISA!!
MSINGI WA HISIA ZA UGANDAMIZAJI WA KIJINSIA
ULIOFICHIKA!!
TATIZO LILILOIBUKA KARNE YA KUMI NA SABA NA KUMI NA
NANE!
SABABU ZA UBORA WA WANAUME KATIKA HISABATI NA FIZIKIA
UHALISIA KUWA UWEZO WA HISABATI NA FIZIKIA SIO UWEZO
MKUBWA WA KIAKILI!
MGOGORO WA KIJINSIA WA NAFASI ZA JUU KABISA ZA UONGOZI
UBONGO NA SIFA ZA MWANAMKE KATIKA VIPINDI MBALIMBALI
VYA UKUAJI
UBONGO WA
KATOTO KAKIKE TUMBONI
KATOTO KA KIKE KAZURI! DADA HELLEN ‘’MIAKA 1-10’’
Lugha ya ‘’Twende!! au Tu...’’
Hellen na rafiki zake tu kina Eunice!!
UBONGO WA MSICHANA MZURI, MIAKA ‘’11-19’’
Safari Ya Mzunguko Wa Mawimbi Ya Estrogen Na
Progesterone
WIKI MBILI ZA KWANZA ZA MZUNGUKO!!
WIKI MBILI ZA MWISHO WA MZUNGUKO!!
KATI KATI YA MZUNGUKO WA MWEZI!!
UMESHAJUA KWANINI HUSHINDA NA SIMU!!
WASICHANA WANAPOFELI KWA WAVULANA!!
SIRI ILIYOFICHIKA ENZI HIZI KWA WAVULANA!!
ANALALA SANA HATA MPAKA SAA SITA!!
Je ni Kweli Ule Msemo wa ‘’Wanawake Wenye Miili
Mikubwa Hawana Shida?
TATIZO KUBWA LA KUWARUHUSU KUFANYA NGONO!!
MABINTI WENYE SIFA ZA KIPEKEE!!
UBONGO WA BINTI MZURI RACHEL ‘’MIAKA 20+’’
Sababu Za Mwanaume Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa
Binti!!
Sababu Za Binti Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa
Mwanaume!!
Muhimu Sana Kujua Kuhusu Mivuto Ya Kimapenzi!!
UBONGO WA BINTI ‘’RACHEL’’ KWENYE MAPENZI MAPYA
BIOLOJIA YA UBONGO WA RACHEL KWENYE PENZI JIPYA!!
Kwa Mara ya Kwanza Kuzima Kwa ACC &PFC Kwa
Rachel!!
Je Wajua Biolojia Pana Ya Kiss!!
NADHARIA ZA KUZIKATAA ‘’HAKUNA JENETIKIA ZA
UAMINIIFU’’
Maisha Baada ya Eunice Kuzaliwa!!
MAMA MBAYA HUTENGENEZA MAMA MBAYA!!
BIOLOJIA YA MIGOGORO MINGI YA WAMAMA NA WAUME ZAO
UBONGO WA MWANAMKE ULIOKOMAA ‘’MIAKA 51+’’
HUWA NA HASIRA KWA WAKATI FULANI HASA NA MME WAKE!!
VIPINDI NA SIFA MBALIMBALI KATIKA UBONGO WA WAKIUME
UBONGO WA KATOTO KA KIUME TUMBONI!
UBONGO WA WATOTO WA KIUME ‘’VICTOR NA ALEN’’ MIAKA
1-11’’
UKITAKA KUMTULIZA MPE GEMU AANGALIE!!
HANA MUDA WA KUKUANGALIA SANA!!
UKIMKATAZA NDIYO KAMA UMEMCHOCHEA!!
HAWAPENDI KUFANANISHWA NA WASICHANA!!
HUPENDA KUWA BINGWA AU MSHINDI!!
MWENZAKE NDIYE KIPAUMBELE CHAKE!!
UFALME KATIKA ULIMWENGU WA WAVULANA!!
NAMNA WANAVYOUNDA MAKUNDI YAO!!
HUPENDA SANA MAGEMU NA FILAMU ZA MAPAMBANO!!
UBONGO WA KIJANA WAKIUME ‘’MIAKA 11-19’’
HAELEWEKI NA HAPENDI UNACHOPENDA
BIOLOJIA YA NGUVU MPYA YA TESTOSTERONE!
SIRI YA MAWAZO YA KIJANA WA KIUME TU!!
HISIA ZA KUBOREKA NA KULALA SANA!!
HISIA ZA KUTOKUBALIANA NA TARATIBU!!
MGOGORO WA PETER, CAREN NA MWALIMU NYAGAWA!!
BIOLOJIA YA CHANZO CHA MGOGORO WA PETER!!
TABIA ZA UBABE NA MIONEKANO YA UGUMU!!
HAPENDI KURUDIA RUDIA NA SAUTI ZA MAKELELE!!
MWONEKANO WA KUJIFANYA HAJALI!!
HUJIDANGANYA WAO NDIO WANAJUA!!
UJINGA HUZIDI WANAPOKUWA PAMOJA!!
MSINGI WA NGUVU ZA MAKUNDI RIKA
HUANDALIWA KISAIKOLOJIA KUFANYA MAPENZI KIMAWAZO!!
UBONGO WA KIJANA WA KIUME, MIAKA 20+
MSINGI MKUBWA ZAIDI WA UFANYAJI KAZI!!
UBONGO WA KIUME ULIOKOMAA!! MIAKA 50+
UNAWEZA
SOMA SURA IFUATAYO FREE.............
kumbuka kufahamu msingi wa sifa zote za tabia za kike, kama inavyoelezwa katika sura hii, unapaswa kurejea tena kusoma sura za mwanzo zinazoelezea kiundani zaidi mifumo ya ubongo wa mtoto wa kike.na pia, sifa nyingi zimeelezwa katika sehemu inayodadavua zaidi utofauti wa ubongo, na sifa zake. kwa wanaume, na wanawake. toka uundwaji wa mimba, mpaka uzeeni. sura ya tatu inadadavua utofauti zaidi katika mifano michache ya visa vya maisha ya uhalisia ya kijinsia.
SURA YA 3
UBONGO NA SIFA ZA MWANAMKE KATIKA YA VIPINDI
MBALIMBALI VYA UKUAJI
Utangulizi
Zipo hatua kadhaa za ukuaji wa mwanamke. Katika hatua
hizi, ni muhimu kutazama sifa na mabadiliko ya msingi kabisa katika kila hatua,
ili kuweza kujua sifa kadhaa za msingi kabisa, ambazo hujenga msingi wa tabia
kadhaa kwa wanawake, katika vipindi mbalimbali vya ukuaji.utambuaji wa sifa
hizi huleta faida kubwa sana ya kuwawezesha wasomaji kujua namna bora kabisa ya
kujitawala au kujijibu maswali kadhaa ya kwanini tabia Fulani hutokea zaidi kwa
kipindi Fulani, na zina lengo gani?
UBONGO WA
KATOTO KAKIKE TUMBONI
Seli zake za ubongo huwa zina chromosomes za (XX), hii
ina maanisha kuwa, huwa zina vinasaba au genes za ukuaji wa ubongo kwa fasta
zaidi, na ubongo hukua ukitengeneza Zaidi network za ubongo, zitakazo sapoti
zaidi tabia za kike. Na hasa huwa katika sehemu za mawasiliano, hisia za
vyakula na mfumo mzima wa ulaji, kumbukumbu za kihisia, mifumo ya kupambana na
hasira. na huku kwa wanawake, huwa haya maendeleo yanafanikiwa kutokana na
Ukosekanaji wa kiwango kikubwa cha Testosterone, ambayo ingeua baadhi ya seli,
na kuzuia maendeleo mapana zaidi ya sifa hizi. Ubongo wa kike huanza kuwa na
uwezo wa kutumia pande zote mbili za ubongo, vizuri kabisa, tokea hatua za
awali kabisa za ukuaji.
Katika hatua hizi za awali ni muhimu kwa mama kutokuwa
na changamoto za misongo ya Mawazo, hii ni kuzuia kuzalisha chembechembe za
stress hormones ‘’cortisol’’, na pia stress na mifumo mibaya ya ulaji,
hupelekea kiwango kikubwa sana cha ‘’free radicals’’, ambazo huenda kuathiri
maendeleo bora ya ubongo wa mtoto.
Maendeleo mapana ya biolojia yanaonesha kuwa, tofauti
na mitazamo ya awali ya kuwa madhara huwa yanamkuta mama kwanza, na kisha kurithishwa
kwa mtoto, au unaweza uita huu mtazamo kama ‘’weismann barrier’’,sasa hivi
inafahamika kuwa, madhara humuathiri mama mpaka seli zitakazo muunda mtoto moja
kwa moja. Kwa hiyo, hata kabla binti hajazaa, tayari kila anachokifanya,
anamuathiri na mtoto wake!
Ni muhimu wamama wajawazito kutokuwa na stress kabisa,
haijalishi ni ujauzito wa mtoto yupi, lakini pia ni muhimu kupunguza na
ikiwezekana kuachana kabisa na ulaji wa bidhaa za kisasa, ambazo huwa na
chembechembe nyingi sana za utunzaji chakula, ambazo huwa na madhara kama
tulivyoona katika injili ya sayansi sehemu ya nne.
Mama anapofurahi zaidi, ndivyo na mtoto wake anapokuwa
na faida kubwa zaidi ya maendeleo ya ukuaji wake wa ubongo, ikiwemo na
kuongezeka kwa ufanisi wa mifumo ya kinga, kupunguza hatari za makosa ya ufundi
wa kijenetikia n.k.
miziki yenye sauti kubwa sana sio mizuri pia, kwa
kuwa, frequency kubwa huweza kuathiri utendaji bora wa jenetikia, tuliona
sehemu ya nne kuwa, DNA ni sensitive sana kwa muziki, hivyo ni muhimu kuchukua
hatua kwa wamama wajawazito, hasa wa zama hizi za midundo mikubwa kila wakati.
Kuchelewa kulala pia huongeza muda wa mzunguko wa cortisol, hivyo uangaliaji
sana wa tamthilia usiku kwa wajawazito unapaswa kuwa na kiwango, kama lengo
litakuwa ni kuzaa binti mwenye akili kama mama yake!!
KATOTO KA KIKE KAZURI! DADA HELLEN ‘’MIAKA 1-10’’
Uwezo wa kuzisoma sura
Sifa ya kwanza ya katoto haka tukaite ‘’Hellen’’, ni
uwezo wa kuzisoma sura! Ubongo wa mtoto wa kike huzaliwa ukiwa upo mbele
kiukuaji kwa mwaka mmoja mpaka miwili mbele, zaidi ya ubongo wa mtoto wa kiume.
Mtoto hellen amezaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kuzisoma sura na kuelewa hisia
za anao waangalia. Wamama wengi ambao huanza kulea Watoto wa kike na kisha kuja
kulea Watoto wa kiume, huisi penginepo Watoto wao wakiume wana shida au
penginepo hawavutiwi sana nao, kwa namna ambavyo huwa hawana muda wa kutazamana
na mama zao kwa kitambo kidogo, kama ambavyo huwa kwa Watoto wa kike.
Hellen hakuathiriwa na kiwango kikubwa cha
testosterone kipindi yupo tumboni, ambacho kingeua seli na mifumo yake ya
kuweza kuelewa mawasiliano na hisia za wengine. Na anapozaliwa tu huwa kwa
haraka sana akiwa na uwezo wa kuwasoma anaowatazama! na kugundua kama ni watu
wenye upendo au wenye kuweza kumhatarisha.
Tafiti iliyofanywa kwa chumba ambacho kilikuwa na
wamama kadhaa na Watoto wao wa kike, na wakiume. na wamama hawa wakapewa kazi
ya kuwazuia tu Watoto wao wasishike moja ya vitu vilivyokuwepo mle ndani, kwa
kuwaangalia tu na kuwakazia macho! Tafiti ilionesha kuwa, Watoto wote wa kike,
wakina Hellen, baada tu ya kuwaangalia mama zao, waliacha kabisa kushika sehemu
ile. Ila Watoto wakiume, wakina victor na alen na wenginewe, ni kama vile mama
zao waliwachochea zaidi kutaka hata kujua zaidi kuna nini pale! Haimaanishi
kuwa Watoto wa kiume ni wakaidi! Ila ina maanisha kuwa, Watoto wa kike huzaliwa
na uwezo mkubwa zaidi wa kuzisoma sura, uwezo huu huwa ni miaka miwili zaidi ya
Watoto wa kiume, ambao nao huja kuupata mbeleni. Inafahamika zaidi kisayansi
kuwa, Watoto wa kike hupitia kipindi kinachoitwa ‘’Infantile puberty’’, kipindi
ambacho huusiana na uzalishwaji wa estrogen nyingi sana, kama ilivyo kwa binti
mkubwa, kwa muda wa miezi 24 toka kuzaliwa! huku Watoto wa kiume wakipitia
kipindi hichohicho kwa muda wa miezi 9 tu. Kipindi hiki huaminiwa kuwawezesha
zaidi Watoto wa kike katika uwezo wao wa ubongo, wa kuchakata taarifa za
mazingira yao.
Kwake hellen unapomtazama, ndipo unamsikiliza,
ukimsikiliza huku unatazama kwingine, ni kama vile huna muda naye, na
hatalifurahia hilo! Hii ni kutokana na Imani yake ya kuwa ulimwengu umejawa
watu wenye aina moja ya kuelewa mawasiliano kama yeye.
Hellen haitaji stress!!
Mazingira ya hellen kwa miaka yake miwili ya kwanza
duniani humjengea uhalisia wa Maisha yake yote! Hii hatari imeonekana kwa
tafiti za Wanyama mammalia wote, mtoto wa kike huathiriwa sana na madhara ya
mazingira yake, mapema zaidi, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchangamana na
mazingira yake. Kitaalamu hii inaitwa ‘’epigenetic imprinting’’, ni kama
ambavyo nilivyoielezea katika sehemu za awali kabisa za tofauti za kijinsia.
Tafiti huonesha kuwa, Wamama wenye misongo ya Mawazo au stress, huwa sio
waleaji wazuri wa Watoto wao, na Watoto wao wakike, huathiriwa moja kwa moja.
Na huchukua uhalisia wa mama zao kama ndiyo uhalisia wa dunia. Na huu ndiyo
msingi wa uwepo wa wadada wenye sifa tofauti tofauti, mara nyingi haya ni
matokeo ya mama wenye uleaji tofauti tofauti. Watoto wa kiume wameonekana
kutoathiriwa na stress za mama zao katika mifumo yao ya fahamu. Kwa hiyo ni
muhimu kupanga kuwa na mama asiye na misongo ya Mawazo, kama unapanga kuwa na
Hellen mzuri.
Usipigane Hellen!
Hii ni sauti ambayo mara nyingi zaidi husikika katika
kichwa chake. Ana uwezo mkubwa wa kusoma sura na kuzijua hatari na akachukua hatua
ya kujiepusha mapema sana. Inatambulika uwezo huu kwa wanawake wa kuzisoma sura,
hujengwa tangia awali kabisa, kwa lengo la kuwawezesha kuzungumza hata na
vitoto vichanga, visivyoweza jielezea. Uwezo mkubwa wa kujua madhara ya hatari
ya kupigana, kwa kuweza kudhibiti hasira, huchochea tabia za kupenda kufanya
amani.
Lugha ya ‘’Twende!! au Tu...’’
Hellen na rafiki zake hupenda kuanzisha shughuli zao
au michezo yao kwa kutumia lugha ya kuwaunganisha Pamoja. Mfano, tujenge
nyumba, twendeni pale, tukapike, n.k.
utasikia akisema, ‘’unaweza niazima ndala zako za kijani! Na mimi nakupa
zangu nyeupe, afu baadae nakurudishia!’’ hii lugha tayari imeshaonesha kujali
na kujilinda. Watoto wa kiume huwa hawawezi kutumia lugha hii kirahisi, ingawa
wanaijua pia, Victor huanza kwa kusema ‘’twende pale dogo! Au kama hauji..’’
hutumia lugha za kulazimisha sana au kutojali hisia za wenzao. Hii nayo
hutokana na uwezo wao mdogo kwa nyuma ya miaka kidogo zaidi ya Watoto wa kike
wanapozaliwa. Watoto wakike wanapotumia hii lugha ‘’affiliative speech’’, huwa
ina nguvu sana, maana, kama mwenzake atakataa! Atajiona mwenye ukatili na
kutojali, lakini kikubwa zaidi, pale anaposema ‘’unaweza..’’ anamaanisha,
utakaposema , Hapana!! Yeye bado yupo salama, maana alikupa tu pendekezo
‘’suggestions’’ na sio kwamba alikuwa amekutegemea sana! Hizi ni akili nyingi
sana.
Hellen na rafiki zake tu kina Eunice!!
Kati ya miaka miwili mpaka sita. Utakuta mara nyingi
sana kina hellen wakicheza na marafiki zao tu wasichana, mara chache sana
huvutiwa na wavulana. Hii ni kutokana na ndani ya dakika chache tu za kucheza
na victor au alen, atajikuta akilia machozi pasipokuwa na chochote mkononi
mwake! Watoto wakiume huwa ni wakorofi kutokana na uwezo wao mdogo wa kujali
hisia za wenzao. Tafiti za magonjwa ya upweke na kutopenda kuchangamana na
kushindwa kabisa kuwa na uwezo wa kukua kiakili ukielewa mazingira yako, ugonjwa
wa ‘’Autism’’. huonesha kuwa, ugonjwa huu huwa mara Nane zaidi kwa Watoto wa
kiume, ukilinganisha na watoto wakike. Hivyo, unaweza pata picha ni kwa namna
gani ambavyo Watoto wa kiume hata bila kuwa na shida hii, huwa na uwezo mdogo
wa kujali, na huku msukumo wao wa homoni za testosterone, ukiwafanya kuanza
kupenda kushindana tangia hatua ya awali kabisa. Hizi sababu humfanya hellen
kuamua kuchukua hatua ya kutafuta wenzake tu wanaoelewana.
Hellen ana misingi yake!!
Usije ukadanganywa kwa sababu ya kumuelezea kuwa ana
uwezo mkubwa wa kujali, na kuelewa! ukahisi unaweza muendesha unavyotaka!
Takwimu zinaonesha Watoto hawa wa kike hupuuzia jambo kama wakiliona halina
maana kwao mara Ishirini zaidi (20x) ya Watoto wakiume. Hellen utamwona na
wenzake wakipendelea michezo ya midoli, ambayo hupenda kuichezesha kuhusu
ajenda za kijamii kama familia, mipangilio n.k. kumbuka Watoto wakiume huitumia
hata midoli ya amani kama magari ya kivita! Takwimu pia huonesha kiwango kidogo
sana cha testosterone kwa wasichana, huwafanya wawe watulivu zaidi katika tabia
zao, ukilinganisha na wenye kiwango kikubwa, ambao huweza hata kuwa ‘’Tom
Boys’’. Mara nyingi Msichana anapotaka kutawala, hujiongezea hatari ya
kuwapoteza wenzake! na hivyo hutumia akili kubwa sana katika kubalansi mambo
hayo mawili.
UBONGO WA MSICHANA MZURI, MIAKA ‘’11-19’’
Kichwani mwake mrembo huyu
Hapa shughuli ndipo huanza!! Miaka ya kumi na kitu au
‘’teenage years’’ huwa ni changamoto sana. Ubongo wa binti hujifuma tena upya,
hukata matawi ya mifumo ya awali, hubadilisha mtazamo wa namna alivyokuwa
akifikiri na kuhisi na kutenda. Humfanya kuwa mraibu wa mwonekano wake,
humfanya kujiona amekuwa mwanamke haswa, biolojia yake hubadilika kuingia
katika hatua ya kupevuka au kuvunja ungo, na hapa kipimo chake huwa ni namna
jamii yake inavyomtazama. Sasa hivi, walimu
wake huwa ni wasichana wenye mionekano mizuri zaidi ya mvuto kwa
wanaume.
Kuteka umakini wa wanaume sasa ndiyo msingi wa hisia
ya kujiamini. Uraibu wa Kuwaza zaidi ya namna atakavyoonekana, huchochewa na
kiwango kikubwa cha homoni za estrogen, ambazo hupamba moto zaidi kwa kipindi
hiki. Wasichana hawa hujali sana mionekano yao ya kuvutia hasa wanapokuwa
wakichangamana na wavulana. Wamama kadhaa hulalamika namna mabinti wao
wanavyovutumia muda mrefu zaidi bafuni na mbele za vioo, hutamani kama
ingewezekana basi, viuno vyao vingekuwa vyembamba zaidi, makalio yao yakatanuka
zaidi na matiti yao yakaongezeka zaidi. Hayo na mengine mengi zaidi hulenga
hasa kuwateka wavulana zaidi!
Huweza kupata Mawazo mengi sana, lakini hasa
yaliyolenga zaidi, je mwonekano wao unaonekana ni wa mvuto kwa wavulana au la!
Hii ni kwa kuwa ubongo wao huwatengenezea uhalisia mpya, wa kuwa na mvuto ndilo
jambo la msingi zaidi.
Wasichokijua Wazazi!!
Wazazi wengi hawajui kuwa kinachotokea zaidi katika
hatua hii ni kuwa, ubongo wa mwanamke hupitia katika hatua ya kujikamilisha,
ukigongelea msumari ya kuwa, Je, amekuwa mwanamke kweli? katika hatua zote za
maendeleo yake ya kuwa mwanamke, je sasa, anaonekana na kukubalika kweli kama
mwanamke, anaonekana kama taswira ya mwanamke kweli anayefahamika na wanaume!
Hivyo hapa ubongo hufanya mithili ya majaribio kujipima kama umefanikiwa
kumuunda mwanamke. Ni kama ilivyo kwa mitihani mingine, kabla ya kuaminiwa kuwa
umekidhi kuwa daktari, unapaswa kujipima, je, naweza pambana na kesi ya mgonjwa
na akapona? Na yeye huwa hivyo hivyo, je? Naweza mvutia mwanaume? hii huitwa
pia ‘’Self-esteem’’. Wazazi wanapaswa kuwasaidia Watoto wao kwa kuwaongezea
uwezo huu wa kujiamini. Mara zote huwa tunasema kuwa, saikolojia ni matokeo ya
fiziolojia, kwa hivyo, kutopitia hatua hii yaweza kuwa ni matokeo ya matatizo
yaliyo makubwa zaidi! Wazazi baadhi hushindana sana na Watoto wao wakiwaona
kama vile wanataka kuwa wahuni, na wengine hata huwalinda kwa kuwafungia!
lakini kumbe huwa tu ni vipofu wa sayansi hii ndogo. Mzazi anapaswa kuwa karibu
na mtoto wake akimuongezea zaidi hisia za kujikubali na kujiamini, na anapaswa
asimtengenezee mazingira ya kumbana. ila anapaswa kumtengenezea msingi wa
kujitambua hatua anayopitia. lakini pia anapaswa kumuonesha madhara kama
hatojua sababu ya msukumo wake. ambayo yanaweza kumpeleka katika tabia chafu za
kuiga na uzinzi!
Safari Ya Mzunguko Wa Mawimbi Ya Estrogen Na
Progesterone
Kwa mara ya kwanza tena tangia kile kipindi cha
‘’infantile puberty’’ ndipo Ubongo wa binti unaanza tena kupitia vipindi vya
kuwa na uwingi mkubwa sana wa homoni ya estrogen, ambayo itakuwa ikifuatana na
Progesterone. Homoni hizi huwa zikiwa katika mzunguko ambao unaongozwa na
sehemu ya Ubongo ya Hypothalamus, ambayo huambatana na Tezi yake kubwa ya
Pituiatary gland, hii huendelea mbele zaidi na kusisimua zaidi tezi ya uzazi
‘’ovaries’’. Kwa Pamoja hii chain huitwa ‘’Hypothalamo-pituitary-ovarian
axis’’. Huwa ikipelekea mabadiliko ya homoni kati ya siku na siku na hata mwezi
na mwezi.
Haya mabadiliko ya kihomoni huufanya ubongo wa
mwanamke kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuhisi au ‘’more sensitive’’ kwa maswala
ya kihisia ‘’emotional nuance’’ , kama vile kukubalika, kukataliwa, kupendwa au
kuchukiwa. Siku zake zingine huwa na ujasiri mkubwa sana, lakini siku zingine
ujasiri wake hupungua kidogo, alipokuwa mdogo alikuwa ana uwezo wa kuhisi hisia
nyingi sana zaidi ya mtoto wa kiume, lakini sasa uwezo wake umekuwa mkubwa
zaidi. Sasa hivi kuna siku utamuambia, nguo yako imekubana sana atakuelewa,
lakini kuna siku ukimuambia hivyo, atatafsiri tofauti kabisa, atasikia
umemwambia kuwa, yeye ni mnene au kibonge sana, na hapaswi kuvaa hiyo nguo!
Tafiti zinaonesha wazi kabisa kuwa sehemu za ubongo za
Hippocampus, hypothalamus na amygdala zina athiriwa na homoni za estrogen na
progesterone. Sehemu hizi Zimeonekana kuwa na receptors nyingi sana za hizi
homoni, hivyo huwezi kupingana na huu ukweli kuwa, tofauti za homoni kwa
vipindi mbalimbali, humpelekea mrembo huyu kuwa na matokeo mbalimbali ya
tafsiri katika ubongo, zinazotegemeana na hivyo vipindi.
Hii picha nimenukuu toka jarida lililoandaliwa na (
Jordan Marrocco, PhD; Bruce S. McEwen, PhD) lililokuwa likielezea tofauti za
kijinsia katika Ubongo, hapo anaonesha sehemu ya ubongo inayohusiana na
kumbukumbu, namna inavyoathiriwa na homoni za estrogen kutokana na kuwa na
receptors za estrogen, anaonesha kuwa, Estrogen hushiriki hata katika uundaji
wa kumbukumbu au ‘’synapses’’, lengo kubwa ni kuonesha kuwa, mabadiliko ya
homoni yana matokeo makubwa sana yanayofahamika sasa hivi katika sehemu mbalimbali
za ubongo. na hivyo basi, tegemea kuwa, vipindi mbalimbali vya mzunguko
havitakuwa na matokeo yaleyale katika namna binti atakuwa akiyachukulia mambo.
Kuhusu Stress!!
Watafiti toka chuo cha Pittsburg cha Saikolojia,
waliwasoma Watoto tokea miaka saba mpaka miaka kumi na sita, waliwatazama
katika kipindi chote, hata wanapoingia katika kupevuka au kuvunja ungo kwa
wasichana, na kubalehe kwa wavulana. walikuwa wakiwaangalia namna ambavyo
wanasisimuliwa na stress kutokana na uzalishwaji wa homoni ya cortisol. Waliona
kuwa, wasichana wakionesha kuguswa sana na matokeo ya cortisol, ukilinganisha
na wavulana. Kitu walichogundua ni kuwa, mapishano ya homoni za estrogen na
progesterone huleta matokeo makubwa sana katika sehemu hiyo ya ubongo ya
Hippocampus, na hiyo ndiyo huchochea zaidi stress. Wasichana hupata stress
zaidi kwa vitu tofauti na vinavyowapa stress wavulana. Wasichana hupata stress
sana kwa vitu vinavyohusiana na mahusiano yake na wanaomzunguka na mazingira,
huku wavulana wakipata stress sana kuhusiana na changamoto za utawala au mifumo
ya kuwaendesha. Mahusiano na Maisha ya kijamii humpa stress sana msichana,
wakati, kuheshimiwa na kutawala huwa ajenda kubwa katika akili ya mvulana.
Umegundua filamu zake!!
Umri huu wasichana hupenda sana filamu za stori za
mahusiano au tamthilia zenye visa vya kijamii na mapenzi na usaliti, huku
wavulana wakipendelea sana mashindano ya mipira pamoja na filamu za ngumi na
kivita!!
WIKI MBILI ZA KWANZA ZA MZUNGUKO!!
Estrogen huwa juu sana, na msichana huwa yuko vizuri
sana, akionesha interest sana na jamii yake, huwa ame relax sana na wenzake.
WIKI MBILI ZA MWISHO WA MZUNGUKO!!
Progesterone huwa juu sana na estrogen huwa chini
sana, huwa na uwezekano mkubwa sana wa kutokufurahishwa, au ku react kutokana
na kuongezeka kwa hali ya kutotulia. na mara nyingi hutamani kuwa mwenyewe.
Alipokuwa mdogo alikuwa na kiwango kisichobadilika badilika cha estrogen,
ijapokuwa kilikuwa kidogo lakini alikuwa ametulia sana, lakini sasa kiwango cha
estrogen na progesterone kimekuwa kikubwa sana, hali hii inamuongezea uwezo
wake wa kuhisi au sensitivity kwa stress zinazotokana na homoni ya cortisol.
JE WAJUA UNAOUITA UMBEA!!
Wavulana wengi huwa hawaelewi kwanini wasichana wengi
huwa wanapenda sana kukaa kirafiki wakifanya kila kitu Pamoja, hata Kwenda
bafuni huongozana wakati mwingine, hupiga stori kila muda Pamoja, wakiwa
wenyewe zaidi! Hii ni kwa kuwa wanawake kibiolojia huwa na amani zaidi
wanapokuwa wao wenyewe zaidi, hii ni kwa kuwa wameendelea zaidi katika uwezo wa
Lugha na kuelewa mazungumzo na maneno. Inafahamika kwa wastani, wanawake
huongea zaidi na kusikiliza zaidi pia kwa Pamoja, na hata sehemu zinazohusiana
na lugha zimeendelea zaidi kwa wanawake kama tulivyoona awali. Mtoto wa kike
huwahi kuongea zaidi ya mtoto wa kiume kwa wastani, na mpaka muda wa miezi
ishirini, mtoto wa kike huwa na misamiati mara mbili au mara tatu zaidi ya
mtoto wa kiume. Watoto wakiume hufikia misamiati yao lakini hushindwa kuwafikia
spidi yao, au uwezo wa kuzungumza. wasichana huzungumza fasta zaidi kwa wastani
hasa wanapokuwa katika mazingira ya kijamii. Wasichana wanapokuwa Pamoja
huambiana siri zao na kuzungumza mambo yao mengi sana. na hupenda sana
kuzungumzia Maisha ya kijamii ya wengine, kitu ambacho wengine huita umbea,
lakini lengo huwa ni kujifunza changamoto na madhara na stress za Maisha, kwa
lengo la kujiepusha na madhara hayo na kwao wenyewe.
Kibiolojia pia inafahamika kuwa, wasichana wanapokuwa
wakiambiana stori za visa vya Maisha yao ya kijamii, mahusiano ya kimapenzi
‘’romantic na sexual implications’’ huwafanya kujisikia raha sana. Huwa ni
kutokana na kuzalishwa kwa homoni za ‘’Dopamine na Oxytocin’’, na homoni hizi
huzalishwa zaidi kwa wasichana kipindi wanachopevuka au kuvunja ungo.
Inatambulika kuwa, Estrogen inapoongezeka huambatana na kuzalishwa oxytocin nyingi
zaidi, ambayo huchochea zaidi hisia za kuwa Pamoja.
KATI KATI YA MZUNGUKO WA MWEZI!!
Hapa huwa na kiwango kikubwa zaidi cha Estrogen,
ubongo wa msichana husukumwa kuzalisha homoni ya Oxytocin nyingi zaidi, na
kiwango cha Dopamine pia huwa ni kikubwa sana. Msichana huwa ni mwongeaji sana
hapa. Hii ni kutokana na msisimko mkubwa sana wa mfumo mzima wa mawasiliano
‘’verbal circuit’’, lakini pia hisia yake ya kutamani ukaribu au ‘’Intimacy’’ huwa
kubwa sana, hupenda kuwa Pamoja, kuwa karibu, kukumbatiwa n.k. haya yote ni
matokeo ya kiwango kikubwa cha oxytocin. Homoni hizi za oxytocin na dopamine
ambazo huwa kwa kiwango kikubwa zaidi baada ya kupevuka, huwa ni matokeo ya
estrogen toka kwenye ovaries. Na hizi zina maana kubwa sana ambayo wengi
hawaijui, Oxytocin huzalishwa zaidi kutokana na ukaribu, na hata yenyewe
huongeza hisia za ukaribu. Hivyo ndivyo pia wasichana hupenda zaidi, na
huridhika zaidi pia. Utakuta wasichana wakipenda kuchezeana nywele,
kukumbatiana, kushikana wakienda kununua vitu na hata kupiga stori za umbea
Pamoja.
UMESHAJUA KWANINI HUSHINDA NA SIMU!!
Hushinda na simu kutwa nzima akipiga stori na wenzake
kwasababu, ukaribu na stori kwake huambatana na uzalishwaji wa kiwango kikubwa
cha homoni ya dopamine na oxytocin, ambayo hupunguzia kabisa mgandamizo wa
stress. Huwa ni shughuli sana kumtenganisha binti na simu yake, kwake
mawasiliano katika hatua hii, huwa na nguvu kama Heroin kwa mwathirika wa
madawa ya kulevya, kwa kuwa zote huambatana na uzalishwaji wa homoni za
dopamine.
WASICHANA WANAPOFELI KWA WAVULANA!!
Kwa namna ambavyo huwa akichat muda mrefu sana na
rafiki zake, wakiambiana kila Habari, wakizungumza umbea kutwa nzima, huisi
sasa anaweza fanya hivyo na kwa rafiki yake mpya wa kiume! Mambo huwa kinyume
kabisa. Hupatwa na ajabu au ‘’surprise’’
kubwa sana kwa kuwa, kwa muda wote ambao atakuwa akiongea na rafiki yake mpya
‘’Greyson’’, kumbe Greyson alikuwa anaboreka tu na stori zake!! Kwake
Greyson kuwa ‘’social’’ au mtu wa stori
stori za kijamii sio kipaumbele kabisa, na hili sio kosa lake, tangia akiwa mdogo,
kiwango kikubwa cha homoni za Testosterone kilimfanya akate channel nyingi sana
ambazo zimemfanya asiwe mtu wa kupendelea mahusiano sana ya kijamii. Na hii
shida huendelea mpaka kipindi cha familia, wanaume huwa sio wapenzi wa stori
ambazo wanawake mara nyingi sana huwa wakizipendelea, wanaume huwa hawazielewi
kwa kweli! na hata wale ambao huwa na uwezo mzuri wa kuzungumza sana, huwapata
wasichana wengi sana kiurafiki kwa sababu hii.
SIRI ILIYOFICHIKA ENZI HIZI KWA WAVULANA!!
Ijapokuwa tutawangalia baadae, lakini kwa ufupi katika
zama hizi wavulana huwa wamejawa na mawazo ya Ngono mpaka mwisho. Wavulana Mawazo ya kufanya
mapenzi huwa yakizunguka vichwani mwao kwa muda wote. Hii ni kutokana na
kiwango kikubwa cha testosterone ambacho huwasukuma zaidi kutaka kufanya ngono,
na hata kiwango cha misisimko ya uume, huwa ni mingi sana kwa siku. Huwa
wakitengeneza taswira za maumbile ya utupu ya mabinti na kutamani sana nafasi
ya kuwakaribia. Hapa vijana huwa hawapendi kabisa kuzungumza hasa na watu
wazima, kwa kuhisi wanaweza somwa akili zao, na kuonekana namna ambavyo
wametekwa na Mawazo hayo. Mara nyingi huwa tu wametulia kwa upweke wanapokuwa
na watu wazima mpaka watakapo kutana na wenzao wa rika lao, ambao hutaniana
kuhusu, mara nyingi kauli zenye maneno ya utupu, na hapo hufurahi sana kwa kuwa
hujiona kuwa wapo Pamoja kisaikolojia. Kwa kipindi chote cha upevukaji,
mitazamo na hisia za wasichana na wavulana hutofautiana kabisa.
Mahusiano Yanapovunjika!!
Mara nyingi wasichana huwa hawapendi kuvunja ukaribu,
hii ni kutokana na kupotea kwa kiwango kikubwa cha homoni za serotonin,
dopamine na oxytocin, ambacho huwapelekea kuwa wahanga wa kiwango kikubwa cha
homoni za stress au cortisol. Hivyo wasichana mara nyingi wanapoona dalili za
awali kabisa za kuvunjika kwa mahusiano yao na wale wanaowapenda, hujaribu
kukwepa ukilinganisha na wavulana, ambao wao kwao, migogoro ni jambo la
kawaida. Msichana aliyeathiriwa na kiwango cha stress kutokana na kuvunjika kwa
uhusiano, anapoelekea kupona, huusiana na uzalishwaji wa homoni ya oxytocin
ambayo huchochea tena uhitaji wa ukaribu na kuwa Pamoja, hiyo tayari ina
maanisha kuwa, kama msemo mmoja uliotolewa na chuo cha Robert Joseph kilichopo
Texas unavyosema, ‘’Uthabiti na hisia za Kujiamini kiume, hutokana na uwezo
wakujitegemea na kuishi mwenyewe, walakini, uthabiti na hisia za kujiamini kwa
wanawake, hutokana na uwezo wake wa kuendeleza mahusiano mazuri na wengine’’.
Huonesha hata ule msemo unaosema kuwa, linapotokea changamoto, mwili husisimka
kwa ajili ya kupambana au kukimbia ‘’Fight or flight’’, msemo huu huonekana
kuwa umeegemea zaidi kwa wanaume! Wanawake mara chache sana husisimka kwa namna
hizo, wanawake huwa wakiangalia zaidi namna ya kutatua changamoto kwa Pamoja
bila kukimbia au kupambana, kwa kuwa, kukimbia kwao ni kuwaacha wanaowapenda. Mfano,
Watoto wao. lakini pia, kupambana kunaweza hatarisha zaidi kama watakuwa
wajawazito au wana Watoto. Tafiti kadhaa kwa Wanyama ikiwemo nyani huonesha, wanawake linapotokea tatizo
huungana kwa Pamoja, na kushirikiana kulitatua kwa Pamoja. bila kujihatarisha
au kuhatarisha! Hii ni kujenga tu msingi wa kuwa, wanawake hukua na tabia ya
kujitenga na changamoto za migogoro tokea awali kabisa katika ukuaji. Baadhi ya
watafiti wa sayansi za watu ‘’anthropologist’’, bwana Joan Silk aligundua kuwa,
kwa nyani, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwezo wa kuchangamana vema na
jamii yake, na kuwa na mafanikio mazuri katika kulea vizuri Watoto wake.
ANALALA SANA HATA MPAKA SAA SITA!!
Wazazi huangaika sana kwa tabia hizi ambazo hutokeza
kwa Watoto katika umri huu. Mtoto huweza kulala usipomuamsha mpaka Katikati ya
siku, huwa mvivu na kuonekana amechoka sana. Lakini sababu ni ndogo sana,
kiwango kikubwa cha homoni za Estrogen hu reset seli za kwenye mtambo
unaotawala mzunguko wa kulala na kuamka katika ubongo ‘’Suprachiasmatic
nucleus’’. Homoni hizi haziishii hapo tu huenda kuathiri hata na uzalishaji wa
homoni zake za ukuaji, na seli
zinazotawala uhemaji. Kumbuka hapo awali mzunguko wa kulala na kuamka kwa
msichana na mvulana ulikuwa sawa, lakini mwaka mmoja kabla ya mwanaume hajaanza
kupitia mabadiliko haya, tayari msichana huanza. na mvulana naye anapokuja
kuanza kupitia vipindi vilevile vya kuchelewa kulala na kuchelewa kuamka, na
kwa ujumla hulala muda refu sana. Mpaka kwa wastani wa miaka ya kumi na kadhaa,
ubongo wa msichana huwa umesogea katika mzunguko wa ulalaji kwa asilimia 37%
hivi zaidi ya wavulana, hii humaanisha kuwa, ubongo wa wasichana huanza kukomaa
kabla ya ubongo wa wavulana. Mabadiliko haya huishia kwa kumfanya mwanamke kuwa
na uwezo wa kuamka Mapema kuliko mwanaume kwa kitambo kidogo kwa milele yote,
na huku ukimfanya mwanaume kuwa na uwezo wa kuchelewa kulala usiku kidogo zaidi
ya mwanamke milele yote. Inashangaza sana kwa namna ambavyo pia Biblia
inaandika kuwa sifa ya mwanamke bora, ni kuwahi kuamka na kuandaa familia yake,
kumbe Biblia ilishajua misingi hii ya homoni katika Ubongo
‘’neuroendocrinoilogy’’ miaka mingi hata kabla ya neno sayansi halijasimikwa.
NI MKOROFI SANA!!
Wazazi wengi hulitambua hili, kuna wakati Binti
anaweza mjibu mama yake hata jamii ikashangaa kama ni kweli anayezungumza ni
mtu na mama yake! Inatambulika kuwa, katika wiki mbili za kwanza za Mzunguko,
Ubongo wa binti huwa unakuwa vizuri sana, na hata huonekana kuwa kuna asilimia
25% zaidi ya uundwaji wa kumbukumbu katika sehemu ya ubongo inayoitwa
‘’hippocampus’’ kutokana na kiwango kikubwa cha homoni za Estrogen, hii yote ni
kusema kuwa ‘’Hana shida!!’’
Tarehe za Shida!!
Stori huanzia hapa, Siku ya 14 ambapo huwa katika
mzunguko wake Ovaries huliachia yai ‘’Ovulation’’, kiwango cha Progesterone
huanza kujaa kikigeuza au shusha viwango vya Estrogen ambavyo vilikwisha kuwepo
juu. Progesterone huwa na matokeo tofauti kabisa katika Hippocampus ikiwemo na
kulewesha kabisa seli za Hippocampus. Hii huufanya ubongo kuwa na msisimko
hafifu, huwa kama umelevywa na pia husisimka zaidi ‘’more irritable’’. Zile
kumbukumbu au taarifa au ‘’connections’’ nyingi ambazo zilikuwa zimeundwa katika
wiki mbili za kwanza pale ambapo kulikuwa na kiwango kikubwa cha Estrogen,
huanza kushushwa nazo kutokana na Progesterone. Sasa basi, siku chache mwishoni
mwa mzunguko huu wa hedhi, Kiwango cha progesterone nacho hushuka ghafla! hii
progesterone ilikuwa ni kama Gundi, kitendo chake cha kuondoka kwa ghafla
hupelekea kuondoka kwa ile hali ya kutulizwa kama gundi inavyozuia kidonda
kisifumuke. Na hivyo hupelekea ubongo sasa katika hizi siku za mwisho wa
mzunguko kuwa na kiwango kikubwa sana cha Stress, kuwa na hamaki, na pia
kutotulia na kusisimka. Na hii ndiyo sababu utakuta Watoto wanashindana kabisa
na wazazi wao kwa ukali! Na mara nyingi huja kutulia baadaye wanapokuwa wamekaa
sawa, hivyo ni muhimu wazazi kutumia elimu hii kuwajua na kuwasaidia Watoto
wao.
Je ni Kweli Ule Msemo wa ‘’Wanawake Wenye Miili
Mikubwa Hawana Shida?
Taasisi ya Afya ya akili ya Bethsesda walirejea
gunduzi ya kuwa, ‘’mipishano ya homoni za mzunguko wa hedhi huusiana na hisia
za misisimko mbalimbali kwenye Ubongo. na hii hutoa Ushahidi wa kushuka kwa
homoni pale mzunguko unapoishia, na hisia za kutotulia kwa baadhi ya wanawake.
Kumbuka Asilimia 80% huathiriwa kidogo tu na10% huathiriwa sana. Hawa
waligundua kuwa, Wanawake wenye Estrogen na Progesterone nyingi sana huwa
hawaathiriwi kabisa na Stress hizi, kwa kuwa, wao huwa na kiwango kikubwa cha
seli za homoni za Serotonin. ambazo huwatuliza kabisa, na hapa mara nyingi huwa
ni wanawake wanene au wenye maumbile makubwa (na wengine pia, unene sio kigezo
pekee). kwa wanawake wengi hawa
serotonins huenda kwenye sehemu za mbele za ubongo ‘’PFC’’ na huko Hushusha hisia ambazo zingesababishwa
na shida ya kushuka kwa homoni mwishoni mwa mzunguko. Na hivyo kuwafanya wawe
vizuri kabisa. Kumbuka hisia hizi kwa wenye estrogen chache sana hupelekea hata
Mawazo ya kupaniki, ukali, msongo wa Mawazo, hofu na ikizidi hata kujinyonga.
Ni muhimu kuwa mwangalifu kwa Wasichana wanaoweza onesha hisia hizi, kwa kuwa,
wanaweza kuwa wahitaji wa msaada mkubwa zaidi wa kitabibu, unaweza onana na
ofisi ya mtaalamu wa shida za fahamu ‘’psychiatrist’’.
Je wajua!!
Sehemu ile ya Hippocampus ambayo inahusiana na kuunda
kumbukumbu, huwa inasisimuliwa sana na homoni za estrogen! Na kwa mantiki hiyo,
katika wiki ya kwanza na ya pili, wasichana au wanawake kwa ujumla huwa wana
uwezekano wa kufanya vizuri kwenye mitihani ambayo itawataka kuwa na
kumbukumbu.
TATIZO KUBWA LA KUWARUHUSU KUFANYA NGONO!!
Jamii nyingi hujikuta wakiwaachia mazingira ya uhuru
mabinti hawa, ambao huwapelekea kuingia katika uzinzi au ngono. Hili ni kosa
kubwa sana. Na mara nyingi mabinti hawa huwa katika kipindi cha kuanzia Kidato
cha kwanza mpaka mwaka wa kwanza wa chuo kwa waliopitia kidato cha tano na cha
sita, lakini mpaka wale wa mwaka wa mwisho kwa vyuo vya kati ambao hawa ni wale
waliounganisha vyuo, hawa wote huwa wana wastani wa miaka 18-19 mpaka
wanapomaliza hizi hatua, lakini utakuta wanapoanza tu kufikia hatua za kati,
huonekana kama vile wamekwisha komaa vya kutosha na huachiwa uhuru wa kuingia
katika ngono!
Kitaalamu hawa mabinti
sehemu zao za hisia zina mhemko mkubwa sana wa kufanya mapenzi tangia tu
wapevuke, lakini sehemu zao na mifumo yao ya ubongo ya kutawala hisia, sehemu
ya ubongo wa mbele ‘’prefrontal cortex’’, huwa tu sehemu hizi zimeotesha seli
nyingi sana ila bado hazijakomaa!! Na
hasa kinachokuwa kinatokea hapa huwa ni hiki, kuna sehemu inayohusiana na
uchakataji wa hisia, inayoitwa ‘’amygdala’’, sehemu hii huwa na connections
nyingi sana na ile sehemu ya mbele ya ubongo ‘’prefrontal cortex’’, sehemu hizi
kipindi cha kupevuka huwa zinatengeneza seli za fahamu au ‘’neurons’’ ambazo
huwa zinaunganisha hizi sehemu mbili, kwa lengo ambalo ni kuwa, Ubongo wa mbele
uje kuwa na uwezo wa kutawala hisia. Sasa basi, kipindi cha kupevuka, hizi seli
huwa bado hazijakomaa kwa kuwa ili zikomae, huwa zinahitaji tabaka moja ambalo
huwa ni kama koti ambalo huzizunguka hizi seli, huwa linaitwa ‘’myelin’’.
Kitendo cha kukomaa kwa ubongo humaanisha kuwa, seli za ubongo sasa
zimeshafunikwa na hizi myelin, na hiko kitendo hukamilika binti anapovuka miaka
19. Na kumbe basi, anapofanya ngono au mapenzi kabla ya miaka 19, ubongo wake
sehemu ya Amygdala huwa inasisimka sana kwa hisia. na yeye mwenyewe, uwezo huo
wa kuzi control hana, na hiyo humharibia kabisa ubongo wake. tena anapoendelea,
huua uwezo wake wote wa kuweza kutawala hisia zake hata atakapokuwa mtu mzima.
Huathiri mamia ya connectons za ubongo zinazounda sifa za utulivu za kike,
ambazo zote huegemea katika networks za ‘’PFC-amygdala connectivity’’. Na hata
hisia za ngono zenyewe huwa hazipati kwa kiwango alichopaswa, kwa kuwa ubongo
wake huwa ukishuhudia mivurugano zaidi ya msisimko!!
MABINTI WENYE SIFA ZA KIPEKEE!!
Inafahamika pia kuwa, mabinti wenye kiwango kikubwa
cha homoni za kiume androgens, ambazo kwa wanawake huwa ni testosterone,
androstenedione na DHEA. huwa na dalili za kuwa wamewahi mapema sana kuanza
kufanya mapenzi. Na huu utafiti ulifanywa na Chuo kikuu cha Utah. Na katika
tafiti yao walichokiona ni kuwa, kadri sura ya binti inavyoonekana zaidi kuwa
ya ghadhabu au ‘’aggressive’’, ndivyo pia kiwango cha homoni ya androstenedione
inavyokuwa ipo kwa wingi zaidi. Chunusi ni dalili kubwa zaidi kuwa kiwango cha
androgens kipo juu. (kumbuka sio lazima chunusi iwe inasababishwa na androgens
na kuashiria kufanya mapenzi mapema!! Sayansi haina uelekeo mmoja, chunusi zina
uwingi wa sababu) chuo hiki waligundua
kuwahi kufanya mapenzi mapema huusiana na sifa za kuongezeka kwa androgens.
ikiwemo zote nilizoziorodhesha juu. Pia ni muhimu kutambua kuwa, kiwango cha
testosterone huwepo kwa kila mwanamke, maana ndicho humsababisha kuwa na hamu
ya kufanya mapenzi. Lakini tafiti huonesha kuwa, kiwango cha hasira kwa
wasichana kiliambatana na kiwango kikubwa cha androgens, na hamu kubwa ya
kufanya mapenzi, Pamoja na chunusi!!
Katika tafiti hii hii katika chuo cha Utah, waligundua
pia kuwa, hata kiwango kikubwa sana cha Estrogens, testosterone na
androstenedione, kiliambatana na hisia za wasichana kujiona wao ni wa pekee
sana, au wa viwango vya juu zaidi ya wenzao!! Wasichana hawa walionekana
wakijiweka katika viwango vya juu zaidi ya jamii ilivyo wachukulia na wengi wao
hawakupendwa sana na wenzao.
Kumbuka kuwa, Tabia ni matokeo ya mambo mengi sana
lakini homoni hujenga msingi wa kuzisoma tabia. Homoni katika ubongo huwa mara
chache sana zinaweza kukupa makisio hasi juu ya tabia, inafahamika kuwa,
maamuzi kuhusu tabia huongozwa zaidi na sehemu kuu kadhaa katika ubongo ambazo
ni Anterior cingulate cortex, Prefrontal cortex, Rostral cingulate cortex na Temporal parietal
junction. Lakini hata hivyo huwezi pingana na nguvu ya homoni. ambayo huwa ni
mithili ya mziki unaopiga nyuma ya kila tukio, na muda mwingine ukibakia
wenyewe tu ukipiga.
UBONGO WA BINTI MZURI RACHEL ‘’MIAKA 20+’’
Maisha na Kazi
Maisha ya Dada Rachel, binti wa miaka 24, baada ya
kazi nzito inayotokana na ratiba ngumu ya kazini kwake tokea asubuhi, anahitaji
muda wa kutulia ili atulize akili yake. Muda wa kutoka unapotimia wa kufunga
kazi za siku, haitaji hata kuagana na rafiki zake kutokana na uchovu. Anapanda
daladala kuelekea nyumbani kwake anakoishi kwa dada yake ambaye naye anafanya
kazi. Anapofika nyumbani anakuta kwa bahati nzuri sana dada yake akiwa
alishapika chakula lakini ametoka kidogo. Anaamua Kwenda kuoga kwanza na kisha
anakaa mezani na kula chakula chake. Anapomaliza kama ilivyo kawaida ya vijana
wa kisasa, anakaa kwenye sofa akijiachia na simu yake mtandaoni kuangalia kama
kuna lolote la kumsisimua kwa wakati huo. Baada tu ya kama dakika kumi,
anaingia Dada yake Anna akiwa na rafiki zake wanne ambao nae anafanya nao kazi,
wawili wakiwa ni wakiume na wawili wa kike.
UMEME WA HISIA!!
Ndani ya sekunde kadhaa tu baada ya Gilbert kuingia
ndani ambaye ni miongoni mwa marafiki wawili wa wakiume wa Anna, ndipo Rachel
alipogundua kuwa kichwa chake ni kama kimepigwa mithili ya shoti ya umeme!!
Gilbert alikuwa ni mrefu, kijana mzuri wa kuvutia ‘’handsome’’, alikuwa na
rangi ya maji ya kunde, sura yake ilikuwa ni ndefu iliyochongoka, alikuwa na
nywele nyingi na nyeusi, macho yake yalikuwa ni meupe. Rachel alijikuta
akisalimiana na rafiki wote wa dada yake, lakini akili yake yote ikiwa imeshachanganywa
na mwonekano wa Gilbert na hasa tabasamu lake jepesi alipokuwa akimsalimia.
Akili ya Rachel ghafla ilihama na kuanza kuwatazama
kwa umakini rafiki za dada ake huku akili yake ikilenga kuwachunguza kama yupo
mmoja ambae anaweza kuwa na ukaribu na Gilbert!! Mapigo yake ya moyo yalikuwa
yako juu, na akiwa hajahisi ukaribu wowote wa Gilbert na rafiki wa dada yake, ambapo
wawili wao tayari walikuwa wapenzi waliojionesha kupitia stori zao, Rachel
akaanza kuangalia Viatu vya Leather vya Gilbert kwa siri, mkanda wake mzuri,
akawa akiangalia vidole vyake kama ana pete!
Na akiwa Katikati ya Mawazo ambayo alikuwa akiyafanya kwa siri sana,
dada yake alishagundua kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma hisia za mdogo
wake. Ghafla!! Gilbert kama mithili ya mtu ambaye naye alikuwa kichwani mwa
Rachel, akawa akitafuta namna ya kumhusisha Rachel katika stori zao ili apate
nafasi ya kupata nafasi ya kumjua Rachel, ambaye naye alikwisha mvutia Gilbert,
kwa kipindi kifupi aliochokuwa amekaa ndani.
Gilbert ‘’Anna,
una mdogo mzuri hivi!! Au ndiyo maana huwa hupendi kutukaribisha!!, kauli hii
ni kama ilimfungulia njia Anna kumfungulia geti dada yake mdogo!!
HOJA YA KIBIOLOJIA
Miaka hii katika kila kichwa cha Binti kwa wastani,
huwa ni kupata mwenzi, atakae weza kumpenda, na kumjali yeye na watoto wake,
atakaojaliwa kuwapata. Vigezo vya kupenda ni vilevile kwa kila stori ya mapenzi
inapoanzia. Watu wengi hawajui kuwa unaweza wadanganya wanasheria, ila huwezi
wadanganya wataalamu wa ubongo, kama wakiamua kufatilia misingi ya utendaji wa
kibiolojia, ambayo imeshatengenezwa miaka na miaka, na sote huifuata tu. Mungu
alipotoa amri zake mlima sinai miaka karibia elfu nne iliyopita tayari
alishajua kuwa, msingi wa utendaji hautakaa ubadilike kamwe. Wanawake wote kwa
miaka yote hufuata misingi ile ile ya kuvutiwa kimapenzi. hisia za mapenzi ni matokeo ya mifumo ya ubongo. ambayo,
haionekani! lakini nayo ni kama mikono, yaani kila aliyenayo huitumia kwa kazi
zilezile, na namna watu huvutiwa kimapenzi huwa ni ileile. Unaposikia Yusufu
alikuwa mzuri wa kumsisimua mke wa Potifa katika Biblia, ndivyo ilivyokuwa pia
kwa Rachel baada ya kukutana na Gilbert!!
Kama Ilivyokuwa kwa mfalme Daudi alipovutiwa na mke wa uria mhiti, ndipo
ilivyokuwa kwa Gilbert alipovutiwa na Rachel.
Sababu Za Mwanaume Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa
Binti!!
Sababu za kuvutiwa kimapenzi. kwanza, huanza na sababu
za mivuto ya mwonekano. Mionekano ya muundo wa Gilbert yote huwa na misingi mikubwa
miwili ya kumvutia mwanamke. Mwanaume ambaye anasifa bora kabisa za uzazi
‘’fertility signs’’, mwenye atawezesha kuzaliwa kwa Watoto imara kabisa kimwili
na kiakili. Na pili, ni mwanaume mwenye uwezo wa kujali na kulinda familia
yake. Hii huwa ni kupitia uwezo mkubwa wa kiuchumi utakaowezesha kupata
mahitaji yote ya msingi, lakini pia uwezo wa nguvu za kimwili, ambao utampatia
mwanamke hisia za usalama kwa kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kupambana na
maadui.
Kama nilivyoeleza awali na hata katika kitabu cha
injili ya sayansi sehemu ya nne, katika msingi wa fiziolojia ya kufeki
mionekano. Ili mtu aonekane mzuri anapaswa kuwa na mfanano wa pande zake mbili
‘’Symmetry’’. anapaswa kuwa na mwonekano
ulionyororo au ‘’smooth’’, anapaswa kuwa na macho makubwa na tabasamu pana. Sifa
hizi kibiolojia zina maana kubwa sana, zinamaanisha kuwa jenetikia ya huyo mtu,
iko imara kwa kutofanya makosa katika uumbaji wake, uimara wa mfumo wa
jenetikia huambatana na uimara wa mifumo yote ikiwemo mfumo wa kinga na hata
biolojia nzima ya mwili. Tabasama zuri humaanisha amani. Ubongo hupenda amani
kama ilivyosababu ya namna watu wengi hupenda Watoto, kwa jinsi wasivyohatari.
Kwa mwanamke, mwanaume kuwa na macho makubwa huwa ni sababu ya kumvutia sana
kutokana na namna huwa rahisi zaidi kwake kuungana nae kihisia, pale anapokuwa
akimtazama na kuungana nae kihisia kwa uwezo wake mkubwa wa ‘’mirror neuron
system’’ au MNS.
Mwanaume mwenye ndevu na nywele nyingi kwa wastani
katika mwili wake, huwa na mvuto mwingi kwa wasichana kutokana na namna ambayo
nywele zake hutengeneza msingi wa ukakamavu wa kiume, ndevu kwa mwanaume
huaminika kumpunguzia eneo lake la uso ambalo lingeweza kusomwa ‘’wanaume huwa
hawapendi kusomwa sura zao, huwa hawapendi kuonesha udhaifu, pia huitwa sura ya
kiume’’, ni kama nywele ndefu zaidi kwa simba au manyoya marefu zaidi kwa
jogoo!! Ndevu huongeza mwonekano wa kiume ambao humwongezea mvuto kwa wanawake,
Ngozi ya wanawake yenye uwezo mkubwa wa kuhisi ‘’more sensitive’’ kutokana na
matokeo ya estrogen nyingi husisimuliwa zaidi inapogusana na nywele nywele za
kiume.
Sauti nzito huwavutia sana mabinti lakini sababu kubwa
ni kuwa, sauti kubwa kwa mwanaume humfanya awe ni tishio zaidi dhidi ya wanaume
wenzake, simba anapounguruma hufanya wadhaifu wote kutulia au kukimbia, na hilo
humfanya jike wake kujihisi salama zaidi, na ndivyo ilivyo kwa wanaume pia,
hata mwili mkubwa huwa na mvuto sana kutokana na namna huashiria nguvu nyingi
na hata kiwango kikubwa cha jasho ambalo huzalisha ‘’androstadinone’’ ya
kumsisimua zaidi mwanamke.
Kuangalia Viatu, mavazi na hata baadae kuulizia kazi
ya Gilbert, vyote hulenga kuangalia uwezo wake wa kiuchumi, hasa ni kwa namna
gani ataweza kummudu yeye Pamoja na Watoto wake. Rachel pia aliangalia pete
katika kidole cha Gilbert kwa lengo la kujilinda, ubongo wa mabinti bado huwa
na uwezo mkubwa wa kufanya mahesabu mapana, huamini kuwa mwanaume mzuri
hutazamwa na wengi. na hivyo, kuweza kukaa akiwa mwenyewe, kunaweza kumaanisha
huyo mwanaume hajatulia! Uwezo wake mzuri wa Prefrontal cortex humsaidia kutosisimuliwa
moja kwa moja na sehemu za hisia, hata akapuuzia hatari zinazoweza kutokea
mbeleni.
Kumbuka, takwimu zilizokwisha fanyika na
mwanasaikolojia David Buss kwa miaka mitano, zinaonesha kuwa, asilimia kubwa
zaidi katika makabila ya jamii 37. Zinaonesha wanawake wengi zaidi huvutiwa
zaidi na wanaume wenye nguvu za kiuchumi, kuliko mionekano ya nje. na pia,
wanaume wenye mionekano mizuri huonekana kuwa na urahisi zaidi wa kuwapata
wanawake!!
Sababu Za Binti Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa
Mwanaume!!
Sayansi za asili zote hukubaliana kuwa sababu ya
kwanza huwa ni sifa za uzazi ‘’fertility signs’’. Ijapokuwa wengi wasiojua
biolojia hii, huisi ni mapenzi tu yanayotokana na maamuzi ya mwanaume. lakini
biolojia hii inasaidia kujua kwanini kuelekea karibu na vijana wote wakiume,
huvutiwa zaidi na aina za sifa zinazofanana! Takwimu huonesha wanaume huvutiwa
zaidi na wasichana walio wadogo kwao kwa umri wa makadirio ya miaka miwili na
nusu na kushuka chini. Hupendelea
wanawake wenye macho yenye mng’ao ‘’bright eyes’’, nywele laini na
zinazoonekana vizuri ‘’shiny’’, midomo laini ‘’full lips’’ na mwili
uliojitenganisha kimaumbule ‘’hourglass figures’’. Sifa hizi zote ukiziangalia
zina msingi uleule wa awali, Umri mdogo humaanisha mwanamke ambaye bado
hajachoka, na hivyo kuashiria kuwa atakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukuzalia
(hii ni kama tu ambavyo timu za mipira
huwa zinapenda kusajili zaidi wachezaji wadogo, kwa lengo hilohilo),ukija pia
kwa maumbille, wanaume wengi hupenda mabinti wenye shepu ambazo msingi wake huwa
ni uzalishwaji wa homoni za Estrogen, katika kipindi baada ya kupevuka, misuli
na mifupa ya wasichana husisimuliwa zaidi na hizi homoni na kufanya Nyonga zao
kuwa ni ndogo, au nyembamba ukilinganisha na Hips kwa wastani wa 1/3
ukilinganisha na kabla ya kupevuka! Wanaume huvutiwa zaidi na mionekano hii
kama ishara ya binti ambaye bado Hajapata ujauzito kwa namna tumbo lake ni
dogo, katika kitabu chake Louann Brizendine ukurasa wa 64, anaeleza kuwa,
msukumo wa homoni za uzazi kwa wanawake wenye afya huwafanya kuunda maumbile
yenye wastani wa 1/3 kati ya nyonga na hips, na hiyo huwa ni ishara ya kiwango
kikubwa zaidi cha estrogen. na pia huashiria urahisi zaidi wa kupata Mimba hata
katika umri wao mdogo, na hii husapotiwa na sayansi za maumbile ‘’anatomy’’
ambazo huonesha maumbile haya huwa na urahisi mkubwa kwa kuzaa Watoto bila
changamoto! sababu zingine za unyororo wa Ngozi, lips n.k. hurejea katika
machaguo ya mwanaume kwa mwanamke mwenye afya na kiwango kikubwa zaidi cha
homoni za uzazi, lakini pia mfanano wa mwonekano au ‘’symmetry’’ huwa na sababu
za ubora wa mifumo ya kijenetikia kama tulivyoona awali, kwa mwanamke pia
uwingi wa nywele huambatana na kiwango kidogo cha homoni za androgens na hivyo
utulivu mkubwa.
Wanaume huwa na kigezo cha tabia kwa kiwango kikubwa
sana kwa mabinti kuliko wengi wa mabinti wanavyofikiria!! Wanaume hupendelea
mabinti wenye uwezo wa kuja kutunza familia zao, na wakawa sio changamoto kwao
kwa kuwa na tabia za kutoka nje ya ndoa zao! Ndani ya sekunde chache sana
mwanaume anapogundua mwanamke anayemfuatilia anaweza kuwa ni mhuni wa kuwa na
wanaume wengi, sehemu yake ya TPJ husisimka na kuanza kutafuta namna ya kukaa
nae mbali, na uwezo wao mkubwa wa kustahimili stress, huwapa wepesi wa kuachana
na uhusiano au ‘’social bond’’ yoyote
ile wanayokuwa wameianzisha, bila hata kujali kiasi gani cha nguvu
walishaitumia.
Muhimu Sana Kujua Kuhusu Mivuto Ya Kimapenzi!!
Biolojia hukusanya sababu zote za mivuto lakini hakuna
binadamu mwenye sifa zote za mivuto hii!! Ni muhimu kutambua hili, wala hakuna
binadamu aliye mzuri kamilifu wa chochote kile ‘’perfect symmetry’’, mara
nyingi Ubongo unapovutiwa na mtu hupuuzia sehemu zote ambazo zingekuwa hazina
dalilii ya uzuri, kwa huyo ambae tayari umeamua kumuona mzuri! Hili ni la
msingi sana ili mtu aweze kujua kuwa, kigezo cha tabia tu kinaweza mfanya mtu
mmoja akavutiwa na binti, na Ubongo wake ukapuuzia kila taarifa kuhusu mwonekano
wake, na vivyo hivyo kigezo cha mwonekano kinaweza pia kumfanya mtu apuuzie
kigezo cha tabia. Kitu kitakachowafanya watu wakae Pamoja ni kigezo cha kwanza
ambacho kimekuwa na nguvu zaidi ya kuwa na msisimko wa kihisia.
UBONGO WA BINTI ‘’RACHEL’’ KWENYE MAPENZI MAPYA
Rachel sasa na Gilbert huchati kila wakati wanapopata
free baada ya kazi, huutumia zaidi usiku kwa mawasiliano. Hupanga na kutumia
siku za weekend kuzunguka Pamoja, Rachel hutamani kujua zaidi kuhusu Gilbert,
familia yake, mipango yake ya kazi, uwekezaji wake n.k. Gilbert humsindikiza
Rachel baada ya mizunguko yao mpaka kwao, na mara nyingi huwa akimpitia
anapotoka tu kazini kila anapopata wakati. Kadri siku zinavyozidi Kwenda ndipo
hisia za kuwa karibu zaidi zinapoongezeka! Kwake Gilbert alishamhakikishia Rachel
kuwa yuko tayari kumuoa na anamsisitiza Rachel akubali ili aweze kuanzisha
harakati za kufunga nae ndoa, maana kila anapokuwa nae huwa anaona anazidi
kupata msukumo mkubwa zaidi wa kuzini nae jambo ambalo linapingana kabisa na
misingi yake ya imani. Kuna siku Rachel alimtembelea Gilbert, ilikuwa ni siku
ya Birthday ya moja ya marafiki wa Gilbert aliyeitwa Magessa, na Rachel
alikubali Kwenda Pamoja na Gilbert, sherehe ilichelewa kuisha kwa kina magessa,
na mpaka ilipohitimu saa nne na nusu hivi za usiku, ndipo Anna alipomshtua
Gilbert ‘’Wee!! Inakuaje na mdogo angu mpaka saa hizi? Gilbert kwa shaka kidogo
‘’ow, am sorry, soon nipo hapo, give me few minutes!!’’ ilibidi Gilbert amuage
rafiki yake magessa na kuondoka na Rachel, kipindi wanaondoka kutoka kwenye
party fupi, na kupita katika njia yenye upenyo kabla ya kutokea kwenye main
road ambapo wanaweza kupanda bajaji, Rachel alidondosha chini simu yake kwa bahati
mbaya, akiwa anataka kuiokota, Gilbert aliiwahi na kumuokotea, alipokuwa
akiinuka baada ya kuchukua simu huku kichwa chake kikiwa katika usawa wa miguu
ya Rachel, akadakwa na hamaki baada ya kuuona vizuri mguu wa Rachel! ambao
ulikuwa wazi kutokana na nguo aliyoivaa
kuwa ni fupi. kama ilivyokawaida ya mitindo ya kisasa, akajikuta akiusindikiza
mpaka kwenye paja, mpaka kiunoni na kisha kifuani, kipindi Rachel naye akijua
kinachoendelea, ndipo Gilbert akajikuta baada tu ya kumpatia simu akimvuta na
kumkumbatia, wakajikuta wakiaangaliana machoni kwa kipindi kama cha sekunde
kumi na kitu, mapigo ya moyo yakaanza kuambatana ‘’synchronize’’, akili ikawa
kama imelevywa, kwa mara ya kwanza wote wakajikuta wakishindwa kujizuia,
wakaanza kupigana kiss huku kila mtu ubongo wake ukiwa kama umepigwa
‘’narcotics’’, wazo likamjia Gilbert akiwa amemshika Rachel kiunoni, je
tunaweza Kwenda kwangu leo!! Rachel akiwa kihisia amekubali kabisa, lakini
alijipa ujasiri na kusema, Hapana! Tupange siku nyingine si leo, ngoja niwahi
nyumbani. Baada ya kufika nyumbani, Rachel akiwa ni kama mtu aliyetoka katika
kifungo Kizito na mwenye Mawazo mengi, na kusisimka! alijikuta hawezi tena
jizuia na kumsimulia dada yake, ambaye tayari alikuwa anajua kila kitu,
akamjibu ‘’Hopefully, you did nothing yet?’’ Rachel, akamjibu ‘’yes, sis..’’
Anna alikuwa ni binti wa dini sana na alitambua hatari kubwa sana ya kufanya
mapenzi kabla ya ndoa, maana huo ni msingi ambao umemfanya hata yeye na mumewe
waweze kuwa na ndoa yenye mafanikio makubwa sana ya uaminifu, mme wake Anna ni
dereva wa magari makubwa, huwa ana muda mchache sana wa kukaa nyumbani, lakini
familia yao imekuwa imara kwa zaidi ya miaka 25. Rachel sasa alimpa ‘’Go
ahead’’ Gilbert ya kufatilia mipango ya ndoa, Kwake Gilbert lilikuwa ni jambo
rahisi sana kutokana na kuwa Baba yake ‘’Masasila’’ alikuwa ni mchungaji
maarufu sana na kaka zake walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, hivyo
haikuchukua muda mrefu hata walipolikamilisha swala hilo. Baada ya Ndoa, Rachel
ambaye awali aliwahi mwambia Gilbert kuwa, hajawahi lala na mwanaume, sirini alishawahi fanya hivyo na mpenzi wake
waliotengana nae kwa kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita, aliyeitwa Juma!
Lakini kwa mara ya kwanza tu baada ya kulala na Gilbert kwa tendo la ndoa,
ndipo alipogundua kuna utofauti mkubwa sana kati ya mpenzi wake wa awali ‘’Juma’’
ambaye alilala naye, na Gilbert! Kwa Gilbert alitumia muda mfupi sana kujikuta
akiridhika ‘’orgasm’’, ukilinganisha na mpenzi wake wa awali, ijapokuwa Gilbert
hakujua lolote! Baada tu ya tendo la ndoa, kwa mara ya kwanza na kuendelea,
ndipo akili yake Rachel ilipojikuta ikimuwaza Gilbert zaidi na zaidi, alikuwa
na Gilbert kila alipoenda kimawazo, alikuwa akimlinda Gilbert kimawazo,
kuchelewa kujibiwa meseji na Gilbert kulimpelekea maumivu makubwa sana! ambayo
alijikuta kwa wakati mwingine hata akiangusha machozi, lakini alishangaa
alipomwambia Gilbert, yeye alishangaa kana kama ilikuwa ni kawaida sana, ila
Gilbert alikuwa akimpenda kwa dhati sana Rachel! Rachel alijikuta akimsamehe na
kumwamini sana Gilbert. Maisha yao yaliunganishwa kiakili na kugongelewa
msumari kimwili kwa namna wanavyozidi kuwa Pamoja!!
BIOLOJIA YA UBONGO WA RACHEL KWENYE PENZI JIPYA!!
Ni visa vilivyojaa lakini vina misingi mikubwa sana ya
kisayansi. Kiwango kikubwa cha Testosterone na nguvu kubwa ya mifumo ya hisia
‘’amygdala’’ na mgandamizo mdogo wa hisia tokea ubongo wa mbele ‘’prefrontal
cortex’’ kwa mwanaume, humfanya kuwa na uwezo mdogo sana wa kudhibiti hisia
zake za mapenzi zinapomuwaka!! Mwanaume siku zote yupo hatarini zaidi kuzini
kuliko mwanamke, sishangai jaribu hili lililomshinda hata mfalme Daudi katika
Biblia. Mwanaume anapoona, huchochewa atende , hii ni kwa namna ambavyo
huzalisha microgram zaidi ya 14,000 za testosterone kila siku. Sio rahisi kuzidhizibiti
kirahisi, ni sawa na lile fungu linalosema ‘’Usiyachochee mapenzi!!’’. Visa
vingi hata vya wanaume kubaka mabinti wao wa kazi, hutokana na sababu hizi.
endapo jamii haitajua tatizo hili, uzinzi utaendelea kuwa ni tatizo
lisilotatulika hata maofisini!! Ni muhimu sana kwa wanaume kuoa wake kama mtume
Paulo alivyosema kuliko kujifanya anakaa ‘’single’’ na bado anazalisha kiwango
kilekile cha testosterone. baadhi huisi kwa kufanya mazoezi unaweza punguza
msukumo huu. lakini mazoezi ndiyo huchochea zaidi testosterone, na kupunguza
‘’estrogens’’ homoni. ambazo zingepunguza msisimko wa mapenzi. Wanawake wote
wanaojua wanapendwa na kuruhusu kuwa na hao wanaume wanaowapenda mazingira ya
ukaribu na usiri, tena hasa wakati wa
giza ambalo huchochea zaidi mihemko ya kimapenzi, kwa namna hushusha kemikali
za ‘’norepinephrine’’ na kuongeza ‘’acetycholine’’ na serotonin. ambazo kwa
Pamoja huongeza msisimko kwa mwanaume, wanawake wanaoruhusu mazingira haya
wategemee tu kuishia katika uzinifu kadri wanavyoongeza zaidi odds.
Gilbert ile siku aliyotoka Party Pamoja na dini yake
yote, lakini alijikuta na yeye hana nguvu tena ya kujizuia, sababu kubwa
ilikuwa ni hiyo!
Kwa upande wa Rachel aliyeweza kujizuia ilihali naye
alikuwa amesisimka sana, sababu kubwa iliyomuwezesha ilikuwa ni uwezo wa Ubongo
wa wanawake! Wanawake wana ubora sana wa sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Anterior
cingulate cortex na pia Prefrontal cortex’’. sehemu hizi huwa zina nguvu sana
ya kuzuia nguvu za hisia tokea sehemu ya hisia ‘’amygdala’’ ambayo nayo ni
ndogo kidogo kwa wanawake, ukilinganisha na ilivyo kwa wanaume! Hii ndiyo siri
ya mafanikio ya Rachel. Kwake mwanamke kufanya mapenzi kuna nguvu lakini sio
kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa mwanaume. Gilbert alipokuwa akimshauri,
kichwani mwake alikuwa akijiuliza maswali mengi sana mfano, vipi kuhusu dada
anna? Vipi kuhusu Gilbert baada ya kulala naye, atanichukuliaje na ilihali
halikuwa lengo lake la awali? Na kwanini niende wakati halikuwa lengo letu la
kukutana leo? Maswali ya mtindo huu yote yalikuwa tu yakizunguka katika ACC na
PFC wakati huo Gilbert mtambo upo OFF na TPJ ‘’temporal parietal junction’’
ikifikiria tu namna ya kufika Ghetto!!
Kwa Mara ya Kwanza Kuzima Kwa ACC &PFC Kwa
Rachel!!
Rachel alipokuwa akilala na Gilbert kwa mara ya kwanza,
alijikuta akiridhika zaidi ya alivyowahi fanya hivyo na Juma! kwa sababu kubwa
moja! Kwa mwanamke kuridhika kimapenzi kunahusiana moja kwa moja na kuridhika
kiakili. Mwanamke anapokuwa bado ana maswali mengi na mashaka mengi kuhusu huyo
mwanaume, mfumo wake wa hisia huwa na msisimko mdogo sana, na hutumia muda mwingi
sana. na anaweza kabisa pia asiridhike au ku ‘’orgasm’’. Lakini mwanamke
anapokuwa amemridhia mwanaume na kumwamini, hujikuta akiridhika kwa haraka
sana. Hii ni kwasababu, ile sehemu ya ubongo inayohusiana na maswali juu ya
hofu na mashaka kuhusu huyo mtu, inayoitwa ‘’anterior cingulate cortex’’, huwa
inaridhika na kujizima, na hivyo kuruhusu mihemko toka kwenye amygdala kuwa na
nguvu moja kwa moja, ya kumsisimua mwanamke mpaka maximum. Rachel alishangaa
kwa sababu hii, kwa kuwa mwanaume wake wa kwanza ‘’juma’’, alikuwa bado
hajamuamini vya kutosha, hasa kutokana na tabia zake za uhuni, ijapokuwa naye
alikuwa na pesa nyingi. na ndio maana ilikuwa vile. kumbuka tafiti
zimethibitisha hoja hii, kwa mfano, wanawake waliopewa dawa za kutuliza misongo
ya mawazo ‘’anti-depressives’’ walionekana kuwahi kuridhika ukilinganisha na
ambao hawakupewa, na walikuwa na mawazo! Na pia wanaume ambao huwa na harufu
chafu za vinywa huwafanya wanawake wao wasiridhike kwa kuwa, harufu mbaya
hufanya sehemu za ubongo za uwepo wa hatari kuamshwa, hasa za maeneo ya shina
la ubongo ‘’pontomedullary chemoreceptors’’.
KUUNGANISHWA KIHISIA
Baada tu ya kulala na Gilbert, na hata Gilbert baada
tu ya kulala na Rachel, kiwango kikubwa sana cha Oxytocin sawa na dozi ya
kutosha ya dawa za kulevya! huzalishwa tokea kwenye Hypothalamus na kisha
sehemu ya nyuma ya pituitary gland. Oxytocin kama tulivyoona awali huusiana
moja kwa moja na viwango vya Dopamine na serotonins, na hizi homoni hujenga
hisia za raha, uraibu wa kuwa Pamoja na oxytocin huwaunganisha wapenzi. Mapenzi
ya kwanza kabisa, huwa na viwango vikubwa zaidi! Kuna kamsemo huwa kanasemwa kwa
wanawake ‘’hutamsahau aliyeanza kukutoa ubikra’’, hoja hii imejengwa katika
msingi huo, ulikuwa ni mpango wa Mungu
kuwa, wapenzi watakao kutana kwa mara ya kwanza waunganishwe zaidi kiakili na
kimwili’’, lakini kitendo cha mwanamke kulala na huyu na kesho na mwingine,
huaribu utendaji wa Oxytocin kwasababu, hii homoni huusiana na Dopamine na
kumbukumbu ya huyo mwenzi. Ni kama mama atakavyolia kwa msiba wa mtoto wake tu,
sio kila mtoto duniani! Hii inamaanisha, hisia
hizi za kuwa Pamoja huusisha, nguvu ya msisimko wa kihisia na taarifa za
huyo mtu. Mpenzi wako huwa ni kama folder katika ubongo wako, unapoweka wengi
maana yake ni kuwa, kwa kiwango kilekile ambacho alipaswa kuwa mmoja, sasa wapo
watano. Yaani kwa oxytocin ileile aliyopaswa apewe mmoja, umeigawa kwa watano,
madhara yake ni kuwa, hutaweza kuwa na nguvu ya mapenzi na hutafaidi mapenzi
kwa kuwa unaathiri mfumo wako wa kihisia. Hii inaweza kuwa ni miongoni
mwasababu za kale katika Biblia za kuruhusu talaka endapo tu mwanamke atakuwa
mzinzi!!
Je Wajua Biolojia Pana Ya Kiss!!
Kitendo tu cha kumpiga kiss mwanaume au mwanamke, mate
yenu yanapokutana, kwenye mate kuna zaidi ya chembechembe elfu moja ‘’bioactive
molecules’’ ambazo ndani tu ya sekunde huenda mpaka kwenye ubongo, na huko
huanza kutafsiri mpaka kiwango cha jenetikia cha huyo mtu, wanasayansi baadhi
husema, kama mtu huyo uliyepigana naye kiss atakuwa anafanana na wewe kiundugu
wa mbali, basi kiss lake halitakuwa na nguvu. Lakini miongoni mwa vitu vya
kuzingatia ni kuwa, kila kiss unalopigana na mtu ambalo litahusisha kubadilishana
nae mate, litajenga kumbukumbu za milele katika ubongo wa huyo mtu, hii ni kama
tu ambavyo ilivyo wa ngono, huaminiwa pia kuwa, chembechembe za mbegu za
mwanaume, ijapokuwa zitaondolewa, lakini kumbukumbu zake za kijenetikia kamwe
hazitaisha kwa huyo binti, inaitwa kitaalamu ‘’male microchimerism’’. ijapokuwa
inaendelea kuchunguzwa kwa tafiti, lakini ziliwahi kuwepo tetesi za tafiti
kuwa, chembechembe hizo huendelea kubakia kama kumbukumbu kwa huyo binti!!
Unaweza fatilia zaidi hili, lakini biolojia inaonesha ni kwa namna gani ukaribu
baada ya kukutana kimwili huwa na matokeo ya kuwaunganisha watu zaidi ya
inavyoonekana. Kumkumbatia mtu baada tu ya sekunde 20 hupelekea kuanza
kuzalishwa kwa oxytocin. ambayo baada ya muda itaanza kujenga hisia za
kumuamini huyo mtu!!
NADHARIA ZA KUZIKATAA ‘’HAKUNA JENETIKIA ZA
UAMINIIFU’’
Kuna wanasayansi ambao husambaza kuwa kuna aina ya
kinasaba au gene inayoitwa ‘’vasopressin gene’’, ambayo wameifanyia utafiti kwa
baadhi ya wadudu, wanaoitwa ‘’Prairie voles’’ na ‘’montane voles’’ . wamegundua
kuwa, kwa prairie voles, gene hii ni ndefu na wadudu hawa huishi na wapenzi wao
wamoja tu, lakini kwa ‘’montane voles’’ gene hii ni fupi na huwa na wapenzi
wengi. Kwa hiyo sasa, huwaaminisha watu kana kama kuwa, wanaume binadamu pia
wana msingi huu, wanaweza kuwa na gene ndefu au fupi!! Hii mitazamo imeshapitwa
na wakati, hakuna gene inayojenga msingi wa tabia, na kama tulivyoona katika
sura iliyopita, maendeleo makubwa zaidi ya biolojia yanathibitisha hoja hii
kwakuwa sasa hivi inatambulika, vinasaba au genes ni sehemu tu ambayo nayo
inaongozwa kama zilivyo zingine, na hata pia utafiti huu uliofanywa na Chuo cha
Maryland, hauna msingi mzuri wa kuelezea tabia za binadamu kwa kujifunza kwa
wadudu, ambao nao hufuata moja kwa moja msingi wa jamii zao.
UBONGO WA MAMA EUNICE!!
Mama na mtoto
Stori hubadilika milele baada ya ujio wa mtoto, na
haitabadilika milele!! Maisha ya jamii
nyingi mama hubadilika hata mtindo wake wa utafutaji, maana wamama wengi ndio
huachiwa zaidi mzigo wote wa kuwalea Watoto wao kiuchumi na kijamii. Wanawake
wengi huanza kuvutiwa na kuwa na Watoto hata kabla ya kuwapata, wanawake hawa
wanapokuwa wakishika Watoto wa wenzao, harufu za vichwa vya Watoto huwasisimua
wanawake kwa kuwa na ‘’pheromones’’, na hizi huwafanya wanawake kuanza
kuzalisha homoni za ‘’oxytocin’’ ambazo huwafanya kuanza kutamani sana kuwa na
watoto.
Baada tu ya kutungwa mimba, mtoto anapoanza tu
kuumbwa, kile kitendo tu cha kuunganika kwa mfumo wa damu wa mama na mtoto,
huanza kupelekea mabadiliko katika mfumo wa homoni wa mama, ambayo, ndiyo
mwanzo wa kubadilika kwake.
Biolojia Mpya ya Umama
Progesterone huanza kujaa ambayo huanza kufanya matiti
yake kusisimka ‘’tender’’ na ubongo wake huanza kama kulewa au kupoa hivi
‘’sedated’’, hisia hizi cha uchovu huambatana na hali yake ya kupenda kulala na
kula zaidi. Sehemu zake za ubongo zinazotawala kiu na njaa huchochewa zaidi na
mabadiliko haya ya homoni. Na lengo kubwa huwa ni kumsisimua kuzalisha damu
hata mara mbili ya damu yake, ‘’kwa ajili ya mtoto’’. Sehemu zake za hisia za
harufu na Ladha huongezeka kimsisimko kwa lengo la kumlinda asije akala vyakula
vyenye kuhatarisha hali ya mtoto wake. Akili yake huelekezwa zaidi kwa kilicho
katika mfuko wake wa uzazi au ‘’uterus’’, unapofika mwezi wa tano, huanza
kuhisi kama kuna vitu maeneo ya chini ya tumbo ‘’abdomen’’
Kiwango cha progesterone huwa hata mara mia zaidi ya
kiwango cha kawaida, progesterone katika ubongo siku zote ni kama dawa za
kutuliza maumivu na kukufanya ulale, kama valium. Hupooza sana ubongo, hizi
homoni zikichangamana na homoni za estrogen ambazo nazo huwa juu, kwa Pamoja
huwa na lengo moja pia la kumlinda mama dhidi ya homoni nyingi sana za stress.
ambazo huwa zinazalishwa na mtoto, homoni za cortisol. Mama kwa hiki kipindi
chote sehemu zake za ubongo zimekuwa zikizuia yale mabadiliko ya mzunguko wa
mwezi, zikikuza sehemu zinazohusiana na ulaji na unywaji na harufu, na sasa
mwishoni kuanzia mwezi wa tano na sita, huanza kutengeneza mifumo ya upendo wa
mtoto. Hapa huusiana na mama kumuwaza sana mtoto wake, akifikiria namna
atakavyombeba n.k. na unapofikia mwezi mmoja kabla ya kuzaa, kiwango cha homoni
za stress toka kwa mtoto huwa ni kingi sana, na kumbuka, homoni hizi huwa sio
kwamba mama naye anakuwa na stress, ila anakuwa hajatulia!! Mwezi mmoja kabla
ya kujifungua, wamama wengi wanaofanya kazi huwa hawawezi kuzingatia vizuri,
vichwa vyao huwa vimechanganyikiwa kisaikolojia!!
JE WAJUA
Kuanzia mwezi wa sita wa ujauzito, Ubongo wa mama huwa
unapungua ukubwa au volume. Picha za fMRI huonesha ubongo wa mama mjamzito
ukizidi kuwa mdogo kwa kipindi hiki, lakini zinapobakia tu wiki kadhaa kabla ya
kujifungua, huanza kukua tena!! Sio kwamba ubongo hupungua ukubwa kwa kupungua
kwa seli au sehemu za ubongo, Hapana, huwa tu unasinyaa!! Na wanasayansi
hukubaliana kuwa hii ni kutokana na mabadiliko mengi ya kikemikali yanayotokea
kipindi hiki, lakini baadae hurejea kawaida.
Maisha Baada ya Eunice Kuzaliwa!!
Mtoto anapokuwa akipita katika njia ya uzazi, maelfu
ya homoni za oxytocin huzalishwa. Maelfu pia ya connections katika ubongo
huundwa. Baada tu ya kuzaliwa mama hujisikia raha sanaa ‘’Euphoria’’ ambayo
huchochewa na oxytocin na dopamine. Lakini pia mama uwezo wake wa kuhisi au
sense ‘’harufu, mguso, kuona na kusikia’’ huwa juu sana. Hii humfanya awe
makini au alert zaidi kwa mtoto wake. Kwa mama, harufu ya Ngozi, kichwa cha
mtoto wake, kinyesi, maziwa anayotema n.k. hutengeneza kumbukumbu kubwa katika
kichwa chake. Na atakuwa na uwezo wa kuzigundua hizi kwa ufanisi wa asilimia
90% hata ukichanganya na za wengine. Miguso ya vidole vya mwanae, sauti za
kutaka kuanza kulia n.k. kwa Pamoja zote hukaa kwenye kumbukumbu za ubongo wake.
ndani ya siku na mwezi, na kuendelea, hisia za ulinzi wa mwanae huzidi
kuongezeka, na huwa na hasira sana katika
kumlinda mwanae. Wamama wengi sasa hivi huwa wepesi kushindana na waume
zao pale wanaposhindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa familia zao, kama
tulivyoona sababu zake awali.
Wazazi wasio waleaji wazuri!!
Kiwango kikubwa cha testosterone kwa wanawake na hata
wanaume hupunguza uwezo wa kulea!! Wanawake wenye kiwango kikubwa cha
testosterone huwa sio waleaji wazuri. tafiti huonesha hivyo. na wababa wenye
kiwango kikubwa cha Prolactin, huwa ni waleaji wazuri sana. wengine hata
wakihisi hisia kama za ujauzito pale wake zao wanapokuwa wajawazito ‘’couvade
syndrome’’, kama tulivyoona awali. Na huwa na msisimko wa chini sana wa kufanya
mapenzi, pale wake zao wanapokuwa katika kipindi chote cha ujauzito. tofauti
kabisa na wenye testosterone nyingi, ambao bado huwa na msisimko mkubwa, hawa
sio waleaji wazuri kutokana na tafiti.
KUHUSU KUZAA
KWA OPERSHENI!!
Binadamu sio kondoo. Kondoo hutumia dakika tano tu
baada ya kumzaa mtoto wake, kuungana nae kihisia za upendo, pale anapomnusa
nusa n.k. ukimtenganisha kwa hizi dakika! Hata ungana na mtoto wake kihisia
kabisa za upendo wa mama na mtoto! binadamu hata azae kwa operesheni, baada tu
ya kuzinduka, hisia za kuungana na mtoto wake huendelea kujengeka kwa kiwango
kilekile. Wengi hawajui kuwa, sehemu za ubongo wa mama zinazosisimuliwa kwa
upendo wa kuwa na mtoto wake, huwa ni zilezile ambazo zilikuwa zinasisimuliwa
alipokuwa na mme wake au mpenzi wake. Na tafiti zaidi na chuo cha London
zimeonesha kuwa, sehemu za ubongo zinazohusiana na kumkosoa mtu, au ukosoaji,
ambazo ni zilezile za ‘’anterior cingulate cortex’’, huzimwa kabisa pale ambapo
mtu humzungumzia anayempenda!! Kwa hiyo hilo linaweza kukupa umakini unapoenda
kumkosoa mtoto kwa mama yake!!
NGUVU YA KUNYONYESHA!!
Kunyonyesha kuna nguvu kubwa sana katika ubongo wa
mama. Mtoto na vidole vyake vidogo, anaposhika titi la mama yake, na kuanza
kulinyonya, hupiga shoti ya uzalishaji wa homoni za oxytocin, dopamine na
Prolactin, kwenye ubongo wa mama yake. Hili humfanya mama kuwa na msisimko
mkubwa sana wa kujisikia raha. Na pia kiwango cha oxytocin hiki huendelea
kumfanya kujisikia uhitaji wa kuwa na mwanae. Tafiti ilifanywa kwa panya wenye
mimba, wakawa wakipewa mazingira ya kuchagua aidha kubonyeza sehemu moja na
kufungua wapate dawa za kulevya za Cocaine, ambazo humfanya ajisikie raha, au
wabonyeze sehemu nyingine wapate kukutana na Watoto wao, wawanyonyeshe!! Panya
hawa kila wakati walichagua Watoto wao!! Ijapokuwa kama ungewapa chakula na
cocaine wangeenda kwa cocaine. Hii ni kwakuwa, kunyonyesha kuna nguvu kubwa
sana ya Oxytocin, na msisimko wa raha kwa wamama kwa Pamoja. Na inafahamika
kuwa, wamama wengine wanapokuwa wakinyonyesha, hutulia sana na muda mwingine
hata kusahau kazi zao. Lakini pia, wamama wengine wamejikuta hata wakishindwa
kubalansi upendo kati ya Watoto wao na waume zao, kutokana na nguvu kubwa ya
ukaribu huu unaotokana na kunyonyesha.
Wamama wengi hujikuta wakishindwa kabisa kuwa mbali na
Watoto wao, hata kwa kitambo kidogo, hii huitwa pia ‘’withdrawal syndrome’’.
Hii hutokana na namna ilivyo strong bond kati ya mama na mtoto wake, kwa gundi
za ubongo kiakili na kihisia, zinazoshikiliwa na homoni.
MAMA MBAYA HUTENGENEZA MAMA MBAYA!!
Mwanasaikolojia Michael Meaney aligundua kuwa, malezi
ya mama huathiri moja kwa moja sehemu za ubongo za mtoto wake wa kike. Kumbuka
tulishaona kuwa, Watoto wakiume hawaathiriwi sana na malezi katika ubongo wao.
Alipojaribu kumchukua panya mtoto na akamweka alelewe na panya anayefanana
kabisa na mama yake ila sio, mama huyu hakumjali mtoto huyu. Mtoto huyu baada
ya muda alipoangaliwa sehemu za hippocampus na amygdala ambazo hutumia Oxytocin
na estrogen, zilionekana kuathiriwa kabisa!! Kumbuka tumeona sifa hizo juu
nyingi sana za umama zimejengwa kwa utendaji wa homoni hizi, sasa basi, kitendo
cha maeneo haya kuathiriwa, maana yake hazitaweza kutumia vizuri homoni hizi,
maana yake pia ni kuwa, unaenda kuwa na mama asiyemleaji mzuri au mwenye
shida!! Hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mama ndiye wakulaumiwa zaidi binti yake
anapoharibika kutokana na biolojia.
Lakini pia imeonekana kuwa, malezi toka kwa wazazi
wanaojali na kuonesha upendo, hujenga Watoto walio smart, wenye afya na wenye uwezo
mkubwa wa kukabiliana na stress. Watoto waliolelewa vibaya huwa na shida nyingi
za kupata stress kirahisi, kusisimka haraka sana kwa mambo madogo, magonjwa na
kuwa na hofu. Hapa ni pa kuwa makini
sana, kuna nadharia katika jamii za wasiojua hili zinazowadanganya kuwa, mtoto
aliyepitia shida huwa na uwezo mkubwa wa kuzikabili! Sio kweli, hiyo huwa tu ni
neema ya Mungu. Na mifano hiyo huwa haina undani wa kifikra, katika watu mia
wanaokumbana na mazingira magumu, wanaweza kumi tu wakafanikiwa, na jamii
huwatumia hawa kama kioo, ilihali uhalisia wa hali unapaswa kuchukuliwa kwa
takwimu za wengi zaidi ambao ndio hao 90. Wanaolelewa vizuri mia, una uwezo
wakupata 90 walio vizuri na kumi tu wenye shida, lakini wasiojua tena, hutumia hawa kumi kujifunzia.
Jamii inapaswa kuondokana na fikra potofu za kujifunzia.
JANGA LISILOONEKANA!!
Kutokana na ugumu wa Maisha, wamama hupaswa kutokuwa
na watoto wao kwa muda mwingi kwa ajili ya kuwalea. Watoto wanapaswa kuachwa
katika mazingira tofauti tofauti sio kwa mapenzi ya wazazi wao, ila ni kutokana
na changamoto za Maisha. milipuko ya magonjwa na tabia za ajabu, huwafanya
wamama kuwa wahanga muda wote wa utendaji wao, katika kuwapambania Watoto wao.
lakini muda huohuo kuwa wahanga wa kihisia wa kuvunjwa moyo kwa namna
wanaowapenda wanapopitia hali ngumu.
Janga lisiloonekana ni kutokuwa na uhakika wa Maisha,
kukosa uhakika wa kuwa na mahitaji ya kukidhi Maisha kwa kila siku ya Mungu!
Jambo hili huongeza stress kwa mama ambayo huathiri uwezo wa uleaji wa mtoto
wake. Kiwango kikubwa cha Cortisol, kilionekana kwa Wanyama ambao, walikuwa
kwenye mazingira ambayo hawana uhakika, kama kesho yake watapata mahitaji yote
ya kukidhi mahitaji yao, na ya Watoto wao! Inasikitisha sana namna ambavyo
wamama hawa hawakuwa wenye nguvu sana za kuungana na wanao, wanapokuwa kwenye
magoti yao, na huu ndiyo msingi wa kuwepo kwa Watoto ambao hawana ujasiri
Pamoja na uwezo wa kuchangamana na jamii zao kwa ujasiri. Hii ni kwa kuwa
walikoseshwa walipokuwa wadogo pale wazazi wao walipokuwa wameathiriwa sana, na
mtindo mgumu wa Maisha.
Ni jukumu la jamii kujua tunapaswa kusaidiana kulea.
Kama ilivyo kwa Wanyama wanavyoshirikiana, hapo awali kulikuwa na mafanikio
sana katika uleaji kwa namna ambavyo jamii zilikuwa zikishirikiana sana kwa
hali na mali. Kadri mfumo wa ubinafsi unavyoongezeka, basi umasikini unazaidi
kuathiri mifumo ya uleaji. Na hivyo pia ni muhimu wapenzi kujua kuwa, kama
mahitaji kwa familia yatakuwa changamoto, ni muhimu kuchelewa kuzaa au kutozaa
Watoto wengi, la sivyo hupelekea tatizo hili linaloitwa ‘’attention disorder’’.
BIOLOJIA YA MIGOGORO MINGI YA WAMAMA NA WAUME ZAO
Ukiachana na
migogoro ambayo sababu zake zinafahamika mfano, migogoro ya kitabia kama wizi,
uzinzi, hasira, umasikini n.k. migogoro mingi sana katika familia, ukiachana na
sababu hizo, huwa inatokana na namna
ambavyo ubongo wa wanawake unavyoyachukulia mambo, huwa ni tofauti na namna
ambavyo ubongo wa wanaume huwa unayachukulia.
Wanawake kwanza kabisa huwa na aina yao ya maumivu
ambayo, ni ya tofauti kwa kiwango ukilinganisha na kwa wanaume. Wanawake huwa
na maumivu ambayo kwa kiingereza huitwa ‘’Gut feelings’’, haya ni maumivu
ambayo anakuwa kama anakitu kimemkaa maeneo ya juu ya tumbo kinamkera!! Wanaume
katika scan za Ubongo huonekana kuwa na msisimko mdogo sana wa aina hii ya
maumivu, tafiti iliyofanywa ilionekana kwa wanaume ni maeneo mawili tu ya
ubongo yakisisimka, wakati wanawake wakionesha maeneo tisa. Inaaminiwa kiwango
kikubwa cha estrogen huwafanya wanawake kuhisi zaidi maumivu ya kimwili na
kihisia. Na pia uwezo wao mkubwa wa kuhisi hisia za vitu, toka kwenye milango
ya fahamu na tumboni, katika ubongo. huwafanya kuwa wakihisi maumivu kwa
kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na ilivyo kwa wanaume.
Tatizo huanzia hapa, Linapotokea tatizo lolote lile
katika familia. Mwanamke huumizwa sana na mwanamke hulichukulia tatizo katika
hisia zake, huumizwa na kulionesha katika mwonekano wake, huonesha huzuni. Hii
hali huitwa ‘’Emotional’’. Mwanamke huitaji kuona anapomweleza mwanaume wake,
au hutaka kuona mme wake, naye analipokea tatizo lile kwa kiwango kilekile.
Shida ni pale mwanaume wake anapokuwa haoneshi kulipokea kama yeye
alivyotegemea! Wanawake wengi huumia sana, kwao huisi hii ni kama namna ya usaliti,
kwao mwonekano ambao mwanaume anauonesha baada ya kulitambua tatizo, ni kama
anasema kuwa, hili sio tatizo langu!! Lakini ukweli ni kuwa, Ubongo wa mwanaume
huwa ni kama unasema, kwa gharama yoyote ile, usioneshe unyonge kwenye sura!!
Hii ni kama nilivyosema katika sayansi za asili za sababu za ndevu, ambazo ni
kuficha hisia za unyonge.
Wanaume pia huwa na shida kubwa sana ya kuchukulia poa
sana mionekano mbalimbali ya kihisia, hasa za huzuni, ambazo wake zao huonesha.
Wanawake huitaji sana kuelewana kupitia lugha ya mionekano ya sura!! Mwanamke
anapokuwa ameumia sana, na mmewe akijua au asipojua maumivu ambayo mkewe
anapitia, anapokuwa haoneshi kwa nje kuguswa, humfanya mke wake kujisikia vibaya
sana. Wataalamu wa ubongo ‘’psychiatrists’’ hunukuu kuwa swala hili hupelekea
migogoro mingi sana katika ngazi za kifamilia.
Wanaume wana uwezo wa kusoma maumivu katika sura za
wanawake kwa asilimia 40% wakati wanawake wanaweza kwa asilimia 90%. Wanaume huwa hawapendi kuwa na mtu
ambaye anajisikia huzuni ‘’sad’’, na hii ni kwa kuwa, ubongo wao haupendi
kuonesha hisia za udhaifu kwao. lakini wanawake wanaonesha kuwa sawa tu, kwa
kuwa na watu wenye huzuni, au na watu wenye furaha. Wanaume huwa hawapendi kuwa na watu
wanapokuwa wanapitia nyakati ngumu za kihisia, hupenda kupambana na hali zao
wenyewe, na hujidanganya kuwa na wanawake hutamani kuwa wenyewe kama wao.
Ubongo wa wanawake huchakata taarifa za kihisia
ikiwemo hizi za huzuni ‘’emotional’’, kwa pande zote mbili za ubongo. wakati
wanaume huchakata hisia hizi kwa upande mmoja tu wa ubongo, kama takwimu toka chuo cha Michigan
inavyoonesha. Ni muhimu kwa wanaume kutambua kuwa, baadhi ya vitu ambavyo kwao
vinaweza kuwa vya kupuuzia, vinaweza kuwa na nguvu kubwa sana kwa wanawake.
Wanawake huwa rahisi zaidi kupoteza usingizi kutokana
na kuwa na msongo wa Mawazo, ukilinganisha na wanaume. na inafahamika hiyo
kutokana na namna homoni za estrogen zilivyoonekana kuwa na nguvu zaidi katika
mfumo wa kulala na kuamka ‘’cirardian rhythm’’. Na pia inafahamika kuwa
wanawake wapo hatarini kupata tatizo lingine la aina ya msongo wa Mawazo
linaloitwa ‘’anxiety’’, ambapo hii ni ile hali ambayo mtu anahisi muda wote
kuwa tatizo linaweza tokea au linatokea. hii hali ya mtu asiweze kutulia, huwa inatokea
kwa wanawake mara nne zaidi ya wanaume.
Kipindi mwanamke anapokuwa na mgogoro na mwanaume
wake, huwa anamwangalia machoni, huwa anaungana nae kihisia, huwa anafanania au
match na mapigo yake ya moyo, huwa ana ‘’match’’ nae mfumo wake wa kuhema, na
kisha anaichukulia hali yake sasa!! Hapo mwanaume anapokuwa anamdanganya, huwa
ana uwezo mkubwa kugundua kwa kuweza kujua kuwa, hakuna uhusiano wa hali yake
na maneno anayoyasema!! Hii ni nguvu kubwa sana ya ‘’mirror neuron system’’
ambayo inawezeshwa na maeneo mengi ya ubongo wa juu Katikati kama ‘’premotor
areas, somato-motor cortex, nyuklia zake za juu na chini, n.k’’ muda wote huu
mwanaume anaweza kuwa bado hajashtuka, lakini mwanamke anapoangusha machozi
baada ya kugundua kuwa anadanganywa! Mfumo wa ubongo wa mwanaume nao huwaka!!
Wanaume hawana uwezo wa kuhimili kuangalia machozi ya wanaowapenda, hushindwa
hata kutawala pia mifumo yao ya hisia, na hii ndiyo sababu wengi huamua
kuondoka au kujaribu kuikimbia hiyo hali kwa gharama zote.
Kadri umri unavyoenda wengi wa wanaume na wanawake
huwa na uwezo wa kutawala hisia zao. Mfano wanaume wanapozidi kuzeeka viwango
vyao vya testosterone hushuka, na prefrontal cortex huwa na nguvu zaidi Pamoja
na estrogen ambayo nayo huongezeka. Hii huwaongezea ubora wa maamuzi wanayoweza
yafanya, na huwa hawana msukumo mkubwa wa hasira kama ulivyo kwa vijana.
UBONGO WA MWANAMKE ULIOKOMAA ‘’MIAKA 51+’’
Ukomavu
Purukushani zote alizozipitia tangia alipoanza kuitwa
Dada mpaka akaitwa Mama Fulani na sasa anaitwa Bibi, zimemfanya amekuwa mtu
mpya kabisa. ubongo wake unapitia mabadiliko makubwa kabisa ambayo yanapindua
kila kitu kilichowahi fanyika katika historia ya Maisha yake. Kuanza miaka
arobaini na kitu mfano 43 na kuendelea wanawake hupitia kipindi kinachoitwa
‘’Perimenopause’’. Hizi huwa ni dalili za kwanza kabisa za kuwa mzunguko wake
wa mwezi unaenda hatiani. Hii huambatana na uzalishaji usioeleweka wa homoni za
estrogen katika ovaries zake. Hali hii huwa na usumbufu mkubwa sana kwa baadhi
ya wanawake na hata baadhi huonesha kabisa dalili mbalimbali za kutokujisikia
vizuri.
Hapa kinachotokea huwa ni hiki, estrogen huwa
inahusiana moja kwa moja na utendaji na uzalishwaji wa homoni mbalimbali za
kujisikia vizuri kichwani, kama vile ‘’norepinephrines, acetylcholine, dopamine
na serotonin’’. Utendaji wa homoni zote hizi huathiriwa kwa kadri ambavyo
viwango vya estrogen kiongozi wao unapoathiriwa. Baadhi ya wataalamu wa afya
huwapatia wagonjwa wao matibabu ya ‘’anti-depressives’’ au dawa za kuzuia msongo wa Mawazo, ambazo
huonekana kuwasaidia, lakini msingi mkubwa hapa huwa ni namna ambavyo dawa hizi
husaidia kurejesha balansi ya awali.
HAJALI WALA HAWAZI!!
Hawa wamama wakubwa bwana huwa hawajali na wala
hawapendi kujali. Hawa swala la Kupeana talaka kwao wala sio la kuwatishia
tena! Wengi wasiojua biolojia hii huisi kuwa, sababu ni kiburi kwasababu ya
Watoto wao wakubwa, lakini tambua tokea leo, wala hawajali hata hao Watoto wao
wakubwa!! Kinachotokea hasa baada ya miaka Hamsini hivi kwa wastani, huwa ni
kustop kwa uzalishaji wa homoni za mzunguko katika ubongo. sasa hivi kile
kiwango kikubwa cha Oxytocin ambacho kilikuwa kinaambatana na estrogen hakipo
tena! Kile kiwango kikubwa cha dopamine ambacho kilikuwa kinasababishwa pia na
estrogen, ambacho kilikuwa kinampa uraibu wa kukutafuta tena na tena, hakipo
tena kama awali. Sio kwamba amekuwa sio mtu wa kupenda tena, ila wastani wa
msukumo ule wa awali haupo tena. Ile Oxytocin ya kumfanya amuwaze mtoto wake
kila wakati haipo tena kama ilivyokuwaga zamani. Hii ni kama tu ambavyo Mungu
mwenyewe alivyoruhusu kuwa, baada ya muda ‘’mwanaume na mkewe wataambatana,
wataondoka nyumbani’’, hiki ni kile kipindi ambacho kila mtu anapaswa kuishi
kwake ila bado tupo Pamoja!! Takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 65% ya talaka
zinazoandikwa kuanzia miaka 50 na zaidi, sababu huwa ni wanawake!!
Kipindi hiki hana malengo makubwa sana juu ya familia
yake kama ilivyokuwa awali. Saivi hana msisimko mkubwa tena wa dopamine kama
mwanzoni, Maisha yake aliyokwisha yafikia yanamtosha. Huwa hana msisimko tena
wa kufanya mapenzi kama ulivyokuwa ukipungua tokea miaka ya arobaini. sasa hivi
hatakubali kufanya tena kwa ajili tu ya kumridhisha mme wake kama alivyokuwa
akiridhia kwa kipindi kilichopita.
Sasa hivi hupendelea sana kufanya vitu ambavyo
vitakuwa vikimfurahisha yeye. Hupenda sana kufanya safari mbalimbali za
kutalii, hupenda kuzurura sehemu mbalimbali kukutana na rafiki zake. Hupenda
sana kukaa na marafiki zake wakizungumzia maswala mbalimbali kuhusu Maisha yake
ya awali, Watoto wake, maswala ya kazini kwake na mengineyo kwa ujumla.
HUWA NA HASIRA KWA WAKATI FULANI HASA NA MME WAKE!!
Sasa hivi ile nguvu ya homoni ya Progesterone ambayo
ilikuwa ikimtuliza awali, haipo tena!! Sasa hivi viwango vya stress vinapopanda juu humfanya kuwa na
ghadhabu ukilinganisha na awali. Sasa hivi kile kiwango cha testosterone hakina
mpinzani wake kama progesterone na estrogen, na hivo huwa na hasira sana. na
huwa na umakini mkubwa anapoamua kufanya mambo yake, hii ni kutokana na uwezo
mkubwa wa kufatilia unaochangiwa na kiwango kikubwa cha testosterone, katika
ubongo wake. Huwa navutiwa sana na mwanamama mfizikia ‘’Sabine Hossenfelder’’
anavyozungumzia fizikia ngumu zaidi, tena bila kuwaza, tena aki enjoy!!
Migogoro na mme wake hasa huwa inasababishwa na
matarajio ya waume zao. Wanaume kwanza wanapozeeka huwa na kiwango kidogo cha
testosterone, na pia huwa na kiwango kikubwa zaidi cha estrogens. Hii huwafanya
kuhitaji zaidi kujaliwa au mtu wa kuwajali, ambaye atawafanya wajisikie tena
kama Watoto. ‘’kumbuka hii hali ya viwango, inafanana na ile iliyokuwepo
kipindi cha udogoni’’. Lakini mambo huwa kinyume kabisa, wamama hawa sasa hivi
hawana huo muda, na hawataki tena kuishi kama watumwa wa mtu!! Hawataki kuwaza
kuamka kumuandalia mtu mahitaji yake tena, au shughuli za muundo huu, hii
huwafanya wanaume wa maeneo mengi kuelekea upande wa pili na kuanza kutafuta
vibinti vidogo!! Na wengi hufanikiwa kutokana na kuwa na faida kubwa mbili,
kwanza, huwa wana uwezo mkubwa wa kiuchumi wa kuweza kuwamiliki mabinti ikiwemo
na mahitaji yao yote.
Lakini pili,
viwango vikubwa vya estrogen huwafanya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kujali
ukilinganisha na vijana, ambao, viwango vikubwa vya testosterone huwafanya
wasiwe watu wa kujali sana, na wakatili kwa baadhi ya mazingira, na pia sio
watu wakutulia sana. lakini pia wazee ambao bado huwa na nguvu za kiume,
ijapokuwa sio kwa msukumo kama wa vijana, bado huwaridhisha tu wanawake ambao
huitaji zaidi kujali ‘’intimacy’’ kuliko kijana anavyoweza kubaliana na hoja
hii. Hizi sababu huwafanya kuwa na
mafanikio tu katika Maisha yao na mabinti wadogo, ambao huweza kuwajali pale
ambapo wake zao hawana muda nao tena!! Maisha haya huendelea hata hapo akili ya
binti itakapohitaji mtoto!! Mgogoro huanzia hapo kwa kuwa mahesabu mapana ya
uwezo mkubwa wa wazee sasa, huwaambia kuwa na mtoto katika Umri wao ni
changamoto sana, na mabinti hawawezi kukubali kutoitwa mama!! Migogoro hii mara
nyingi huishia kwa hitimisho ambalo lisingesapotiwa na mwandishi!!
Lengo kubwa la kuyajua haya ni hili, kila mtu ajue
kipindi alicho nacho na msukumo mkubwa zaidi alio nao, kwa lengo la kujiepusha
zaidi pale msukumo unapokuelekeza katika upande mbaya!! Kumbuka binadamu sio
roboti na ndio maana unaweza soma kitabu hiki na kikakusaidia kwa kuwa, Pamoja
na kuwa homoni na sifa za ubongo zinaweza kukusukuma kuelekea katika jambo
Fulani, lakini akili na maarifa kama utakuwa ukijua, zinaweza kukusaidia
ukajiepusha. Hii ni sawa na pale hasira zinapokutaka utukane, lakini akili ikakuzuia,
hiyo inamaanisha hasira ambayo ni matokeo ya fiziolojia ya homoni na mengineyo,
huwezwa tulizwa na akili!! Kutokujua ndiko kufa, watu wanaangamia kwa
kutokujua. Nimewahi kutana na wamama wa miaka 50 nakuendelea, wapo baadhi wasio
na shida hizi kabisa, na hasa ni wale walio na Imani nzuri. lakini wapo wengi
sana ambao huishi mfumo huu wa Maisha kwa kutokujua kipi kinachowasukuma. Na
jamii zetu zina wazee wengi sana wahanga wa familia zao kutokana na tabia hizi,
tunapaswa kutambua na kusaidiana kila inapowezekana.
NAMNA YA KUPATA KITABU FULL COPY.
Unaweza wasiliana nasi kupitia
MOBILE NO: +255 6139 069 30 DR. BRIGHTON SHOO
FULL SOFTCOPY 5,000/=TSH
FULL HARDCOPY 10,000/=TSH
KUMBUKA!!
Injili ya sayansi Q5 haina ajenda yoyote ya Biashara,
lakini haki miliki ya kitabu inamilikiwa na Dr.Brighton Shoo. kwa Lengo la
kukuza taasisi ya Injili ya Sayansi. na pia, kuwasilisha maarifa kwa idadi
kubwa zaidi. Ubarikiwe unaposoma, unapoelewa, na unapofikiria kuwasaidia
wengine.
Kupata full soft copy link👇👇👇

Join the conversation