Jipatie maarifa kutoka vitabu bora vilivyoandikwa na Dr Brighton shoo kuusu imani, sayansi, afya, teknolojia, asili, malezi, saikolojia na mazingira

INJIILI YA SAYANSI Q5

INJILI YA SAYANSI Q5


Injili ya sayansi Q5 ni kitabu kinachoangazia tofauti za ubongo wa jinsia ya kiume na ubongo wa jinsia ya kike. Kwa karne nyingi sana, tofauti juu ya namna ubongo wa kike na ubongo wa kiume unavyo tofautiana, zimekuwa zikitafakariwa kwa changamoto kubwa sana. Hii ni kutokana na uwepo wa teknolojia ndogo sana ya mbinu za kiutafiti, za sayansi ya ubongo kwa hapo awali. Si rahisi na haiwezekani kwa mtu asiyemtaalamu au mzoefu wa taaluma za ubongo kuweza kugundua tofauti za ubongo wa mwanamke na wa mwanaume kwa kuuangalia kwa nje.

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kutambua sifa mbalimbali za ubongo wa kike na wa kiume kisayansi zaidi. Utambuzi husaidia kwanza, kuondokana na mitazamo hasi kama ya kuamini hakuna tofauti za kijinsia katika ubongo. pili, husaidia kujua tofauti na sifa mbalimbali za Ubongo kulingana na jinsia Fulani. pia husaidia kujua ubora zaidi wa mpangilio wa asili kimajukumu na ufanisi zaidi, pale mtu wa jinsia Fulani, anapojijua zaidi sifa zake, na kuutumia ubora wake.

Kitabu hiki hakina hoja zozote zinazoelekeza mitazamo juu ya ubora wa jinsia moja zaidi ya nyingine kwa ujumla! Lakini kinatoa sababu bora zaidi za kwanini jinsia moja huonekana bora zaidi ya jinsia nyingine katika sifa Fulani, kutokana na tofauti za kijinsia.

Kitabu hiki kinamsaidia msomaji kujua msukumo wa sifa zake nyingi sana, zinazotokana na msukumo wa jinsia yake, kutokana na  mifumo ya mwili wake kijinsia, katika vipindi vyote vya ukuaji. Na kinasaidia sana wazazi na walezi, kujua namna wanaweza kuwasaidia Watoto na vijana wao, kutokana na shida za ukuaji, ambazo kama mtu ataelewa msingi wake, basi atajua  namna ya kushughulika nazo.

Kitabu hiki kina malengo mengi sana, na miongoni ni kupambana na matatizo mengi sana yanayotokana na kutoelewa tofauti za kijinsia. na kupelekea kufeli kwa majukumu baadhi kiutendaji, kwa kuchanganywa kimtazamo  hata watu wakaamini wanawake na wanaume ni matokeo tu ya mabadiliko kadhaa, na hata, wanaweza wakabadishwa kuwa namna yeyote ile. Pia msomaji ataelewa ubora zaidi wa Ubongo wa wanawake, na ubora zaidi wa  Ubongo wa wanaume. hii itamsaidia kujua thamani ya tofauti zetu za kijinsia, na namna bora zaidi ya kunufaika nazo kama zawadi ya asili. na pia hata kuvumuliana panapotokea udhaifu unaotokana na tofauti za kijinsia.

Changamoto kubwa zaidi katika kitabu hiki ni namna nyepesi ya kuwasilisha ajenda baadhi kwa baadhi ya wasomaji walioathiriwa na mitazamo ya kiugandamizaji ya kijinsia, kama wanaume wanaoamini kuwa wao, ni kichwa kwa kila jambo, au wanawake ni wadhaifu kiuwezo kwa ujumla!  lakini pia wanawake wanaoamini wao wanaweza kila jambo, na wamekuwa wakikandamizwa kifikra. Pia kuna changamoto ya tabia za Ubongo wa Mashoga ambao hutumiwa na baadhi ya wanasayansi kama ishara ya kutokuwepo kwa uthabiti wa mipaka ya kijinsia, kitabu hiki kinatoa majibu mazuri zaidi ya kuondokana na fikra hizo.

Ubora wa kitabu hiki ni namna ambavyo hakijaegemea katika mitazamo ya kifalsafa, lakini kimejikita katika matokeo ya tafiti ya kisayansi, hasa sayansi ya Utendaji wa Ubongo ‘’Neurology’’, saikolojia ‘’psychology’’, Sayansi za mifumo ya homoni ‘’Endocrinology’’, Tafiti za Sayansi ya Ubongo kwa Ujumla ‘’Neurosciences’’,  Mitazamo ya kijamii ‘’Cultural Views’’ na mwisho zaidi ni Biblia ‘’Bible’’  ambayo hujenga msingi hasa panapobakia makisio katika Sayansi  Za mabadiliko ‘’Evolutionary Sciences’’.

SHUKURANI

Kwanza kabisa Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha  kuelewa kiundani swali nililokuwa nikijiuliza sana awali ‘’Kuna maana gani ya Mungu kuwa wa Haki na Usawa, kama aliamua Kuumba Jinsia moja kuwa Bora zaidi ya nyingine? Na akawa anachagua mmoja kuzaliwa mdhaifu na mwingine kuwa mwenye nguvu? hakuna anayechagua kuzaliwa jinsia yeyote ile! mtazamo wowote ule uliojikita kuamini kuna Jinsia moja Bora zaidi ya nyingine Kwa Ujumla, umejengwa katika msingi wa kuamini Mungu ni mgandamizaji (hii ni hoja pendwa kwa wanasayansi wasioamini wakisema’’Vitabu vya Imani vina ukandamizaji wa kijinsia’’), ni kweli wapo sahihi Kwa kuwa hawaelewi kiundani.

Nilianza kuamua kuandika  baada ya kugundua hisia za maumivu ya ugandamizaji kijinsia kwa karne nyingi nyuma, zimepelekea misukumo mingi hasi, ambayo inapelekea kila kukicha kutokea kwa madhara makubwa katika ngazi za mifumo mikubwa mpaka kwa mtu mmoja mmoja, kwa kutojua nini kipo nyuma ya Ubongo kwa kila jinsia.  Na kibaya zaidi, wanataaluma wengi sana, na wazazi, hawajui namna bora kabisa za kushughulika na changamoto za kijinsia, na malezi yamekuwa ni shida kubwa mfano wake haujawahi tokea!

Natambua mchamgo mkubwa sana wa familia yangu, Mama yangu Dementina F. Mkote,  Baba yangu Godwin E.Shoo, Ndugu zangu Neema, Catherine, Grayson, Eunice, Victor, Alen, Peter, Stanley, Bruno, Beti, Daudi, Alestida, Judith na Gracious Shoo. Shangazi zangu Lilian Shoo, Anith Mkote, Alfonsina Mkote na wenginewe, wajomba zangu Mario mkote, Frank Mmary, Ernest Shoo, Ignas Mkote, Francis mkote na wenginewe. Bibi yangu Betila Mkote. Familia yangu imechangia sana mtazamo wangu mpana wa thamani na tofauti za kijinsia, bila kuathiriwa na falsafa hasi, na hii ni kutokana na kutanguliza msingi wa Biblia, na Uzoefu wa kujifunza elimu za sayansi, tamaduni na Jamii.

Natambua mchango mkubwa sana wa marafiki zangu, Dr. John , Dr. Emannuel, Dr.Mpogo Issa, Dr. Magessa, Dr. Mathew, Dr. Anatory, Dr. Mwangosi, Dr. Alex, Dr. Eric, Dr. Pascal, Dr. Bernard, Dr.Mpoki, Dr.Salim, Dr. Luckydube Mwaipape, Dr. Martina mgeni, Dr. Zephania bertha, Dr. Sweetbeth, Dr.Winston, Dr.Adela, Dr. Ntemi, Dr.Masasila, Dr. Kajange, Dr. Kapinga, Dr.Aidan, Dr. Daniel, Dr.Edison Kavenuke, Dr.Aweza james, Dr.Manyerere, Dr.Gilbert Shayo, Dr. Juma, Dr. Joshua, Dr. masasila, Dr. Amos, Dr. Careem, Dr.Chedela na wenginewe. Hawa wamekuwa Pamoja na mimi katika hatua mbalimbali nilizokuwa nikijifunza kwa undani sifa mbalimbali za tofauti za kijinsia kwa Wanyama, na kwa binadamu.

Natambua mchango mkubwa sana wa marafiki zangu, waliokuwa wakinisapoti katika kipindi naendelea na uandishi wa kitabu hiki, Edward Singo, Hagai, Samuel, Bright na Amara nyongole, Ernest B Jonass, Katemi, Miss Esta, Mr.Kanolo, Mr. Alex, Mr. Nyange, na wenginewe.

Natambua mchango mkubwa sana wa mtaalamu wa Ubongo na afya ya akili ‘’neuropsychiatrist’’ Mama Louann Brizendine, ambaye amekwisha Andika kitabu kuhusiana pia na tofauti za kijinsia, Nimetumia nukuu zake baadhi, japo si kwa baadhi zilizo na mashaka! kuna tafiti nyingi sana ambazo nitatoa nukuu kwa heshima ya watafiti. Kumbuka yapo masomo mengi ambayo yanaunda upekee wa kitabu hiki, ukiachana tu na nukuu zilizokwisha nukuliwa kwa vitabu na tafiti mbalimbali.

USHAURI WA NAMNA YA KUSOMA NA MATUMIZI YA LUGHA

Kwa mtu ambaye hatakuwa na msingi mzuri kabisa wa masomo ya sayansi, anaweza kuanza kusoma sura ya tatu na sura ya nne. Lakini pia anaweza pitia sehemu kadha wa kadha katika sura ya kwanza na sura ya pili. Kitabu hiki kinahusisha matumizi ya lugha ya Kiswahili, na matumizi ya lugha ya kiingereza kwa maneno na vitendo visivyo na tafsiri za Kiswahili za moja kwa moja. Uchambuzi kadhaa ambao unaweza onekana kuwa ni wa kina sana, una malengo mapana zaidi ya kuziondoa hoja hatarishi za kifalsafa, na mitazamo hasi isiyo na misingi ya ukweli.

pia kitabu kinahusisha matumizi ya visa vya wahusika kwa sehemu baadhi ya sura ya tatu, na sura ya nne. wahusika hawa na visa vyao ni vya kutungwa. msomaji anapaswa kutambua njia pekee bora zaidi ya kuileta sayansi ya kina katika jamii, ni kupitia kurejelea tabia zilizozoeleka.

                                                                   YALIYOMO

SURA YA 1. Error! Bookmark not defined.

MSINGI WA TOFAUTI ZA UBONGO KULINGANA NA JINSIA.. Error! Bookmark not defined.

HISTORIA.. Error! Bookmark not defined.

KWANINI MSUKUMO WA KUSOMA TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA NI MDOGO?  Error! Bookmark not defined.

KWANINI INAPASWA KUJIFUNZA TENA SAYANSI YA UTOFAUTI WA UBONGO KIJINSIA?  Error! Bookmark not defined.

UTANGULIZI Error! Bookmark not defined.

MAKUNDI MAKUBWA MATATU YA TOFAUTI ZA UBONGO KIJINSIA. Error! Bookmark not defined.

AINA YA KWANZA YA TOFAUTI ZA KIJINSIA.. Error! Bookmark not defined.

AINA YA PILI YA TOFAUTI ZA KIJINSIA.. Error! Bookmark not defined.

AINA YA TATU YA TOFAUTI KIJINSIA.. Error! Bookmark not defined.

Jambo Moja laweza leta madhara tofauti kwa jinsia ya kike na kiume!!. Error! Bookmark not defined.

SABABU NA ASILI YA JINSIA.. Error! Bookmark not defined.

NAMNA JENETIKIA NA HOMONI ZINAVYOSABABISHA JINSIA YA KIUME NA KIKE  Error! Bookmark not defined.

NADHARIA ZA UTOKEAJI WA MASHOGA AU USHOGA.. Error! Bookmark not defined.

Sababu za maendeleo ya ukuaji tumboni Error! Bookmark not defined.

Sababu za Mama kuzaa Watoto wakiume wengi Error! Bookmark not defined.

Sababu za jenetikia za Kinasaba cha Ushoga ‘’Xq28’’ Error! Bookmark not defined.

Kielelezo kwa Kondoo na ushoga. Error! Bookmark not defined.

Kielelezo cha mapacha na ushoga. Error! Bookmark not defined.

Tezi ya Thyroid na Ushoga. Error! Bookmark not defined.

Ushoga na faida za ‘’natural selection’’ Error! Bookmark not defined.

Sababu za Ushoga kwa tafiti za kisaikolojia. Error! Bookmark not defined.

MAFANIKIO MAKUBWA YA NADHARIA ZA USHOGA KWA JAMII ZA WASOMI Error! Bookmark not defined.

MAFANIKIO MAKUBWA YA NADHARIA ZA USHOGA KWA JAMII ZA WANA DINI Error! Bookmark not defined.

NAMNA BIOLOJIA YA KISASA ZAIDI INAVYOSAPOTIANA NA BIBLIA KUWA USHOGA SIO HALI YA KIJINSIA YENYE SABABU ZA KUPOKELEWA KIMAADILI Error! Bookmark not defined.

HOJA YA KWANZA.. Error! Bookmark not defined.

JE UNAWEZA WAJIBU KUHUSU Xq28 (Gay gene-Kinasaba cha ushoga)?  Error! Bookmark not defined.

HOJA YA PILI Error! Bookmark not defined.

Ushoga kwa namna nyingine ni Changamoto ya Kibiolojia na sio Jinsia!!  Error! Bookmark not defined.

HOJA YA TATU.. Error! Bookmark not defined.

HOJA YA NNE. Error! Bookmark not defined.

Hakuna Hisia ya Asili ya Mwanaume kutamani Kuingiliwa!. Error! Bookmark not defined.

Wanyama sio Kielelezo cha Ushoga!. Error! Bookmark not defined.

HOJA YA TANO.. Error! Bookmark not defined.

HOJA YA SITA.. Error! Bookmark not defined.

HOJA YA SABA.. Error! Bookmark not defined.

NAMNA YA KUWASAIDIA MASHOGA KWA UPENDO.. Error! Bookmark not defined.

HITIMISHO LA SEHEMU YA KWANZA.. Error! Bookmark not defined.

SURA YA 2. Error! Bookmark not defined.

KINACHOUTOFAUTISHA  UBONGO WA KIUME NA WA KIKE. Error! Bookmark not defined.

Utangulizi Error! Bookmark not defined.

SEHEMU ZA UBONGO ZILIZOTOFAUTIANA KULINGANA NA JINSIA.. Error! Bookmark not defined.

Sehemu Za Ubongo Zilizoendelea Zaidi Kwa Wanawake. Error! Bookmark not defined.

Anterior cingulate cortex (ACC). Error! Bookmark not defined.

Prefrontal Cortex (PFC). Error! Bookmark not defined.

Insular cortex. Error! Bookmark not defined.

Hypothalamus. Error! Bookmark not defined.

Hippocampus. Error! Bookmark not defined.

Corpus Callosum.. Error! Bookmark not defined.

Broca’s Area. Error! Bookmark not defined.

Wernicke’s Area. Error! Bookmark not defined.

Mfumo wa Hisia wa Kuiga na kuhisi Huruma ‘’Mirror Neuron system’’ au MNS. Error! Bookmark not defined.

Mfumo wa kuchunguza na kuzisoma Sura za Vitu na uzingatiaji. Error! Bookmark not defined.

Uwezo mkubwa wa kutumia Lugha na kutumia maneno ‘’Verbal skills’’ Error! Bookmark not defined.

Upana wa Ubongo ‘’cortical thickness’’ Error! Bookmark not defined.

HOMONI ZENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWA WANAWAKE. Error! Bookmark not defined.

Estrogen. Error! Bookmark not defined.

Progesterone. Error! Bookmark not defined.

Oxytocin. Error! Bookmark not defined.

Cortisol Error! Bookmark not defined.

DHEA au ‘’Dihydroepiandrostedione’’ Error! Bookmark not defined.

Androstenedione. Error! Bookmark not defined.

Allopregnenolone. Error! Bookmark not defined.

Testosterone. Error! Bookmark not defined.

Prolactin. Error! Bookmark not defined.

SEHEMU ZA UBONGO ZILIZOENDELEA ZAIDI KWA WANAUME. Error! Bookmark not defined.

Medial Preoptic Area (MPOA). Error! Bookmark not defined.

Temporal Parietal Junction (TPJ). Error! Bookmark not defined.

Tatizo vs mwanaume vs mwanamke!!. Error! Bookmark not defined.

Dorsal Premammilary Nucleus ‘’DPN’’ Error! Bookmark not defined.

Amygdala. Error! Bookmark not defined.

Rostral Cingulate Zone ‘’RCZ’’ Error! Bookmark not defined.

Ventral Tegmental Area ‘’VTA’’ Error! Bookmark not defined.

Periaqueductal gray ‘’PAG’’ Error! Bookmark not defined.

Uwezo wa kuchakata taarifa kwa kuumba Maumbo ya Taswira Kichwani. ‘’Spatial Skills’’ Error! Bookmark not defined.

Ukubwa wa Ubongo kwa Ujumla ‘’brain Volume’’. Error! Bookmark not defined.

HOMONI ZENYE MATOKEO MAKUBWA ZAIDI KWA WANAUME. Error! Bookmark not defined.

Testosterone. Error! Bookmark not defined.

Vasopressin. Error! Bookmark not defined.

Mullerian Inhibiting Substance ‘’MIS’’. Error! Bookmark not defined.

Oxytocin. Error! Bookmark not defined.

Prolactin. Error! Bookmark not defined.

Baba ana dalili za ujauzito Kama mkewe!. Error! Bookmark not defined.

Cortisol Error! Bookmark not defined.

Androstenedione. Error! Bookmark not defined.

Dopamine. Error! Bookmark not defined.

Estrogen. Error! Bookmark not defined.

NADHARIA  ZA UTOFAUTI WA UBONGO ZILIZOPITWA NA WAKATI Error! Bookmark not defined.

WATU WALIOENDELEA ZAIDI KATIKA UBONGO WA KUSHOTO AU UBONGO WA KULIA   Error! Bookmark not defined.

‘’left brained or right brained’’ Error! Bookmark not defined.

WATU WALIOBORA UPANDE WA KUSHOTO ‘’left brained’’ Error! Bookmark not defined.

WATU WALIOBORA UPANDE WA KULIA ‘’right brained’’ Error! Bookmark not defined.

CHANGAMOTO KUBWA ZA HII NADHARIA.. Error! Bookmark not defined.

NADHARIA ZA KUWA UBONGO WA KIUME NA WA KIKE NI SAWA KABISA!!  Error! Bookmark not defined.

MSINGI WA HISIA ZA UGANDAMIZAJI WA KIJINSIA ULIOFICHIKA!!. Error! Bookmark not defined.

TATIZO LILILOIBUKA KARNE YA KUMI NA SABA NA KUMI NA NANE!. Error! Bookmark not defined.

SABABU ZA UBORA WA WANAUME KATIKA HISABATI NA FIZIKIA.. Error! Bookmark not defined.

UHALISIA KUWA UWEZO WA HISABATI NA FIZIKIA SIO UWEZO MKUBWA WA KIAKILI!  Error! Bookmark not defined.

MGOGORO WA KIJINSIA WA NAFASI ZA JUU KABISA ZA UONGOZI Error! Bookmark not defined.

SURA YA 3. 13

UBONGO NA SIFA ZA MWANAMKE KATIKA VIPINDI MBALIMBALI VYA UKUAJI 13

Utangulizi 13

UBONGO WA  KATOTO KAKIKE TUMBONI 13

KATOTO KA KIKE KAZURI! DADA HELLEN ‘’MIAKA 1-10’’ 14

Uwezo wa kuzisoma sura. 14

Hellen haitaji stress!!. 16

Usipigane Hellen!. 16

Lugha ya ‘’Twende!! au Tu...’’ 16

Hellen na rafiki zake tu kina Eunice!!. 17

Hellen ana misingi yake!!. 17

UBONGO WA MSICHANA MZURI, MIAKA ‘’11-19’’ 18

Kichwani mwake mrembo huyu. 18

Wasichokijua Wazazi!!. 19

Safari Ya Mzunguko Wa Mawimbi Ya Estrogen Na Progesterone. 20

Kuhusu Stress!!. 22

Umegundua filamu zake!!. 22

WIKI MBILI ZA KWANZA ZA MZUNGUKO!!. 22

WIKI MBILI ZA MWISHO WA MZUNGUKO!!. 22

JE WAJUA UNAOUITA UMBEA!!. 23

KATI KATI YA MZUNGUKO WA MWEZI!!. 23

UMESHAJUA KWANINI HUSHINDA NA SIMU!!. 24

WASICHANA WANAPOFELI KWA WAVULANA!!. 24

SIRI ILIYOFICHIKA ENZI HIZI KWA WAVULANA!!. 25

Mahusiano Yanapovunjika!!. 25

ANALALA SANA HATA MPAKA SAA SITA!!. 26

NI MKOROFI SANA!!. 27

Tarehe za Shida!!. 27

Je ni Kweli Ule Msemo wa ‘’Wanawake Wenye Miili Mikubwa Hawana Shida?  28

TATIZO KUBWA LA KUWARUHUSU KUFANYA NGONO!!. 29

MABINTI WENYE SIFA ZA KIPEKEE!!. 30

UBONGO WA BINTI MZURI RACHEL ‘’MIAKA 20+’’ 31

Maisha na Kazi 31

UMEME WA HISIA!!. 31

HOJA YA KIBIOLOJIA.. 32

Sababu Za Mwanaume Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa Binti!!. 32

Sababu Za Binti Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa Mwanaume!!. 34

Muhimu Sana Kujua Kuhusu Mivuto Ya Kimapenzi!!. 36

UBONGO WA BINTI ‘’RACHEL’’ KWENYE MAPENZI MAPYA.. 36

BIOLOJIA YA UBONGO WA RACHEL KWENYE PENZI JIPYA!!. 38

Kwa Mara ya Kwanza Kuzima Kwa ACC &PFC Kwa Rachel!!. 39

KUUNGANISHWA KIHISIA.. 40

Je Wajua Biolojia Pana Ya Kiss!!. 41

NADHARIA ZA KUZIKATAA ‘’HAKUNA JENETIKIA ZA UAMINIIFU’’ 41

UBONGO WA MAMA EUNICE!!. 42

Mama na mtoto. 42

Biolojia Mpya ya Umama. 42

Maisha Baada ya Eunice Kuzaliwa!!. 43

Wazazi wasio waleaji wazuri!!. 44

KUHUSU KUZAA KWA OPERSHENI!!. 44

NGUVU YA KUNYONYESHA!!. 45

MAMA MBAYA HUTENGENEZA MAMA MBAYA!!. 45

JANGA LISILOONEKANA!!. 46

BIOLOJIA YA MIGOGORO MINGI YA WAMAMA NA WAUME  ZAO.. 47

UBONGO WA MWANAMKE ULIOKOMAA ‘’MIAKA 51+’’ 50

Ukomavu. 50

HAJALI WALA HAWAZI!!. 50

HUWA NA HASIRA KWA WAKATI FULANI HASA NA MME WAKE!!. 51

SURA YA 4. Error! Bookmark not defined.

VIPINDI NA SIFA MBALIMBALI KATIKA UBONGO WA WAKIUME. Error! Bookmark not defined.

Utangulizi Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA KATOTO KA KIUME TUMBONI!. Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA WATOTO WA KIUME ‘’VICTOR NA ALEN’’ MIAKA 1-11’’ Error! Bookmark not defined.

UKITAKA KUMTULIZA MPE GEMU AANGALIE!!. Error! Bookmark not defined.

USIMPE SHUGHULI MOJA!!. Error! Bookmark not defined.

HABEMBELEZEKI KIRAHISI!!. Error! Bookmark not defined.

HANA MUDA WA KUKUANGALIA SANA!!. Error! Bookmark not defined.

UKIMKATAZA NDIYO KAMA UMEMCHOCHEA!!. Error! Bookmark not defined.

MIDOLI NA MICHEZO YA KUIME!!. Error! Bookmark not defined.

HAWAPENDI KUFANANISHWA NA WASICHANA!!. Error! Bookmark not defined.

HUPENDA KUWA BINGWA AU MSHINDI!!. Error! Bookmark not defined.

KUPIGANA KWAO NI MICHEZO!!. Error! Bookmark not defined.

MWENZAKE NDIYE KIPAUMBELE CHAKE!!. Error! Bookmark not defined.

UFALME KATIKA ULIMWENGU WA WAVULANA!!. Error! Bookmark not defined.

NAMNA WANAVYOUNDA MAKUNDI YAO!!. Error! Bookmark not defined.

HUPENDA SANA MAGEMU NA FILAMU ZA MAPAMBANO!!. Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA KIJANA WAKIUME ‘’MIAKA 11-19’’ Error! Bookmark not defined.

HAELEWEKI NA HAPENDI UNACHOPENDA.. Error! Bookmark not defined.

BIOLOJIA YA NGUVU MPYA YA TESTOSTERONE!. Error! Bookmark not defined.

SIRI YA MAWAZO YA KIJANA WA KIUME TU!!. Error! Bookmark not defined.

HISIA ZA KUBOREKA NA KULALA SANA!!. Error! Bookmark not defined.

HISIA ZA KUTOKUBALIANA NA TARATIBU!!. Error! Bookmark not defined.

MGOGORO WA PETER, CAREN NA MWALIMU NYAGAWA!!. Error! Bookmark not defined.

BIOLOJIA YA CHANZO CHA MGOGORO WA PETER!!. Error! Bookmark not defined.

TABIA ZA UBABE NA MIONEKANO YA UGUMU!!. Error! Bookmark not defined.

HAPENDI KURUDIA RUDIA NA SAUTI ZA MAKELELE!!. Error! Bookmark not defined.

MWONEKANO WA KUJIFANYA HAJALI!!. Error! Bookmark not defined.

SIRI YA KUTOJALI!!. Error! Bookmark not defined.

NGUVU YA MASHINDANO!!. Error! Bookmark not defined.

HUJIDANGANYA WAO NDIO WANAJUA!!. Error! Bookmark not defined.

UJINGA HUZIDI WANAPOKUWA PAMOJA!!. Error! Bookmark not defined.

MSINGI WA NGUVU ZA MAKUNDI RIKA.. Error! Bookmark not defined.

HUANDALIWA KISAIKOLOJIA KUFANYA MAPENZI KIMAWAZO!!. Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA KIJANA WA KIUME, MIAKA 20+. Error! Bookmark not defined.

KUPENDA AU KUTAMANI!!. Error! Bookmark not defined.

MSINGI MKUBWA ZAIDI WA UFANYAJI KAZI!!. Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA BABA.. Error! Bookmark not defined.

Malezi ya Baba. Error! Bookmark not defined.

Baba na Vitisho vya Ukali Error! Bookmark not defined.

Baba na  binti yake. Error! Bookmark not defined.

UBONGO WA KIUME ULIOKOMAA!! MIAKA 50+

UNAWEZA SOMA SURA IFUATAYO FREE.............

kumbuka kufahamu msingi wa sifa zote za tabia za kike, kama inavyoelezwa katika sura hii, unapaswa kurejea tena kusoma sura za mwanzo zinazoelezea kiundani zaidi mifumo ya ubongo wa mtoto wa kike.na pia, sifa nyingi zimeelezwa katika sehemu inayodadavua zaidi utofauti wa ubongo, na sifa zake. kwa wanaume, na wanawake. toka uundwaji wa mimba, mpaka uzeeni. sura ya tatu inadadavua utofauti zaidi katika mifano michache ya visa vya maisha ya uhalisia ya kijinsia.

SURA YA 3

UBONGO NA SIFA ZA MWANAMKE KATIKA YA VIPINDI MBALIMBALI VYA UKUAJI

Utangulizi

Zipo hatua kadhaa za ukuaji wa mwanamke. Katika hatua hizi, ni muhimu kutazama sifa na mabadiliko ya msingi kabisa katika kila hatua, ili kuweza kujua sifa kadhaa za msingi kabisa, ambazo hujenga msingi wa tabia kadhaa kwa wanawake, katika vipindi mbalimbali vya ukuaji.utambuaji wa sifa hizi huleta faida kubwa sana ya kuwawezesha wasomaji kujua namna bora kabisa ya kujitawala au kujijibu maswali kadhaa ya kwanini tabia Fulani hutokea zaidi kwa kipindi Fulani, na zina lengo gani?

UBONGO WA  KATOTO KAKIKE TUMBONI

Seli zake za ubongo huwa zina chromosomes za (XX), hii ina maanisha kuwa, huwa zina vinasaba au genes za ukuaji wa ubongo kwa fasta zaidi, na ubongo hukua ukitengeneza Zaidi network za ubongo, zitakazo sapoti zaidi tabia za kike. Na hasa huwa katika sehemu za mawasiliano, hisia za vyakula na mfumo mzima wa ulaji, kumbukumbu za kihisia, mifumo ya kupambana na hasira. na huku kwa wanawake, huwa haya maendeleo yanafanikiwa kutokana na Ukosekanaji wa kiwango kikubwa cha Testosterone, ambayo ingeua baadhi ya seli, na kuzuia maendeleo mapana zaidi ya sifa hizi. Ubongo wa kike huanza kuwa na uwezo wa kutumia pande zote mbili za ubongo, vizuri kabisa, tokea hatua za awali kabisa za ukuaji.

Katika hatua hizi za awali ni muhimu kwa mama kutokuwa na changamoto za misongo ya Mawazo, hii ni kuzuia kuzalisha chembechembe za stress hormones ‘’cortisol’’, na pia stress na mifumo mibaya ya ulaji, hupelekea kiwango kikubwa sana cha ‘’free radicals’’, ambazo huenda kuathiri maendeleo bora ya ubongo wa mtoto.

Maendeleo mapana ya biolojia yanaonesha kuwa, tofauti na mitazamo ya awali ya kuwa madhara huwa yanamkuta mama kwanza, na kisha kurithishwa kwa mtoto, au unaweza uita huu mtazamo kama ‘’weismann barrier’’,sasa hivi inafahamika kuwa, madhara humuathiri mama mpaka seli zitakazo muunda mtoto moja kwa moja. Kwa hiyo, hata kabla binti hajazaa, tayari kila anachokifanya, anamuathiri na mtoto wake!

Ni muhimu wamama wajawazito kutokuwa na stress kabisa, haijalishi ni ujauzito wa mtoto yupi, lakini pia ni muhimu kupunguza na ikiwezekana kuachana kabisa na ulaji wa bidhaa za kisasa, ambazo huwa na chembechembe nyingi sana za utunzaji chakula, ambazo huwa na madhara kama tulivyoona katika injili ya sayansi sehemu ya nne.

Mama anapofurahi zaidi, ndivyo na mtoto wake anapokuwa na faida kubwa zaidi ya maendeleo ya ukuaji wake wa ubongo, ikiwemo na kuongezeka kwa ufanisi wa mifumo ya kinga, kupunguza hatari za makosa ya ufundi wa kijenetikia n.k.

miziki yenye sauti kubwa sana sio mizuri pia, kwa kuwa, frequency kubwa huweza kuathiri utendaji bora wa jenetikia, tuliona sehemu ya nne kuwa, DNA ni sensitive sana kwa muziki, hivyo ni muhimu kuchukua hatua kwa wamama wajawazito, hasa wa zama hizi za midundo mikubwa kila wakati. Kuchelewa kulala pia huongeza muda wa mzunguko wa cortisol, hivyo uangaliaji sana wa tamthilia usiku kwa wajawazito unapaswa kuwa na kiwango, kama lengo litakuwa ni kuzaa binti mwenye akili kama mama yake!!

KATOTO KA KIKE KAZURI! DADA HELLEN ‘’MIAKA 1-10’’

Uwezo wa kuzisoma sura

Sifa ya kwanza ya katoto haka tukaite ‘’Hellen’’, ni uwezo wa kuzisoma sura! Ubongo wa mtoto wa kike huzaliwa ukiwa upo mbele kiukuaji kwa mwaka mmoja mpaka miwili mbele, zaidi ya ubongo wa mtoto wa kiume. Mtoto hellen amezaliwa akiwa tayari ana uwezo wa kuzisoma sura na kuelewa hisia za anao waangalia. Wamama wengi ambao huanza kulea Watoto wa kike na kisha kuja kulea Watoto wa kiume, huisi penginepo Watoto wao wakiume wana shida au penginepo hawavutiwi sana nao, kwa namna ambavyo huwa hawana muda wa kutazamana na mama zao kwa kitambo kidogo, kama ambavyo huwa kwa Watoto wa kike.

Hellen hakuathiriwa na kiwango kikubwa cha testosterone kipindi yupo tumboni, ambacho kingeua seli na mifumo yake ya kuweza kuelewa mawasiliano na hisia za wengine. Na anapozaliwa tu huwa kwa haraka sana akiwa na uwezo wa kuwasoma anaowatazama! na kugundua kama ni watu wenye upendo au wenye kuweza kumhatarisha.

Tafiti iliyofanywa kwa chumba ambacho kilikuwa na wamama kadhaa na Watoto wao wa kike, na wakiume. na wamama hawa wakapewa kazi ya kuwazuia tu Watoto wao wasishike moja ya vitu vilivyokuwepo mle ndani, kwa kuwaangalia tu na kuwakazia macho! Tafiti ilionesha kuwa, Watoto wote wa kike, wakina Hellen, baada tu ya kuwaangalia mama zao, waliacha kabisa kushika sehemu ile. Ila Watoto wakiume, wakina victor na alen na wenginewe, ni kama vile mama zao waliwachochea zaidi kutaka hata kujua zaidi kuna nini pale! Haimaanishi kuwa Watoto wa kiume ni wakaidi! Ila ina maanisha kuwa, Watoto wa kike huzaliwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuzisoma sura, uwezo huu huwa ni miaka miwili zaidi ya Watoto wa kiume, ambao nao huja kuupata mbeleni. Inafahamika zaidi kisayansi kuwa, Watoto wa kike hupitia kipindi kinachoitwa ‘’Infantile puberty’’, kipindi ambacho huusiana na uzalishwaji wa estrogen nyingi sana, kama ilivyo kwa binti mkubwa, kwa muda wa miezi 24 toka kuzaliwa! huku Watoto wa kiume wakipitia kipindi hichohicho kwa muda wa miezi 9 tu. Kipindi hiki huaminiwa kuwawezesha zaidi Watoto wa kike katika uwezo wao wa ubongo, wa kuchakata taarifa za mazingira yao.

Kwake hellen unapomtazama, ndipo unamsikiliza, ukimsikiliza huku unatazama kwingine, ni kama vile huna muda naye, na hatalifurahia hilo! Hii ni kutokana na Imani yake ya kuwa ulimwengu umejawa watu wenye aina moja ya kuelewa mawasiliano kama yeye.

Hellen haitaji stress!!

Mazingira ya hellen kwa miaka yake miwili ya kwanza duniani humjengea uhalisia wa Maisha yake yote! Hii hatari imeonekana kwa tafiti za Wanyama mammalia wote, mtoto wa kike huathiriwa sana na madhara ya mazingira yake, mapema zaidi, kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuchangamana na mazingira yake. Kitaalamu hii inaitwa ‘’epigenetic imprinting’’, ni kama ambavyo nilivyoielezea katika sehemu za awali kabisa za tofauti za kijinsia. Tafiti huonesha kuwa, Wamama wenye misongo ya Mawazo au stress, huwa sio waleaji wazuri wa Watoto wao, na Watoto wao wakike, huathiriwa moja kwa moja. Na huchukua uhalisia wa mama zao kama ndiyo uhalisia wa dunia. Na huu ndiyo msingi wa uwepo wa wadada wenye sifa tofauti tofauti, mara nyingi haya ni matokeo ya mama wenye uleaji tofauti tofauti. Watoto wa kiume wameonekana kutoathiriwa na stress za mama zao katika mifumo yao ya fahamu. Kwa hiyo ni muhimu kupanga kuwa na mama asiye na misongo ya Mawazo, kama unapanga kuwa na Hellen mzuri.

Usipigane Hellen!

Hii ni sauti ambayo mara nyingi zaidi husikika katika kichwa chake. Ana uwezo mkubwa wa kusoma sura na kuzijua hatari na akachukua hatua ya kujiepusha mapema sana. Inatambulika uwezo huu kwa wanawake wa kuzisoma sura, hujengwa tangia awali kabisa, kwa lengo la kuwawezesha kuzungumza hata na vitoto vichanga, visivyoweza jielezea. Uwezo mkubwa wa kujua madhara ya hatari ya kupigana, kwa kuweza kudhibiti hasira, huchochea tabia za kupenda kufanya amani.

Lugha ya ‘’Twende!! au Tu...’’

Hellen na rafiki zake hupenda kuanzisha shughuli zao au michezo yao kwa kutumia lugha ya kuwaunganisha Pamoja. Mfano, tujenge nyumba, twendeni pale, tukapike, n.k.  utasikia akisema, ‘’unaweza niazima ndala zako za kijani! Na mimi nakupa zangu nyeupe, afu baadae nakurudishia!’’ hii lugha tayari imeshaonesha kujali na kujilinda. Watoto wa kiume huwa hawawezi kutumia lugha hii kirahisi, ingawa wanaijua pia, Victor huanza kwa kusema ‘’twende pale dogo! Au kama hauji..’’ hutumia lugha za kulazimisha sana au kutojali hisia za wenzao. Hii nayo hutokana na uwezo wao mdogo kwa nyuma ya miaka kidogo zaidi ya Watoto wa kike wanapozaliwa. Watoto wakike wanapotumia hii lugha ‘’affiliative speech’’, huwa ina nguvu sana, maana, kama mwenzake atakataa! Atajiona mwenye ukatili na kutojali, lakini kikubwa zaidi, pale anaposema ‘’unaweza..’’ anamaanisha, utakaposema , Hapana!! Yeye bado yupo salama, maana alikupa tu pendekezo ‘’suggestions’’ na sio kwamba alikuwa amekutegemea sana! Hizi ni akili nyingi sana.

Hellen na rafiki zake tu kina Eunice!!

Kati ya miaka miwili mpaka sita. Utakuta mara nyingi sana kina hellen wakicheza na marafiki zao tu wasichana, mara chache sana huvutiwa na wavulana. Hii ni kutokana na ndani ya dakika chache tu za kucheza na victor au alen, atajikuta akilia machozi pasipokuwa na chochote mkononi mwake! Watoto wakiume huwa ni wakorofi kutokana na uwezo wao mdogo wa kujali hisia za wenzao. Tafiti za magonjwa ya upweke na kutopenda kuchangamana na kushindwa kabisa kuwa na uwezo wa kukua kiakili ukielewa mazingira yako, ugonjwa wa ‘’Autism’’. huonesha kuwa, ugonjwa huu huwa mara Nane zaidi kwa Watoto wa kiume, ukilinganisha na watoto wakike. Hivyo, unaweza pata picha ni kwa namna gani ambavyo Watoto wa kiume hata bila kuwa na shida hii, huwa na uwezo mdogo wa kujali, na huku msukumo wao wa homoni za testosterone, ukiwafanya kuanza kupenda kushindana tangia hatua ya awali kabisa. Hizi sababu humfanya hellen kuamua kuchukua hatua ya kutafuta wenzake tu wanaoelewana.

Hellen ana misingi yake!!

Usije ukadanganywa kwa sababu ya kumuelezea kuwa ana uwezo mkubwa wa kujali, na kuelewa! ukahisi unaweza muendesha unavyotaka! Takwimu zinaonesha Watoto hawa wa kike hupuuzia jambo kama wakiliona halina maana kwao mara Ishirini zaidi (20x) ya Watoto wakiume. Hellen utamwona na wenzake wakipendelea michezo ya midoli, ambayo hupenda kuichezesha kuhusu ajenda za kijamii kama familia, mipangilio n.k. kumbuka Watoto wakiume huitumia hata midoli ya amani kama magari ya kivita! Takwimu pia huonesha kiwango kidogo sana cha testosterone kwa wasichana, huwafanya wawe watulivu zaidi katika tabia zao, ukilinganisha na wenye kiwango kikubwa, ambao huweza hata kuwa ‘’Tom Boys’’. Mara nyingi Msichana anapotaka kutawala, hujiongezea hatari ya kuwapoteza wenzake! na hivyo hutumia akili kubwa sana katika kubalansi mambo hayo mawili.

 

 

 

 

 

UBONGO WA MSICHANA MZURI, MIAKA ‘’11-19’’

Kichwani mwake mrembo huyu

Hapa shughuli ndipo huanza!! Miaka ya kumi na kitu au ‘’teenage years’’ huwa ni changamoto sana. Ubongo wa binti hujifuma tena upya, hukata matawi ya mifumo ya awali, hubadilisha mtazamo wa namna alivyokuwa akifikiri na kuhisi na kutenda. Humfanya kuwa mraibu wa mwonekano wake, humfanya kujiona amekuwa mwanamke haswa, biolojia yake hubadilika kuingia katika hatua ya kupevuka au kuvunja ungo, na hapa kipimo chake huwa ni namna jamii yake inavyomtazama. Sasa hivi, walimu  wake huwa ni wasichana wenye mionekano mizuri zaidi ya mvuto kwa wanaume.

Kuteka umakini wa wanaume sasa ndiyo msingi wa hisia ya kujiamini. Uraibu wa Kuwaza zaidi ya namna atakavyoonekana, huchochewa na kiwango kikubwa cha homoni za estrogen, ambazo hupamba moto zaidi kwa kipindi hiki. Wasichana hawa hujali sana mionekano yao ya kuvutia hasa wanapokuwa wakichangamana na wavulana. Wamama kadhaa hulalamika namna mabinti wao wanavyovutumia muda mrefu zaidi bafuni na mbele za vioo, hutamani kama ingewezekana basi, viuno vyao vingekuwa vyembamba zaidi, makalio yao yakatanuka zaidi na matiti yao yakaongezeka zaidi. Hayo na mengine mengi zaidi hulenga hasa kuwateka wavulana zaidi!

Huweza kupata Mawazo mengi sana, lakini hasa yaliyolenga zaidi, je mwonekano wao unaonekana ni wa mvuto kwa wavulana au la! Hii ni kwa kuwa ubongo wao huwatengenezea uhalisia mpya, wa kuwa na mvuto ndilo jambo la msingi zaidi.

Wasichokijua Wazazi!!

Wazazi wengi hawajui kuwa kinachotokea zaidi katika hatua hii ni kuwa, ubongo wa mwanamke hupitia katika hatua ya kujikamilisha, ukigongelea msumari ya kuwa, Je, amekuwa mwanamke kweli? katika hatua zote za maendeleo yake ya kuwa mwanamke, je sasa, anaonekana na kukubalika kweli kama mwanamke, anaonekana kama taswira ya mwanamke kweli anayefahamika na wanaume! Hivyo hapa ubongo hufanya mithili ya majaribio kujipima kama umefanikiwa kumuunda mwanamke. Ni kama ilivyo kwa mitihani mingine, kabla ya kuaminiwa kuwa umekidhi kuwa daktari, unapaswa kujipima, je, naweza pambana na kesi ya mgonjwa na akapona? Na yeye huwa hivyo hivyo, je? Naweza mvutia mwanaume? hii huitwa pia ‘’Self-esteem’’. Wazazi wanapaswa kuwasaidia Watoto wao kwa kuwaongezea uwezo huu wa kujiamini. Mara zote huwa tunasema kuwa, saikolojia ni matokeo ya fiziolojia, kwa hivyo, kutopitia hatua hii yaweza kuwa ni matokeo ya matatizo yaliyo makubwa zaidi! Wazazi baadhi hushindana sana na Watoto wao wakiwaona kama vile wanataka kuwa wahuni, na wengine hata huwalinda kwa kuwafungia! lakini kumbe huwa tu ni vipofu wa sayansi hii ndogo. Mzazi anapaswa kuwa karibu na mtoto wake akimuongezea zaidi hisia za kujikubali na kujiamini, na anapaswa asimtengenezee mazingira ya kumbana. ila anapaswa kumtengenezea msingi wa kujitambua hatua anayopitia. lakini pia anapaswa kumuonesha madhara kama hatojua sababu ya msukumo wake. ambayo yanaweza kumpeleka katika tabia chafu za kuiga na uzinzi!

Safari Ya Mzunguko Wa Mawimbi Ya Estrogen Na Progesterone

Kwa mara ya kwanza tena tangia kile kipindi cha ‘’infantile puberty’’ ndipo Ubongo wa binti unaanza tena kupitia vipindi vya kuwa na uwingi mkubwa sana wa homoni ya estrogen, ambayo itakuwa ikifuatana na Progesterone. Homoni hizi huwa zikiwa katika mzunguko ambao unaongozwa na sehemu ya Ubongo ya Hypothalamus, ambayo huambatana na Tezi yake kubwa ya Pituiatary gland, hii huendelea mbele zaidi na kusisimua zaidi tezi ya uzazi ‘’ovaries’’. Kwa Pamoja hii chain huitwa ‘’Hypothalamo-pituitary-ovarian axis’’. Huwa ikipelekea mabadiliko ya homoni kati ya siku na siku na hata mwezi na mwezi.

Haya mabadiliko ya kihomoni huufanya ubongo wa mwanamke kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuhisi au ‘’more sensitive’’ kwa maswala ya kihisia ‘’emotional nuance’’ , kama vile kukubalika, kukataliwa, kupendwa au kuchukiwa. Siku zake zingine huwa na ujasiri mkubwa sana, lakini siku zingine ujasiri wake hupungua kidogo, alipokuwa mdogo alikuwa ana uwezo wa kuhisi hisia nyingi sana zaidi ya mtoto wa kiume, lakini sasa uwezo wake umekuwa mkubwa zaidi. Sasa hivi kuna siku utamuambia, nguo yako imekubana sana atakuelewa, lakini kuna siku ukimuambia hivyo, atatafsiri tofauti kabisa, atasikia umemwambia kuwa, yeye ni mnene au kibonge sana, na hapaswi kuvaa hiyo nguo!

Tafiti zinaonesha wazi kabisa kuwa sehemu za ubongo za Hippocampus, hypothalamus na amygdala zina athiriwa na homoni za estrogen na progesterone. Sehemu hizi Zimeonekana kuwa na receptors nyingi sana za hizi homoni, hivyo huwezi kupingana na huu ukweli kuwa, tofauti za homoni kwa vipindi mbalimbali, humpelekea mrembo huyu kuwa na matokeo mbalimbali ya tafsiri katika ubongo, zinazotegemeana na hivyo vipindi.

Hii picha nimenukuu toka jarida lililoandaliwa na ( Jordan Marrocco, PhD; Bruce S. McEwen, PhD) lililokuwa likielezea tofauti za kijinsia katika Ubongo, hapo anaonesha sehemu ya ubongo inayohusiana na kumbukumbu, namna inavyoathiriwa na homoni za estrogen kutokana na kuwa na receptors za estrogen, anaonesha kuwa, Estrogen hushiriki hata katika uundaji wa kumbukumbu au ‘’synapses’’, lengo kubwa ni kuonesha kuwa, mabadiliko ya homoni yana matokeo makubwa sana yanayofahamika sasa hivi katika sehemu mbalimbali za ubongo. na hivyo basi, tegemea kuwa, vipindi mbalimbali vya mzunguko havitakuwa na matokeo yaleyale katika namna binti atakuwa akiyachukulia mambo.

Kuhusu Stress!!

Watafiti toka chuo cha Pittsburg cha Saikolojia, waliwasoma Watoto tokea miaka saba mpaka miaka kumi na sita, waliwatazama katika kipindi chote, hata wanapoingia katika kupevuka au kuvunja ungo kwa wasichana, na kubalehe kwa wavulana. walikuwa wakiwaangalia namna ambavyo wanasisimuliwa na stress kutokana na uzalishwaji wa homoni ya cortisol. Waliona kuwa, wasichana wakionesha kuguswa sana na matokeo ya cortisol, ukilinganisha na wavulana. Kitu walichogundua ni kuwa, mapishano ya homoni za estrogen na progesterone huleta matokeo makubwa sana katika sehemu hiyo ya ubongo ya Hippocampus, na hiyo ndiyo huchochea zaidi stress. Wasichana hupata stress zaidi kwa vitu tofauti na vinavyowapa stress wavulana. Wasichana hupata stress sana kwa vitu vinavyohusiana na mahusiano yake na wanaomzunguka na mazingira, huku wavulana wakipata stress sana kuhusiana na changamoto za utawala au mifumo ya kuwaendesha. Mahusiano na Maisha ya kijamii humpa stress sana msichana, wakati, kuheshimiwa na kutawala huwa ajenda kubwa katika akili ya mvulana.

Umegundua filamu zake!!

Umri huu wasichana hupenda sana filamu za stori za mahusiano au tamthilia zenye visa vya kijamii na mapenzi na usaliti, huku wavulana wakipendelea sana mashindano ya mipira pamoja na filamu za ngumi na kivita!!

WIKI MBILI ZA KWANZA ZA MZUNGUKO!!

Estrogen huwa juu sana, na msichana huwa yuko vizuri sana, akionesha interest sana na jamii yake, huwa ame relax sana na wenzake.

WIKI MBILI ZA MWISHO WA MZUNGUKO!!

Progesterone huwa juu sana na estrogen huwa chini sana, huwa na uwezekano mkubwa sana wa kutokufurahishwa, au ku react kutokana na kuongezeka kwa hali ya kutotulia. na mara nyingi hutamani kuwa mwenyewe. Alipokuwa mdogo alikuwa na kiwango kisichobadilika badilika cha estrogen, ijapokuwa kilikuwa kidogo lakini alikuwa ametulia sana, lakini sasa kiwango cha estrogen na progesterone kimekuwa kikubwa sana, hali hii inamuongezea uwezo wake wa kuhisi au sensitivity kwa stress zinazotokana na homoni ya cortisol.

JE WAJUA UNAOUITA UMBEA!!

Wavulana wengi huwa hawaelewi kwanini wasichana wengi huwa wanapenda sana kukaa kirafiki wakifanya kila kitu Pamoja, hata Kwenda bafuni huongozana wakati mwingine, hupiga stori kila muda Pamoja, wakiwa wenyewe zaidi! Hii ni kwa kuwa wanawake kibiolojia huwa na amani zaidi wanapokuwa wao wenyewe zaidi, hii ni kwa kuwa wameendelea zaidi katika uwezo wa Lugha na kuelewa mazungumzo na maneno. Inafahamika kwa wastani, wanawake huongea zaidi na kusikiliza zaidi pia kwa Pamoja, na hata sehemu zinazohusiana na lugha zimeendelea zaidi kwa wanawake kama tulivyoona awali. Mtoto wa kike huwahi kuongea zaidi ya mtoto wa kiume kwa wastani, na mpaka muda wa miezi ishirini, mtoto wa kike huwa na misamiati mara mbili au mara tatu zaidi ya mtoto wa kiume. Watoto wakiume hufikia misamiati yao lakini hushindwa kuwafikia spidi yao, au uwezo wa kuzungumza. wasichana huzungumza fasta zaidi kwa wastani hasa wanapokuwa katika mazingira ya kijamii. Wasichana wanapokuwa Pamoja huambiana siri zao na kuzungumza mambo yao mengi sana. na hupenda sana kuzungumzia Maisha ya kijamii ya wengine, kitu ambacho wengine huita umbea, lakini lengo huwa ni kujifunza changamoto na madhara na stress za Maisha, kwa lengo la kujiepusha na madhara hayo na kwao wenyewe.

Kibiolojia pia inafahamika kuwa, wasichana wanapokuwa wakiambiana stori za visa vya Maisha yao ya kijamii, mahusiano ya kimapenzi ‘’romantic na sexual implications’’ huwafanya kujisikia raha sana. Huwa ni kutokana na kuzalishwa kwa homoni za ‘’Dopamine na Oxytocin’’, na homoni hizi huzalishwa zaidi kwa wasichana kipindi wanachopevuka au kuvunja ungo. Inatambulika kuwa, Estrogen inapoongezeka huambatana na kuzalishwa oxytocin nyingi zaidi, ambayo huchochea zaidi hisia za kuwa Pamoja.

KATI KATI YA MZUNGUKO WA MWEZI!!

Hapa huwa na kiwango kikubwa zaidi cha Estrogen, ubongo wa msichana husukumwa kuzalisha homoni ya Oxytocin nyingi zaidi, na kiwango cha Dopamine pia huwa ni kikubwa sana. Msichana huwa ni mwongeaji sana hapa. Hii ni kutokana na msisimko mkubwa sana wa mfumo mzima wa mawasiliano ‘’verbal circuit’’, lakini pia hisia yake ya kutamani ukaribu au ‘’Intimacy’’ huwa kubwa sana, hupenda kuwa Pamoja, kuwa karibu, kukumbatiwa n.k. haya yote ni matokeo ya kiwango kikubwa cha oxytocin. Homoni hizi za oxytocin na dopamine ambazo huwa kwa kiwango kikubwa zaidi baada ya kupevuka, huwa ni matokeo ya estrogen toka kwenye ovaries. Na hizi zina maana kubwa sana ambayo wengi hawaijui, Oxytocin huzalishwa zaidi kutokana na ukaribu, na hata yenyewe huongeza hisia za ukaribu. Hivyo ndivyo pia wasichana hupenda zaidi, na huridhika zaidi pia. Utakuta wasichana wakipenda kuchezeana nywele, kukumbatiana, kushikana wakienda kununua vitu na hata kupiga stori za umbea Pamoja.

UMESHAJUA KWANINI HUSHINDA NA SIMU!!

Hushinda na simu kutwa nzima akipiga stori na wenzake kwasababu, ukaribu na stori kwake huambatana na uzalishwaji wa kiwango kikubwa cha homoni ya dopamine na oxytocin, ambayo hupunguzia kabisa mgandamizo wa stress. Huwa ni shughuli sana kumtenganisha binti na simu yake, kwake mawasiliano katika hatua hii, huwa na nguvu kama Heroin kwa mwathirika wa madawa ya kulevya, kwa kuwa zote huambatana na uzalishwaji wa homoni za dopamine.

WASICHANA WANAPOFELI KWA WAVULANA!!

Kwa namna ambavyo huwa akichat muda mrefu sana na rafiki zake, wakiambiana kila Habari, wakizungumza umbea kutwa nzima, huisi sasa anaweza fanya hivyo na kwa rafiki yake mpya wa kiume! Mambo huwa kinyume kabisa. Hupatwa na  ajabu au ‘’surprise’’ kubwa sana kwa kuwa, kwa muda wote ambao atakuwa akiongea na rafiki yake mpya ‘’Greyson’’, kumbe Greyson alikuwa anaboreka tu na stori zake!! Kwake Greyson  kuwa ‘’social’’ au mtu wa stori stori za kijamii sio kipaumbele kabisa, na hili sio kosa lake, tangia akiwa mdogo, kiwango kikubwa cha homoni za Testosterone kilimfanya akate channel nyingi sana ambazo zimemfanya asiwe mtu wa kupendelea mahusiano sana ya kijamii. Na hii shida huendelea mpaka kipindi cha familia, wanaume huwa sio wapenzi wa stori ambazo wanawake mara nyingi sana huwa wakizipendelea, wanaume huwa hawazielewi kwa kweli! na hata wale ambao huwa na uwezo mzuri wa kuzungumza sana, huwapata wasichana wengi sana kiurafiki kwa sababu hii.

SIRI ILIYOFICHIKA ENZI HIZI KWA WAVULANA!!

Ijapokuwa tutawangalia baadae, lakini kwa ufupi katika zama hizi wavulana huwa wamejawa na mawazo ya Ngono  mpaka mwisho. Wavulana Mawazo ya kufanya mapenzi huwa yakizunguka vichwani mwao kwa muda wote. Hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha testosterone ambacho huwasukuma zaidi kutaka kufanya ngono, na hata kiwango cha misisimko ya uume, huwa ni mingi sana kwa siku. Huwa wakitengeneza taswira za maumbile ya utupu ya mabinti na kutamani sana nafasi ya kuwakaribia. Hapa vijana huwa hawapendi kabisa kuzungumza hasa na watu wazima, kwa kuhisi wanaweza somwa akili zao, na kuonekana namna ambavyo wametekwa na Mawazo hayo. Mara nyingi huwa tu wametulia kwa upweke wanapokuwa na watu wazima mpaka watakapo kutana na wenzao wa rika lao, ambao hutaniana kuhusu, mara nyingi kauli zenye maneno ya utupu, na hapo hufurahi sana kwa kuwa hujiona kuwa wapo Pamoja kisaikolojia. Kwa kipindi chote cha upevukaji, mitazamo na hisia za wasichana na wavulana hutofautiana kabisa.

Mahusiano Yanapovunjika!!

Mara nyingi wasichana huwa hawapendi kuvunja ukaribu, hii ni kutokana na kupotea kwa kiwango kikubwa cha homoni za serotonin, dopamine na oxytocin, ambacho huwapelekea kuwa wahanga wa kiwango kikubwa cha homoni za stress au cortisol. Hivyo wasichana mara nyingi wanapoona dalili za awali kabisa za kuvunjika kwa mahusiano yao na wale wanaowapenda, hujaribu kukwepa ukilinganisha na wavulana, ambao wao kwao, migogoro ni jambo la kawaida. Msichana aliyeathiriwa na kiwango cha stress kutokana na kuvunjika kwa uhusiano, anapoelekea kupona, huusiana na uzalishwaji wa homoni ya oxytocin ambayo huchochea tena uhitaji wa ukaribu na kuwa Pamoja, hiyo tayari ina maanisha kuwa, kama msemo mmoja uliotolewa na chuo cha Robert Joseph kilichopo Texas unavyosema, ‘’Uthabiti na hisia za Kujiamini kiume, hutokana na uwezo wakujitegemea na kuishi mwenyewe, walakini, uthabiti na hisia za kujiamini kwa wanawake, hutokana na uwezo wake wa kuendeleza mahusiano mazuri na wengine’’. Huonesha hata ule msemo unaosema kuwa, linapotokea changamoto, mwili husisimka kwa ajili ya kupambana au kukimbia ‘’Fight or flight’’, msemo huu huonekana kuwa umeegemea zaidi kwa wanaume! Wanawake mara chache sana husisimka kwa namna hizo, wanawake huwa wakiangalia zaidi namna ya kutatua changamoto kwa Pamoja bila kukimbia au kupambana, kwa kuwa, kukimbia kwao ni kuwaacha wanaowapenda. Mfano, Watoto wao. lakini pia, kupambana kunaweza hatarisha zaidi kama watakuwa wajawazito au wana Watoto. Tafiti kadhaa kwa Wanyama ikiwemo  nyani huonesha, wanawake linapotokea tatizo huungana kwa Pamoja, na kushirikiana kulitatua kwa Pamoja. bila kujihatarisha au kuhatarisha! Hii ni kujenga tu msingi wa kuwa, wanawake hukua na tabia ya kujitenga na changamoto za migogoro tokea awali kabisa katika ukuaji. Baadhi ya watafiti wa sayansi za watu ‘’anthropologist’’, bwana Joan Silk aligundua kuwa, kwa nyani, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uwezo wa kuchangamana vema na jamii yake, na kuwa na mafanikio mazuri katika kulea vizuri Watoto wake.

ANALALA SANA HATA MPAKA SAA SITA!!

Wazazi huangaika sana kwa tabia hizi ambazo hutokeza kwa Watoto katika umri huu. Mtoto huweza kulala usipomuamsha mpaka Katikati ya siku, huwa mvivu na kuonekana amechoka sana. Lakini sababu ni ndogo sana, kiwango kikubwa cha homoni za Estrogen hu reset seli za kwenye mtambo unaotawala mzunguko wa kulala na kuamka katika ubongo ‘’Suprachiasmatic nucleus’’. Homoni hizi haziishii hapo tu huenda kuathiri hata na uzalishaji wa homoni zake za ukuaji,  na seli zinazotawala uhemaji. Kumbuka hapo awali mzunguko wa kulala na kuamka kwa msichana na mvulana ulikuwa sawa, lakini mwaka mmoja kabla ya mwanaume hajaanza kupitia mabadiliko haya, tayari msichana huanza. na mvulana naye anapokuja kuanza kupitia vipindi vilevile vya kuchelewa kulala na kuchelewa kuamka, na kwa ujumla hulala muda refu sana. Mpaka kwa wastani wa miaka ya kumi na kadhaa, ubongo wa msichana huwa umesogea katika mzunguko wa ulalaji kwa asilimia 37% hivi zaidi ya wavulana, hii humaanisha kuwa, ubongo wa wasichana huanza kukomaa kabla ya ubongo wa wavulana. Mabadiliko haya huishia kwa kumfanya mwanamke kuwa na uwezo wa kuamka Mapema kuliko mwanaume kwa kitambo kidogo kwa milele yote, na huku ukimfanya mwanaume kuwa na uwezo wa kuchelewa kulala usiku kidogo zaidi ya mwanamke milele yote. Inashangaza sana kwa namna ambavyo pia Biblia inaandika kuwa sifa ya mwanamke bora, ni kuwahi kuamka na kuandaa familia yake, kumbe Biblia ilishajua misingi hii ya homoni katika Ubongo ‘’neuroendocrinoilogy’’ miaka mingi hata kabla ya neno sayansi halijasimikwa.

NI MKOROFI SANA!!

Wazazi wengi hulitambua hili, kuna wakati Binti anaweza mjibu mama yake hata jamii ikashangaa kama ni kweli anayezungumza ni mtu na mama yake! Inatambulika kuwa, katika wiki mbili za kwanza za Mzunguko, Ubongo wa binti huwa unakuwa vizuri sana, na hata huonekana kuwa kuna asilimia 25% zaidi ya uundwaji wa kumbukumbu katika sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’hippocampus’’ kutokana na kiwango kikubwa cha homoni za Estrogen, hii yote ni kusema  kuwa ‘’Hana shida!!’’

Tarehe za Shida!!

Stori huanzia hapa, Siku ya 14 ambapo huwa katika mzunguko wake Ovaries huliachia yai ‘’Ovulation’’, kiwango cha Progesterone huanza kujaa kikigeuza au shusha viwango vya Estrogen ambavyo vilikwisha kuwepo juu. Progesterone huwa na matokeo tofauti kabisa katika Hippocampus ikiwemo na kulewesha kabisa seli za Hippocampus. Hii huufanya ubongo kuwa na msisimko hafifu, huwa kama umelevywa na pia husisimka zaidi ‘’more irritable’’. Zile kumbukumbu au taarifa au ‘’connections’’ nyingi ambazo zilikuwa zimeundwa katika wiki mbili za kwanza pale ambapo kulikuwa na kiwango kikubwa cha Estrogen, huanza kushushwa nazo kutokana na Progesterone. Sasa basi, siku chache mwishoni mwa mzunguko huu wa hedhi, Kiwango cha progesterone nacho hushuka ghafla! hii progesterone ilikuwa ni kama Gundi, kitendo chake cha kuondoka kwa ghafla hupelekea kuondoka kwa ile hali ya kutulizwa kama gundi inavyozuia kidonda kisifumuke. Na hivyo hupelekea ubongo sasa katika hizi siku za mwisho wa mzunguko kuwa na kiwango kikubwa sana cha Stress, kuwa na hamaki, na pia kutotulia na kusisimka. Na hii ndiyo sababu utakuta Watoto wanashindana kabisa na wazazi wao kwa ukali! Na mara nyingi huja kutulia baadaye wanapokuwa wamekaa sawa, hivyo ni muhimu wazazi kutumia elimu hii kuwajua na kuwasaidia Watoto wao.

Je ni Kweli Ule Msemo wa ‘’Wanawake Wenye Miili Mikubwa Hawana Shida?

Taasisi ya Afya ya akili ya Bethsesda walirejea gunduzi ya kuwa, ‘’mipishano ya homoni za mzunguko wa hedhi huusiana na hisia za misisimko mbalimbali kwenye Ubongo. na hii hutoa Ushahidi wa kushuka kwa homoni pale mzunguko unapoishia, na hisia za kutotulia kwa baadhi ya wanawake. Kumbuka Asilimia 80% huathiriwa kidogo tu na10% huathiriwa sana. Hawa waligundua kuwa, Wanawake wenye Estrogen na Progesterone nyingi sana huwa hawaathiriwi kabisa na Stress hizi, kwa kuwa, wao huwa na kiwango kikubwa cha seli za homoni za Serotonin. ambazo huwatuliza kabisa, na hapa mara nyingi huwa ni wanawake wanene au wenye maumbile makubwa (na wengine pia, unene sio kigezo pekee). kwa wanawake wengi  hawa serotonins huenda kwenye sehemu za mbele za ubongo ‘’PFC’’  na huko Hushusha hisia ambazo zingesababishwa na shida ya kushuka kwa homoni mwishoni mwa mzunguko. Na hivyo kuwafanya wawe vizuri kabisa. Kumbuka hisia hizi kwa wenye estrogen chache sana hupelekea hata Mawazo ya kupaniki, ukali, msongo wa Mawazo, hofu na ikizidi hata kujinyonga. Ni muhimu kuwa mwangalifu kwa Wasichana wanaoweza onesha hisia hizi, kwa kuwa, wanaweza kuwa wahitaji wa msaada mkubwa zaidi wa kitabibu, unaweza onana na ofisi ya mtaalamu wa shida za fahamu ‘’psychiatrist’’.

 Je wajua!!

Sehemu ile ya Hippocampus ambayo inahusiana na kuunda kumbukumbu, huwa inasisimuliwa sana na homoni za estrogen! Na kwa mantiki hiyo, katika wiki ya kwanza na ya pili, wasichana au wanawake kwa ujumla huwa wana uwezekano wa kufanya vizuri kwenye mitihani ambayo itawataka kuwa na kumbukumbu.

TATIZO KUBWA LA KUWARUHUSU KUFANYA NGONO!!

Jamii nyingi hujikuta wakiwaachia mazingira ya uhuru mabinti hawa, ambao huwapelekea kuingia katika uzinzi au ngono. Hili ni kosa kubwa sana. Na mara nyingi mabinti hawa huwa katika kipindi cha kuanzia Kidato cha kwanza mpaka mwaka wa kwanza wa chuo kwa waliopitia kidato cha tano na cha sita, lakini mpaka wale wa mwaka wa mwisho kwa vyuo vya kati ambao hawa ni wale waliounganisha vyuo, hawa wote huwa wana wastani wa miaka 18-19 mpaka wanapomaliza hizi hatua, lakini utakuta wanapoanza tu kufikia hatua za kati, huonekana kama vile wamekwisha komaa vya kutosha na huachiwa uhuru wa kuingia katika ngono!

Kitaalamu hawa mabinti  sehemu zao za hisia zina mhemko mkubwa sana wa kufanya mapenzi tangia tu wapevuke, lakini sehemu zao na mifumo yao ya ubongo ya kutawala hisia, sehemu ya ubongo wa mbele ‘’prefrontal cortex’’, huwa tu sehemu hizi zimeotesha seli nyingi sana ila bado hazijakomaa!!  Na hasa kinachokuwa kinatokea hapa huwa ni hiki, kuna sehemu inayohusiana na uchakataji wa hisia, inayoitwa ‘’amygdala’’, sehemu hii huwa na connections nyingi sana na ile sehemu ya mbele ya ubongo ‘’prefrontal cortex’’, sehemu hizi kipindi cha kupevuka huwa zinatengeneza seli za fahamu au ‘’neurons’’ ambazo huwa zinaunganisha hizi sehemu mbili, kwa lengo ambalo ni kuwa, Ubongo wa mbele uje kuwa na uwezo wa kutawala hisia. Sasa basi, kipindi cha kupevuka, hizi seli huwa bado hazijakomaa kwa kuwa ili zikomae, huwa zinahitaji tabaka moja ambalo huwa ni kama koti ambalo huzizunguka hizi seli, huwa linaitwa ‘’myelin’’. Kitendo cha kukomaa kwa ubongo humaanisha kuwa, seli za ubongo sasa zimeshafunikwa na hizi myelin, na hiko kitendo hukamilika binti anapovuka miaka 19. Na kumbe basi, anapofanya ngono au mapenzi kabla ya miaka 19, ubongo wake sehemu ya Amygdala huwa inasisimka sana kwa hisia. na yeye mwenyewe, uwezo huo wa kuzi control hana, na hiyo humharibia kabisa ubongo wake. tena anapoendelea, huua uwezo wake wote wa kuweza kutawala hisia zake hata atakapokuwa mtu mzima. Huathiri mamia ya connectons za ubongo zinazounda sifa za utulivu za kike, ambazo zote huegemea katika networks za ‘’PFC-amygdala connectivity’’. Na hata hisia za ngono zenyewe huwa hazipati kwa kiwango alichopaswa, kwa kuwa ubongo wake huwa ukishuhudia mivurugano zaidi ya msisimko!!

MABINTI WENYE SIFA ZA KIPEKEE!!

Inafahamika pia kuwa, mabinti wenye kiwango kikubwa cha homoni za kiume androgens, ambazo kwa wanawake huwa ni testosterone, androstenedione na DHEA. huwa na dalili za kuwa wamewahi mapema sana kuanza kufanya mapenzi. Na huu utafiti ulifanywa na Chuo kikuu cha Utah. Na katika tafiti yao walichokiona ni kuwa, kadri sura ya binti inavyoonekana zaidi kuwa ya ghadhabu au ‘’aggressive’’, ndivyo pia kiwango cha homoni ya androstenedione inavyokuwa ipo kwa wingi zaidi. Chunusi ni dalili kubwa zaidi kuwa kiwango cha androgens kipo juu. (kumbuka sio lazima chunusi iwe inasababishwa na androgens na kuashiria kufanya mapenzi mapema!! Sayansi haina uelekeo mmoja, chunusi zina uwingi wa sababu)  chuo hiki waligundua kuwahi kufanya mapenzi mapema huusiana na sifa za kuongezeka kwa androgens. ikiwemo zote nilizoziorodhesha juu. Pia ni muhimu kutambua kuwa, kiwango cha testosterone huwepo kwa kila mwanamke, maana ndicho humsababisha kuwa na hamu ya kufanya mapenzi. Lakini tafiti huonesha kuwa, kiwango cha hasira kwa wasichana kiliambatana na kiwango kikubwa cha androgens, na hamu kubwa ya kufanya mapenzi, Pamoja na chunusi!!

Katika tafiti hii hii katika chuo cha Utah, waligundua pia kuwa, hata kiwango kikubwa sana cha Estrogens, testosterone na androstenedione, kiliambatana na hisia za wasichana kujiona wao ni wa pekee sana, au wa viwango vya juu zaidi ya wenzao!! Wasichana hawa walionekana wakijiweka katika viwango vya juu zaidi ya jamii ilivyo wachukulia na wengi wao hawakupendwa sana na wenzao.

Kumbuka kuwa, Tabia ni matokeo ya mambo mengi sana lakini homoni hujenga msingi wa kuzisoma tabia. Homoni katika ubongo huwa mara chache sana zinaweza kukupa makisio hasi juu ya tabia, inafahamika kuwa, maamuzi kuhusu tabia huongozwa zaidi na sehemu kuu kadhaa katika ubongo ambazo ni Anterior cingulate cortex, Prefrontal cortex,  Rostral cingulate cortex na Temporal parietal junction. Lakini hata hivyo huwezi pingana na nguvu ya homoni. ambayo huwa ni mithili ya mziki unaopiga nyuma ya kila tukio, na muda mwingine ukibakia wenyewe tu ukipiga.

UBONGO WA BINTI MZURI RACHEL ‘’MIAKA 20+’’

Maisha na Kazi

Maisha ya Dada Rachel, binti wa miaka 24, baada ya kazi nzito inayotokana na ratiba ngumu ya kazini kwake tokea asubuhi, anahitaji muda wa kutulia ili atulize akili yake. Muda wa kutoka unapotimia wa kufunga kazi za siku, haitaji hata kuagana na rafiki zake kutokana na uchovu. Anapanda daladala kuelekea nyumbani kwake anakoishi kwa dada yake ambaye naye anafanya kazi. Anapofika nyumbani anakuta kwa bahati nzuri sana dada yake akiwa alishapika chakula lakini ametoka kidogo. Anaamua Kwenda kuoga kwanza na kisha anakaa mezani na kula chakula chake. Anapomaliza kama ilivyo kawaida ya vijana wa kisasa, anakaa kwenye sofa akijiachia na simu yake mtandaoni kuangalia kama kuna lolote la kumsisimua kwa wakati huo. Baada tu ya kama dakika kumi, anaingia Dada yake Anna akiwa na rafiki zake wanne ambao nae anafanya nao kazi, wawili wakiwa ni wakiume na wawili wa kike.

UMEME WA HISIA!!

Ndani ya sekunde kadhaa tu baada ya Gilbert kuingia ndani ambaye ni miongoni mwa marafiki wawili wa wakiume wa Anna, ndipo Rachel alipogundua kuwa kichwa chake ni kama kimepigwa mithili ya shoti ya umeme!! Gilbert alikuwa ni mrefu, kijana mzuri wa kuvutia ‘’handsome’’, alikuwa na rangi ya maji ya kunde, sura yake ilikuwa ni ndefu iliyochongoka, alikuwa na nywele nyingi na nyeusi, macho yake yalikuwa ni meupe. Rachel alijikuta akisalimiana na rafiki wote wa dada yake, lakini akili yake yote ikiwa imeshachanganywa na mwonekano wa Gilbert na hasa tabasamu lake jepesi alipokuwa akimsalimia.

Akili ya Rachel ghafla ilihama na kuanza kuwatazama kwa umakini rafiki za dada ake huku akili yake ikilenga kuwachunguza kama yupo mmoja ambae anaweza kuwa na ukaribu na Gilbert!! Mapigo yake ya moyo yalikuwa yako juu, na akiwa hajahisi ukaribu wowote wa Gilbert na rafiki wa dada yake, ambapo wawili wao tayari walikuwa wapenzi waliojionesha kupitia stori zao, Rachel akaanza kuangalia Viatu vya Leather vya Gilbert kwa siri, mkanda wake mzuri, akawa akiangalia vidole vyake kama ana pete!  Na akiwa Katikati ya Mawazo ambayo alikuwa akiyafanya kwa siri sana, dada yake alishagundua kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma hisia za mdogo wake. Ghafla!! Gilbert kama mithili ya mtu ambaye naye alikuwa kichwani mwa Rachel, akawa akitafuta namna ya kumhusisha Rachel katika stori zao ili apate nafasi ya kupata nafasi ya kumjua Rachel, ambaye naye alikwisha mvutia Gilbert, kwa kipindi kifupi aliochokuwa amekaa ndani.

Gilbert  ‘’Anna, una mdogo mzuri hivi!! Au ndiyo maana huwa hupendi kutukaribisha!!, kauli hii ni kama ilimfungulia njia Anna kumfungulia geti dada yake mdogo!! 

HOJA YA KIBIOLOJIA

Miaka hii katika kila kichwa cha Binti kwa wastani, huwa ni kupata mwenzi, atakae weza kumpenda, na kumjali yeye na watoto wake, atakaojaliwa kuwapata. Vigezo vya kupenda ni vilevile kwa kila stori ya mapenzi inapoanzia. Watu wengi hawajui kuwa unaweza wadanganya wanasheria, ila huwezi wadanganya wataalamu wa ubongo, kama wakiamua kufatilia misingi ya utendaji wa kibiolojia, ambayo imeshatengenezwa miaka na miaka, na sote huifuata tu. Mungu alipotoa amri zake mlima sinai miaka karibia elfu nne iliyopita tayari alishajua kuwa, msingi wa utendaji hautakaa ubadilike kamwe. Wanawake wote kwa miaka yote hufuata misingi ile ile ya kuvutiwa kimapenzi. hisia za mapenzi  ni matokeo ya mifumo ya ubongo. ambayo, haionekani! lakini nayo ni kama mikono, yaani kila aliyenayo huitumia kwa kazi zilezile, na namna watu huvutiwa kimapenzi huwa ni ileile. Unaposikia Yusufu alikuwa mzuri wa kumsisimua mke wa Potifa katika Biblia, ndivyo ilivyokuwa pia kwa Rachel baada ya kukutana na Gilbert!!  Kama Ilivyokuwa kwa mfalme Daudi alipovutiwa na mke wa uria mhiti, ndipo ilivyokuwa kwa Gilbert alipovutiwa na Rachel.

Sababu Za Mwanaume Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa Binti!!

Sababu za kuvutiwa kimapenzi. kwanza, huanza na sababu za mivuto ya mwonekano. Mionekano ya muundo wa Gilbert yote huwa na misingi mikubwa miwili ya kumvutia mwanamke. Mwanaume ambaye anasifa bora kabisa za uzazi ‘’fertility signs’’, mwenye atawezesha kuzaliwa kwa Watoto imara kabisa kimwili na kiakili. Na pili, ni mwanaume mwenye uwezo wa kujali na kulinda familia yake. Hii huwa ni kupitia uwezo mkubwa wa kiuchumi utakaowezesha kupata mahitaji yote ya msingi, lakini pia uwezo wa nguvu za kimwili, ambao utampatia mwanamke hisia za usalama kwa kuwa na mwanaume mwenye uwezo wa kupambana na maadui.

Kama nilivyoeleza awali na hata katika kitabu cha injili ya sayansi sehemu ya nne, katika msingi wa fiziolojia ya kufeki mionekano. Ili mtu aonekane mzuri anapaswa kuwa na mfanano wa pande zake mbili ‘’Symmetry’’.  anapaswa kuwa na mwonekano ulionyororo au ‘’smooth’’, anapaswa kuwa na macho makubwa na tabasamu pana. Sifa hizi kibiolojia zina maana kubwa sana, zinamaanisha kuwa jenetikia ya huyo mtu, iko imara kwa kutofanya makosa katika uumbaji wake, uimara wa mfumo wa jenetikia huambatana na uimara wa mifumo yote ikiwemo mfumo wa kinga na hata biolojia nzima ya mwili. Tabasama zuri humaanisha amani. Ubongo hupenda amani kama ilivyosababu ya namna watu wengi hupenda Watoto, kwa jinsi wasivyohatari. Kwa mwanamke, mwanaume kuwa na macho makubwa huwa ni sababu ya kumvutia sana kutokana na namna huwa rahisi zaidi kwake kuungana nae kihisia, pale anapokuwa akimtazama na kuungana nae kihisia kwa uwezo wake mkubwa wa ‘’mirror neuron system’’ au MNS.

Mwanaume mwenye ndevu na nywele nyingi kwa wastani katika mwili wake, huwa na mvuto mwingi kwa wasichana kutokana na namna ambayo nywele zake hutengeneza msingi wa ukakamavu wa kiume, ndevu kwa mwanaume huaminika kumpunguzia eneo lake la uso ambalo lingeweza kusomwa ‘’wanaume huwa hawapendi kusomwa sura zao, huwa hawapendi kuonesha udhaifu, pia huitwa sura ya kiume’’, ni kama nywele ndefu zaidi kwa simba au manyoya marefu zaidi kwa jogoo!! Ndevu huongeza mwonekano wa kiume ambao humwongezea mvuto kwa wanawake, Ngozi ya wanawake yenye uwezo mkubwa wa kuhisi ‘’more sensitive’’ kutokana na matokeo ya estrogen nyingi husisimuliwa zaidi inapogusana na nywele nywele za kiume.

Sauti nzito huwavutia sana mabinti lakini sababu kubwa ni kuwa, sauti kubwa kwa mwanaume humfanya awe ni tishio zaidi dhidi ya wanaume wenzake, simba anapounguruma hufanya wadhaifu wote kutulia au kukimbia, na hilo humfanya jike wake kujihisi salama zaidi, na ndivyo ilivyo kwa wanaume pia, hata mwili mkubwa huwa na mvuto sana kutokana na namna huashiria nguvu nyingi na hata kiwango kikubwa cha jasho ambalo huzalisha ‘’androstadinone’’ ya kumsisimua zaidi mwanamke.

Kuangalia Viatu, mavazi na hata baadae kuulizia kazi ya Gilbert, vyote hulenga kuangalia uwezo wake wa kiuchumi, hasa ni kwa namna gani ataweza kummudu yeye Pamoja na Watoto wake. Rachel pia aliangalia pete katika kidole cha Gilbert kwa lengo la kujilinda, ubongo wa mabinti bado huwa na uwezo mkubwa wa kufanya mahesabu mapana, huamini kuwa mwanaume mzuri hutazamwa na wengi. na hivyo, kuweza kukaa akiwa mwenyewe, kunaweza kumaanisha huyo mwanaume hajatulia! Uwezo wake mzuri wa Prefrontal cortex humsaidia kutosisimuliwa moja kwa moja na sehemu za hisia, hata akapuuzia hatari zinazoweza kutokea mbeleni.

Kumbuka, takwimu zilizokwisha fanyika na mwanasaikolojia David Buss kwa miaka mitano, zinaonesha kuwa, asilimia kubwa zaidi katika makabila ya jamii 37. Zinaonesha wanawake wengi zaidi huvutiwa zaidi na wanaume wenye nguvu za kiuchumi, kuliko mionekano ya nje. na pia, wanaume wenye mionekano mizuri huonekana kuwa na urahisi zaidi wa kuwapata wanawake!!

Sababu Za Binti Mwenye Mvuto Wa Kimapenzi Kwa Mwanaume!!

Sayansi za asili zote hukubaliana kuwa sababu ya kwanza huwa ni sifa za uzazi ‘’fertility signs’’. Ijapokuwa wengi wasiojua biolojia hii, huisi ni mapenzi tu yanayotokana na maamuzi ya mwanaume. lakini biolojia hii inasaidia kujua kwanini kuelekea karibu na vijana wote wakiume, huvutiwa zaidi na aina za sifa zinazofanana! Takwimu huonesha wanaume huvutiwa zaidi na wasichana walio wadogo kwao kwa umri wa makadirio ya miaka miwili na nusu na  kushuka chini. Hupendelea wanawake wenye macho yenye mng’ao ‘’bright eyes’’, nywele laini na zinazoonekana vizuri ‘’shiny’’, midomo laini ‘’full lips’’ na mwili uliojitenganisha kimaumbule ‘’hourglass figures’’. Sifa hizi zote ukiziangalia zina msingi uleule wa awali, Umri mdogo humaanisha mwanamke ambaye bado hajachoka, na hivyo kuashiria kuwa atakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukuzalia (hii ni kama tu ambavyo  timu za mipira huwa zinapenda kusajili zaidi wachezaji wadogo, kwa lengo hilohilo),ukija pia kwa maumbille, wanaume wengi hupenda mabinti wenye shepu ambazo msingi wake huwa ni uzalishwaji wa homoni za Estrogen, katika kipindi baada ya kupevuka, misuli na mifupa ya wasichana husisimuliwa zaidi na hizi homoni na kufanya Nyonga zao kuwa ni ndogo, au nyembamba ukilinganisha na Hips kwa wastani wa 1/3 ukilinganisha na kabla ya kupevuka! Wanaume huvutiwa zaidi na mionekano hii kama ishara ya binti ambaye bado Hajapata ujauzito kwa namna tumbo lake ni dogo, katika kitabu chake Louann Brizendine ukurasa wa 64, anaeleza kuwa, msukumo wa homoni za uzazi kwa wanawake wenye afya huwafanya kuunda maumbile yenye wastani wa 1/3 kati ya nyonga na hips, na hiyo huwa ni ishara ya kiwango kikubwa zaidi cha estrogen. na pia huashiria urahisi zaidi wa kupata Mimba hata katika umri wao mdogo, na hii husapotiwa na sayansi za maumbile ‘’anatomy’’ ambazo huonesha maumbile haya huwa na urahisi mkubwa kwa kuzaa Watoto bila changamoto! sababu zingine za unyororo wa Ngozi, lips n.k. hurejea katika machaguo ya mwanaume kwa mwanamke mwenye afya na kiwango kikubwa zaidi cha homoni za uzazi, lakini pia mfanano wa mwonekano au ‘’symmetry’’ huwa na sababu za ubora wa mifumo ya kijenetikia kama tulivyoona awali, kwa mwanamke pia uwingi wa nywele huambatana na kiwango kidogo cha homoni za androgens na hivyo utulivu mkubwa.

Wanaume huwa na kigezo cha tabia kwa kiwango kikubwa sana kwa mabinti kuliko wengi wa mabinti wanavyofikiria!! Wanaume hupendelea mabinti wenye uwezo wa kuja kutunza familia zao, na wakawa sio changamoto kwao kwa kuwa na tabia za kutoka nje ya ndoa zao! Ndani ya sekunde chache sana mwanaume anapogundua mwanamke anayemfuatilia anaweza kuwa ni mhuni wa kuwa na wanaume wengi, sehemu yake ya TPJ husisimka na kuanza kutafuta namna ya kukaa nae mbali, na uwezo wao mkubwa wa kustahimili stress, huwapa wepesi wa kuachana na uhusiano au  ‘’social bond’’ yoyote ile wanayokuwa wameianzisha, bila hata kujali kiasi gani cha nguvu walishaitumia.

Muhimu Sana Kujua Kuhusu Mivuto Ya Kimapenzi!!

Biolojia hukusanya sababu zote za mivuto lakini hakuna binadamu mwenye sifa zote za mivuto hii!! Ni muhimu kutambua hili, wala hakuna binadamu aliye mzuri kamilifu wa chochote kile ‘’perfect symmetry’’, mara nyingi Ubongo unapovutiwa na mtu hupuuzia sehemu zote ambazo zingekuwa hazina dalilii ya uzuri, kwa huyo ambae tayari umeamua kumuona mzuri! Hili ni la msingi sana ili mtu aweze kujua kuwa, kigezo cha tabia tu kinaweza mfanya mtu mmoja akavutiwa na binti, na Ubongo wake ukapuuzia kila taarifa kuhusu mwonekano wake, na vivyo hivyo kigezo cha mwonekano kinaweza pia kumfanya mtu apuuzie kigezo cha tabia. Kitu kitakachowafanya watu wakae Pamoja ni kigezo cha kwanza ambacho kimekuwa na nguvu zaidi ya kuwa na msisimko wa kihisia.

UBONGO WA BINTI ‘’RACHEL’’ KWENYE MAPENZI MAPYA

Rachel sasa na Gilbert huchati kila wakati wanapopata free baada ya kazi, huutumia zaidi usiku kwa mawasiliano. Hupanga na kutumia siku za weekend kuzunguka Pamoja, Rachel hutamani kujua zaidi kuhusu Gilbert, familia yake, mipango yake ya kazi, uwekezaji wake n.k. Gilbert humsindikiza Rachel baada ya mizunguko yao mpaka kwao, na mara nyingi huwa akimpitia anapotoka tu kazini kila anapopata wakati. Kadri siku zinavyozidi Kwenda ndipo hisia za kuwa karibu zaidi zinapoongezeka! Kwake Gilbert alishamhakikishia Rachel kuwa yuko tayari kumuoa na anamsisitiza Rachel akubali ili aweze kuanzisha harakati za kufunga nae ndoa, maana kila anapokuwa nae huwa anaona anazidi kupata msukumo mkubwa zaidi wa kuzini nae jambo ambalo linapingana kabisa na misingi yake ya imani. Kuna siku Rachel alimtembelea Gilbert, ilikuwa ni siku ya Birthday ya moja ya marafiki wa Gilbert aliyeitwa Magessa, na Rachel alikubali Kwenda Pamoja na Gilbert, sherehe ilichelewa kuisha kwa kina magessa, na mpaka ilipohitimu saa nne na nusu hivi za usiku, ndipo Anna alipomshtua Gilbert ‘’Wee!! Inakuaje na mdogo angu mpaka saa hizi? Gilbert kwa shaka kidogo ‘’ow, am sorry, soon nipo hapo, give me few minutes!!’’ ilibidi Gilbert amuage rafiki yake magessa na kuondoka na Rachel, kipindi wanaondoka kutoka kwenye party fupi, na kupita katika njia yenye upenyo kabla ya kutokea kwenye main road ambapo wanaweza kupanda bajaji, Rachel alidondosha chini simu yake kwa bahati mbaya, akiwa anataka kuiokota, Gilbert aliiwahi na kumuokotea, alipokuwa akiinuka baada ya kuchukua simu huku kichwa chake kikiwa katika usawa wa miguu ya Rachel, akadakwa na hamaki baada ya kuuona vizuri mguu wa Rachel! ambao ulikuwa wazi kutokana na nguo  aliyoivaa kuwa ni fupi. kama ilivyokawaida ya mitindo ya kisasa, akajikuta akiusindikiza mpaka kwenye paja, mpaka kiunoni na kisha kifuani, kipindi Rachel naye akijua kinachoendelea, ndipo Gilbert akajikuta baada tu ya kumpatia simu akimvuta na kumkumbatia, wakajikuta wakiaangaliana machoni kwa kipindi kama cha sekunde kumi na kitu, mapigo ya moyo yakaanza kuambatana ‘’synchronize’’, akili ikawa kama imelevywa, kwa mara ya kwanza wote wakajikuta wakishindwa kujizuia, wakaanza kupigana kiss huku kila mtu ubongo wake ukiwa kama umepigwa ‘’narcotics’’, wazo likamjia Gilbert akiwa amemshika Rachel kiunoni, je tunaweza Kwenda kwangu leo!! Rachel akiwa kihisia amekubali kabisa, lakini alijipa ujasiri na kusema, Hapana! Tupange siku nyingine si leo, ngoja niwahi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani, Rachel akiwa ni kama mtu aliyetoka katika kifungo Kizito na mwenye Mawazo mengi, na kusisimka! alijikuta hawezi tena jizuia na kumsimulia dada yake, ambaye tayari alikuwa anajua kila kitu, akamjibu ‘’Hopefully, you did nothing yet?’’ Rachel, akamjibu ‘’yes, sis..’’ Anna alikuwa ni binti wa dini sana na alitambua hatari kubwa sana ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa, maana huo ni msingi ambao umemfanya hata yeye na mumewe waweze kuwa na ndoa yenye mafanikio makubwa sana ya uaminifu, mme wake Anna ni dereva wa magari makubwa, huwa ana muda mchache sana wa kukaa nyumbani, lakini familia yao imekuwa imara kwa zaidi ya miaka 25. Rachel sasa alimpa ‘’Go ahead’’ Gilbert ya kufatilia mipango ya ndoa, Kwake Gilbert lilikuwa ni jambo rahisi sana kutokana na kuwa Baba yake ‘’Masasila’’ alikuwa ni mchungaji maarufu sana na kaka zake walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, hivyo haikuchukua muda mrefu hata walipolikamilisha swala hilo. Baada ya Ndoa, Rachel ambaye awali aliwahi mwambia Gilbert kuwa, hajawahi lala na mwanaume,  sirini alishawahi fanya hivyo na mpenzi wake waliotengana nae kwa kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita, aliyeitwa Juma! Lakini kwa mara ya kwanza tu baada ya kulala na Gilbert kwa tendo la ndoa, ndipo alipogundua kuna utofauti mkubwa sana kati ya mpenzi wake wa awali ‘’Juma’’ ambaye alilala naye, na Gilbert! Kwa Gilbert alitumia muda mfupi sana kujikuta akiridhika ‘’orgasm’’, ukilinganisha na mpenzi wake wa awali, ijapokuwa Gilbert hakujua lolote! Baada tu ya tendo la ndoa, kwa mara ya kwanza na kuendelea, ndipo akili yake Rachel ilipojikuta ikimuwaza Gilbert zaidi na zaidi, alikuwa na Gilbert kila alipoenda kimawazo, alikuwa akimlinda Gilbert kimawazo, kuchelewa kujibiwa meseji na Gilbert kulimpelekea maumivu makubwa sana! ambayo alijikuta kwa wakati mwingine hata akiangusha machozi, lakini alishangaa alipomwambia Gilbert, yeye alishangaa kana kama ilikuwa ni kawaida sana, ila Gilbert alikuwa akimpenda kwa dhati sana Rachel! Rachel alijikuta akimsamehe na kumwamini sana Gilbert. Maisha yao yaliunganishwa kiakili na kugongelewa msumari kimwili kwa namna wanavyozidi kuwa Pamoja!!

BIOLOJIA YA UBONGO WA RACHEL KWENYE PENZI JIPYA!!

Ni visa vilivyojaa lakini vina misingi mikubwa sana ya kisayansi. Kiwango kikubwa cha Testosterone na nguvu kubwa ya mifumo ya hisia ‘’amygdala’’ na mgandamizo mdogo wa hisia tokea ubongo wa mbele ‘’prefrontal cortex’’ kwa mwanaume, humfanya kuwa na uwezo mdogo sana wa kudhibiti hisia zake za mapenzi zinapomuwaka!! Mwanaume siku zote yupo hatarini zaidi kuzini kuliko mwanamke, sishangai jaribu hili lililomshinda hata mfalme Daudi katika Biblia. Mwanaume anapoona, huchochewa atende , hii ni kwa namna ambavyo huzalisha microgram zaidi ya 14,000 za testosterone kila siku. Sio rahisi kuzidhizibiti kirahisi, ni sawa na lile fungu linalosema ‘’Usiyachochee mapenzi!!’’. Visa vingi hata vya wanaume kubaka mabinti wao wa kazi, hutokana na sababu hizi. endapo jamii haitajua tatizo hili, uzinzi utaendelea kuwa ni tatizo lisilotatulika hata maofisini!! Ni muhimu sana kwa wanaume kuoa wake kama mtume Paulo alivyosema kuliko kujifanya anakaa ‘’single’’ na bado anazalisha kiwango kilekile cha testosterone. baadhi huisi kwa kufanya mazoezi unaweza punguza msukumo huu. lakini mazoezi ndiyo huchochea zaidi testosterone, na kupunguza ‘’estrogens’’ homoni. ambazo zingepunguza msisimko wa mapenzi. Wanawake wote wanaojua wanapendwa na kuruhusu kuwa na hao wanaume wanaowapenda mazingira ya ukaribu na usiri, tena hasa wakati  wa giza ambalo huchochea zaidi mihemko ya kimapenzi, kwa namna hushusha kemikali za ‘’norepinephrine’’ na kuongeza ‘’acetycholine’’ na serotonin. ambazo kwa Pamoja huongeza msisimko kwa mwanaume, wanawake wanaoruhusu mazingira haya wategemee tu kuishia katika uzinifu kadri wanavyoongeza zaidi odds.

Gilbert ile siku aliyotoka Party Pamoja na dini yake yote, lakini alijikuta na yeye hana nguvu tena ya kujizuia, sababu kubwa ilikuwa ni hiyo!

Kwa upande wa Rachel aliyeweza kujizuia ilihali naye alikuwa amesisimka sana, sababu kubwa iliyomuwezesha ilikuwa ni uwezo wa Ubongo wa wanawake! Wanawake wana ubora sana wa sehemu ya ubongo inayoitwa ‘’Anterior cingulate cortex na pia Prefrontal cortex’’. sehemu hizi huwa zina nguvu sana ya kuzuia nguvu za hisia tokea sehemu ya hisia ‘’amygdala’’ ambayo nayo ni ndogo kidogo kwa wanawake, ukilinganisha na ilivyo kwa wanaume! Hii ndiyo siri ya mafanikio ya Rachel. Kwake mwanamke kufanya mapenzi kuna nguvu lakini sio kwa kiwango kikubwa kama ilivyo kwa mwanaume. Gilbert alipokuwa akimshauri, kichwani mwake alikuwa akijiuliza maswali mengi sana mfano, vipi kuhusu dada anna? Vipi kuhusu Gilbert baada ya kulala naye, atanichukuliaje na ilihali halikuwa lengo lake la awali? Na kwanini niende wakati halikuwa lengo letu la kukutana leo? Maswali ya mtindo huu yote yalikuwa tu yakizunguka katika ACC na PFC wakati huo Gilbert mtambo upo OFF na TPJ ‘’temporal parietal junction’’ ikifikiria tu namna ya kufika Ghetto!!

Kwa Mara ya Kwanza Kuzima Kwa ACC &PFC Kwa Rachel!!

Rachel alipokuwa akilala na Gilbert kwa mara ya kwanza, alijikuta akiridhika zaidi ya alivyowahi fanya hivyo na Juma! kwa sababu kubwa moja! Kwa mwanamke kuridhika kimapenzi kunahusiana moja kwa moja na kuridhika kiakili. Mwanamke anapokuwa bado ana maswali mengi na mashaka mengi kuhusu huyo mwanaume, mfumo wake wa hisia huwa na msisimko mdogo sana, na hutumia muda mwingi sana. na anaweza kabisa pia asiridhike au ku ‘’orgasm’’. Lakini mwanamke anapokuwa amemridhia mwanaume na kumwamini, hujikuta akiridhika kwa haraka sana. Hii ni kwasababu, ile sehemu ya ubongo inayohusiana na maswali juu ya hofu na mashaka kuhusu huyo mtu, inayoitwa ‘’anterior cingulate cortex’’, huwa inaridhika na kujizima, na hivyo kuruhusu mihemko toka kwenye amygdala kuwa na nguvu moja kwa moja, ya kumsisimua mwanamke mpaka maximum. Rachel alishangaa kwa sababu hii, kwa kuwa mwanaume wake wa kwanza ‘’juma’’, alikuwa bado hajamuamini vya kutosha, hasa kutokana na tabia zake za uhuni, ijapokuwa naye alikuwa na pesa nyingi. na ndio maana ilikuwa vile. kumbuka tafiti zimethibitisha hoja hii, kwa mfano, wanawake waliopewa dawa za kutuliza misongo ya mawazo ‘’anti-depressives’’ walionekana kuwahi kuridhika ukilinganisha na ambao hawakupewa, na walikuwa na mawazo! Na pia wanaume ambao huwa na harufu chafu za vinywa huwafanya wanawake wao wasiridhike kwa kuwa, harufu mbaya hufanya sehemu za ubongo za uwepo wa hatari kuamshwa, hasa za maeneo ya shina la ubongo ‘’pontomedullary chemoreceptors’’.

KUUNGANISHWA KIHISIA

Baada tu ya kulala na Gilbert, na hata Gilbert baada tu ya kulala na Rachel, kiwango kikubwa sana cha Oxytocin sawa na dozi ya kutosha ya dawa za kulevya! huzalishwa tokea kwenye Hypothalamus na kisha sehemu ya nyuma ya pituitary gland. Oxytocin kama tulivyoona awali huusiana moja kwa moja na viwango vya Dopamine na serotonins, na hizi homoni hujenga hisia za raha, uraibu wa kuwa Pamoja na oxytocin huwaunganisha wapenzi. Mapenzi ya kwanza kabisa, huwa na viwango vikubwa zaidi! Kuna kamsemo huwa kanasemwa kwa wanawake ‘’hutamsahau aliyeanza kukutoa ubikra’’, hoja hii imejengwa katika msingi  huo, ulikuwa ni mpango wa Mungu kuwa, wapenzi watakao kutana kwa mara ya kwanza waunganishwe zaidi kiakili na kimwili’’, lakini kitendo cha mwanamke kulala na huyu na kesho na mwingine, huaribu utendaji wa Oxytocin kwasababu, hii homoni huusiana na Dopamine na kumbukumbu ya huyo mwenzi. Ni kama mama atakavyolia kwa msiba wa mtoto wake tu, sio kila mtoto duniani! Hii inamaanisha, hisia  hizi za kuwa Pamoja huusisha, nguvu ya msisimko wa kihisia na taarifa za huyo mtu. Mpenzi wako huwa ni kama folder katika ubongo wako, unapoweka wengi maana yake ni kuwa, kwa kiwango kilekile ambacho alipaswa kuwa mmoja, sasa wapo watano. Yaani kwa oxytocin ileile aliyopaswa apewe mmoja, umeigawa kwa watano, madhara yake ni kuwa, hutaweza kuwa na nguvu ya mapenzi na hutafaidi mapenzi kwa kuwa unaathiri mfumo wako wa kihisia. Hii inaweza kuwa ni miongoni mwasababu za kale katika Biblia za kuruhusu talaka endapo tu mwanamke atakuwa mzinzi!!

Je Wajua Biolojia Pana Ya Kiss!!

Kitendo tu cha kumpiga kiss mwanaume au mwanamke, mate yenu yanapokutana, kwenye mate kuna zaidi ya chembechembe elfu moja ‘’bioactive molecules’’ ambazo ndani tu ya sekunde huenda mpaka kwenye ubongo, na huko huanza kutafsiri mpaka kiwango cha jenetikia cha huyo mtu, wanasayansi baadhi husema, kama mtu huyo uliyepigana naye kiss atakuwa anafanana na wewe kiundugu wa mbali, basi kiss lake halitakuwa na nguvu. Lakini miongoni mwa vitu vya kuzingatia ni kuwa, kila kiss unalopigana na mtu ambalo litahusisha kubadilishana nae mate, litajenga kumbukumbu za milele katika ubongo wa huyo mtu, hii ni kama tu ambavyo ilivyo wa ngono, huaminiwa pia kuwa, chembechembe za mbegu za mwanaume, ijapokuwa zitaondolewa, lakini kumbukumbu zake za kijenetikia kamwe hazitaisha kwa huyo binti, inaitwa kitaalamu ‘’male microchimerism’’. ijapokuwa inaendelea kuchunguzwa kwa tafiti, lakini ziliwahi kuwepo tetesi za tafiti kuwa, chembechembe hizo huendelea kubakia kama kumbukumbu kwa huyo binti!! Unaweza fatilia zaidi hili, lakini biolojia inaonesha ni kwa namna gani ukaribu baada ya kukutana kimwili huwa na matokeo ya kuwaunganisha watu zaidi ya inavyoonekana. Kumkumbatia mtu baada tu ya sekunde 20 hupelekea kuanza kuzalishwa kwa oxytocin. ambayo baada ya muda itaanza kujenga hisia za kumuamini huyo mtu!!

NADHARIA ZA KUZIKATAA ‘’HAKUNA JENETIKIA ZA UAMINIIFU’’

Kuna wanasayansi ambao husambaza kuwa kuna aina ya kinasaba au gene inayoitwa ‘’vasopressin gene’’, ambayo wameifanyia utafiti kwa baadhi ya wadudu, wanaoitwa ‘’Prairie voles’’ na ‘’montane voles’’ . wamegundua kuwa, kwa prairie voles, gene hii ni ndefu na wadudu hawa huishi na wapenzi wao wamoja tu, lakini kwa ‘’montane voles’’ gene hii ni fupi na huwa na wapenzi wengi. Kwa hiyo sasa, huwaaminisha watu kana kama kuwa, wanaume binadamu pia wana msingi huu, wanaweza kuwa na gene ndefu au fupi!! Hii mitazamo imeshapitwa na wakati, hakuna gene inayojenga msingi wa tabia, na kama tulivyoona katika sura iliyopita, maendeleo makubwa zaidi ya biolojia yanathibitisha hoja hii kwakuwa sasa hivi inatambulika, vinasaba au genes ni sehemu tu ambayo nayo inaongozwa kama zilivyo zingine, na hata pia utafiti huu uliofanywa na Chuo cha Maryland, hauna msingi mzuri wa kuelezea tabia za binadamu kwa kujifunza kwa wadudu, ambao nao hufuata moja kwa moja msingi wa jamii zao.

UBONGO WA MAMA EUNICE!!

Mama na mtoto

Stori hubadilika milele baada ya ujio wa mtoto, na haitabadilika milele!!  Maisha ya jamii nyingi mama hubadilika hata mtindo wake wa utafutaji, maana wamama wengi ndio huachiwa zaidi mzigo wote wa kuwalea Watoto wao kiuchumi na kijamii. Wanawake wengi huanza kuvutiwa na kuwa na Watoto hata kabla ya kuwapata, wanawake hawa wanapokuwa wakishika Watoto wa wenzao, harufu za vichwa vya Watoto huwasisimua wanawake kwa kuwa na ‘’pheromones’’, na hizi huwafanya wanawake kuanza kuzalisha homoni za ‘’oxytocin’’ ambazo huwafanya kuanza kutamani sana kuwa na watoto.

Baada tu ya kutungwa mimba, mtoto anapoanza tu kuumbwa, kile kitendo tu cha kuunganika kwa mfumo wa damu wa mama na mtoto, huanza kupelekea mabadiliko katika mfumo wa homoni wa mama, ambayo, ndiyo mwanzo wa kubadilika kwake.

Biolojia Mpya ya Umama

Progesterone huanza kujaa ambayo huanza kufanya matiti yake kusisimka ‘’tender’’ na ubongo wake huanza kama kulewa au kupoa hivi ‘’sedated’’, hisia hizi cha uchovu huambatana na hali yake ya kupenda kulala na kula zaidi. Sehemu zake za ubongo zinazotawala kiu na njaa huchochewa zaidi na mabadiliko haya ya homoni. Na lengo kubwa huwa ni kumsisimua kuzalisha damu hata mara mbili ya damu yake, ‘’kwa ajili ya mtoto’’. Sehemu zake za hisia za harufu na Ladha huongezeka kimsisimko kwa lengo la kumlinda asije akala vyakula vyenye kuhatarisha hali ya mtoto wake. Akili yake huelekezwa zaidi kwa kilicho katika mfuko wake wa uzazi au ‘’uterus’’, unapofika mwezi wa tano, huanza kuhisi kama kuna vitu maeneo ya chini ya tumbo ‘’abdomen’’

Kiwango cha progesterone huwa hata mara mia zaidi ya kiwango cha kawaida, progesterone katika ubongo siku zote ni kama dawa za kutuliza maumivu na kukufanya ulale, kama valium. Hupooza sana ubongo, hizi homoni zikichangamana na homoni za estrogen ambazo nazo huwa juu, kwa Pamoja huwa na lengo moja pia la kumlinda mama dhidi ya homoni nyingi sana za stress. ambazo huwa zinazalishwa na mtoto, homoni za cortisol. Mama kwa hiki kipindi chote sehemu zake za ubongo zimekuwa zikizuia yale mabadiliko ya mzunguko wa mwezi, zikikuza sehemu zinazohusiana na ulaji na unywaji na harufu, na sasa mwishoni kuanzia mwezi wa tano na sita, huanza kutengeneza mifumo ya upendo wa mtoto. Hapa huusiana na mama kumuwaza sana mtoto wake, akifikiria namna atakavyombeba n.k. na unapofikia mwezi mmoja kabla ya kuzaa, kiwango cha homoni za stress toka kwa mtoto huwa ni kingi sana, na kumbuka, homoni hizi huwa sio kwamba mama naye anakuwa na stress, ila anakuwa hajatulia!! Mwezi mmoja kabla ya kujifungua, wamama wengi wanaofanya kazi huwa hawawezi kuzingatia vizuri, vichwa vyao huwa vimechanganyikiwa kisaikolojia!!

JE WAJUA

Kuanzia mwezi wa sita wa ujauzito, Ubongo wa mama huwa unapungua ukubwa au volume. Picha za fMRI huonesha ubongo wa mama mjamzito ukizidi kuwa mdogo kwa kipindi hiki, lakini zinapobakia tu wiki kadhaa kabla ya kujifungua, huanza kukua tena!! Sio kwamba ubongo hupungua ukubwa kwa kupungua kwa seli au sehemu za ubongo, Hapana, huwa tu unasinyaa!! Na wanasayansi hukubaliana kuwa hii ni kutokana na mabadiliko mengi ya kikemikali yanayotokea kipindi hiki, lakini baadae hurejea kawaida.

Maisha Baada ya Eunice Kuzaliwa!!

Mtoto anapokuwa akipita katika njia ya uzazi, maelfu ya homoni za oxytocin huzalishwa. Maelfu pia ya connections katika ubongo huundwa. Baada tu ya kuzaliwa mama hujisikia raha sanaa ‘’Euphoria’’ ambayo huchochewa na oxytocin na dopamine. Lakini pia mama uwezo wake wa kuhisi au sense ‘’harufu, mguso, kuona na kusikia’’ huwa juu sana. Hii humfanya awe makini au alert zaidi kwa mtoto wake. Kwa mama, harufu ya Ngozi, kichwa cha mtoto wake, kinyesi, maziwa anayotema n.k. hutengeneza kumbukumbu kubwa katika kichwa chake. Na atakuwa na uwezo wa kuzigundua hizi kwa ufanisi wa asilimia 90% hata ukichanganya na za wengine. Miguso ya vidole vya mwanae, sauti za kutaka kuanza kulia n.k. kwa Pamoja zote hukaa kwenye kumbukumbu za ubongo wake. ndani ya siku na mwezi, na kuendelea, hisia za ulinzi wa mwanae huzidi kuongezeka, na huwa na hasira sana katika  kumlinda mwanae. Wamama wengi sasa hivi huwa wepesi kushindana na waume zao pale wanaposhindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa familia zao, kama tulivyoona sababu zake awali.

Wazazi wasio waleaji wazuri!!

Kiwango kikubwa cha testosterone kwa wanawake na hata wanaume hupunguza uwezo wa kulea!! Wanawake wenye kiwango kikubwa cha testosterone huwa sio waleaji wazuri. tafiti huonesha hivyo. na wababa wenye kiwango kikubwa cha Prolactin, huwa ni waleaji wazuri sana. wengine hata wakihisi hisia kama za ujauzito pale wake zao wanapokuwa wajawazito ‘’couvade syndrome’’, kama tulivyoona awali. Na huwa na msisimko wa chini sana wa kufanya mapenzi, pale wake zao wanapokuwa katika kipindi chote cha ujauzito. tofauti kabisa na wenye testosterone nyingi, ambao bado huwa na msisimko mkubwa, hawa sio waleaji wazuri kutokana na tafiti.

 KUHUSU KUZAA KWA OPERSHENI!!

Binadamu sio kondoo. Kondoo hutumia dakika tano tu baada ya kumzaa mtoto wake, kuungana nae kihisia za upendo, pale anapomnusa nusa n.k. ukimtenganisha kwa hizi dakika! Hata ungana na mtoto wake kihisia kabisa za upendo wa mama na mtoto! binadamu hata azae kwa operesheni, baada tu ya kuzinduka, hisia za kuungana na mtoto wake huendelea kujengeka kwa kiwango kilekile. Wengi hawajui kuwa, sehemu za ubongo wa mama zinazosisimuliwa kwa upendo wa kuwa na mtoto wake, huwa ni zilezile ambazo zilikuwa zinasisimuliwa alipokuwa na mme wake au mpenzi wake. Na tafiti zaidi na chuo cha London zimeonesha kuwa, sehemu za ubongo zinazohusiana na kumkosoa mtu, au ukosoaji, ambazo ni zilezile za ‘’anterior cingulate cortex’’, huzimwa kabisa pale ambapo mtu humzungumzia anayempenda!! Kwa hiyo hilo linaweza kukupa umakini unapoenda kumkosoa mtoto kwa mama yake!!

NGUVU YA KUNYONYESHA!!

Kunyonyesha kuna nguvu kubwa sana katika ubongo wa mama. Mtoto na vidole vyake vidogo, anaposhika titi la mama yake, na kuanza kulinyonya, hupiga shoti ya uzalishaji wa homoni za oxytocin, dopamine na Prolactin, kwenye ubongo wa mama yake. Hili humfanya mama kuwa na msisimko mkubwa sana wa kujisikia raha. Na pia kiwango cha oxytocin hiki huendelea kumfanya kujisikia uhitaji wa kuwa na mwanae. Tafiti ilifanywa kwa panya wenye mimba, wakawa wakipewa mazingira ya kuchagua aidha kubonyeza sehemu moja na kufungua wapate dawa za kulevya za Cocaine, ambazo humfanya ajisikie raha, au wabonyeze sehemu nyingine wapate kukutana na Watoto wao, wawanyonyeshe!! Panya hawa kila wakati walichagua Watoto wao!! Ijapokuwa kama ungewapa chakula na cocaine wangeenda kwa cocaine. Hii ni kwakuwa, kunyonyesha kuna nguvu kubwa sana ya Oxytocin, na msisimko wa raha kwa wamama kwa Pamoja. Na inafahamika kuwa, wamama wengine wanapokuwa wakinyonyesha, hutulia sana na muda mwingine hata kusahau kazi zao. Lakini pia, wamama wengine wamejikuta hata wakishindwa kubalansi upendo kati ya Watoto wao na waume zao, kutokana na nguvu kubwa ya ukaribu huu unaotokana na kunyonyesha.

Wamama wengi hujikuta wakishindwa kabisa kuwa mbali na Watoto wao, hata kwa kitambo kidogo, hii huitwa pia ‘’withdrawal syndrome’’. Hii hutokana na namna ilivyo strong bond kati ya mama na mtoto wake, kwa gundi za ubongo kiakili na kihisia, zinazoshikiliwa na homoni.

MAMA MBAYA HUTENGENEZA MAMA MBAYA!!

Mwanasaikolojia Michael Meaney aligundua kuwa, malezi ya mama huathiri moja kwa moja sehemu za ubongo za mtoto wake wa kike. Kumbuka tulishaona kuwa, Watoto wakiume hawaathiriwi sana na malezi katika ubongo wao. Alipojaribu kumchukua panya mtoto na akamweka alelewe na panya anayefanana kabisa na mama yake ila sio, mama huyu hakumjali mtoto huyu. Mtoto huyu baada ya muda alipoangaliwa sehemu za hippocampus na amygdala ambazo hutumia Oxytocin na estrogen, zilionekana kuathiriwa kabisa!! Kumbuka tumeona sifa hizo juu nyingi sana za umama zimejengwa kwa utendaji wa homoni hizi, sasa basi, kitendo cha maeneo haya kuathiriwa, maana yake hazitaweza kutumia vizuri homoni hizi, maana yake pia ni kuwa, unaenda kuwa na mama asiyemleaji mzuri au mwenye shida!! Hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mama ndiye wakulaumiwa zaidi binti yake anapoharibika kutokana na biolojia.

Lakini pia imeonekana kuwa, malezi toka kwa wazazi wanaojali na kuonesha upendo, hujenga Watoto walio smart, wenye afya na wenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na stress. Watoto waliolelewa vibaya huwa na shida nyingi za kupata stress kirahisi, kusisimka haraka sana kwa mambo madogo, magonjwa na kuwa na hofu.  Hapa ni pa kuwa makini sana, kuna nadharia katika jamii za wasiojua hili zinazowadanganya kuwa, mtoto aliyepitia shida huwa na uwezo mkubwa wa kuzikabili! Sio kweli, hiyo huwa tu ni neema ya Mungu. Na mifano hiyo huwa haina undani wa kifikra, katika watu mia wanaokumbana na mazingira magumu, wanaweza kumi tu wakafanikiwa, na jamii huwatumia hawa kama kioo, ilihali uhalisia wa hali unapaswa kuchukuliwa kwa takwimu za wengi zaidi ambao ndio hao 90. Wanaolelewa vizuri mia, una uwezo wakupata 90 walio vizuri na kumi tu wenye shida, lakini  wasiojua tena, hutumia hawa kumi kujifunzia. Jamii inapaswa kuondokana na fikra potofu za kujifunzia.

JANGA LISILOONEKANA!!

Kutokana na ugumu wa Maisha, wamama hupaswa kutokuwa na watoto wao kwa muda mwingi kwa ajili ya kuwalea. Watoto wanapaswa kuachwa katika mazingira tofauti tofauti sio kwa mapenzi ya wazazi wao, ila ni kutokana na changamoto za Maisha. milipuko ya magonjwa na tabia za ajabu, huwafanya wamama kuwa wahanga muda wote wa utendaji wao, katika kuwapambania Watoto wao. lakini muda huohuo kuwa wahanga wa kihisia wa kuvunjwa moyo kwa namna wanaowapenda wanapopitia hali ngumu.

Janga lisiloonekana ni kutokuwa na uhakika wa Maisha, kukosa uhakika wa kuwa na mahitaji ya kukidhi Maisha kwa kila siku ya Mungu! Jambo hili huongeza stress kwa mama ambayo huathiri uwezo wa uleaji wa mtoto wake. Kiwango kikubwa cha Cortisol, kilionekana kwa Wanyama ambao, walikuwa kwenye mazingira ambayo hawana uhakika, kama kesho yake watapata mahitaji yote ya kukidhi mahitaji yao, na ya Watoto wao! Inasikitisha sana namna ambavyo wamama hawa hawakuwa wenye nguvu sana za kuungana na wanao, wanapokuwa kwenye magoti yao, na huu ndiyo msingi wa kuwepo kwa Watoto ambao hawana ujasiri Pamoja na uwezo wa kuchangamana na jamii zao kwa ujasiri. Hii ni kwa kuwa walikoseshwa walipokuwa wadogo pale wazazi wao walipokuwa wameathiriwa sana, na mtindo mgumu wa Maisha.

Ni jukumu la jamii kujua tunapaswa kusaidiana kulea. Kama ilivyo kwa Wanyama wanavyoshirikiana, hapo awali kulikuwa na mafanikio sana katika uleaji kwa namna ambavyo jamii zilikuwa zikishirikiana sana kwa hali na mali. Kadri mfumo wa ubinafsi unavyoongezeka, basi umasikini unazaidi kuathiri mifumo ya uleaji. Na hivyo pia ni muhimu wapenzi kujua kuwa, kama mahitaji kwa familia yatakuwa changamoto, ni muhimu kuchelewa kuzaa au kutozaa Watoto wengi, la sivyo hupelekea tatizo hili linaloitwa ‘’attention disorder’’.

BIOLOJIA YA MIGOGORO MINGI YA WAMAMA NA WAUME ZAO

Ukiachana  na migogoro ambayo sababu zake zinafahamika mfano, migogoro ya kitabia kama wizi, uzinzi, hasira, umasikini n.k. migogoro mingi sana katika familia, ukiachana na sababu hizo, huwa inatokana  na namna ambavyo ubongo wa wanawake unavyoyachukulia mambo, huwa ni tofauti na namna ambavyo ubongo wa wanaume huwa unayachukulia.

Wanawake kwanza kabisa huwa na aina yao ya maumivu ambayo, ni ya tofauti kwa kiwango ukilinganisha na kwa wanaume. Wanawake huwa na maumivu ambayo kwa kiingereza huitwa ‘’Gut feelings’’, haya ni maumivu ambayo anakuwa kama anakitu kimemkaa maeneo ya juu ya tumbo kinamkera!! Wanaume katika scan za Ubongo huonekana kuwa na msisimko mdogo sana wa aina hii ya maumivu, tafiti iliyofanywa ilionekana kwa wanaume ni maeneo mawili tu ya ubongo yakisisimka, wakati wanawake wakionesha maeneo tisa. Inaaminiwa kiwango kikubwa cha estrogen huwafanya wanawake kuhisi zaidi maumivu ya kimwili na kihisia. Na pia uwezo wao mkubwa wa kuhisi hisia za vitu, toka kwenye milango ya fahamu na tumboni, katika ubongo. huwafanya kuwa wakihisi maumivu kwa kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na ilivyo kwa wanaume.

Tatizo huanzia hapa, Linapotokea tatizo lolote lile katika familia. Mwanamke huumizwa sana na mwanamke hulichukulia tatizo katika hisia zake, huumizwa na kulionesha katika mwonekano wake, huonesha huzuni. Hii hali huitwa ‘’Emotional’’. Mwanamke huitaji kuona anapomweleza mwanaume wake, au hutaka kuona mme wake, naye analipokea tatizo lile kwa kiwango kilekile. Shida ni pale mwanaume wake anapokuwa haoneshi kulipokea kama yeye alivyotegemea! Wanawake wengi huumia sana, kwao huisi hii ni kama namna ya usaliti, kwao mwonekano ambao mwanaume anauonesha baada ya kulitambua tatizo, ni kama anasema kuwa, hili sio tatizo langu!! Lakini ukweli ni kuwa, Ubongo wa mwanaume huwa ni kama unasema, kwa gharama yoyote ile, usioneshe unyonge kwenye sura!! Hii ni kama nilivyosema katika sayansi za asili za sababu za ndevu, ambazo ni kuficha hisia za unyonge.

Wanaume pia huwa na shida kubwa sana ya kuchukulia poa sana mionekano mbalimbali ya kihisia, hasa za huzuni, ambazo wake zao huonesha. Wanawake huitaji sana kuelewana kupitia lugha ya mionekano ya sura!! Mwanamke anapokuwa ameumia sana, na mmewe akijua au asipojua maumivu ambayo mkewe anapitia, anapokuwa haoneshi kwa nje kuguswa, humfanya mke wake kujisikia vibaya sana. Wataalamu wa ubongo ‘’psychiatrists’’ hunukuu kuwa swala hili hupelekea migogoro mingi sana katika ngazi za kifamilia.

Wanaume wana uwezo wa kusoma maumivu katika sura za wanawake kwa asilimia 40% wakati wanawake wanaweza kwa asilimia  90%. Wanaume huwa hawapendi kuwa na mtu ambaye anajisikia huzuni ‘’sad’’, na hii ni kwa kuwa, ubongo wao haupendi kuonesha hisia za udhaifu kwao. lakini wanawake wanaonesha kuwa sawa tu, kwa kuwa na watu wenye huzuni, au na watu wenye furaha.  Wanaume huwa hawapendi kuwa na watu wanapokuwa wanapitia nyakati ngumu za kihisia, hupenda kupambana na hali zao wenyewe, na hujidanganya kuwa na wanawake hutamani kuwa wenyewe kama wao.

Ubongo wa wanawake huchakata taarifa za kihisia ikiwemo hizi za huzuni ‘’emotional’’, kwa pande zote mbili za ubongo. wakati wanaume huchakata hisia hizi kwa upande mmoja tu wa  ubongo, kama takwimu toka chuo cha Michigan inavyoonesha. Ni muhimu kwa wanaume kutambua kuwa, baadhi ya vitu ambavyo kwao vinaweza kuwa vya kupuuzia, vinaweza kuwa na nguvu kubwa sana kwa wanawake.

Wanawake huwa rahisi zaidi kupoteza usingizi kutokana na kuwa na msongo wa Mawazo, ukilinganisha na wanaume. na inafahamika hiyo kutokana na namna homoni za estrogen zilivyoonekana kuwa na nguvu zaidi katika mfumo wa kulala na kuamka ‘’cirardian rhythm’’. Na pia inafahamika kuwa wanawake wapo hatarini kupata tatizo lingine la aina ya msongo wa Mawazo linaloitwa ‘’anxiety’’, ambapo hii ni ile hali ambayo mtu anahisi muda wote kuwa tatizo linaweza tokea au linatokea. hii hali ya mtu asiweze kutulia, huwa inatokea kwa wanawake mara nne zaidi ya wanaume.

Kipindi mwanamke anapokuwa na mgogoro na mwanaume wake, huwa anamwangalia machoni, huwa anaungana nae kihisia, huwa anafanania au match na mapigo yake ya moyo, huwa ana ‘’match’’ nae mfumo wake wa kuhema, na kisha anaichukulia hali yake sasa!! Hapo mwanaume anapokuwa anamdanganya, huwa ana uwezo mkubwa kugundua kwa kuweza kujua kuwa, hakuna uhusiano wa hali yake na maneno anayoyasema!! Hii ni nguvu kubwa sana ya ‘’mirror neuron system’’ ambayo inawezeshwa na maeneo mengi ya ubongo wa juu Katikati kama ‘’premotor areas, somato-motor cortex, nyuklia zake za juu na chini, n.k’’ muda wote huu mwanaume anaweza kuwa bado hajashtuka, lakini mwanamke anapoangusha machozi baada ya kugundua kuwa anadanganywa! Mfumo wa ubongo wa mwanaume nao huwaka!! Wanaume hawana uwezo wa kuhimili kuangalia machozi ya wanaowapenda, hushindwa hata kutawala pia mifumo yao ya hisia, na hii ndiyo sababu wengi huamua kuondoka au kujaribu kuikimbia hiyo hali kwa gharama zote.

Kadri umri unavyoenda wengi wa wanaume na wanawake huwa na uwezo wa kutawala hisia zao. Mfano wanaume wanapozidi kuzeeka viwango vyao vya testosterone hushuka, na prefrontal cortex huwa na nguvu zaidi Pamoja na estrogen ambayo nayo huongezeka. Hii huwaongezea ubora wa maamuzi wanayoweza yafanya, na huwa hawana msukumo mkubwa wa hasira kama ulivyo kwa vijana.

UBONGO WA MWANAMKE ULIOKOMAA ‘’MIAKA 51+’’

Ukomavu

Purukushani zote alizozipitia tangia alipoanza kuitwa Dada mpaka akaitwa Mama Fulani na sasa anaitwa Bibi, zimemfanya amekuwa mtu mpya kabisa. ubongo wake unapitia mabadiliko makubwa kabisa ambayo yanapindua kila kitu kilichowahi fanyika katika historia ya Maisha yake. Kuanza miaka arobaini na kitu mfano 43 na kuendelea wanawake hupitia kipindi kinachoitwa ‘’Perimenopause’’. Hizi huwa ni dalili za kwanza kabisa za kuwa mzunguko wake wa mwezi unaenda hatiani. Hii huambatana na uzalishaji usioeleweka wa homoni za estrogen katika ovaries zake. Hali hii huwa na usumbufu mkubwa sana kwa baadhi ya wanawake na hata baadhi huonesha kabisa dalili mbalimbali za kutokujisikia vizuri.

Hapa kinachotokea huwa ni hiki, estrogen huwa inahusiana moja kwa moja na utendaji na uzalishwaji wa homoni mbalimbali za kujisikia vizuri kichwani, kama vile ‘’norepinephrines, acetylcholine, dopamine na serotonin’’. Utendaji wa homoni zote hizi huathiriwa kwa kadri ambavyo viwango vya estrogen kiongozi wao unapoathiriwa. Baadhi ya wataalamu wa afya huwapatia wagonjwa wao matibabu ya ‘’anti-depressives’’  au dawa za kuzuia msongo wa Mawazo, ambazo huonekana kuwasaidia, lakini msingi mkubwa hapa huwa ni namna ambavyo dawa hizi husaidia kurejesha balansi ya awali.

HAJALI WALA HAWAZI!!

Hawa wamama wakubwa bwana huwa hawajali na wala hawapendi kujali. Hawa swala la Kupeana talaka kwao wala sio la kuwatishia tena! Wengi wasiojua biolojia hii huisi kuwa, sababu ni kiburi kwasababu ya Watoto wao wakubwa, lakini tambua tokea leo, wala hawajali hata hao Watoto wao wakubwa!! Kinachotokea hasa baada ya miaka Hamsini hivi kwa wastani, huwa ni kustop kwa uzalishaji wa homoni za mzunguko katika ubongo. sasa hivi kile kiwango kikubwa cha Oxytocin ambacho kilikuwa kinaambatana na estrogen hakipo tena! Kile kiwango kikubwa cha dopamine ambacho kilikuwa kinasababishwa pia na estrogen, ambacho kilikuwa kinampa uraibu wa kukutafuta tena na tena, hakipo tena kama awali. Sio kwamba amekuwa sio mtu wa kupenda tena, ila wastani wa msukumo ule wa awali haupo tena. Ile Oxytocin ya kumfanya amuwaze mtoto wake kila wakati haipo tena kama ilivyokuwaga zamani. Hii ni kama tu ambavyo Mungu mwenyewe alivyoruhusu kuwa, baada ya muda ‘’mwanaume na mkewe wataambatana, wataondoka nyumbani’’, hiki ni kile kipindi ambacho kila mtu anapaswa kuishi kwake ila bado tupo Pamoja!! Takwimu zinaonesha kuwa, asilimia 65% ya talaka zinazoandikwa kuanzia miaka 50 na zaidi, sababu huwa ni wanawake!!

Kipindi hiki hana malengo makubwa sana juu ya familia yake kama ilivyokuwa awali. Saivi hana msisimko mkubwa tena wa dopamine kama mwanzoni, Maisha yake aliyokwisha yafikia yanamtosha. Huwa hana msisimko tena wa kufanya mapenzi kama ulivyokuwa ukipungua tokea miaka ya arobaini. sasa hivi hatakubali kufanya tena kwa ajili tu ya kumridhisha mme wake kama alivyokuwa akiridhia kwa kipindi kilichopita.

Sasa hivi hupendelea sana kufanya vitu ambavyo vitakuwa vikimfurahisha yeye. Hupenda sana kufanya safari mbalimbali za kutalii, hupenda kuzurura sehemu mbalimbali kukutana na rafiki zake. Hupenda sana kukaa na marafiki zake wakizungumzia maswala mbalimbali kuhusu Maisha yake ya awali, Watoto wake, maswala ya kazini kwake na mengineyo kwa ujumla.

HUWA NA HASIRA KWA WAKATI FULANI HASA NA MME WAKE!!

Sasa hivi ile nguvu ya homoni ya Progesterone ambayo ilikuwa ikimtuliza awali, haipo tena!! Sasa hivi viwango  vya stress vinapopanda juu humfanya kuwa na ghadhabu ukilinganisha na awali. Sasa hivi kile kiwango cha testosterone hakina mpinzani wake kama progesterone na estrogen, na hivo huwa na hasira sana. na huwa na umakini mkubwa anapoamua kufanya mambo yake, hii ni kutokana na uwezo mkubwa wa kufatilia unaochangiwa na kiwango kikubwa cha testosterone, katika ubongo wake. Huwa navutiwa sana na mwanamama mfizikia ‘’Sabine Hossenfelder’’ anavyozungumzia fizikia ngumu zaidi, tena bila kuwaza, tena aki enjoy!!

Migogoro na mme wake hasa huwa inasababishwa na matarajio ya waume zao. Wanaume kwanza wanapozeeka huwa na kiwango kidogo cha testosterone, na pia huwa na kiwango kikubwa zaidi cha estrogens. Hii huwafanya kuhitaji zaidi kujaliwa au mtu wa kuwajali, ambaye atawafanya wajisikie tena kama Watoto. ‘’kumbuka hii hali ya viwango, inafanana na ile iliyokuwepo kipindi cha udogoni’’. Lakini mambo huwa kinyume kabisa, wamama hawa sasa hivi hawana huo muda, na hawataki tena kuishi kama watumwa wa mtu!! Hawataki kuwaza kuamka kumuandalia mtu mahitaji yake tena, au shughuli za muundo huu, hii huwafanya wanaume wa maeneo mengi kuelekea upande wa pili na kuanza kutafuta vibinti vidogo!! Na wengi hufanikiwa kutokana na kuwa na faida kubwa mbili, kwanza, huwa wana uwezo mkubwa wa kiuchumi wa kuweza kuwamiliki mabinti ikiwemo na mahitaji yao yote.

 Lakini pili, viwango vikubwa vya estrogen huwafanya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kujali ukilinganisha na vijana, ambao, viwango vikubwa vya testosterone huwafanya wasiwe watu wa kujali sana, na wakatili kwa baadhi ya mazingira, na pia sio watu wakutulia sana. lakini pia wazee ambao bado huwa na nguvu za kiume, ijapokuwa sio kwa msukumo kama wa vijana, bado huwaridhisha tu wanawake ambao huitaji zaidi kujali ‘’intimacy’’ kuliko kijana anavyoweza kubaliana na hoja hii. Hizi sababu  huwafanya kuwa na mafanikio tu katika Maisha yao na mabinti wadogo, ambao huweza kuwajali pale ambapo wake zao hawana muda nao tena!! Maisha haya huendelea hata hapo akili ya binti itakapohitaji mtoto!! Mgogoro huanzia hapo kwa kuwa mahesabu mapana ya uwezo mkubwa wa wazee sasa, huwaambia kuwa na mtoto katika Umri wao ni changamoto sana, na mabinti hawawezi kukubali kutoitwa mama!! Migogoro hii mara nyingi huishia kwa hitimisho ambalo lisingesapotiwa na mwandishi!!

Lengo kubwa la kuyajua haya ni hili, kila mtu ajue kipindi alicho nacho na msukumo mkubwa zaidi alio nao, kwa lengo la kujiepusha zaidi pale msukumo unapokuelekeza katika upande mbaya!! Kumbuka binadamu sio roboti na ndio maana unaweza soma kitabu hiki na kikakusaidia kwa kuwa, Pamoja na kuwa homoni na sifa za ubongo zinaweza kukusukuma kuelekea katika jambo Fulani, lakini akili na maarifa kama utakuwa ukijua, zinaweza kukusaidia ukajiepusha. Hii ni sawa na pale hasira zinapokutaka utukane, lakini akili ikakuzuia, hiyo inamaanisha hasira ambayo ni matokeo ya fiziolojia ya homoni na mengineyo, huwezwa tulizwa na akili!! Kutokujua ndiko kufa, watu wanaangamia kwa kutokujua. Nimewahi kutana na wamama wa miaka 50 nakuendelea, wapo baadhi wasio na shida hizi kabisa, na hasa ni wale walio na Imani nzuri. lakini wapo wengi sana ambao huishi mfumo huu wa Maisha kwa kutokujua kipi kinachowasukuma. Na jamii zetu zina wazee wengi sana wahanga wa familia zao kutokana na tabia hizi, tunapaswa kutambua na kusaidiana kila inapowezekana.

NAMNA YA KUPATA KITABU FULL COPY.

Unaweza wasiliana nasi kupitia

brightonshoo7@gmail.com

MOBILE NO: +255 6139 069 30  DR. BRIGHTON SHOO

FULL SOFTCOPY 5,000/=TSH

FULL HARDCOPY 10,000/=TSH

KUMBUKA!!

Injili ya sayansi Q5 haina ajenda yoyote ya Biashara, lakini haki miliki ya kitabu inamilikiwa na Dr.Brighton Shoo. kwa Lengo la kukuza taasisi ya Injili ya Sayansi. na pia, kuwasilisha maarifa kwa idadi kubwa zaidi. Ubarikiwe unaposoma, unapoelewa, na unapofikiria kuwasaidia wengine.

 

 

  Kupata full soft copy link👇👇👇

Pay Now