SIRI YA MAISHA MAREFU
TOPIC 1: MAJI NA UMRI MREFU
Utangulizi
wastani wa watu wengi huisi wanakunywa maji, lakini kiuhalisia wengi wao huwa hawanywi maji ya kutosha. Wengi hutegemea hisia ya kiu ya maji kama alarm ya kuwashtua kunywa maji. Hii ni hatari. Wapo watu wanaosubiria kukauka Kwa Midomo, au mate kuwa mazito kama dalili ya kupungukiwa maji, hii nayo ni hatari. Wengi wa Hawa watu huwa katika hatua za mwisho kabisa za mwili kupungukiwa maji "dehydration".
Wengi hawatambui kuwa Ubongo hushindwa kutofautisha hamu ya maji ya kunywa, na hamu ya Chakula, au vinywaji. Wengi hunywa soda, Juisi, au hata hula Vyakula ilihali walikuwa tu wanahisi hamu ya maji. Hii inatokana na kuwa, Ubongo hushusha hisia ya kiu ya maji unapokunywa Juisi, au hata kula Vyakula kadhaa, SI Kwa kuwa umetosheka na maji! La hasha, bali sababu umesitisha kuzalisha zaidi homoni za hamu ya maji, Kwa kuchanganywa na uwepo wa Juisi au Vyakula.
Je WAJUA!
Sababu ya mwisho ya Vifo vyote ni upungufu wa maji "dehydration". Na ndiyo maana mgonjwa yoyote wa Nusu kaputi yule huanza kusaidiwa Kwa Drip za maji.
je WAJUA!!
Ukila sana usiku unaamka sana na Njaa! Si kweli, unaamka sana na kiu ya maji. Lakini unahisi ni hamu ya Chakula
ZINGATIA
mwili wote ni asilimia kuanzia 70~75% maji. Damu ina maji asilimia~ 93%. Ubongo una asilimia 85% maji. Vimiminika vyote vya mwilini, kama uteute wa ndani ya mifupa (synovial fluid & nucleus pulposus) vimejaa maji zaidi ya asilimia 96%, Tumboni yapo maji zaidi ya asilimia 90%. Seli zetu zimejazwa na maji nje na ndani ya chembechembe, zaidi ya asilimia 60~70%, hivi ndivyo ilivyo hata na Kwa homoni Kwa namna zimeshamiri zaidi maji.
MAJI NA UHAI
matendo yote ya kibiolojia yanategemea sana maji. Bahati mbaya wengi hufundishwa umuhimu wa maji kama miongoni mwa sehemu za Chakula. Wengi huyaweka maji katika sehemu sawa na protini, Wanga, vitamini, mafuta na madini. Kwa Elimu ya muundo huu, hata wasomi hawawezi kuelezea umuhimu wa maji mwilini. Unaweza jaribu hili Kwa kuwauliza wawili watatu unaofahamiana nao! Wengi utagundua wakitumia lugha ya "maji yanasaidia jambo Fulani! .." lugha hii Ndiyo wengi huielewa, yaani huyaweka maji kama nyuma ya vitu vya msingi zaidi mwilini, na kuwa maji yenyewe siyo ya muhimu Kwa kujitegemea.
Sehemu hii haitaleza kirefu sana kuhusiana na umuhimu wa maji, namna yanaweza hata kutatua magonjwa na shida mbalimbali, Kwa kufanya hivyo nitakuwa kama naandika Tena kitabu nikichokwisha kiandika kuhusiana na namna maji yanatatua magonjwa Sugu. Sehemu hii itahusiana na namna maji yanaweza msaidia mtu kutozeeka haraka, kuzeeka vizuri, na kuishi miaka mirefu yenye afya.
MAJI NA UZEE
Inafahamika kuwa kadri mtu anavyozeeka, au kuelekea uzeeni. Uwezo wake wa kutunza maji mwilini na katika seli zake unazidi kushuka. Kiwango Cha maji yaliyo ndani ya seli ukilinganisha na yaliyo nje ya seli hushuka kutoka wastani wa 1.1 mpaka 0.8. wengi hushindwa kuelewa kwanini uwezo huu wa kutunza maji hupungua, lakini yapo mengi yanayofahamika kuhusiana na swala hili.
Kwanza, kadri mtu anavyozeeka, ndivyo ngozi yake inavyozidi kushindwa kufyonza mionzi ya Mwanga wa Jua na kutengeneza Vitamin D. hapa ni kama unapata mantiki hii, kadri mtu anavyozidi kuzeeka, ndivyo anavyopungukiwa zaidi Mwanga na maji. Yaani, huyu mtu Sasa anahitaji maji mengi sana, na vipindi virefu zaidi vya Mwanga.
Watu wengi wanapoelekea uzeeni, hisia zao za kiu ya maji hushuka zaidi, hivyo Kwa wastani huisi kiu Kwa kiwango kidogo zaidi. Na kumbuka, hisia hizi hushuka Kwa kuwa wazee wengi huwa na utendaji mdogo Kwa wastani wa uzalishaji wa homoni zote, ziwe za uzazi, au za hamu za maji.
Unapozaliwa unakuwa na maji mengi sana asilimia 80%, unapofika miaka 70, 80 mpaka 90, unabakia asilimia 50-55%, Tena mwili ukibakiwa na uwezo mdogo sana wa kufyonza Mwanga wa Jua wenye kuwezesha kuzalisha vitamin D, ambayo inahusiana Moja Kwa Moja na homoni zingine zote, na ndiyo husaidia Kinga ya mwili, na vitamin A ambayo inahusiana na afya ya ngozi na kuweza kuona.(Wazee wengi huwa na shida ya kuona, kutokana na upungufu wa vitamin A inayoathiriwa na vitamin D, pia kupungukiwa na ufanisi wa Neva za kuona, kutokana na shida za Kihomoni na cover za Neva za kuona)
LENGO LA STORI FUPI
samahani Kwa wasio na msingi mkubwa wa sayansi, lakini wajikaze maana hata wanaosoma sayansi wengi nao hawalijui hili vizuri.ndo maana ni marachache sana unaweza kutana na mtaalamu anayeweza kukwambia unaweza kuzuia kuzeeka Kwa kunywa sana maji, na kuwahi sana kuamka, na Kutotumia sana taa za kisasa, na kutembea Walahu nusu saa asubuhi na jioni. ( Na Sio stori za ule sana Chakula Fulani, au dawa Fulani za wafanyabiashara)
Tambua hili, mionzi ya Mwanga wa Jua wa asubuhi na jioni huwa na mionzi ya Infrared rays, na Red light, ambayo hii huingia katika ngozi na kusisimua kuzalisha vitamin D, lakini kubwa zaidi, unapofika ndani ya seli za mwili, huingia hata ndani ya chembechembe za seli zinazozalisha nishati, kuamua seli ife au iishi, zinazoitwa "Mitochondria". Mwanga huu hukutana na maji yaliyo ndani ya chembechembe hizi. Na hapo Sasa, huyasisimua maji haya kutengeneza tabaka linaloitwa EZ (heko Kwa Gerald Pollack), ambalo hili Sasa huwezesha protini na chembechembe zote za Ndani ya seli kufanya kazi kama inavyopaswa. Mwanga huu wa asubuhi hauishii hapo tu, Kwa msaada wa maji ambayo mtu huyu huwa ameyanywa yakutosha, au amejizoesha kunywa, basi maji haya hulowanisha chembechembe zinazoitwa "melanin", na chembechembe hizi ambazo ndani ya seli huwa kama chip za Semiconductors za kwenye simu, hushusha Umeme wa unaozalishwa katika Kuta za chembechembe hizi za mitochondria mpaka umeme sawa na Moja ya Trillion ya unit Moja ya ampere. Unajua kazi ya umeme huu? Huu umeme ndiyo huuwezesha mwili kuponyesha makovu, vidonda, tishu zilizokufa, kila kilichoharibika katika mwili wa Binadamu.
Kumbe mwanga na maji ndiyo dawa kuu za Uhai. Kadri wazee wengi wanapopungukiwa vitu hivi viwili, hupelekea chembechembe hizi za mitochondria kuvujisha Kuta zake, na kupelekea kupotea Kwa vipisi vinavyokaaga katika Kuta hizi vinavyoitwa "CC", hizi zikivuja tu zikaingia katika seli toka chembechembe za mitochondria, basi seli hufa Moja Kwa Moja.
Ndo ujue Sasa ukisikia kinachomfanya mtu kuzeeka ni kushamiri zaidi Kwa kemikali Sumu "free radicals" basi utambue hizi Sumu zote huwa zinatoka kutoka chembechembe hizi za mitochondria. Na kemikali hizi huvuja kutokana na upungufu wa maji, ambao huwa hatari zaidi unapozeeka. Na upungufu huu ndo hupelekea Sasa mitochondria kuzalisha umeme mkali sana toka chembechembe za melanin, ambazo hupelekea kushamiri Kwa umeme hata kuvuja Kwa chembechembe za electrons zinazopelekea kushamiri Kwa kemikali Sumu. na mitochondria Sasa huamua tu kusisimua protini ambazo ndizo chinja chinja, zinazoitwa "Caspases". Hizi protini huua seli za mwili Moja Kwa Moja, hiki kitendo kinaitwa "apoptosis".
Ni muhimu Kwa wasomaji wanasayansi kutambua kuwa, hutaona ongezeko la Moja Kwa Moja la kemikali Sumu "free radicals" Kwa wazee, hii ni Kwa kuwa namna seli zinavyokufa katika kipindi hiki "uzee " apoptosis", ni uuaji wa kimyakimya "silent death". Maana yake ni kuwa, kitu Pekee utakachokiona ni upungufu wa chembechembe hizi za mitochondria. Na kamwe usijaribu kuwapa sana wazee Hawa "antioxidants" kama Vitamin C ukihisi Kwa kufanya hivi utatatua shida ya uzee, SI kweli! Kemikali hizi Sumu "Free radicals" pia zinafaida zake mwilini, maana huzipa seli taarifa kuhusiana na afya ya seli kwamba inapaswa kuisha, au Inapaswa kuendelea.
Jambo la mwisho la muhimu Kwa wasomaji kutambua ni kuwa, kadri mtu anavyoelekea uzeeni, huwa anashida sana ya stress, na hii ndiyo sababu wengi sana huwa na shida ya Misongo ya mawazo. Hii inatokana na kuwa, wazee wengi huwa na shida ya Upungufu wa maji, na hivyo damu zao huwa nzito na hivyo Ubongo husisimua sana uzalishaji wa homoni "vasopressin", ambayo hii kadri inavyozalishwa, huchochea sana stress zikiwa na logic ya kuongeza Presha ya damu. Vasopressin hii ambayo ndiyo homoni ya stress huwa na lengo la kuongeza kiwango Cha maji ndani ya chembechembe za mitochondria. kwanini zinaongeza maji?
Nilishasema sababu ni kuongeza uponaji wa tishu za mwili "regeneration", na kuongeza uzalishaji wa seli za mwili "stem cells production".
Hii ina maana gani? Kumbe dawa kuu ya kutatua shida za kukosa Usingizi uzeeni, kuondoa msongo wa mawazo na usahaulifu, na shida zinginezo kama za Figo na moyo. Ni kunywa maji ya kutosha. Hii ni kwa kuwa maji ni dawa kuu ya kushusha Vasopressin "Anti-vasopressin", na hii Sio shida kuelewa. Maana kazi kuu ya vasopressin ni kutunza maji, na ndiyo maana pia huitwa ''kizuia upotevu wa maji" au "anti-diuretic hormone". Sasa, ukinywa maji, tayari Ubongo wako hautakuwa na haja ya kuzalisha zaidi vasopressin, Kwa lugha nyingine, kumbe Kwa kunywa maji, unashusha stress Moja Kwa Moja. Kwanini? Kwa kuwa upungufu wa maji ndiyo stress zenyewe.
Jambo jingine la ajabu sana, Mwanga wa Jua ule wa kuanzia saa 11:30, hata wa mpaka saa Nne, usio na frequency za Blue, hushusha stress. "Sunlight is Anti-vasopressin". Ndiyo maana, watu wanaoamka mapema sana na kunywa maji, na kutowasha taa za mianga ya Kisasa, huwa hawana stress, maana wameshatumia vitu vikubwa viwili vinavyoshusha vasopressin.
Sehemu inayokuja tutaangalia namna Mwanga wa alfajiri na alasiri pia unavyosisimua nyuklia Moja wapo katika Ubongo inayoitwa "POMC", ambayo inaposisimka huzalisha homoni kuu inayoitwa "Alpha -MSH". Hii ndo homoni inayoongoza utendaji na uzalishwaji wa homoni zingine zote, na ndiyo homoni ambayo hushusha hisia zote za Maumivu, na ndiyo homoni ambayo huongoza uzalishaji wa homoni kuu ya "Leptin". Ambayo ndiyo hutawala hisia za kuridhika, huuwezesha Ubongo kutawala utendaji wa seli zote za mwili. Watu wanapokuwa na leptin Kwa wastani mzuri, basi pia huwa na homoni za adiponectin za kutosha, ambazo hizo ndizo huupa mwili uwezo wa kupambana na changamoto zote za kujaa Kwa mafuta, na hushusha hatari za kujawa na mafuta kadri Umri unavyosonga.
Kwanini nimeelezea hili katika sehemu ya maji? Ni Kwa sababu bado homoni zote ili ziundwe zinahitaji mwili tayari uwe na maji ya kutosha. Kwanini? Kwasababu mwili unapopungukiwa maji, husisimua mfumo wa stress " HPA-axis", huu unapowaka, huzimisha mfumo wa Ubongo wa kuzalisha homoni zingine ikiwemo mfumo wa homoni za uzazi "HPG-axis". Hii ni kama, mwili hauwezi kubali kuzalisha homoni za uzazi Wakati unatambua upo katika mazingira yenye hatari kubwa sana. Kitaalamu hii pia huitwa "pregnenolone steal syndrome", yaani, unapokuwa katika stress, mwili Hutumia cholesterol zote kuzalisha zaidi "cortisol" ambayo nayo ni "stress hormone".
Mengineyo
Sehemu hii inaelezea Kwa wazi zaidi ni Kwanini shida zote za uzeeni hutokea kutokana tu na upungufu wa maji, na upungufu wa Mwanga. Wazee pia huwa hawana Nguvu za mifupa, hii ni kutokana na upungufu wa vitamin D inayofyonza madini ya mifupa "calcium" toka katika Utumbo. Lakini pia upungufu wa maji huifanya mifupa kuwa kama zege lilipongukiwa maji, hulegea, katika kitabu nimeelezea namna mianga ya Kisasa, upungufu wa ATP' au nishati, n.k. namna ambavyo huamasisha changamoto hizi.
Wazee pia huwa na mvi nyingi kama ishara ya Upungufu wa chembechembe za melanin, na ndivyo huwa pia upungufu wa nywele, na kulegea Kwa ngozi, haya yote yanaweza punguzwa Kwa unywaji wa Maji, na kupata nyakati za kutosha katika mianga ya UV.
SULUHISHO KWA WAZEE NA WAZEE WATARAJIWA
1 kunywa maji ya kutosha, kuanzia Lita mbili na nusu, mpaka Lita tatu, hata Lita tatu na nusu Kwa maeneo yenye Joto sana. Unywaji huu usiwe Kwa mara Moja, utawanyike ndani ya masaa kumi na mbili. Na usiwe nusu saa kabla na baada ya Chakula.
2.unywaji wa maji uambatane na matumizi ya chumvi ya mawe SI chini ya gramu Nne Kwa siku. ( Sio chumvi ya mezani, chumvi ya mawe ina madini zaidi ya 84, ikiwemo na ya magnesium, ambayo haya husaidia kubalansi kiwango Cha maji nje ya seli)
Kwanini?
Kwasababu maji yote yaliyo nje ya seli "ECF" hushikiliwa na chumvi hii, hivyo ukipungukiwa chumvi hii, utapungukiwa na Maji, ijapokuwa hospitalini utaambiwa umepungukiwa Chumvi " hyponatremia". lakini hoja ni kuwa, hata ukifia Mtoni, bado utakufa Kwa upungufu wa maji! Usishangae, maana bado upungufu wa Oksijeni hupelekea upungufu wa maji ambayo ndiyo huundwa katika Mitochondria, na ndiyo ambayo hutawala Biolojia ya uhai. Kwa hiyo umekufa Mtoni, lakini umekufa Kwa upungufu wa maji, Kwa kupungukiwa Oksijeni.
3.unywaji wa maji uambatane na kutembea tembea, hii ni Kusaidia maji yasukumwe Kila Kona ya mwili. Na unapotembea, unavunja mafuta yanayozuia mishipa ya damu isipitishe maji vizuri.
4.Mzee Usinywe kahawa, wala soda, wala chai ya rangi, wala Pombe. Maana Kwa kufanya hivi, unapoteza zaidi maji ilihali tayari una upungufu wa maji. Vinywaji hivi vina Caffeine ambayo husisimua upotezaji wa maji zaidi, na hu boost stress Kwa kusisimua "adrenaline".
5.Mzee usipende kutumia dawa za Maumivu, kama "NSAIDs" hii ni Kwa kuwa, dawa hizi hublock " Prostaglandins" na hublock pia "Histamines", kipindi ambacho kemikali hizi ndizo hujiusisha na kusambaza zaidi maji mwilini, na pia, Maumivu haya huwa ndiyo alarm ya mwili kusisimua Uponaji "Regeneration".
Wengi hawajui kuwa mwili ili uanze kujiponyesha, lazima uhisi kwanza Maumivu. Katika tafiti za mijusi (zilizofanywa na Robert O Becker na wengineo), mijusi ambao huweza jiunda kata mikia yao ikikatwa. utagundua kama utaua Neva zao za fahamu, hawataweza Tena jiponesha. Ndivyo ilivyo pia, badala ya kukimbilia paracetamol, unaweza tumia maji, na Mwanga, na hata Baridi Kama tutakavyoona katika sehemu zijazo.
6.mzee inabidi uongeze sana kutumia matunda, kama maparachichi, ili kuongeza kiwango Cha madini, na maji mwilini. Maji yaliyo katika matunda ni bora sana Kwa mwili.
7.mwisho, Mzee anapaswa kutumia sana Supu za nyama. Hasa wanyama wanaolishwa majani, na kuku wa kienyeji, au Samaki. Usitumie nyama zilizopikwa Kwa mafuta ya Mbegu. Wazee wengi wanaopatwa na stroke huogopa Cholesterol, lakini wengi wao hawajui Cholesterol inapoungana na vitamin A chini ya uwepo wa homoni za thyroid "T3 na T4", ndiyo hutengeneza homoni zingine zote za mwili ambazo wao huwa Wana upungufu. Mzee mwenye uwezo kiuchumi badala ya kutumia mkate na chai asubuhi, basi ili asizeeke haraka, angepaswa kutumia mayai ya kuchemsha na siagi "Sio ya Kisasa", angetumia kachumbari badala ya kutumia mchuzi uliojaa mafuta ya Mbegu.
Mwili unapopungukiwa stress, huacha kuvunjavunja Collagen zilizo katika ngozi, na kuiacha ngozi kuwa imara, uwepo wa vitamin C na madini ya Copper na Zinc yakutosha huwezesha nywele kuwa imara na kutopoteza rangi Kwa haraka sana, matunda kama Machungwa, maembe, n.k. husaidia sana kubalansi madini haya, na Kwa kufanya hivi ikiwa Mzee na mtu huyu ana maji, basi ngozi ya mtu huyu huwa imara, nzuri, na yakuvutia.
Kumbuka
Kunywa maji haijawahi kuwa kazi rahisi! Pia, kunywa maji huleta kero ya kukojoa kojoa. Hii husaidia kusafisha Figo, kutoa sumu mwilini. Na pia, humfanya mtu asikae sana chini Kwa kero za kwenda kukojoa. Watu wengi wanapofikia tu lita Moja ya maji hujisahau kabisa kuendelea kunywa maji! Hili huwafanya kufeli kuelewa umuhimu wa kuendelea kunywa maji, na kushindwa kutatua tatizo la kuwahi kuzeeka na kufa.
Hupaswi kusubiria kiu kunywa maji, inapaswa kuwa sehemu ya maisha yako.
KUHUSU MWANDISHI
Dr. shoo anaamini Mungu alimuumba mwanadamu toka katika maji. Yaani, Kila kilichoumbwa kuanzia siku ya pili, kilianzia katika maji yaliyokuwepo siku ya kwanza, ambayo Mungu alianza kuyaumba na Roho yake ikawa ikielea katika vilindi vya maji haya.
Sayari ya Dunia ndiyo sayari Pekee yanye maji kama inavyoonekana toka katika Picha za satalaiti. Wanasayansi wa anga huiita Dunia "Water planet". Ina asilimia 75% maji.
Hakuna namna unaweza elezea asili ya maji katika Dunia. namna Pekee ni kupitia Kutambua "Uumbaji wa Mungu" mwandishi ameandika kitabu kizima kinachoelezea tu Sayari ya Dunia, na asili ya maji yake, na chanzo Cha maji ya chumvi yaliyopo Duniani. Na hata kinaelezea kwanini ongezeko la madini ya Deuterium kwenye maji kipindi Cha Gharika ya Nuhu ndiyo chanzo kikuu Cha kushuka Kwa Umri wa kuishi toka miaka 900, mpaka miaka 600 na Kisha 120. Madini haya pamoja na Carbon-14. Ndiyo chanzo kikuu Cha kushuka Kwa Uhai wa wanadamu kutokana na kuathiri Moja Kwa Moja utendaji wa Mitochondria au chembechembe za Uhai.
je WAJUA!
Kwa kunywa maji unaongeza Kinga dhidi ya magonjwa ya Virusi. Maana Virusi wengi Hutumia sensa za "ACE" kuingia ndani ya seli, na Kwa kunywa maji ya kutosha, mwili huwa na kiwango kidogo sana Cha "ACE" Kwa kuwa huwa hakuna haja ya mfumo mzima wa kutunza maji "RAAS". na ukiwa umeamka asubuhi pia, mwili huzalisha Vitamin D ambayo nayo husisimua sensa za Kinga dhidi ya Virusi " Immune cells", na huwa Mwanga wa alfajiri huzalisha pia "NO" ambazo husisimua sana mishipa ya damu kujitanua, kurelax, na mfumo mzima wa Kinga. Vitamin D ya asubuhi pia hushusha Rennin katika Figo, hivyo Kusaidia zaidi kushusha Presha ya damu, na afya nzima ya mwili.
je WAJUA!!
Magonjwa mengi ya Virusi na mengineyo husambaa zaidi kupitia vimiminika vya mwili hasa damu, na uteute wa sehemu za uzazi. Sababu vimelea wengi sana hubebwa na maji maji ya mwilini, ila vimiminika vya uzazi huwa na vimelea wengi zaidi maana huwa na Kinga chini kidogo ya wastani, ili kuzuia muitikio wa Kinga wa jinsia Moja kuua seli za uzazi toka jinsia nyingine. Hivyo ni hatari sana kuzoelea uzinzi, na namna za mapenzi yanayohusisha kujikutanisha sana na vimiminika vya uzazi Kwa kinywa.
Je WAJUA!!!
unywaji unywaji wa vitu vya sukari, na hata damu za Wenye ugonjwa wa Kisukari, huwa nzito sana. Na uzito huu wa damu, au kupungukiwa huku Kwa maji, huwafanya kuwa na kiu sana, na huwafanya kuwa na Kinga dhaifu sana.
KUJIFUNZA ZAIDI
Unaweza jipatia Kitabu chako Cha Mwanga na Maji Tiba kuu za Magonjwa ya Kisasa.
Unaweza jifunza zaidi katika blog yetu ya Injili ya Sayansi.
Unaweza sikiliza baadhi ya masomo yetu yaliyo YouTube Kwa chaneli ya Injili ya Sayansi.
Unaweza pia tupata Redioni Kwa chaneli ya AWR-fm, na semina kadhaa.
AHSANTE NA UBARIKIWE NA YESU KRISTO.
MAWASILIANO
brightonshoo7@gmail.com
0628231767


Join the conversation